Meza Huru

Follow Meza Huru
Share on
Copy link to clipboard

Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.

Meza Huru


    • Nov 25, 2022 LATEST EPISODE
    • infrequent NEW EPISODES
    • 1h 34m AVG DURATION
    • 19 EPISODES


    Search for episodes from Meza Huru with a specific topic:

    Latest episodes from Meza Huru

    Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18

    Play Episode Listen Later Nov 25, 2022 150:38


    Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo.  nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)?  Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo? Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare

    Mezani na KIBACHA Part II

    Play Episode Listen Later Nov 22, 2022 101:22


    Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Mwamba huyu hapa

    Mezani na KIBACHA Part I

    Play Episode Listen Later Nov 18, 2022 99:08


    Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania. Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT. Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo. Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa

    Mezani na DOLO #15

    Play Episode Listen Later Nov 11, 2022 129:20


    Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK.  Kutoka maeneo ya TEMEKE.  Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo,  mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK. #MezaniNaDolo  #MezaHuru

    Mezani na KR MULLAH #14

    Play Episode Listen Later Nov 4, 2022 90:54


    KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk. Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba. #MezaniNaKakaRashidi #MezaHuru

    Mezani na RAS INNO #13

    Play Episode Listen Later Oct 28, 2022 126:05


    Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania. Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo. Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia, Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu. #MezaniNaRasInno #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0... Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp... Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

    Mezani na CAROLA KINASHA #12

    Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 137:24


    Carola Kinasha, ukimuona huwezi kuamini ana miongo sita duniani. First lady wa Bene Bene na baadaye Shada. Msomi wa chuo kikuu aliyechagua kufanya muziki kama kazi. Mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa stahiki na haki za utunzi, na moja walioupeleka mbali sana muziki wa asili ya Afrika. Ni mcheshi na mwenye maarifa mengi sana kuhusu maisha na safari ya muziki wetu tangu miaka ya themanini mpaka leo hii. Unajua kisa chake na Remmy Ongala kilichozaa kibao maarufu cha Karola? Unajua nini maana ya segese? Unajua kwamba yeye ni mtu aliyekuwa nyuma ya chorus nzuri na tamu za Bongofleva yetu hii? Carola Kinasha ni nyota wa muziki wetu na Almasi inayowaka kama taa. Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu #MezaniNaCarolaKinasha #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0... Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp... Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

    Mezani na MIKE TEE #11

    Play Episode Listen Later Oct 14, 2022 118:40


    Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu. Mike Tee alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 90, akiimba kwaya kanisani na taratibu akaanza kujifunza kuandika na kuimba mistari kupitia mashairi ya gazetini baada ya kukutana na Ntwa mmoja wa waanzilishi wa WWA (Wagumu Weusi Asilia). Amefanya kazi na watayarishaji kama P Funk na Master Jay, amefanya hits na wasanii kama Juma Nature, Q Chief, Mad Ice na Komando Jide Unajua kuhusu ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya? Mike Tee amenyoosha taarifa. Sitaki kumalizia stori yake. Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu #MezaniNaMikeTee #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0... Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp... Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

    Mezani na UNCLE JOHN KITIME #10

    Play Episode Listen Later Oct 7, 2022 137:30


    Mzee Kitime ama Ango "Uncle" Kitime kama mwenyewe anavyojitanabaisha kwenye mitandao. Ni mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi kutoka Kilimanjaro Band maarufu kama "Wana Njenje", mmoja wa wanakamati ya kutetea muziki wa dansi na tasnia ya muziki kwa ujumla, Mtangazaji wa Radio, Muigizaji wa Filamu, Mchekeshaji na Mtunza historia ya Music wa Tanzania. Tumekaa naye na kupata historia ya muziki wake na harakati zake tangu mwaka 1967 hadi leo akiwa na JFK BAND. Jumuika nasi mezani tumsikilize Gwiji huyu wa Tasnia yetu, Karibu. #MezaniNaJOHNKITIME #MezaHuru Anchor - https://anchor.fm/meza-huru Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0... Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683 Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797 Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087 Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp... Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... Twitter - https://twitter.com/MezaHuru Instagram - https://instagram/mezahurupodcast

    Mezani na MASTER JAY Part II

    Play Episode Listen Later Sep 30, 2022 58:38


    Sehemu ya pili ya maongezi na Master Jay. Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini

    Mezani na MASTER JAY Part I

    Play Episode Listen Later Sep 23, 2022 86:36


    Nani asiyemfahamu Master Jay? Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini

    Mezani na BONILUV #TheGodfather Part II

    Play Episode Listen Later Sep 16, 2022 79:32


    Sehemu ya pili na Kaka Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv. Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya Poppaluv

    Mezani na BONILUV #TheGodfather Part I

    Play Episode Listen Later Sep 9, 2022 77:09


    Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tumsikilize Poppaluv

    Mezani na DUNGA #05

    Play Episode Listen Later Sep 2, 2022 115:00


    #MezaniNaDunga #MezaHuru #Dunga Wengi wetu tunamfahamu kwa jina la Dunga ama Mandugu. Jina lake kamili ni Ambrose Akula Akwabi. Huyu ni mtu muhimu sana katika muziki wetu. Amekuwepo tangu enzi tunajitafuta. Dunga na kaka yake (Shakii) wanaunda Mandugu Digital. Amefanya kazi nyingi sana mashuhuri na nyingine unaweza usiamini anahusika nazo. Jumuika nasi mezani, tumsikilize Mwamba Huyu

    Mezani na JORS BLESS #04

    Play Episode Listen Later Aug 26, 2022 92:28


    Johnson Sululu a.k.a Jorsbless ni sehemu ya kizazi bora cha utayarishaji na uandaaji wa midundo katika tasnia ya muziki Tanzania Amefanya kazi na wasanii kama Mapacha, Rama Dee, Nikki Wa Pili , Adili n.k Unakumbuka kuhusu ANTI-VIRUS Movement? Tumeligusia hili pia

    Mezani na MEJAH #03

    Play Episode Listen Later Aug 19, 2022 78:58


    MEJAH ni Mwana Hip Hop na Mjasiriamali aliyegeuza mahaba yake ya uchora machata(GRAFFITI), Kusafiri, Kuendesha baiskeli kuwa sehemu ya kipato chake Tumepata nafasi ya kuzungumza nae na anatupitisha katika historia ya maisha yake kuanzia kuandika sehemu ya wimbo wa JCB wa Kundi la Watengwa,Kuuza majarida mbalimbali mfano "The Source" mpaka kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Graffiti kupitia kundi la Wachata Bila kusahau ni Classmate wa January Makamba

    "Kwenda Mbele"

    Play Episode Listen Later Aug 14, 2022 56:59


    A Conversation with Duke Part ii

    "The First Session"

    Play Episode Listen Later Aug 11, 2022 50:10


    First part of Duke opening up about his journey in Tanzanian Music.

    #KaribuMezaHuru

    Play Episode Listen Later Aug 9, 2022 0:34


    A Conversation about Music in Tanzania. From genesis to where it's now. A 20yrs+ journey in the game. Looking at this history from a perspective of our guest. This is Meza Huru, Karibu.

    Claim Meza Huru

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel