POPULARITY
Categories
Kwa zaidi ya muongo mmoja, eneo la Nyiragongo lililoko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) limekumbwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu wa kudumu kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha. Maelfu ya familia wamekimbia makazi yao na watoto wengi kulazimishwa kujiunga na makundi hayo ya kijeshi. Kati ya mwaka 2024 na 2025, kuzuka upya kwa mapigano kunakohusishwa na kuibuka tena kwa waasi wa M23 kumeongeza zaidi hali ya hatari kwa wakazi wa eneo hilo, hasa watoto na vijana. Ili kuleta ahueni kwa wakazi, Umoja wa Mataifa umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana basi na Anold Kayanda kwenye makala hii.
Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au kwingineko. Mkiwa mbali na familia zenu, mbali na nchi yenu, katika mazingira yenye changamoto, na wakati mwingine katika hali hatarishi.”Anawapa moyo zaidi askari lakini akiwakumbusha kuwa wao ni kioo cha ulimwengu wazingatie maadili“Na tunathamini sana kujitolea kwenu. Tunathamini sana kwamba mnaenda kuwasaidia ndugu zenu katika nchi nyingine, iwe ni nchi jirani au sehemu iliyo mbali. Mnapokwenda, mnaliwakilisha dunia. Mnawakilisha watu wa dunia.”Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang'are akamthibitishia mgeni kwamba askari hawa wameiva na hakuna kisingizio chochote cha kutozingatia maadili huko wameandako, kisha akawahoji, Nao wanajibu, “twende pamoja, turudi pamoja.”
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika maadhimisho ya siku ya Ziwa duniani; Maandalizi ya walinda amani kwenda kuhudumu CAR ma DRC; Msaada wa MONUSCO kwa wakazi wa Kivu Kaskazini; Aliyerejesha fadhila kwa WFP.Leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ziwa Duniani yakibeba maudhui "Ziwa ni uti wa mgongo wa sayari yetu" na ili kuthibitisha hilo tunakupeleka Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako , Bosco Cosmas kutoka Radio washirika SAUT FM anamulika maoni ya wananchi ni kwa vipi ziwa Victoria limekuwa msaada na mkombozi kwao.Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Anold Kayanda anatupeleka eneo la Maziwa Makuu barani Afrika kusikia harakati za Umoja wa Mataifa kuinua wakazi waliokumbwa kwenye mizozo.Mashinani kutana na Moses Komakech Meneja wa ghala la chakula la shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP lililoko Gulu katika jimbo la Acholi Kaskazini mwa Uganda ambapo baada ya kuwa mnufaika wa mgao wa chakula wa WFP, sasa anaendesha ghala la shirika hilo linalohudumia wakimbizi 800,000.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakulatea-Ripoti mpya kwa jina Maendeleo katika Maji ya Kunywa na Kujisafi Majumbani iliyozinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kwamba, licha ya hatua kupigwa, mtu 1 kati ya 4 duniani bado hana upatikanaji wa maji salama ya kunywa. -Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imetoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha mfumo wa “mzunguko” unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kumaliza vifungo vyao. - Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR leo limepongeza Serikali ya Kifalme ya Thailand kwa kupitisha azimio litakalowapa wakimbizi wa muda mrefu kutoka Myanmar haki ya kufanya kazi nchini Thailand.-Katika mada kwa kina tunamulika uzinduzi wa shule ya kwanza ya Akili Mnemba iliyoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women huko ukanda wa Asia na Pasifiki-Na mashinani utamsikia Ibrahim Al-Najjar mkimbizi huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli akielezea hali tete ya ajira hivi sasa tangu vita ianze Oktoba 7, 2023.
Baada ya miaka miwili ya vita katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel Ijumaa tarehe 22 Agosti Umoja wa Mataifa ukatangaza jambo baya zaidi, ripoti ya njaa duniani IPC ikathibitisha wananchi wa Gaza rasmi wana kabiliwa na baa la njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ni moja kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo pamoja na hali ya vita yamekuwa yakitoa msaada wa chakula huko Gaza na wameeleza kwamba baa la njaa lazima likomeshwe kwa gharama yoyote ile. Kusitishwa kwa mapigano mara moja na kukomesha mzozo ni muhimu ili kuruhusu misaada kuweza kuingizwa Gaza ili kuokoa maisha. Makala hii Leah Mushi anamuangazia mmoja wa watoto wanaokabiliwa na njaa
Leo Agosti 25 ni miaka minane tangu kufurushwa kwa wingi watu wa kabila la Rohingya kutoka katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa mshikamano wa kimataifa kuwasaidia kwani mateso kwa watu hao yanaendelea kuwa mabaya zaidi kila uchao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Asante AssumptaMyanmar (zamani ikiitwa Burma) ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye zaidi ya makabila 100, inayopakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.Warohingya wanafurushwa na kuteswa kwasababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria kwa madai kuwa walitoka Bangladesh ingawa wameishi vizazi na vizazi nchini Myanmar. Pia sababu ya imani yao kwa uislamu miongoni mwa sababu nyingine.Ni miaka minane sasa tangu ufurushwaji mkubwa wa jami hii kutoka jimbo la Rakhine pwani ya Magharibi mwa Myanmar. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaonya kuwa Warohingya na raia wengine bado wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu na kufurushwa. Anaeleza wasiwasi wake kuhusu tarifa za kufukuzwa na kupunguzwa kwa nafasi za hifadhi katika ukanda huo, huku wakimbizi walioko Bangladesh wakikabiliana na upungufu mkubwa wa msaada wa chakula, elimu na huduma za afya.Guterres anasisitiza tena wito wake wa kulindwa kwa raia wote kwa mujibu wa sheria za kimataifa na anataka mshikamano mkubwa wa kimataifa. Hata hivyo ana matumaini kuwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Rohingya utakaofanyika New York mwezi ujao utasaidia kupata suluhu za kudumu.Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anaeleza kuwa jeshi la Myanmar na Jeshi la Rakhine bado wanaendeleza uhalifu mkubwa dhidi ya Rohingya bila kuchukuliwa hatua, kinyume na sheria za kimataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na anatoa wito wa kukomesha matendo hayo ili kuvunja mzunguko wa vurugu.
Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje? kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa mapacha wengine wawili ambao sasa wana umri wa miezi tisa na kwa bahati mbaya wote wana utapiamlo kutokana na changamoto ya chakula.“Hapa Dori tumebarikiwa watoto mapacha lakini wametukuta hatua makazi, hatuna chochote na tuna njaa na kibaya zaidi sikuwa hata na maziwa ya kutosha kuwanyonyesha”Watoto wa Fadima wamekuwa wakiishi kwa msaada wa kibinadamu unaotolewa na mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF ambayo sasa inasema hali yao inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya kimataifa misaada wanayoitoa na hivyo kuhatarisha maisha na mustakabali wa watoto wake. Fadima anasema“Unapotawanywa na machafuko huwezi kufanya kazi, unakuwa kama mtu asiye na ajira na hapo ndio madhila yanapokuwa makubwa zaidi, lakini bado hapa ni bora kuliko ningesalia kijijini kwetu.”Kwa mujibu wa UNICEF Burkina Faso ni moja ya migogoro ya kibinadamu iliyopuuzwa zaidi duniani. Ingawa UNICEF iko hapa kusaidia, lakini inasema msaada zaidi unahitajika haraka.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.
Tarehe 18 Agosti mwaka 2025 siku ya Jumatano, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama walikutana kujadili Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL/Da'esh.Walikabidhiwa ripoti hiyo ya 21 ikimulika vitisho vinavyotokana na kikundi hicho ambacho kirefu chake ni Islamic State in Iraq and the Levant au pia Da'esh. Ripoti ikigusia tishio la kikundi hicho katika maeneo mbalimbali duniani, lakini makala hii initajikita zaidi barani Afrika!
Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki hii hapa makao makuu ya Umoja wa mataifa kuangazia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL kijulikanacho pia kama Da'esh.Na katika mashinani fursa ni yake Abraham Mwani mwandishi wa habari za wakimbizi kutoka Radio Pacis miongoni mwa wananufaika wa mafunzo ya UNESCO ya kuwezesha vyombo vya habari kusimulia vyema habari za wakimbizi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura.Na katika mashinani Mwanzilishi na mratibu wa Kundi la Utetezi la Darfur, Ikhlass Ahmed amelielezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York kwa njia ya video jinsi wanavyokabiliwa na kuenea kwa kasi kwa unyanyasaji wa kingono.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano. Flora Nducha anafafanua zaidi
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi pamoja kuhakikisha wanatoa fursa ya ufikiaji wa kibinadamu kwa watuwenye uhitaji na kunakuwepo na uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu zikijumuisha ulinzi kwa wahudumu wa kibinadamu na wa Umoja wa Mataifa”.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi ya kundi la waasi wa Allied Democratic Forces, ADF kati ya tarehe 9 na 16 Agosti, katika maeneo ya Beni na Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, yaliyoua raia 52, wakiwemo wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamehusisha utekaji nyara, uporaji, na uchomaji wa nyumba na magari, na kuwaacha wakazi ambao tayari wako katika hali ngumu ya kibinadamu katika mateso zaidi.Na katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya wahudumu wa binadamu, huduma na kujitolea kwa wanachama 270 wa Kikozi cha Polisi cha walinda amani kutoka Ghana wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), wakiwemo maafisa wanawake 63, ilitambuliwa kwa kutunukiwa Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Heshima kwa juhudi zao, zikiwa ni pamoja na kuwalinda raia, kuwezesha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kukuza haki za binadamu na kujenga amani. Bismark Achaab, Msimamizi Mkuu wa Kitengo hicho anatoa shukrani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Kuelekeza maadhimisho hayo hapo kesho Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masual ya Watoto UNICEF limetengeneza makala inayoangazia watoa huduma wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Leah Mushi anatujuza kilichopo katika makala hiyo.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.
Jaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Na katika mashinani nampisha Mchanga Omari Kombo kutoka Pemba Zanzibar ambaye ni mnufaika wa mpango mpya wa afya ya uzazi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF na wadau wake umewasaidia wanawake wajawazito kama kuondokana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya njema.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Kutana na Godlove Makunge, kijana huyu wa kitanzania ambaye safari ya maisha yake imedhihirisha kuwa chochote unachoweka nia na utashi kitafanikiwa. Godlove ambaye elimu yake ni ya kidato cha nne, hakuweza kuendelea na masomo zaidi. Alichukuliwa na mtu mmoja afanye kazi za ndani kutoka Morogoro hadi Lindi na kisha akaishia Mtwara, kusini-mashariki mwa Tanzania ambako huko aliona fursa ya kujipatia kipato kutokana na taka zilizokuwa zinasambaa mitaani. Aliasisi kampuni ya usafi na mazingira iitwayo Shikamana Investment. Sasa kampuni yao ya ubia imeajiri vijana 6. Alishiriki mafunzo ya uchumi rejeleshi yaliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP mkoani Mtwara. Sawiche Wamunza, Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati UNDP alizungumza na Bwana Makunge baada ya mafunzo hayo ili afahamu amejifunza nini.
Jaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambaye baada ya mafunzo ya siku tatu ya uchumi rejeleshi katika mkoa wa Mtwara, Kusini-Mashariki mwa Tanzania alizungumza na Godlove Makunge Muasisi na Mkurugenzi wa kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira, iitwayo Shikamana Investment. Bwana Makunge anaanza kwa kuelezea mtazamo wa jamii kwake baada ya kuamua kuanza kuzoa taka.Na katika Radwa Ahmed, Mkimbizi kutoka Sudan ambaye alianza kwa kuoka mikate kwa ajili ya familia yake, na kwa ufadhili wa shirika la Umoja wakimbizi Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameweza kuigeuza talanta yake kuwa biashara ya kuuza mikate na kuajiri wakimbizi wenzake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
Australia ita tambua Palestina kama taifa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa Septemba.
Wakati dunia ikiendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya za kiuchumi, vijana wamepaza sauti kueleza wasiwasi wao wa kuwa na Watoto siku za usoni. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii aliyotuandalia kutoka kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA ambayo iliwahoji vijana kutaka kufahamu iwapo wangependa kuwa na Watoto kwa siku za usoni.
Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nchini Kenya wanaolima mbogamboga kupitia mradi uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wa kilimo cha bustani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain, wadau kwa kushirikiaa na ofisi ya Uwekezaji na Uendelezaji Teknolojia, ITPO ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO wanachukua hatua kuondolea wanawake umaskini kwa kuimarisha talanta walizonazo. Mengine ni kama yafuatayo..Leo ni siku ya Kimataifa ya vijana duniani maadhinisho yanafanyika jijini Nairobi nchini Kenya chini ya ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia vijana ujumbe maalum akisema “Kwa kijana: Sauti yako, mawazo yako na uongozi ni muhimu.”Je, vijana wanasemaje kuhusu siku hii? Kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania, Sabrina Saidi wa Idhaa hii amezungumza na baadhi yao.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP limepokea zaidi ya dola milioni 2 kutoka Japan kwa ajili ya msaada wa chakula nchini Malawi. Kwa msaada huu WFP inatarajia kusambazana tani 1970 za mahindi katika msimu wa mwambo kwa mwaka 2025/ 2026.Na katika mashinani fursa ni yake Maryam Bukar Hassan al maaruf Alhanislam, mshairi kutoka Nigeria ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu na Mchechemuzi wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Amani. Hivi karibuni alighani shairi lake kwenye tamasha la majira ya joto hapa jijini New York, nchini Marekani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo. Sabrina Said na taarifa zaidi.
Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii.
Jaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.Na katika mashinani fursa ni yake Mariam Kazungu kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya, ambaye anasema Watoto wake wamenufaika kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa utoaji wa chanjo dhidi ya homa ya tumbo na ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Sabrina Moshi na maelezo zaidi.
Huko mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.
Jaridani leo tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza, na mradi wa mlo shuleni unaowezesha watoto kuendelea na masomo nchini Uganda. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu.Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Makala inakupeleka Mtwara, kusini mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.Na katika mashinani Patriciah Akinyi, Mwathirika wa jeraha linaloweza kuzuilika wakati wa kujifungua ambaye pia ni mnufaika wa matibabu ya upasuaji wa kurekebisha jeraha hilo la fistula nchini Kenya inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA, anasimulia kilichomkumba.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Jaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpango mpya wa kuonesha faida za nchi hizo kwa muunganiko wao kwa njia ya ardhi amesema…. hii leo LLDCs zinatumia vema uwepo wao kimkakati, katikati ya Afrika na muunganiko wa kikanda kuwa vitovu muhimu vya kuunganisha nchi kiuchumi , biashara na ubunifu. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu leo wamesema ili kuzuia vifo zaidi na mateso kutokana na njaa huko Gaza, Israel inapaswa kurejesha mara moja ruhusa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu kuingia bila vikwazo vyovyote eneo la Palestina inalokalia kimabavu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado. Kelvin Keitany na maelezo zaidi.
Jaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado.Na mashinani fursa ni yake Dkt. Beatrice mwilike, Mkunga Bingwa na Rais wa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambaye kupitia mradi unaolenga uzazi salama kwa watoto milioni 10 ifikapo 2030 lililozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA kwa kusaidiana na serikali ya Denmark, anasema wakunga wanatumia appu na njia za kisasa zinazowapa taarifa sahihi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Leah Mushi na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva, Uswisi unakofanyika mkutano utakaweka mwelekeo wa jinsi ya kukabiliana na uchafuzi unaotokana na plastiki duniani, Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani, UNEP, ameonya kwamba, “uchafuzi wa plastiki tayari upo katika mazingira, baharini, na hata katika miili yetu. Tukizidi kuendelea kwa mwelekeo huu, dunia yote itazama katika uchafuzi wa plastiki.”Na mashinani leo tuko katika shoroba za makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wageni hutoka kila pembe ya Dunia kutembelea jengo hili la kihistoria. Mwalimu Maria Rulands ni mmoja wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan. Anold Kayanda anafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula. Simulizi zaidi anayo Assumpta Massoi.
Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula. Ripoti ya Selina Jerobon inayotokana na video iliyochapishwa mtandao wa X na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipaletina, UNRWA, inafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo. Katika makala Leah Mushi anatuletea habari njema kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026.Na mashinani tutakupeleka nchini Ethiopia, kumulika harakati za kujikwamua kiuchumi katikati ya janga la ukame.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025. Jukwaa hili lilifanyika kwa siku 4 likileta pamoja vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani na wadau wa maendeleo na uchumi ili kujadili changamoto zinazowakabili vijana na kutoa mapendekezo ya kuboresha dunia kuelekea usawa na maendeleo endelevu chini ya Ajenda ya 2030 au Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Miongoni mwa vijana walioshirikki ni Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania. Akizungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa hii, Bi. Kapwani alianza kwa kuelezea alichokuwa anasongesha mbele baada ya kushiriki mkutano wa Zama Zijazo au Summit of The Future uliopitisha Mkataba wa Zama Zijazo au PACT OF THE FUTURE mwezi SEptemba mwaka jana 2024.
Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Makala inakupeleka Kenya kwake Kevin Keitany wa Radio washirika Radio Domus akimulika siku ya kimataifa ya urafiki inayoadhimishwa leo Julai 30, ikimulika urafiki katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya watu zaidi ya mmoja, jamii, tamaduni na hata mataifa na mchango wake katika amani na utulivu duniani. Kelvin anamulika urafiki kati ya watu wawili.Na katika mashinani tuelekee jijini Geneva, Uswisi ambako unafanyika Mkutano wa Sita wa Spika wa Mabunge Duniani kumsikia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani akitoa wito kwa viongozi wenzake kuutetea Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Sharon Jebichii na taarifa zaidi.