Podcasts about uchaguzi ceni

  • 2PODCASTS
  • 5EPISODES
  • 11mAVG DURATION
  • ?INFREQUENT EPISODES
  • Oct 20, 2021LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about uchaguzi ceni

Latest podcast episodes about uchaguzi ceni

Wimbi la Siasa
Wimbi la Siasa - Siasa za Tume ya Uchaguzi nchini DRC kuelekea Uchaguzi 2023

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Oct 20, 2021 9:22


Wanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka muungano wa Lamuka na Ensamble wamekataa uteuzi wa Dennis Kadima kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi CENI kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2023. Itakuwaje ? Tunachambua.

Mjadala wa Wiki
Mjadala wa Wiki - Wananchi wa DRC kupiga kura siku ya Jumapili

Mjadala wa Wiki

Play Episode Listen Later Dec 19, 2018 14:01


Wananchi wa DRC watapiga kura siku ya Jumapili, kumchagua rais mpya. Kampeni zinamalizika wiki hii kuelekea Uchaguzi huo wa kihistoria. Ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Emmanuel Shadary kutoka chama tawala, Martin Fayulu kutoka muungano wa upinzani wa Lamuka, na Felix Tshisekedi. Tume ya Uchaguzi CENI inasema iko tayari kwa uchaguzi huu licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiweko kuteketea moto vya baadhi ya vifaa vya kupigia kura.

Mjadala wa Wiki
Mjadala wa Wiki - Siasa za mashine za kupigia kura nchini DRC

Mjadala wa Wiki

Play Episode Listen Later Oct 10, 2018 14:14


Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, bado kuna mvutano wa matumizi ya mashine za kupigia kura. Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia yanataka zisitumiwe kwa hofu ya wizi wa kura, lakini Tume ya Uchaguzi CENI, inasisitiza kuwa ni sharti zitumiwe. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili mwafaka kupatikana. Tunajadili hili kwa kina.

wiki drc kura umoja tume baraza mataifa tunajadili uchaguzi ceni
Wimbi la Siasa
Wimbi la Siasa - Jean Pierre Bemba hatihati kugombea Urais DRC

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Oct 3, 2018 10:01


Majina ya wagombea Urais ya awali yametangazwa huku Jean Pierre Bemba akienguliwa na yeye kuapa kukata rufaa kugai haki yake wakati Tume huru ya Uchaguzi CENI ikidai hawezi kugombea kutokana na kesi yake katika mahakama ya ICC. Je unafikiri hali itakuaje na nini hatima ya kiongozi huyo wa upinzani? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa suala hilo.

Wimbi la Siasa
Wimbi la Siasa - Tume Huru ya Uchaguzi DRC, CENI yatangaza majina ya wagombea Urais

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Oct 3, 2018 10:04


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi CENI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC, Corneille Nangaa ametangaza majina ya wagombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu huku wanasiasa wa upinzani Jean Pierre Bemba na mwenzake Moise Katumbi wakikosa nafasi ya kugombea kutokana na sababu mbalimbali. Je unataka kujua nguvu ya upinzani inasimama katika nafasi gani? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa.