Podcasts about wakati

  • 64PODCASTS
  • 569EPISODES
  • 15mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 29, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about wakati

Show all podcasts related to wakati

Latest podcast episodes about wakati

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala Leo:'Kwa ajili yetu, kupitia sisi': Ombi la wenyeji la kusema ukweli na uhusiano wakati wa Wiki ya Maridhiano

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 29, 2026 11:23


Matukio yanayo ongozwa na jamii yanafanyika kote nchini kuadhimisha Wiki ya Kitaifa ya Maridhiano, ambayo ilianza Mei 27 na ita isha Juni 03.

Habari za UN
21 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 21, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi.Hadi sasa  Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewasili Bunia, mashariki mwa DRC, ndani ya siku nne kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya maabara, PPE na mahema ya kuhudumia wagonjwa. Wakati huo huo MONUSCO inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu njia za kujikinga, huku WHO ikisema zaidi ya watu 600 wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa tangu mlipuko huo kuanza.Tukisalia na Ebola, Ili vifaa vya Ebola vifike kwa wakati, wako mashujaa nyuma ya pazia wanaohakikisha kila mzigo unasafiri salama. Miongoni mwao ni Milton Oloo, mwenye miaka 30 ya uzoefu wa kupakia mizigo JKIA nchini Kenya, ambaye sasa yuko mstari wa mbele kusaidia safari za ndege za Umoja wa Mataifa, UNHAS. “Tunachokifanya hapa leo ni kuhakikisha kwamba mizigo inayoelekea Congo DRC imepangwa vizuri na kupakiwa ipasavyo ili isiharibike. Pia naona fahari na Maisha ya watu yanayookolewa  nafurahi”.Na jukwaa la 13 la miji dunini WUF13 linaelekea ukingoni Baku Azerbaijan likijadili changamoto ya makazi duniani, Rehema Kishoa kutoka Tanzania Mkurugenzi Msaidizi wa Uzingatiaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi anasema wao wamechukua hatua kukabili changamoto hiyo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Radio Maria Tanzania
Kwanini Yesu alilala wakati wa dhoruba?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 29:17


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani . Mwezeshaji ni Frateri Noah Joshua Mwamfupe, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Kwanini Yesu alilala wakati wa dhoruba? Tarehe 08 Machi 2026   L'articolo Kwanini Yesu alilala wakati wa dhoruba? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je sahihi kwa katekista kuvaa Saplisi wakati wa ibada?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 23:10


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Barnabas Mushi, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Je sahihi kwa katekista kuvaa Saplisi wakati wa ibada? Pia naomba kujua maana ya kila vazi linalovaliwa wakati wa adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu. Tarehe 29 Machi 2026 L'articolo Je sahihi kwa katekista kuvaa Saplisi wakati wa ibada? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Kwanini katika misiba ya Mapadre pamoja na Maaskofu wanavaa mavazi meupe  na wakati wa misiba ya walei wanavaa zambarau?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 27:16


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Godfrey Msaki, kutoka Parokia ya Mtakatifu Gabriel Malaika Mkuu – Mbagala, Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Swali ni Kwanini katika misiba ya Mapadre pamoja na Maaskofu wanavaa mavazi meupe  na wakati wa misiba ya walei wanavaa zambarau? Tarehe 24 Machi 2026 L'articolo Kwanini katika misiba ya Mapadre pamoja na Maaskofu wanavaa mavazi meupe  na wakati wa misiba ya walei wanavaa zambarau? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Kwanini Yesu alimkubalia Dismasi kuawatakua pamoja mbinguni kabla hajamuondolea dhambi wakati yeye ni mdhambi?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 25:20


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Kostantine Haruna, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Yesu alipokua Msalabani alimwambia Dismasi leo tutakua pamoja peponi nahi nibaada yakumwomba aingie pepo je hii siyo rushwa na kwanini alimkubalia kabla hajamuondolea dhambi wakati yeye ni mdhambi? Tarehe 20 […] L'articolo Kwanini Yesu alimkubalia Dismasi kuawatakua pamoja mbinguni kabla hajamuondolea dhambi wakati yeye ni mdhambi? proviene da Radio Maria.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Watu 518 walifariki Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzi, mapigano bado yanaendelea DRC

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Apr 25, 2026 20:11


Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita.  Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa 14 alikamilisha ziara ya siku kumi barani Afrika juma hili; na katika mzozo wa Mashariki ya kati, Marekani yaongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran, hatua sawa ikichukuliwa kati ya Israeli na Lebanon.

israel iran kenya israelis uganda lebanon congo tanzania afrika burundi drc kinshasa watu wakati jamhuri marekani oktoba kiongozi mashariki uchaguzi kidemokrasia tunaangazia
Habari za UN
21 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 21, 2026 11:32


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mmoja wa walioshiriki mkutano wa CSW70, Masidis Scholastica Madowo Mbunge katika Bunge la Kaunti ya Siaya akiwakilisha kata ya South East Alego jimbo la Magharibi mwa Kenya, ili kuangazia kile anachokifanya kwenye Kaunti yake kuhakikisha wanawake wanapata haki hizo.Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kutafanyika mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja huo ambapo wagombea wanne wamejitokeza kuwania wawili wanaume na wawili wanawake. Wagombea hao ni Michelle Bachelet kutoka nchini Chile, Rafael Grossi kutoka nchini Argentina, Rebeca Grynspan kutoka Costa Rica, na Macky Sall kutoka nchini Senegal.Wakati huo huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amesema mchakato wa kumchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu itakayoamua mwelekeo wa taasisi hiyo na mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kabla ya kuanza kwa mdahalo huo wa wazi, Baerbock ameeleza kuwa uchaguzi huo una umuhimu mkubwa duniani kote, ukigusa maisha ya zaidi ya watu bilioni nane, “Uamuzi huu si wa kiutawala tu, bali ni ujumbe kuhusu maadili na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo.”Takribani wahamiaji 8,000 waliripotiwa kufariki dunia au kutoweka duniani kote mwaka 2025, na kufanya jumla ya wahamiaji waliopoteza maisha tangu 2014 kufikia zaidi ya watu 82,000, hii imebainishwa katika takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Takwimu hizo pia zinaonesha athari kubwa kwa familia, ambapo takribani watu 340,000 wameathirika moja kwa moja. IOM imeonya kuwa njia za uhamiaji si salama na zinazidi kuwa hatari.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA" Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
16 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
15 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 15, 2026 11:11


Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za Umoja wa Mataifa za kutafuta suluhu ya vita nchini Sudan pamoja na simulizi za wakimbizi ikiwa leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini humo, na miundombinu na ujenzi wenye mnepo nchini Tanzania.Wakati vita nchini Sudan ikiingia mwaka wa nne tangu kuvuka kwa mapigano baina ya jeshi la Sudan na kikosi vya msaada wa haraka RSF, hii leo huko Berlin nchini Ujerumani unafanyika mkutano wa Kimataifa ukilenga kurejesha mgogoro wa Sudan katika ajenda ya juu ya kidiplomasia duniani.Leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini Sudan 15 Aprili 2023, mgogoro ambao umegeuka kuwa moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Mamilioni ya watu wamekwama katikati ya mapigano, kuwa wakimbizi wa ndani na nje, njaa na ukosefu wa makazi, huku mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yakionya kuwa mateso yanaendelea kuongezeka kila uchao.Katika kuunga mkono lengo namba 9 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kuhusu miundombinu na ujenzi wenye mnepo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania, limeingia makubaliano ya kimkakati na Taasisi ya wanawake wasanifu Majenzi, TAWAH, kwa ajili ya kuboresha sekta ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

berlin tanzania sudan sdgs undp rsf umoja hii katika wakati wanawake mataifa aprili maendeleo shirika kimataifa ujerumani
Habari za UN
Wanadiplomasia wanakutana kusaka suluhu ya vita Sudan ikiingia mwaka wa 4

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 15, 2026 3:00


Wakati vita nchini Sudan ikiingia mwaka wa nne tangu kuvuka kwa mapigano baina ya jeshi la Sudan na kikosi vya msaada wa haraka RSF, hii leo huko Berlin nchini Ujerumani unafanyika mkutano wa Kimataifa ukilenga kurejesha mgogoro wa Sudan katika ajenda ya juu ya kidiplomasia duniani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mush

berlin sudan msf rsf wakati mwaka kimataifa ujerumani kusaka
Habari za UN
13 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 13, 2026 11:37


Hii leo jaridani tunaangazia mlango Bahari wa Hormuz, mafuriko na ukarabati wa miundombinu huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, na juhudi za FAO nchini Tanzania za kuwapatia mafunzo jamii kuhusu lishe bora.Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani.Kufuatia mafuriko makubwa yanayoendelea kuharibu miundombinu na kukwamisha ulinzi wa amani huko  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS unaendelea kujitahidi kukarabati miundombinu kama njia mojawapo ya kuongeza ustahimilivu na kuchochea amani.Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), maafisa ugani wa kilimo, wataalamu wa lishe na afya mkoani Kigoma waliungana kuandaa tukio la Siku ya Afya na Lishe Mitaani au SALIMI sambamba na Siku ya Shamba la Mkulima ili kuwapatia wakulima na wanajamii elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji na matumizi ya mazao yenye lishe.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

iran tanzania hormuz fao umoja hii bahari siku afya pamoja wakati mataifa aprili unmiss marekani shirika mashariki sudan kusini
Habari za UN
Kuvurugika kwa meli kupita mlango bahari wa Hormuz kunazua wasiwasi kuhusu bei za chakula na minyororo ya usambazaji duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 13, 2026 3:25


Wakati mazungumzo ya kumaliza vita huko Mashariki ya Kati baina ya Marekani na Iran yakigonga mwamba mwishoni mwa wiki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limeonya kuwa kuvurugika kwa meli kupita katika mlango Bahari wa Hormuz kunaleta hatari zinazoongezeka si tu kwenye nishati bali pia katika mifumo ya chakula duniani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

Habari za UN
09 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 9, 2026 9:58


Jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa CSW70 akieleza ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya Lebanon tarehe 8 Aprili, mashambulizi ambayo yamesababisha mamia ya raia kuuawa na kujeruhiwa, wakiwemo watoto, sambamba na kuharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya kiraia. Taarifa iliyotolewa New York, Marekani na Msemaji wa Umoja wa Mataifa inamnukuu Guterres akionesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la vifo miongoni mwa raia na kutoa pole kwa watu na Serikali ya Lebanon, akiwatakia nafuu ya haraka wale waliojeruhiwa.Katika tukio jingine hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezindua Mfuko wa Urejeshaji wa Palestina uliopewa jina la Horizon Fund, akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kusaidia wananchi wa Palestina kurejesha maisha yao na kujenga mustakabali bora. Akizungumza kupitia ujumbe wa video wakati wa uzinduzi uliofanyika Ramallah, huko Ukingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, Guterres amesema mfuko huo ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Taifa la Palestina.Wakati mgogoro wa Sudan ukikaribia kutimiza miaka mitatu, zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Sudan walioko nchini Chad wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupunguzwa kwa msaada muhimu wa kibinadamu. Onyo hilo limetolewa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa ambayo ni lile la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) pamoja na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wakitanabaisha kuwa huduma za msingi kama chakula, maji, malazi, ulinzi na huduma za afya zitalazimika kupunguzwa zaidi katika miezi ijayo iwapo pengo la ufadhili la dola milioni 428 halitazibwa haraka.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
Huduma za afya ziko ukingoni kuporomoka kabisa huko Gaza kuliko wakati mwingine wowote

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 8, 2026 2:50


Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Hatari ya barabarani wakati wa Pasaka ya zua wito wa kuteuliwa kwa waziri wa usalama

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 7, 2026 12:35


Serikali inasema mahitaji ya mafuta yaliongezeka kwa theluthi moja wakati wa mapumziko ya Pasaka.

hatari habari wakati pasaka waziri serikali
Habari za UN
02 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 2, 2026 11:45


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kupata ujumbe wa Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana amabye kwa kuwa mwaka huu 2026 ameshiriki tena katika  mkutano wa CSW70 anatueleza ni kwa kiasi gani wameweza kulitekeleza malengo ya mikutano haya katika nchini humo.Vita Mashariki ya Kati vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia mwezi wa pili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hapa makao makuu ya UN jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari akisisitiza sio tu vita hivyo vikome bali pia anaendeleza diplomasia za kusaka suluhu. Guterres amesema, Ninamtuma Mjumbe wangu Maalum Jean Arnault. Lengo ni kuunga mkono jitihada za kikanda. Lazima tupate njia ya amani ya kutoka katika hali hii. Ujumbe wangu uko wazi. Kwa Marekani na Israeli, ni wakati muafaka kusitisha vita vinavyosababisha mateso makubwa ya kibinadamu na tayari vinaanzisha athari mbaya za kiuchumi. Kwa Iran, isitishe kushambulia majirani zake.. Ripoti mpya ya Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika, (ECA)  imependekeza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa deni la umma barani Afrika, ikionya kwamba uendelevu hautegemei tu kiwango cha kukopa bali pia ubora wa taasisi, mifumo ya kisheria, na uwazi. Ikitolewa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, ripoti hiyo inataja udhaifu kama vile uwezo mdogo wa kufanya uchambuzi wa hatari, na ushawishi wa mashinikizo ya kisiasa katika maamuzi ya kukopa ikisema kuwa kuboresha usimamizi ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa deni la umma linachangia ukuaji wa uchumi endelevu badala ya kuwa chanzo cha kuyumba kifedha.Wakati dunia hii leo ikiadhimisha Siku ya Uelewa wa Usonji, familia katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli,  zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka katika kuwahudumia watoto usonji katikati ya mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu. Katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Jiji la Gaza, Layan Abu Qousa mwenye umri wa miaka 16, ambaye ana usonji, anaishi na familia yake katika magofu ya nyumba yao. Familia yake inasema hali ngumu ya maisha imeongeza changamoto zinazohusiana na hali yake, huku ukosefu wa utulivu na mkwamo wa kupata huduma za kitaalamu ukiendelea kudhoofisha ustawi wake.Na katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari RFI-Ki
Kombe la Dunia : Hofu ya dhuluma za wakati wa kombe la dunia

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 10:00


Ripoti ya shirika la Amnesty Interenational imeonya kuwa Kombe la Dunia la mwaka huu linaweza kuchangia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dunaini kutokana mpango wa mataifa wenyeji kuweka mikakati kali za uhamiaji na ufuatiliaji wa karibu wa mashabiki wa kigeni   Je, unahisi mashabiki kutoka Afrika Mashariki watakuwa salama kushabikia timu zao kule Merekani,Mexico na Canada? Skiza maoni ya waskilizaji.

canada mexico dunia eac wakati afrika mashariki kombe ripoti
Habari RFI-Ki
Kombe la Dunia : Hofu ya dhuluma za wakati wa kombe la dunia

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 10:00


Ripoti ya shirika la Amnesty Interenational imeonya kuwa Kombe la Dunia la mwaka huu linaweza kuchangia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dunaini kutokana mpango wa mataifa wenyeji kuweka mikakati kali za uhamiaji na ufuatiliaji wa karibu wa mashabiki wa kigeni   Je, unahisi mashabiki kutoka Afrika Mashariki watakuwa salama kushabikia timu zao kule Merekani,Mexico na Canada? Skiza maoni ya waskilizaji.

canada mexico dunia eac wakati afrika mashariki kombe ripoti
Habari za UN
30 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 30, 2026 11:29


Hii leo jaridani tunaangazia migogoro yanayoendelea Mashariki ya Kati, ujumbe wa Katibu Mkuu leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, na kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa Isiolo nchini Kenya.Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospital.Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kila mtu kujifunza upya yamna ya kufanya manunuzi ya vitu na mapishi ambayo hayatasababisha umwagaji wa chakula ili kunusuru mifumo ya ikolojia na afya ya binadamu.Nchini Kenya katika kaunti za Isiolo, Garissa, Samburu na Mto Tana, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeendesha kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa, sambamba na kupatia wananchi fedha taslimu bila masharti kama mojawapo ya kujengea jamii mnepo wakati wa ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Kuwa na orodha ya manunuzi kutasaidia kupunguza utupaji wa chakula

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 30, 2026 2:53


Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kila mtu kujifunza upya yamna ya kufanya manunuzi ya vitu na mapishi ambayo hayatasababisha umwagaji wa chakula ili kunusuru mifumo ya ikolojia na afya ya binadamu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 

taka umoja kuwa wakati mataifa kimataifa mazingira
SBS Swahili - SBS Swahili
SBS Learn Eng Ep 70 Jinsi yakufanya mazungumzo wakati wa BBQ

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 30, 2026 11:40


Je, unajua jinsi ya kufanya mazungumzo wakati wa BBQ?

Habari za UN
Makpandu: Hofu yatanda kwa wakimbizi wa Sudan walio kambini Makpandu Sudan Kusini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 27, 2026 2:38


Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS.Kwa muda mrefu kambi ya wakimbizi ya Makpandu imeonekana kuwa kimbilio, lakini sasa imegeuka kuwa eneo la mashaka, na hofu. Bekia Mahadi Ali, mama wa watoto wanane aliyekimbia vita nchini Sudan akitarajia kupata hifadhi, sasa amejikuta akiishi kwa wasiwasi mkubwa baada ya ghasia kuibuka upya katika eneo hili. Furaha ya kupata usalama imetoweka, ulinzi umepungua, Bekia anahofia maisha yake na ya familia yake."Hakuna usalama kabisa hapa kambini na tunaogopa, nilikimbia na wanangu bila baba yao. Watoto hawa ni jukumu langu, tulikuja hapa kutafuta kimbilio lakini hawawezi kwenda shule, sina cha kufanya. Ninachoomba tuhamishwe kutoka kambi hii,”Wakimbizi katika kambi ya Makpandu wanaripoti kuwa watu wenye silaha huingia ndani ya kambi mara kwa mara, wakifyatua risasi hovyo, kuwatishia watu, na kupora au kuchoma moto mali za raia. Omar Ibrahim, ni mkimbizi mwingine kutoka Sudan, anafunguka."Wakati mwingine tunawachukua wanawake na watoto wetu kwenda kulala vichakani kwa sababu hakuna uhakika wa usalama ndani ya kambi. Hatuwezi hata kwenda shambani kulima. Tunaiomba Serikali na Umoja wa Mataifa waingilie kati, tulikimbia risasi nchini Sudan, lakini tumekutana na risasi zilezile tena hapa."Kufuatia shambulio la hivi karibuni lililosababisha kifo cha mkimbizi mmoja wa Sudan, kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kimefanya doria katika kambi hiyo ya Makpandu ili kutathmini hali ya usalama. Thomas Bazawi, ni Afisa wa Ulinzi, Mpito na Urejeshwaji wa UNMISS, anafafnua jukumu lao.“Jukumu letu ni kusaidia kurejesha imani kwa kushirikiana na jamii, mamlaka za mitaa, vikosi vya usalama na wengineo. Tunafanya kazi na wadau wote kuimarisha usalama ili watu waweze kujiamini na kuendeleza maisha yao tena.”Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa uwekezaji katika amani kupitia mpango wa Hatua kwa Ajili ya Kulinda Amani (A4P) ni muhimu kwa usalama wa wakimbizi wanaokimbia migogoro ya silaha.

sudan hakuna umoja kwa watoto wakati hatua mataifa unmiss ujumbe sudan kusini
Wimbi la Siasa
DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Mar 25, 2026 10:09


Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 

congo drc bunge drcongo felix tshisekedi wakati spika jamhuri katiba kidemokrasia udps
Habari za UN
Madhara ya vita vya Israeli/Marekani dhidi ya Iran yazidi kudhihirika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 23, 2026 3:15


Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiingia wiki ya nne tangu uanze tarehe 28 mwezi uliopita wa Februari, Umoja wa Mataifa leo umeonya kuwa athari mbaya za kibinadamu na uchumi wa kimataifa zinaongezeka wakati mzozo huo ukivuruga kabisa njia muhimu za usambazaji wa bidhaa ndani ya Mashariki ya Kati na kwingineko duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi.Asante Assumpta. Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati sasa umevuka mipaka ya eneo hilo, ukiathiri pia Asia na Afrika, hasa katika biashara na usafirishaji.Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Miradi na Huduma, UNOPS inaonya kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kutokana na athari za kibinadamu na kiuchumi. Mkuu wa shirika hilo, Jorge Moreira da Silva, amesema kuvurugika kwa usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz kumesababisha mshtuko mkubwa wa kiuchumi duniani.Amesema “Nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika zina uwezekano mkubwa wa kubeba gharama kubwa zaidi hali inayotishia usalama wa chakula,” na kuongeza kuwa njaa duniani inaweza kuongezeka kwa makumi ya mamilioni ya watu.Pia amesema mgogoro huu unazidisha hali mbaya iliyopo katika nchi kama Sudan, Sudan Kusini, Afghanistan, Yemen, na Somalia, ambapo mifumo ya chakula tayari ni dhaifuAmeonya pia kuwa mashambulizi dhidi ya meli na kuvunjika kwa minyororo ya usambazaji kunazuia upatikanaji wa dawa na misaada, hasa Gaza, huku vita vikienea vinaweza pia kuhatarisha fedha zinazotumwa nyumbani kwa familia, hasa Asia Kusini.Nchini Lebanon, kwa mujibu wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, zaidi ya watu 1,000 wameuawa na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, wakiwemo wahudumu wa afya, wanahabari na wafanyakazi wa misaada.Watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Naibu Mkurugenzi wa UNICEF, Ted Chaiban, anasema “Watoto wanaouawa au kujeruhiwa ni sawa na darasa moja kila siku.”UNICEF inaonya pia juu ya athari kubwa za kisaikolojia kwa watoto na wahudumu wa misaada.Katika Ukanda wa Gaza, hali inazidi kuwa mbaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestna UNRWA,  limesema  mamia ya watu wamepata ulemavu wa kudumu huku huduma za afya na misaada zikizidi kuwa finyu.Wakati huo huo, hofu ya usalama wa nyuklia inaongezeka kufuatia mashambulizi karibu kweny vituo nyeti nchini Iran na Israel. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA,  Rafael Grossi, ameonya kuwa: “Hakuna hatua ya kijeshi inayopaswa kuhatarisha usalama wa vituo vya nyuklia.”Ingawa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa a Afya Duniani WHO,  tayari linaanza maandalizi ya dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa bila hatua za haraka za kupunguza mzozo, dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu na kiuchumi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: SES NSW yapokea simu 450 zakuomba msaada wakati wa mafuriko magharibi mwa Sydney

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 27, 2026 14:05


Mvua kubwa imesababisha mafuriko ya ghafla katika sehemu za Sydney usiku kucha wa Alhamisi hadi Ijumaa, wafanyakazi wakujitolea wa S-E-S wakitoa huduma za uokoaji 44 za maji ya haraka.

simu habari wakati magharibi alhamisi
Habari za UN
Wakazi katika ukanda wa Gaza wahaha kumudu mlo wakati wa mfungo wa Ramadhani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 18, 2026 2:54


Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kipindi kinachoambatana na sio tu ibada bali pia mlo kama vile futari na daku. Hata hivyo kwa wakazi wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na kimabavu na Israeli hali si hali kwani mlo na mengine yanayoambatana na kipindi hiki vinasalia kuwa ndoto. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo:Maelfu wanadai fidia baada ya Huduma za Australia kutumia sheria za msaada wa watoto visivyo

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 29, 2026 7:30


Ripoti muhimu imefichua kuwa Service Australia ilikwepa kwa makusudi sheria za malezi ya watoto kwa muda wa miaka sita, ikiwa imezuia ndani kwa ndani malipo kwa zaidi ya wazazi 16,000 ambao walitoa chini ya asilimia 35 ya huduma kwa watoto wao. Wakati shirika hilo lilipinga kuwa sheria ilileta "matokeo yasiyotarajiwa" kwa kuulazimisha walezi wakuu kulipa wale wenye majukumu kidogo ya huduma, Ombudsman aliamua kwamba kupuuza sheria si chaguo kwa watumishi wa umma.

Habari za UN
23 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 23, 2026 11:40


Hii leo jaridani tunaangazia miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, AI katika elimu na juhudi za kuhakikisha wananchi wamepata huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi nchini Niger.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hii leo historia na dharura vilikutana chini ya paa moja. Ni miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC lifanye kikao chake cha kwanza tarehe 23 Januari 1946 na linaadhimisha hatua hii muhimu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni wa maamuzi kwa mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa.Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
UNESCO yataja dhana potofu, na hatari ya kutumia AI mashuleni

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 23, 2026 3:09


Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Habari za UN
07 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 7, 2026 11:50


Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa haki za binadamu na uchaguzi mkuu nchini Uganda, juhudi za Rwanda za kutokomeza Saratani ya shingo ya kizazi, na mafunzo kwa ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au kinengunengu yaliyoendeshwa Kigoma Tanzania.Wakati nchi ya Uganda ikijiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu wa Januari, wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa ikionya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Uganda si rafiki kwa uchaguzi wa amani.Saratani ya shingo ya kizazi ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi zaidi nchini Rwanda kwani takribani kila mwaka kati ya wagonjwa wapya 1230, 830 hufariki dunia. Ili kupunguza mzigo wa ugonjwa huu na kuokoa maisha, mwaka 2020 Rwanda ilianzisha mkakati wa kitaifa unaoendana na lengo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) la kuondoa saratani ya shingo ya kizazi ifikapo 2030.Mafunzo kwa vitendo ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au Kinengunengu yaliyoendeshwa mkoani Kigoma kaskazini-magharibi mwa Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, nchini huko yameendelea kusambaa na sasa  yamebisha hodi kwenye viunga vya mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam kwa lengo la kusaidia wafugaji kujiongezea kipato badala ya kupoteza vifaranga kwa vifo au kuliwa na kunguru.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

dar uganda rwanda tanzania fao umoja ili hii afya wakati mataifa shirika uchaguzi mkuu ufugaji
Habari za UN
Uchaguzi nchini Uganda hauwezi kuwa huru bila kulindwa kwa Haki za Binadamu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 7, 2026 3:19


Wakati nchi ya Uganda ikijiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu wa Januari, wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa ikionya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Uganda si rafiki kwa uchaguzi wa amani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

uganda bila umoja haki kuwa wakati mataifa uchaguzi uchaguzi mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo:China yaongeza ushuru kwa bidhaa za nyama ya ng'ombe

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 5:56


Biashara ya nyama ya ng'ombe ya dola bilioni ya Australia inakabiliwa na mabadiliko makubwa kutokana na hatua ya China kuweka ushuru wa asilimia Hamsini na tano kwa uingizaji wa bidhaa zinazozidi vikomo vya kila mwaka vilivyowekwa kwa ukali. Wakati serikali ya China inadai kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakulima wake dhidi ya usambazaji usiokuwa na kipimo, viongozi wa sekta ya Australia na Upinzani Mkuu wanatoa onyo kuwa nyongeza hii ya ushuru inakiuka makubaliano ya biashara huru baina ya Australia na Chini ya muda mrefu.

Habari za UN
02 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 2, 2025 12:39


Hii leo jaridani tukiendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu siku 16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, leo tunaelekea Mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusikia hisia za wanawake kuhusu ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.Watu takribani 100,000 wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR likionya kuwa mashambulizi yanaongezeka na kuyakumba hata maeneo yaliyokuwa salama. Mwakilishi wa UNHCR, Xavier Creach, amesema mgogoro “unazidi kuzorota kwa kasi ya kutisha” huku familia zikikimbia usiku gizani wakati watu wenye silaha wakivamia vijiji vyao. UNHCR inasema linahitaji dola milioni 38.2 kukidhi mahitaji yanayoongezeka.Kaskazini mwa Asia, dhoruba za kitropiki na mvua zisizo za kawaida zimesababisha vifo vya mamia na watu wengi kukimbia makazi yao, imesema WMO. Clare Nullis, msemaji wa shirika hilo, alisema Indonesia, Ufilipino, Sri Lanka, Thailand na Vietnam ndizo zimeathirika zaidi. “Tunahitaji kuzingatia kuwa Asia iko hatarini sana kutokana na mafuriko,” amesema Nullis, akibainisha kuwa dhoruba karibu na Ekweta ni nadra na jamii hazina uzoefu wa kukabiliana nazo. Indonesia pekee, watu 604 wamefariki, 464 hawajulikani walipo, na 2,600 wamejeruhiwa, huku zaidi ya milioni 1.5 wakiathirika na 570,000 wakikimbia makazi yao.Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumwa leo Desemba      2 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani ILO limeonya kuhusu kuongezeka kwa utumwa wa kisasa wa binadamu, likionesha kuwa watu milioni 10 zaidi walikuwa wakiishi katika kazi za kulazimisha au ndoa za shuruti mwaka 2021 ikilinganishwa na mwaka 2016. Makadirio haya mapya yanaweka idadi ya walioathirika duniani kote kuwa watu milioni 50 huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wenye hatari kubwa zaidi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Australia yafafanuliwa;bei za upangaji zinaendelea kupanda wakati gharama ya maisha inaongezeka.

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Dec 1, 2025 6:12


Licha ya viwango vya riba kutulia, stress ya kodi bado haijabadilika kote Australia. Katika miji mingi mikubwa, kaya bado zinatoa karibu theluthi moja ya mapato yao ili kuweka paa juu ya vichwa vyao. Na mara nyingine tena, Perth inashika nafasi mbaya zaidi. Jiji kuu lisilopatikana kwa urahisi zaidi nchini limeporomoka hata zaidi — likirekodi kushuka kwa asilimia nne zaidi katika uwezo wa kumudu gharama juu ya rekodi ya chini ya mwaka uliopita.

SBS Swahili - SBS Swahili
Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kuanzia desemba

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 11, 2025 6:40


Mtandao wa Reddit na jukwaa la Kick zitaongezwa kwenye majukwaa yanayohitajika kuzuia watumiaji walio na umri chini ya miaka 16, sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa mwezi Desemba. Marufuku ya Australia ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16, ambayo inajumuisha majukwaa nane kuu, inategemea tathmini zinazoendelea za eSafety ambazo zinaweza kufafanua kati ya huduma za mitandao ya kijamii, ujumbe, na michezo, kuelezea ni kwanini majukwaa kama Steam na Twitch hayakujumuishwa. Wakati serikali ilihakikishiwa na Roblox kwamba wataanzisha teknolojia za kuthibitisha umri ili kupunguza tabia za uwindaji wa watoto, watetezi wa haki za kidigitali wanatahadharisha kwamba marufuku haya yanaweza kuhamasisha watoto kutumia majukwaa madogo yasiyo na uangalizi ambapo wanaweza kukumbana na madhara makubwa zaidi.

Habari za UN
Akiwa Doha, Rais wa Baraza Kuu aona watoto wa kipalestina walivyo na matumaini licha ya zahma walizopita

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2025 4:06


Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock ametembelea wakimbizi wa kipalestina huko Doha nchini Qatar kuwajulia hali na kujionea maisha yao baada ya kuondolewa wakati wa vita kali huko Ukanda wa Gaza eneo la wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel na kuletwa nchini Qatar kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Leah Mushi anatupa taswira ya ziara yake hiyo.Wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar nchi hiyo ilitenga eneo maalum na kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya makazi kwa wale walioenda kutazama mechi za kombe la Dunia, eneo hilo pia lilikuwa na kiwanja cha mpira, eneo hilo ni Al-Thumama maarufu kama Al-Thumama complex katika mji wa Doha.Mtoto na simulizi kupitia pichaEneo hilo sasa limegeuzwa makazi ya dharura kwa zaidi ya wakimbizi 1,700 wa Kipalestina ambao waliondolewa nchini mwao wakati wa vita Kali kati ya majeshi ya Israel na wanamgambo wa Hamas vita ambayo imesitishwa hivi sasa. Wakimbizi hao wa kipalestina wakiwa katika eneo la Al-Thumama wanapatiwa matibabu ya kawaida, ya viungo na usaidizi wa kijamii.Rais wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amefika katika eneo hilo ili kuwajulia hali.Kwanza alikutana na watoto, video inamuonesha akizungumza na mtoto wa kiume ambaye ameandika kitabu kwa njia ya picha na ndoto yake ni kitafsiriwe kutoka kiarabu kwenda lugha mbalimbali. toto huyo akatia saini nakala ya kitabu chake na kumpa Rais wa Baraza Kuu.Watoto licha ya majeraha bado wana matumainiKisha, Rais Baerbock anaonekana akizungumza na familia nyingine, pembeni mtoto mmoja mwenye umri kama wa miaka mwili hivi mkono wake wa kulia unaonekana umekatwa chini kidogo ya bega. Mtoto huyo anarukaruka kwenye kochi huku wanafamilia yake wakizungumza na mgeni.Anatoka akitembea kwenda eneo jingine lakini ndani ya eneo hilo hilo la Al-Thumama kwenye chuo cha ufundi stadi na kujionea namna wanawake wanavyojishughulisha na kazi za mikono ikiwemo ufumaji kwa kutumia mashine za kisasa za mkono.Akitoka huko akiwa na wanawake kadhaa akawa anaelekea eneo lenye hospitali … njiani akakutana na mwanamke akiwa kwenye kiti mwendo, wakasimama na mwanamke huyo akawapa vitafunywa wakala na kufurahia huku Rais wa Baraza Kuu akisifu kwa utamu wa vitafunio hivyo.Baada ya hapo safari ya kwenda hospitali ikaendelea, na huko akakutana na madaktari na kujionea mashine mbalimbali za kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina.Ziara hiyo aliyoianza tangu mchana kweupe alihitimisha giza likiwa limeshatanda nje na akatoa ujumbe kwa dunia kile alichojionea.Amesema, “nimeona yale hawa watoto walipitia, nyuso zao ziliungua kwa moto, wamepoteza mikono, wazazi, familia nzima, lakini bado wanaonesha ujasiri na wanamatumaini na maisha yao ya baadae, wakijaribu kurejea shuleni na hii inaweka mkazo wa jukumu letu ni lipi kama jumuiya ya kimataifa. Tunapaswa kukomesha kabisa mgogoro huu uliodumu kwa muongo mmoja, mzozo wa muda mrefu na kwamba amani ya kudumu haita hakikishwa kwa kupitia vita, ugaidi wala kukalia eneo kimabavu bali kwa makubaliano ya amani ya kuwa na mataifa mawili yanayojitegemea, kupelekea kwa taifa huru la Kipalestina ambapo kizazi kijacho kinaweza kuishi kwa heshima pia.”

Habari za UN
Hali si hali huko El Fasher nchini Sudan, watoto 'walipa gharama' zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 29, 2025 2:43


Ghasia zinazoendelea kwa kasi zinawakwamisha zaidi watoto katikati ya mashambulizi ya mabomu yasiyokoma, mapigano makali, na uhaba mkubwa wa chakula, maji salama na dawa kwa zaidi ya siku 500 sasa.“Hakuna mtoto aliye salama,” anasema Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kupitia taarifa iliyotolewa na makao makuu ya shirika hilo jijini New York, Marekani leo.Taarifa hiyo pia inamnukuu Catherine Russell akisema, “ingawa athari kamili bado haijulikani kutokana na kukatika kwa mawasiliano kote nchini Sudan, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 130,000 huko Al Fasher wako katika hatari kubwa ya kukiukwa haki zao, huku kukiripotiwa visa vya utekaji nyara, mauaji na ukataji viungo vya mwili, pamoja na ukatili wa kingono.”Pia kuna taarifa za wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu kukamatwa au kuuawa.UNICEF inatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano, kuhakikisha upatikanaji salama na usiokatizwa wa misaada ya kibinadamu, ulinzi wa raia hasa watoto, na kupatiwa uhakika wa njia salama kwa familia zinazotafuta hifadhi, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Wale wanaohusika na ukiukaji lazima wawajibishwe.Wakati huohuo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limethibitisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewataarifu kuwa viongozi  wawili wa juu wa WFP nchini  wametangazwa kuwa watu wasiotakiwa nchini Sudan na hivyo wameamriwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, bila maelezo yoyote.WFP inaeleza kwamba uamuzi huu wa kuwafukuza Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan na Mratibu wa Dharura wa WFP nchini humo unakuja katika kipindi muhimu kwani mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan hayajawahi kuwa makubwa zaidi kama kipindi hiki, huku zaidi ya watu milioni 24 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na jamii zikikumbwa na baa la njaa.Wakati ambapo WFP na washirika wake wanapaswa kupanua wigo wa msaada, uamuzi huu unalazimisha shirika kubadilisha uongozi bila mpango, jambo linalohatarisha shughuli zinazowaunga mkono mamilioni ya Wasudani walio hatarini kukumbwa na njaa kali, utapiamlo, na hata kifo kutokana na njaa.WFP na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kuzungumza na mamlaka za Sudan kupinga hatua hii na kutaka ufafanuzi wa uamuzi huo.Tags: Sudan, El Fasher, WFP, UNICEF

Habari za UN
Mwanaharakati Dkt.Owusu: Ni wakati wa sauti zetu vijana zisikilizwe kwa vitendo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 26, 2025 2:10


Katika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana wa Uingereza na Ghana, Dkt. Khadija Owusu ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili.Owusu, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Akaya inayowakilisha wasichana wa zama hizi, anasema vijana hawapaswi kuzungumziwa tu, bali wajumuishwe moja kwa moja katika kuandaa Suluhu za changamoto zinazoihusu dunia wakiwemo na wao "Mara nyingi tunazungumza kuwa tunataka ushiriki zaidi wa vijana wakati umefika wa kuacha kuzungumza tu kuhusu kuhitaji vijana wengi, bali tuwe na vijana wengi."Niko hapa kuwakilisha maelfu ya wasichanaAnasema ushiriki wake katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa vijana si wa kibinafsi tu, bali unaakisi sauti za wasichana na vijana wengi wanaosaidiwa na taasisi yake ya Akaya."Niko hapa kuwakilisha si mimi peke yangu, si Uingereza tu, na si Ghana tu, bali Taasisi ya Akaya, na wasichana na vijana wengi tunaowahudumia nchini kote."Owusu anaamini vijana wa Kiafrika, hususan wasichana, wanapaswa kupata nafasi kubwa zaidi katika jmaukwaa ya kimataifa kama Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kupaza sauti zao."Bado tunahitaji kuona vijana zaidi kama sisi kwenye vyumba vya mikutano, Waafrika zaidi, vijana zaidi wa Kiafrika na wasichana wa Kiafrika kwenye vyumba vya mijadala, wakishiriki majadiliano kwa sababu tunaleta mabadiliko halisi."Owusu anasema ujumbe wake kwa vijana barani Afrika ni kubeba vipaji vyao, wajiamini, na kuendeleza ndoto zao kwani kila kitu kinawezekana. 

new york ghana afrika owusu umoja kiswahili sauti wakati vijana dkt mataifa vitendo uingereza miongoni
Habari za UN
25 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 25, 2025 11:20


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani  ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi' chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.”Kando ya hotuba za viongozi, kunafanyika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa Programu ya Dunia kwa ajili ya vijana. Je vijana kutoka Malawi wana ujumbe gani? Mwakilishi wao kwenye mkutano huu Rachel Mganga Wanangwa anasema, “Ujumbe kutoka vijana wa Malawi ni wekezeni kwetu, tusaidieni, shirikianeni nasi, na wanashiriki kwenye meza za mazungumzo ili kuhakikisha kuwa sauti zao zinawakilishiwa.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Asante UN lakini msichoke kusaka amani ya DRC: Mkimbizi Uganda

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 22, 2025 4:43


Wakati dunia ikiadhimisha miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake. Kwako Kibego.

radio uganda sudan unhcr asante umoja congo drc wakati lakini jamhuri mataifa kidemokrasia kusaka sudan kusini
Habari za UN
Kengele ya amani yagongwa UN kuikumbusha dunia wakati wa kuchua hatua kuidumisha ni sasa: Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 12, 2025 3:18


Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia. Flora Nducha amefuatilia hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii. Karibu Flora(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Natts --bellLeo, mlio mzito wa Kengele ya Amani umesikika kwenye Makao Makuu ya Umoja wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na na burudani ya muziki wa allaNatts........Kisha Katibu Mkuu Guterres akawageukia washiriki na kusema “miaka ni themanini iliyopita Umoja wa Mataifa kuzaliwakutoka kwenye majivu ya vita ili kusaka amani”, akatoa ujumbe ulio wazi,sasa  jukumu la amani duniani ni la dharura kuliko wakati mwingine wowote.Wakati migogoro ikienea na mamilioni ya raia wakiendelea kunaswa kwenye mzunguko wa ghasia, Katibu Mkuu ametahadharisha kwa onyo kali “Amani imo hatarini.”Amesema haki za binadamu na sheria za kimataifa zinakanyagwa, na kuacha nyuma kile alichokiita “mandhari yanayodhalilisha ubinadamu wetu wa pamoja.”Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu  ya siku ya Amani “Tuchukue Hatua Sasa kwa Dunia yenye Amanisi maneno ya kupita tu, bali ni wito wa dhati wa kuchukua hatua. Guterres amewakumbusha wanachama wa Umoja wa Mataifa na raia kila mahali kwamba amani haiji kwa bahati. Inajengwa hatua kwa hatua, kwa maelewano, ujasiri, na vitendo.“Ni lazima tuchukue hatua kunyamazisha bunduki na kukuza diplomasia. Ni lazima tuchukue hatua kuwalinda raia na kutetea Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ni lazima tuchukue hatua kushughulikia chanzo cha migogoro kuanzia ukosefu wa usawa na kutengwa, hadi kauli za chuki, na janga la tabianchi.”Katibu Mkuu amesisitiza kwamba amani bado iko ndani ya uwezo wa binadamu lakini ni iwapo tu tutaichagua. Ameiitaja kama nguvu kubwa zaidi kwa mustakabali bora, na kuwataka watu wote kuwaunga mkono wale wanaojenga amani, hususan wanawake na vijana walioko mstari wa mbele wa matumaini.Natts kengele.....muzukiKengele ya Amani ilipopigwa  iliyotengenezwa miongo kadhaa iliyopita kutokana na sarafu na medali zilizotolewa na watu wa kawaida kote duniani Guterres amewakumbusha hwashiriki wa hafla hiyo ishara yake “Hata katika dunia iliyogawanyika, bado tunaweza kuungana na kuiacha amani ishike hatamu.”Amehitimisha kwa kusema Katika Siku ya Kimataifa ya Amani, mlio wa kengele unatoa si tu wito wa kimya cha tafakuri, bali pia wito wa kuchukua hatua kwa viongozi, kwa raia, na kwa vizazi vijavyo.Natts muziki..

dunia guterres hata sasa umoja siku wakati hatua mataifa kimataifa septemba
Habari za UN
WMO: Ubora wa hewa duniani wazidi kuzorota japo kuna nafuu Asia na Ulaya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 5, 2025 2:59


Wakati mabilioni ya watu wakiendelea kuvuta hewa chafu inayosababisha zaidi ya vifo vya mapema milioni 4.5 kila mwaka, wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa (5 Septemba) wamebainisha madhara ya chembe ndogo ndogo za moshi kutoka katika moto wa nyika ambazo husafiri umbali mrefu duniani kote. Philip Mwihava na maelezo zaidi.(Taarifa ya Mwihava)“Ubora wa hewa hauheshimu mipaka,” anasema Lorenzo Labrador, Afisa wa Kisayansi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Anaendelea kueleza kwamba, “moshi na uchafuzi unaotokana na moto wa nyika katika msimu huu wa kihistoria katika Rasi ya Iberia tayari umepatikana Ulaya Magharibi, kwa hiyo athari zake hazibaki tu kwenye Rasi ya Iberia, bali zinaweza kusambaa kote barani Ulaya.”Akiwasilisha taarifa ya WMO kuhusu Hewa Safi na Tabianchi, ambayo inakusanya data kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, leo jijini Geneva, Uswisi Bwana Labrador ametangaza mwendelezo wa mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani.Ameonyesha ramani ya dunia ya mwaka 2024 iliyoonesha alama za chembechembe ndogo zinazojulikana kama “PM 2.5” kutokana na moto wa nyika, zikionekana kwa alama nyekundu kwenye maeneo ya Chile, Brazil na Ecuador, pamoja na Canada, Afrika ya Kati na Siberia. Takwimu hizo zinathibitisha mwenendo wa kuendelea kwa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita.Kwa upande wa habari njema, mwanasayansi huyo wa WMO amesisitiza kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika baadhi ya maeneo ya dunia.(Sauti ya Labrador) - sauti ya kiume“Tunaona mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa hasa kwa kuhusiana na PM 2.5, na pia tunaona kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika maeneo fulani ya dunia, hasa mashariki mwa China na Ulaya, mwaka baada ya mwaka.”Mfano mzuri uliotolewa katika taarifa ya leo mashariki mwa China, katika miji kama Shanghai, ambako kumepigwa hatua katika kuboresha ubora wa hewa kwa kufungua bustani zaidi na kupanda miti mingi. Na ingawa bado kuna msongamano mkubwa wa magari, mengi sasa ni ya umeme.Hata hivyo WMO inasema licha ya mafanikio hayo, miji michache tu duniani ina viwango vya ubora wa hewa chini ya vile vinavyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO). Hii inamaanisha kuwa, licha ya maboresho ya karibuni, ubora wa hewa bado ni changamoto kubwa kwa afya ya umma.Umoja wa Mataifa unaongoza juhudi za kupambana na uchafuzi wa hewa majumbani ambao ni mojawapo ya vitisho vikubwa zaidi kwa afya ya umma duniani na hasa ni hatari kwa watoto.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 26 Agosti 2025

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 26, 2025 16:07


Serikali ya Albanese inatarajiwa kuleta mbele mpango wakupanua mfumo unao ruhusu wanao nunua nyumba ya kwanza, kuweka amana ya hadi asilimia tano. Wakati marudio ya awali ya mpango huo yalikuwa na kikomo cha kila mwaka kwa washiriki, mfuno huo kwa sasa utakuwa wazi wa kila mtu anaye nunua nyumba.

Habari za UN
WHO: Mataifa mengine tafadhali fuateni mfano wa UAE kupokea wagonjwa kutoka Gaza

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 22, 2025 2:11


Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.

israel gaza uae umoja wakati mataifa shirika falme
Habari za UN
22 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 22, 2025 11:12


Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki hii hapa makao makuu ya Umoja wa mataifa kuangazia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL kijulikanacho pia kama Da'esh.Na katika mashinani fursa ni yake Abraham Mwani mwandishi wa habari za wakimbizi kutoka Radio Pacis miongoni mwa wananufaika wa mafunzo ya UNESCO ya kuwezesha vyombo vya habari kusimulia vyema habari za wakimbizi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Vijana waeleza mustakabali wa maisha yao na iwapo wangependa kuwa wazazi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 13, 2025 2:43


Wakati dunia ikiendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya za kiuchumi, vijana wamepaza sauti kueleza wasiwasi wao wa kuwa na Watoto siku za usoni. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii aliyotuandalia kutoka kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA ambayo iliwahoji vijana kutaka kufahamu iwapo wangependa kuwa na Watoto kwa siku za usoni.

Habari za UN
31 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 31, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri  wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Mauaji ya raia Komanda, Ituri, MONUSCO yalaani waasi wa ADF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 1:47


 MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Taarifa iliyotolewa na MONUSCO jijini katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa imeeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa za uhakika, shambulio hilo lililofanywa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) limesababisha vifo vya raia wasiopungua 43 (wanawake 19, wanaume 15 na watoto 9).Inaripotiwa kuwa waathirika wengi waliuawa kwa kutumia silaha za jadi wakiwa ndani ya nyumba ya ibada. Watu kadhaa walitekwa nyara. Nyumba na maduka pia yalichomwa moto, jambo ambalo limezidisha zaidi hali mbaya ya mazingira ya kibinadamu ambayo tayari ni ya kutisha katika jimbo hilo.Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Masuala ya Ulinzi na Operesheni ambaye pia ndiye Kaimu Mkuu wa MONUSCO, Vivian van de Perre, amenukuliwa akisema, “mashambulizi haya ya kulenga raia wasio na hatia, hasa ndani ya nyumba za ibada, ni ya kushtusha na ni kinyume kabisa na viwango vyote vya haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. MONUSCO itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka za DRC ili kuwalinda raia kwa mujibu wa mamlaka yake.”Kwa kushirikiana na mamlaka za eneo, MONUSCO imetoa msaada kwa hatua za awali, ikiwemo kuratibu shughuli za maziko na kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi. Wakati huohuo, MONUSCO imeongeza juhudi za kiusalama ndani na nje ya eneo la Komanda kwa kuongeza idadi ya doria katika eneo hilo.MONUSCO imeweka wazi kuwa inasalia na dhamira thabiti ya kushirikiana na mamlaka za DRC na jamii za wenyeji kusaidia kuzuia mashambulizi mengine, kuwalinda raia, kupunguza mvutano, na kuchangia katika kuimarisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kivita.Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umeeleza masikitiko na ghadhabu kubwa juu ya vitendo hivi vya kikatili, ambavyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu. Ujumbe huu unatoa rambirambi zake za dhati kwa familia na jamii zilizoathirika na unasisitiza mshikamano wake na wakazi wa maeneo hayo. MONUSCO pia inazitaka mamlaka za DRC kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji haya na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.Aidha, MONUSCO imeurudia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yote ya waasi kutoka nchi za nje kuweka silaha chini bila masharti na kurejea katika nchi zao za asili.

Habari za UN
15 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 15, 2025 10:57


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Ajira amesema …lazima tuhakikishe kuwa vijana wanapata ujuzi ambao ni wa maana, unaoweza kutumika katika mazingira mbalimbali, na unaotambuliwa na waajiri.Na kaika mashinani tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya, ambako kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domus, tunamsikia Dennis Mabuku, Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora katika kampuni ya BOC Kenya. Dennis anaeleza jinsi wanavyoichakata hewa ya kawaida na kuisafisha ili kupata  hewa safi ya oksijeni kwa ajili ya matumizi ya hospitali na mabaki mengine kwa ajili ya matumizi mengine ya viwandani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

kenya gaza israelis tanzania sera nairobi boc umoja hii haki ghf afya julai wakati wanawake mataifa ajira marekani mkuu shirika mazingira magharibi ubora mkurugenzi