Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Ripoti ya siri ya watalaam wa Umoja wa Mataifa imeishtumu Rwanda kwa kutoa maagizo na kudhibiti shughuli za waasi wa M23.
Kamishna wa zamani wa tume yakifalme ame kosoa serikali, kwa kufeli kuchukua hatua haraka kwa mfumo wakitaifa wakufanya ukaguzi kwa ajili yakufanya kazi na watoto.
Huenda umesikia kwamba wa Australia ‘ni maarufu kwa kunywa', haswa wakati wa matukio makubwa ya michezo au katika siku kuu za umma.
Wanachama wa jumuiya ya DR Congo wanao ishi jimboni NSW, Australia walijumuika kwa sherehe maalum katika uwanja wa Fairfield Park, Fairfield, NSW.
Mamia ya wafanyakazi wa huduma za dharura, helikopta na magari yawataalam yako katika hali ya tahadhari wakati kimbunga kina elekea katika maeneo ya kanda yanayo endelea kupona mafuriko mabaya katika eneo la Kaskazini New South Wales.
Uwakilishi wa WaAustralia wa Asili katika vyombo vya habari kihistoria umechangiwa na mila potofu na kutengwa ila, hali hii inabadilika pole pole.
Anthony Albanese amesema Australia haita ongeza matumizi yake ya ulinzi mwezi wa Aprili ijayo kama sehemu ya mkakati wa ulinzi wa taifa, baada ya wito kutoka Marekani kupiga jeki bajeti ya Ulinzi.
Wanachama wa Jumuiya yawa Kenya wanao ishi Victoria (KCV), wanashiriki katika uchaguzi wa bodi mpya ya viongozi wao.
Waziri Mkuu wa Anthony Albanese ametetea msimamo wa serikali kwa matumizi ya ulinzi, nakutupilia mbali wito kutoka utawala wa Trump kuongeza matumizi hadi asilimia 3.5 ya pato la taifa.
Unapenda theluji kiasi gani? Au ume wahi iona?
Waziri wa fedha wa shirikisho Katy Gallagher ametetea bajeti ya ulinzi ya Australia, wakati kuna shinikizo kutoka humu ndani na kutoka ng'ambo.
Je, unajua jinsi yakufanya marejesho ya ushuru?
Neno goons lina sifa mbaya katika jamii, haswa kwa vijana wengi ambao hu husishwa na maswala yanayo enda kinyume na sheria na maadili mazuri.
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia imesimamisha uhamishaji kwa mabasi kutoka Israel, kufuatia shambulizi la Marekani katika vifaa vya nyuklia vya Iran ila, inajiandaa kwa uwezekano wakufanya uhamisho kama anga ya Israel itafunguliwa tena.
Je, unajua jinsi ya kuzunguza kuhusu jinsi yakupanda bustani ya jamii na miema?
Tangu 2024, serikali ya shirikisho imezindua sera kadhaa zaku zuia idadi ya wanafunzi wakimataifa, pamoja naku ongeza ada ya maombi ya viza ya wanafunzi na, kupunguza kasi muda wa usindikaji wa viza.
Australia imesimamisha oparesheni katika ubalozi wake katika mji mkuu wa Iran, nakuamuru kuondoka kwa maafisa wote wa Australia kwa sababu yakudorora kwa mazingira ya usalama.
Haipendezi kufikiria kuhusu matukio yanayo weka nyumba na mali yako hatarini, ila haviko kawaida.
Ulaya imechukua nafasi yaku fanya mashauriano na Iran, mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ujerumain na Ufaransa wanazungumza na mshirika wao kutoka Iran.
Wachezaji wa soka katika mashindano mjini Perth, wanafanya mengi zaidi yakufunga magoli, wanajenga madaraja kati ya jamii naku mulika nguvu ya jamii zawakimbizi wa Magharibi Australia.
Waziri Mkuu Anthony Albanese amefanya mikutano na rais mpya wa Korea Kusini, pamoja na katibu mkuu wa NATO pembezoni mwa mkutano wa G7.
Uhuru wa vyombo vya habari na vyombo vya habari tofauti ni alama muhimu ya afya nzuri ya demokrasia ambako raia na waandishi wa habari wana mamkalaka ya kujielezeza, kupata taarifa na kuchapisha bila hofu ya kuingiliwa au adhabu kutoka kwa serikali.
Waziri Mkuu Anthony Albanese, amesema mazungumzo kati yake na mshiriki wake kutoka Canada katika mkutano wa G7, ilikuwa fursa yaku imarisha tena uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Wiki hii timu ya mpira wa miguu ya taifa Socceroos, ili fuzu kwa Kombe la Dunia tena baada yakupata ushindi dhidi wenyeji wao Saudi Arabia.
Balozi wa zamani wa Australia nchini Marekani, Arthur Sinodinos, amesema mkataba wa AUKUS unastahili kuwa kipaumbele kikuu katika mkutano kati ya Waziri Mkuu Anthony Albanese na Rais wa Marekani Donald Trump.
Mwaka jana pekee, zaidi ya kesi 3200 za ulaghai wa mapenzi zili ripotiwa nawa Australia.
Kiongozi wa Tasmania wa chama cha Liberal anatarajiwa kuitisha rasmi uchaguzi wa mapema hii leo, hatua itakayo rejesha jimbo hilo la kisiwa katika uchaguzi wa pili katika muda wa miaka mbili.
SBS ina sherehekea miaka 50.
Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu amefariki akiwa na umri wa miaka 68.
Bunge ya Tasmania yapitisha kura yakutokuwa na imani kwa kiongozi wa jimbo hilo Jeremy Rockliff. Mswada huo ulio wasilishwa na kiongozi wa chama cha Labor Dean Winter, ulipita kwa kura 18 dhidi ya 17, Spika wa Labor Michelle O'Byrne alipiga kura iliyo toa uamuzi wa muswada huo.
Unajua mtu anaye toa mchango usio wa kawaida katika jamii? Anaweza kuwa mtu kutoka mazingira yoyote, au mwenye taaluma yoyote.
Marekani imetumia kura yake ya turufu dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililo kuwa likiomba kusitishwa kwa vita pamoja na misaada yakibinadam kuruhusiwa kuingia katika ukanda wa Gaza bila vizuizi.
Uchambuzi mpya wa hazina ume onesha gharama ya Kimbunga Alfred na mafuriko mengine katika majimbo ya New South Wales na Queensland imefika takriban $2.2 bilioni dollars.
Seneta Dorinda Cox wa Magharibi Australia ametangaza anahama kutoka chama cha Greens, na atakuwa Seneta wa chama cha Labor hii leo Juni 3.
Australia has a dark chapter of history that many are still learning about. Following European settlement, Aboriginal and Torres Strait Islander children were removed from their families and forced into non-Indigenous society. The trauma and abuse they experienced left deep scars, and the pain still echoes through the generations. But communities are creating positive change. Today these people are recognised as survivors of the Stolen Generations. - Australia ina sura ya giza ya historia ambayo wengi bado wanajifunza kuhusu. Kufuatia ujio wa wazungu, watoto wa wa, Aboriginal na Wanavisiwa wa Torres Strait wali ondolewa kutoka familia zao, nakulazimishwa kuishi katika jumuiya zisizo za kiasili. Kiwewe na unyanyasaji walio pitia uliacha makovu makubwa, na uchungu huo bado una hisika kupitia vizazi. Ila Jamii zinaleta mabadiliko chanya. Leo hawa watu wanatambuliwa kama wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa.
Wakati inaweza chukua zaidi ya mwaka kwa baadhi ya madai ya bima ya mafuriko kutatuliwa, malipo ya mara moja kwa walio athirika jimboni New South Wales yata anza kutolewa leo 30 Mei 2025.
Siku nane baada ya upinzani wa mseto kuachana, vyama vya Liberal na Nationals vime tangaza kuwa vime rudiana tena.
Idadi ya nyumba zilizo haribika kabisa katika mafuriko jimboni New South Wales imeongezeka mara mbili nakufika takriban 800. Huduma ya dharura ya jimbo [[SES]] imesema nyumba 794 katika kanda ya pwani ya kati ya kaskazini, zime zingatiwa kuwa haziwezi tumiwa tena baada ya zaidi ya tathmini 5000 za uharibifu kufanywa.
Matukio yame fanyika kote nchini Kuadhimisha Siku ya Kitaifa yakuomba msamaha 26 Mei, hatua ambayo ni kukiri kuondolewa kwa lazima kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza kutoka kwa familia na tamaduni zao.
Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema hatua ya Israel kuzuia msaada “hai kubaliki kabisa”. Israel ina ruhusu msaada mdogo wakibinadam kuingia Gaza, baada ya takriban miezi mitatu yaku izuia, hali iliyo sababisha uhaba wa chakula na matibabu.
Ukosefu wa vyakula na bidhaa zingine muhimu, umelazimisha UNHCR kuomba msaada wa dharura kwa wakimbizi wenye asili ya Sudan Kusini, walio kimbilia DRC.
Kiongozi wa New South Wales, Chris Minns, amesema rasilimali za ziada zinatolewa kwa jumuiya ambazo zime athiriwa kwa mafuriko, katika eneo la kati ya pwaZaidi ya idadi ya watu elfu 48,000 kwa sasa wame tengwa kwa sababu ya maji ya mafuriko.
Je, unajua jinsi ya kuzungumzia sifa zako za kukimbia au kufanya riadha?
Mandhari yakupendaza na tofauti ya Australia, kuanzia pwani hadi jangwani na yote yaliyo katikati, ni nyumbani kwa mimea ya asili na wanyama wakushangaza.
Jimbo la Victoria lina tarajia kupata ziada yake ya kwanza tangu janga la UVIKO-19, wakati serikali ya Allan itakapo toa bajeti ya jimbo hii leo Jumanne 20 Mei 2025.
Wiki ya kitaifa yakujitolea ime anza, ita kuwa kuanzia 19 Mei hadi 25 Mei 2025.
Kiongozi wa Upinzani wa Shirikisho Sussan Ley, amesema kuungana tenana wanawake itakuwa kipaumbele chake kama kiongozi wa Upinzani wa shirikisho.
Baadhi ya wanachama wa jumuiya yawa Afrika wanao ishi Melbourne, Victoria wame kuwa waki kabiliana na wakati mgumu katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa jimbo na shirikisho.
Sussan Ley ame chaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Liberal. Bi Ley alikuwa Naibu Kiongozi wa chama hicho cha Liberal, alimshinda mpinzani wake mwekahazina kivuli Angus Taylor, katika kura yakumchagua kiongozi mpya muda mfupi ulio pita mjini Canberra.
Tanya Plibersek ame shushwa cheo nakupewa wizara ya Huduma za Jamii, wakati Anthony Albanese anatangaza baraza lake la mawaziri, atakao fanya kazi nao katika muhula wake wa pili serikalini.
Anthony Albanese akosolewa kwa kumshasha cheo waziri pekee Muislamu katika baraza lake la mawaziri, wakati vyama vya upinzani vya ongeza juhudi yaku wachagua viongozi wao wapya.