POPULARITY
Mwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili kwa maelezo au habari zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Uganda, elimu kwa watoto nchini Sudan leo ikitimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini humo, na juhudi za wanawake za kuhifadhi misitu huko Narok nchini Kenya.Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa na ukandamizaji, vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, na waandishi wa habari.Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani yanchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP), nchini Kenya, kupitia mradi wa kuhimili tabianchi au Climate Promise Guarantee, limewawezesha wanawake wa jamii ya asili katika Kaunti ya Narok, nchini humo kuongoza juhudi za uhifadhi wa misitu huku wakilinda urithi wao wa kitamaduni na kuboresha maisha ya familia zao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa na ukandamizaji, vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, na waandishi wa habari. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa haki za binadamu na uchaguzi mkuu nchini Uganda, juhudi za Rwanda za kutokomeza Saratani ya shingo ya kizazi, na mafunzo kwa ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au kinengunengu yaliyoendeshwa Kigoma Tanzania.Wakati nchi ya Uganda ikijiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu wa Januari, wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa ikionya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Uganda si rafiki kwa uchaguzi wa amani.Saratani ya shingo ya kizazi ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi zaidi nchini Rwanda kwani takribani kila mwaka kati ya wagonjwa wapya 1230, 830 hufariki dunia. Ili kupunguza mzigo wa ugonjwa huu na kuokoa maisha, mwaka 2020 Rwanda ilianzisha mkakati wa kitaifa unaoendana na lengo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) la kuondoa saratani ya shingo ya kizazi ifikapo 2030.Mafunzo kwa vitendo ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au Kinengunengu yaliyoendeshwa mkoani Kigoma kaskazini-magharibi mwa Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, nchini huko yameendelea kusambaa na sasa yamebisha hodi kwenye viunga vya mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam kwa lengo la kusaidia wafugaji kujiongezea kipato badala ya kupoteza vifaranga kwa vifo au kuliwa na kunguru.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Wakati nchi ya Uganda ikijiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu wa Januari, wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa ikionya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Uganda si rafiki kwa uchaguzi wa amani. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement-ODM kina kiongozi mpya, Seneta Oburu Oginga, kaka yake kiongozi wa zamani wa chama hicho Hayati Raila Odinga aliyefariki dunia mwezi Oktoba. Je, atafanyaje, kukiunganisha chama hicho ambacho kinaonekana kugawanyika kuhusu ushirikiano wake na uongozi wa rais William Ruto ? Tunachambua.
Katika makala yetu leo tunaangazia pakubwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania ambapo Rais Samia Suluhu aliapishwa siku ya Jumatatu kuongoza muhula wa pili, hata hivyo ni uchaguzi ambao ulikumbwa na utata huku waangalizi kutoka jumuiya ya Afrika kusini SADC na wale wa umoja wa Afrika AU wakisema haukuzingatia vigezo vya demokrasia. Tunaangazia pia taarifa ya Rais Paul Biya, wa Cameroon kuapishwa Alhamisi iliyopita kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa nane, huku upinzani ukiitisha maandamano kupinga matokeo yaliyompa Biya ushindi. Lakini pia tutaangazia kongamano la kimataifa la mazingira, COP30 ambalo linafanyika huko Belem, nchini Brazil, kati ya Novemba 10 na 21.
Machafuko yalikumba uchaguzi mkuu wa Tanzania, uliofanyika Oktoba 29, 2025 na rais Samia Suluhu Hassan kutangazwa mshindi kwa kupata asilimia 97.6 ya kura. Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimesema ushindi wa Samia ni kichekesho cha demokrasia. Anapaswa kufanya nini ili kuirejesha Tanzania katika utulivu wa kisiasa ? Tunachambua.
Uchaguzi mkuu uliofanyika katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, na ambao uligubikwa na maandamano; mkutano wa Paris nchini Ufaransa kuhusu amani ya mashariki mwa DRC na eneo la maziwa makuu, siasa za nchini Kenya, Uganda lakini pia mauaji yaliyotekelezwa na kundi la RSF nchini Sudan, hali nchini Cameroon na Madagascar, kurejewa kwa mashambulizi nchini Ukraine, na huko Israeli dhidi ya Hamas
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
Tanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu kuanzia Agosti 28, kuelekea kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025. Rais Samia Suluhu Hassan, kutoka chama tawala CCM, anawania uongozi wa nchi hiyo. Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.
Karibu katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Joseph Kasongwa Mwaiswelo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ambapo leo tunaangazia juu ya Thamani ya kura wakati wa uchaguzi Mkuu. Studio Kuu Mikocheni mtangazaji wako ni mimi Esther Magai Hangu nikishirikiana na Geofrey Rweyunga kutpka studio ndogo Jijini […] L'articolo Je, unafahamu thamani ya ya kura yako katika kipindi cha uchaguzi Mkuu? proviene da Radio Maria.
Mwezi Oktoba 2025, wananchi wa Tanzania, watashiriki kwenye uchaguzi Mkuu, kuwachagua madiwani, wabunge na rais. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kinashinikiza mageuzi kwenye sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.Je, kitafanikiwa katika harakati zake ?
