Mjadala wa Wiki

Follow Mjadala wa Wiki
Share on
Copy link to clipboard

Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzu…

Rfi - RFI


    • Sep 29, 2021 LATEST EPISODE
    • infrequent NEW EPISODES
    • 13m AVG DURATION
    • 30 EPISODES


    Search for episodes from Mjadala wa Wiki with a specific topic:

    Latest episodes from Mjadala wa Wiki

    Rais wa DRC Felix Tshisekedi athibitisha kuwa uchaguzi utafanyika mwaka 2023

    Play Episode Listen Later Sep 29, 2021 10:01


    Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi amewaambia viongozi wa dunia kuwa uchaguzi mkuu utafanyika nchini mwake mwaka 2023 kama ilivyopangwa kikatiba.Kauli hii pia imeungwa mkono na spika wa Bunge la kitaifa huko DRC Chistophe Mboso Nkodia wakati wa Mkutano wake na Raia kwenye mji wa Kinshasa Siku ya Jumapili iliyopita.Hata hivyo Tume ya Uchaguzi inayotakiwa kuandaa uchaguzi huo, haijawekwa wazi.

    Joto la kisiasa kuelekea uchaguzi nchini Kenya 2022

    Play Episode Listen Later Sep 15, 2021 10:10


    Makala haya mJadala wa wiki tunajadili siasa za Kenya kuelekea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa rais wa hapo mwakani.

    Mapinduzi nchini Guinea na hali ya kisiasa kwa watawala barani Afrika

    Play Episode Listen Later Sep 10, 2021 10:30


    Kwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Guinea na nini sababu za kutokea mapinduzi ya serikali barani Afrika. Swala ni kwa nini imejengeka dhana kwamba kiongozi anayeng'ang'ania madaraka mwisho wake siku zote ni mapinduzi ya kijeshi, nini kifanyike ili ifike mahali demokrasia na watawala waheshimu katiba za nchi zao? Mjadala wa wiki na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka 

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amtaka naibu wake ajiuzulu

    Play Episode Listen Later Aug 25, 2021 13:41


    Kwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Kenya. Wiki hii, rais Uhuru Kenyatta amemwambia naibu wake William Ruto ajiuzulu iwapo anaona  hafurahishwi na ajenda ya serikali ambayo yeye ni mdau mkubwa.

    Siku 100 za Waziri Mkuu wa DRC Sama Lukonde

    Play Episode Listen Later Aug 12, 2021 9:55


    Tunajadili siku 100 za serikali ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Sama Lukonde.

    Siasa za vyama nchini Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu

    Play Episode Listen Later Jul 15, 2021 10:11


    Kenya inajiandaa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2022. Vyama vya siasa vimeanza maandalizi kujiweka tayari kwa uchaguzi huo. Lakini je, vyama hivi vimejiandaa  vya kutosha ? Tunajadili.

    Mjadala wa Wiki - Miaka minne ya rais wa Tanzania John Magufuli

    Play Episode Listen Later Nov 6, 2019 15:00


    Rais wa Tanzania John Magufuli, ametimiza miaka minne madarakani, je ni mafaniko gani na changamoto zipi zilizoshuhudiwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ?

    Mjadala wa Wiki - Hatima ya Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji

    Play Episode Listen Later Oct 16, 2019 12:04


    Wananchi wa Msumbiji, wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu baada ya kupiga kura siku ya Jumanne. Ni uchaguzi ambao wachambuzi wa siasa wanasema ni kipimo cha demokrasia na utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya waasi wa Renamo na serikali, miezi miwili iliyopita. Tunajadili suala hili.

    Mjadala wa Wiki - Dunia kuangazia mabadiliko ya tabia nchi

    Play Episode Listen Later Sep 25, 2019 11:40


    Mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kuyeyuka kwa theluji katika milima mbalimbali Duniani hatua inayoisukuma nchi ya Ufaransa kuja na mradi wa kufanya utafiti ili kuhifadhi barafu unaoitwa Kumbukumbu ya Barafu iliyopo katika Mlima mrefu barani Afrika wa Kilimanjaro. Hayo yanajiri wakati huu dunia ikiangazia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mjadala wa Wiki - Rais wa DRC Felix Tshisekedi azuru Ubelgiji kuimarisha uhusiano

    Play Episode Listen Later Sep 18, 2019 13:05


    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi,yupo ziarani nchini Ubelgiji. Ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya, baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa DRC mapema mwaka huu. Tshisekedi yupo nchini Ubelgji, kuhimiza ushirikano kati ya nchi hizo mbili, uhusiano ambao ulikuwa baridi wakati wa uongozi wa rais wa zamani Joseph Kabila. Je, ziara hii ina umuhimu gani kwa raia wa DRC na kwanini inazua maswalimengi maswali miongoni mwa raia wa DRC wauishio nje na ndnai ya nchi ?  Kujadiki hili, tunauganba na Raphae Bakema, mchambuzi wa siasa za DRC naeneo la Maziwa Makuu, akiwa Goma lakini Profesa Malonga Pacique akiwajijini Kgali. 

