Podcasts about kidemokrasia

  • 18PODCASTS
  • 471EPISODES
  • 8mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 20, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about kidemokrasia

Latest podcast episodes about kidemokrasia

Habari za UN
20 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 20, 2025 12:20


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika wafugaji wa nyuki nchini Tanzania leo ikiwa ni siku ya nyuki duniani iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 Desemba mwaka 2017 kupitia azimio namba A/72/211.Baada ya miaka mitatu ya majadiliano, leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya unaoendelea Geneva, Uswisi, nchi zimepitisha rasmi makubaliano ya kihistoria ya kuzuia, kujiandaa, na kukabiliana vyema na majanga ya magonjwa kwa siku zijazo. Taratibu zote zitakapopitishwa na angalau nchi 60, mkataba utaanza kutumika rasmi mwakani.Kutokana na mamlaka za Israeli kulegeza kwa muda mzingiro uliodumu kwa wiki 11, angalau sasa matumaini kidogo yamerejea Gaza, yameeleza leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya dharura, OCHA, Jens Laerke amesema tayari wamepata ruhusa ya kuyavusha malori matano yaliyokuwa yamezuiliwa jana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetahadharisha  leo kwamba bila ufadhili zaidi, huenda katika muda wa wiki chache zijazo likalazimika kusitisha msaada wa chakula kwa takribani nusu ya watu linaowahudumia kwa sasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Na katika mashinani, fursa ni yake Hanan Al-Dayya, Mkimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, akisimulia  madhara ya mashambulizi yanayoendelea kutoka Israeli.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
16 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 16, 2025 12:25


Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula, na takwimu za afya za janga la COVID-19 kusababisha vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane  ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.Katika makala Leah Mushi anatupeleka nchini Tanzania kusikia namna wanawake wenye ulemavu walivyoweza kujikwamua kutoka kwenye changamoto mbalimbali ikiwemo za kiuchumi na kuchangamkia fursa za uongozi.Na katika fursa ni yake Bernadette Kambonesa, mkimbizi wa ndani kutoka kijiji cha Bogoro, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumzia manufaa yatokanayo na uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Nyumba yetu ilivamiwa na tulilazimika kukimbia hadi hapa Burundi – Mkimbizi Charles

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 14, 2025 4:43


Mapigano yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, yamesababisha zaidi ya watu 70,000 kukimbia makazi yao na kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Burundi wakitafuta usalama.

Wimbi la Siasa
Rwanda na DRC zawasilisha mapendekezo kuhusu mkataba wa amani

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later May 7, 2025 10:23


Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mkataba wa amani kwa Marekani, kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kudumu mwezi Juni, jijini Washington. Harakati hizi, zitazaa matunda ?

Habari za UN
05 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 10:52


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani,  VoTAN      uliofanyika wiki iliyopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), fursa ni yake Rawhiyeh, mkimbizi kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israel ambaye anasimulia kwa uchungu madhila yanayowakumba yeye na familia yake baada ya kupoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
MONUSCO yapatia wanawake wakimbizi DRC mafunzo ya ushoni

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 2:31


Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO). Sharon Jebichii na taarifa kamili.

Habari za UN
Walinda amani wa UN kutoka Bangladeshi na Indonesia wapewa medali nchini DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 1:49


Huko Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Bangladesh na Indonesia, wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wamepatiwa medali kwa mchango wao wa ulinzi wa raia, moja ya jukumu kubwa la ujumbe huo. Assumpta Masso amefuatilia hafla hiyo na kuandaa ripoti hii.

Habari za UN
30 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 11:14


Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa mpox, na walinda amabini wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo. Makala inamuulika siku siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz namashinani tunasalia hapa makao maku kusikia ujumbe wa mwakilishi wa shirika la watu wa jamii za Asili.Maambukizi ya ugonjwa wa mpox kutokana na aina ya virusi vya monkeypox clade Ib /ˈmʌŋ.ki.pɑks kleɪd one bee/ (MPXV) yanaendelea kuripotiwa hasa barani Afrika, ambapo mataifa kumi na moja yameripoti maambukizi ya ndani ya jamii katika kipindi cha wiki sita zilizopita. Hiyo kwa mujibu wa ripoti 51 ya Shrika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu hali ya mlipuko wa mpox katika nchi mbalimbali duniani.Huko Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Bangladesh na Indonesia, wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wamepatiwa medali kwa mchango wao wa ulinzi wa raia, moja ya jukumu kubwa la ujumbe huo..Makala ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz Flora Nducha anamulika umuhimu wa jazz maadhimisho ya mwaka ambapo maudhui yanachagiza "Amani, umoja, ubunifu na uhuru miongoni mwa tamaduni."Na katika mashinani leo fursa ni yake mshiriki  jukwaa la watu wa asili hapa Makao makuu Helena Steenkamp Mwakilishi wa Shirika la Watu wa jamii za Asili Kusini mwa Jangwa la Kalahari Afrika Kusini anazungumzia alichokipata hadi sasa kwenye jukwaa hilo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
29 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 29, 2025 11:44


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari  na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati  kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili  katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
‘Nenda rudi' ya wakimbizi wa DR Congo nchini Burundi mazingira ya kuishi yakiendelea kuwa tete

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 25, 2025 2:02


Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu huku wengine wakifanya safari za nenda rudi wakivuka mto uliosheheni viboko na mamba. Taarifa zaidi na Selina Jerobon.

Habari za UN
25 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 25, 2025 10:57


Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani  na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
22 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 22, 2025 9:56


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Msasani nchini Tanzania kusikia namna vijana na serikali wanavyolinda Mama Dunia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari ujumbe wa Katibu Mkuu, watoto kulinda mazingira DRC, na kifo cha Papa Francis.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa' kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka. Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.Kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kukumbuka mchango wake wa kutetea walio taabuni. Mathalani shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekumbuka wito wake wa kutaka kila mtu kukaribisha, kusindikiza na kujumuisha wale wote wanaobisha hodi kwenye milango yao.Na mashinani  kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
16 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2025 9:57


Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya;  wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza  umuhimu wa mikutano hii.Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani  nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.

Habari za UN
Uhaba wa fedha watishia ukarimu wa Zambia kwa wakimbizi - UNHCR

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2025 2:05


Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi  Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo  ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema  “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi,  UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao  unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.

Habari za UN
11 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 9:57


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya watoto nchini DR Congo, na masuala y awanawake nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia harakati za vijana za kusongesha Ajenda2030, na mashinani tunasalia huko huko kumulika misaada kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limeripoti kwamba huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kila nusu saa takribani mtoto mmoja anaripotiwa kubakwa huku ghasia zikiendelea katikati ya janga linalozidi kukua la ufadhili finyu wa kifedha.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya kwa Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na Winifred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor aliyeshiriki majadiliano ya wiki iliyopita kuhusu malengo ya maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madri, anaeleza nini kama kijana anapaswa kufanya      kuchangia ajenda hiyo ya maendeleo.Na katika mashinani Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, akizungumza kutoka kituo cha shirika hilo kilichopo Mombasa, Kenya anaeleza juhudi wanazofanya kuwasaidia wakimbizi wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Mtoto aliyebakwa na kutiwa ujauzito DRC asema "siko tayari kuwa mama"

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 1:58


Mtoto mmoja alibakwa katika kila nusu saa huko Mashariki mwa Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati mapigano yaliposhika kasi mwanzoni mwa mwaka huu kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa M23, katikati ya ufadhili finyu wa kifedha, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Habari za UN
08 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 8, 2025 11:50


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Stadi za kuoka mikate zaleta furaha kwa mkimbizi Thérèse huko Beni nchini DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 2, 2025 1:52


Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha. Sharon jebichii na taarifa zaidi.

Habari za UN
02 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 2, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji, na wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Tanzania kwa mada hiyo hiyo ya elimu kuhusu usonji, na mashinani tunakwenda Gaza.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote.Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha.Makala leo kama tulivyokujulisha ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usonji, Assumpta Massoi anamulika jinsi shirika moja la kiraia nchini Tanzania linapigia chepuo harakati hizo.Na katika mashinani fursa ni yake Marah Hajjo, msichana mdogo kutoka Gaza huko Palestina Mashariki ya Kati ambaye anasimulia mabadiliko makubwa ya sikukuu ya Eid El Fitr ambayo mwaka huu ilighubikwa na kiza cha vifusi na mateso kutokana na mashambulizi kutoka Israeli.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!  

Habari za UN
Baada ya kukimbilia Burundi, wakimbizi wa DRC wakubwa na uhaba wa mahitaji muhimu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 26, 2025 2:06


Hali ya kibinadamu ya wakimbizi zaidi ya 100,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokimbilia nchini Burundi kusaka usalama kutokana na mapigano mashariki mwa nchi yao katika katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, iliyopita ni ya mashaka, wakati huu ambapo ufadhili unazidi kukumbwa na mkwamo, wakikabiliwa na uhaba wa huduma kama chakula, huku kukiwa na pengo la ufadhili. Je ni madhila yapi?  Sharon Jebichii anafafanua zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

Habari za UN
25 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 25, 2025 11:16


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki takriban milioni 1.9.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa ya Bahari ya Atlantiki, ikiwakumbuka mamilioni ya Waafrika walioteswa, kunyanyaswa, na kunyimwa utu wao. Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kwa zaidi ya karne nne, mamilioni ya Waafrika walitekwa kwa nguvu, kusafirishwa kwa meli hadi mataifa ya kigeni, na kufanyishwa kazi katika hali mbaya za kikatili.”Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Lea mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa amekimbilia Burundi na familia anasilimua hali ilivyokuwa wakati wa kukimbia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  

Habari za UN
20 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2025 12:27


Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani ni Finland na ya mwisho kabisa ni Afghanistani. Katika 10 bora zenye furaha hakuna hata moja ya Afrika, ilihali kwenye 10 za mwisho nchi za Afrika ni 7 ambazo ni Lesotho, Comoro, Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Malawi na Sierra Leone.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukikaribia ukingoni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tumemuuliza mshiriki Wakili Rosemary Mwaipopo kutoka Tanzania mkutano umekidhi kiu yake ya kusongesha usawa wa kijinsia?Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
10 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 10, 2025 10:56


Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 na wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC kwenda Burundi. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon, kulikoni?Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000.Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi.Makala leo tunamwangazia Fatuma Mfumia, dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhuduia Watoto, UNICEF Tanzania.Na mashinani mashinani fursa ni yake Ghada Dawiche's ambaye licha ya machungu yaliyomkumba baada ya kupoteza bintiye aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Lebanon, pamoja na mjukuu wake wa kiume wakati kombora la Israeli lilipopiga nyumba yao nchini  Lebanon, anasema Umoja, nguvu na tumaini ndio ujumbe mkuu anaowapa wanawake wote waliopoteza wapendwa wao vitani na katika kupigania haki za wanawake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
UNHCR: Zaidi ya wakimbizi 63,000 wa DRC wamewasili Burundi wengi wanaishi kwenye uwanja wa Rugombo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 10, 2025 2:07


Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.

Habari za UN
Vilabu vya Dimitra vyaimarisha usawa wa kijinsia na uchumi DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 5, 2025 4:50


Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limesaidia kujenga utangamano wa kijamii kwa kuboresha maisha kwenye eneo la Walungu jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Limefanya hivyo kupitia vilabu vya Dimitra ambavyo hupatia wanawake, wanaume na vijana fursa ya uongozi wa kuleta mabadiliko chanya kwa kutatua changamoto zilizo kwenye jamii yao bila hata kuwa tegemezi kwa msaada wa nje. Mradi huu ulitekelezwa kati ya mwaka 2008 na 2023 na sasa tunamulika ni kwa vipi umeleta mafanikio. Sharon Jebichii anaelezea kwenye makala hii kupitia video iliyoandaliwa na FAO. 

Habari za UN
05 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 5, 2025 9:58


Hii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra  nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiMakala inakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) ulioanzishwa kati ya mwaka 2008 hadi 2023 umeleta mabadiliko chanya ukiimarisha usawa wa kijinsia. Mwenyeji wako ni Sharon Jebichii.Ibrahim Al-Ghandour, mpalestina huyu akiwa eneo la Gaza mbele ya nyumba yake iliyogeuzwa kifusi kutokana na mashambulizi ya Israeli akielezea maoni yake ya mfungo unaoendelea wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Habari za UN
Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 5, 2025 1:57


Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja na watetezi walioko mashinani," amesema Lawlor na kuongeza kuwa watu hao wanaishi kwa hofu na hatari ni halisi na kwama hivi karibuni, mtetezi mmoja alimpa taarifa kuwa waasi wa M23 wameandaa orodha ya watetezi wa haki za binadamu watakaokamatwa katika maeneo waliyoyadhibiti.Mtaalamu huyo  amesema amepokea ripoti za kuaminika za watetezi wa haki za binadamu kushikiliwa bila mawasiliano, kutoweshwa kwa nguvu, na kuteswa huko Rutshuru na Masisi, Kivu Kaskazini, huku takribani watetezi sita wa haki za binadamu wakiripotiwa kutoweka baada ya kujaribu kutoroka Goma baada ya jiji hilo kuchukuliwa na M23."Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu hawakuwa na chaguo jingine ila kukimbia makazi yao. Wale wanaofanikisha kufika katika miji mingine wanakosa rasilimali za kupata malazi au kukidhi mahitaji yao ya kila siku," amesema na kwamba, "wengine wamebaki katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi lakini wana hofu kubwa kuhusu usalama wao. Mtetezi mmoja alimuuliza jinsi wanavyoweza kuendelea kujificha huku M23 ikianza kufanya ukaguzi huko Goma.Tangu magereza yalipovunjwa  huko Goma, Kalehe, Bukavu, na Uvira, maelfu ya wafungwa, wakiwemo wahalifu wakatili na viongozi wa makundi yenye silaha waliohukumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofikia uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, walitoroka na kuingia mitaani. Baadhi yao wanawatishia watetezi wa haki za binadamu waliotoa msaada wa matibabu, kisaikolojia na msaada wa kisheria kwa waathiriwa na mashahidi waliotoa ushahidi wakati wa kesi hizo. Na wakati huo huo watetezi wa haki za binadamu wakikabiliwa na vitisho na hofu ya kulipiziwa kisasi, waathiriwa hawana wa kuwategemea, ameeleza mtaalamu huyo.Katika mazingira ambayo tayari ni magumu kwa watetezi wa haki za binadamu, Mtaalamu huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza hatari kubwa ya ukatili wa kingono inayowakabili watetezi wa haki wa kike."Tunajua kuwa ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro mashariki mwa DRC ni wa kiwango cha juu, na kwamba wanawake wanaopinga ukiukwaji wa haki za binadamu katika muktadha huu, na wanaojitokeza kwa kazi yao, mara nyingi ndio wanaoathirika zaidi," Lawlor amesema akiongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kufikiria kwamba miaka 25 tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na usalama, matukio haya yanatokea mbele ya ulimwengu unaoonekana kutokuwa na msimamo thabiti.Mtaalamu huyo pia ameelekeza umakini kwa hatari wanazokabiliana nazo watetezi wa haki za binadamu katika maeneo ya vijijini na yaliyojitenga, ikiwa ni pamoja na mauaji, kutoweshwa kwa nguvu, na utekaji nyara, na akaangazia athari za kisaikolojia zinazowakumba wale walioko mashinani."Watetezi tayari walikuwa wakikabiliwa na vitisho katika eneo hilo – kutoka kwa serikali na makundi yenye silaha  lakini kama alivyonieleza mtetezi mmoja wa haki za binadamu wa…

Habari za UN
03 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2025 11:49


Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu  Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu

Habari za UN
Burundi yahamishia wakimbizi wa DRC eneo salama zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2025 3:48


Machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) yanaendelea kufurusha watu na wengine wanaamua kukimbilia nchi jirani ikiwemo Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Burundi limesema wazi kuwa katika wiki mbili za mwezi Februari kuanzia tarehe 14 walipokea wakimbizi zaidi ya 60,000, wengi wakiwa tayari walishafurushwa awali. Kwa waliowasili katika eneo la Kaburantwa  nchini Burundi, bado wanahofia usalama. Serikali ya Burundi imetenga eneo lingine salama zaidi na sasa wanahamishiwa huko. Je ni wapi? Assumpta Massoi kwa msaada wa video ya UNHCR Burundi anasimulia zaidi. 

Habari za UN
Viongozi wababe, wa kiimla na wenye fedha wanasigina haki za binadamu duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 3, 2025 2:57


Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk  amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk  ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk  amesisitiza haja ya kudumisha usitishaji mapiganona kutoa wito wa mchakato wa amani unaozingatia haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya kujitawala na uwajibikaji. Ametaka kuachiliwa kwa mateka, kukomeshwa kwa vizuizi vya kiholela, na kuanza tena kwa msaada wa kibinadamu mara moja ndani ya Gaza.Kuhujsu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine amersema bado ni suala la kutia wasiwasi, huku raia wakiishi kwa hofu ya mara kwa mara kutokana na mashambulizi yasiyokoma.Türk  amekemea vikali vikwazo vya Shirikisho la Urusi juu ya haki za msingi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kuelezea masikitiko yake kuhusu ripoti za mauaji ya kiholela na mateso ya kimfumo ya wafungwa wa vita wa Kiukraine.Almeihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kuelekea amani endelevu inayoheshimu haki na matarajio ya watu wa Ukraine.Türk  pia ameelekeza mawazo kwenye maeneo mengine yenye migogoro, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Myanmar, Haiti, na Sudan.Alielezea jinsi watawala wa kiimla, wanasiasa wahubiri wa chuki, na walanguzi wanavyotumia machafuko kwa faida zao binafsi.Amesema Athari za migogoro huenea zaidi ya mstari wa mbele, zikiathiri minyororo ya usambazaji duniani na nafasi za kidijitali.Ametoa  wito kwa watu binafsi kutambua jukumu lao la pamoja kwa kufanya maamuzi ya kimaadili ya ununuzi, kushiriki kisiasa, na kuunga mkono uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.Hata hivyo amesema demokrasia zilizoimarika haziko salama dhidi ya kudorora kwa haki za binadamu. Türk  ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mwelekeo nchini Marekani, ambako maendeleo kuhusu usawa wa kijinsia na sera za kupinga ubaguzi yanarudi nyuma.Pia amekosoa Shirikisho la Urusi kwa ukandamizaji wake wa jamii za kiraia na vyombo vya habari huru, ambapo wapinzani wanakabiliwa na unyanyasaji, kukamatwa, au kufurushwa.Kudhoofika kwa haki za binadamu katika mataifa yenye nguvu, Türk  alionya kwamba kunaweka mfano hatari kwa ulimwengu mzima, akisisitiza hitaji la dharura la mshikamano wa kimataifa na uwajibikaji kuhusu haki za binadamu.

Habari za UN
28 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 11:19


Hii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye amenufaika na Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali kwa hisani ya ILO, serikali ya Kenya na wadau.Na mashinani fursa ni yake Ashura Hamis Sayid kutoka Tanzania ambaye ni Mratibu wa Mpango wa U-report unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ili kuwapa vijana uhuru wa kujieleza      na kutoa maoni yao juu ya maswala mbalimbali .Ameweza kutufafanulia zaidi madhumuni ya mpango huu na jinsi gani inatumika katika jamii.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 3:25


Kama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibindoni ujuzi wake mwingine. Ujuzi binafsi, ufundi wa kushona nguo.Celestin sasa anafundisha wanawake wadogo shughuli za kushona nguo.Hatimaye mwaka jana, 2024, kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali (RPL), uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO utaalamu wake wa kushona nguo ambao haukuwa na cheti, ukathibitishwa rasmi na akapata cheti, hali ambayo imemfungulia milango ya kuomba ajira rasmi.

Habari za UN
27 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 27, 2025 11:04


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji chakula mwezi Julai mwaka huu huko Addis Ababa, Ethiopia, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amezungumza hivi karibuni akiwa Nairobi, Kenya kwenye kikao cha maandalizi ambako alitembelea jiko la Giga, mpango wa Chakula kwa ajili ya Elimu, unaoendeshwa na Wawira Njiru, mshindi wa tuzo ya Mtu Maarufu Kenya mwaka 2021.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
25 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 25, 2025 11:10


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC ambako ghasia za hivi karibuni huko Goma zimeongeza mahitaji ya huduma za afya, WHO imechangia vifaa muhimu vya matibabu ili kukabialiana na hali hiyo. Pata pia muhtasari wa habari na mashinani.Kufuatia ripoti za kuweko kwa ugonjwa usiojulikana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao tayari umeambukiza mamia ya watu na kusababisha makumi ya vifo, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ugonjwa huo uliotangazwa kwa chapisho la kikanda la WHO.Kampeni ya chanjo ya polio inayoendelea ukanda wa Gaza kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya polio na kuzuia tishio la ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine na nchi jirani, imekuwa na mafanikio makubwa kwani hata eneo la Gaza Kaskazini, mwitikio ulikuwa mkubwa licha ya mvua na baridi kali.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo limetangaza kuwa sitisho la mapigano Gaza limewezesha kufikisha eneo hilo kwa wastani maradufu ya shehena za vyakula kilichokuwa kinapelekwa kabla ya sitisho la mapigano.Katika mashinani, hivi majuzi Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, UNICEF katika ripoti yake lilibaini kwamba mtoto 1 kati ya watano nchini Ukraine ameripoti kupoteza ndugu au rafiki wa karibu tangu kuzidi kuongezeka kwa vita miaka mitatu sasa. Akitafakari juu ya zama zijazo, Toby Fricker, Afisa Mkuu wa mawasiliano wa Shirika hilo nchini Ukraine anasema UNICEF inaendelea kushikamana nao.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Ukraine: Miaka 3 ya kumbukumbu mbaya, juhudi zifanyike mzozo uishe - Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 24, 2025 2:29


Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu. Selina Jerobon na taarifa kamili..

Habari za UN
24 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 24, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya lugha mama, tunakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
21 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 21, 2025 11:04


Hii leo jaridani tunaangazia mahitaji ya wakimbizi wanaokimbia machafuko DRC wakielekea nchini Burundi, na hali ya wakimbizi wa ndani Gaza wakati huu wa msimu wa baridi. Makala tunakurejesha nchini DRC na mashinani tunakwenda nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, familia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Evarist Mapesa anakupeleka eneo la mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na Burundi kufuatilia mmiminiko wa wakimbizi kutoka DR Congo.Na mashinani fursa ni yake Regnihadah Mpete kutoka Tanzania ambaye anatumia kiswahili, lugha ya taifa nchini Tanzania kufundisha vikundi vya wanawake wilayani Biharamulo, mkoani Kagera jinsi ya kujikinga na magonjwa. Mafunzo serikali  kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) kupitia TIP ambao ni Mtandao wa Madhehebu ya Dini mbalimbaliMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 21, 2025 5:03


Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Habari za UN
20 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 20, 2025 10:37


Hii leo jaridani mada kwa kina ikimulika harakati za uhamasishaji kabla na baada ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni na mchango wa redio katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kuchagiza maendeleo ya jamii huko Ramogi nchini DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa maneno.Idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioingia Burundi kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, mashariki mwa DRC sasa imeongezeka na kufikia 20,000.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, limechapicha picha zikionesha wakimbizi walio njiani wakipikiwa chakula, wakati huu ambapo M23 wametwaa miji ya Goma jimboni  Kivu Kaskazini, na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini.Na katika hatua nyingine ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikipatiwa jina UNJHRO imeripoti jinsi kutoroka kwa wafungwa kwenye gereza la Goma jimboni Kivu Kaskazini kulivyoleta hofu na mashaka kwenye jamii.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Mkimbizi kutoka DRC aliyekimbilia Uganda akumbuka ukatili uliofanywa na waasi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 19, 2025 2:08


Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo. Kufahamu msingi wa kauli hiyo ya Twagirayesu, ungana na Sharon Jebiichi.

Habari za UN
19 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 19, 2025 9:55


Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang'are, Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) akitoa wito kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono ulinzi wa amani duniani kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo walinda amani. Anold Kayanda anasimulia.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya redio duniani fursa ni yake Irene munyua kutoka Kenya akieleza washirika wetu Radio Domus kuhusu umuhimu wa radio kwa jamii katika maisha ya kila siku.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
OCHA yasihi kufunguliwa kwa viwanja vya ndege Goma na Kavumu - DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 19, 2025 1:55


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Habari za UN
18 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 10:34


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka DRC katika mji wa Goma uliokuwa mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ambao sasa uko mikoni mwa waasi wa kundi la M23. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imesema hali huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inazorota kwa kasi kubwa, na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ukatili kama vile watu kuuawa kiholela, wakiwemo watoto, wakati huu ambapo waasi wa M23 yaripotiwa wametwaa mji wa Bukavu, jimboni Kivu Kusini.Wakati hayo ya kiendelea ndani ya DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeripoti kuwa katika siku chache zilizopita, wakongo kati ya 10,000 na 15,000 wamevuka mpaka wa DRC na kuingia Burundi wakikimbia mapigano.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 5 kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini. kwa ajili ya kujengea mnepo na kuimarisha upatikanaji wa chakula kwa familia za maeneo kame nchini Kenya.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, fursa ni yake Faraja Kashindi Malumalu kutoka Tanzania ambaye ni mkimbizi katika kambi la Nyarugusi na mfanyakazi wa kituo hicho cha matibabu  ambaye anaonesha furaha kutokana na ujenzi wa kituo kipya cha wagonjwa wa ukimwi ambao umesaidia kuhifadhi faragha(privacy) ya wagonjwa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Mashambulizi yakishamiri DRC, sinfohamu yakumba wakimbizi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 2:37


Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya harakati inahoyitajika. Anold Kayanda na ripoti kamili.

Habari za UN
Doria za pamoja za MONUSCO na FARDC huko Ituri DRC zaimarisha usalama

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 1:58


Katika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Habari za UN
14 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 11:25


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko na hali ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani inatupeleka nchini  Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR), kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya haraka inahoyitajika..Katika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia.Makala leo inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 63 wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC kuhusu maendeleo ya jamii. Flora Nducha amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka Kenya.Na mashinani fursa ni yake Albertine Yantijba ,manusurawa ukatili wa kijinsia kutoka Sango CAR , ambaye anatueleza jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) limeletamabadiliko baada ya kuanzishwa kwa maeneo salama ya wasichana kujieleza na kuhudumiwa”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
13 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 13, 2025 11:05


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika siku ya redio duniani, maudhui yakiwa Radio na Tabianchi, na ni kwa vipi chombo kinachodaiwa kutwamishwa na maendeleo ya teknolojia kinaendelea kusaidia kuelimisha umma kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Teonas Aswile wa TBC Taifa nchini Tanzania anaeleza.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo hali inazidi kuwa tete na leo Mkurugenzi Mtendaji wa shirkika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa mwa  nchi hiyo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo watoto na familia wanakabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.Naibu mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masiala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Edmore Tondhlana akizungumza na UN News amesema hali nchini Sudan inaendelea kuwa janga la kibinadamu wakati vita ikishika kasi na watu wakiendelea kufurushwa makwao. Amesema "Tunashuhudia hali ambapo Sudan ina mahitaji ya kibinadamu yaliyo miongoni mwa makubwa zaidi duniani. Takriban watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hili ni ongezeko la takriban watu milioni tano zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita, pia, Sudan ina idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza makazi yao.Na leo ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikibeba maudhui Redio na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO lengo la maudhui haya ni kudhihirisha jukumu la redio katika kusambaza ujumbe na kuelimisha kuhusu changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kutanabaisha kuhusu hatua endelevu na kuwapa sauti wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno “MSUMBI”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
12 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana      mwenye  umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa  Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa  msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma  sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
Wakimbizi Goma waanza kufungasha virago huku wakiwa na hofu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 1:45


Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea. Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.

Habari za UN
Akibomoa kibanda chake Goma DRC, mkimbizi asema ana hofu kurejea Saké

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 1:45


Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo.Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.Akiwa katika harakati za kubomoa kibanda chake katika kambi ya nane ya CEPAC Mugunga huko Goma, Bwana Bakulu anasema walishangaa, bila kuwa tayari, kuambiwa warudi walikotoka."Tumepatiwa saa 72 tuwe tumeondoka na kurejea Saké, kwani vita vimeisha. Sisi hatua uhakika kamili kwa sababu tuliondoka Saké kutokana na vita. Kama inabidi kusukumwa tuondoke, hatuna la kuchagua,” amesema Bwana Bakulu.Ana hofu ya kurejea Saké, akisema, “kule tulikuwa tunaishi Sake na tukirejea tutaishi vipi? Tunaomba viongozi wajitahidi watusaidie ili watuhakikishia usalama.Alipoeleza hali halisi amesema, “ hii siku ya leo hapa unaniona, watu wamepita hapa wakifanya vurugu, wananyang'anya kila kitu ulichonacho, iwe simu wanabeba. Sasa tunashindwa kufahamu amani iko katika kiwango gani?”Kwa mujibu wa Bwana Bakulu, walishaamua kuwa hawataweza kurudi na kama ni kufa basi watafia Goma, lakini sasa wamelazimishwa kurejea Saké.