Kiongozi wa upinzani wa shirikisho Peter Dutton, ame tupa nje mpango wake waku walazimisha wafanyakazi wa umma kurejea ofisini aki kiri sera hiyo ilikuwa kosa.
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Nchini Ghana, rais wa zamani John Dramani Mahama alipata ushindi mkubwa na kumaliza uongozi wa miaka minane wa chama tawala New Patriotic Party (NPP) chake rais Nana Akufo-Addo, anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kufuatia Donald J Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi. Taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi jijini New York, Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imemnukuu Guterres akisema napongeza wananchi wa Marekani kwa ushiriki wao katika mchakato wa demokorasia.Kisha akasema nampongeza Rais Mteule Donald J. Trump na ninarejelea imani yangu kwamba ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa kimataifa.Guterres amesema Umoja wa Mataiifa uko tayari kufanya kazi kwa kina na serikali ijayo ya Marekani il ikutatua changamoto kubwa zinazokabili dunia hivi sasa.Trump ambaye anawakilisha chama cha Repablikani, anakuwa Rais wa 47 wa Marekani.Amemshinda Makamu wa Rais Kamala Harris ambaye alikuwa anagombea kiti cha urais kupitia chama cha Demokrati.Hii ni mara ya pili Trump ataongoza Marekani kwani alikuwa Rais wa 45 wa Marekani kuanzia Januari 20, 2017 hadi Januari 20, 2021 baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2016.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Wapiga kura katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu, baada ya zoezi hilo kuongezewa muda, wa siku moja, ambao haukutarajiwa, na ambao uliwafanya baadhi ya wagombea wa upinzani kulalamika, wakidai kwamba hiyo ilikuwa ni njama ya kuiba kura.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Sudan Kusini na mradi wa maji nchini Rwanda. Makala tunasalia huko huko Sudan Kusini na Mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni? Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika.Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF Vanessa Nakate amefanya ziara nchini Rwanda kujionea namna mradi wa pampu ya kuvutia maji inayotumia nishati ya umeme wa jua au Sola ilivyoleta manufaa kwa wanawake na wasichana barubaru 11,000 waliokuwa wakitembea umbali mrefu kusaka hmaji.Katika makala Assumpta Massoi anafuatilia ziara ya wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.Na tunakupeleka nchini Zimbabwe ambako vijana wameweza sio tu kijikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini bali pia kuhifadhi mazingira na tutasikia kutoka kwa mmoja wao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika."Ikiwa imesalia miezi 17 tu kwenye ratiba ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, narudia kile nilichokisema katika mkutano wa awali na waandishi wa habari, kwamba mwaka 2023 ni mwaka wa 'kutengeneza au kuvunja'," amesema Bwana Haysom mapema leo Agosti pili alipozungumza na vyombo vya Habari mjini Juba ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo changa zaidi duniani. Ghasia miongoni mwa jamii za Sudan Kusini zinaendelea kuongezeka pamoja na shinikizo la kuongezeka kwa ufinyu wa rasilimali huku maelfu ya watu wakiendelea kuingia nchini humo wakikimbia mapigano katika nchi jirani ya Sudan. Kwa mujibu wa Bwana Haysom, miongoni mwa hatua muhimu ambazo inabidi zichukuliwe ni pamoja na hitaji la kuunda upya vyombo vitatu muhimu, ambavyo ni, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, na Baraza la Vyama vya Kisiasa; kukamilisha mipango ya mpito ya usalama; kuendeleza mchakato wa kudumu wa kutengeneza katiba; na kuunda nafasi za kiraia na kisiasa ambapo kila raia ana uhuru wa kujadili na kujihusisha na uchaguzi wa kisiasa na kikatiba bila woga. "Kufanya uchaguzi tu hakutoshi - uaminifu, uwazi na ushirikishwaji wa mchakato ndio unaoleta uhalali. Hii ni pamoja na kwamba vyama vya siasa lazima viweze kujiandikisha na kufanya kampeni kwa uhuru; asasi ya kiraia kwa ajili ya elimu ya uraia na kuwa waangalizi wa mchakato. Inajumuisha vyombo vya habari vinavyoweza kuripoti kuhusu mchakato huo na kutoa nafasi kwa sauti na maoni mbalimbali kwa wapiga kura kufanya uamuzi sahihi,” amesema Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. Aidha Bwana Haysom amesisitiza kuwa UNMISS itaendelea kuiunga mkono Sudan Kusini katika michakato ya uchaguzi na uundaji wa katiba kwa kushirikiana na wadau wa kikanda kama vile Muungano wa Afrika (AU) na mamlaka ya pamoja ya kitaifa kwa ajili ya maendeleo kwenye eneo la Pembe ya Afrika (IGAD).
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa, bwana Nicolas de Rivière, Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa makundi yenye silaha, vyovyote vile yalivyo, lazima yasitishe operesheni zao ili kushiriki katika mchakato wa amani, “Ni wakati muhimu wakuchukua hatua na kwamba vikundi vyote vyenye silaha, kwa hali yao lazima visitishe shughuli zao na washiriki katika mchakato wa kisiasa. Naomba makundi ya kigeni yajiondoe na makundi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni pia yajiondoe ili hatimaye amani irejee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo”.Ujumbe huo umekuja nchini DRC wakati kukitarajiwa kuwa na uchaguzi mkuu wa raisi pamoja na wabunge mwezi decembe mwaka huu huku bwana Michel Xavier Biang Balozi wa Gabon kwenye Umoja wa Mataifa akisisitiza lazima uchaguzi huo uwe wa haki, wa uwazi na salama, “ Tuko katika mwaka ambao utakuwa mwaka wa uchaguzi, ujumbe wetu ni wakuhimiza wanasiasa wa pande zote kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, na wa kuaminika kwa mujibu wa Katiba ya DRC na sheria ya uchaguzi. Tuko hapa kuunga mkono hatua ya MONUSCO na kukumbusha kwamba MONUSCO ni sehemu ya fursa ya suluhu”.Wajumbe hao watakutana na watu kutoka tabaka mbali mbali ikiwemo mashirika ya kiraia na Rais wa DRC Félix Tshisekedi jijini Kinshasa na baadae watakwenda mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini, ambako mapigano yamezidi kurindima kwa miezi kadhaa sasa kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamkambo wa M23.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na kashfa ya utakatishaji wa fedha amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ANC. Je safari yake ya kisiasa itakumbana na vizingiti? Kennes Bwire amaefanya mazungumzo na mchambuzi wa siasa za Afrika kusini Peter Bigenda, akiwa Johannesburg.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ameipongeza serikali ya Kenya kwa kile alichoeleza ni hatua muhimu ya kuelekea uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Kenya, kufuatia uamuzi wake wa wa kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimataifa kuwafungulia mashitaka maafisa wakuu wa polisi kwa mauaji, ubakaji na utesaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2017. Leah Mushi anataarifa zaidi.Taarifa iliyotolewa hii leo huko Geneva, Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imemnukuu Kamishna Mkuu wa Umoja wa Matifa wa Haki za binadamu Volter Turk akipongeza Kenya na kusema hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kutumia Sheria ya Kimataifa ya Uhalifu kushtaki uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mahakama zake za ndani.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2017, Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu ilirekodi vifo 94 na matukio 201 yakihusiana na unyanyasaji wa kingono na zaidi ya majeruhi 300 wengi wao wakieleza kufanyiwa vitendo hivyo na vikosi vya usalama.Bwana Turk amesema “Uamuzi uliochukuliwa leo na Kenya ni wa msingi, ni hatua nzuri kuelekea haki na uwajibikaji kwa waathirika na familia za waathirika, wa ghasia za uchaguzi, na inaweza kuimarisha na kuzuia ukiukaji wa haki za binadamu kwa siku zijazo.”Amebainisha kuwa uamuzi huo wa Kenya unatokana na maendeleo ya hivi karibuni ya taasisi za Kenya zinazoungwa mkono na Ofisi yake ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu katika kuimarisha uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu.Kamishna Mkuu Türk amesema ofisi yake itaendelea kujitolea kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Kenya kuendeleza uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kushughulikia mauaji ya kiholela na kulazimisha watu kutoweka.
Mrengo wakisiasa wa Azimio One Kenya unajiandaa kuwasilisha ombi lakubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo.
Kinara wa mrengo wa Azimio One Kenya Raila Odinga, amewania urais mara tano bila mafanikio.
Ni nadra kwa tume ya uchaguzi ya Kenya, kusifiwa kwa jinsi ilivyo simamia uchaguzi mkuu.
Tume huru ya uchaguzi wa Kenya IEBC, kwa mara nyingine inasimamia uchaguzi mkuu miaka mitano baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 ulio paka tume hilo tope lakuganda.
Tasmania inatoa mvutio mwingi kwa siku ya uchaguzi mkuu, Jumamosi 21 Mei kwa watazamaji wa uchaguzi.
Wiki ya tatu ya kampeni ya uchaguzi mkuu ili tawaliwa na shinikizo za gharama za maisha, baada ya mfumuko wa bei kuongezeka kwa 5.1%.
Wiki ya pili ya kampeni za uchaguzi mkuu zime tumbukia katika vita vya kampeni zakutisha kati ya vyama viwili vikubwa nchini.
Mseto wa United Democratic Alliance (UDA) ume mtangaza rasmi Naibu Rais wa Kenya, William Samoei Ruto kuwa kinara wake katika uchaguzi mkuu wa 9 Agosti 2022. - Mseto wa United Democratic Alliance (UDA) ume mtangaza rasmi Naibu Rais wa Kenya, William Samoei Ruto kuwa kinara wake katika uchaguzi mkuu wa 9 Agosti 2022.
Joto la siasa nchini Kenya laendelea kuongezeka baada ya mseto wa Azimio kumuidhinisha Raila Odinga kuwa kinara wao katika uchaguzi mkuu 9 Agosti 2022.