    Mjadala wa Wiki - Baraza huru laundwa nchini Sudan

    Play Episode Listen Later Aug 21, 2019 15:32


    Baraza huru kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia limeundwa nchini Sudan, kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, je, litatimiza mahitaji ya raia wa Sudan ? Tunajadili.

    Mjadala wa Wiki - Mkutano wa 39 SADC kuangazia uchumi wa viwanda

    Play Episode Listen Later Aug 7, 2019 15:16


    Karibu katika makala ya mjadala wa wiki.Kikao cha 39 cha viongozi wa mataifa ya SADC kinataraji kuanza jijini Dar es salaam nchini Tanzania ajenda kuu ni kujadili mkakati wa kiuchumi kwa kuhimiza viwanda katika mataifa hayo.Fuatilia kwa kina,wachambuzi Wetengere Kitojo na Saidi Msonga wameangazia kinaga ubaga katika makala haya na mwandishi wetu Martha Saranga.

    Mjadala wa Wiki - Nani atamaliza Ebola nchini DRC ?

    Play Episode Listen Later Jul 24, 2019 15:39


    Wiki hii Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Oly Ilunga alitangaza kujiuzulu, baada ya kushtumu uamuzi wa rais Felix Tshekedi kumwondoa kwenye Kamati maalum ya kupambana na janga la ugonjwa hatari wa Ebola, ambao tangu mwezi Agosti mwaka 2018, umesababisha vifio vya watu 1,700 na wengine zaidi ya 200 kuambukizwa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Nani atasaidia kumaliza Ebola nchini DRC na juhudi za WHO zinafua dafu ?

    Mjadala wa Wiki - Mauaji nchini Ethiopia yanalenga kuharibu mipango ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ?

    Play Episode Listen Later Jun 26, 2019 12:47


    Mnadhimu Mkuu wa jeshi  nchini Ethiopia Jenerali Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake jijini Addis Ababa, sawa na rais wa jimbo la Amharic Ambachew Mekonen ambaye alishambuliwa na watu wenye silaha. Ni mauaji yanayokuja wakati huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed akiendeleza mageuzi nchini mwake.     Hii inamaanisha nini ? Tunachambua na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Haji Kaburu, Comrad Sambala wote wakiwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Emmanuel Makundi, anashiriki pia, ni Mwanhabari wa RFI Kiswahili.

    Mjadala wa Wiki - Machafuko nchini Sudan, maafa na majeruhi yaripotiwa

    Play Episode Listen Later Jun 5, 2019 14:39


    Wiki hii, uongozi wa kijeshi nchini Sudan, uliamua kuvunja kambi ya waandamanaji jijini Khartoum ambao wamekuwa wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.Watu zaidi ya 60 walipoteza maisha na mamia kujeruhiwa. Nini hatima ya Sudan ? Tunajadili.

    Mjadala wa Wiki - DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano

    Play Episode Listen Later May 23, 2019 12:12


    Hatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?

    Mjadala wa Wiki - Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu ataka maandamano dhidi ya rais Tshisekedi

    Play Episode Listen Later May 2, 2019 15:18


    Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu, anataka maandamano yafanyike nchini humo kumshinikiza rais Felix Thisekedi aondoke madarakani kama ilivyokuwa nchini Sudan na Algeria. Fayulu anasema yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018. Tunachambua hili kwa kina.

    Mjadala wa Wiki - Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu

    Play Episode Listen Later Apr 3, 2019 12:01


    Baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20 hatimaye Abdulaziz Bouteflika amelazimika kusalimu amri na kujiuzulu kama rais wa nchi wa Algeria. Nini hatima ya nchi ya Algeria baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambaye tangu mwaka 2013 amekuwa akitumia gari la magurumu baada ya kupatwa na kiharusi. Kwa mujibu wa Katiba, Spika wa Senate sasa ndio rais wa muda hadi pale Uchaguzi mpya utakapofanyika.

    Mjadala wa Wiki - IS ladhoofishwa Syria na Iraq

    Play Episode Listen Later Mar 27, 2019 12:55


    Baada ya miezi ya mapigano, kikundi cha jihadi cha Kiislam (IS) kimepoteza Baghuz, kijiji cha mashariki mwa Siria ambacho kinaelezwa kuhitimisha utawala wa kihalifa nchini syria.Kama ambavyo mwishoni mwa 2017, IS ilivyopoteza ngome zake za Mosul nchini Iraq na Raqqa nchini Syria.

    Mjadala wa Wiki - Mvutano kati ya Rwanda na Uganda Marekani yatia neno

    Play Episode Listen Later Mar 13, 2019 12:12


    Makala ya mjadala inaangazia mvutano wa kidiplomasi akati yamataifa mawili ya Afrika mashariki,Uganda na Rwanda wakati huu jumuiya ya Afrika mashariki ikiwa  kimya..wachambuzi Abbas Mwalimu na Haji Kaburu wanadadavua kwa kina.

