POPULARITY
Categories
Waziri Mkuu amesifu msaada wa wanachama wa kongamano la Visiwa vya Pasifiki, Australia inapo saka uenyeji wa kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa la, COP-31.
Leo jaridani Assumpta Massoi anamulika kauli ya OHCHR kufuatia maandamano yanayoendelea Nepal; Utipwatipwa 'wapiku' utapiamlo na harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huko Karamoja nchini Uganda,Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahKaramoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ameonesha wasiwasi mkubwa kufuatia ghasia zinazoendelea na kushika kasi nchini Nepal, huko barani Asia, ambako maandamano dhidi ya ufisadi na marufuku ya mitandao ya kijamii yamesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatupasha zaidi.Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, akizungumza mjini Geneva amesema“nimeshtushwa na ongezeko la ghasia nchini Nepal ambalo limesababisha vifo kadhaa na kujeruhi mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali.”Katika siku za karibuni, maandamano yaliyoanzia katika mji mkuu Kathmandu sasa yamesambaa katika miji na vijiji vya Nepal, yakiacha barabara zikifunikwa na mabaki ya vitu vilivyoteketezwa kwa moto na kulazimisha maduka kufungwa pia kuhofia usalama.Kwa mujibu wa duru za habari maandamano hayo yanayoo nngozwa na vijana wa kati ya umri wa miaka 13 hadi 28 au Gen Z yameshakatili Maisha ya takribani watu 22, kusababisha waziri mkuu wa nchi hiyo KP Sharma Oli kujiuzulu na kuliwasha moto jengo la bunge .Türk ametoa wito kwa vikosi vya usalama kujiepusha na mapambano na waandamanajI akisema, “Naomba vikosi vya usalama waoneshe uvumilivu wa hali ya juu, na kuepusha umwagaji damu na madhara zaidi. Vurugu siyo suluhisho. Mazungumzo ndiyo njia bora na ya pekee ya kushughulikia malalamiko ya watu wa Nepal. Ni muhimu sauti za vijana zisikike.”Waandamanaji wanasema wameshikwa na hasira kutokana na ufisadi na marufuku ya serikali juu ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, ingawa kwa sasa huduma za mitandao ya kijamii zimerejea. Türk anasema anatambua haki yao ya kusikika, lakini pia amewasihi wawe na uwajibikaji.“Nawakumbusha waandamanaji kuwa nao pia lazima washikamane na kuzingatia dhamira ya kukusanyika kwa amani na wajiepushe na ghasia.”Türk ametaka uchunguzi wa haraka, wa wazi na huru ufanyike kuhusu madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi ya vikosi vya usalama, huku pia akilaani mashambulizi dhidi ya majengo ya umma, biashara, na hata maafisa waandamizi wa serikali.Amesisitiza kuwa dunia inathamini safari ya Nepal kutoka kwenye migogoro hadi kuwa na demokrasia yenye amani na ametoa mwito kwa wadau wote kulinda mafanikio hayo. Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia kupitia mazungumzo na hatua za kujenga imani ambazo zinaweza kusaidia kupunguza mvutano na kurejesha hali ya utulivu.
Kwa mara ya kwanza idadi ya watoto na vijana wa umri wa kwenda shule wenye unene wa kupindukiaau utipwatipwa imezidi idadi ya watoto wenye utapiamlo duniani ikiathiri watoto milioni 188 sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto 10 imesema leo ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tuungane na Leah Mushi kusikia zaidi kuhusu ripoti hiyo, karibu LeahRipoti hii mpya ya UNICEF iitwayo “Faida kwenye vyakula: Jinsi Mazingira ya Chakula yanavyowaangusha watoto” imechambua takwimu kutoka nchi zaidi ya 190 na kubaini kwamba kiwango cha watoto wenye utapiamlo kimepungua tangu mwaka 2000, lakini wale wenye unene wa kupindukia kimeongezeka mara tatu.Kwa sasa, utipwatipwa umeenea katika kila eneo la dunia isipokuwa Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia Kusini. Nchi za visiwa vidogo vya Pasifiki ndizo zinaongoza kwa kuwa na viwango vya juu zaidi, ikiwemo Niue yenye asilimia 38 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 19 wakiwa na unene wa kupindukia.Nini kimesababisha?UNICEF inasema mabadiliko ya mifumo ya lishe kutoka vyakula vya asili hadi vyakula vya kutengenezwa kwa haraka na vya bei nafuu lakini vyenye sukari, mafuta na chumvi nyingi ndiyo chanzo kikuu cha ongezeko hili.Pia inatahadharisha kuwa matangazo ya kidijitali ya vinywaji vyenye sukari na vyakula vya viwandani yanawafikia vijana wengi, hata katika nchi zenye migogoro.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema utipwatipwa ni changamoto kubwa ya kiafya kwa watoto kwa sababu huongeza hatari ya kupata kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo katika maisha ya baadaye.Russell amesema “Tunapozungumza kuhusu utapiamlo, hatuzungumzii tu kuhusu watoto wenye uzito mdogo, utipwatipwa ni changamoto kubwa inayoendelea kuongezeka ambayo inaweza kuathiri afya na maendeleo ya watoto. Vyakula vya viwandani vinazidi kuongezeka na kuchukua nafasi ya matunda, mboga mboga na protini katika wakati ambao lishe ina jukumu muhimu katika ukuaji wa watoto, ukuaji wa utambuzi na afya ya akili.”Nini kifanyike?Ili kukabiliana na hali hii, UNICEF inazitaka serikali kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kupiga marufuku uuzaji wa vyakula visivyo na lishe shuleni, kudhibiti matangazo ya vyakula vyenye sukari na mafuta, na kuweka sera za kusaidia familia kupata chakula bora na chenye lishe.Kwa mujibu wa UNICEF, bila hatua za haraka, gharama za kiafya na kiuchumi zitakazotokana na tatizo la utipwatipwa wa utotoni zinatarajiwa kupindukia dola trilioni 4 kila mwaka ifikapo mwaka 2035.Zipo juhudi za kupambana na hali hiyo ambazo zimeanza kuchukuliwa na baadhi ya nchi, mfano mzuri ni Mexico ambayo hivi karibuni imepiga marufuku uuzaji wa vyakula vilivyosindikwa na vile vyenye chumvi, sukari na mafuta mengi katika maeneo ya shule za umma.
Karamoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, linakabiliwa na changamoto kubwa za tabianchi kama vile ukame wa mara kwa mara na milipuko ya magonjwa ya mimea na mifugo, hali inayotishia uhakika wa chakula. Kupitia mradi wa PROACT, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), na Mpango wa chakula Duniani (WFP) pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya, EU, wameshirikiana katika kuimarisha mifumo ya kushughulikia mabadiliko ya kiikolojia na kijamii. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda) Video iliyoandaliwa na FAO inaanza ikionesha wana jamii katika eneo la Karamoja wanavyojihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kilimo na ufugaji licha ya changamoto za tabianchi. Dustan Balaba Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Uganda anaeleza kuhusu mradi huu mpya akisema,"Wadau wameweza kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya haraka katika upatikanaji wa taarifa na tunatumia maendeleo ya kiteknolojia kwa manufaa yetu. Tumejiandaa vyema kutabiri matukio mengi ya tabianchi.”Mpango huu unalenga kutumia mifumo ya tahadhari ya mapema na hatua za kabla ya majanga ili kukuza uwezo wa jamii za Karamoja kukabiliana na majanga, pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali kwa ushirikiano.Lokong Robert, Kaimu Afisa wa Kilimo wa Wilaya Kaabong anaeleza akisema, "Tunachagua kaya hizo. Baada ya kuchagua tunapewa maelezo juu ya madhumuni ya kuwachagua. viongozi wa meneo, maafisa wa ugani, na washauri wa ujenzi wa uwezo waliajiriwa na FAO huenda kukusanya taarifa katika kata."Naye Stella Nagujja, mtaalamu wa usimamizi wa hatari za tabianchi WFP Uganda anasema "mshikamano kati ya mamlaka zetu tofauti ulitufanya tufikiri kuwa itakuwa kimkakati kushirikiana na FAO ili kuokoa maisha na kuwafikia jamii zilizo katika mazingira magumu."Lakini kiini cha mradi huu kipo katika sauti za watu waliopokea huduma na kunufaika moja kwa moja. Kuanzia Moroto hadi Nabilatuk, jamii si wapokeaji tu wa msaada, bali ni washiriki kamilifu katika kujenga uwezo wao wa kujitegemea.Jolly Aisu, afisa kilimo wilaya ya Nakapiripirit, anasema , “tunapanga ziara za mashambani ili kutusaidia kutambua na kuchambua ugonjwa au mdudu gani ameshambulia mimea ya mkulima. Kisha kutoka hapo tunawaelekeza cha kufanya kutumia taarifa kutoka katika mifumo ya tahadhari ya mapema na mipango iliyo wazi.”Hata hivyo, pamoja na maendeleo haya, changamoto bado zipo. Rasilimali chache na hali ya ukosefu wa usalama miongoni mwa jamii vinaweza kuhatarisha mafanikio ya mradi huu.Lukeng Emmanuel, Mkulima wa Kaabong anatamatisha kwa kusema, "Tunashindwa hata kununua dawa ya kunyunyizia kwa sababu kile kidogo tunachokipata hapa tunatumia kwa chakula, karo ya shule, na matibabu. Tunaliacha shamba lipambane kivyake hadi tutakapopata pesa kidogo ya kununua dawa ndipo tunanyunyizia."
Je umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea? Skiza makala haya kuskia hisia za waskilizaji wetu.
-Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80 chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo dola milioni 1 za kimarekani kutoka Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limefanya mabadiliko muhimu katika orodha yake ya dawa muhimu duniani au Essential Medicines List – EML na orodha ya dawa muhimu kwa watoto (EMLc) ikijumuisha dawa za kisasa za saratani, kisukari, unene uliopitiliza na magonjwa mengine sugu.Orodha za WHO za dawa muhimu ni nyenzo za mwongozo zinazotumiwa na zaidi ya nchi 150 kupanga ununuzi, bima za afya na upatikanaji wa dawa. Kwa lugha rahisi, dawa zinazoorodheshwa hapa huwa na nafasi kubwa zaidi ya kununuliwa na kutolewa kwa wagonjwa kupitia huduma za umma kwani wanachama wa WHO wanaziweka dawa hizi kama kipaumbele cha kiafya kwa mamilioni ya watu duniani.WHO wakati wakitangaza orodha hiyo mpya waliweka bayana kuwa dawa hizi mpya si za majaribio, bali ni zile ambazo zimethibitishwa kitabibu kuwa zinaokoa maisha, kupunguza madhara ya magonjwa na kuboresha maisha ya wagonjwa.Nini maana yake?Kuongezwa kwa dawa hizi ni hatua ya mbele katika safari ya kuhakikisha afya bora kwa wote. Inamaanisha wagonjwa zaidi wa saratani, kisukari na magonjwa mengine sugu wanaweza kuwa na matumaini ya maisha marefu na bora. Pia ni wito kwa mataifa kuchukua hatua ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa haki na usawa, bila kumwacha mtu yeyote nyuma.Changamoto ya bei na usawa wa kiafyaChangamoto kubwa sasa ni bei kubwa ya dawa hizi mpya, ambazo zinaweza kufanya wagonjwa wengi kushindwa kuzipata.WHO inapendekeza mikakati ya kupunguza gharama na kuhakikisha dawa hizi zinapatikana kwenye ngazi ya huduma za msingi za afya.Deusdedit Mubangizi, Mkurugenzi wa Sera na Viwango vya Dawa WHO, anasema “Sehemu kubwa ya matumizi ya nje ya mfuko wa magonjwa yasiyoambukiza yanaelekezwa kwenye dawa, ikiwa ni pamoja na zile zinazoainishwa kama muhimu na ambazo kimsingi, zinapaswa kupatikana kwabei rahisi kwa kila mtu. Ili kufikia upatikanaji sawa wa dawa muhimu kunahitajika mwitikio madhubuti wa mfumo wa afya unaoungwa mkono na dhamira dhabiti ya kisiasa, ushirikiano wa sekta nyingi na programu zinazozingatia watu ambazo hazimwachi mtu nyuma.”Kwa maneno mengine, dawa hizi haziwezi kuwa za matajiri pekee lazima mifumo ya afya, serikali na sekta binafsi zishirikiane kuhakikisha kila mtu anayehitaji anapata dawa kwa gharama nafuu.© UNOCHA/Ali Haj SuleimanDaktari akimpatia matibabu mgonjwa wa Saratani huko nchini SyriaSaratani, kisukari na unene uliopitiliza ni changamotoSaratani na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu kwa mamilioni ya watu duniani kila mwaka. Kwa mfano, saratani pekee inaua karibu watu milioni 10 kila mwaka.Kuongeza dawa mpya za saratani kama pembrolizumab na atezolizumab, ambazo zinasaidia kinga ya mwili kushambulia chembe chembe za saratani, kunaleta matumaini mapya hasa kwa wagonjwa katika nchi zenye rasilimali chache.Kwa upande mwingine, dawa za kundi la GLP-1 receptor agonists kama semaglutide na tirzepatide zimeingizwa kwenye orodha ili kusaidia wagonjwa wa kisukari cha aina ya pili wanaoishi pia na unene uliopitiliza au matatizo ya moyo na figo. Dawa hizi husaidia kudhibiti sukari, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na figo, na pia kusaidia kupunguza uzito.
Huko Bunia, jimboni Ituri Mashariki Mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, amepongeza juhudi za pamoja za walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo, FARDC, katika juhudi za kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha.Akizungumza wakati wa ziara yake iliyoanza Septemba 6, Mashariki mwa DRC katika jimbo la Ituri Lacroix amesema ushirikiano na kuaminiana kati ya mamlaka za jimbo la Ituri na vikosi vya Umoja wa Mataifa ni msingi muhimu wa kurejesha amani.Anasema “Nipo katika eneo liitwalo Fataki, katika jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hapa kuna kambi ya MONUSCO yenye kikosi cha Nepal, pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani. Maelfu ya watu wanalindwa hapa na wenzetu wa MONUSCO, na wanapatiwa msaada wa kibinadamu pamoja na ulinzi.”Gavana wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, alikaribisha msaada wa MONUSCO katika operesheni za kijeshi na mazungumzo ya amani, yakiwemo dhidi ya kundi la CRP katika eneo la Djugu Ituri ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani sasa wananufaika na ulinzi wa pamoja wa FARDC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Lacroix amesema “Katika jimbo la Ituri pekee kuna makambi kadhaa ya wakimbizi wa ndani, ambayo yanalindwa na MONUSCO, ambapo makumi ya maelfu kwa hakika mamia ya maelfu ya watu wanalindwa na wenzetu wa MONUSCO na wanapatiwa msaada.”Mkuu huyo wa operesheni za ulinzi wa amani ameohitimisha kwa kusema ziara hii ni muhimu sana kwani “Nipo hapa kuonyesha kile ambacho MONUSCO hufanya kila siku, tofauti ambayo MONUSCO inaleta katika kuwalinda raia hawa, tofauti kati ya kuwa salama au kuwa katika hatari kubwa, na nilitaka pia kutoa shukrani zangu kwa wenzetu wa MONUSCO. Aidha, nilitaka kuwasikiliza wananchi, hawa wakimbizi wa ndani, pamoja na jamii, na kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao zaidi ili kuboresha hali na kupiga hatua katika kukabiliana na ghasia ambazo bado zinaendelea katika eneo hilo.”Baada ya zira yake jimboni Itari Lacrix ameelekea katika mji Mkuu Kinshasa ambako amekutana na na kuzungumza na maafisa wa serikali.
Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu, Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."
Karibu kusikiliza jarida la Habari za Umoja wa Mataifa ambapo leo tunakuletea taarifa kuhusu hali ya hewa na athari za moto wa nyika, tutaelekea Gaza kusikia kutoka kwa mashuhuda wa madhila wayapatayo watoto na wananchi wa Gaza na kisha tutaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanaendesha mafunzo ya usalama barabarani.
