Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.
Huku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.
Kila binaadamu hapa duniani ana haki ya uhuru na usawa - kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binaadamu. Lakini katika mataifa mengi barani Afrika, utakuta haki hizi zinaendelea kukanyagwa na kukiukwa.
Katika kipindi hiki, tutageuka na kuangazia sekta ya muziki na kupata nafasi ya kumfahamu Chimere Emejuobi, mwimbaji kutoka Lagos. Muziki ni muhimu sana katika jamii nchini Nigeria.
Hatutazungumzia juu ya taaluma fulani, lakini ni juu ya wale wote ambao hawana ajira. Idadi ya wasio na ajira hususan miongoni mwa vijana imeongezeka sana barani Afrika. Kila kijana mmoja kati ya watano hana ajira.
Katika mji mkuu wa Kenya, tunakutana na watu wanaofanya shughuli zao ambazo ziko nje ya sekta rasmi ya uchumi. Wanashughulika kinyume na sheria bila ya kuwa na elimu stahiki, mfano biashara ya kiwango cha rejareja.
Tutaiangazia sekta ya elimu huko Lagos Nigeria. Kwa jumla waalimu hulipwa mshahara mdogo. Lakini kwa baadhi yao, la muhimu ni hamasa ya kufundisha na hamu ya kuwapatia ufahamu wanafunzi wao.
Katika kipindi hiki tutapata nafasi ya kumfahamu kijana mmoja nchini Uganda ambaye ni meneja wa hoteli. Je kuna ugumu gani wa kufanya kazi ya umeneja wa hoteli katika nchi zinazoendelea kama Uganda?
Mtandao wa Intaneti ni lango kuu la kujiunga na jamii duniani. Hata hivyo bado watu wengi hawana uwezo wa kuitumia. Wafanyakazi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanajaribu kulibadilisha suala hili.
Kuna taaluma ambazo zinachukuliwa kuwa ni za wanaume tu. Ni wanawake wangapi wanaoweza kurekebisha magari au pikipiki? Estelle Christian Ouedraogo, kutoka Burkina Faso, ni miongoni mwao. Tujiunge naye!
Katika mfulululizo huu, tutakutambulisha kwa vijana wa kiafrika wenye taaluma mbalimbali, na kukupatia undani wa shughuli zao. Kwanza tutapata nafasi ya kumfahamu Judith ambaye ni nesi katika hospitali huko nchini Kenya.
“Wanaopata, wanaoweka. Anayepata kitu fulani njiani anaruhusiwa kukimiliki” Je, ni rahisi namna hiyo kila mara? Sikiliza hadithi ya kobe na tumbiri mjanja aliyelazimika kupata adhabu kuokoa mkia wake!
Hadithi yetu inatokea zamani za kale, wakati tausi alipokuwa angali mweupe. Jifunze jinsi alivyopata rangi zake nyingi na wakati huo huo kuiharibu sauti yake
Siku moja bundi mzee na nyenje kijana wanakuwa majirani. Mwanzoni wanafurahia kuishi kwa pamoja, lakini kadri muda unavyopita bundi anakasirika na nyenje anavunjika moyo. Watafanya nini?
Katika hadithi hii, marafiki zetu wanyama wenye njaa wanalazimika kutafuta njia ya kuchuma matunda mtini. Inaonekana kuwa kazi rahisi lakini mti wa maajabu wa marula unawafunza somo zuri
Mwanamke kizee akamwambia Amadou. “Usijiingize katika hali usizoweza kukabiliana nazo! Fuata maagizo yangu.” Lakini wakati mwingine inahitaji uhodari mkubwa mtu kukubali udhaifu wake, kama Amadou atakavyogundua
Kassi na Kaloo – marafiki wasioweza kutenganishwa! Angalau hali ilikuwa hivyo kabla farasi hao wawili wa kupendeza kupandwa na wafalme wawili mahasimu. Watafanya nini wakati vita vitakapozuka kati ya falme zinazopigana?
Je unaamini hirizi za bahati na mawe ya mazingaombwe? Sawa, zuia wazo hilo na tumruhusu ngiri atueleze hadithi yake kuhusu kilichomuokoa, na vipi
Fuata nyayo za Lipua! Njiwa jasiri ana kibarua cha umuhimu mkubwa. Je Lipua atamshinda mfalme mlafi na muovu Karamba na kuwaokoa ndege wenzake wasife kutokana na njaa?
Zamani paliondokea simba na fisi mwenye njaa. Kilichoanza kama uhusiano wa ajabu lakini wa furaha, kinamalizika huku fisi akiwa amejeruhiwa maisha yake yote na tai akipoteza manyoya yake kadhaa
Katika mfululizo mwingine wa kusisimua, tunautembelea ulimwengu wa mjusi kafiri Sindakh na chura aitwaye Mbott – hadithi kuhusu urafiki, uaminifu na usaliti
Malaika ndiyo kwanza amerejea kutoka katika mahafali mjini na anakwenda nyumbani kusherehekea na familia yake. Huko ndiko majaaliwa yake yatakapoamuliwa
Huko chuoni, Malaika anawajibika kumaliza elimu ya vitendo ili kukamilisha mwaka wa masomo. Kwa msaada wa rafiki yake Malaika amefanikiwa kupata shirika atakakofanyia mafunzo hayo. Je anafaulu mtihani wake wa mwisho?
Malaika anakwenda nyumbani kwa likizo yake ya kwanza. Anaitembelea shule yake ya zamani kuwahamasisha vijana kusoma na kuzuia mipango mingine ya wazazi wake kutaka aolewe. Je anaweza kuingiliana na maisha ya kijijini?
Malaika anajifunza kuwa kuna vitu vya kujifunza nje ya masomo. Cindy, mkaazi mwenzake anamuonyesha jinsi ya kufurahia maisha ya chuoni lakini bado anakabiliwa na changamoto ya kutojiangusha yeye mwenyewe au kijiji chake
Kwa msaada wa kijiji chake, na mkopo binafsi, Malaika hivi sasa anaweza kulipia ada ya chuo kikuu.Mwalimu wake wa zamani anamsindikiza katika jiji kubwa kumsaidia kujisajili na kupata makazi chuoni.
Tutajifunza zaidi kupitia hadithi ya Malaika, jinsi ya kusoma chuo kikuu. Msichana huyo wa kijijini alijitofautisha na wengine alipowashinda wavulana wote katika mtihani wake wa mwisho shuleni. Je nini mustakhbali wake?
Zapcom na timu yake wameibadili taswira ya kijiji chao. Katika kipindi hiki cha mwisho, timu yetu inatuaga huku ikiendelea kutafuta fursa kubwa zinazotolewa na teknolojia mpya ya mawasiliano kwa bara laf Afrika.
Huku fursa za teknolojia mpya ya mawasiliano zikiongezeka, inatoa mwanya wa kupanua biashara. Bonyeza hapa uungane na timu yetu.
Mjomba Kiilu amekasirika na ameifukuza timu kwenye mkahawa wa intaneti. Lakini timu hiyo imefanya kosa gani?
Oh Hapana! Kompyuta zote kwenye mkahawa wa intaneti zimeathiriwa na virusi. Nini kimefanyika? Na watalitatua vipi tatizo hilo?
Zapcom na timu yake wanagundua fursa chungu tele za mawasiliano ya kisasa kila kuchao. Wanajifunza pia jinsi ya kutumia ujuzi huu mpya katika maisha yao ya kila siku – hata katika mkahawa mdogo wa mjomba Kiilu kijijini.
Hufanya nini na simu ya zamani ya mkononi? Hutengenezwa na vifaa gani? Na husababisha athari gani kwa mazingira? Timu yetu inajaribu kujibu maswali haya.
Zapcom na timu yake walionekana kupata mawazo mapya kila mara. Hata hivyo kuna shinikizo kubwa. Ukosefu wa miundombinu hausaidii hali. Je timu hii inakabiliana vipi na hali hii?
Mkahawa mpya wa huduma za intaneti umefunguliwa na unafanya kazi. Lakini kuna changamoto nyingi ambazo marafiki zetu wanajifunza kukabiliana nazo huku biashara ikikua.
Rafiki yetu kijana Zapcom na timu yake wanakaribia kutimiza ndoto yao. Je watafaulu?
Anayetufungulia kipindi hiki ni Zapcom, kijana chipukizi mwenye shauku kutokana na elimu mpya aliyojifunza. Ndoto yake kubwa ni kukiinua kijiji chake. Tuungane naye.
Katika kipindi chetu cha mwisho, babu Peter anatueleza kuhusu enzi mbaya ya historia. Kupitia hadithi zake tumejifunza mengi katika mfululizo wa vipindi hivi. Kwa bahati nzuri, tunaweza kuvikamilisha kwa furaha!
Tangu katikati ya karne ya 20 mataifa yote ya Afrika wamejipatia uhuru. La huzuni ni kwamba baadhi yao yalilazimika kupigana vita vya umwagaji damu kujikomboa, hasa yale yaliyokuwa chini ya utawala wa Wareno. Sawa, babu?
Si siri kwamba eneo kubwa la Afrika lilitawaliwa na makoloni Wazungu. Lakini ilikuwaje babu Peter? Ni kitu gani walichokitaka? Na kuzigawa nchi na watawala wao kulifanyika vipi?
Katika ufalme wa zamani wa Ashanti, msichana kuvunja ungo na kuwa mwanamke lilikuwa tukio kubwa, na kila mtu alialikwa kusherekea kukua kwake! Hiyo ilikuwa mpaka ngoma zilipopigwa kutangaza kuwasili kwa mzungu
Shuleni, baadhi ya wanafunzi hawataki kucheza na Philip tena – kwa sababu ni mzungu. Lakini je anaweza kulaumiwa kwa yale mababu zake waliyoyafanya? Walifanya nini hasa? Na je, maisha yalikuwaje kama mtumwa? Tuulize!