POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kushuhudia mafunzo ya ukufunzi kwa wanadhimu wa Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkataba wa amani DRC na Rwanda, UKIMWI, na maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Kiswahili, na uchambuzi wa neno.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha mkataba wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda uliotiwa saini tarehe 27 mwezi uliopita wa Juni, huku wakishukuru Marekani, Qatar na Muungano wa Afrika kwa juhudi za usuluhishi.Ukata uliosababishwa na wahisani kukata au kupunguza ghafla na kwa kiasi kikubwa ufadhili kwenye miradi ya kupambana na UKIMWI umekuwa na madhara kwa nchi zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa huo, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS.Leo kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juu ya Mangu wametuma ujumbe wao wa umuhimu wa lugha hiyo kupitia ngonjera.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti.
Hii leo jaridanitunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na mauaji yaliyofanyika nchini Rwanda kati ya mwaka 1972 hadi 1973. Makala tunamulika inayochukuliwa nchini Kenya za kutekeleza haki za watu wenye ulemavu wa kutoona, na mashinani tunakwenda DRC, kulikoni?Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya viziwi wasioona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya.Na mashinani, fursa ni yake Tom Fletcher, Mratibu wa Umoja wa mataifa wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura akihitimisha ziara yake Goma Mashariki mwa DRC amezungumza na waandishi wa habari akieleza kuwa raia wameteseka vya kutosha na ukata unawazidishia madhila”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya ulemavu wa uziwi na kutoona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya. Sharon Jebichii na makala zaidi.
Karibu katika Makala yetu ya Leo Jumapili ambayo ni maalum kabisa kuhusu historia ya siku ya Muziki dunia ambayo huadhumishwa kila ifikapo Juni 21. Uko nami Ali Bilali mtangazaji wqko asiependa makuu Bienvenue ama Karibu.
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi”, tukisikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kazi wanazozifanya kuinua Maisha ya wakimbizi, na pia tunakuletea sauti za wakimbizi kutoka DRC, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria.Tukisalia na siku ya wakimbizi duniani tunaelekea eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR anakupeleka Kusini-Magharibi mwa Burundi kwenye kituo cha wakimbizi cha Musenyi kumsikia mkimbizi kutoka DRC ambaye ananufaika na kauli mbiu ya siku ya wakimbizi mwaka huu ya Mshikamano na Wakimbizi.Na mashianani tukisalia na siku ya wakimbizi duniani, tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumsikia mtoto mkimbizi ambaye alitumikishwa katika vita na waasi wenye silaha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika juhuddi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu kwenye masuala mbalimbali katika jamii, tukipata ujumbe wa Abeida Rashid Abdallah Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ya kisiwani humo amabye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa CSW69.Watu wa Ukraine hawapaswi kulazimika kujificha kusaka hifadhi kila jua lizamapo, amesema Matthias Schmale, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, kufuatia mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo yaliyofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv, Odesa na miji mingine na kuua raia 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 50.Mfumo wa afya wa huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli unazidi kudarimika, ukizidiwa uwezo kutokana na idadi kubwa ya watu waliouawa au kujeruhiwa karibu na maeneo ya usambazaji wa misaada, amesema Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO Dkt. Thanon Gargavanis. Akizungumza na waandishi wa habari Geneva, Uswisi kutokea Gaza, Dkt Gargavanis amesema “tuko katika hali mbaya kila siku ya uwezo wetu wa kutoa huduma kikamilifu au kukumbwa na janga kamili.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupambana na kuenea kwa Jangwa na ukame na mwaka huu 2025 inasisitiza hatua za dharura kurejesha ubora wa ardhi na kusongesha maendeleo endelevu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake ametaka hatua zichukuliwe huku akionya kuwa uharibifu wa ardhi unazidi kuongezeka duniani kote na kugharimu uchumi wa dunia kwa takriban dola bilioni 880 kila mwaka, kiasi kikubwa kuliko uwekezaji unaohitajika kurekebisha hali hiyo.Na katika mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupambana na jangwa na ukame inayobeba maudhui Rejesha ardhi, fungua fursa Meja Katja Dorner kutoka Boni kupitia video iyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa UNCCD anatoa ujumbe kuhusu matumizi endelevu ya ardhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Leo Ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha umma kuhusu Ualbino, Anold Kayanda wa idhaa hii anazungumza na Khadija Shaaban Taya almaarufu Keisha, Mbunge katika Bunge la Tanzania alipohudhuria mkutano wa mkataba wa watu wenye ulemavu uliofanyika wiki hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Keisha anaanza kwa kueleza anavyoithamini siku ya leo.
Juni 12, ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Inakadriwa, takriban watoto milioni 200 kote duniani wanatumikishwa badala ya kuwa shuleni. Tunakuuliza, serikali yako inafanya vya kutosha kukomesha utumwa wa watoto? Unamfahamu mtoto anayefanyishwa kazi?
Juni 12, ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Inakadriwa, takriban watoto milioni 200 kote duniani wanatumikishwa badala ya kuwa shuleni. Tunakuuliza, serikali yako inafanya vya kutosha kukomesha utumwa wa watoto? Unamfahamu mtoto anayefanyishwa kazi?
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF unaonesha licha ya hatua zilizopigwa, ajira kwa watoto bado inaathiri watoto milioni 138 duniani kote, kati yao milioni 54 wakifanya kazi hatarishi ambazo zinaweza kuhatarisha afya yao, usalama wao au maendeleo yao kwa ujumla.Nchini Sudan Kusini watu wako katika hatari ya njaa katika miezi ijayo, kutokana na kuongezeka kwa mapigano katika jimbo la Upper Nile. Utafiti mpya kutoka katika Mfumo wa Uainishaji wa Viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) unaonesha kudorora kwa hali ya chakula na lishe katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyoathiriwa na mapigano katika miezi ya karibuni.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Was bringt Menschen dazu, sich beruflich und in ihrer Freizeit stundenlang über Autos und Motorräder zu unterhalten? In dieser Folge erzählen wir, wie unsere Faszination angefangen hat. Von Kisten voller Matchbox-Autos über Computerspiele, Postern von Autohelden, endlosen Staus auf dem Straßenteppich und prägenden Momenten hinterm Lenker. Außerdem: Clemens testet den Audi A6 Avant e-tron performance und Sebastian hat Neuigkeiten zur KTM-Rettung.
Uchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.
Siku nane baada ya upinzani wa mseto kuachana, vyama vya Liberal na Nationals vime tangaza kuwa vime rudiana tena.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ikitupeleka nchini DRC, Sierra Leone na Ghana. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno "MISHEMISHE.”Leo ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani ambayo mwaka huu inajikita na maudhui ya “mustakabali wa ulinzi wa amani.”Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema walinda amani wa Umoja wa Matafa wako katika changamoto kubwa “Leo hii, walinda amani wanakabiliwa na hali zinazozidi kuwa ngumu katika dunia inayozidi kuwa na changamoto, ikiwemo uugawanyika na kutofautiana kwa mitazamo duniani kunazidi kuongezeka, operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa, hatari zaidi kutokana na wingi wa vitisho kama vile ugaidi na walinda amani kulengwa kwa makusudi kupitia taarifa potofu zenye madhara makubwa na changamoto zinazovuka mipaka kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi hadi uhalifu wa kimataifa.Kikosi cha 11 cha Tanzania kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimeungana na walinda amani wengine kuadhimisha Siku ya Walinda Amani Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika Mavivi, yakiongozwa na Brigedia Jenerali Diamond Meshack Madie, Mnadhimu Mkuu wa Vikosi vya MONUSCO.Shirika la Umja wa Mataifa la Mazingira UNEP limezindua mpango mpya wa dola milioni 15 kusaidia uwekezaji endelevu katika Bonde la Kongo – moja ya mifumo muhimu zaidi ya ikolojia duniani. Mpango huu unalenga kufungua fursa za biashara rafiki kwa mazingira kwa wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta za kijani. Msitu wa mvua wa Bonde la Kongo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kaboni duniani na ni makazi ya watu zaidi ya milioni 75, wakiwemo jamii za asili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "MISHEMISHE.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Matukio yame fanyika kote nchini Kuadhimisha Siku ya Kitaifa yakuomba msamaha 26 Mei, hatua ambayo ni kukiri kuondolewa kwa lazima kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza kutoka kwa familia na tamaduni zao.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya, na wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao. Makala tukwenda nchini Kenya kumulika ufukaji wa nyuki, na mashinani tunakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa IMO kuhusu Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia.Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu.Tangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.Katika makala tunaelekea Kajiado nchini Kenya, ambako juhudi za utunzaji mazingira kupitia mradi wa ufugaji wa nyuki unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa kushirikiana na idara ya misitu ya Kenya KFS hazichangii tu katika kukuza uchumi wa jamii, bali pia kulinda mazingira. Kupitia Makala hii iliyoandaliwa na Sharon Jebichii, Bwana Mureithi mmoja wa wanufaika wa mradi huo anaanza kwa kueleza mafanikio yao.Nakatika mashinani, fursa ni yake Arsenio Dominguez, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafirishaji Majini, IMO akitoa ujumbe wa ujumuishaji na usawa wa kijinsia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia ambayo huadhimishwa tarehe 18 mwezi Mei kila mwaka.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani, VoTAN uliofanyika wiki iliyopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), fursa ni yake Rawhiyeh, mkimbizi kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israel ambaye anasimulia kwa uchungu madhila yanayowakumba yeye na familia yake baada ya kupoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3 tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wake. Pia tunamulika hali ya msaada wa kibinadamu nchini Sudan.Kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari Mei 3, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari kila uchao huku teknolojia mpya ya akili mnemba au AI ingawa licha ya manufaa nayo pia inaibua hatari mpya kwenye uhuru wa kujieleza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, (WFP) tayari limeanza usambazaji wa chakula katika maeneo mbalimbali ya Sudan ambako watu wanakabiliwa na jaa huku wengine wakilazimika kuhama kambi moja hadi nyingine.Makala inamulika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Mei 3 ambayo mwaka huu ikijikita na athari za Akili Mnemba au AI katika uhuru wa habari za vyombo vya habari. Ili kufahamu AI inavyoleta mabadiliko katika vyombo vya habari hususan Afrika Mashariki ambako pia pengo la kidijitali ni kubwa."Na mashinani fursa ni yake Volker Turk Kamishna, Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito wa mshikamano dunia itakapoadhimisha kesho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
On election day the Australian Electoral Commission anticipates one million voters to pass through their voting centres every hour. Voting is compulsory for everyone on the electoral roll, so all Australians should familiarise themselves with the voting process before election day. - Siku ya uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Australia inatarajia wapiga kura milioni moja, watapita katika vituo vya kupiga kura kila saa moja. Ni lazima kupiga kura kwa kila mtu ambaye yuko katika sajili yakupiga kura, kwa hiyo wa Australia wote wana stahili jifahamisha na mchakato wa kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura.
Leo tarehe 30 Aprili dunia nzima inaburudika kwa pamoja kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Jazz, Kuanzia New Orleans hadi Nairobi, Tokyo hadi Tunis, miji inawasha taa majukwaani na mioyoni kusherehekea midundo yenye ladha ya kale, ya kisasa na yenye mvuto wa kipekee. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO linasema Jazz ni zaidi ya muziki, ni daraja la kuunganisha watu na kuleta utangamano. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini. Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata ya Umoja wa Mataifa inayolenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Je, wajumbe wa Umoja wa Mataifa hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na mmjoa wao Balozi Yabesh Monari wa Kenya, lakini kwanza ni muhtasari wa habari na ufafanuzi wa maneno.Mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio jipya la Urusi dhidi Ukraine lililosababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto na mwanamke mjamzito. Bwana Schmale amesema shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya makazi jijini Kyiv na maeneo ya jirani ni ukiukaji wa kutisha wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba matumizi haya ya nguvu yasiyo na maana lazima yakome.Wiki ya Chanjo Duniani ikiwaimeanza leo, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO, na la kuhudumia Watoto, UNICEF, na Ubia wa chanjo duniani, Gavi wametoa onyo kwamba milipuko ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo inaongezeka kwa kasi. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, anasema, “Chanjo zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 150 katika kipindi cha miongo mitano iliyopita. Kupunguzwa kwa ufadhili wa afya ya kimataifa kumeweka hatarini mafanikio haya yaliyopatikana kwa juhudi kubwa.”Na ikiwa pia leo Siku ya kimataifa wasichana katika Teknolojia ya mawasiliano, ICT, Mshauri wa masoko ya kidijitali nchini Kenya Maryann Mwangi akizungumza na washirika wetu Redio Domus amehimiza wasichana kujikita kwenye ICT kwani huu ndio mustakabali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri, kuhusu siku ya leo iliyoanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO mnamo mwaka 1995.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na harakati za utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Burundi, kulikoni?Hali si hali huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambako wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari za kiafya ambako panya na wadudu kama vile viroboto na nzi wamesambaa kutokana na mlundikano wa taka na ukosefu wa huduma muhimu kama vile maji safi na salama.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.Makala ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assumpta Massoi amezungumza na Rosemary Mwaipopo, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kiraia la DaySpring Foundation nchini Tanzania. Yeye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 uliofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita wa Machi.Na mashinanileo ikiwa leo ni siku ya afya duniani, kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus, fursa ni yake Padri Thaddeus Mukaya wa kanisa la katoliki la Parokia ya Embulbul ambalo pamoja na wadau wengine waliandaa huduma za bure za matibabu kwa wenyeji wa eneo hilo ili kusaidia jamii ambazo haziwezi kujimudu kimaisha.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Siku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha ulinzi wa raia na kupanua teknolojia na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea.Makala ambayo inamulika majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yamejikita na ufadhili wa maendeleo, Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid.Na mashinani leo utamsikia mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Bayero jimboni Kano nchini Nigeria anayeshiriki mkutano wa majadiliano ya ufadhili wa maendeleo endelevu unaofanyika Nairobi Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji, na wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Tanzania kwa mada hiyo hiyo ya elimu kuhusu usonji, na mashinani tunakwenda Gaza.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote.Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha.Makala leo kama tulivyokujulisha ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usonji, Assumpta Massoi anamulika jinsi shirika moja la kiraia nchini Tanzania linapigia chepuo harakati hizo.Na katika mashinani fursa ni yake Marah Hajjo, msichana mdogo kutoka Gaza huko Palestina Mashariki ya Kati ambaye anasimulia mabadiliko makubwa ya sikukuu ya Eid El Fitr ambayo mwaka huu ilighubikwa na kiza cha vifusi na mateso kutokana na mashambulizi kutoka Israeli.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Umoja wa Mataifa watuma salamu za rambirambi kufuatia tetemeko barani Asia.UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo, Tanzania.Makala ni kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kutozalisha Taka.Mashinani tunamulika ubunifu wa Janet Chemitei wa Tengeneza Cafe katika urejelezaji nguo nchini Kenya.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki takriban milioni 1.9.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa ya Bahari ya Atlantiki, ikiwakumbuka mamilioni ya Waafrika walioteswa, kunyanyaswa, na kunyimwa utu wao. Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kwa zaidi ya karne nne, mamilioni ya Waafrika walitekwa kwa nguvu, kusafirishwa kwa meli hadi mataifa ya kigeni, na kufanyishwa kazi katika hali mbaya za kikatili.”Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Lea mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa amekimbilia Burundi na familia anasilimua hali ilivyokuwa wakati wa kukimbia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.Viongozi wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel huko Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa kusitisha uhasama mara moja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha mshtuko na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usitishaji mapigano, kurejesha misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kuhakikisha kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka waliobaki.Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Bi. Anita Kiki Gbeho, na kuonesha wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo, akiwataka wahusika wote kuheshimu raia, wahudumu wa misaada, na miundombinu muhimu.Siku ya 7 ya mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, Tanzania ina tukio la kando kuonesha harakati za kumwinua mwanamke kiuchumi na miongoni mwa wazungumzaji ni Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Benki ya CRDB nchini Tanzania ambaye ameieleza Idhaa ya Umoja wa Mataifa ujumbe wake kwenye tukio hilo kuhusu walivyosaidia wanawake kuondokana na kikwazo cha kukosa dhamana wanapotaka kujikwamua kiuchumi.Na katika mashinani tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mkutano unaoendelea wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69, kusikia ujumbe wa mshiriki wa kuwaunga mkono wasichana na wanawake na kutokomeza ndoa za utotoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Against the backdrop of the Israel-Hamas war, incidents of Islamophobia in Australia have surged – whether verbal, physical or online. What's the lasting impact on victims, and what can be done? - Kufuatia vita vya Israel-Hamas, matukio yawa Islamu kunyanyaswa yame ongezeka nchini Australia, iwe kwa maneno, kimwili au mtandaoni. Athari ya kudumu kwa wa athiriwa ni gani, na nini kinaweza fanywa?
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Je, nini kinaweza kutokea kwa jamii ya Watanzania wote ikiwa wanaume wataamua kushikamana na kuungana ili kuvunja dhana potofu zinazochochea unyanyasaji wa kijinsia?Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, tulishiriki mazungumzo ya wazi na wanaume na wanawake wa jiji la Mbeya, tukijadili kwa kina:
Hii leo jaridani mada kwa kina ikimulika harakati za uhamasishaji kabla na baada ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni na mchango wa redio katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kuchagiza maendeleo ya jamii huko Ramogi nchini DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa maneno.Idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioingia Burundi kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, mashariki mwa DRC sasa imeongezeka na kufikia 20,000.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, limechapicha picha zikionesha wakimbizi walio njiani wakipikiwa chakula, wakati huu ambapo M23 wametwaa miji ya Goma jimboni Kivu Kaskazini, na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini.Na katika hatua nyingine ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikipatiwa jina UNJHRO imeripoti jinsi kutoroka kwa wafungwa kwenye gereza la Goma jimboni Kivu Kaskazini kulivyoleta hofu na mashaka kwenye jamii.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana mwenye umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kushuhudia sintofahamu na maombi ya wakazi wa Goma baada ya waasi wa M23 kutwaa mji huo. Mashinani tunakwenda Somalia na pia tunakuletea muhutasari wa habari.Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bruno Lemarquis, ametoa wito wa kufunguliwa haraka kwa Uwanja wa Ndege wa Goma. Amesema uwanja huu uliofungwa kutokana na mapigano kati ya vikosi vya jeshi la DRC na waasi wa M23 ni muhimu kwa usafirishaji wa misaada ya kibinadamu. Hospitali zimejaa na maelfu ya raia hawana msaada wa dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, (UNFPA), na la misaada ya kibinadamu na dharura (OCHA) leo yamesisitiza kuwa kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani kunawaacha mamilioni 'hatarini'. Hayo yakijiri tayari imefahamika kuwa Rais Donald Trump anaiondoa Marekani katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na pia kuacha kulifadhili shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Saratani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeeleza kiasi takwimu kuhusu ugonjwa huo kwamba mathalani kwa mwaka 2020 saratani ilisababisha vifo karibu milioni 10 sawa na kifo kimoja kati ya sita duniani. Aidha WHO imebainisha kuwa saratani zinazojitokeza zaidi ni saratani ya matiti, mapafu na utumbo mpana.Na katika mashinani fursa ni yake Safiya Jeylaani, mkazi wa Barawe katika Jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia ambye baada ya kuhudhuria hafla ya kujadili umuhimu wa upatikanaji wa huduma za afya kwa Wasomali wote katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa anasema jamii wanapaswa kuelimishwa kuhusu afya kutumia lugha mama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kutoka Sudan wengi wakiwa ni wanawake na watoto na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linawasaidia.Na katika mashinani Lodja Salizre, Mkimbizi wa ndani katika kambi ya Loda jimboni Ituri kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC akileleza ni kwa jinsi gani vita inayoendelea vimeameathiri yeye na familia yake na jinsi ambavyo uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo inavyosaidia maisha ya kila siku ya wakazi wake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox's Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza kuhusu vifaa mbalimbali ikiwemo msumeno wa mabomba, spana na kadhalika.ILOMradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox's Bazaar nchini Bangladesh.Na ndoto yake ni kwamba nikihitimu masomo nitakwenda kuungana na kaka yangu kwenye duka lake linalounza vifaa vya ujenzi. Nataka niwe mjasiriamali kama yeye, nijitegemee na nisaidie familia yangu. Siku hizi kwenye nyingi zilizoendelea na hata hapa Bangladesh wasichana wanafanya aina zote za kazi.Wanaweza kufanya kazi ngumu kama wanaume, nami nataka kuwa hivyo.Video ya ILO inamalizika mnufaika huyu amekamilisha kufunga bomba na sasa maji yanatoka, na mkufunzi anatumia maji hayo kunawa mikono.Malengo namba 4, 5, na 8 ya SDGs yanatekelezwaMradi huu ulizinduliwa mwezi Septemba mwaka 2023 ukifadhiliwa na…