Wakati mabilioni ya watu wakiendelea kuvuta hewa chafu inayosababisha zaidi ya vifo vya mapema milioni 4.5 kila mwaka, wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa (5 Septemba) wamebainisha madhara ya chembe ndogo ndogo za moshi kutoka katika moto wa nyika ambazo husafiri umbali mrefu duniani kote. Philip Mwihava na maelezo zaidi.(Taarifa ya Mwihava)“Ubora wa hewa hauheshimu mipaka,” anasema Lorenzo Labrador, Afisa wa Kisayansi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Anaendelea kueleza kwamba, “moshi na uchafuzi unaotokana na moto wa nyika katika msimu huu wa kihistoria katika Rasi ya Iberia tayari umepatikana Ulaya Magharibi, kwa hiyo athari zake hazibaki tu kwenye Rasi ya Iberia, bali zinaweza kusambaa kote barani Ulaya.”Akiwasilisha taarifa ya WMO kuhusu Hewa Safi na Tabianchi, ambayo inakusanya data kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, leo jijini Geneva, Uswisi Bwana Labrador ametangaza mwendelezo wa mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani.Ameonyesha ramani ya dunia ya mwaka 2024 iliyoonesha alama za chembechembe ndogo zinazojulikana kama “PM 2.5” kutokana na moto wa nyika, zikionekana kwa alama nyekundu kwenye maeneo ya Chile, Brazil na Ecuador, pamoja na Canada, Afrika ya Kati na Siberia. Takwimu hizo zinathibitisha mwenendo wa kuendelea kwa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita.Kwa upande wa habari njema, mwanasayansi huyo wa WMO amesisitiza kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika baadhi ya maeneo ya dunia.(Sauti ya Labrador) - sauti ya kiume“Tunaona mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa hasa kwa kuhusiana na PM 2.5, na pia tunaona kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika maeneo fulani ya dunia, hasa mashariki mwa China na Ulaya, mwaka baada ya mwaka.”Mfano mzuri uliotolewa katika taarifa ya leo mashariki mwa China, katika miji kama Shanghai, ambako kumepigwa hatua katika kuboresha ubora wa hewa kwa kufungua bustani zaidi na kupanda miti mingi. Na ingawa bado kuna msongamano mkubwa wa magari, mengi sasa ni ya umeme.Hata hivyo WMO inasema licha ya mafanikio hayo, miji michache tu duniani ina viwango vya ubora wa hewa chini ya vile vinavyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO). Hii inamaanisha kuwa, licha ya maboresho ya karibuni, ubora wa hewa bado ni changamoto kubwa kwa afya ya umma.Umoja wa Mataifa unaongoza juhudi za kupambana na uchafuzi wa hewa majumbani ambao ni mojawapo ya vitisho vikubwa zaidi kwa afya ya umma duniani na hasa ni hatari kwa watoto.
Sasa twende Gaza, hii ni hadithi ya maisha, ya watoto wa Gaza wanaokabiliana na baa la njaa, hofu, na kuporomoka kwa kila kitu kinachowaweka hai. Ni hadithi inayoelezwa kupitia macho ya wale wanaoshuhudia mateso kila siku wakiwemo madaktari, akina mama, na wahudumu wa kibinadamu wanaopiga kengele ya tahadhari. Miongoni mwa wahudumu hao ni Tess Ingram afisa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Flora Nducha anasimulia alichokishudia(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Tess aliyefunga safari na kushuhudia hali halisi Gaza akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji wa Al Mawasi amesema mwenye macho haambiwi tazama na alichokishuhudia ni cha kutisha kwani jiji hilo sasa linazidi kuzama kwenye lindi la baa la njaa, vituo vya lishe vimefungwa, familia zinalia na kuhaha na watoto wanakufa kila uchao bila msaada.(Tess Ingram- Sheillah)“Jiji la Gaza, kimbilio la mwisho kwa familia za Kaskazini, linakuwa mahali ambapo utoto hauwezi kuishi. Ni jiji la hofu, wakimbizi na mazishi.”Anasema zaidi ya nusu ya vituo vya lishe vya watoto vimefungwa na kina mama wanapofika hospitalini wakiwa wamebeba watoto wao unaoweza kuhesabu mbavu sababu ya kukonda wanaambulia patupu kwani msaada ni haba na kwengine hakuna kabisa.(Tess Ingram 2-Sheilah):“Kilichokuwa hakifikiriki si jambo lijalo ni hali ambayo iko hapa tayari. Kuanguka kwa huduma muhimu na kunawaacha watoto wasiojiweza Gaza wakihaha kusalia uhai.”Tess anasema ukiingia katika vituo vya msaada ndio utatambua wanachokipitia watoto wa Gaza kwani, mateso yanaonekana bayana(Tess Ingram 3-Sheillah)“Saa moja tu ndani ya kliniki ya lishe inatosha kuondoa shaka na shuku yoyote uliyonayo ya endapo Gaza kuna baa la njaa.”UNICEF inasisitiza wito wake kuwa raia walindwe, msaada wa chakula na dawa upelekwe kwa wahitaji bila vizuizi. Kwa sababu watoto wa Gaza bado wako hai na dunia ina uwezo wa kuamua endapo wasalie hai.
Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu kama "moto taxi" nchini CAR na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.Kwa mujibu wa MINUSCA Hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama na kujenga uhusiano mwema kati ya vikosi vya usalama na raia.Akizungumza kuhusu umuhimu wa hatua hii, Kamanda wa Mkoa wa Plateaux(PLATIU) na Bas-Oubangui(BA OBANGI), Douflé Avi Chico( DOFLE AVII CHIKO BERNAA) Bernard, amesema,CUT- Sauti ya Douflé Avi Chico Bernard“Kwa kushirikiana na MINUSCA, kupitia brigedi yao ya magari, tunafanya kazi ya kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara, waendesha pikipiki au teksi, ili kupunguza ajali nyingi ambazo kwa bahati mbaya zinagharimu maisha ya watu. Tutaendelea na kampeni hizi kubwa ili kurekebisha hali hii.”Kwa upande wa watumiaji wa barabara, dereva wa pikipiki za abiria, Jean Terence Bokassa (JANI TEREE BOKASA), ameomba serikali iimarishe udhibiti wa sekta hiyo.CUT- Sauti ya Jean Terence Bokassa“Tunaomba serikali ihakikishe usalama wa waendesha pikipiki za abiria kwa sababu sisi ni watu kama wengine. Tunatoka nje kutafuta riziki, lakini maisha yetu yako hatarini. Tungependa serikali itusaidie kwa kuwafundisha ndugu zetu ambao hawana leseni ya udereva kanuni za barabarani ili kuhakikisha usalama wao.”Nattss.. Sauti za magari honi nk.Doria hii ya pamoja inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na ISF, wote wakiwa wamejitolea kulinda raia na kupunguza ajali za barabarani na MINUSCA inasema wananchi wakipata uelewa wa kutosha basio sio tu barabara zitakuwa salama bali pia idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vitapungua.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT lataka wakusanyaji na wachakataji wa taka watambuliwe kwani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha mazingira safi na salama mijini-Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza Papua New Guinea kwa kuwa kisima cha kuvuna hewa ukaa na kuzitaka nchi za G-20 kuwajibika katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi-Nchini Mali, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya juu ya kuzorota zaidi kwa hali ya haki za binadamu. -Na leo katika jifunze Kiswahili Je wafahamu maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"? basi msikilize mtaalam wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, hii leo utasikia juhudi zinazofanyika kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Kutoka barani Afrika utasikia juhudi za kulinda raia wa Sudan Kusini wanaoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko jimboni Tambura na kutoka nchini Tanzania utasikia msaada kwa wakimbizi walioko magharibi mwa taifa hilo.
Juhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko.Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ambao walikuwa wa kwanza kupeleka msaada kwenye eneo la tukio, Bwana John Aylieff, akiwa mjini Kabul amesema, “WFP inaweza tu kumudu kuwalisha waathirika wa tetemeko la ardhi kwa wiki chache zijazo kabla ya ufadhili kuisha.”Kwa upande wake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linapeleka msaada muhimu wa dharura kutoka maghala yake yaliyopo Kabul, ikiwemo mahema, blanketi na taa za sola. Pia maelfu ya wanajamii wa eneo hilo wameelekea eneo lililoathirika kusaidia juhudi za uokoaji, wakiwa na maji na chakula.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwaka 2016, wamekuwa wakitoa huduma muhimu ikiwemo kufunga mifumo ya maji, kujenga vyoo, na kusambaza sabuni na mahitaji mengine ya usafi.Miongoni mwa wanaofanya mabadiliko kupitia msaada huo ni Ahunga Msama, mkimbizi mwenye umri wa miaka 55 kutoka DR Congo, ambaye ni afisa msimamizii wa huduma za maji, usafi, kujisafi na usafi wa mazingiira WASH katika kambi ya Nyarugusu.(AHUNGA CLIP 1)“Ninasaidia jamii yetu ya kambi ya Nyarugusu ili wawe wanapata maji safi na salama”Ahunga anasema jamii yake iliteseka sana iliteseka sana kwa magonjwa yanayosababishwa na maji machafu ndio maana aliamua kuchukua hatua kulinda afya zao. Kila siku ahakikisha watu wanapata maji safi na huduma za usafi salama.Akiwa pamoja na wakimbizi wenzake, Ahunga anapita nyumba kwa nyumba kufundisha familia jinsi ya kuzuia magonjwa kupitia usafi kwani anaamini elimu ni ufunguo(AHUNGA CLIP 2)“Tunasaidia kuelimisha jamii yetu ili wawe wasafi. Wawe na vyoo, wawe na mabafu, wawe na vichanja na wawe na mashimo ya takataka.”Watu wakielewa, wanaweza kujilinda.Anasema watu wakieelewa ni rahisi kujilinda na juhudi zake zinaokoa maisha na kuhamasisha wengine, zikionyesha kwamba hata katika mazingira magumu, wakimbizi wanaweza kuongoza mabadiliko katika jamii zao na anasema hilo ni la muhimu sana kwani(AHUNGA CLIP 3)“Tunasaidia jamii yetu ili wajilinde na magonjwa ya milipuko”Kwa msaada wa UNHCR na Baraza la Wakimbizi la Norway, maelfu ya wakimbizi katika kambi za wakimbizi za Kigoma sasa wana maji salama, usafi wa mazingira ni bora, na wana matumaini mapya ya maisha.
Katika jitihada za kuimarisha amani na usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake wa amani nchini humo UNMISS wameendelea kuimarisha ulinzi na kuongeza doria za magari usiku na mchana huko Greater Tambura katika jimbo la Equatoria Magharibi.Sabrina Saidi anaangazia juhudi za UNMISS katika kuhakikisha hali ya usalama inarejea na wananchi waliokimbilia katika kambi za wakimbizi kusakama usalama wanarejea makwao.TAARIFA YA SABRINA SAIDI)NAT...Video ya UNMISS inaanza kwa kumulika doria zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko katika kaunti ya Greater Tambura katika jimbo la Western Equatoria, kusini-magharibi mwa nchi ya Sudan Kusini karibu na mipaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Tangu mwaka 2021, mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, umeendelea kugharimu maisha ya watu wengi na kuwalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.Wananchi waliokumbwa na hofu wamekuwa wakijificha vichakani, wengine wakikimbilia nchi jirani, huku wengi wakitafuta hifadhi katika kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani zilizopo maeneo ya karibu.Ili kuwalinda vyema raia UNMISS wameimarisha uwepo wao katika eneo hilo na kuongeza doria za magari usiku na mchana, wakipita katika barabara mbovu zilizotapakaa tope na kuharibiwa na mvua. Walinda amani hao maarufu kama 'Blue Helmets', wamekuwa wakitembelea kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani na kuzungumza na jamii mbalimbali za kikabila zilizopata hifadhi huko.Tereza Martin ni mmoja wa wakimbizi wa ndani aliyepata hifadhi na hapo, anazungumza kwa hofu na simanzi...CUT: Sauti ya Tereza Martin"Hatuelewi chanzo cha mzozo huu. Tumekuwa tukiishi katika kambi hii kwa takribani miaka sita, tukiishi kwa njaa na mateso. Makazi yetu ya muda ni mabovu. Msimu wa mvua umefanya hali kuwa mbaya zaidi, sasa tunalala juu ya maji ya mvua. Hatuwezi kwenda shambani kwa hofu ya kushambuliwa. Tunaomba serikali na wadau kutuangalia kwa jicho la huruma."NAT....Margret Dominic naye ni mkimbizi wa ndani kambini hapo, anasema doria hizi zinampa amani CUT: Sauti ya Margret Dominic-"Hatuwezi kutoka nje ya kambi. Tunaweza kulala kwa sababu wanapiga doria usiku. Kama wasingekuwepo, hatujui kama tungeweza hata kupata usingizi."Emmanuel Dukundane ni Afisa wa Masuala ya Kiraia wa UNMISS, anasema wanajenga kambi mpya katika maeneo ya kimkakati.CUT: Sauti ya Emmanuel DukundaneHili lina maana kubwa sana kwa sababu tuna rasilimali nyingi, na kwa kujiweka katika kambi hiyo mpya, tutaweza kufanya doria zaidi, kufanya mazungumzo zaidi, na kuwezesha mchakato wa upatanisho na amani kwa ujumla."Ingawa UNMISS itaendelea kuisaidia serikali ya Sudan Kusini katika kuwalinda raia wa Greater Tambura, amani ya kweli na upatanisho wa kudumu vinapaswa kukubaliwa na kupatikana kupitia juhudi za jamii husika na viongozi wao wenyewe.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.Nchini Afghanistan ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea juzi jumapili, wafanyakazi wa misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanafikisha misaada kwa waathirika. Akizungumza na waandishi wa habari kutokea Kabul Afghanistan Indrika Ratwatte ambaye ni mwakilishi wa UN nchini humo amesema “Sio rahisi kufika maeneo yaliyoathirika kitu ambacho kinawafanya majeruhi waendelee kufungiwa.” Ametaja juhudi za haraka zinazofanyika ni pamoja na kuzika miili ya waathirika na kufukia mifugo ili kuzuia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka.”.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Jaridani leo tunaangazia Majaribio ya Nyuklia, na machafuko nchini Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Nepal na mashinani tunasalia huko huko Sudana Kusini, kulikoni?Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa yakupinga Majaribio ya Nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu kuongezeka kwa hatari za nyuklia kufuatia mvutano wa kisiasa unaondelea duniani na amehimiza kuridhiwa kwa mkataba wa kupiga marufuku majaribio hayo ya kinyuklia.Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo.Makala tunakwenda nchini Nepal kumulika suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.Na katika mashinani fursa ni yake Anna Pita, Msimamizi wa hospitali ya Kator nchini Sudan Kusini akieleza ni kwa jinsi gani mifumo ya nishati ya jua iliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na wadau wake inabadilisha utoaji wa huduma katika hospitali na vituo vya afya nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ametoa wito kwa mataifa yote kuridhia mara moja Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBT), akisema “ni wakati wa kunyamazisha mabomu kabla hayajasikika tena.”
Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo. Kupitia video ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIMSS Flora Nducha anamulika kauli za baadhi ya wanawake waathirika wanaosihi katika kambi ya wakimbizi wa ndani.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipaka ya Ukraine kama inavyotambuliwa kimataifa.Kuhusu Mashariki ya Kati Katibu Mkuu António Guterres akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ameonya kuwa operesheni za kijeshi mjini Gaza zitakuwa na zahma kubwa na amesisitiza “hili lazima likome.” Amesema njaa si tishio tena bali janga la sasa, huku raia, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wakiuawa wakati “macho ya dunia yakitazama.” Guterres ameikumbusha Israel wajibu wake wa kisheria kulinda raia na kuruhusu msaada wa kibinadamu bila vikwazo akisema “Hakuna visingizio tena. Hakuna vizuizi tena. Hakuna uongo tena,” akitoa wito wa usitishaji mapigano haraka na kuachiliwa kwa mateka wote.Kikosi cha 11 cha Tanzania TANZBATT 11 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kimetoa msaada wa magodoro kwa raia walioathirika na machafuko ya karibuni katika kijiji Oicha jimboni Kivu Kaskazini. Miongoni mwao ni Bi Masika Jistine na Mzee Bahati Paluku ambao hawakusita kuonesha furaha yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
“Leaders have to be a little delusional and have a lot of audacity.” From the first minutes, Jerjuan Howard plants that flag and then shows the receipts—why “youth development, community development must go hand in hand,” how a Gen Z squad of 30-and-under staff is running a league of 300 students across 20+ schools, and why “Detroiters…have everything that we need already—it's just about coming together to make it happen.” In this Detroit is Different conversation, Jerjuan and Khary trace a straight line from porch talk to policy: debates on whether to demolish the RenCen, backyard chickens and food grading ordinances, and the big one—“African cultural sovereignty… vs. political representation.” Jerjuan calls himself a middleman between elders and the youth—“my grandma used to say, ‘eat the meat and throw away the bones'”—so Umoja turns what kids already love (“kids already like to argue”) into a vehicle for critical thinking, city pride, and leadership. We dig into the audacity behind taking Detroit kids to Africa, the team-captain model that makes students league ambassadors, and why “indirect action is… just as responsible” as bad policy when communities are ignored. He lays out the build on Puritan: the open-air Umoja Village, a once–25-year-vacant building becoming a Black-authored bookstore and third space one block away (“for us and by us”), and a community-driven health clinic on deck—proof that Legacy Black Detroit isn't nostalgia, it's blueprint. Detroit is Different is a podcast hosted by Khary Frazier covering people adding to the culture of an American Classic city. Visit www.detroitisdifferent.com to hear, see and experience more of what makes Detroit different. Follow, like, share, and subscribe to the Podcast on iTunes, Google Play, and Sticher. Comment, suggest and connect with the podcast by emailing info@detroitisdifferent.com
Kwa zaidi ya muongo mmoja, eneo la Nyiragongo lililoko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) limekumbwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu wa kudumu kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha. Maelfu ya familia wamekimbia makazi yao na watoto wengi kulazimishwa kujiunga na makundi hayo ya kijeshi. Kati ya mwaka 2024 na 2025, kuzuka upya kwa mapigano kunakohusishwa na kuibuka tena kwa waasi wa M23 kumeongeza zaidi hali ya hatari kwa wakazi wa eneo hilo, hasa watoto na vijana. Ili kuleta ahueni kwa wakazi, Umoja wa Mataifa umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana basi na Anold Kayanda kwenye makala hii.
Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au kwingineko. Mkiwa mbali na familia zenu, mbali na nchi yenu, katika mazingira yenye changamoto, na wakati mwingine katika hali hatarishi.”Anawapa moyo zaidi askari lakini akiwakumbusha kuwa wao ni kioo cha ulimwengu wazingatie maadili“Na tunathamini sana kujitolea kwenu. Tunathamini sana kwamba mnaenda kuwasaidia ndugu zenu katika nchi nyingine, iwe ni nchi jirani au sehemu iliyo mbali. Mnapokwenda, mnaliwakilisha dunia. Mnawakilisha watu wa dunia.”Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang'are akamthibitishia mgeni kwamba askari hawa wameiva na hakuna kisingizio chochote cha kutozingatia maadili huko wameandako, kisha akawahoji, Nao wanajibu, “twende pamoja, turudi pamoja.”
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika maadhimisho ya siku ya Ziwa duniani; Maandalizi ya walinda amani kwenda kuhudumu CAR ma DRC; Msaada wa MONUSCO kwa wakazi wa Kivu Kaskazini; Aliyerejesha fadhila kwa WFP.Leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ziwa Duniani yakibeba maudhui "Ziwa ni uti wa mgongo wa sayari yetu" na ili kuthibitisha hilo tunakupeleka Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako , Bosco Cosmas kutoka Radio washirika SAUT FM anamulika maoni ya wananchi ni kwa vipi ziwa Victoria limekuwa msaada na mkombozi kwao.Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Anold Kayanda anatupeleka eneo la Maziwa Makuu barani Afrika kusikia harakati za Umoja wa Mataifa kuinua wakazi waliokumbwa kwenye mizozo.Mashinani kutana na Moses Komakech Meneja wa ghala la chakula la shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP lililoko Gulu katika jimbo la Acholi Kaskazini mwa Uganda ambapo baada ya kuwa mnufaika wa mgao wa chakula wa WFP, sasa anaendesha ghala la shirika hilo linalohudumia wakimbizi 800,000.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakulatea-Ripoti mpya kwa jina Maendeleo katika Maji ya Kunywa na Kujisafi Majumbani iliyozinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kwamba, licha ya hatua kupigwa, mtu 1 kati ya 4 duniani bado hana upatikanaji wa maji salama ya kunywa. -Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imetoa wito kwa mamlaka za Misri kukomesha mfumo wa “mzunguko” unaofanya wakosoaji wa Serikali kuzuiliwa kiholela na kwa muda mrefu, hata baada ya kumaliza vifungo vyao. - Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR leo limepongeza Serikali ya Kifalme ya Thailand kwa kupitisha azimio litakalowapa wakimbizi wa muda mrefu kutoka Myanmar haki ya kufanya kazi nchini Thailand.-Katika mada kwa kina tunamulika uzinduzi wa shule ya kwanza ya Akili Mnemba iliyoanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women huko ukanda wa Asia na Pasifiki-Na mashinani utamsikia Ibrahim Al-Najjar mkimbizi huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli akielezea hali tete ya ajira hivi sasa tangu vita ianze Oktoba 7, 2023.
Baada ya miaka miwili ya vita katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel Ijumaa tarehe 22 Agosti Umoja wa Mataifa ukatangaza jambo baya zaidi, ripoti ya njaa duniani IPC ikathibitisha wananchi wa Gaza rasmi wana kabiliwa na baa la njaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ni moja kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo pamoja na hali ya vita yamekuwa yakitoa msaada wa chakula huko Gaza na wameeleza kwamba baa la njaa lazima likomeshwe kwa gharama yoyote ile. Kusitishwa kwa mapigano mara moja na kukomesha mzozo ni muhimu ili kuruhusu misaada kuweza kuingizwa Gaza ili kuokoa maisha. Makala hii Leah Mushi anamuangazia mmoja wa watoto wanaokabiliwa na njaa
Leo Agosti 25 ni miaka minane tangu kufurushwa kwa wingi watu wa kabila la Rohingya kutoka katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa mshikamano wa kimataifa kuwasaidia kwani mateso kwa watu hao yanaendelea kuwa mabaya zaidi kila uchao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Asante AssumptaMyanmar (zamani ikiitwa Burma) ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye zaidi ya makabila 100, inayopakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.Warohingya wanafurushwa na kuteswa kwasababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria kwa madai kuwa walitoka Bangladesh ingawa wameishi vizazi na vizazi nchini Myanmar. Pia sababu ya imani yao kwa uislamu miongoni mwa sababu nyingine.Ni miaka minane sasa tangu ufurushwaji mkubwa wa jami hii kutoka jimbo la Rakhine pwani ya Magharibi mwa Myanmar. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaonya kuwa Warohingya na raia wengine bado wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu na kufurushwa. Anaeleza wasiwasi wake kuhusu tarifa za kufukuzwa na kupunguzwa kwa nafasi za hifadhi katika ukanda huo, huku wakimbizi walioko Bangladesh wakikabiliana na upungufu mkubwa wa msaada wa chakula, elimu na huduma za afya.Guterres anasisitiza tena wito wake wa kulindwa kwa raia wote kwa mujibu wa sheria za kimataifa na anataka mshikamano mkubwa wa kimataifa. Hata hivyo ana matumaini kuwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Rohingya utakaofanyika New York mwezi ujao utasaidia kupata suluhu za kudumu.Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anaeleza kuwa jeshi la Myanmar na Jeshi la Rakhine bado wanaendeleza uhalifu mkubwa dhidi ya Rohingya bila kuchukuliwa hatua, kinyume na sheria za kimataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na anatoa wito wa kukomesha matendo hayo ili kuvunja mzunguko wa vurugu.
Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje? kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa mapacha wengine wawili ambao sasa wana umri wa miezi tisa na kwa bahati mbaya wote wana utapiamlo kutokana na changamoto ya chakula.“Hapa Dori tumebarikiwa watoto mapacha lakini wametukuta hatua makazi, hatuna chochote na tuna njaa na kibaya zaidi sikuwa hata na maziwa ya kutosha kuwanyonyesha”Watoto wa Fadima wamekuwa wakiishi kwa msaada wa kibinadamu unaotolewa na mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF ambayo sasa inasema hali yao inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya kimataifa misaada wanayoitoa na hivyo kuhatarisha maisha na mustakabali wa watoto wake. Fadima anasema“Unapotawanywa na machafuko huwezi kufanya kazi, unakuwa kama mtu asiye na ajira na hapo ndio madhila yanapokuwa makubwa zaidi, lakini bado hapa ni bora kuliko ningesalia kijijini kwetu.”Kwa mujibu wa UNICEF Burkina Faso ni moja ya migogoro ya kibinadamu iliyopuuzwa zaidi duniani. Ingawa UNICEF iko hapa kusaidia, lakini inasema msaada zaidi unahitajika haraka.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.
Tarehe 18 Agosti mwaka 2025 siku ya Jumatano, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama walikutana kujadili Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL/Da'esh.Walikabidhiwa ripoti hiyo ya 21 ikimulika vitisho vinavyotokana na kikundi hicho ambacho kirefu chake ni Islamic State in Iraq and the Levant au pia Da'esh. Ripoti ikigusia tishio la kikundi hicho katika maeneo mbalimbali duniani, lakini makala hii initajikita zaidi barani Afrika!
Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki hii hapa makao makuu ya Umoja wa mataifa kuangazia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL kijulikanacho pia kama Da'esh.Na katika mashinani fursa ni yake Abraham Mwani mwandishi wa habari za wakimbizi kutoka Radio Pacis miongoni mwa wananufaika wa mafunzo ya UNESCO ya kuwezesha vyombo vya habari kusimulia vyema habari za wakimbizi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.”Flora Nducha na taarifa zaidi
Jaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura.Na katika mashinani Mwanzilishi na mratibu wa Kundi la Utetezi la Darfur, Ikhlass Ahmed amelielezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York kwa njia ya video jinsi wanavyokabiliwa na kuenea kwa kasi kwa unyanyasaji wa kingono.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano. Flora Nducha anafafanua zaidi
Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi pamoja kuhakikisha wanatoa fursa ya ufikiaji wa kibinadamu kwa watuwenye uhitaji na kunakuwepo na uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu zikijumuisha ulinzi kwa wahudumu wa kibinadamu na wa Umoja wa Mataifa”.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi ya kundi la waasi wa Allied Democratic Forces, ADF kati ya tarehe 9 na 16 Agosti, katika maeneo ya Beni na Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, yaliyoua raia 52, wakiwemo wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamehusisha utekaji nyara, uporaji, na uchomaji wa nyumba na magari, na kuwaacha wakazi ambao tayari wako katika hali ngumu ya kibinadamu katika mateso zaidi.Na katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya wahudumu wa binadamu, huduma na kujitolea kwa wanachama 270 wa Kikozi cha Polisi cha walinda amani kutoka Ghana wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), wakiwemo maafisa wanawake 63, ilitambuliwa kwa kutunukiwa Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Heshima kwa juhudi zao, zikiwa ni pamoja na kuwalinda raia, kuwezesha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kukuza haki za binadamu na kujenga amani. Bismark Achaab, Msimamizi Mkuu wa Kitengo hicho anatoa shukrani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Kuelekeza maadhimisho hayo hapo kesho Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masual ya Watoto UNICEF limetengeneza makala inayoangazia watoa huduma wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Leah Mushi anatujuza kilichopo katika makala hiyo.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.
Jaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Na katika mashinani nampisha Mchanga Omari Kombo kutoka Pemba Zanzibar ambaye ni mnufaika wa mpango mpya wa afya ya uzazi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF na wadau wake umewasaidia wanawake wajawazito kama kuondokana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya njema.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
Kutana na Godlove Makunge, kijana huyu wa kitanzania ambaye safari ya maisha yake imedhihirisha kuwa chochote unachoweka nia na utashi kitafanikiwa. Godlove ambaye elimu yake ni ya kidato cha nne, hakuweza kuendelea na masomo zaidi. Alichukuliwa na mtu mmoja afanye kazi za ndani kutoka Morogoro hadi Lindi na kisha akaishia Mtwara, kusini-mashariki mwa Tanzania ambako huko aliona fursa ya kujipatia kipato kutokana na taka zilizokuwa zinasambaa mitaani. Aliasisi kampuni ya usafi na mazingira iitwayo Shikamana Investment. Sasa kampuni yao ya ubia imeajiri vijana 6. Alishiriki mafunzo ya uchumi rejeleshi yaliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP mkoani Mtwara. Sawiche Wamunza, Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati UNDP alizungumza na Bwana Makunge baada ya mafunzo hayo ili afahamu amejifunza nini.
Jaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambaye baada ya mafunzo ya siku tatu ya uchumi rejeleshi katika mkoa wa Mtwara, Kusini-Mashariki mwa Tanzania alizungumza na Godlove Makunge Muasisi na Mkurugenzi wa kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira, iitwayo Shikamana Investment. Bwana Makunge anaanza kwa kuelezea mtazamo wa jamii kwake baada ya kuamua kuanza kuzoa taka.Na katika Radwa Ahmed, Mkimbizi kutoka Sudan ambaye alianza kwa kuoka mikate kwa ajili ya familia yake, na kwa ufadhili wa shirika la Umoja wakimbizi Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameweza kuigeuza talanta yake kuwa biashara ya kuuza mikate na kuajiri wakimbizi wenzake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Australia ita tambua Palestina kama taifa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa Septemba.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nchini Kenya wanaolima mbogamboga kupitia mradi uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wa kilimo cha bustani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!