POPULARITY
Categories
Je, umewahi kujiuliza Mwezi ulitoka wapi?
About one in five Australian men will be diagnosed with prostate cancer in their lifetime. Understanding the prostate, your risk and the options for testing can help with early detection and treatment. In this episode of Australia Explained, learn about prostate cancer, PSA testing, treatment and support. - Karibu mwanaume mmoja kati ya watano wa Australia atagunduliwa ana saratani ya tezi dume katika maisha yake. Kuelewa tezi dume, hatari yako na chaguzi za kupima kunaweza kusaidia katika kugundua na kutibu mapema. Katika makala haya ya Australia Yafafanuliwa, jifunze kuhusu saratani ya tezi dume, upimaji wa PSA, matibabu na usaidizi.
Karibu kwenye sayari ya mwisho ya Mfumo wetu wa Jua, NEPTUNI, sayari ya barafu (ice giant) iliyo mbali zaidi na Jua, kwa umbali wa kilomita bilioni 4.5.
Karibu katika makala yetu ya leo Jumapili Changu Chako Chako Changu. Makala haya hukuletea Historia na tamaduni ya makabila mbalimbali, le Parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletza Historia ya watu wa kabila la Wahehe, kutoka chini Tanzania na kwenye Muziki nitakuletea msanii kutoka nchini Uganda Made Ice, Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu.
Karibu katika makala changu chako chako chako changu Jumapili ya leo nakuletea sehemu ya 3 na ya mwisho ya historia ya waswahili wa Burundi, ambapo sehemu ya mwisho mgeni wetu atatueleza harakati za kumtambuwa mswahili wa Burundi Na kwenye Muziki nitakuletea Mwanamuzi nguli wa miondoko ya Contry kutoka nchini Marekani Dolly Parton ambae amefariki dunia juma hili. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama karibu. Nifuate kwenye mitandao ya kijamii @billybilali
Leo jaridani kuna Mada kwa Kina inakupeleka Uganda kumulika Siku ya Ziwa duniani hususan Ziwa Albert.Lakini pia kuna Muhtasari ukiwasilishwa na Leah Mushi akiangazia kumalizika kwa mlipuko wa Ebola, Uganda; Kauli ya Katibu Mkuu wa UM kuhusu maambukizi ya Ebola nchini DR Congo na kisha chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.Jifunze Kiswahili leo inabisha hodi nchini Burundi kwa Mwenyekiti wa CHAWARUNDI Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Karibu katika Makala changu chako chako change, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya historia ya waswahili wa Burundi na kwenye muziki nitakuletea mwanamuziki Lady Jay D. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu. Nifuatilie @billybilali
Karibu uungane nami Partick Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, ambapo leo studio nipo na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba akiendelea kujibu maswali ya wasikilizaji wetu, moja ya swali alilojibu ni je, mtu akibatizwa katika dhehebu lingine awaweza kubatizwa tena? L'articolo Je, Mtu akibatizwa katika dhehebu lingine anaweza kubatizwa tena? proviene da Radio Maria.
Karibu uungane nami Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoka akiendelea kujibu maswali ya msikilizaji na moja la maswali hayo ni je, Tanzania kuna jumla ya majimbo mangapi Katoliki? L'articolo Je, unafahamu Tanzania kuna jumla ya Majimbo Katoliki Mangapi? proviene da Radio Maria.
Karibu katika kipindi cha Tafakari Nasi, tunaungana na Padre John Bosco, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kilimahewa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam akitutafakarisha juu ya mambo sita bora na muhimu kuliko fedha, umaarufu na madaraka. L'articolo Fahamu mambo sita muhimu kuliko fedha proviene da Radio Maria.
Karibu katika Makala haya yanayozungumzia historia ya waswahili wa Burundi. Mntangazaji wako Ali Bilali alikutana na mwanahistoria kutoka Buyenzi Mzee Anzuruni ambae anaeleza kwa kina hapa historia ya waswahili wa taifa hilo. Nifuatilie kwenye mtandao wa kijamii @billy bilali
Karibu usikilize jarida la habari za UN ambalo leo habari zake zote zimetoka barani Afrika. Utasikia kuhusu juhudi za kutoa chanjo wa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 huko nchini Somalia.Utasikia namna FAO inavyowasaidia wananchi huko Zanzibar kuongeza ubora wa zao la Mwani.Na mwisho utasikia ufinyu wa bajeti unavyoathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini.
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo utasikia mahojiano na kijana kutoka nchini Kenya Feisal Kirwa aliyekuwa akishiriki mafunzo kwa Vitendo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa muda wa miezi sita na sasa amehitimu mafunzo hayo. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari.
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong anatarajiwa kwenda Ufilipino kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Asia Mashariki na Jukwaa la Kikanda la ASEAN.Tume ya Dhamana na Uwekezaji ya Australia inasema imepata rekodi ya dola milioni 830 katika amri za adhabu za kiraia wakati wa Mwaka wa Fedha wa 2025-2026. Tume hiyo ilianzisha chunguzi zaidi ya 250, ambazo zilisababisha hatia 25 za jinai na watu 11 kuhukumiwa kifungo cha gerezani.Karibu watu 930 wamefariki dunia kutokana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya afya nchini humo. Vifo hivyo vimerekodiwa miongoni mwa visa 2,344 vya maambukizi vilivyothibitishwa hadi siku ya Jumamosi imesema wizara hiyo hii leo. Vifo vipya vilirekodiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, idadi ya juu kabisa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja.Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania imetekwa nyara na maharamia wanaoshukiwa kuwa wa Somalia katika pwani ya Yemen, vimebaini vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo kuhusu tukio hilo. Meli hiyo imehamishwa hadi majini katika eneo la Bari kaskazini mashariki mwa Somalia, kulingana na maafisa wa eneo hilo.
Karibu kusikiliza kipindi cha Nena Nami Bwana, ambapo Askofu Almachius Vincent Rweyongeza anatafakari Neno la Mungu na kutoa mafundisho yanayolenga kuimarisha imani, matumaini na upendo katika maisha ya kila siku ya Mkristo. Tunakukaribisha usikilize tafakari hii, uibariki kwa kuishiriki na wengine, na usisahau kujiunga na chaneli yetu ili kuendelea kupokea mafundisho na vipindi vingine vya […] L'articolo Nena Nami Bwana na Askofu Almachius Vincent Rweyongeza proviene da Radio Maria.
Katika kipindi hiki, Frateri Ayuto Kongo kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho anafafanua maana ya neno ibada katika muktadha wa Kikristo, akieleza msingi wake katika imani na namna linavyopaswa kuonekana katika maisha ya kila siku. Karibu utazame L'articolo Neno “Ibada” katika muktadha wa Kikristo linaelewekaje? proviene da Radio Maria.
Karibu katika Makala yrtu ya leo jumapili change chako chako change Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki ambapo leo nakuletea kwa mara nyingine tena historia ya watu wa kabila la wabembe. Na kwenye Muziki nitakuletea historia ya mwanamuziki Mista Gave aliefariki dunia juma hili huko Uvira. Mazishi ya msanii Gave yamepangwa kufanyika Julai 22 hapo Uvira. mimi ni Ali Bilali mtangazaji asiependa makuu, Bienvenue, ama karibu. fuatilia pia @billybilali
Karibu katika makala yetu ya leo changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea historia ya lugha ya kiswahili. Na kwenye muziki nitakuletea muziki kutoka bendi ya Lelele Afrika kutoka Mombasa nchini Kenya. Mimi ni Ali Bilali, bienvenue, ama Karibu.
Karibu katika Makala yetu ya leo change chako chako changu maalum kabisa kuhusu kumbukumbu ya miaka 16 tangu kuzanzishwa kwa matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya RFI yalianza kurindima Julay 5 mwaka 2025 Mubashara jijini Dar es salaam nchini Tanzania kabla ya kuhamia jijini Nairobi baadae. Utawasikiliza baadhi ya watangaezaji, lakini pia nitakuletea burudani ya Muziki kutoka nchini Kenya Otile Brown na kibao chake kipya kabisa NI wewe. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue. Insert………
The recent panel discussion at MahoganyBooks, celebrating Char Adams's debut nonfiction work, 'Black Owned: The Revolutionary Life of the Black Bookstore,' provided a profound exploration of the pivotal role that Black bookstores play in community consciousness and cultural identity. Moderated by Derrick Young, the co-owner of MahoganyBooks, the panel included influential figures such as Shirikiana Gerima, founder of Sankofa Video and Bookstore, Ramunda Lark Young, also a co-owner of MahoganyBooks, and Paul Coates, a prominent publisher and activist. Throughout the discourse, the speakers delved into the nuances of intentional curation and the delicate balance of censorship—addressing how the selection of books can reflect and shape community narratives. They emphasized that Black bookstores are not merely commercial entities, but rather vital cultural institutions that foster a sense of identity and belonging. Adams articulated her vision of a collaborative ecosystem among Black bookstores, highlighting the importance of mutual support and resilience in the face of economic challenges. This discussion not only illuminated the historical significance of Black bookstores but also pointed towards a future where they continue to thrive as hubs of education and community engagement.Takeaways:The discussion illuminated the profound role of Black bookstores in transforming community consciousness, transcending mere profit motivations.Panelists emphasized the importance of intentional curation in bookstores, reflecting a commitment to community over commercial interests.The historical impact of Black bookstores like Karibu was recalled, demonstrating their pivotal role in fostering literary culture and community.Char Adams's insights on the collaborative nature of the Black book ecosystem highlighted the necessity of unity among bookstores and authors.The conversation addressed the evolution of technology in bookselling, illustrating how online platforms have expanded access and community engagement.Through shared experiences, the panelists underscored the resilience and adaptability of Black bookstores in navigating contemporary challenges.Hosts & Guests:Char AdamsRamunda Lark YoungShirikiana GerimaPaul CoatesDerrick A. Young (Host)Podcast Credits:Production: Muse ProAudio: Christian Jones (https://www.instagram.com/cjthegenesis)Add it to your LibraryBlack-Owned: The Revolutionary Life of the Black BookstoreMentioned in this episode:African AncestryWe are the pioneers of genetic ancestry tracing for Black people globally, reconnecting you to your specific African roots–the country and the people. Our scientists compare your DNA markers to the largest African reference database in the world in order to find your African origin up to 2000 years ago.African Ancestry
Karibu katika makala changu chako chako changu Jumapili ya leo, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea historia ya uhuru wa Burundi na kwenye kipengele cha utamaduni nitakuletea tamasha la Umutwenzi lililoandaliwa na wasanii wa Burundi katika mkesha wa siku ya Uhuru wa Burundi na kwenye Muziki nitakuletea kibao cha wasanii wa Burundi walioshirikiana Pamoja. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue.
Karibu katika Makala changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea Makala kuhusu tamaduni mbalimbali ambazo zimepitwa na wakati katika makabila mbalimbali, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Dully Sikes kutoka nchini Tanzania. Mimi ni Ali Bilali, Binevenue ama Karibu.
Karibu katika Makala yetu ya leo changu chako chako changu, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophone na Muziki. Mimi ni Ali Bilali nakukaribisha karibu, ama Bienvenue. Kumbuka pia kunifuatilia @billy bilali
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknolojia za malipo ya mtandaoni hasa kupitia simu, jina langu ni Emmanuel Makundi, Karibu.
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknolojia za malipo ya mtandaoni hasa kupitia simu, jina langu ni Emmanuel Makundi, Karibu.
Karibu kwenye kipindi cha habari Rafiki ,mada ikiwa kuhusu maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo yatafanyika Ijumaa,huku kauli mbiu ikiwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Tumekuuliza, serikali ya nchi yako inafanya vya kutosha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ? Na je , sekta binafsi na wananchi wanapaswa kufanya nini sasa,ili kuimarisha mazingira,,karibu tuandamane pamoja .
Karibu kwenye kipindi cha habari Rafiki ,mada ikiwa kuhusu maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo yatafanyika Ijumaa,huku kauli mbiu ikiwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Tumekuuliza, serikali ya nchi yako inafanya vya kutosha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ? Na je , sekta binafsi na wananchi wanapaswa kufanya nini sasa,ili kuimarisha mazingira,,karibu tuandamane pamoja .
Karibu katika Makala yetu ya leo changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophone na Muziki ambapo leo nakuleteza historia ya xenophobia (chuki au woga dhidi ya wageni) tutaungana naye Mariam Posho joélle akiwa nchini Afrika kusini na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Mario na wimbo wake mpya Mombasa. Kumbuka kunifuatilia @billy bilali
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangazwa kwa mara nyingine kugundulika kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC katika jimbo la Ituri lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya 17 kwa mlipuko wa Ebola kutokea DRC tangu kugunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976. Wagonjwa 13 vimethibitishwa na taasisi ya utafiti wa tiba ya INRB mjini Kinshasa. Dkt. Tedros amesema tayari wametuma wataalamu, vifaa tiba na ameruhusu kutolewa kwa dola laki tano kusaidia kudhibiti mlipuko huo na kuwahudumia wagonjwa.Hali ya kibinadamu nchini Somalia inazidi kuwa mbaya kuliko ilivyotarajiwa hapo awali. Akuzungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi afisa mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia George Conway amesema “Hivi sasa Takriban watu milioni sita nchini Somalia amba ni sawa na mtu mmoja kati ya sita anakabiliwa na njaa ikimaanisha kuwa anaruka muda wa kula chakula, au anaenda siku kadhaa bila chakula cha kutosha. Watoto ndio wanaolipa gharama kubwa zaidi. Karibu watoto milioni mbili wana utapiamlo mkali, ikimaanisha kuwa wana utapiamlo mbaya na dhaifu kimwili, na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kuugua au kufa.”.Na leo ni siku ya Kimataifa ya Familia, Umoja wa Mataifa unasema maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia jinsi umaskini, ukosefu wa huduma muhimu na msaada mdogo wa malezi vinavyoathiri familia na kudhoofisha maendeleo bora ya watoto. Maadhimisho ya mwaka huu yanaweka mkazo maalum kwenye hatua jumuishi za ulinzi wa kijamii kama vile ruzuku za watoto, likizo za uzazi zenye malipo, huduma nafuu za malezi ya watoto na elimu ya awali kwa watoto wadogo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Karibu usikilize Kipindi cha Walinde watoto Mwezeshaji ni Davis John kutoka Chuo Kikuu Kikatoliki Mwenge Jimbo Katoliki Moshi Mada ni Namna ya kumsilikiza mtoto aliyejeruhiwa Kimwili au kingono Mtangazaji Elizabeth Masanja Tarehe 19 Aprili 2026 L'articolo Namna ya kumsilikiza mtoto aliyejeruhiwa Kimwili au kingono proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Ujumbe wa Biblia. Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino-SAUT,Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. Mada ni Maadaui wanne wa mwanadamu Tarehe 02 Machi 2026 L'articolo Fahamu faida za kanunia ya imani proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Walinde watoto Padre Peter Siamo kutoka Chuo Kikuu Kikatoliki Mwenge Jimbo Katoliki Moshi Swali ni Ushauri nasaha kwa watoto Mtangazaji Peter Alphaxad. Tarehe 29 Machi 2026 L'articolo Tujifunze juu ya mtoto kabala ya kumpatia ushauri nasaha. proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Walinde watoto Wawezeshaji ni Sista Mariselina John na Sista Patricia Kijuu Mada ni Utoaji ripoti juu ya unyanyasaji wa watoto Mtangazaji Elizabeth Masanja Tarehe 01 Machi 2026 L'articolo Hii ndiyo njia ya utoaji ripoti juu ya unyanyasaji wa watoto proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Familia Bora nyumba Aminifu. Mada ni Tafakari ya kipindi cha Kwaresima? Tarehe 15 Machi 2026 L'articolo Maandalizi ya familia na Sakramenti ya kitubio kuelekea Pasaka. proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Utume wa Walei Mwezeshaji Bwana Gordon Rwenyagira, Mjumbe kamati ya Uinjilishaji Jimbo kuu Katoliki Dar es Salaam Mada ni Kanzi ya Uongozi Tarehe 20 Machi 2026 L'articolo Hii ndiyo furaha ya Utume wetu proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Pro_life Utetezi wa Uhai Wawezeshaji kutoka Prolife Tanzania Anthon Liepa, Janet Akkaro na Bi Grace Shayo Mada ni Malezi ya Mtoto baada ya kuzaliwa Tarehe 14 Aprili 2026 L'articolo Fahamu wajibu wa Wazazi na jamii katika malezi ya mtoto. proviene da Radio Maria.
Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Desderius Mwambaluka, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Naomba kujua Maisha ya Mitume wa Yesu na vifo vyao baada ya yesu kupaa. Tarehe 22 Machi 2026 L'articolo Fahamu Maisha ya Mitume wa Yesu na vifo vyao baada ya yesu kupaa? proviene da Radio Maria.
Karibu kwenye msururu mpya wa vipindi vya uchambuzi wangu wa maudhui tofauti tofauti katika maisha yetu. Natumai utafurahia
Hii leo jaridani mwenyeji wako Flora Nducha anamulika Mashariki ya Kati, mzozo Sudan Kusini unavyoendelea kuleta machungu kwa raia. Ingawa hivyo kuna habari njema ya jinsi FAO inavyoleta nuru kwa wakulima nchini Somalia kwa kukarabati mifereji ya umwagiliaji. Karibu!===========================Vita huko Mashariki ya Kati vinaendelea leo ikiwa ni siku ya 28, mashambulizi yanasababisha hofu, mateso, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu katika eneo lote. Huko Geneva, Uswisi wanadiplomasia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo wanajadili shambulizi la shule lililotokea Minab, Iran, ambalo limeua zaidi ya watoto 100. Leah Mushi anasimulizi hii ya kusikitisha.Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudani Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Rashid Malekela anatupeleka kufahamu maisha ya wakimbizi huo yapoje?Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.
Hii leo jaridani tunamulika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), hali Mashariki ya Kati, Amerika ya Kati, kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania na katika kujifunza lugha ya Kiswahili ni uchambuzi wa neno, 'Nyapanyapa.'MUHTASARIMabaraza ya Umoja wa Mataifa lile la Usalama na lile la Haki za Binadamu kwa nyakati tofauti yajadili hali ya usalama na haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Huko Mashariki ya Kati hali ya usalama na kibinadamu yazidi kuwa tete Lebanon na Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea kila uchao.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO azungumzia hali tete ya afya nchini Cuba kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya umeme.MADA KWA KINA: Jinsimafunzo ya kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi yalivyoanza kuonesha matokeo chanya huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania. Mradi ni wa FAO kwa kushirikiana na SMZ.JIFUNZE KISWAHILI- Mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania anafafanua maana ya neno 'Nyapanyapa.'Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEMBUA" . Kama umezoea kuwa unapembua mchele basi fahamu kuna zaidi ya maana hiyo. Karibu.
Karibu katika muziki Ijumaa, makala maalumu ya RFI Kiswahili inayokuletea vibao vya kukumbukwa vilivyoacha alama kubwa katika historia ya muziki wa dunia.Wiki hii tunasafiri kimuziki kutoka Marekani, kupitia Karibiani, hadi Afrika Mashariki na Afrika ya Kati, tukifurahia nyimbo zenye ujumbe wa furaha, mapenzi, imani na utu. Safari yetu inaanza nchini Marekani kwa kibao “Celebration” cha kundi la Kool & The Gang wimbo uliogeuka kuwa nembo ya sherehe duniani kote, ukiwahamasisha watu kusahau huzuni na kusherehekea maisha. Kutoka hapo tunatua Karibiani kupitia “Jamaica Farewell” wa Don Williams, wimbo wenye ladha ya country na mguso wa kisiwa, unaoelezea mapenzi, kumbukumbu na uchungu wa kuaga ardhi unayoipenda. Safari inaendelea nyumbani Afrika Mashariki kwa kibao cha Kiswahili “Mulofa wangu” cha marehemu Daudi Kabaka kutoka Kenya, wimbo wa mapenzi uliojaa hisia nzito na lugha tamu, unaothibitisha ubora wa muziki wa zamani wa Afrika Mashariki. Tunafunga safari yetu Afrika ya Kati kwa “Le Bon Samaritain” wa gwiji wa rumba Papa Noël kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wimbo unaochanganya ala za gitaa za kipekee na ujumbe wa utu, huruma na kusaidiana katika jamii.
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa ambapo hii leo mada kwa kina inaangazia juhudi za kuwa na nishati safi nchini Tanzania ambapo vijana watazungumzia mradi wao wa kuchakata taka za plastiki na kupata nishati safi ya kupikia. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari ukiangazia wakimbizi wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC, Masuala ya Haki za Binadamu nchini Burundi na Matumaini ya watoto wa Gaza. Mwenyeji wako ni Leah Mushi.
Karibu mmoja kati ya Waustralia wanne hawatafuti msaada wanapopata matatizo ya afya ya akili wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua. Wataalamu wanasema kwamba taarifa zilizotolewa na Gidget Foundation zinaonyesha ukosefu wa kuelewa dalili na ishara, pamoja na unyanyapaa unaoendelea kuhusu suala hili.
Hii leo Jaridani, Anold Kayanda anakupeleka nchini Kenya kusikia usaidizi wa FAO kwenye harakati za kuondokana na njaa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupitia uimarishaji wa sekta ya kilimo. Lakini pia kuna Muhtasari kutoka kwa Leah Mushi akimulika:Baa la Njaa kuthibitishwa huko El Fasher na Kadugli nchini SudanAzimio la Doha lenye lengo la kuimarisha maendeleo ya jamii dunianiKauli ya Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa OCHA akiwa huko Doha, Qatar kufuatia kupitishwa kwa azimio hilo.Na kipengele cha Jifunze Kiswahili leo kinaelezea matumizi ya neno Mhanga na Wahanga.Karibu!
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, leo utasikia mengi ikiwemo mkutano wa kujadili kuhusu tahadhari za mapema unaoenda sambamba na miaka 75 tangu kuanzishwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO. Pia utasikia juhudi za mashirika ya UN kusaidia wananchi huko mashinani na kuboresha maisha yao. UNDP nchini Tanzania na UNMISS huko jimboni Yambui nchini Sudan Kusini. Mtangazaji wako ni Leah Mushi.
Karibu usikilize jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo tunaangazia masuala ya amani pamoja na ushirikiano wa nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea duniani. Pia utasikia habari kutoka mashinani nchini Kenya kuhusu mradi wa UNICEF kwenye kilimo uliowainua kiuchumi vijana. Mtangazaji wako ni Leah Mushi.
Karibu kusikiliza jarida la Habari za Umoja wa Mataifa ambapo leo tunakuletea taarifa kuhusu hali ya hewa na athari za moto wa nyika, tutaelekea Gaza kusikia kutoka kwa mashuhuda wa madhila wayapatayo watoto na wananchi wa Gaza na kisha tutaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanaendesha mafunzo ya usalama barabarani.
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, hii leo utasikia juhudi zinazofanyika kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Kutoka barani Afrika utasikia juhudi za kulinda raia wa Sudan Kusini wanaoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko jimboni Tambura na kutoka nchini Tanzania utasikia msaada kwa wakimbizi walioko magharibi mwa taifa hilo.
Discover more Sincerely Accra!Touchdown Nairobi! Sincerely Accra links up with Tonio Kibz from The Sandwich podcast for a fun conversation on life as a young person in Nairobi vs Accra. Grab a snack, cos you know it's about to be nothing short of a good time! Press play!Opening MusicOshe - Reynolds The Gentleman ft. Fra!Music BridgesMeka Ho Bi Woka Ho Bi - Pure Akan One Bebe - OliveTheBoy Body - Black Sherif Arizona - Cina Soul ft. Mr. Drew EX - AbideenCheat on You - Kidi ft. Gyakie Music CloserMariana - Moffy ft. Notse A GCR Production - Africa's Premiere Podcast Network