    Mjadala wa Wiki - Mzozo kati ya Rwanda na Uganda kuhusu mpaka wa Katuna

    Play Episode Listen Later Mar 6, 2019 11:29


    Nchi za Rwanda na Uganda zinashuhudia mvutano wa kidiplomasia. Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwaficha maadui wa serikali yake, suala ambalo Uganda inakanusha vikali.

    Mjadala wa Wiki - Mustakabali wa DRC baada ya matokeo ya uchaguzi

    Play Episode Listen Later Jan 31, 2019 11:46


    Baada ya tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kumtangaza mshindi wa kiti cha uraisi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi,tunaangazia nini matarajio ya raia sasa,nini mustakabali wa DRC wakati huu upinzani wa lamuka ukipinga matokeo hayo kwa kudai udanganyifu ulifanyika.

    Mjadala wa Wiki - Mzozo wa kisiasa nchini Venezuela

    Play Episode Listen Later Jan 30, 2019 11:35


    Venezuela imejikuta katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi, kiongozi wa upinzani  Juan Guaido amejiapisha kuwa rais, huku kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro akitishia kumchukulia hatua kali. Tunajadili hili kwa kina.

    Mjadala wa Wiki - Wananchi wa DRC bado wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu

    Play Episode Listen Later Jan 9, 2019 17:01


    Mamilioni ya raia wa DRC, pamoja na dunia, inasubiri Tume ya Uchaguzi kumtangaza mshindi wa Uchaguzi wa urais, baada ya wananchi kupiga kura Desemba 30 2018. Nani atashinda Uchaguzi huu na ni kwanini matokeo yamechelewa ? Tunachambua suala hili kwa kina.

    Mjadala wa Wiki - Raia wa DRC waendelea kusubiri matokeo,mtandao wazimwa

    Play Episode Listen Later Jan 2, 2019 11:43


    Makala ya mjadala wa wiki inaangazia hali ya mambo nchini DRC wakati huu raia wakisubiri matokeo ya kura ya uraisi wabunge na viongozi wa wilaya kote nchini humo kunashuhudiwa mtandao ukizimwa kwa sababu kiusalama kama ambavyo serikali imeeleza...karibu,wazungumzaji ni Cyllile Muhongya na Jaribu muliwavyo wote wakiwa Mashariki mwa DRC.

    Mjadala wa Wiki - DRC ipo tayari kwa Uchaguzi wa Desemba 30, 2018 ?

    Play Episode Listen Later Dec 26, 2018 17:07


    Wananchi wa DRC, wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais mpya na viongozi wengine, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili, tukiwa na Steven Chondo, mmoja wa maafisa wa kampeni wa mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, lakini pia Reubens Mikindo , Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani UDPS, ambacho mgombea wake ni Felix Tshisekedi.

    Mjadala wa Wiki - Wananchi wa DRC kupiga kura siku ya Jumapili

    Play Episode Listen Later Dec 19, 2018 14:01


    Wananchi wa DRC watapiga kura siku ya Jumapili, kumchagua rais mpya. Kampeni zinamalizika wiki hii kuelekea Uchaguzi huo wa kihistoria. Ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, Emmanuel Shadary kutoka chama tawala, Martin Fayulu kutoka muungano wa upinzani wa Lamuka, na Felix Tshisekedi. Tume ya Uchaguzi CENI inasema iko tayari kwa uchaguzi huu licha ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiweko kuteketea moto vya baadhi ya vifaa vya kupigia kura.

    Mjadala wa Wiki - Marekani: Democratics washinda bunge la wawakilishi, Republican watawala Senate

    Play Episode Listen Later Nov 7, 2018 13:13


    Chama cha Republican cha rais Donald Trump, kimepata ushindi katika bunge la Senate huku kile cha Denocratic, kikirejesha udhibiti wa bunge la wawakilishi, baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge, Maseneta na Magavana, uliofanyika siku ya Jumanne. Matokeo haya yanamaanisha nini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kujadili hili, ni Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa mjini Arusha nchini Tanzania na Dokta Brian Wanyama, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii mjini Bungoma nchini Kenya.

    Mjadala wa Wiki - Rais Paul Biya achaguliwa tena kuongoza Cameroon kwa muhula wa saba

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2018 13:03


    Rais wa Cameroon Paul Biya, ametangazwa mshindi kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa saba, kuendeleza uongozi wake wa miaka 36. Upinzani umekataa kutambua ushindi huu. Ushindi huu una maana gani kwa demokrasia ya Cameroon na bara la Afrika ? Tunajadili.

    Mjadala wa Wiki - Siasa za mashine za kupigia kura nchini DRC

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2018 14:14


    Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, bado kuna mvutano wa matumizi ya mashine za kupigia kura. Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia yanataka zisitumiwe kwa hofu ya wizi wa kura, lakini Tume ya Uchaguzi CENI, inasisitiza kuwa ni sharti zitumiwe. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili mwafaka kupatikana. Tunajadili hili kwa kina.

    Claim Mjadala wa Wiki

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel