POPULARITY
Baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani, waasi wa M23/AFC waliondoka kwenye mji wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivyo, rais Felix Tshisekedi ameelezea kitendo hicho kama kiini macho kwa jumuiya ya Kimataifa, kauli ambayo imeungwa na mkono na jeshi la FARDC wanaosema, waasi hao wamejificha katika milima inayopatikana na mji huo. Kuchambua kinachoendelea, tunaungana Mali Ali akiwa jijini Paris na François Alwende akiwa jijini Nairobi.
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa ambapo hii leo mada kwa kina inaangazia juhudi za kuwa na nishati safi nchini Tanzania ambapo vijana watazungumzia mradi wao wa kuchakata taka za plastiki na kupata nishati safi ya kupikia. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari ukiangazia wakimbizi wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC, Masuala ya Haki za Binadamu nchini Burundi na Matumaini ya watoto wa Gaza. Mwenyeji wako ni Leah Mushi.
Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili, akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Sheilah Jepng'etich na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia tiba asili, machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ubakaji unaotumika kama silaha ya vita nchini humo humo.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa tiba za asili.Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hofadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka.Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili, akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hifadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, si shwari licha ya kutiwa saini kwa mkataba unaolenga kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka 30. Waasi wa M23/AFC wameudhibiti mji wa Uvira. Marekani inaonya kuichukulia hatua Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao ambao sasa wameahidi kuondoa vikosi vyake katika mji huo, lakini kwa masharti. Tunachambua kwa kina.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kwake Afisa Habari wa UN Stella Vuzo ambaye kandoni mwa mkutano wa UNEA-7 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki, alizungumza na Frida Amani, Mchechemuzi wa UNEP wa masuala ya mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema aina mpya ya virusi vya mafua inaenea kwa kasi duniani, ikiwa imeripotiwa katika zaidi ya nchi 30. WHO wanasema licha ya aina hiyo kutosababisha ugonjwa mkali zaidi wa mafua, chanjo bado ni kinga bora zaidi dhidi ya madhara makubwa na kulazwa hospitalini na inawahimiza wananchi, hasa makundi yaliyo hatarini, kupata chanjo mapema huku ikionya kuwa msimu huu wa likizo unaweza kuongeza maambukizi ya magonjwa ya njia ya hewa.Tuelekee Bujumbura Burundi ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo wamepatiwa hifadhi baada ya kukimbia machafuko nchini mwao. Innocent Chubaka kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR aliyeko katika kambi ya muda ya Mugara katika jimbo la Rumonge nchini Burundi anasema “tumepokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Congo ambao wamefika kupitia njia ya ziwa wakiwa na mitumbwi kuu kuu.Na kwa mara nyingine tena Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amezisihi pande zote katika mzozo nchini Sudan na Mataifa yenye ushawishi kuhakikisha mapigano yanasitishwa mara moja na kuzuia ukatili. Turk amelaani vikali mauaji ya raia zaidi ya watu 104 pia mauaji ya walinda amani sita wa Umoja wa Mataifa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Kaduguli, Kordofan Kusini, mnamo Desemba 13.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Makala hii imeangazia kwa sehemu kubwa hali iliyojiri kwenye mji wa Uvira mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Kenya kutoka kwa mkoloni wake Uingereza,nacho chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania chasema watu zaidi ya elfu mbili waliuawa wakati wa machafuko ya wakati wa uchaguzi wa octoba 29, na mengine mengi
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia mradi wa kilimo cha mpunga ulivyoleta ustawi kwa jamii ya katikati mwa Sudan unaofanikishwa kwa msaada wa mafunzo wa walinda amani wa UN kutoka Korea Kusini wanaohudumu katika UNMISS kupitia wanasayansi na wakulima wa eneo la Bor katika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Mapigano makali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha watu zaidi ya 200,000, na kusitisha msaada wa chakula kwa maelfu. Umoja wa Mataifa unasema hali katika Kivu Kusini imezorota kwa kasi, huku msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP ukisimama na shule zaidi ya 30 zikigeuzwa makazi ya dharura. Katika taarifa yake, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema hali imefikia kiwango cha hatari, akionya: “Familia zinazoishi kwa njaa sasa zinagawana chakula chao cha mwisho na watu waliokimbia makazi. Hii ni dharura inayovuka mipaka.” UN inazitaka pande zote kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu misaada kufika kwa walio hatarini.Mkutano wa kikao cha 7 wa Baraza La Mazingira la Umoja wa Mataifa UNE-7 unaeelekea ukingoni jijini Nairobi Kenya na miongoni mwa washiriki ni kijana mwanaharakati wa mazingira kutoka asasi ya Umoja wa Mataifa YUNA nchini Tanzania Ally MwamzoraNa leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Milima, ukisisitiza umuhimu wa milima kama “kitovu cha maji ya dunia.” Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, takriban asilimia 70 ya maji safi ya Dunia yamehifadhiwa kama theluji au barafu, yakitoa mito inayosambaza maji ya kunywa, kilimo, viwanda, na umeme wa maji na takriban watu bilioni mbili, ikiwa ni pamoja na jamii nyingi za asili, wanategemea maji ya milima kwa mahitaji yao ya kila siku, maisha, na tamaduni zao. Wataalamu wanasisitiza kuwa kulinda mazingira ya milima ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa vizazi vijavyo.Katika kujifunza lugha Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "“MWENDAWAZIMU HAPEWI UPANGA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangaziz siku ya Haki za Binadamu tukikuletea ujumbe wa Volker Türk, Safari ya manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu, na vikosi vya 4 na 5 vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania nchini DRC.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametumia Siku ya Haki za Binadamu hii leo kutoa onyo kali akisema ulinzi wa haki za binadamu uko mashakani wakati migogoro na ukandamizaji vinaongezeka kwa kasi isiyo na mfano.Kwa manusura wengi wa usafirishaji haramu wa binadamu, msaada hukatika mapema mno. Kutokana na rasilimali chache na mifumo isiyotoa huduma za muda mrefu, wengi hutolewa kwenye mfumo bila kupata usaidizi wa kutosha wa kisaikolojia au utambuzi unaozidi simulizi zao. Malaika Oringo, mama, mwanaharakati, na manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu ameamua kubadilisha hali hiyo. Kama mwanzilishi wa shirika la Footprint to Freedom, linaloongozwa na manusura na linalolenga kuwawezesha na kuwarejesha katika jamii waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, anatetea kuhakikisha sauti za manusura zinakuwa kiini cha utungaji wa sera na hatua za serikali duniani.Kikosi cha 4 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB MONUSCO, kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC kwa gwaride maalumu la makabidhiano lililofanywa na Tanzqrf ya 4 pamoja na Tanzqrf ya 5 katika makao makuu ya kikosi hico mjini Beni Mavivi katika jimbo la kivu kaskazini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kikosi cha 4 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB MONUSCO, kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC kwa gwaride maalumu la makabidhiano lililofanywa na Tanzqrf ya 4 pamoja na Tanzqrf ya 5 katika makao makuu ya kikosi hico mjini Beni Mavivi katika jimbo la kivu kaskazini. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Habibu Shaban
In this Jamhuri Day episode, Rev. Jotham Munene reflects on Kenya's journey to independence and what it truly means to live as a republic. He highlights our shared responsibility to participate in nation-building, uphold unity, pray for our leaders, and remain grateful for the freedoms we enjoy. It's a timely call to honor our heritage, embrace our role as citizens, and keep investing in the Kenya God has placed us in.#citamchurchonline #ChurchEverydayGet in touch with us:http://www.citam.org/churchonline@citam.org(+254) 784 277 277(+254) 728 221 221
Makala hii imeangazia kwa kina chimbuko la watu wa kabila la wanande, ambao kati yao wapo ambao wamejikita mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maarufu kama wayira na pia wengine ambao wamejikita katika mji wa Kasese na maeneo mengine nchini Uganda na ambao wanafahamika kama Bakonzo, kufahamu zaidi sikiliza makala hii na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na leo zinaanza siku 16 za uanaharakati kuelimisha umma kuhusu janga la ukatili wa kijinsia, tunamsikia mmoja wa waathirika wa ukatili wa kingono.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa onyo kali kuhusu ongezeko la ukatili mtandaoni dhidi ya wanawake na wasichana.Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya wanawake UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC inaonya kwamba mwaka 2024, wanawake na wasichana 50,000 waliuawa na wapenzi au jamaa sawa na mwanamke mmoja kila dakika 10.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonya kwamba uchumi wa Eneo la Palestina Linalokaliwa kwa Mabavu na Israel umerudi nyuma miaka 22 kwa muda usiozidi miaka miwili kwani umeingia katika hali mbaya zaidi ya mdororo kuwahi kurekodiwa, huku miongo ya maendeleo ikifutwa na operesheni za kijeshi zilizodumu kwa muda mrefu pamoja na vizuizi vya muda mrefu.Katika kujifunza lugha Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MADUYUNI"Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya maendeleo na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika, mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Gaza na ukatili wa kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametoa ujumbe mzito kwenye Mkutano wa Muungano wa Afrika AU na Muungano wa Ulaya EU, unaofanyika mjini Luanda, Angola akionya kuwa dunia “inabadilika kwa kiwango cha kutisha,” huku janga la tabianchi, ukosefu wa usawa na mvutano wa kimataifa vikichochea misukosuko mipya duniani.Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake yangalikuwa vipi.Mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Ukanda wa Gaza yamemalizika majuzi baada ya siku nne mfululizo za michuano. Mashindano haya yanaandaliwa na Chama cha Soka cha Watu Waliokatwa Viungo cha Palestina kama sehemu ya juhudi za kuwasaidia majeruhi na kuthibitisha ushiriki wao endelevu katika shughuli rasmi za michezo.Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake yangalikuwa vipi. Je ilikuwaje? Tuungane na Sheilah Jepngetich kwa simulizi zaidi.
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mbinu bunifu za kilimo cha kakao nchini Peru, na mradi wa miundombinu wa kupunguza athari ya mafuriko na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii nchini Rwanda.Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi.Katika msitu wa Amazon upande wa nchi ya Peru, jamii za watu wa asilizimeonesha namna mbinu bunifu za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Yote haya yanakuja wakati dunia ikiendelea kujadili mustakabali wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa COP30 unaoendelea huko Belém, Brazil.Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo, kwa wakati mwingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Jarida hii leo tunamulika harakati za kuzuia mauaji ya kimbari El Fasher, Sudan, hakuna dalili za kumalizika kwa janga la njaa mashariki mwa DRC na furaha kwa watoto waliopatiwa mabegi ya kwenda shule huko Tigray, Ethiopia.Unapokabiliana na ukatili na mauaji ya kimbari ni vema kuhakikisha wanaotekeleza wanafahamu kuwa wanafuatiliwa na kutazamwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao, amesema Chaloka Beyani Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari.Mgogoro katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unaendelea kuwa mbaya huku mapigano yakizidi, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuzidisha njaa kali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeeleza leo.Nchini Ethiopia, Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Tigray watoto wamefurahia kupatiwa vifaa kwa ajili ya kurejea upya shuleni baada ya vita ya muda mrefu, shukrani kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Uchaguzi mkuu uliofanyika katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, na ambao uligubikwa na maandamano; mkutano wa Paris nchini Ufaransa kuhusu amani ya mashariki mwa DRC na eneo la maziwa makuu, siasa za nchini Kenya, Uganda lakini pia mauaji yaliyotekelezwa na kundi la RSF nchini Sudan, hali nchini Cameroon na Madagascar, kurejewa kwa mashambulizi nchini Ukraine, na huko Israeli dhidi ya Hamas
Leo jaridani tunamulika kimbunga Melissa huko Karibea, uhamishaji wagonjwa kutoka Gaza kwenda nchi za nje kupata huduma za kigeni na hali tete kwa watoto nchini Sudan. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaAntonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha athari kubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, limeongoza uhamishwaji wa kwanza wagonjwa kutoka Gaza tangu awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano. Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura. Flora Nducha na taarifa zaidi.Nchini Sudan hususani katika eneo la El Faher kusinimagharibi mwa nchi, hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya kila siku, huku ghasia, njaa, na vizuizi vya utoaji misaada vikiendelea kuathiri mamilioni ya watu wakiwemo watoto waliokwama katika maeneo ya vita. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati huu Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake, Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha madhara makubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Taarifa hiyo imemnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba “ana wasiwasi mkubwa” na anashikamana na serikali pamoja na wananchi walioathiriwa vibaya na Kimbunga Melissa.”Katibu Mkuu pia “Amewapa pole familia zote za waliopoteza wapendwa wao katika kimbunga hicho na anawatakia majeruhi wote ahueni ya haraka.”Umoja wa Mataifa umeanza kutoa msaada wa dharura, huku timu zake zikiwa tayari mashinani kusaidia kutathmini madhara na kusaidia juhudi za kitaifa. Pia, umetoa dola milioni nne kwa Haiti na vile vile dola milione nne kwa Cuba kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) ili kusaidia jamii kujiandaa na kupunguza madhara ya kimbunga hicho.Taarifa hiyo imesema Umoja wa Mataifa uko tayari “kutuma wahudumu wa ziada kwa muda mfupi na kuzindua maombi ya misaada ya dharura kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu yatakayosababishwa na kimbunga hicho.”Kimbunga Melissa ni miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Karibea, na kinatishia maisha ya mamilioni ya watu kutokana na mafuriko, uharibifu na watu kufurushwa katika makazi yao.
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea-Gaza Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP lasema usitishaji wa mapigano umeleta afueni kwa wakaazi kwani sasa misaada inaendelea kuwafikia wenye uhitaji-Naibu Mratibu wa Misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amekuwa ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na kujionea hali halisi ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani na msaada wa kibinadamu-Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa leo limesema katika tathimini yake kuwa ukataji wa misitu umepungua duniani kote ingawa bado kuna shinikizo na hatua zaidi zahitajika-Katika mada kwa kina tunakupeleka nchini Tanzania ambako Vyuo Vikuu vinachukua hatua ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan lile namba 17 la ubia kupitia umataifishaji. -Na kwenye jifunze Kiswahili unapata ufafanuzi wa methali " “NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
Hii leo jaridani tunaangazia tunzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer, juhudi za wapiga picha wanawake kwenye maeneo yenye mizozo katika kusongesha amani na usalama, na wafugaji Samburu nchini Kenya.Mwaka huu, Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer imekwenda kwa Olukemi Ibikunle, afisa wa magereza kutoka Nigeria anayehudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO. Tunzo hii inatambua mchango wake mkubwa katika kazi za haki na magereza kwenye operesheni za kulinda amani, pamoja na ujasiri wake wa kuvunja vizingiti vya kijinsia katika maeneo yanayoongozwa na wanaume.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuna maonesho ya picha 32 zinazoonesha harakati za wanawake kwenye maeneo yenye mizozo kusongesha amani na usalama, kwa mujibu wa azimio namba 1325 lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa miaka 25 iliyopita. Maonesho ya picha hizi zilizopigwa na wanawake yamepatiwa jina Kupitia Lensi Yake na yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau ili kudhihirisha ujasiri wa wanawake katikati ya mazingira hatarishi, wakihaha kuleta amani kwenye maeneo yao.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya wanatekeleza mradi unaowashirikisha wananchi wa Kauti ya Samburu katika kuhakika kuna upatikanaji wa chakula kwani eneo hilo linahali ya ukame ikiwa ni hatua mojawapo ya kutafsiri na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs huko mashinani. Tuungane na Sheilah Jepngetich anayetuletea tarifa hii iliyoandaliwa na UNICEF Kenya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Mwaka huu, Tunzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer imekwenda kwa Olukemi Ibikunle, afisa wa magereza kutoka Nigeria anayehudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO. Tunzo hii inatambua mchango wake mkubwa katika kazi za haki na magereza kwenye operesheni za kulinda amani, pamoja na ujasiri wake wa kuvunja vizingiti vya kijinsia katika maeneo yanayoongozwa na wanaume. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Ikiwa ni zaidi ya miaka minane tangu zaidi ya wakimbizi 750,000 waislamu wa kabila la warohingya wakimbie Myanmar kuelekea kwenye kambi kubwa nchini Bangladesh, mgogoro huo bado haujapatiwa suluhisho na leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa viongozi wamekutana kusaka suluhu ya kudumu kwa warohingya na makabila mengine madogo nchini Myanmar. Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia Afisa Mtawala Mkuu wa UN Courtenay Rattray amesema, “mgogoro huu, ambao umezidi kuongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi Myanmar ya mwaka 2021, unasigina haki za binadamu, utu na usalama wa mamilioni ya watu na unatishia uthabiti wa kikanda. Haitoshi tu kutathmini hali ilivyo. Tunapaswa pia kuendeleza mshikamano na kubuni suluhisho.”Amani nchini DRC imesalia bado ahadi, ni kauli ya Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama lililokutana leo kujadili hali Mashariki mwa DRC. Anasema hali inazidi kuwa tete. “Ghasia zinaendelea kushamiri jimboni Kivu Kaskazini hususan eneo la Rutshuru tangu waasi wa M23 watwae eneo hilo. Kuanzia mwezi Juni na kuendelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepokea maombi lukuki ya watu wakitaka ulinzi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na M23.”.Na mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamesisitiza wito wa kupatikana kwa sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, ili kupunguza machungu wakati huu ambapo Mpango wa Marekani wa Vipengele 20 unaibua matumaini ya kukomeshwa kwa mapigano. Ricardo Pires, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF amesema, “ni muhimu tupate sitisho la mapigano na misaada iweze sio tu kuingia na kuepusha baa la njaa, bali pia kuelekezwa maeneo ya kusini. Lakini vile vile kuhakikisha watoto na familia zao wanapata malazi bora wakati huu majira ya baridi kali yanakaribia. La sivyo italeta zahma ya afya kwa watoto na familia zao.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Ilikuwa majira ya saa tatu na dakika chache hivi asubuhi ya leo saa za New York nchini Marekani ambapo Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu amepewa fursa ya kuhutubia na ndipo ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukakosa utulivu. Wajumbe kwa makundi walinyanyuka katika viti vyao na kuondoka huku wakiwaacha maafisa wa Israel wakimpigia makofi kiongozi wao na pia nchi zinazoiunga mkono Israel zikasalia katika viti vyao ikiwemo Marekani.Baadhi ya wajumbe watoka njeKatika eneo la walipotakiwa kukaa wawakilishi wa Palestina kulikuwa wazi, huku katika eneo la Iran ikibakia picha iliyokusanya sura za baadhi ya watu wao waliouawa na mashambulizi ya Israel. Bwana Netanyahu kwa mara nyingine tena ameingia na ubao wenye picha ya ramani ya eneo la Mashariki ya Kati akiutumia kuishambulia Iran na kwa kutumia kalamu akiweka alama ya vema kuonesha namna ambavyo Israel imefanikiwa kupambana na ngome za Irani katika ukanda huo. Katika suti yake, kifuani upande wa kulia, Bwana Netanyahu pia ameweka kibandiko chenye QR Code na akawaambia watu kuwa Israel bado inakumbuka tukio walilofanyiwa na Hamas mwezi Oktoba mwaka juzi na kwamba ikiwa watu wamesahau hilo basi waelekeze simu zao kwenye QR Code hiyo kwenye nguo yake ili iwaoneshe madhara yaliyofanywa na Hamas.Majina ya mateka yakasomwaWaziri Mkuu huyo wa Israel ameyasoma majina ya mateka ambao bado wako mikononi mwa Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza na pia akaueleza mkutano kuwa amesambaza vipaza sauti au spika katika eneo lote la Gaza ili anapoongea leo, azungumze moja kwa moja na mateka huko walikofichwa. Na hapo akabadilisha lugha na kuongea kwa kihebrania akiwaahidi kuwa atawakomboa. Vilevile amedokeza kuwa kwa namna ya kiintelijensia Israel imefanya simu leo ziweze kusambaza hotuba katika ukanda wa Gaza na hivyo akautumia muda huo kupeleka ujumbe mkali kwa Hamas kuwa ataendelea kuwadhibiti. Bwana Netanyahu pia ameingia ukumbini na vibao viwili vyenye maswali na majibu ya kuchagua japokuwa jibu sahihi kwa mujibu wake na waliojibu kuwa ni All the Above, yaani majibu yote ni sahihi. Maswali yote yalikuwa yakiwatuhumu Iran, Hamas, Al Caeda, Hezbollah na Houthi kuwa pia wanaitakia kifo Marekani na wameua watu wengi Ulaya. Huenda hotuba hii ya Netanyahu ikaingia katika orodha ya hotuba tano ndefu zaidi baada ya ile ya Rais wa Marekani Donald Trump wa Marekani, Ya Mahmoud Abbass wa Palestina na Félix-Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao wote hao walitumia zaidi ya dakika arobaini licha ya muda wa hotuba uliopangwa kuwa angalau dakika 15.
Wakati dunia ikiadhimisha miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake. Kwako Kibego.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa washirirki ya mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hasa maadhimisho ya miaka 80 ya umoja huo. Pia tunamulika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita viwili vya dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa UN ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.Tukisalia na maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa , moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake.Kando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa watoa mada kwenye mashauriano hayo ambayo matokeo yake yatawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Taratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.
-Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80 chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo dola milioni 1 za kimarekani kutoka Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI
Huko Bunia, jimboni Ituri Mashariki Mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, amepongeza juhudi za pamoja za walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo, FARDC, katika juhudi za kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha.Akizungumza wakati wa ziara yake iliyoanza Septemba 6, Mashariki mwa DRC katika jimbo la Ituri Lacroix amesema ushirikiano na kuaminiana kati ya mamlaka za jimbo la Ituri na vikosi vya Umoja wa Mataifa ni msingi muhimu wa kurejesha amani.Anasema “Nipo katika eneo liitwalo Fataki, katika jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hapa kuna kambi ya MONUSCO yenye kikosi cha Nepal, pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani. Maelfu ya watu wanalindwa hapa na wenzetu wa MONUSCO, na wanapatiwa msaada wa kibinadamu pamoja na ulinzi.”Gavana wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, alikaribisha msaada wa MONUSCO katika operesheni za kijeshi na mazungumzo ya amani, yakiwemo dhidi ya kundi la CRP katika eneo la Djugu Ituri ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani sasa wananufaika na ulinzi wa pamoja wa FARDC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Lacroix amesema “Katika jimbo la Ituri pekee kuna makambi kadhaa ya wakimbizi wa ndani, ambayo yanalindwa na MONUSCO, ambapo makumi ya maelfu kwa hakika mamia ya maelfu ya watu wanalindwa na wenzetu wa MONUSCO na wanapatiwa msaada.”Mkuu huyo wa operesheni za ulinzi wa amani ameohitimisha kwa kusema ziara hii ni muhimu sana kwani “Nipo hapa kuonyesha kile ambacho MONUSCO hufanya kila siku, tofauti ambayo MONUSCO inaleta katika kuwalinda raia hawa, tofauti kati ya kuwa salama au kuwa katika hatari kubwa, na nilitaka pia kutoa shukrani zangu kwa wenzetu wa MONUSCO. Aidha, nilitaka kuwasikiliza wananchi, hawa wakimbizi wa ndani, pamoja na jamii, na kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao zaidi ili kuboresha hali na kupiga hatua katika kukabiliana na ghasia ambazo bado zinaendelea katika eneo hilo.”Baada ya zira yake jimboni Itari Lacrix ameelekea katika mji Mkuu Kinshasa ambako amekutana na na kuzungumza na maafisa wa serikali.
Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu kama "moto taxi" nchini CAR na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.Kwa mujibu wa MINUSCA Hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama na kujenga uhusiano mwema kati ya vikosi vya usalama na raia.Akizungumza kuhusu umuhimu wa hatua hii, Kamanda wa Mkoa wa Plateaux(PLATIU) na Bas-Oubangui(BA OBANGI), Douflé Avi Chico( DOFLE AVII CHIKO BERNAA) Bernard, amesema,CUT- Sauti ya Douflé Avi Chico Bernard“Kwa kushirikiana na MINUSCA, kupitia brigedi yao ya magari, tunafanya kazi ya kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara, waendesha pikipiki au teksi, ili kupunguza ajali nyingi ambazo kwa bahati mbaya zinagharimu maisha ya watu. Tutaendelea na kampeni hizi kubwa ili kurekebisha hali hii.”Kwa upande wa watumiaji wa barabara, dereva wa pikipiki za abiria, Jean Terence Bokassa (JANI TEREE BOKASA), ameomba serikali iimarishe udhibiti wa sekta hiyo.CUT- Sauti ya Jean Terence Bokassa“Tunaomba serikali ihakikishe usalama wa waendesha pikipiki za abiria kwa sababu sisi ni watu kama wengine. Tunatoka nje kutafuta riziki, lakini maisha yetu yako hatarini. Tungependa serikali itusaidie kwa kuwafundisha ndugu zetu ambao hawana leseni ya udereva kanuni za barabarani ili kuhakikisha usalama wao.”Nattss.. Sauti za magari honi nk.Doria hii ya pamoja inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na ISF, wote wakiwa wamejitolea kulinda raia na kupunguza ajali za barabarani na MINUSCA inasema wananchi wakipata uelewa wa kutosha basio sio tu barabara zitakuwa salama bali pia idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vitapungua.
Karibu kusikiliza jarida la Habari za Umoja wa Mataifa ambapo leo tunakuletea taarifa kuhusu hali ya hewa na athari za moto wa nyika, tutaelekea Gaza kusikia kutoka kwa mashuhuda wa madhila wayapatayo watoto na wananchi wa Gaza na kisha tutaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanaendesha mafunzo ya usalama barabarani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwaka 2016, wamekuwa wakitoa huduma muhimu ikiwemo kufunga mifumo ya maji, kujenga vyoo, na kusambaza sabuni na mahitaji mengine ya usafi.Miongoni mwa wanaofanya mabadiliko kupitia msaada huo ni Ahunga Msama, mkimbizi mwenye umri wa miaka 55 kutoka DR Congo, ambaye ni afisa msimamizii wa huduma za maji, usafi, kujisafi na usafi wa mazingiira WASH katika kambi ya Nyarugusu.(AHUNGA CLIP 1)“Ninasaidia jamii yetu ya kambi ya Nyarugusu ili wawe wanapata maji safi na salama”Ahunga anasema jamii yake iliteseka sana iliteseka sana kwa magonjwa yanayosababishwa na maji machafu ndio maana aliamua kuchukua hatua kulinda afya zao. Kila siku ahakikisha watu wanapata maji safi na huduma za usafi salama.Akiwa pamoja na wakimbizi wenzake, Ahunga anapita nyumba kwa nyumba kufundisha familia jinsi ya kuzuia magonjwa kupitia usafi kwani anaamini elimu ni ufunguo(AHUNGA CLIP 2)“Tunasaidia kuelimisha jamii yetu ili wawe wasafi. Wawe na vyoo, wawe na mabafu, wawe na vichanja na wawe na mashimo ya takataka.”Watu wakielewa, wanaweza kujilinda.Anasema watu wakieelewa ni rahisi kujilinda na juhudi zake zinaokoa maisha na kuhamasisha wengine, zikionyesha kwamba hata katika mazingira magumu, wakimbizi wanaweza kuongoza mabadiliko katika jamii zao na anasema hilo ni la muhimu sana kwani(AHUNGA CLIP 3)“Tunasaidia jamii yetu ili wajilinde na magonjwa ya milipuko”Kwa msaada wa UNHCR na Baraza la Wakimbizi la Norway, maelfu ya wakimbizi katika kambi za wakimbizi za Kigoma sasa wana maji salama, usafi wa mazingira ni bora, na wana matumaini mapya ya maisha.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipaka ya Ukraine kama inavyotambuliwa kimataifa.Kuhusu Mashariki ya Kati Katibu Mkuu António Guterres akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ameonya kuwa operesheni za kijeshi mjini Gaza zitakuwa na zahma kubwa na amesisitiza “hili lazima likome.” Amesema njaa si tishio tena bali janga la sasa, huku raia, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wakiuawa wakati “macho ya dunia yakitazama.” Guterres ameikumbusha Israel wajibu wake wa kisheria kulinda raia na kuruhusu msaada wa kibinadamu bila vikwazo akisema “Hakuna visingizio tena. Hakuna vizuizi tena. Hakuna uongo tena,” akitoa wito wa usitishaji mapigano haraka na kuachiliwa kwa mateka wote.Kikosi cha 11 cha Tanzania TANZBATT 11 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kimetoa msaada wa magodoro kwa raia walioathirika na machafuko ya karibuni katika kijiji Oicha jimboni Kivu Kaskazini. Miongoni mwao ni Bi Masika Jistine na Mzee Bahati Paluku ambao hawakusita kuonesha furaha yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au kwingineko. Mkiwa mbali na familia zenu, mbali na nchi yenu, katika mazingira yenye changamoto, na wakati mwingine katika hali hatarishi.”Anawapa moyo zaidi askari lakini akiwakumbusha kuwa wao ni kioo cha ulimwengu wazingatie maadili“Na tunathamini sana kujitolea kwenu. Tunathamini sana kwamba mnaenda kuwasaidia ndugu zenu katika nchi nyingine, iwe ni nchi jirani au sehemu iliyo mbali. Mnapokwenda, mnaliwakilisha dunia. Mnawakilisha watu wa dunia.”Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang'are akamthibitishia mgeni kwamba askari hawa wameiva na hakuna kisingizio chochote cha kutozingatia maadili huko wameandako, kisha akawahoji, Nao wanajibu, “twende pamoja, turudi pamoja.”
Kwa zaidi ya muongo mmoja, eneo la Nyiragongo lililoko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) limekumbwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu wa kudumu kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha. Maelfu ya familia wamekimbia makazi yao na watoto wengi kulazimishwa kujiunga na makundi hayo ya kijeshi. Kati ya mwaka 2024 na 2025, kuzuka upya kwa mapigano kunakohusishwa na kuibuka tena kwa waasi wa M23 kumeongeza zaidi hali ya hatari kwa wakazi wa eneo hilo, hasa watoto na vijana. Ili kuleta ahueni kwa wakazi, Umoja wa Mataifa umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana basi na Anold Kayanda kwenye makala hii.
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi pamoja kuhakikisha wanatoa fursa ya ufikiaji wa kibinadamu kwa watuwenye uhitaji na kunakuwepo na uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu zikijumuisha ulinzi kwa wahudumu wa kibinadamu na wa Umoja wa Mataifa”.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi ya kundi la waasi wa Allied Democratic Forces, ADF kati ya tarehe 9 na 16 Agosti, katika maeneo ya Beni na Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, yaliyoua raia 52, wakiwemo wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamehusisha utekaji nyara, uporaji, na uchomaji wa nyumba na magari, na kuwaacha wakazi ambao tayari wako katika hali ngumu ya kibinadamu katika mateso zaidi.Na katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya wahudumu wa binadamu, huduma na kujitolea kwa wanachama 270 wa Kikozi cha Polisi cha walinda amani kutoka Ghana wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), wakiwemo maafisa wanawake 63, ilitambuliwa kwa kutunukiwa Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Heshima kwa juhudi zao, zikiwa ni pamoja na kuwalinda raia, kuwezesha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kukuza haki za binadamu na kujenga amani. Bismark Achaab, Msimamizi Mkuu wa Kitengo hicho anatoa shukrani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mauaji Ituri, DRC; Haki za binadamu hususan suala la Israeli kukalia Palestina kimabavu; Mifumo ya kuzalisha chakula; Mradi wa umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola huko Bidibidi, Uganda. MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Volker Türk ameyahimiza mataifa yote ulimwenguni kuchukua hatua za haraka ili Israel ikomeshe uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayoikalia kimabavu, na kuhakikisha suluhu ya mataifa mawili inapatikana. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiKatika makala Sabrina Said anakupeleka Addis Ababa nchini Ethiopia, kumulika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa viongozi kuhusu mifumo ya uzalishaji chakula. Mkutano huu ni wa pili na unafanyika kwa siku tatu, leo ikiwa ni siku ya pili. Mashinani: Mary, Mkimbizi mwenye umri wa miaka 26 kutoka Sudan Kusini anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda. Yeye ni mkulima wa nyanya kutoka kikundi cha wakulima cha Anika ambao ni wanufaika wa mradi wa umwagiliaji wa Sola uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP.
MONUSCO, ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imelaani vikali shambulio lililoanza usiku wa juzi tarehe 26 hadi jana 27 Julai 2025 huko Komanda eneo la Irumu, takribani kilomita 60 kusini-magharibi mwa Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Taarifa iliyotolewa na MONUSCO jijini katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa imeeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa za uhakika, shambulio hilo lililofanywa na wapiganaji wa kundi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) limesababisha vifo vya raia wasiopungua 43 (wanawake 19, wanaume 15 na watoto 9).Inaripotiwa kuwa waathirika wengi waliuawa kwa kutumia silaha za jadi wakiwa ndani ya nyumba ya ibada. Watu kadhaa walitekwa nyara. Nyumba na maduka pia yalichomwa moto, jambo ambalo limezidisha zaidi hali mbaya ya mazingira ya kibinadamu ambayo tayari ni ya kutisha katika jimbo hilo.Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Masuala ya Ulinzi na Operesheni ambaye pia ndiye Kaimu Mkuu wa MONUSCO, Vivian van de Perre, amenukuliwa akisema, “mashambulizi haya ya kulenga raia wasio na hatia, hasa ndani ya nyumba za ibada, ni ya kushtusha na ni kinyume kabisa na viwango vyote vya haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. MONUSCO itaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka za DRC ili kuwalinda raia kwa mujibu wa mamlaka yake.”Kwa kushirikiana na mamlaka za eneo, MONUSCO imetoa msaada kwa hatua za awali, ikiwemo kuratibu shughuli za maziko na kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi. Wakati huohuo, MONUSCO imeongeza juhudi za kiusalama ndani na nje ya eneo la Komanda kwa kuongeza idadi ya doria katika eneo hilo.MONUSCO imeweka wazi kuwa inasalia na dhamira thabiti ya kushirikiana na mamlaka za DRC na jamii za wenyeji kusaidia kuzuia mashambulizi mengine, kuwalinda raia, kupunguza mvutano, na kuchangia katika kuimarisha utulivu katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kivita.Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umeeleza masikitiko na ghadhabu kubwa juu ya vitendo hivi vya kikatili, ambavyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu. Ujumbe huu unatoa rambirambi zake za dhati kwa familia na jamii zilizoathirika na unasisitiza mshikamano wake na wakazi wa maeneo hayo. MONUSCO pia inazitaka mamlaka za DRC kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji haya na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.Aidha, MONUSCO imeurudia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yote ya waasi kutoka nchi za nje kuweka silaha chini bila masharti na kurejea katika nchi zao za asili.
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Nigeria, na mradi wa nishati ya sola ya kusaidia wakulima nchini Ethiopia. Makala inakupeleka nchini Afrika Kusini na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata.Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia. Katika makalaShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.Na katika mashinani Noella Bagula, Mwanachama wa Alleluyah Safe Space ambaye ni mama mkimbizi wa ndani kutoka Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambako wanawake na wasichana wanapitia ukatili wa kijinsia katika migogoro. Bi Bagula anasema yeye sasa anajua jinsi ya kujilinda katika hali hatari kufuatia mafunzo yanayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya uzazi, (UNFPA) katika maeneo salama yaliyotengwa kwa ajili yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Afrika Mashariki Fest ya nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na Uganda inayotumia kampeni yake ya “Twende Zetu Butiama” ili kuyatumimiza malengo hayo.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO katika eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli limeongoza uhamishaji wa wagonjwa 35, wengi wao watoto kwenda Jordan, kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na huduma za afya kuvurugwa Gaza. WHO inasema zaidi ya watu 10,000 Gaza wanahitaji kuhamishiwa nchi nyingine kwa ajili ya matibabu.Harakati za kusaka amani ya kudumua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinazidi kushamiri ambapo hatua za hivi karibuni ni kutoka Muungano wa Afrika, (AU) zikiongozwa na marais wa zamani, Sahle Work Zewde wa Ethiopia, na Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, (CAR).kuelekea mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP30 huko Brazil baadaye mwaka huu, huko Nairobi, nchini Kenya bara la Afrika linajipanga kuhakikisha mkutano huo unakuwa na tija. Dkt. Richard Muyungi, Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu na mabalozi wanaoshughulikia masuala ya tabianchi barani Afrika, anasema wanachokitaka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIKWANYUKWANYU!.Mwenyeji wako ni Leah Moshi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya malengo ya maendeleo endelevu, na mradi wa uvuvi unaosaidia kupunguza migogoro Ituri DRC. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu, HLPF la mwaka huu wa 2025 limeanza leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wadau kutoka katika nyanja mbalimbali duniani wanakutana kujadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Kutoka msituni kupigana upande wa waasi hadi kuingia ziwani na kuwa mtaalamu wa ufugaji wa samaki, ndio simulizi tunayopata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, simulizi ya matumaini kwa mustakabali wa jamii iliyogubikwa na vita kila uchao.Katika makala tunakupeleka mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako kuelekea siku ya kimataifa ya vijana na stadi hapo kesho Julai 15, Sabrina Said anazungumza na mmoja wa vijana anayetumia majukwaa ya kidijitali kutoa elimu ya uelimishaji rika.Na kaika mashinani leo fursa ni yake Imam Ustaadhi Matano Bin Salim kutoka Kaunti ya Mombasa nchini Kenya, ambaye amewezesha shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kufika kwenye kituo cha mafunzo ya dini kupatia watoto chanjo. Akisema typhoid ni homa ya tumbo, na measles ni ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kutoka msituni kupigana upande wa waasi hadi kuingia ziwani na kuwa mtaalamu wa ufugaji wa samaki, ndio simulizi tunayopata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, simulizi ya matumaini kwa mustakabali wa jamii iliyogubikwa na vita kila uchao. Mwenyeji wako ni Sharon Jebichii.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya nchini Burundi, na elimu ya upatanishi kwa jamii Ituri nchini DRC. Makala tunakupeleka nchini Kenya kumulika kilimo kichopatia riziki jamii na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki za wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuoandoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu.Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana.Katika makala Sharon Jebichii anatupeleka Kaunti ya Tana River huko Kenya kumulika juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti katika kilimo, ambayo imeleta mabadiliko na matumaini kwa jamii za wakulima.Na kaika mashinani leo ikiwa siku ya idadi ya watu duniani, nampisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, Dkt. Natalia Kanem akizungumzia umuhimu wa takwimu katika kuboresha maisha ya wakazi wa dunia!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana. Sabrina Saidi na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kushuhudia mafunzo ya ukufunzi kwa wanadhimu wa Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkataba wa amani DRC na Rwanda, UKIMWI, na maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Kiswahili, na uchambuzi wa neno.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekaribisha mkataba wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda uliotiwa saini tarehe 27 mwezi uliopita wa Juni, huku wakishukuru Marekani, Qatar na Muungano wa Afrika kwa juhudi za usuluhishi.Ukata uliosababishwa na wahisani kukata au kupunguza ghafla na kwa kiasi kikubwa ufadhili kwenye miradi ya kupambana na UKIMWI umekuwa na madhara kwa nchi zilizoathiriwa vibaya na ugonjwa huo, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS.Leo kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juu ya Mangu wametuma ujumbe wao wa umuhimu wa lugha hiyo kupitia ngonjera.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "CHARAKAMU na BARAKALA!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akiwa barani Afrika; na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani. Makala tunakwenda nchini Burundi na mashinanitunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani barani Afrika ambapo juzi tarehe 7 aliingia nchini Gambia, kwa njia ya mtandao wa X ameonesha namna ziara yake ilivyokuwa ya mafanikio kwa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali nchini humo katika harakati za kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani, (WSIS) ukiingia siku ya 3 hii leo huko Geneva, Uswisi, washiriki wanapazia sauti umuhimu wa kila mtu kokote pale aliko afikiwe na teknolojia inayomwezesha kupokea taarifa kwa urahisi, usahihi na kwa haraka.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.Na katika mashinani fursa ni yake Dkt. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambaye katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa kila msichana anahitaji huduma muhimu za afya uzazi ili waweze kuendelea na elimu, akitaja mfano wa kazi zao nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!