Kenyan volleyball player
POPULARITY
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapema kwa Wote katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika kwenye jukwaa la kimataifa la Akili Mnemba na Tabianchi jijini Shanghai na kutoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mifumo ya tahadhari za mapema inayotumia akili mnemba ili kuzuia majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo amesema "tahadhari lazima zifikie kila mtu aliyeko hatarini kwa lugha wanazoelewa na mifumo ya mawasiliano wanayoweza kuiamini."Kesho Julai 18 ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, huko Geneva, Uswisi hii leo mashindano ya 18 ya Nelson Mandela ya Mahakama ya Kimataifa ya Kuigiza yamefikia kilele kwa timu ya Chuo Kikuu cha Midlands State kutoka Zimbabwe kuibuka mshindi ilihali Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya kimeshika nafasi ya pili.Hii leo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na marafiki wa mpira wa miguu au kabumbu, wamezindua kampeni ya mwaka mmoja ya Dunia Moja, Mchezo Mmoja, Lengo Moja kwa lengo la kutumia mpira wa miguu kama kichochea cha kuimarisha afya ya akili kwa vijana, tukio linalofanyika siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanaume. Akizungumza mapema kabla ya tukio hilo Sahira Al Nahari, ambaye ni Kiongozi kijana mchechemuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs amesema, "kwa hiyo, mpira wa miguu una mengi ya kutufundisha. Tunapokabiliwa na janga la kimataifa, hebu tuzielekeze fikra zetu kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Tunapotazama kinachotokea viwanjani, tunajifunza nidhamu, ustahimilivu, na jinsi ya kuinuka tena baada ya kupoteza jambo muhimu sana."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia malengo ya maendeleo endelevu, uhuru wa usafiri katika maji, na shughuli za Redio Miraya za kutumia redio kujenga amani na kutoa tahadhari za mapema za hali ya hewa nchini Sudan Kusini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi.Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho, Julai 9, ni miaka 15 tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake kutoka Sudan. Hata hivyo, matumaini ya amani yalitikiswa miaka miwili baadaye, mwezi Desemba 2013, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya serikali na makundi pinzani, hali iliyoendelea kuwaathiri mamilioni ya wananchi hadi leo. Katika juhudi za kurejesha amani, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Equatoria Magharibi, umezindua kampeni mpya iitwayo "Tusikilizeni, Chukueni Hatua Sasa" (Hear Us, Act Now), inayolenga kuimarisha maridhiano, mshikamano wa kijamii na kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa amani. Feissal Kirwa, kupitia video ya UNMISS, amefuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo na sasa anatuletea mada hii kwa kina.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili..Ripoti mpya ya hali ya saratani duniani kwa mwaka huu wa 2026 iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani (WHO) na shirika lake tanzu la utafiti wa saratani, IARC ikionya kuwa unyanyapaa ni moja ya vikwazo vya kutokomeza saratani wakati huu idadi ya wagonjwa ikikadiriwa kuongezeka maradufu ifikapo 2050, manusura wa saratani ya titi Abigael Hartz mkazi wa Ireland lakini anatokea Nigeria anasimulia alichoshuhudia alipotembelea hospitali moja ya kupima saratani Nigeria.Wiki mbili tangu matetemeko makubwa ya ardhi yapige mji mkuu wa Venezuela, Caracas na viunga vyake, idadi ya waliokufa imeripotiwa kufikia 3,685, majeruhi 16,740 na waliookolewa 6,462, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Msaada wa Dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko nchini humo na anasema.. “Hapa ni La Guaira, ambalo kwa hakika ndilo eneo lililokumbwa zaidi na janga hili. Nimekutana na mama mmoja aliyepoteza watoto wake watano waliokuwa kwenye jengo lililo kule. Bado anasubiri kwa matumaini, ingawa matumaini hayo yanazidi kufifia, kwamba huenda watoto wake bado wakapatikana wakiwa hai. Kwa hiyo, tupo hapa katikati ya vifusi na harufu ya miili ya waliopoteza maisha, tukijitahidi kuwafikishia manusura chakula, maji na huduma za matibabu, huku tukiwasaidia kuanza kufikiria namna ya kujenga upya maisha yao. Lakini safari ya kurejea katika hali ya kawaida bado ni ndefu sana.”wakati huu ambapo ripoti za vyombo vya Habari zinaeleza kuwa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo limekamilisha awamu mpya ya mashambulizi dhidi ya Iran, yakilenga zaidi ya maeneo 80 zikiwemo meli tatu za kibiashara zilizokuwa zinapita Mlango wa Bahari wa Hormuz huko Ghuba ya Uajemi, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari, IMO Arsenio Dominguez amelaani mashambulizi hayo mapya akionya kuwa kwa mara nyingine maisha ya mabaharia wasio na hatia yanawekwa hatarini.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili nampisha John Kibego wa redio washirika, Kazi Njema Redio nchini Uganda, kukueleza kuhusu harakati za kukuza lugha hiyo barani Afrika wakati huu ambapo UNESCO imeshaitangaza miaka mitano iliyopita kuwa lugha ya kimataifa.John, anamulika mpango wa ujenzi wa makao makuu ya kamisheni ya Kiswhaili ya Mungano wa Afrika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ikiwa leo ni maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili chini ya Kaulimbiu "Kiswahili kwa Amani, Mshikamano na Diplomasia ya Uchumi wa Dunia" Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Togolani Mavura anafafanua ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili inaweza kuyafanikisha hayo.Ugonjwa wa Ebola umeendelea kusambaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na idadi ya vifo vya watu imevuka 500 limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. Mwakilishi wa WHO nchini humo, Dkt. Anne Ancia akizungumza kwa njia ya video kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri mashariki mwa DRC ambako ni kitovu cha mlipuko huu, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwamba kufikia tarehe 4 mwezi huu, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imerekodi wagonjwa 1,561, vikiwemo vifo 506. Taarifa njema ni kuwa…“Jaribio la kitabibu lilianza tarehe 2 Julai kwa lengo la kubaini tiba madhubuti dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo.”Na asubuhi hii kwa saa za New York Marekani, kwa mara ya 34 tangu mwaka 1992, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekaa ili kujadili umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba tangu mwaka 1960. Katika barua ya mwaliko ambayo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amewapelekea wajumbe wa Baraza anasema, “ninayo heshima kukujulisha kwamba nimepokea barua iliyoambatanishwa ya tarehe 16 Juni 2026 kutoka kwa Mhe. Bwana Ernesto Soberón Guzmán, Mwakilishi wa Kudumu wa Cuba katika Umoja wa Mataifa, akiomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kujadili ajenda namba 38 yenye kichwa: “Umuhimu wa kukomeshwa kwa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tunaangazia fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo au kwa lugha ya kiingereza Internship hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Rashid Malekela kutoka Mwanza Tanzania, ambaye aliomba na kupata fursa hiyo anazungumzia na Leah Mushi wa Idhaa hii kueleza ni nini faida yake.Mashirika ya misaada nchini Ukraine leo Alhamisi Julai 2 yameongeza juhudi za kutoa msaada kufuatia ongezeko kubwa la mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Urusi usiku wa jana, yakiwemo yale yaliyolenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kuwa miongoni mwa mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa dhidi ya mji huo.Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa zama za sasa Ashwini K.P ameonya kuwa ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, ubaguzi dhidi ya jamii za pembezoni, na aina nyingine za kutovumiliana zinazohusiana na misingi hiyo bado vimejikita kwa kina katika ngazi zote za michezo duniani. Kwenye ripoti yake kwa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu, mtaalamu amesema michezo ina uwezo wa kukuza ujumuishi, usawa na mshikamano wa kijamii, lakini bado inaendelea kuakisi na kuendeleza mifumo ya ubaguzi wa rangi na kimaeneo unaoshuhudiwa katika jamii kwa ujumla.Na huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania kumeanza mdahalo wa siku mbili wa vijana na amani ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na mmoja wa washiriki anatoa maoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Ikiwa ni siku chache baada ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wasioona na viziwi inayoadhimishwa tarehe 27 Juni kila mwaka, Rashid Malekela wa Idhaa hii anakupeleka Mashariki ya Kati akimmulika mkazi mwenye ulemavu ambaye anakumbwa na changamoto katikati ya vita.Wakati harakati za uokozi na usaidizi zikiendelea nchini Venezuela baada ya matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1700 hadi sasa, leo hii ikiwa ni siku ya saba Emily Camargo akiwa kwenye kituo cha hifadhi kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jimboni La Guaira anaelezea alivyonusurika akisema, “kila kitu kilichonizunguka kiliporomoka na kunizingira, isipokuwa nilipokuweko. Nashukuru kwa sababu jengo la pembeni yetu halikuanguka. Hakuna kilichonipata. Hapa ndio tunalala, mimi, mume wangu , wifi yangu na mbwa wangu. Binadamu yangu na mpenzi wake hatujui waliko tumewatafuta hadi hospitalini, na kwenye orodha, hakuna dalili.”Jopo Huru la Kimataifa la Kisayansi la Umoja wa Mataifa kuhusu akili mnemba, limetoa ripoti leo inayoonesha kuwa teknolojia hiyo inaendelea kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi kuliko uwezo wa serikali kuandaa sera na kanuni zinazoendana nayo. Miaka michache iliyopita, akili mnemba ilikuwa ikitumika zaidi kujibu maswali au kuandika maandishi rahisi. Leo, teknolojia hii inaweza kutengeneza picha na video zenye uhalisia mkubwa na hata kufanya baadhi ya kazi bila usimamizi wa karibu wa binadamu lakini mifumo ya udhibiti na sheria za usalama haijafanikiwa kuendana na mabadiliko hayo.Baada ya miongo kadhaa hatimaye hii leo Umoja wa Mataifa umeondoa kanuni ya kifedha iliyokuwa ikiulazimisha kurejesha kwa nchi wanachama fedha ambazo hazikutumika hata kama fedha hizo hazikuwa zimewasilishwa kabisa. Uamuzi huo uliofanywa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne unafuatia mapendekezo ya Kamati ya Tano, ya Baraza hilo ambayo inashughulikia masuala ya utawala na bajeti. Kanuni ilikwamisha ajira ndani ya Umoja wa Mataifa na operesheni za ulinzi wa amani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kuwa kanuni hiyo ilikuwa inahatarisha uthabiti wa Umoja wa Mataifa na kwa uamuzi huu, Baraza limeanzisha mbinu mpya itakayohakikisha kuwa fedha ambazo hazijatumika zinarejeshwa kwa nchi wanachama pale tu zinapokuwa zimewasilishwa taslimu na kupokelewa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGURU."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGURU."
What does it truly mean for the Church to be a place where everyone belongs?In this message, Rev. Dr. Phidel challenges the Church to move from pity to belonging by embracing people with disabilities, caregivers, and families with hidden pain as valued members of the Body of Christ.#ChurchForEverybody #DisabilityInclusion #citamchurchonline #ChurchEveryday
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka mjini Caracas nchini Venezuela, mshikamano na raia wa nchi hiyo wadhihirika wakati huu wakiwa kwenye majonzi baada ya matetemeko ya ardhi kukumba wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Nchini Venezuela Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa msaada kufuatia matetemeko mawili ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo wiki iliyopita. Mathalani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limeripoti leo kwamba tayari limetoa zaidi ya tani elfu tatu za chakula, kiasi kinachotosha kusaidia familia zaidi ya elfu kumi kwa kipindi cha miezi miwili.”Huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC, raia wameelezea haki zao zinazokiukwa ikiwemo kuzuiwa kupatiwa misaada ukatili wa kingono na mauaji. Maelezo hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa inayochunguza hali ya haki za binadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ikiwa ni ripoti yao ya kwanza mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi?”.Na, michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu inaendelea huku dunia ikishuhudia ongezeko la joto kali. Katika juhudi za kulinda wachezaji, wafanyakazi na mashabiki dhidi ya athari za joto, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “WHO tunashirikiana na FIFA na nchi zinazoandaa michuano hiyo katika kampeni iitwayo Beat the Heat inayolenga kuweka mipango ya utekelezaji, kutoa elimu kwa wananchi, kuanzisha mifumo ya tahadhari za mapema, kuboresha upatikanaji wa maji salama ya kunywa, pamoja na kuweka maeneo ya kujipooza.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Caregiving is a sacred act of love, but even the strongest caregivers need grace, rest, and support. In this episode, Rev. Phidel shares a biblical encouragement for those carrying the weight of caring for others and reminds us that God sees every sacrifice made in love.#citamchurchonline #ChurchEverydayGet in touch with us:http://www.citam.org/churchonline@citam.org(+254) 784 277 277(+254) 728 221 221
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Leah Mushi ameketi chini na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nassriya Nassir Ali akieleza safari yake ya uongozi wa nafasi za umma kupitia mkalimani wake wa lugha ya alama Tusajigwa Ernest. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari na jifunze Kiswahili.Janga la tabianchi linakaribia kwa kasi zaidi kuliko inavyodhaniwa ameonya leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, huku akitoa wito wa hatua saba za haraka kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuachana na matumizi ya mafuta ya kisukuku. Akizungumza mjini London kwenye mkutano wa hatua dhidi ya tabianchi, ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na Serikali zichukue hatua madhubuti za tabianchi, dunia iongeze matumizi ya nishati safi, ilinde jamii zilizo hatarini, ihakikishe ufadhili wa haki kwa nchi zinazoendelea, isimamie kwa uwajibikaji matumizi ya teknolojia ya akili mnemba na kupambana na upotoshaji wa taarifa kuhusu tabianchi. Guterres amesema hatua hizo ni muhimu ili kudhibiti ongezeko la joto duniani na kuzuia madhara makubwa zaidi kwa binadamu na mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limekaribisha makubaliano mapya kati ya DRC na Rwanda ya kusaidia wakimbizi kurejea nyumbani kwa hiari, usalama na heshima. Katika mkutano uliofanyika Addis Ababa Ethiopia, serikali za nchi hizo mbili zimeahidi kuimarisha ushirikiano kwa msaada wa UNHCR ili kuwezesha urejeaji salama wa wakimbizi.Zaidi ya wagonjwa 1,000 vya Ebola wamethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku watu 254 wakifariki dunia kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO likiongeza kuwa wagonjwa 100 wamepona, jambo linaloonesha kuwa huduma ya afya ya haraka inaweza kuokoa maisha.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "TANUWINI"Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "TANUWINI"
In today's episode, Rev. Phidel reflects on what it means to be truly seen by God amid disability, neurodivergence, caregiving, and hidden pain. Discover how the Church can foster understanding, dignity, belonging, and compassionate support for every individual and family.#citamchurchonline #ChurchEverydayGet in touch with us:http://www.citam.org/churchonline@citam.org(+254) 784 277 277(+254) 728 221 221
Life doesn't always unfold the way we prayed, planned, or expected. In this powerful reflection, Rev. Dr. Phidel explores how faith can remain strong even when life feels unfair. Addressing disability, caregiving, hidden pain, and unanswered questions, this message offers biblical encouragement for families, caregivers, and anyone carrying heavy burdens.#FaithWhenLifeFeelsUnfair #FaithInHardTimes #CITAMChurchOnline #ChurchEveryday
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho kutwa Alhamisi ya Juni 11, macho na masikio yanaelekezwa Mexico, Canada na hapa Marekani kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu, au soka al maarufu kabumbu. Ingawa hivyo zama za sasa za mchezo huo maarufu zaidi duniani zinakumbwa na madhara ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Ongezeko la joto kali linavuruga mechi na kuzua wasiwasi kuhusu mustakabali wa mchezo huo. Ni kwa kuzingatia hilo, Sekretarieti ya Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC inamulika suala hilo na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwani hivi sasa madhara ya joto kali kwenye kabumbu ni dhahiri. Feissal Kirwa anamulika hilo kupitia video iliyoandaliwa na UNFCCC.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Takriban watoto milioni 138 duniani kote bado wako katika ajira za watoto, wakiwemo watoto milioni 54 wanaofanya kazi hatarishi. Hayo yamo katika ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO. Katika ujumbe wakwe kwenye ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert F. Houngbo, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kubadili hali hii.“Habari njema ni kwamba hadi sasa tuna wagonjwa 19 ambao wamepona, hivyo utambuzi wa mapema na matibabu vinaokoa maisha,” Huyo ni Mkurugenzi wa Operesheni za Tahadhari na Hatua za Dharura za Afya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO), Dkt. Abdirahman Mahamud, akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo kwa njia ya video kutoka Bunia katika Jimbo la Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, jimbo ambalo linachangia asilimia 94 ya wagonjwa wote wa Ebola.Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umeanza leo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York na utaendelea hadi 11 Juni. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu? Ili kupata majawabu Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameendelea kusisitiza umuhimu wa ugunduzi wa mapema kwani hatua zikichukuliwa haraka wagonjwa wa Ebola wanapona. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Geneva Usiswi baada kurejea kutoka ziarani mashariki mwa DRC amesema, Kufikia sasa, watu sita wamepona nchini DRC na wawili nchini Uganda, jambo linaloonesha kuwa watu wanaweza kupona Ebola iwapo watapata huduma za afya na kwenda vituo vya afya mara tu wanapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.Kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA wiki ijayo hapa Marekani na katika nchi jirani, Canada na Mexico, Shirika la Afya la Nchi za Amerika (PAHO) limetoa wito kwa nchi za bara la Amerika kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa wa surua na Rubella kufuatia mikusanyiko mikubwa inayotarajiwa na milipuko inayoendelea ya surua na ongezeko la safari za kimataifa vinaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo. Shirika hilo linazitaka mamlaka za afya kubaini maeneo yaliyo katika hatari kubwa na kuimarisha hatua za kukabiliana haraka ili kuzuia maambukizi zaidi. Na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani wanachagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028. Kutoka Barani Afrika mgombea mmoja ni Zimbabwe ambaye hata hivyo anatarajiwa kupita kwani hana mpinzani katika nafasi hiyo. Nchi zitakazochaguliwa zinachukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Mtalaam wetu Onni Sigalla kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA anafafanua maana ya neno “CHOTORA”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu.Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema baada ya kuthibitisha kuanza kwa hali ya El Niño, ukionya kuwa mabadiliko hayo ya joto la Bahari ya Pasifiki yataleta viwango vya juu vya joto kuliko kawaida karibu kila mahali duniani kati ya mwezi Juni mpaka Agosti na kuchochea matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani WMO, Celeste Saulo amesema "Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu El Niño ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa duniani na mifumo ya mabadiliko ya tabianchi, bahari yenye joto, huongeza joto na unyevu kwenye mfumo wa hali ya hewa ambao unaweza kutumika kuzidisha hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na joto kali, na mvua kubwa.”.'Zinakaribia siku 100 sasa tangu kuanza kwa mzozo wa Mashariki ya Kati ambao athari zake zimesambaa duniani kote kwani umevuruga njia za usafirishaji na umeongeza gharama za usafiri na kuchelewesha utoaji wa huduma muhimu. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limeeleza kuwa fedha nyingi sasa zinatumika kwenye usafirishaji badala ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto. Gharama za kusafirisha chanjo kwenda baadhi ya nchi barani Afrika zimeongezeka kwa hadi asilimia 70, huku gharama za kusafirisha chakula tiba, na vifaa vya elimu, nazo zikipanda kwa kiwango kikubwa. Shirika hilo linaonya kuwa hali hiyo inalazimisha kufanya maamuzi magumu kuhusu ni watoto gani wapate msaada kwanza". Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC na Uganda mwezi uliopita wa Mei ambapo mpaka sasa watu 49 wamepoteza maisha, 48 nchini DRC na mmoja nchini Uganda. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza jumuiya za kimataifa kutoa usaidizi unaohitajika ili kudhibiti mlipuko. Pia amelihimiza nchi kutoweka vikwazo vya usafiri kwa DRC, ili kuhakikisha msaada wa kiafya na kibinadamu unaweza kufikia kiwango kinachohitajika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "CHOTORA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililohudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Amon Manyama, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania. Rashid Malekela wa Idhaa hii alituwakilisha na amezungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno kama neno "PEKEPEKE."Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa UNCERF umetoa dola milioni 60 kusaidia muitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC. Tayari vifaa tiba vimewasilishwa nchini humo na sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine wanaendelea na usaidizi ikiwemo kuweka vituo vya kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi na kuhakikisha utunzaji salama wa wagonjwa..Mwakilishi wa mpya wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Togolani Mavura amewasilisha rasmi nyaraka zake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jijini New York Marekani na kueleza yale aliyokuja nayo.shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema fedha zinazotumwa nyumbani na watu waishio ughaibuni au diaspora sasa zimezidi kiwango cha fedha za misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. IOM imeeleza pia namna diaspora walivyo na msaada mkubwa wakati wa majanga kwa kutuma fedha haraka, huduma na usaidizi kupitia mitandao ya kuaminika katika nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Haiti, Ufilipino na Ukraine.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mlipuko wa Ebola nchini DRC na Uganda na ujumbe wa Profesa Mohamed Yakub Janabi Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika kuhusu hatua WHO inachukua kudhibiti ugonjwa huo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo..Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya video kwa washiriki wa Mkutano wa 79 wa Baraza la Afya Duniani ulioanza leo mjini Geneva, Uswisi amesema changamoto za afya duniani hazijawahi kuwa kubwa kiasi hiki na hivyo akawakumbusha wahudhuriaji kwamba mkutano huu ni fursa muhimu kwa Mataifa Wanachama kuoanisha na kuharakisha juhudi za kukabiliana na changamoto za afya duniani..Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa nchi za Afrika kuwajumuisha wakimbizi, watu wasio na uraia, na wale walio katika hatari ya kukosa uraia katika mifumo ya kitaifa ya vitambulisho vya kidijitali. UNHCR imetoa ushauri huo katika mkutano wa ID4Africa uliofanyika mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Nchi za Kenya na Uganda ni miongoni mwa nchi zilizotumika kama mfano mzuri..Na kundi la watoto kutoka nchi mbalimbali lililotumia miezi 15 kuandaa muongozo waliouita ‘Tujumuisheni' wakilenga kushughulikia upungufu katika ushiriki bora wa watoto kwenye uamuzi wa msuala mbalimbali kwa ngazi zote, wametoa wito kwa mashirika yanayofanya kazi na watoto na vijana kuutumia muongo wa viwango hivyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya.''
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Côte d'Ivoire ambako wakulima wameshuhudia kuimarika taratibu kwa uzalishaji wa kakao baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kusaidia wakulima nchini humo kurejesha ardhi katika ubora wake na kuongeza uzalishaji kupitia mbinu endelevu za kilimo mseto cha misitu, mazao na mifugo..Afrika imekuwa mstari wa mbele kushinikiza mfumo mpya wa kifedha unaozingatia usawa kwa nchi zinazoendelea. Na leo katika mkutano wa kuangazia mustakbali wa Afrika, Africa Forward huko Nairobi nchini Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezipongeza nchi za Afrika kwa kuongoza juhudi hizo za mageuzi ya mifumo ya fedha duniani. Kuhusu utajiri wa madini yanayopatikana Afrika kunufaisha nchi nyingine nje ya bara hilo Guterres amesema “Hakuna tena unyonyaji wala uporaji. Watu wa Afrika lazima wanufaike kwanza, na zaidi kutokana na rasilimali za Afrika.”.Taarifa mpya kuhusu virusi vya hanta ni kwamba hadi sasa wagonjwa walioripotiwa ni 11, na watu watatu wamefariki dunia. Kati ya wagonjwa hao, tisa wamethibitishwa kuwa na virusi vya Andes huku wawili wakihesabika kuwa wagonjwa wanaoshukiwa lilesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. WHO pia wameipongeza serikali ya Hispania kwa ushirikiano wake katika mchakato mzima wa kuwaondoa salama na kuwarejesha makwao abiria takriban 150 kutoka nchi 23 waliokuwa katika meli ya kitalii ya MV Hondius ambapo humo ndio mlipuko wa hanta ulipotokoea.ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hivi karibuni kuhusu Malengo ya Misitu Duniani, Global Forest Goals kwa mwaka 2026 ikieleza bayana kuwa misitu ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha uhakika wa chakula na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu duniani. Nchini Kenya mkazi mmoja ameeleza bayana jinsi wanavyonufaika na msitu asili wa Ngong ulioko takribani kilometa sita kutoka mji mkuu Nairobi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya''Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Hanta kwenye meli ya kifahari ya Hondius kutoka Argentina na kulazimika kutia nanga nchini Cabo Verde, hii leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliosababisha hadi sasa vifo vya watu 3 wakiwemo wanandoa wawili unaendelea.Tukisalia na mlipuko huo wa virusi vya Hanta, Mwakilishi wa WHO nchini Cabo Verde amesema hivi sasa meli hiyo Hondius iko njiani kuelekea visiwa vya Canary nchini Hispania, “na kwenye meli tuna daktari wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna madaktari wawili wa Kiholanzi ambao wameimarisha timu, na kuna mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mlipuko ambaye atasafiri na meli hadi bandari inayofuata ambayo ni visiwa vya Canary. Kwa sasa hakuna mtu mgonjwa kwenye meli, lakini iwapo mtu ataugua, basi kutakuwa na madaktari na vifaa vya matibabu vya kuwahudumia wakati wa safari.”Nchini Tanzania hivi karibuni ripoti ya uainishaji wa viwango vya upatikanaji wa chakula nchini humo iliyoandaliwa kwa pamoja na serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO ilieleza kuwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri za wilaya za Same, Maswa na Monduli yako katika kiwango cha tatu yaani (IPC 3).Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
How does a Christian missionary, fully devoted to spreading his faith across the world, end up becoming an Orthodox Jewish rabbi?Meet Rabbi Gershom Baraza, who grew up in Spain and went all in on his mission, even learning Chinese to teach Christianity. But along the way, something didn't sit right. What began as small questions turned into a relentless search for truth, forcing him to reevaluate everything he believed. His journey is a powerful reminder of what it means to truly seek the emes, no matter where it leads.More from Rabbi GershomPhone: https://keyphone.tech/Hechsher: https://www.koshercertification.cn/en/pages/our-rabbisShul: https://www.brightonshule.org.au/about-us✬ SPONSORS OF THE EPISODE ✬► Hiring4Less: The Smart Way To Grow Your BusinessHire a full-time remote employee for only $7 an hour. Get huge talent at a low cost with overseas employees and no lock in contracts.→ Call, Text or WhatsApp: 845-682-0990→ Visit: https://hiring4less.com/](https://hiring4less.com/► Bitbean: Software Built RightAI can move fast, but without the right people behind it, it can break your business just as quickly. Bitbean builds powerful, reliable systems designed by real engineers who understand your business first, then use AI to accelerate the process.→ https://bitbean.com/► Hodu Lashem: Don't Forget The GoodStart noticing the moments of hashgacha in your life by writing them down. Build your own HoduLashem file and strengthen your emunah one moment at a time.→ https://bit.ly/LivingLchaim► Wheels To Lease: #1 Car CompanyFor over 35 years, Wheels To Lease has offered stress-free car buying with upfront pricing, no hidden fees, and door-to-door delivery.→ CALL/TEXT: 718-871-8715→ EMAIL: inspire@wheelstolease.com→ WEB: https://bit.ly/41lnzYU✬ IN MEMORY OF ✬This episode is in memory of:• Miriam Sarah bas Yaakov Moshe• Shimon Dovid ben Yaakov Shloima#iftnLchaim.#jewishpodcast #judaism #conversion #faith #truth #torah #emunah #christian #spain #china #israel #australia
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba 2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo juzi Jumanne na jana Jumatano wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipata fursa kunadi serra zao mbele ya nchi wanachama kwenye Baraza Kuu wakiwemo wawakilishi wa asasi za kiraia walioweza kuwauliza maswali. Miongoni mwa wawakilishi hao ni Irene Kitoti, Mwanzilishi na mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Genesis For Children Organization ya nchini Tanzania aliyezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Kutokana na mafanikio ya kihistoria kwa afya ya umma ya eneo la Karibe, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO limeipongeza nchi ya Bahamas kwa kuwa taifa la hivi karibuni zaidi katika ukanda huo wa Karibe kuthibitishwa kuwa limekomesha maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus, kupitia taarifa ya shirika hilo ameipongeza Bahamas kwa mafanikio haya makubwa, yanayoimarisha miaka ya dhamira ya kisiasa na kujitolea kwa wahudumu wa afya.Ikiwa leo imetimia miaka 15 tangu kuanza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika Teknolojia ya Habari na Mawasilino, TEHAMA au ICT, Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano (ITU), Doreen Bogdan-Martin katika ujumbe wake mahususi wa maadhimisho ya mwaka huu amesema, “kwa sasa tunaishi katika kipindi cha mabadiliko makubwa na ya kusisimua zaidi ya kiteknolojia katika historia ya binadamu lakini vilevile kwa sasa fursa zinazohusiana na mabadiliko haya ya kiteknolojia hazimfikii kila mtu kwa usawa”.Mgogoro wa usafirishaji katika Mlango Bahari wa Hormuz uliosababishwa na vita vya Mashariki ya Kati umefichua tishio jipya: upungufu wa madini ya kimkakati yanayoendesha uchumi duniani kote na sasa nchi huenda zitaanza kuhaha kuyapata. Katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Geneva Uswisi, Dario Liguti, Mkurugenzi wa Kitengo cha Nishati Endelevu cha Tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya, UNICE amesema, “hatua ya kwanza, mbali na ongezeko la bei bila shaka, itakuwa viwanda kupunguza matumizi yake yake ya madini ya kimkakati na hivyo kupunguza uzalishaji… iwe ni paneli za sola, sumaku, betri na kadhalika, katika siku zijazo.”Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUPARAMA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUPARAMA."
Are we truly living like Jesus is alive? As we walk in the newness of life, resurrection becomes visible through compassion, inclusion, and genuine love for one another. This message challenges us to build a Christ-centered community where everyone belongs, is valued, and is embraced as part of God's family.#FaithThatWelcomesAll #Revival #CITAMChurchOnline #ChurchEveryday
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA"
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mmoja wa walioshiriki mkutano wa CSW70, Masidis Scholastica Madowo Mbunge katika Bunge la Kaunti ya Siaya akiwakilisha kata ya South East Alego jimbo la Magharibi mwa Kenya, ili kuangazia kile anachokifanya kwenye Kaunti yake kuhakikisha wanawake wanapata haki hizo.Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kutafanyika mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja huo ambapo wagombea wanne wamejitokeza kuwania wawili wanaume na wawili wanawake. Wagombea hao ni Michelle Bachelet kutoka nchini Chile, Rafael Grossi kutoka nchini Argentina, Rebeca Grynspan kutoka Costa Rica, na Macky Sall kutoka nchini Senegal.Wakati huo huo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amesema mchakato wa kumchagua Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu itakayoamua mwelekeo wa taasisi hiyo na mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kabla ya kuanza kwa mdahalo huo wa wazi, Baerbock ameeleza kuwa uchaguzi huo una umuhimu mkubwa duniani kote, ukigusa maisha ya zaidi ya watu bilioni nane, “Uamuzi huu si wa kiutawala tu, bali ni ujumbe kuhusu maadili na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo.”Takribani wahamiaji 8,000 waliripotiwa kufariki dunia au kutoweka duniani kote mwaka 2025, na kufanya jumla ya wahamiaji waliopoteza maisha tangu 2014 kufikia zaidi ya watu 82,000, hii imebainishwa katika takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Takwimu hizo pia zinaonesha athari kubwa kwa familia, ambapo takribani watu 340,000 wameathirika moja kwa moja. IOM imeonya kuwa njia za uhamiaji si salama na zinazidi kuwa hatari.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Mtaalam wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UNYUMBA" Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
In this message, Rev. Phidel reminds us that God often works in quiet ways, not just in dramatic moments. Miracles can look like peace, strength for one more day, and steady progress that may go unnoticed but is never unseen by God.#citamchurchonline #ChurchEverydayGet in touch with us:http://www.citam.org/churchonline@citam.org(+254) 784 277 277(+254) 728 221 221
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Waziri wa sheria na ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Emmanuel Ugirashebuja amezungumza na Idhaa hii na anaeleza siri ya wananchi wa Rwanda kuweza kuishi kwa amani baada ya mauaji hayo.Kama mapigano yataendelea nchini Sudan hadi mwaka 2030, umaskini wa kupindukia unaweza kuongezeka na kuvuka asilimia 60, huku watu wengine milioni 34 wakitumbukia kwenye ufukara, imesema Ripoti ya uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliyotolewa leo Sudan na Marekani ikiwa kesho inatimia miaka mitatu kamili tangu kuanza kwa vita.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa kauli zao tofauti tofauti kuhusu miaka mitatu ya vita nchini Sudan ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto wanaendelea kulipa gharama ya vita kwani zaidi ya watoto 245 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu Januari hadi Machi mwaka huu, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani au droni yamesababisha takriban asilimia 80 ya majeruhi na vifo hivyo.Mzozo wa Israeli na Lebanon ulioshika kasi baada ya wapiganaji wa Hezbollah kushambulia Israeli kupinga hatua ya Marekani na Israeli kushambulia Iran, hii leo huko Washington DC, hapa Marekani kunafanyika mazungumzo kati ya Israel na Lebanon. Umoja wa Mataifa unasihi pande zote kutumia diplomasia kumaliza uhasama na kusongesha azimio namba 1701 la Baraza la Usalama linalozuia mapigano mpakani mwa mataifa hayo mawili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUDA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KUDA"
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kia inayotorejesha katika mkutano wa CSW7O amabko Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku ya 31 , zaidi ya watu 200,000 wamevuka mpaka wa Lebanon na kuingia Syria tangu mashambulizi baina ya Israeli na Hezbollah yaanze mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya Marekani na Israeli kushambulia Iran. Ripoti mpya ya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, inaonya kuwa idadi kubwa ya watu nchini Iran inaweza kutumbukia kwenye umaskini kadri misukosuko ya kiuchumi inavyozidi kuathiri maisha ya kila siku. Shirika hilo linasema hali hiyo inahatarisha kufuta mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka kadhaa, huku Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kikitarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa sawa na kupotea kwa zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, leo limeomba dola milioni 277 kusaidia watu walio hatarini zaidi waliokumbwa na mizozo na ukosefu wa makazi nchini Sudan na nchi jirani kwa mwaka huu wa 2026, wakati mgogoro huo ukikaribia kuingia mwaka wake wa tatu. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope ameonya kuwa familia zinakabiliwa na “chaguo ngumu lisilowezekana kati ya kubaki bila huduma muhimu au kurejea katika jamii zilizosambaratishwa na vita”. Fedha hizo zitatumika kuimarisha mifumo ya kibinadamu, kupanua njia za misaada, na kuimarisha operesheni za kuvuka mipaka ili kusaidia waathirika kuishi na kujijenga upya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."
Hii leo jaridani mwenyeji wako Flora Nducha anamulika Mashariki ya Kati, mzozo Sudan Kusini unavyoendelea kuleta machungu kwa raia. Ingawa hivyo kuna habari njema ya jinsi FAO inavyoleta nuru kwa wakulima nchini Somalia kwa kukarabati mifereji ya umwagiliaji. Karibu!===========================Vita huko Mashariki ya Kati vinaendelea leo ikiwa ni siku ya 28, mashambulizi yanasababisha hofu, mateso, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu katika eneo lote. Huko Geneva, Uswisi wanadiplomasia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo wanajadili shambulizi la shule lililotokea Minab, Iran, ambalo limeua zaidi ya watoto 100. Leah Mushi anasimulizi hii ya kusikitisha.Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudani Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Rashid Malekela anatupeleka kufahamu maisha ya wakimbizi huo yapoje?Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.
Katika mjadala wa dharura kuhusu “shambulizi la anga dhidi ya Shule ya Wasichana ya Shajareh Tayyebeh huko Minab, nchini Iran, Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limejadili tukio hilo kama ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu.”Mjadala huu wa dharura unafanyika kufuatia tukio hilo lililotajwa kuwa la kutisha lililofanyika siku ya kwanza kabisa ya mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran. Simulizi ya mamaTuanze na simulizi ya Mohaddeseh Fallahat, huyu ni mama wa Iran aliyepoteza watoto wake wawili katika shambulizi hilo ambaye anasema “asubuhi ile ilikuwa kama kawaida.” Aliwafunga wanawe gidamu za viatu na kuwavalisha mabegi mgongoni na hakukuwa na dalili yoyote kwamba hiyo ingekuwa mara ya mwisho, kuonana nao.Anasema “Walipotoka mlangoni, waliniambia, ‘Mama, njoo utuchukue baada ya shule.' Sentensi hiyo rahisi sasa inajirudia akilini mwangu mara elfu moja, na kila mara moyo wangu unaungua kwa maumivu. Hakuna mama anayewahi kufikiria atampeleka mtoto wake shuleni kwa tabasamu, kisha akumbane na ukimya. Hakuna mama aliyejiandaa kusikia maneno haya: ‘Mtoto wako hatarudi tena.'” © Mshiriki Jengo moja katika eneo la mashariki mwa Tehran likionesha dalili za uharibifu uliosababishwa na mabomu.WaokoajiAkizungumza na waandishi wa habari huko Geneva akiwa Tehran kupitia mawasiliano ya satelaiti, Mkuu wa shirika la Msalaba mwekundu na Hilal nyekundu IFRC, Maria Martinez amesema zaidi ya watu 1,900 wameuawa, wakiwemo wanawake na watoto, na takriban watu 20,000 wamejeruhiwa.Martinez amesimulia masahibu yanayowakuta watoa huduma ya kwanza “Moja ya nyakati za kushtusha na kuvunja moyo ni pale mhudumu wa uokoaji na utafutaji alipogundua miili ya wafamilia yake mwenyewe chini ya vifusi vya jengo lililoshambuliwa.Katika mji wa Qom, kusini mwa Tehran, mhudumu mwingine aliokoa mwili wa shangazi yake pamoja na mume wake na mtoto wao mdogo.” Huo ndio uhalisia wanaokumbana nao wahudumu wa kibinadamu, wanaokoa maisha huku wakibeba maumivu makubwa yasiyovumilika ya kupoteza wapendwa wao.UN GenevaMjadala wa Baraza la Haki za Binadamu ukifanyika Geneva UswisiKauli ya UNTofauti zozote zilizopo kati ya nchi na nchi, sote tunaweza kukubaliana kuwa hazitatatuliwa kwa kuwaua wanafunzi.Akizungumza katika mjadala huo wa dharura, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito kwa mamlaka za kijeshi za Marekani kuchapisha haraka iwezekanavyo matokeo ya uchunguzi wao kuhusu shambulizi hilo. Türk amesema “Mashambulizi ya mabomu katika Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab yameibua hofu kubwa na maumivu makali. Picha za madarasa yaliyoharibiwa na wazazi waliogubikwa na huzuni zinaonesha wazi ni nani hulipa gharama kubwa zaidi ya vita: raia wasio na uwezo wowote katika maamuzi yaliyopelekea mzozo. Katika tukio hili, inaripotiwa kuwa wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa shule, na wapendwa wao 168 wameathirika.Maafisa waandamizi wa Marekani wamesema shambulizi hilo linafanyiwa uchunguzi. Natoa wito mchakato huo ukamilike haraka iwezekanavyo, na matokeo yake yawekwe wazi kwa umma. Lazima kuwe na haki kwa madhara makubwa yaliyosababishwa.”
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "NYAPANYAPA" katika muktadha wa uwindaji.Bwana Sigalla anasema "nyapanyapa ni tabia ya mwindaji ambayo anatembea kwa kunyata sana, pole pole ili asisikike wakati anawinda.Anakuwa ananyemelea. Lengo ni kuhakikisha anamsogelea mnyama ama kumshika au kuweza kuwinda mnyama vizuri."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo baada ya takribani wiki mbili mkutano wa 70 wa CSW70 unakunja jamvi. Maudhui yalikuwa kuendeleza Haki, Sheria na Kuchagiza Hatua kwa ajili ya wanawake na wasichana, na sasa washiriki wanaeleza Idhaa hii wanachoondoka nacho.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Brussels Ubelgiji kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati akiwa a na Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya António Costa, ametoa ujumbe mahsusi kwa wahusika wakuu wa mzozo huo. Amesema “Kwanza kwa Marekani na Israel, ni wakati muafaka kumaliza vita hivi ambavyo viko hatarini kutodhibitiwa kabisa, vikisababisha mateso makubwa kwa raia, na athari zake zinaenea katika uchumi wa dunia kwa kiwango cha kutisha, zikiwa na uwezekano wa kusababisha madhara makubwa zaidi hasa kwa nchi zenye maendeleo duni”Kisha ujumbe wake wa pili ni “Kwa Iran, acheni kushambulia majirani zenu. Hawakuwa sehemu ya mgogoro huu. Baraza la Usalama limelaani mashambulizi haya na kuamuru yasitishwe, pamoja na kuagiza kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.”Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Furaha hapo Kesho Machi 20 raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo lililoghubikwa na mizozo ya silaha wanaeleza furaha kwao inamaanisha nini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEMBUA" . Kama umezoea kuwa unapembua mchele basi fahamu kuna zaidi ya maana hiyo. Karibu.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kesho Ijumaa tarehe 13 Februari ikiwa ni ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikijikita katika Redio na Akili tunakupeleka mashariki mwa DRC, kwa George Musubao kutoka Televishen na Radio washirika Canal Victoire Du People Kasindi.Leo tarehe 12 Februari ni siku ya Kimataifa ya Kuzuia Itikadi Kali Zinazochochea Ugaidi, ikiwa ni maadhimisho ya nne tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu kauli mbiu inasema “Kuzuia ugaidi wa kikatili katika enzi ya teknolojia mpya na zinazoibuka”. Ugaidi na itikadi kali vinaendelea kuwa tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia, huku vikigusa watu wa rika, dini na tamaduni mbalimbali na ndio maana Umoja wa Mataifa unasema ingawa teknolojia kama akili mnemba au AI, mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali inaweza kusaidia juhudi za kuzuia misimamo mikali, pia inatumiwa na magaidi kueneza chuki, upotoshaji na kuhamasisha vurugu ndio maana shirika hilo linahimiza ushirikiano wa kimataifa, matumizi ya teknolojia kwa uwajibikaji na suluhisho shirikishi zinazoheshimu haki za binadamu ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali.Barani Ulaya ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametoa tamko kali akilaani mashambulizi ya mfululizo yanayofanywa na nchi ya Urusi dhidi ya mifumo ya nishati nchini Ukraine. Taarifa iliyotolewa leo kutoka Geneva, Uswisi, imeeleza kuwa mashambulizi hayo yanawanyima raia mahitaji muhimu ikiwemo mifumo ya kupasha joto, maji, na umeme katikati ya msimu wa baridi kali uliopitiliza.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo wiki ijayo, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe akisema kuwa “Katika zama hizi ngumu na za mgawanyiko, hebu tuitikie wito wa stahmala wa Ramadhani. Kuziba pengo la mgawanyiko. Kufikisha msaada na matumaini kwa wale wanaoumini. Na kulinda haki na utu wa kila mtu…..Hebu Mwezi huu Mtukufu ututie hamasa ya kufanya kazi pamoja ili kujenga dunia yenye amani zaidi, ukarimu na haki kwa watu wote. Ramadhani njema.”Na Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UNGUKA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!