Kijerumani cha biashara kwa wazungumzaji walioendelea: Marktplatz ni somo la Kijerumani linalokufunza jinsi ya kutekeleza biashara zako za kila siku na mambo ya kiafisi.

Maadili ya MashirikaMtindo wa uongozi, mfumo wa nyadhifa, mashirika yanavyojitambulisha: Jinsi makampuni yanavyowasiliana na kujiwasilisha.Mada: Mashirika yanavyojitambulisha, lengo la mashirika, mtindo wa uongozi

Chama cha WafanyibiasharaMashauriano, taarifa, ushawishi: Jinsi uchumi wa Ujerumani unavyojisimamia na kujidhihirisha.Mada: Vyama vya kibiashara na kiuchumi vya Kijerumani

Uchukuzi wa ndani na utaratibu wa usafirishaji BandariniKontena, mifereji, ada za uchukuzi: Vipi na kwanini mizigo husafirishwa kwa kutumia mito na bahari.Mada: Uchukuzi wa ndani

Haki ya kufanya biasharaKugawana kazi, ushirikiano, usimamizi: Jinsi makampuni yanavyojitanua na kuendeleza utaalamu.Mada: Haki ya kufanya biashara, makubaliano ya vibali, maduka mengi

Mabadiliko ya kimuundo katika KilimoMaziwa, nafaka, ruzuku: Jinsi ambavyo sekta ya kilimo ilivyobadilika katika kipindi cha miongo kadha iliyopita.Mada: Kilimo

Viwanda vinavyobadilikaMakaa ya mawe, upungufu wa ajira: Jinsi Bonde la Ruhr nchini Ujerumani linavyoathiriwa na kutoweka kwa viwanda vya kiasili.Mada: Viwanda vya makaa ya mawe na chuma cha pua, ruzuku kwa makaa ya mawe, mabadiliko ya kimuundo

Kukabiliana na Maji-takaVichafuzi, mitambo ya kusafisha maji-taka, kuondoa maji-taka: Jinsi ya kuhifadhi na kuhakikisha usafi wa maji.Mada: Maji-taka, utunzaji mazingira

Kurundikana Kwa TakaTaka, kutumia upya bidhaa, uchumi shirikishi: Jinsi ya kupunguza taka na kulinda mazingira.Mada: Taka, kutumia upya bidhaa, usimamizi wa mazingira, kanuni za kufunga bidhaa.

Changamoto za Kitamaduni – Maonyesho ya Kibiashara mjini Cologne Uwasilishaji, mawasiliano, kuagiza: Jinsi ya kuwasilisha bidhaa kwenye sekta ya biashara.Mada: Maonyesho ya kibiashara

Endelea Kusoma Barua za maombi, mafunzo ya kazi, vyeti: Mambo ambayo wafanyakazi wanaweza kuyafanya kuboresha ujuzi wao.Mada: Uwekevu, mafunzo ya kazi, vyuo vya ufundi

Utumizi wa Mitambo na Kujipanga upyaMakundi ya utoaji bidhaa, uwasilishaji mfululizo, mashine zifanyazo kazi zenyewe/ roboti: Jinsi makampuni yanavyolenga kupunguza wafanyikazi na gharama za kuhifadhi.Mada: Kupunguza utoaji bidhaa, kuagiza bidhaa kutoka kwengine, baraza la wafanyikazi, mafunzo mapya, kufidia, kustaafu mapema, kutumia mitambo, kujipanga upya/ kujirekebisha

Utafiti na MaendeleoUshindani, majaribio, ukubalifu sokoni: Jinsi ya kuasisi bidhaa.Mada: Hataza, utafiti, kuendeleza, uvumbuzi

UuzajiTathmini ya masoko, kundi linalolengwa, sura ya bidhaa: Jinsi ya kufanya bidhaa mpya ionekana ya kuvutia na ifaulu sokoni.Mada. Uuzaji, usambazaji, mauzo, upangaji bidhaa

Matawi ya KigeniMahali, gharama za kazi, viwango vya kimazingira. Sababu za makampuni kuwekeza na kutengenezea bidhaa ng’ambo.Vitega-uchumi vya moja kwa moja, mikataba midogo, tanzu, matawi ya kigeni

Ubia – Kampuni ya KrohneBiashara-nje, upanuzi, ushirikiano: Jinsi makampuni yanavyoshirikiana katika nchi tofauti.Mada: Ushirikiano, kuungana, ubia

Uchukuzi unahitaji mawasiliano mema Gharama za usafirishaji, tofauti za bei, miadi ya kupakua: Jinsi bidhaa zinavyofika zinakopelekwa kote duniani. Mada: Uchukuzi wa kibiashara, jinsi ya kusafirisha, mfumo wa kusafirisha

Uchukuzi wa Kibiashara Wakati wa kuondoka, gharama za upakiaji: Jinsi, mahali na sababu ya bidhaa kusafirishwa. Mada: Uchukuzi wa kibiashara, jinsi ya kusafirisha, mfumo wa usafirishaji

Kufadhili MashirikaGharama, kufungua akaunti, kufilisika: Mahali fedha ya kuanzisha biashara mpya inapopatikana na jinsi inavyoweza kutoa faida.Mada: Deni kwenye akaunti ya benki, kufadhili mashirika, kufilisika, hisa

Kutaka Ushauri Lugha, utamaduni, sheria: Mambo muhimu wakati unapohamia ng’ambo, na mahali ambapo wafanyabiashara wanaweza kupata taarifa. Mada: Kutaka ushauri, bima ya jamii, masoko yanayoibuka, kukodi (kukodisha) kupanga (kupangisha)

Gharama na Mauzo ya njeHatari za uwasilishaji, kupata mkopo, uwezo wa kulipa madeni: Wakati ambapo mteja anashindwa kulipa ilhali mtoaji bidhaa anahitaji kujilinda. Mada: Mauzo ya nje, biashara-nje, mauzo yenye masharti, kukopa mtoaji bidhaa, kupata mkopo

Huduma ya Wateja Mkahawani Huduma, wema, kuelekeza wateja: Je sifa zipi muhimu zaidi kwa kampuni bora ya kutoa huduma? Mada: Kampuni ya kutoa huduma, kuelekeza wateja, mkahawa

Hesabu na Kupanga beiLikizo jumlishi, ziara za makundi, safari zenye vivutio: Jinsi matawi tofauti ya sekta ya utalii yanavyofanya kazi,Mada: Hesabu, ziara za makundi, kupanga bei, likizo jumlishi, Safari zenye vivutio, Sekta ya utalii

Mikataba ya Uuzaji, Dhamana, DhimaJe wateja wana haki na majukumu gani wanaponunua bidhaa fulani?Mada: Mikataba ya Uuzaji, dhamana, dhima, AGB, BGB, TÜV

Kazi ya mikono – Njia ya KujitegemeaMtaji wa kuanzia, mahali, upangaji wa bidhaa: Jinsi ya kupata kampuni.Mada: Mtaji wa kuanzia,mahali, upangaji wa bidhaa

Soko la Samaki – Ushindani wa waziUfanisi wa masoko, mawazo ya kibiashara, kuanzisha biashara: Jinsi ya kuimarisha soko.Mada: Ufanisi wa masoko, mawazo ya kibiashara, kuanzisha biashara

Kioski – Kila Kitu Mahali PamojaMagazeti, peremende, sigara: Jinsi ya kuendesha biashara ndogo ya kifamilia.Mada: Biashara ya Familia, Kioski, Uuzaji-wa jumla jumla