Noa Bongo – Uchumi na Mazingira

Follow Noa Bongo – Uchumi na Mazingira
Share on
Copy link to clipboard

Katika mfululizo wa vipindi vyetu utapata fursa ya kujifunza kuhusu masuala ya uchumi na biashara pamoja na mazingira.

DW.COM | Deutsche Welle


    • Mar 13, 2014 LATEST EPISODE
    • infrequent NEW EPISODES
    • 11m AVG DURATION
    • 35 EPISODES


    More podcasts from DW.COM | Deutsche Welle

    Search for episodes from Noa Bongo – Uchumi na Mazingira with a specific topic:

    Latest episodes from Noa Bongo – Uchumi na Mazingira

    Mti unapoanguka… - Kukatwa kwa misitu barani Afrika

    Play Episode Listen Later Mar 13, 2014 12:30


    Afrika ina kiwango kikubwa cha ukataji misitu kuliko mabara mengine yote duniani. Hili lina athari kubwa kwa maisha ya Waafrika kama hawa katika mchezo wetu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi baada ya vita vya kikatili.

    Anasa ya Kuazima – Hatari ya Kuchukua Mkopo

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2013 11:58


    Tatizo linaanzia na ari ya kutaka kumiliki baiskeli mpya ya kifahari. JD hana fedha za kutosha lakini anashindwa kuvumilia na kuchukua mkopo – ingawa hajui atakavyoulipa mkopo huo. Je, somo hili litamuathiri vipi JD?

    Ufisadi - Tembo chumbani

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2013 11:58


    Iwe shuleni, kazini au hata barabarani, familia ya Odhiambo inajikuta ikishinikizwa na athari za ufisadi licha ya juhudi za kutaka kuishi maisha huru yasiyo na dosari ya uovu huu. Watawezaje kuepukana na vitendo hivyo?

    Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika

    Play Episode Listen Later May 10, 2012 11:43


    Hulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.

    dw kazi hili noa bongo
    Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika

    Play Episode Listen Later May 25, 2011 9:59


    Vipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 10 – Habari nzuri sana

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Katika awamu ya mwisho ya safari, tunaona mabadiliko katika hadithi wakati Tingo anapoonyesha nia ya dhati katika chama. Baki na Zeina wanapatana kwa kinywaji. Tujiunge nao!

    Uhamiaji mijini – Kipindi 09 – Fikra zilizogubikwa na wingu jeusi

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Tingo hafurahii ufanisi wa chama na huenda akawa na njama fulani. Hii itakuwa na maana gani kwa mashujaa wetu?

    Uhamiaji mijini – Kipindi 08 – Furaha ya mapenzi

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Hadari amebadili nia na Baki amebadili mipango – hatua inayomfurahisha sana Zeina. Tufuatilie mabadiliko yote yanayoendelea.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 07 – Kushindwa kwa rushwa

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Katika kipindi hiki Baki anapelekwa hospitalini – nini kilichotokea? Lakini kwanza tutafute jinsi chama kinavyoendelea na vipi mashujaa wetu chipukizi wanavyokabiliana na changamoto.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 06 – Kukabiliwa na vikwazo huku ukiniwa na shinikizo

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Kwa nini Ben anakataa pendekezo zuri kutoka kwa Tingo, ingawa chama kinahitaji fedha? Kipindi kinapofikia tamati, kitu kingine kinaendelea kati ya Ben na Nana.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 05 – Umuhimu gani wa kuwa sahihi iwapo uko peke yako

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Mpaka sasa kila kitu kinaonekana kwenda kulingana na mpango. Wanakijiji wanauonaje mradi huo? Tunaungana na mashujaa watatu katika mkutano na Hadari na tusikilize huku wakifanya mkutano wao wa kwanza wa mwaka.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 04 – Ndoto ya kila mwanamke

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Hatua kwa hatua, marafiki zetu wanapiga hatua wanapojaribu na kuungwa mkono na wanakijiji. Hata hivyo uhusiano kati ya Baki na Zeina unaonekana ukichukua mkondo tofauti.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 03 – Kipato cha kila siku

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Baki, Zeina na Ben wanataka kuanza kwa ufanisi. Kwa bahati mbaya kurejea kijijini huenda kusiwe rahisi kama inavyoonekana na si kila mtu anafurahia kuwaona.

    Uhamiaji mijini – Kipindi 02 – Kuwa na majukumu uhamishoni

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Ungana na marafiki zetu wanapofikiria kuvumbua mpango wa biashara kwa chama chao cha kilimo. Lakini Baki ana jambo lengine akilini mwake.

    Uhamiaji mijini– Kipindi 01 –Bila kazi mjini hakufai

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 12:26


    Katika vipindi hivi vipya, Ben, Baki na Zeina watatueleza matukio yasiyo ya kawaida wanapoamua kuondoka mjini kwenda kijijini kutimiza ndoto zao.

    Mazingira Afrika – Kipindi 10 – Vyakula vya baharini

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Kwa nini ni muhimu kuwafundisha wavuvi kutumia nyavu ili kuwalinda kaa? Juhudi gani zinaweza kuchukuliwa kuwalinda Papa? Sikiliza na ufahamu zaidi juu ya hilo na mengine.

    Mazingira Afrika – Kipindi 9 – Uvuvi wenye madhara

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Kipindi hiki kinazungumzia uvuvi wa kutumia baruti unavyoathiri matumbawe ambayo yanahitaji karne kujengeka, lakini yanaweza kuharibiwa kwa sekunde moja tu. Nini kinachowakumba wanyama na mimea ya baharini?

    Mazingira Afrika – Kipindi 8 – Jangwa

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Majangwa barani Afrika yamekuwa yakiongezeka. Hii ni kutokana na shughuli za kibinaadamu duniani kwa mfano ongezeko la malisho pamoja na ukataji miti. Je, ni jinsi gani wakulima wanawajibika kwa hali hiyo?

    Mazingira Afrika – Kipindi 7 – Ukataji miti

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Ukataji miti umesababisha madhara makubwa kwa mazingira. Bara la Afrika limepoteza misitu mingi kuliko bara lingine lolote. Fahamu kuhusiana na biashara haramu ya mbao pamoja na madhara yake.

    Mazingira Afrika – Kipindi 6 –Nishati Endelevu

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Mahitaji ya mafuta, mkaa na gesi bado ni makubwa. Lakini vyanzo vya nishati hii si vya kudumu, kwa hivyo tutapata wapi nishati hii? Tutaangazia nishati nyingine mbadala na inayoweza kutumika tena kama vile upepo na jua.

    Mazingira Afrika – Kipindi 5 - Kuni

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Afrika inategemea kuni kwa ajili ya kupikia lakini mahitaji ya mkaa yameharibu misitu barani humo. Hebu tuangalie njia mbadala kama vile kupika chakula kwa kutumia joto na mwanga wa jua.

    Mazingira Afrika – Kipindi 4 – Magari na Baiskeli

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Gari ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hali ya hewa. Hutoa hewa ya kaboni inayochangia ongezeko la ujoto duniani. Gundua faida za usafiri wa umma pamoja na baiskeli.

    Mazingira Afrika – Kipindi 3 –Nyama pori

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Shughuli za kibinaadamu huwa na madhara kwa maisha ya wanyamapori. Tunajua athari za biashara haramu ya nyamapori ambayo ni ya kawaida Afrika. Ni viumbe gani ambao wako katika hatari ya kutoweka?

    Mazingira Afrika – Kipindi 2 – Elimu ya wadudu waharibifu

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Elimu ya wadudu waharibifu inaweza kuongeza mazao yetu lakini ina madhara makubwa kwa mazingira. Tutaona jinsi sumu ya kuua wadudu inavyojipenyeza kwenye ardhi na maji. Tutajifunza jinsi ya kufanya kilimo cha zao moja.

    Mazingira Afrika – Kipindi 1 - Takataka

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 9:57


    Suala la takataka limekuwa ni tatizo sugu. Na kwa serikali za Afrika kulishughulikia suala hilo ni jukumu kubwa. Tutaelezea hatari ya mifuko ya plastiki kwa viumbe wa baharini, jinsi inavyoharibu mazingira ya majini.

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 10

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Bi Kimasi anaeleza motisha wake wa kupigania nishati zinazoweza kutumika tena na tena. Bodi ya kitaifa inafanya mkutano na waandishi wa habari – Je tangazo lao litalifurahisha jopo letu? Tega sikio!

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 09

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Pendekezo la marafiki zetu linakaribia kukamilika. Lakini je hiyo ina maana wanaweza kuishawishi bodi ya kitaifa ya umeme? Na kwa nini wazo la Alex kuhusu nishati ya upepo linapingwa na wenzake? Haichafui mazingira, ama?

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 08

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:55


    Ng'ombe wana uhusiano gani na mabadiliko ya hali ya hewa?Jifunze huku marafiki zetu wakiendelea na juhudi zao. Lakini wale wanaounga mkono ujenzi wa kiwanda cha umeme si rahisi kushawishika! Je wana njama gani?

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 07

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Wasiwasi zaidi unachomoza! Lakini kwa bahati nzuri, ufanisi nao unabisha hodi. Juhudi zao hatimaye zitafaulu wakati wanapopata msaada usiotarajiwa. Tega sikio!

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 06

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Nishati zinazoweza kutumika tena na tena ni mada pana, kama marafiki zetu wanavyokaribia kugundua. Hakuna anayeonekana kuwa na ujuzi kwa sasa. Jopo lao linahitaji kujiandaa kwa kibarua kigumu. Je, wataweza kusonga mbele?

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 05

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Mkutano na mwanabiolojia wa viumbe wa baharini unadhihirisha taarifa za kutisha kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Lakini mivutano inazidi miongoni mwa marafiki zetu na juhudi za kuwatisha! Je, watafanya nini?

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 04

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Marafiki zetu wanakwenda kwenye wingu kubwa la moshi yaani mjini kukutana na mwanasayansi wa mazingira. Kwa bahati mbaya wanaounga mkono ujenzi wa kiwanda cha umeme wameanza kuzitatiza juhudi za jopo la vijana!

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 03

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Je athari za kubadilika kwa hali ya hewa ni zipi? Ni nani anayenufaika na anayepata hasara? Na je marafiki zetu chipukizi wanapanga kufanya nini kuhusu kiwanda cha umeme? Tega sikio!

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 02

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:56


    Lorna anajifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati huo huo, Alex anagundua kile ambacho babake na mshirika wake wa kibiashara wanafikiri ni muhimu zaidi – kiwanda cha umeme au mazingira. Unaweza kuagua?

    Mabadiliko ya Hali ya Hewa – Kipindi cha 01

    Play Episode Listen Later Mar 16, 2011 11:55


    Jiunge nasi wakati tunapokutana na vijana wanne chipukizi - Joshua, Carol, Lorna na Alex ambao wanasikia mipango ya ujenzi wa kiwanda cha umeme. Pia tutachunguza athari za gesi chafu za viwandani. Je, kuna uhusiano?

    Claim Noa Bongo – Uchumi na Mazingira

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel