POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya hospitali ya Médecins Sans Frontières (MSF) huko Old Fangak, Jimbo la Jonglei mapema majuzi asubuhi ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takribani raia saba na kujeruhi wengine. Shambulio hilo lilifanyika baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) kutoa onyo la kufanya shambulizi iwapo dai lao la kuachiliwa meli zao zilizotekwa halitatekelezwa.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, iliyotolewa leo imeonesha jinsi mahali mtu anakozaliwa kulivyo na mchango katika maisha yake. Ripoti inasema, “mahali mtu anakozaliwa huweza kuamua kama ataishi zaidi ya miongo mitatu kuliko mtu mwingine aliyezaliwa katika nchi yenye hali duni za makazi, elimu na fursa za ajira.”Na mashinani leo nampa fursa Dorcas Awortwe, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Maendeleo ya Kanda ya Kati kutoka Ghana, aliyeshiriki kwenye mkutano wa jukwaa la watu wa asili hapa Makao Makuu wiki iliyopita anazungumzia changamoto zinazowakabili watu wa asili katika jamii yake na ombi lake kwa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.
Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi
Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.
Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokasia ya Congo DRC, Na masuala ya afya nchini Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville. Makala inatupeleka nchini Tanzania, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa.Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu.Katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania anaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linalotilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.Na mashinani fursa ni yake Ahmed kutoka kaunti ya Laikipia nchini Kenya, ambaye kupitia video iliyoandalia na Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM anaeleza jinsi ambavyo ukame wa mara kwa mara unavyoathiri mifugo ya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hujambo Msikilizaji wa Radio Maria Tanzania Sauti ya Kikristo Nyumbani mwako, karibu ufuatilie makala maalumu tuliyokutayarishia, kuhusu namna wanawake walioshinda nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024, watakavyotekeleza ahadi zao kwa wananchi. Mtayarishaji na msimulizi wa Makala haya ni Agatha Kisimba. Karibu. L'articolo Wafahamu namna Viongozi Wanawake watakavyotekeleza ahadi zao kwa wananchi. proviene da Radio Maria.
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Syria, na kampeni ya chanjo ya polio huko Pokot nchini Kenya. Makala tunasalia huko huko DRC na mashinani tnakwenda nchini Msumbiji, kulikoni?Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa.Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza mama ambaye alipatiwa ujauzito na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kisha kujifungua mtoto ambaye anasimulia kadhia ya kutomfahamu baba na wito wake kwa mama yake mzazi. Msimulizi wako ni George Musubao mwandishi wa Idhaa ya Umoja wa MAtaifa nchini DRC.Katika mashinani wakati huu ambapo Dunia inaendelea kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Benilde Nhalivilo. Mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la kitaifa la haki za watoto nchini Msumbiji ambaye kupitia video ya Benki ya dunia barani Africa anasisitiza utekelezaji wa sheria kuhakikisha mustakabali usio na ukatili wa kijinsia katika elimu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria. Taarifa iliyoandaliwa na Anold Kayanda inaeleza zaidi.
Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited inayoendesha Mradi wa Kipeto Energy jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa.”Mradi wa Kipeto wa kampuni hiyo unatoa nishani ya umeme kwa kaya 250,000 katika eneo la Esilanke kaunti ya Kajiado nchini Kenya ukizalisha megawati 100 za umeme tangu 2021 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya taifa, lakini pia unasaidia kuwajengea wananchi nyumba bora na kuwapa huduma muhimu ya maji. Stela Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amezungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo wa nishati ya upepo ya Kipeto kuhusu faida za mradi huo, na anaanza kwa kujitambulisha..
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kuandamana ni haki ya wananchi wa Kenya, na inalinda na Katiba ya sasa ya nchi. Bora tu maandamano haya yafanywe kwa amani bila kuvuruga usalama. Hatua ya maafisa wa usalama kuwakabili waandamanaji wanaoandamana kwa amani ni uvunjaji wa sheria.
Wananchi wa Rwanda wanajiandaa kupiga kura tarehe 15 mwezi Julai kumchagua rais na wabunge.Wiki iiyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea urais ambao ni rais Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994, Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana mgombea binafsi.Mwanasiasa na mpinzani wa Kagame, Diane Rwigara, kutoka chama cha People Salvation Movement, ombi lake lilikataliwa. Tunachambua maandalizi ya uchaguzi nchini Rwanda. Wachambuzi wetu ni Edwin Kegoli akiwa Nairobi na Mali Ali akiwa jijini Paris
Vikao vinavyoendelea vya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka wa 2024 visiwe tu kwa nia ya kujifanya kuheshimu Katiba. Wacha maoni ya Wakenya yatiliwe maanani na kuheshimiwa.
Serikali ya Tanzania yasema wananchi walivamia eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
Mswada wa Fedha wa Mwaka wa 2024/2025 una baadhi ya mapendekezo ambayo kimsingi yatamuongezea Mkenya mzigo wa ushuru ambao tayari ni mzito. Sepetuko inakariri kuwa kamwe haiwezekani kwa nchi kujiendeleza kupitia kuwatoza wananchi wake kodi nyingi! Haiwezekani.
Mgombea urais kwa tikiti ya upinzani wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, mgeni kisiasa, lakini ambaye ni maarufu miongoni mwa vijana wasioridhishwa na utawala uliopo, aliahidi Jumatatu kutawala kwa unyenyekevu na uwazi, wakati akisubiri kutangazwa kuwa rais ajaye.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Serikali ya Tanzania yatoa sababu za upungufu wa sukari, umeme na sarafu ya dola, lakini wachambuzi na wananchi wengi hawajaridhishwa.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. Mwandishi wetu wa nchini DRC, George Musubao amefuatilia na kuandaa makala hii.
Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu. Mwandishi wetu wa DRC George Musubao amefika huko na kutuandalia makala ifuatayo. Kwako George.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama miongoni mwa wakimbizi wa ndani katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia nchini humo kufuatia tukio la jana Alhamis ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa na wengine kuuawa.Video iliyorekodiwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) inaonesha gari la wagonjwa la Umoja wa Mataifa likisindikizwa na walinda amani likipita katika barabara ya vumbi katikati ya umati wa wakimbizi wa ndani katika eneo la Malakal nchini Sudan Kusini. Kila mmoja aliyefanikiwa kusalia na chochote katika anavyovimiliki, amekibebeba kichwani, mgongoni au mkononi. Jana muda wa mchana ghasia zilizuka kati ya jamii mbili za wakimbizi wa ndani ambazo zimehifadhiwa katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia. UNMISS inasema vurugu hizo zilichochewa na tukio la kuchomana visu huku ripoti za awali zikitaja raia watatu kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa hadi kufikia jana Alhamisi mchana. Kabla ya hapo, hiyo-hiyo jana Alhamis asubuhi, milio ya risasi ilitanda alfajiri katika mji mkuu wa jimbo la Upper Nile, Malakal, karibu na makazi ya UNMISS.Walinda amani wa UNMISS waliingia kazini haraka kwa kuwa hali ya wasiwasi imekuwa ikiendelea hapa tangu mwisho wa wiki iliyopita, wakati mzozo katika kituo cha maji uliongezeka haraka na kuwa mzozo kamili ambapo mtu mmoja mwenye umri wa miaka 32 aliuawa. Kwa kuwa kambi ya walinda amani iko karibu na kambi ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi kwa raia, mara zote walinda amani wako chonjo kuchukua hatua ya haraka pindi tu wanapopokea taarifa ya vurugu. Wakati wa mapigano ya mwezi uliopita, wanajeshi na polisi walinda amani walitumwa mara moja ili kutuliza hali hiyo. Polisi na walinda amani wa kijeshi kwa sasa wanashika doria ndani ya eneo hilo na kuzunguka eneo la nje, kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini ili kuondoa hofu miongoni mwa jamii iliyokimbia makazi yao. Zaidi ya hayo, walinda amani matabibu katika hospitali ya UNMISS wanatoa huduma ya dharura kwa baadhi ya waliojeruhiwa. Kwa mujibu wa usajili wa kibayometriki wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), kufikia Desemba mwaka jana 2022, baadhi ya watu 37,032 waliokimbia makazi yao wanajihifadhi katika Eneo la Ulinzi la Umoja wa Mataifa la Malakal.
Hii leo jaridani tuanaangazi ripoti ya WHO ya vikoleza utamu visivyo sukari halisia, na huduma za afya zizazotolewa nchini Malawai kupitia kilniki za kuhama kwa njia ya magari. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs. Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.Katika Mkala, leo ikiwa ni siku ya familia duniani nakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amemulika ni vipi familia inajitahidi kukidhi mahitaji licha ya changamoto za usalama.Katika mashinani na tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama linavyokuza nidhamu na kuboresha usafi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) linasema kimbunga Freddy kilichotokea kati ya Februari 5 na Machi 14 kiliwaacha watoto wa Malawi milioni 2.9 hatarini na katika uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu. Na katika msingi huo bado UNICEF inawaomba wahisani duniani kote kuichangia dola za Marekani milioni 52.4 kupitia ombi la Hatua ya Kibinadamu kwa ajili ya kufanikisha kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watoto na wanawake nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na wale walioathiriwa na Kimbunga Freddy hicho. Hata hivyo UNICEF katika hali hiyo hiyo ya uhaba wa ufadhili bado ilifanikiwa kutoa msaada kwa watu walioalazimika kuishi kwenye makambi baada ya kimbunga hicho. Mary Kwatani ni mmoja wao, “Nilikuja kambini kwa sababu nilipoteza nyumba yangu kutokana na mafuriko. Nilikuja hapa kutafuta makazi kwa sababu afya ya watoto wangu ilikuwa mbaya kutokana na lishe duni.” Kwa haraka UNICEF ilichukua hatua ikaleta kiliniki za kwenye magari ili kuleta huduma tiba kwa ajili ya, wajawazito na wanaonyesha na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Mary Kwatani ni mnufaika anasema, "Kiliniki hizi zinazotembea zimekuwa msaada kwangu kwa sababu nilikuwa nasafiri umbali mrefu kufika hospitalini lakini sasa wahudumu wa afya wanaweza kutufikia kupitia kiliniki zinazohama." Kimbunga Freddy ambacho kilizipiga nchi kadhaa kusini mwa Afrika, kwa Malawi kiliathiri moja kwa moja wilaya 15 zilizopo kusini mwa nchi ya Malawi na kuathiri maisha ya watu na makazi.
Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.Maelfu ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya sherehe hizo katika mji wa Aweil, wakitazama na kushiriki kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za kitamaduni. Leah Mushi anasimulia hali ilivyokuwa
Katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake nchini Somalia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewapongeza watu wa Somalia akisema licha ya changamoto lukuki zinazowaandama wameendelea kuwa imara na kuonyesha mnepo wa hali ya juu, akiwataka kuendelea kufanya hivyo kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho. Flora Nducha na tarifa zaidiAntonio Guterres ametoa pongezi hizo katika mkutano na waandishi wa habari wa kuhitimisha zira yake ya mshikamano mjini Moghadishu akisema tangu alipofika mara ya mwisho nchini humo miaka sita iliyopita kuna mabadiliko kwani sasa Somalia hatua kubwa zimepigwa katika mchakato wa amani , usalama na maendeleo endelevu.Amempongeza pia Rais wa taifa hilo la Pembe ya Afrika Hassan Sheikh Mohamud kwa juhudi zake za kusongesha mchakato wa amani na usalama na kuainisha umuhimu wa kuwa na ushirikiano imara sio tun a Umoja wa Mataifa bali nan chi wanachama wa serikali ya shirikisho ili kushughulikia tishio la magaidi wa Al-Shabaab.Katibu Mkuu amewahakikishia Wasomali dhamira ya Umoja wa Mataifa kulisaidia juhudi za taifa hilo na za kikanda katika kulinda haki za binadamu na kupambana na ugaidi na uhalifu wa itikadi kali ikiwemo kupitia mpango wa muungano wa Afrika nchini humo.Guterres ameongeza kuwa “Ziara yangu ya mwisho mwaka 2017 ilikuwa wakati wa operesheni kubwa ya kuepusha baa la njaa. Leo hii hali kwa mara nyingie ni ya kutia hofu, kwani mabadiliko ya tabianchi yameleta zahma kubwa, misimu 5 isiyo na mvua ambayo si kawaida na ukame tayari umeshakatili Maisha ya watu 43,000 2022 pekee na kutawanya watu wengine milioni 1.4 huku asilimia 80 wakiwa ni wanawake na Watoto.”Amesem changamoto hizo na ukiongeza na mfumuko wa bei ya chakulaumezifanya jamii za masikini kusukumwa kwenye ukingo wa njaa akikadiria kwamba kati ya sasa na Juni Wasomali milioni 6.5 watakabiliwa na viwango vya juu vya kutokuwa na uhakika wa chakula hali inayodhihirisha kwamba baa la njaa bado linanyemelea.Amesisitiza kuwa hatua lazima zichukuliwe sasa kuepusha janga kubwa Zaidi hasa akiwasihi wahisani kunyoosha mkono Zaidi kwani ombi la kibinadamu kwa ajili ya Somalia 2023 ambalo n idola bilioni 2.6 zimefadhiliwa kwa asilimia 15 pekee hadi sasa. Hata hivyo Katibu Mkuu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani amewapa matumaini Wasomali kwa ahadi ya Umoja wa Mataifa kushikamana nao katika kusongesha amani na usalama, maendeleo endelevu, haki za binadamu na ujenzi wa mustakbali bora kwa Wasomali wote.
Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – MINUSCA wametoa huduma ya maji safi na salama kwa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï. Siku ya leo ni shangwe isiyo na kifani kwa wananachi wa kijiji cha Savaderi Kilichoko mkoani Mambéré-Kadéï baada ya kikosi cha TANZBAT6 kutoa msaada wa kuwagawia maji waliyobeba kwenye magari yao maalum.Wananchi hawa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama. Afisa jamii na walinda amani kutoka Tanzania Luteni Alyoice Tyraphone Deusi, kwa niaba ya Mkuu wa TANZBAT06 Luteni kanali Amin Stephen Mshana, baada ya kutoa huduma hiyo ya maji katika vijiji kadhaa akasema wameona ni njia rahisi ya uhusiano bora na jamii.Kwa upande wake Bi Christin Mamaduu, mmoja wa akina mama wa eneo hilo baada ya kutua ndoo ya maji kichwani alitoa shukrani zake kwa walinda amani kutoka Tanzania chini ya MINUSCA. “Tunashukuru sana kwa walinda amani kutoka Tanzania kwa jinsi walivyo amua kutupa msaada wa maji safi hapa nyumbani maana hatuna maji safi hapa kwetu. Huwa tunapata maji ya bomba mara mbili tu kwa wiki na huwa tunanunua. Watu tunakuwa wengi sana, wanasukumana mpaka kuumia. Lakini leo tunajisikia amani kupata maji bila fujo yeyote. Mungu awabariki walinda amani wa Tanzania kwa upendo wao wanaouonyesha hapa kwetu."
Wananchi wa Kijiji cha Difolo katika viunga vya mji wa Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamewashukuru walinda amani wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MINUSCA) baada ya wanalinda amani hao kuwafundisha wananchi hao kulima kwa kutumia jembe la mkono badala ya kulima kwa kutumia panga. Kapteni Mwijage Francis Inyoma ni Afisa Habari wa kikosi hicho ameandaa makala hii.
Wananchi wa eneo la Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wameeleza furaha yao baada ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA kutoka kikosi cha 6 cha Tanzania, TANBAT 6 , kutumia wataalamu wake wa afya kutoa matibabu na dawa kwenye zahanati ya Potopoto wilayani Mambéré-Kadéï.Kapteni Nashiru Bakari Mzengo Mganga Mkuu wa TANBAT 6 amekabidhi dawa kwa mganga mkuu wa Zahanati ya Potopoto katika wilaya ya Mambéré-Kadéï hapa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.Shughuli hizi zimetanguliwa na TANBAT 6 kufanya usafi katika eneo la zahanati na kisha kuwafanyia matibabu wagonjwa kadhaa waliokuja kupata huduma katika zahanati hii ya Potopoto.Bi. Janiruh akiwa amembeba mtoto wake ni mwananchi wa eneo hili kwa niaba ya wananchi wengine anaeleza alivyoipokea hatua hiiya walinda amani wa Umoja wa Mataifa akisema, "Tanzania na wanajeshi wake wana upendo sana kwetu tangu waanze jukumu la ulinzi wa amani tumeshuhudia mambo mengi mazuri kwao moja wapo ni kama hili hapa la kutupatia matibabu na dawa za kutumia ni jambo ambalo sisi kama wananchi wa Afrika ya kati tunajivunia kuwa na walinda amani kama hawa ambapo ushirikiano walio nao kwetu ni mkubwa zaidi ya upendo. "Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hosiptali ya Potopoto, Dkt Sineh ametoa shukrani akisema, "shukrani zetu zimfikie mkuu wa kikosi cha TANBAT6 cha kutoka Tanzania Kwa kutoa watabibu wa afya na kuja hapa kutoa matibabu Kwa wagonjwa wetu lakini pia kuamua Kufanya usafi na kutukabidhi dawa. Upendo huu ni mkubwa sana na niwahakikishie dawa hizi zilizokabidhiwa kwetu tutahakikisha tunawatibu raia wetu Ili wafaidike na walinda amani hawa wa Tanzania."
Jaridani hii leo tutakupeleka Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na huko Lesvos nchini Ugiriki. Makala tunabisha hodi nchini Rwanda, na mashinani tunakwenda huko Walungu jimboni Kivu Kusini, kulikoni?Wananchi wa eneo la Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wameeleza furaha yao baada ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA kutoka kikosi cha 6 cha Tanzania, TANBAT 6 , kutumia wataalamu wake wa afya kutoa matibabu na dawa kwenye zahanati ya Potopoto wilayani Mambéré-Kadéï.Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kesi iliyoanza huko Lesvos nchini Ugiriki dhidi ya watetezi 24 wa haki za binadamu wanaoshtakiwa kwa kutekeleza jukumu la kuokoa wahamiaji ambao walikumbwa na zahma baharini wakati wakikimbilia barani Ulaya kusaka maisha bora.Katika makala leo tunabisha hodi nchini Rwanda kumulika jinsi vijana wawili ndugu wameukumbatia wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka vijana kutofikiria ajira ni ofisini pekee kwani baada ya kuhitimu mafunzo ya Chuo Kikuu na kusaka ajira kwa muda mrefu bila mafanikio, walikata shauri na kuamua kujiajiri katika sekta ya Sanaa ya kuuza bidhaa za kitamaduni. Je safari yao ilikuwaje?Na katika mashinani tunakwenda huko Walungu jimboni Kivu Kusini kumulika suala la lishe. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA Kanda ya magharibi Brigedia Jenerali Zarrar Haider ametembelea kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 6 kilichoweka kambi Berberati, Mambéré-Kadéï.Brigedia Jenerali Zarrar Haider ametua katika kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa akitokea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na moja kwa moja akakutana na maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na askari walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi hiki cha sita kutoka Tanzania.Amewakumbusha walinzi wa amani kuendeleza kazi nzuri wanayoendelea nayo ya ulinzi wa amani ikiwemo kuendeleza ushirikiano na taasisi za dini, afya na wadau wengine wa ulinzi wa amani ndani ya MINUSCA.Aidha amewakumbusha kujua wajibu wao ikiwemo kufahamu ni wakati gani watatumia nguvu na kuwa makini sana na mabomu ya ardhini wanapokuwa katika majukumu ya ya ulinzi wa amani lakini pia kuendelea na kuwa makini na ugonjwa wa COVID -19 na malaria ili watekeleze majukumu yao ya ulinzi wa amani.Kwa upande wa TANBAT 6, akitoa shukrani kwa niaba ya kikosi hicho, Mkuu wa kikundi hicho Luteni Kanali Amini Stephen Mshana kuendeleza yote aliyoahidi. « Umesisitiza kuhusu ushirikiano na wadau wakiwemo makao makuu, viongozi wa serikali na wenzetu vikosi vya ulinzi vinavyotuzunguka. Mkuu tunafanya hivyo na tutaendelea kushirikiana nao. Tunatambua kwamba MINUSCA ni jumuishi na ulinzi wa wananchi ni jukumu la pamoja kwa hiyo hakuna namna TANBAT 6 itatimiza jukumu lake bila ushirikiano. Nami kama kamanda wa kikosi nitalilisisitiza katika kila hali »
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema mwaka 2022 umegubikwa na changamoto lukuki za kiafya , kuanzia janga la COVID-19, Ebola, Mpoxy hadi vita vilivyokatili na kujeruhi wengi hata hivypo linasema kuna matumaini kwa mwaka ujao, yapi?Taarifa ya tathmini ya kiafya ulimwenguni iliyotolewa leo na WHO nchini Geneva Uswisi imeeleza mwaka 2022, umeendelea kushuhudia uwepo wa janga la COVID-19 pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa Mpox hapo awali ikifahamika kama Monkeypox ambao ulienea kwa kasi katika nchi mbalimbali duniani.Katika pembe ya Afrika na Ukanda wa Sahel nchi nyingi zimekabiliwa na milipuko ya kipindupindu, utapiamlo na magonjwa mengine nyemelezi kutokana na ukameWananchi wa Ethiopia na Ukraine wamekabiliwa na kifo na uharibifu unaoletwa na vita. Ebola ilipiga hodi nchini Uganda, na mafuriko makubwa nchini Pakistan yameweka mzigo mkubwa kwenye sekta ya afya yan chi hiyo.Bila kutaja matishio mengine mengi kwa afya ambayo watu hukabiliana nayo mwaka hadi mwaka, magonjwa yatokanayo na mazingira, bidhaa wanazotumia, maeneo wanayoishi na kufanya kazi, na ukosefu wao wa ufikiaji wa huduma muhimu za afya.Hata hivyo Pamoja na changamoto zote hizi, mwaka unamalizika kwa matumaini, kwani wagonjwa wa COVID-19 na Mpox wameendelea kupungua, huku kukiwa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola kuripotiwa tangu tarehe 27 mwezi uliopita wa Novemba.WHO imeeeleza ina matumaini kwamba kila moja ya dharura hizi itatangazwa imemalizika mwaka ujao.Hata hivyo ugonjwa wa malaria bado unatesa wananchi wengi duniani lakini kuna juhudi zinafanyika kila mahali kuhakikisha hakuna ongezeko Zaidi na ingawa idadi ya wagonjwa imeongezeka lakini kasi ya wagonjwa imepungua ikilinganisha na miaka uliyopita.Juhudi nyingine zinazofanyw ana WHO ni Pamoja na kutoa ripoti za kina za kimataifa na miongozo kwa serikali katika maeneo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kubadilisha huduma za afya ya akili, kuongeza viwango vya mazoezi ya mwili, na kuzuia magonjwa ya kinywa ambayo yanaathiri karibu nusu ya idadi ya watu ulimwenguni.
Jaridani leo tunakuletea habari kutoka Kenya na DR Congo, makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinanio tunakuletea ujumbe kuhusu wanawake kushirikishwa katika shughuli za ulinzi wa amani.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepongeza hatua zinazochukuliwa na serikali ya Kenya kutatua tatizo la muda mrefu la kutokuwa na utaifa kwa watu wa jamii ya Pemba wanaoishi nchini humo. Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wameendelea kuhamasishana kuimarisha ushirikiano kati yao ili kufikia lengo kuu la kuleta amani nchini humo. Anayetuletea taarifa hii kwa kina ni Kapteni Denisia Lihaya ambaye ni Afisa Habari wa Kikundi cha 9 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB na kile cha utayari QRF chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.Makala tunakupeleka mashariki mwa Tanzania mkoani Morogoro kwake Hamad Rashid wa redio washirika MVIWATA FM kusikia harakati za wakulima kulinda, kuhifadhi na kutumia mbegu za asili za mazao. Na katika mashinani tutasikia kuhusu umuhimu wa kushirikisha wanawake katika shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!
Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wameendelea kuhamasishana kuimarisha ushirikiano kati yao ili kufikia lengo kuu la kuleta amani nchini humo. Anayetuletea taarifa hii kwa kina ni Kapteni Denisia Lihaya ambaye ni Afisa Habari wa Kikundi cha 9 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB na kile cha utayari QRF chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO. Ashantie Sengemoja ni mmoja wa wananchi wa eneo la Beni, Mavivi kaskazini mashariki mwa DRC, yeye ni miongoni mwa wanaotoa wito kwa wananchi wenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushirikiana na majeshi ya wananchi wa Tanzania walioko katika jukumu la ulinzi wa amani katika eneo la Beni. “Wananchi wa DRC tushikamane na hawa askari wa Tanzania. Sisi sote ni ndugu tusifanye ubaguzi kwa askrai wa Tanzania. Sisi sote tuko vizuri kabisa.” Anasema Bi. Sengemoja. Naye Koplo Janet Mbinda mmoja wa walinda amani kutoka Tanzania anasema, “ujumbe wangu kwa wananchi wa DRC tushirikiane vizuri ili kufanikisha jukumu letu lililotuleta mahali hapa. Na sisi tunaahidi kwamba tutafanya kazi vile ipasavyo.” Luteni Kanali Barakaeli Jackson Mley ni Mkuu wa Kikundi cha 9 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 anasema mpango wao ni kwamba wana mpango mkakati kwa kushirikiana pamoja na “majeshi rafiki kwa maana ya Jeshi la Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC (FRDC) na MONUSCO, tumejipanga vizuri na moja ya kazi ya majeshi ni kufanya mafunzo na mafunzo tunayoyafanya pamoja na operesheni tunazozifanya ni za pamoja. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana.” Kamanda huyo anaeleza zaidi kwamba hawana mpango wa kukata tamaa kuhusu mpango wao wa kuleta kutimiza lengo lililowapeleka nchini humo kwani, “Jeshini hakuna kukata tamaa, tutahakikisha mpaka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inapata amani.”
Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli ambaye ni Mkuu wa Utumishi katika Jeshi la Tanzania ametoa wito kwa Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo yao ya ukosefu wa amani. Meja Jenerali Simuli ametoa wito huo alipoongoza ujumbe wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika ziara yao nchini DRC ili kujionea shughuli za mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO ambamo kwa nyakati tofauti, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wamekuwa wakihudumu katika vikosi mbalimbali kikikwemo cha kujibu mashambulizi, FIB. Kwanza alihudhuria hafla ya kuwavisha nishani za Umoja wa Mataifa askari wa Tanzania wanaolinda amani nchini DRC. Nats.. Kisha wito wake kwa raia wa DRC, Sauti ya Meja Jenerali Simuli..“Mimi ujumbe ambao ningeweza kuwapa wacongoman (Raia wa Congo), kama ndugu zangu, kaka zangu, dada zangu, waafrika wenzangu, ni kwamba matatizo yakijitokeza basi wakae mezani kwa pamoja na kuyazunumza kwa pamoja na kupata kile ambacho wanakihitaji. Kwa sababu ili nvhi iendelee inahitaji amani. Mkitulia mtakwenda mbele sana. Na nchi ya DR Congo nina Imani wananchi wakikaa vizuri, wakiacha munkari, yaani wakiacha hasira, wakakaa mezani na kuzungumza, matatizo yatakwisha.” Na je Meja Jenerali Paul Simuli ana ujumbe gani kwa walinda amani? Sauti ya Meja Jenerali Simuli..“Walinda amani ninawaomba waelekee kwenye yale majukumu ambayo wamekuja kuyatekeleza hapa kwa wenzetu (DRC). Kwa sababu jambo lao kubwa ni kuwalinda wananchi ambao wanapata madhara.”
Tarehe 24 Oktoba dunia ilisherehekea siku ya Umoja wa Mataifa kwa kuadhimishwa miaka 77 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945. Ingawa kuanzishwa kwake kuliangalia zaidi masuala ya Amani na usalama na Haki za Binadamu lakini Shirika hili kubwa la kimataifa limezidi kupanua wigo wake na sasa wanashiriki katika sekta zote duniani, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya watu wote na kuhakikisha wana ustawi wa maisha na pale kwenye changamoto shirika husika la Umoja wa Mataifa hutafuta ufumbuzi. Na Hili ndio lililotokea nchini Tanzania katika Mkoa wa Simuyu ulioko Kaskazini mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki.Wananchi wa kijiji cha Njiapanda wilayani Bariadi katika Mkoa wa Simiyu walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kutupa mazao yao na kupata hasara, kwanini? Sababu walikosa masoko ya uhakika ya mazoa yao. Uongozi wa wilaya ya Bariadi uliona changamoto hii na namna inavyorudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuwasilisha ombi kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mitaji UNCDF ili waweze kuwasaidia wananchi hao kupata soko la uhakika na kumaliza tatizo la utupaji mazao. Je UNCDF wamefanyaje kumaliza changamoto za wananchi hao? Tuungane na Leah Mushi anayetujuza zaidi.
Katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2020 mpaka mwaka 2030 watu milioni 500 wanakadiriwa kuwa watakuwa wameugua magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, utipwatipwa na magonjwa ya moyo kutokana na kutofanya mazoezi ya mwili, imesema ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi Ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni hasara kubwa kwa uchumi wa kila serikali. Inakadiriwa kuwa serikali zitaingia gharama ya dola bilioni 27 kila mwaka kutibu wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kufikia mwaka 2030 takriban dola bilioni 300 zitatumika kutibu wagonjwa hao. Gharama hii kubwa imeainishwa katika ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO ambalo katika utafiti walioshirikisha nchi 194 kuhusu kufanya mazoezi ya mwili na namna serikali zinavyohamasisha wananchi wake kushirika katika mazoezi hayo, wamegundua kiujumla kuna maendeleo kidogo sana kwenye kampeni za uhamasishaji wananchi kufanya mazoezi ambayo matokeo yake ni kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile utipwatipwa, kisukari na magonjwa ya moyo na hivyo serikali kujipunguzia mzigo wa kuwahudumia wagonjwa hao. Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema baada ya kutolewa ripoti hii wanaamini mataifa na wadau watachukua hatua kwakuwa lengo lao ni kuona wananchi wanahamasishwa kufanya mazoezi sababu tatizo linazidi kuwa kubwa. Dkt Tedros amesema “Tunahitaji kuona nchi nyingi zinaongeza na kutekeleza sera za kusaidia wananchi kushirika zaidi katika mazoezi kwa kutembea, kuendesha baiskeli na kushiriki kwenye michezo mingine mingi ya kimwili. Faida ni kubwa si tu kwa afya ya mwili bali kiakili na jamii nzima itanufaika, mazingira yatakuwa bora na kiuchumi pia.” Takwimu walizokusanya zinaonesha kuwa duniani kote chini ya asilimia 50 ya nchi zina será za kitaifa za kufanya mazoezi ya mwili na kati ya hizo ni asilimia 40 ndio zinazofanya kazi. Na kama hiyo haitoshi ni asilimia 30 pekee ya nchi zenye será ndio zimeweka miongozi ya namna ya kutekeleza sera hizo. WHO imesema ingawa karibu nchi zote zinaripoti kuwa na mfumo wa kufuatilia shughuli za kimwili kwa watu wazima, asilimia 75 ya nchi hufuatilia shughuli za kimwili kwa vijana, na chini ya asilimia 30 hufuatilia iwapo watoto chini ya miaka 5 wanafanya mazoezi ya mwili au lah. Je WHO inafanya nini katika kusaidia mataifa kutoka katika hali ya wananchi wake kuwa tipwatipwa? Hii leo WHO wamekumbusha nchi kuhakikisha zinatekeleza mpango wa utekelezaji wa ufanyaji mazoezi ya viungio au GAPPA ya mwaka 2018-2030 ambayo imeweka mapendekezo ya sera 20 miongoni mwazo ni kuhamasisha mataifa kutengeneza barabra zilizo salama kwa watu kufanya mazoezi na kutoa fursa za kufanya mazoezi katika maeneo kama vituo vya malezi ya watoto, mashuleni na mahala pa kazi. Kiujumla ripoti hiyo inatoa wito kwa nchi kuweka kipaumbele katika shughuli za mazoezi ya kimwili kama jambo muhimu katika kuboresha afya na kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa katika sera zote muhimu, na kuweka kanuni, miongozo na kutoa mafunzo ili kuhakikisha zinatekelezwa kwa ufanisi kwa manufaa ya mataifa yao.
Wakazi wa Beni, Kivu kaskazini, na Ituri wameiomba serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kutangaza mauaji ya mara kwa mara katika eneo lao kuwa ya kimbari.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema wananchi wengi wa Tunisia hivi sasa wanakabiliwa na machaguo magumu ya kubaki ndani ya nchi yao na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha na uhaba wa chakula au kukimbia nje ya nchi yao na kutojua nini kitatokea huko waendako. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. Katika soko la Kairouan nchini Tunisia mwanamke anaonekana akiwa sokoni akinunua nyanya na anasema….. "Naweza kusema nini? Bei zinapanda! Watu maskini hawawezi tena kumudu chochote. Ni kama dunia inawaka moto.” Mwingine naye anasema... “Hakuna sukari, inamaana nilazima nichukue teksi ini niende mbali sana kununua kilo moja ya sukari." Wakati wananchi wakilalamikia bei juu na kukosa bidhaa, wamiliki wa maduka ya jumla nao wanasema nao hawana bidhaa za kutosha kwa ajili ya wateja wao. Samia Zwabi ni mmiliki wa duka la vyakula na anasema .... “Hatuwezi kufanya kazi. Tunafanya kazi kwa nusu ya uwezo wetu. Mteja anapokuja, hawezi kupata mahitaji yote ya msingi. Wateja wanaomba kitu ambacho sina. Sio kwa uchaguzi wetu hata sisi tunahitaji kuwa na uwezo wa kufanya kazi ili kuweza kulisha watoto wetu.” Wananchi wengi wa Tunisia kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa vyakula muhimu, mafuta na bidhaa muhimu za kilimo na hii yote unaelezwa kusababishwa zaidi na vita nchini Ukraine. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji Safa Msehli anasema kwa sasa majaribu yamewafika shingoni wananchi na wengine wameamua kukimbia. “Nadhani kile ambacho mzozo wa Ukraine umeibua tena, ni maamuzi magumu ambayo watu wanapaswa kufanya kila siku, kwa sababu watu wanaolazimika kukimbia makazi yao, watu wanaolazimika kukimbia nchi yao, hawachukui uamuzi huo kirahisi.” Kupitia Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kufikisha mahitaji ya chakula kwenye maeneo ya uhitaji zaidi, na miezi miwili tu baada ya kuanza kwake zaidi ya tani 85,000 za ngano kutoka Ukraine zimewasili katika bandari za Tunisia. Kiujumla wananchi wengi katika nchi mbalimbali wanakabiliwa na changamoto kama za Tunisia kutokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa, mafuta na huku changamoto nyingine za mabadiliko ya tabianchi zikififisha kabisa uwezo wao wa kujikimu hata kwa kilimo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari ikiwa ni kuelekea Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN unaoanza wiki ijayo akisema ujumbe wake mkuu kwa viongozi watakaoshiriki ni dhahiri ya kwamba wachukue hatua kupunguza kiwango cha joto duniani. Guterres amesema atawaeleza kuwa “msifurishe dunia leo, msiizamishe kesho,” kwa kutambua kuwa mkutano huu wa Baraza Kuu unafanyika zama za sasa zinazokabiliwa na tishio kubwa. Ametaja tishio hilo kuwa ni pamoja na mgawanyiko mkubwa wa kijiografia na kimkakati, mgawanyiko aliosema ni mkubwa kuwahi kutokea tangu zama za vita baridi. Katibu Mkuu amesema, “Mgawanyiko huu unakwamisha hatua za pamoja za kukabiliana na changamoto zinazotukabili. Dunia imekumbwa na vita, changamoto za tabianchi, chuki zimezaga, na aibu kubwa inakabili dunia kutokana na umaskini, njaa na ukosefu wa usawa.” Akifafanua kuhusu tabianchi amerejelea kile alichoshuhudia wakati wa ziara yake ya kuonesha mshikamano na Pakistani ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa. Theluthi moja ya G20 ingalikuwa imefurika, pengine wangepunguza uchafuzi Katibu Mkuu amesema, “kinachotokea Pakistan, kinadhihirisha kutotosheleza kwa hatua za kimataifa dhidi ya janga la tabianchi ambayo kitovu chake ni ukosefu wa haki na usaliti.” Hata hivyo amesema iwe ni Pakistan, Pembe ya Afrika au Sahel, nchi za visiwa vidogo au zinazoendelea, suala ni kwamba nchi zilizo hatarini zaidi ambazo hazijasababisha janga la tabianchi ndio zinaathirika na janga lililochochewa na wachafuzi wakuu wambao ni kutoka nchi za kundi la nchi 20 au G20. “Iwapo theluthi moja ya kundi la G20 ingalikuwa imezama au imefunikwa kw amaji leo hii, kama ambavyo inaweza kuwa kesho, pengine wangaliona rahisi kupunguza viwango vya utoaji wa hewa chafuzi,” amesema Guterres. Hivyo amesema nchi zote, zile za G20 zikiongoza njia, lazima ziongeze viwango vya kitaifa vya kupunguza utoaji wa hewa chafuzi hadi pale kiwango kinachotakiwa cha nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi kitakapofikiwa. Amepatia msisitizo suala la uwekezaji katika miradi ya kuhimili na kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi akisema, hatua zisipochukuliwa sasa, fedha zisipotolewa sasa, majanga yataongezeka maradufu, huku madhara yake yakidumu miaka na miaka ijayo, ikiwemo kuongeza ukosefu wa utulivu na kuchochea uhamiaji duniani kote. Ubinafsi na Uzawa vyateketeza mshikamano uliomo kwenye Chata ya UN Bwana Guterres amesema changamoto lukuki zinazokumba Dunia hivi sasa ni matokeo ya ubinafsi na uzawa, mambo ambayo amesema yanateketeza mshikamano ulioainishwa kwenye Chata ya Umoja wa Mataifa. Nchini Ukraine vita inasambaratisha nchi huku ikidororesha uchumi wa dunia. Licha ya Makubaliano ya kusafirisha nafaka kupitia baharí nyeusi, na makubaliano ya kupeleka soko la dunia chakula na mbolea kutoka Urusi, bado kuna hatari ya matukio ya uhaba wa chakula duniani mwaka huu. Gharama za maisha zinapanda na kufikia viwango vya juu, waathirika zaidi wakiwa watu maskini. Haki za wanawake na watoto wa kike ndio zinazidi kusiginwa. Nchi nyingi zinazoendelea hazina uwezo wa kifedha unaotakiwa kujikwamua baada ya janga la COVID-19. Wanasiasa wanajinufaisha na umaskini wa wananchi Mshikamano wa kwenye Chata ya UN unararuliwa na ubinafsi na uzawa,” amesema Katibu Mkuu akisema wanaofanya hivyo ni wanasiasa ambao wanatumia mazingira duni ya maskini ili kujunifaisha kisiasa. Guterres amesema hotuba yake itamulika masuala hayo sambamba na kuwasilisha mapendekezo kwani “kadri ufa unavyozidi kupanuka na imani inatoweka, lazima tuungane kuleta majawabu.” Amesema majawabu hayo ni kama yake yatakayotolewa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Marekebisho ya Mfumo wa Elimu. Katibu Mkuu amesema watu wanataka kuona matokeo kwenye maisha yao ya kila siku la sivyo watapoteza imani na serikali na taasisi zao na kisha watapoteza pia imani na mustakhbali wao. Amesema Mjadala Mkuu wa mwaka huu lazima ulete matumaini na matumaini hayo yanaweza kupatikana kupitia mazungumzo yanayogusa moyo wa Umoja wa Mataifa na lazima ifanyike hivyo wiki ijayo ili kukabili migawanyiko yote.
Kuanzia wiki hii viongozi wa ulimwengu wanamiminika jijini New York Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kushiriki Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mambo kadhaa yatajadiliwa ikiwemo amani, haki za binadamu, uchumi na kuilinda sayari dunia dhidi ya uharibifu unaochochea majanga. Ulimwengu tayari umebaini kuwa changamoto zimefungana na hivyo majawabu yanapaswa kutafutwa kwa kushirikiana. Katika maeneo ambayo ushirikiano umefanyika ili kutafuta ufumbuzi wa jambo, matunda yameonekana. Mathalani nchini Tanzania, shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wananchi wa wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wanaendelea na mradi wa kutatua changamoto ya umeme na maji, masuala mtambuka ambayo yanagusa sekta nyingine kama elimu, afya, uchumi na mazingira. Mradi wa umeme wa nishati ya jua kupitia ufadhili wa shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF umeanza kuzaa matunda kwa wananchi kama anavyosimulia Jongo Sudi wa redio washirika Ruangwa FM.
Katika jarida hii leo utasikia wito wa kusaidia wakulima wa Somalia ili kuiokoa nchi isiingie katika janga kubwa la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linatumia wafanyakazi wa kijamii kuhamasisha wakazi wa vitongoji vya mji mkuu, Kinshasa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona, au COVID-19 kwa kuwa baadhi ya watu bado wanasuasua kupatiwa chanjo hiyo. Wananchi wa Turkana Kenya wamepaaza sauti ya madhila yanayowasibu na UNICEF kueleza nini wanafanya kusaidia katika eneo la usafi na kujisafi.
Jamii katika eneo la Abu Gaw, Darfur Kaskazini, Sudan, imeanza kufaidika na kituo kipya cha afya katika Kijiji chao. Kituo ambacho kimejengwa kutokana na ushirikiano wa jamii, UNHCR na WHO baada ya kuwa kimeharibiwa tangu mwaka 2004 ambapo wananchi waliyakimbia makazi hayo. Happiness Palangyo wa Radio washirika Radio Uhai FM ya Tabora Tanzania anasimulia.
Jumuiya ya kimataifa zimehimizwa kuchukua hatua za pamoja na za haraka ili kukomesha wimbi la ghasia nchini Myanmar kwakile kilichoelezwa kuwa jeshi limejihusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao baadhi yao unaweza kuwa uhalifu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Anold Kayanda. Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet hii leo jijini Geneva Uswisi wakati ikitolewa ripoti ya 49 ya kikao cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo imetanabaisha kuwa jeshi na vikosi vya usalama vya Myanmar vimeonesha kutojali kabisa maisha ya binadamu, huku wakishambulia maeneo yenye wakazi wengi kwa mashambulizi ya anga na silaha nzito na kuwalenga kwa makusudi raia, ambao wengi wao wamekuwa wakiuawa. Wananchi kupigwa risasi kichwani, kuchomwa moto hadi kufa, kukamatwa kiholela, kuteswa au kutumika kama ngao za binadamu ni baadhi ya matukio yaliyoripotiwa kwenye ripoti hiyo. Mauaji ya watu wengi nayo yameripotiwa kufanyika ambapo mwezi Julai mwaka 2021 katika Mkoa wa Sagaing, askari waliwaua watu 40 katika mfululizo wa mashambulizi, wanakijiji walipata mabaki ya baadhi ya wahanga wakiwa bado wamefungwa mikono na miguu migongoni. Mwezi Disemba katika Jimbo la Kayah, wanajeshi walichoma moto takriban miili ya watu 40 wakiwemo wanaume, wanawake na watoto. Wanakijiji walieleza kugundua mabaki hayo kwenye malori kadhaa, huku miili ikipatikana katika sehemu zinazoonyesha kuwa walijaribu kutoroka na kuteketezwa wakiwa hai. Wafungwa nao waliripoti kukabiliwa na mateso na aina zingine za unyanyasaji wakati wa mahojiano ya muda mrefu katika vituo vya kijeshi kote Myanmar. Ikiwa hayo ni baadhi tuu ya matukio yaliyoainishwa kwenye ripoti Kamishna Bachelet ameseme ”Hatua za maana za jumuiya ya kimataifa zinahitajika haraka kuchukuliwa ili kukomesha watu wengine zaidi kupokonywa haki zao, maisha yao na riziki zao.” Amehitimisha ripoti yake kwakueleza ukiukwaji wa haki za binadamu ni mpana sana nchini Myanmar pamoja na ukioukwaji wa sheria za kimataifa na watu wa Myanmara wanateseka hivyo jumuiya za kimataifa zinahitajika kutoa mwitikio thabiti na kwa umoja.