POPULARITY
Siasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana na siasa. Tunachambua kauli za viongozi hao wa kisiasa.
Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadauwa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo' iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.
Karibu usikilize Kipindi cha Elimu Jamii kuhusu “Kampeni ya Fursa Sana” inayoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili uizfahamu fursa zinazopatikana kwenye mitandao ya kijamii. Wawezeshaji wa Kipindi hiki ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka TCRA Bi. Herieth Shija pamoja na Mhandisi Mohamed Bokko pia kutoka TCRA. Mtangazaji ni Agatha Kisimba. L'articolo UNAJUA KUWA MITANDAO YA KIJAMII NI FURSA YA AJIRA..? proviene da Radio Maria.
Siku za hedhi huchukuliwa kuwa swala la wanawake na halifai kuzungumzwa hadharani kwa jamii nyingi .Hali hii imesababisha wanawake na wasichana kupitia unyanyapaa ijapokuwa hili ni swala la haki ya uzazi
Takribani watoto milioni 1.3 nchini Malawi wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni maalum ya siku nne, kufuatia kugunduliwa kwa mgonjwa mpya wa polio mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Huyu ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa tangu mwaka 2022, wakati virusi vya polio pori vilivyokuwa na uhusiano wa kijenetiki na mlipuko ulioripotiwa nchini Pakistan vilipobainika. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Nchini Uganda, kuelekea uchaguzi mkuu, kumeripotiwa matukio ya wanahabari kushambuliwa na vyombo vya usalama wakati wakiripoti kampeni za uchaguzi na hasa za upinzani. Matukio kama haya yameshuhudiwa pia katika nchi nyingine za Afrika.
Nchini Uganda, kuelekea uchaguzi mkuu, kumeripotiwa matukio ya wanahabari kushambuliwa na vyombo vya usalama wakati wakiripoti kampeni za uchaguzi na hasa za upinzani. Matukio kama haya yameshuhudiwa pia katika nchi nyingine za Afrika.
Kampeni za uchaguzi nchini Uganda zimezidi kupamba moto kuelekea uchaguzi mkuu January 15 2025 ambapo Rais Yoweri Museveni aliyeingia madarakani mwaka wa 1986, anagombea tena muhula wa saba huku akishindana na wagombea wengine miongoni mwao mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine. Kampeni za mwaka huu zinafanyika huku mgombea wa Upinzani Bobi wine akilalamika kushambuliwa na maafisa wa usalama. Kupata mengi zaidi ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
Mada ya leo ni kuhusu kinara wa upinzani nchini Uganda Bob Wine pamoja na baadhi ya wagombea wengine wa upinzani wameendelea kunyanyaswa na vyombo vya usalama wanapoendelea na kampeni zao, tume ya uchaguzi ikilaani vitendo hivyo.Yanayofanyika Uganda yanashuhudiwa pia kwenye mataifa kadhaa ya Afrika .Tumemuuliza msikilizaji Hatua hii ya vyombo vya usalama inaathiri vipi demokrasia na nini kifanyike kujenga mazingira sawa ..Karibu
Mada ya leo ni kuhusu kinara wa upinzani nchini Uganda Bob Wine pamoja na baadhi ya wagombea wengine wa upinzani wameendelea kunyanyaswa na vyombo vya usalama wanapoendelea na kampeni zao, tume ya uchaguzi ikilaani vitendo hivyo.Yanayofanyika Uganda yanashuhudiwa pia kwenye mataifa kadhaa ya Afrika .Tumemuuliza msikilizaji Hatua hii ya vyombo vya usalama inaathiri vipi demokrasia na nini kifanyike kujenga mazingira sawa ..Karibu
Ripoti nyingi huonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ni akina mama au watoto Hii ni kutokana na wao kutangamana moja kwa moja na mazingira ambayo huwa makazi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa mbali mbali. Vimelea hao hukaa mchangani,kwenye maji au hupatikana kwenye kinyesi .
Kumekuwa na hisia mseto kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya rais mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani nchini Uganda, hali ya nchini Tanzania wakati huu wananchi wakijiandaa kushiriki uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu, maandamano ya vijana Gen Z nchini Madagascar, na mashambulio ya mjini Manchester Uingereza.Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uganda, uliopangwa kufanyika Januari 12, 2026, zilianza Septemba 29. Kuna wagombea wanane wa urais, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 39. Mpinzani wake mkuu ni Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 43. Nini kinachotarajiwa kwenye kampeni hizi ?
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
Kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi oktoba mwaka huu nchini Tanzania, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame dhidi ya mzozo wa mashariki mwa DRC, mapigano makali kati ya jeshi la Congo FARDC na washirika wao wazalendo maeneo ya milima ya Fizi, hali nchini Sudan, ziara ya rais wa senegal jijini Paris ufaransa, Urusi yaendeleza mashambulio huko Kiev Ukraine licha ya shinikizo za Kimataifa na mengineyo.
Tanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu kuanzia Agosti 28, kuelekea kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025. Rais Samia Suluhu Hassan, kutoka chama tawala CCM, anawania uongozi wa nchi hiyo. Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.
Watoto wana jukumu muhimu katika uhifadhi wa mazingira na wanyamapori kwa kushiriki kikamilifu katika mipango kama vile kupanda miti, udhibiti wa taka, na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mazingira na wanyamapori. Kuwashirikisha watoto katika shughuli hizi kunakuza hisia ya uwakili, kuwaunganisha na mazingira wanayoishi, na kukuza mazoea endelevu kwa siku zijazo.
Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wameendesha kampeni ya afya na kusaidia wakimbizi wa ndani kupata matibabu katika eneo hilo lililogubikwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
Kampeni za uchaguzi wa shirikisho wa 2025 zina karibia tamati.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC ambako ghasia za hivi karibuni huko Goma zimeongeza mahitaji ya huduma za afya, WHO imechangia vifaa muhimu vya matibabu ili kukabialiana na hali hiyo. Pata pia muhtasari wa habari na mashinani.Kufuatia ripoti za kuweko kwa ugonjwa usiojulikana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao tayari umeambukiza mamia ya watu na kusababisha makumi ya vifo, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ugonjwa huo uliotangazwa kwa chapisho la kikanda la WHO.Kampeni ya chanjo ya polio inayoendelea ukanda wa Gaza kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya polio na kuzuia tishio la ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine na nchi jirani, imekuwa na mafanikio makubwa kwani hata eneo la Gaza Kaskazini, mwitikio ulikuwa mkubwa licha ya mvua na baridi kali.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo limetangaza kuwa sitisho la mapigano Gaza limewezesha kufikisha eneo hilo kwa wastani maradufu ya shehena za vyakula kilichokuwa kinapelekwa kabla ya sitisho la mapigano.Katika mashinani, hivi majuzi Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, UNICEF katika ripoti yake lilibaini kwamba mtoto 1 kati ya watano nchini Ukraine ameripoti kupoteza ndugu au rafiki wa karibu tangu kuzidi kuongezeka kwa vita miaka mitatu sasa. Akitafakari juu ya zama zijazo, Toby Fricker, Afisa Mkuu wa mawasiliano wa Shirika hilo nchini Ukraine anasema UNICEF inaendelea kushikamana nao.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika makala ya leo Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania ambako katika kuhamasisha elimu iliyo salama inayolenga kumlea na kumfundisha mtoto kwa njia chanya zisizoumiza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF) linamuangazia Mwalimu Magesa Stanslaus ambaye amebadilika kutoka katika matumizi ya viboko na sasa anatumia motisha tofauti kuwarekebisha wanafunzi wake.
Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Asante Anold, kampeni hiyo iliyoahirishwa ilitakiwa kuanza leo n ani duru ya mwisho ya chango ya kampeni iliyolenga kuwachanja watoto 119,279 kote Gaza Kaskazini kwa dozi ya pili ya chanjo ya polio aina ya nOPV2, lakini hali ya sasa imefanya iwe vigumu kwa familia kupeleka watoto wao kwenye vituo vya chanjo, na kwa wahudumu wa afya kuendesha huduma kwa usalama.Mashambulizi ya makombora yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya kiraia yamepunguza maeneo yanayokubaliwa kwa usitishaji wa uhasama kwa mnajili ya masuala ya kibinadamu kuwa kwenye Jiji la Gaza pekee, ikilinganishwa na wakati wa awamu ya kwanza ya chanjo iliyofanyika tarehe 1-12 Septemba 2024.Hali hii inahatarisha kufikiwa kwa lengo la angalau asilimia 90 ya watoto kuchanjwa, jambo ambalo ni muhimu ili kukomesha usambaaji wa virusi vya polio na kulinda afya za watoto.WHO na UNICEF wamesema kuwa kucheleweshwa kwa chanjo ya polio kunaweza kuongeza hatari ya virusi kuenea zaidi Gaza na maeneo Jirani na kuchelewesha utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ndani ya wiki sita kunapunguza uwezo wa chanjo hiyo kuimarisha kinga za watoto na kuzuia maambukizi.Tangu duru ya pili ilipoanza tarehe 14 Oktoba 2024, jumla ya watoto 442,855 wenye umri wa chini ya miaka kumi wamefanikiwa kuchanjwa katika maeneo ya kati na kusini mwa Gaza.UNICEF na WHO wanatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo kutekeleza usitishaji mapigano wa kibinadamu na kuhakikisha kuwa raia, wahudumu wa afya, na miundombinu ya kiraia kama shule na hospitali inakingwa dhidi ya mashambulizi.Mashirika hayo yamesisitiza umuhimu wa kuanza tena kampeni ya chanjo mara moja ili kuzuia kupooza kwa watoto na kuimarisha kinga dhidi ya polio.Katika juhudi za kuhakikisha huduma bora, takribani watoto 357,802 pia walipatiwa virutubisho vya vitamini A kama sehemu ya juhudi za kuunganisha chanjo ya polio na huduma zingine muhimu za afya.Mashirika ya WHO na UNICEF ymesisitiza kuwa kusitisha vita na kuwezesha chanjo ni hatua muhimu ili kuzuia mlipuko wa polio kuendelea na kulinda afya ya watoto wote Gaza.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, watoto waliopokea chanjo hiyo kupitia kampeni ya dharura ya chanjo Gaza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 10.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X zamani Twitter Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Adhanon Ghebreyesus amesema “Tunafurahia timu zote za wahudumu wa afya, zilizoendesha operesheni hii ngumu. Tunashukuru sana kwa familia kwa imani na ushirikiano wao. Haya ni mafanikio makubwa huku kukiwa na hali mbaya ya kila siku ya maisha katika Ukanda wa Gaza. Hebu fikiria nini kingeweza kufikiwa endapo kungekuwa na ushitishwaji mapigano.”Awamu ya kwanza ya chango ilianza Septemba Mosi na lengo lilikuwa ni katika kila duru kuchanja zaidi ya watoto 640 000 wa umri wa chini ya miaka 10.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema maelfu kwa maelfu ya watoto wmechanjwa na kukamilika kwa awamu hiyo ya kwanza ya chanjo ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo na wadau wote walioshiriki kwani wamefikia lengo kwa asilimia 90 ingawa sasa changamoto ni kutoa dozi ya pili ya chanjo hiyo katika awamu ya pili ya kampeni inayotarajiwa katika wiki zijazo.Dozi za chanjo ya polio zaidi ya milioni 1.6 ziliwasili Gaza ili kukamilisha awamu zote mbili za chanjo inayohusisha wahudumu wa afya zaidi ya 2700.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kiongozi wa upinzani wa shirikisho Peter Dutton amesema atafanya kura nyingine ya maoni, kama kura yakuweka sauti yawa Australia wa kwanza bungeni ndani ya katiba inafeli.
Kampeni za uchaguzi mkuu zime anza katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mwanamuziki wa Nigeria Chioma Ogbonna akifahamika kwa jina la usanii “Cill” ni mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG Action Campaign ambaye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni Duniani, LDC5. Moja ya nyimbo zake maarufu ni Woman alioutoa mwaka 2021 ukiwa mahususi kwa ajili ya Siku ya Mwanamke Duniani. Ni wimbo ambao unaeleza nguvu ya mwanamke licha ya kukatishwa tamaa. Nyimbo zake nyingine maarufu za Cill ni pamoja na Tatarata, Kachifo, Permit me na nyinginezo kadhaa. Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na msanii huyu mjini Doha nchini Qatar.
Hii leo jaridani tunasalia hapa makao makuu kukuletea yaliyojiri kwenye Jukwaa la kudumu la watu wa asili, na pia kukupeleka nchini DRC kumulika faida ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga. Makala tunaangazia SDG 17 na Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Jukwaa la kudumu la watu wa asili limeanza rasmi ambapo katika ufunguzi wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na majukumu muhimu ya jamii za asili hususan katika kulinda mazingira na mbinu nyingine mbadala za maisha, watu hawa wanazidi kuwa masikini na kuzitaka nchi zote duniani zihakikishe zinawasaidia kuondokana na umasikini.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga imeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.Katika makala Mwanamuziki Chioma Ogbonna (tamka Obona) “Cill” au Cillsoul wa Nigeria ambaye ni Mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs na anaeleza anavyoutumia kipaji chake kusongesha malengo hayo 17.Na katika mashini tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama limeboresha elimu shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
Kampeni ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu iliyoanza tarehe 25 mwezi huu huko Kivu Kaskazini nchini jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC imekunja jamvi jana Jumanne ya tarehe 30 mwezi hu uwa Januari ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO lilizindua kampeni hiyo ya chanjo kwa wakimbizi wa ndani katika kambi ya wakimbizi hao ya Kanyaruchinya wilayani nyiragongo katika mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini.Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ambaye ameshuhudia uzinduzi huo amesema uliongozwa na Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Jenerali Ndima Constant, na Mwakilishi wa shirika WHO nchini DRC kwa lengo la kuokoa mamia ya familia hususan za wakimbizi wa ndani ambao tayari makumi kwa makumi wameripotiwa kupata ugonjwa huo na wengine wamefariki dunia.Jean Bruno, ni Mkuu wa Ofisi ya WHO Kivu Kaskazini na anasema ameridhishwa na shauku ya siku ya kwanza na zaidi ya yote amesema,« Tumewalenga watu 364,127 ambao ni wakimbizi wa ndani, pamoja na familia zinazowapokea. Tayari tumepokea dozi 364,150 ambazo zipo na zitatumika. chanjo itafanyika kwa awamu ya dozi moja na tutafanya hivyo kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba kwenye maeneo haya . Tumeridhika na ukweli ni kwamba kumekuwa na dhamira muhimu kwa upande wa serikali kwenye ngazi ya taifa na mkoa, lakini pia tumekuwa na hakikisho kutoka kwa jamii ya watu na wakimbizi wa ndani ambayo imekubali chanjo hiyo ambayo itafanyika kwa wakati».Eneo la Nyiragongo lilipokea idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na waaasi wa M23 huku watu 233 elfu waliokimbia makazi yao, zaidi ya 95% yao wamelundikana kwenye makanisa, shule, viwanja vya michezo na maeneo yasio salama kwa afya yao.Gavana wa Kivu Kaskazini, Jenerali Ndima Constant, anakiri kwamba janga la kipindupindu linaathiri sana eneo la Nyiragongo akisema kwamba hadi Jumanne ya Januari 24 wagonjwa 3706 wa kipindupindu walisajiliwa huku kukiwa na vifo 16 na ili kupunguza mlolongo wa maambukizi amewasihi raia kupata chanjo akishukuru WHO kwa msaada wao.« Madhumuni ya kampeni hii ya chanjo ni kulinda idadi ya watu dhidi ya kipindupindu katika jimbo la Kivu Kaskazini na hasa katika maeneo ya watu waliofurushwa ili kupunguza vifo. Mabibi na mabwana, wageni mashuhuri, ili kufunga maoni yangu, ningependa kuwakumbusha kuwa pamoja na chanjo utakayopokea, kufuata hatua za kuzuia maambukizi ni muhimu..”Ametaja njia za kujikunga kuwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi na sabuni au majivu, kunywa maji yaliyotakasishwa tu au yaliyochemshwa. Kupika na kufunika milo yetu, matumizi sahihi ya vyoo huku tukiwa wasafi na kuweka usafi kwenye maeneo yetu ya makazi kila wakati.Waliokimbia makazi yao wanafahamu tishio hilo kwa sababu janga hilo limeathiri zaidi ya 89% ya waliokimbia makazi katika miezi ya hivi karibuni na chanjo inatekelezwa nyumba kwa nyumba.Watu waliohamishwa wanasubiri dozi zao nyumbani. Damaseni Butera ni miongoni mwa watu wa kwanza kupata dozi moja dhidi ya kipindupindu na anashukuru mpango huu wa WHO na anasema, «chanjo ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya magonjwa kama kipindupindu, malaria na mengine.Tumejifunza habari kuhusu chanjo hiyo, tumefurahi sana kwa sababu tutakuwa na kinga, asante sana kwa shirika la WHO ambalo lilitufikiria. Asante sana»Kando na hilo, Mweze Shemba, aliyekimbia kutoka kijiji cha Kiwanja, pia alinufaika na chanjo hii. Licha ya njaa,yeye anapendelea kujilinda pamoja na familia yake dhidi ya janga hili akisema, «kilichonifanya nipate chanjo ya leo hapa katika kambi ya wakimbizi ni kwa sababu tunapatwa na magonjwa ya taabu. kama vile kuharana kutapika hasa tunapokunywa maji machafu. Lakini wakati tunapata hii chanjo tunaona kama vile ni kinga kwetu tunashukuru sana »Katika juhudi za kuepusha msongamano wa wagonjwa wa janga hili , WHO ilijenga vitalu 3 kama kitengo cha matibabu ya wagonjwa wa Kipindupindu (UTC) katika eneo la Bushagara na…
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya ulaya tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali katikati ya mwezi Novemba mwaka 2022 wamebaini kuongezeka kwa wagonjwa wanaolazwa kutokana na magonjwa ya homa ya mafua makali au flu, matatizo ya kupumua na COVID-19. Walio hatarini zaidi kupata maambukizi ya magonjwa hayo ni wahudumu wa afya pamoja na wazee, ndio maana wanaendesha kampeni ya kutoa chanjo. Katika msimu wa baridi mwaka uliopita WHO ukanda wa Ulaya ilifanikiwa kutoa chanjo ya homa ya mafua makali kwa asilimia 65 ya kundi la watu walio hatarini ambao wengi ni wazee na wahudumu wa afya na msimu huu wa baridi lengo ni kuwafikia asilimia 75 ya watu hao. Afisa wa kiufundi wa WHO Kyrgyzstan Kasymbekova Kaliya, anasema wanafahamu namna ugonjwa wa guo ulivyo hatari.…. “tunajua kwamba ugonjwa huu wa homa ya mafua makali unaweza kusababisha matatizo makubwa hasa kwa wazee wenye umri zaidi ya miaka 65, wale ambao wana magonjwa sugu ya moyo, mapafu, kisukari, na wenye hali ya uzio”. Chanjo imeanza kutolewa kwa makundi yaliyo hatarini kuathirika zaidi ya homa ya mafua makali kama anavyoeleza Baktygul Mamatova, mtaalamu wa Kinga katika kituo cha afya cha Bishkek, “Sisi, wahudumu wa afya, kama kundi lililo hatarini ndio tumekuwa wa kwanza kupata chanjo. Siwezi sema kwamba siwezi kupata magonjwa, napata, lakini kwa kuwa nimepata chanjo ni rahisi kuhimili.” Wazee wanfahamu umuhimu wa kupata chanjo kama anavyoeleza Kanai Alamanov, aliyefika katika kituo cha afya cha Bishkek, “Hapo awali, kulikuwa na uhamasishaji wa kupata chanjo dhidi ya virusi vya CORONA nami nilikuja kupata chanjo hiyo ya COVID-19, na sasa ni chanjo ya homa ya mafua makali. Chanjo hii inatupa fursa ya kujikinga na magonjwa, inatupa aina fulani ya hakikisho la maisha yenye afya.” Chanjo hazitolewi kwa wale wanaoenda hospitali pekee, wanaoishi katika nyumba maalum za kutunza wazee nao hufuatwa na kupewa chanjo kama anavyothibitisha Ludmila Kinda Ivanovna, “Mimi ninaugua sana. Mwili wangu haukubali kabisa kutumia aina nyingi ya dawa ikiwemo zile za viua vijasumu, nina pumu , nina matatizo ya moyo, nilishapata mstuko wa moyo mara mbili. Kiufupi mwili wangu ni dhaifi sana hivyo chanjo ina maana kubwa sana kwangu.”
Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo wamekabidhi jengo kwa ajili ya mahali pa wagonjwa na wahudumu wa afya kula chakula katika Kituo cha Afya cha Mavivi, mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.Akikabidhi jengo hilo Kamanda wa kikosi cha tisa cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania Luteni Kanali Barakael Mley amesema jengo hilo litabaki kuwa kumbukumbu ya uhusiano mzuri baina ya walinda Amani wa kikundi cha Tisa na wananchi wa maeneo ya Mavivi na maeneo jirani,Akiongea kwa niaba ya Maganga mkuu wa hospital ya Oicha na wananchi wa maeneo ya Mavivi Dr Kasereka Nzala amewapongeza walinda Amani hao wa Tanzania wanaohudumu chini ya mwamvuli wa MONUSCO wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali katika kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao ya uwajibikaji,Kwa upande wake afisa Mahusiano wa kikosi cha tisa cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania Kepteni Paul Mwesongo amebainisha kuwa hali ya uhusiano baina ya wananchi na walinda Amani hao,Naye bi Kavathama Clarice, mwenyekiti wa kamati ya Afya katika kituo cha afya cha Mavivi amesema,
Kikosi cha tisa cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 kinachohudumu ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, kimeanzisha kampeni iliyopewa jina la “Afya na Amani” ambayo inahusisha utoaji wa dawa za binadamu katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za baadhi ya maeneo ya uwajibikaji ya Kikosi hicho ndani ya mji wa Beni, kaskazini mashariki mwa DRC.Akipokea dawa hizo muuguzi Mkuu wa Kituo cha afya cha Mavivi, Kisu Kanyambala Janvier, amewashukuru TANZBATT 9 kwa msaada huo na kusema kwamba utawasaidia wananchi wote.“Tunashukuru sana kikundi cha watanzania wa MONUSCO kwa msaada waliotuletea na ni msaada mkubwa wa dawa, tulikuwa na ulazima wa kuipata hii dawa na tulikuwa tunaikosa. Tunashukuru sana msaada huu utasaidia wakina mama, watoto na watu wote.” Anasema Kanyambala.Aidha Kanyambala amebainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa walinda amani wa Tanzania katika eneo hilo kuwasaidia wananchi kwani waliwajengea wodi ya akina mama na watoto na ujenzi wa kantini kwa ajili ya wagonjwa kula chakula ambayo ipo mbioni kukamilika.Kwa upande wake Kamanda Kikosi wa TANZBATT 9 Luteni Kanali Barakael Jackson Mley amesisitiza kuhusu suala la ushirikiano baina ya walinda amani wa MONUSCO na wananchi na kueleza kuwa wananchi wanapokuwa na afya nzuri wataweza kushiriki vyema katika kuleta amani ya maeneo yao, “sisi ujumbe wetu mkubwa ni ushirikiano ili kutatua changamoto za kiusalama tulizo nazo, bila ushirikiano baina ya raia na kikundi chetu cha tisa cha ulinzi wa Amani kutoka Tanzania hatutaweza kufanikisha jukumu hili”. Akisisitiza umuhimu wa kampeni hiyo kwa jamii, Kavumba Dezanji ambaye ni kiongozi wa wanawake katika eneo la Mbau amesema, “nasema afya mbele ya yote, ukiwa na afya njema utafanya kazi yoyote ya maendeleo.” Aidha, Dezanji ameomba usalama uboreshwe katika eneo la Mbau na kuomba mradi kama huo wa Afya na Amani uendelee katika mji huo.Naye Bukuka Makofi Chifu wa kimila wa eneo la Mavivi, amewashukuru walinda amani kutoka Tanzania kwa msaada huo na kusema “ni kitu cha kushukuru sana, inaonesha kama wanaendelea kutuonesha ushirikiano na upendo, mwanzo wa mwaka sisi kama tumebarikiwa kwa sababu tulikuwa na shida ya dawa kutokana na eneo hili kupokea watu wengi kutoka sehemu nyingine, hii itaendelea kutusapoti sana.” Kampeni ya Afya na Amani ni kampeni iliyoanza kuanzia tarehe 03 mwezi huu wa Januari na itadumu hadi tarehe 13 januari 2023.
Tunapo ingia katika majira ya joto, shirika la Royal Life Saving Australia, limezindua kampeni mpya kukabiliana na ongezeko kubwa kwa idadi ya visa vya vifo vinavyo sababishwa na kuzama majini nchini Australia.
Katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiweno lengo namba 3 linalolenga Afya bora na ustawi, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Malawi linaendesha kampeni ya M'mera mpoyamba inayohamasisha wajawazito kufika katika vituo vya afya angalau mara nne kabla ya kujifunga na kuhakikisha wanapata saa moja ya ziada ya kulala ili kujihakikishia ujauzito salama na kujifungua mtoto mwenye afya bora. Kampeni hiyo inaendeshwa kwa njia mbalimbali ikiwemo mchezo wa video ambao Leah Mushi wa Idhaa hiiya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ameutafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Kenya, zina endelea kupamba moto haswa baada ya vyama kufanya mchujo wa wagombea pamoja nakuwatea vinara na manaibu wao.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umezindua kampeni ya ulinzi wa raia ili kusaidia upatikanaji wa amani pamoja na kuwezesha mamlaka za serikali nchini humo kutekeleza majukumu yake.
Wiki ya tatu ya kampeni ya uchaguzi mkuu ili tawaliwa na shinikizo za gharama za maisha, baada ya mfumuko wa bei kuongezeka kwa 5.1%.
Kiongozi wa chama cha Labor Anthony Albanese, amaliza siku yake ya tatu akijitenga baada yakuambukizwa UVIKO-19.
Nchini Kenya harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF za kuondoa fikra potofu katika kaunti ya Kisumu kuhusu chanjo dhidi ya Corona au COVID-19 zimezaa matunda na sasa hata wale waliokuwa wamesita kupata chanjo hiyo wameanza kupata.