POPULARITY
Afrika ina kiwango kikubwa cha ukataji misitu kuliko mabara mengine yote duniani. Hili lina athari kubwa kwa maisha ya Waafrika kama hawa katika mchezo wetu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi baada ya vita vya kikatili.
Huku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.
Hulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.
Vipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.