Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Bri…
Kwame anafurahia kurudi kwenye kituo cha utafiti ambapo Profesa Omar anamwelezea Natalie kuhusu utafiti wake....
Hatimaye Prosefa Omar aokolewa,watekaji nyara watiwa nguvuni na Kwame apongezwa na kila mtu kwa ushujaa wake wa kufatilia hadi kufanikisha Profesa Omar anapatikana.
Profesa anakutwa hoi,Kwame anawashawishi askari polisi kuwatia nguvuni watekaji kabla hawajatoroka au kuwadhuru.
Kwame na polisi wanakubaliana kumtanguliza Kwame mahali aliposhikiliwa Profesa Omar ili kuhakikisha usalama wake kabla ya kumuokoa na kuwatia nguvuni watekaji nyara...
Safari hii,Polisi wanamzuia Kwame kumpata Profesa Omar akiwa peke yake.Wanampangia njama kali asifanikiwe,lakini anafanikiwa kuwashawishi na kuambatana nao kuelekea katika dimbwi la Garkoe kumwokoa Profesa Omar.....fuatilia
Mambao yamekuwa mambo,Profesa Abubakar na daktarai wabainika kuwa profesa bandia na daktari bandia...fuatilia..
Katika siku ya leo polisi wapata taarifa za madai kutoka kwa watekaji nyara wa Profesa Omar ambao wanadai pesa ili kumwacha huru.Endelea..
Kwamé na Nathalie wanatafuta kufungua jalada ya kompyuta ya mkononi ya Profesa Omar,ili wajue siri iliyopo nyuma ya kutekwa nyara kwa Profesa huyo, je, watafanikiwa? Sikiliza uburudike.
Katika makala haya tutamuona kwame akipata mkanganyiko baada ya kumuona mtu aliyemdhania kuwa ni rafiki wa profesa Omar, je ni nani mtu huyo? na nini kitatokea?fuatilia mchezo huu wa redio kutoka hapa rfi kiswahili.
Endelea kufuatilia mambo anayokumbana nayo Kwame katika harakati za kumwokoa Profesa Omar.
Sehemu ya 12 ya Makala ya Talisman Brise inazungumzia kuhusu ushawishi wa Clement wa Kwame kuelekea Niamey kukutana na Profesa Kouaga
Kwame ampata Profesa Omar na kipande cha herizi yake, na sasa anaamuwa kwenda Niamey
Katika mchezo huu jumapili ya leo Kwame anafikiria kumtumia mganga wa jadi ili kumpata Profesa Omar, fuatilia mchezo huu upate kufahamu mengi kutoka RFI
Clément, mtembezaji wa watalii wa Tondiedo, anaampa maelekezo juu ya tafiti ya profesa na profesa Kouada wanazofanya kwa ajili ya mimea...
Polisi hawatamchukulia Kwame kama gaidi tena
Kule kituoni, polisi wawili wanamuuliza masuali mazito. Ana jaribu kujibu kama anavyowezo. Mwishoni wanamwachia. Wakati anapoondoka anapata habari kuwa wateka nyara wa profesa Omar wanaomba pesa ili wamwachie huru (Sehemu za harakati - maswali)
Kwamé hamuamini mtu na anaamua kupeleleza mwenyewe. Lakini anakamatwa na polisi ambao wanampeleka kituoni. Haelewi vizuri wanamtakia nini na anaishia mahabusu. Nathalie anamkana...(Sehemu za harakati - kufungwa)
Katika muendelezo wa mchezo huu Kwame bado anaendelea na jitihada za kubaini wapi alipo Profesa Omar,ambapo leo anakutana na askari kujua nini kitajiri fuatilia mchezo huu.
Kwame bado anaendelea na jitihada zake za kumtafuta Proffesa Omar huko Tondiedo, Je atafanikiwa kumpata? fuatilia makala haya .
Kule Tondiedo, Kwamé anakutana na Clément, mtembezaji wa watalii na mwanafunzi Chuo Kikuu cha Niamey. Anamjua Profesa Omar. Hii inaweza kuwa sehemu ya kuanzia...Jioni kwenye mgahawa, anasikia sauti ambayo si ya kawaida inayomfuata...halafu kule redioni wanazungumzia kutekwa nyara kwa Professa na GIETA, shirika lisilo la serekali linalo dhamini tafiti za profesa. Kwamé, hawaamini.
Baada ya kutekwa nyara kwa Profesa Omar, Kwamé anaamua kwenda Tondiedo kwa ajili ya kupata faharasa. Lakini pikipiki inaharibika, halafu, mtu wa ajabu ambaye anadhani anamfahamu anamzuia...
Kwamé, mtunza bustani kwenye kituo cha utafiti wa kilimo, Gorom Gorom, anahadithia hadithi yake kwa shangazi yake: Huku akiwa anafanya kazi kwenye bustani, bosi wake, Profesa Omar anatekwa nyara huku yeye akishuhudia...(Sehemu za harakati - uhoga).