POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD. Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za hatua za kupambana na UKIMWI, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hasa kwa watoto DRC, na ujumbe katika siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lililo lujani ni la lusu”.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni kuboresha zao hilo na kuinua pato la mkulima.Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Lebanon amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa mapema leo Alhamisi baada ya makombora ya mizinga kulenga eneo lao la kazi karibu na Marjayoun kusini mashariki mwa nchi hiyo, imesema taarifa ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo muda wowote kuanzia sasa.Shirika la Umja wa Mataifa la afya Duniani, WHO, limesema chakula kisicho salama kinaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma duniani, kikisababisha takribani wagonjwa milioni 866 na vifo milioni 1.5 kila mwaka, huku watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari kubwa zaidi. Kwa mujibu wa ripoti mpya watoto hao wadogo, ambao ni asilimia 9 tu ya idadi ya watu duniani, wanachangia karibu theluthi moja ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula.Leo ni siku ya watoto wasio na hatia waathirika wa ukatili duniani, maadhimisho haya yanakuja wakati ambapo ripoti ya Mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Migogoro ya Silaha inaonesha kwamba ukatili dhidi ya watoto katika migogoro ya silaha ulifikia viwango visivyo vya kawaida mwaka 2024, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 25 la ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikilinganishwa na mwaka uliopita.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi.Hadi sasa Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewasili Bunia, mashariki mwa DRC, ndani ya siku nne kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya maabara, PPE na mahema ya kuhudumia wagonjwa. Wakati huo huo MONUSCO inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu njia za kujikinga, huku WHO ikisema zaidi ya watu 600 wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa tangu mlipuko huo kuanza.Tukisalia na Ebola, Ili vifaa vya Ebola vifike kwa wakati, wako mashujaa nyuma ya pazia wanaohakikisha kila mzigo unasafiri salama. Miongoni mwao ni Milton Oloo, mwenye miaka 30 ya uzoefu wa kupakia mizigo JKIA nchini Kenya, ambaye sasa yuko mstari wa mbele kusaidia safari za ndege za Umoja wa Mataifa, UNHAS. “Tunachokifanya hapa leo ni kuhakikisha kwamba mizigo inayoelekea Congo DRC imepangwa vizuri na kupakiwa ipasavyo ili isiharibike. Pia naona fahari na Maisha ya watu yanayookolewa nafurahi”.Na jukwaa la 13 la miji dunini WUF13 linaelekea ukingoni Baku Azerbaijan likijadili changamoto ya makazi duniani, Rehema Kishoa kutoka Tanzania Mkurugenzi Msaidizi wa Uzingatiaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi anasema wao wamechukua hatua kukabili changamoto hiyo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”
Karibu usikilize Ujumbe wa Biblia. Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino-SAUT,Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. Mada ni Maadaui wanne wa mwanadamu Tarehe 02 Machi 2026 L'articolo Fahamu faida za kanunia ya imani proviene da Radio Maria.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU”
Katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kupata ujumbe wa Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana amabye kwa kuwa mwaka huu 2026 ameshiriki tena katika mkutano wa CSW70 anatueleza ni kwa kiasi gani wameweza kulitekeleza malengo ya mikutano haya katika nchini humo.Vita Mashariki ya Kati vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia mwezi wa pili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hapa makao makuu ya UN jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari akisisitiza sio tu vita hivyo vikome bali pia anaendeleza diplomasia za kusaka suluhu. Guterres amesema, Ninamtuma Mjumbe wangu Maalum Jean Arnault. Lengo ni kuunga mkono jitihada za kikanda. Lazima tupate njia ya amani ya kutoka katika hali hii. Ujumbe wangu uko wazi. Kwa Marekani na Israeli, ni wakati muafaka kusitisha vita vinavyosababisha mateso makubwa ya kibinadamu na tayari vinaanzisha athari mbaya za kiuchumi. Kwa Iran, isitishe kushambulia majirani zake.. Ripoti mpya ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika, (ECA) imependekeza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa deni la umma barani Afrika, ikionya kwamba uendelevu hautegemei tu kiwango cha kukopa bali pia ubora wa taasisi, mifumo ya kisheria, na uwazi. Ikitolewa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, ripoti hiyo inataja udhaifu kama vile uwezo mdogo wa kufanya uchambuzi wa hatari, na ushawishi wa mashinikizo ya kisiasa katika maamuzi ya kukopa ikisema kuwa kuboresha usimamizi ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa deni la umma linachangia ukuaji wa uchumi endelevu badala ya kuwa chanzo cha kuyumba kifedha.Wakati dunia hii leo ikiadhimisha Siku ya Uelewa wa Usonji, familia katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka katika kuwahudumia watoto usonji katikati ya mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu. Katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Jiji la Gaza, Layan Abu Qousa mwenye umri wa miaka 16, ambaye ana usonji, anaishi na familia yake katika magofu ya nyumba yao. Familia yake inasema hali ngumu ya maisha imeongeza changamoto zinazohusiana na hali yake, huku ukosefu wa utulivu na mkwamo wa kupata huduma za kitaalamu ukiendelea kudhoofisha ustawi wake.Na katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Ateteaye mtuku ni tanguko la bure."Dkt. Gitonga anasema, "Mtuku ni mtu asiyefaa au asiyeweza kutegemeeka. Methali hii ina maana kwamba mtu asiyetegemeeka kamwe katika jamii na ambaye hana utu, kumtetea ni kujidhalilisha wewe mwenyewe. Ni kazi bure isiyo na faida. Ukimtetea apate labda cheo au kazi fulani utajilaumu mwenyewe kwani hatawajibika hata kamwe. Inatuelimisha kwamba iwapo utakuwa radhi kumtetea mtuku basi kuwa tayari kuhusishwa naye. Tetea walio wema si waovu."
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania ambako UNHCR inasema ufadhili endelevu na wa uhakika unahitajka ili kuendeleza ulinzi wa wakimbizi na kusaidia urejeaji na ujumuishaji wa raia wanaorudi nchini Burundi. Pia tunakuletea jifunze Kiswahili.Ushirikiano wa kimataifa kupitia mikataba ya kimataifa ya kudhibiti dawa umesaidia watu duniani kote, imesema hii leo Bodi ya Kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya, INCB wakati ikizindua ripoti ya mwaka 2025 kuhusu hali yad awa za kulevya duniani.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu wamelaani vikali ukatili unaodaiwa kufanywa na kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, dhidi ya watetezi wa haki za binadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Na leo ikiwa ni siku ya tatu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague Uholanzi kuthibitisha iwapo kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakamani Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusianana kile kilichoitwa “vita dhidi ya dawa za kulevya” nchini mwake, wakili upande wa utetezi, Nicholas Kaufmann amesema hakuna uhusiano uliothibitishwa kati ya hotuba zake za “kipekee, zenye kauli kali” na mauaji anayotuhumiwa kuyafanya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ANUIAYE KUKUTUKANA HAKOSI MATANGO”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ANUIAYE KUKUTUKANA HAKOSI MATANGO”
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimsikia Barbara Batte Guevara, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Havana nchini Cuba. Kwa kushirikiana na Tanzania chuo hicho ambacho mwezi uliopita kimetimiza miaka 298 tangu kuanzishwa kwake, hivi karibuni kimetoa fursa kwa Wacuba kujifunza lugha ya Kiswahili.Anold Kayanda wa Idhaa hii amemtembelea Profesa Barbara Batte katika jiji la Havana nchini Cuba ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kama zifuatazo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Kimataifa wa Akili Mnemba au AI wenye thamani ya dola bilioni 3, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inawanufaisha watu wote duniani, badala ya kuwa mali ya mataifa machache au kampuni chache zenye nguvu. Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa kujadili Athari za AI huko New Delhi nchini India, Guterres amesema mustakabali wa AI unapaswa kujengwa kwa ushirikiano wa kimataifa”.Mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi ambayo inakalia kimabavu yanatia hofu ya uwezekano wa utokomezaji wa kabila, imesema Ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR), ya kuanzia Novemba 1 2024 hadi Desemba 31 2025. Ripoti inasema mashambulizi ya Israeli yameweka mazingira ambamo kwamo wapalestina kama kundi watashindwa kuendelea kuishi Gaza huku Ajith Sunghay, Mkuu wa Ofisi ya OHCHR Palestina akisema, “ripoti inachambua mwenendo wa mapigano ya jeshi la Israeli, linaloendelea kuua idadi kubwa ya raia, kusababisha njaa, kuwahamisha takribani wakazi wote wa Gaza, tena zaidi ya mara moja — na kuharibu miundombinu iliyosalia ya kiraia ya Gaza.”wanamgambo wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan walitekeleza kampeni iliyoratibiwa ya uharibifu dhidi ya jamii zisizo za kiarabu ndani ya mji wa El-Fasher na viunga vyake, kampeni yenye viashiria vya mauaji ya kimbari, imeeleza ripoti mpya iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan. Ripoti imetaja vitendo hivyo ni pamoja na kuua wanachama wa kundi la kikabila linalolindwa; kusababisha madhara makubwa ya kimwili na kiakili; ambavyo ni vipengele muhimu vya kosa la mauaji ya kimbari chini ya sheria za kimataifa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunawasikiliza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Havana wanaojifunza lughaya Kiswahili. Tuanze na Yibran Nunez Batte.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Karibu uungane nami Martin Joseph, katika kipindi cha Tumsifu Maria, MMuwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya Majina mengine ya Mama Maria. L'articolo Mfahamu Bikiria Maria Mama wa huruma. proviene da Radio Maria.
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni Wakatoliki wanasemaje juu ya ndoto? L'articolo Je Wakatiliki wanasemaje kuhusu ndoto ? proviene da Radio Maria.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Atokeapo mtoto wa fuko mshike japo wawinda fuko.”
Hii leo jaridani Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Wakili Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kutoka Tanzania aliyehudhuria Mkutano wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii (CSocD64).Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakumba watoto nchini Sudan. Mashirika hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu wamenasema ghasia zisizoisha, njaa na magonjwa vinawasababisha watoto kupoteza Maisha na kudhoofika, huku mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na vikwazo vya upatikanaji wa misaada vikizorotesha juhudi za kuwaokoa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa UNICEF, Ricardo Pires, amesema “Katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Darfur Kaskazini, zaidi ya nusu ya watoto wote wanakabiliwa na utapiamlo mkali, si makadirio, si mfano, imethibitishwa.”.Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania TANZBAT 12 kinachohusumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kimeendelea kudumisha uhusiano wa kijamii na wakazi wa mji wa Beni Mashariki mwa DRC, kwa kutoa msaada wa vifaa vya elimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Ngite iliyopo eneo la Mavivi. Mkuu wa shule hiyo Neema Nyamwaka amewashukuru walinada amani hao kutoka Tanzania kwa kujali sekta ya elimu.Leo ni siku ya mikunde duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO likisistiza umuhimu kwa chakula hicho kwa lishe na mazingira. Huko Kigoma Tanzania FAO kupitia mpango wa Pamoja wa KJP imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima kuhusu umuhimu wa mazao ya jamii ya mikunde huyu ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Atokeapo mtoto wa fuko mshike japo wawinda fuko.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni kwanini Mkatoliki akihamia katika ulokole anakuwa makaidi na mbishi? L'articolo Tufanye nini tunapokutana na watu wanaobishana kuhusu ukatoliki? proviene da Radio Maria.
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni Je Mapdre wa Kanisa Katoliki wanaruhusiwa kutoa pepo? L'articolo Je Mapdre wa Kanisa Katoliki wanaruhusiwa kutoa pepo? proviene da Radio Maria.
Ungana nami Mtangazaji wako Catherine Kaberege katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni Je Mapdre wa Kanisa Katoliki wanaruhusiwa […] L'articolo Siyo kila Padre au Mlei anaruhusiwa kutoa mapepo bali wale wenye kibali maalum proviene da Radio Maria.
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni kwanini Mkatoliki akihamia katika ulokole anakuwa makaidi na mbishi? L'articolo Ijue sababu ya ubishe kwa wale wanaohasi ukatoliki. proviene da Radio Maria.
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni Wakatoliki wanasemaje juu ya kula nguruwe, kunywa pombe na kunywa damu za wanyama wakati imekatazwa kwenye Biblia? L'articolo Wakatoliki wanasemaje juu ya kula Nguruwe, kunywa pombe na kunywa damu za wanyama? proviene da Radio Maria.
Nchini Vietnam taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona anajitahidi kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano licha ya vikwazo anavyokumbana navyo kila uchao, na hii ni kwa sababu si kwamba njia ni rahisi bali kwa sababu dhamira yake ni kubwa zaidi. Assumpta Massoi anasimulia zaidi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO.
Hii leo jaridani tunaangazia walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona nchini Vietnam, na harakati za kutokomeza ukeketaji nchini Kenya.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) umetoa taarifa kwamba umefahamishwa na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa kuwa Afrika Kusini itaondoa vikosi na wanajeshi wake waliobaki ndani ya MONUSCO. Ninamualika Rashid Malekela aliyeifuatilia kwa kina taarifa hiyo ili atueleza zaidi.Nchini Vietnam taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona anajitahidi kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano licha ya vikwazo anavyokumbana navyo kila uchao, na hii ni kwa sababu si kwamba njia ni rahisi bali kwa sababu dhamira yake ni kubwa zaidi.Ukeketaji au FGM ni jinamizi linalowaandama waathirika maisha yao yote likisababisha changamoto sio tu za kimwili lakini pia za kiafya na kuwaacha na makovu yasiyofutika. Katika Kaunti ya Tana River Kusini Mashariki mwa Kenya tunakutana na manusura na shujaa mwanaharakati wa kupambana na mila hiyo potofu ya ukeketaji Saadia Hussein, raia wa Somalia anayeishi Kenya hivi sasa. Mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Brighter Society Initiative anatusimulia safari yake ya machungu ya ukeketaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Karibu uungane na Padre Titus Amigu, Mtalaam wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia akiendelea kujibu Maswali ya Msikilizaji na moja ya Maswali hayo ni kwanini Mkatoliki akihamia katika ulokole anakuwa makaidi na mbishi? L'articolo Je, ni kweli mtu akitoka katika Kanisa Katoliki na kwenda katika Madhehebu mengine anakuwa mbishi na mkaidi? proviene da Radio Maria.
Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na mmomonyoko wa udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU kimetoa ripoti inayotangaza kuingia katika“zama za kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kulikoni ? Flora Nducha anaeleza kwa kina ripoti hiyo.
Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji, ripoti inayomulika kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, na mradi unaolenga kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.Kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji kutokana na mvua zinazoendelea, serikali ya nchi hiyo ya kusinimashariki mwa Afrika imetangaza kuwa hadi kufikia sasa imerekodi vifo vya watu 120 na maelfu ya nyumba zimeharibiwa huku kiwango kikubwa cha fecha kikihitajika.Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU leo kimetoa ripoti ikitangaza kuingia kwa “enzi ya kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Utafiti mpya umebaini kuwa miti kote Australia inakufa kwa kasi zaidi kuliko inavyokua, hali ambayo inachangia ongezeko la utoaji wa kaboni. Utafiti huo, unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Western Sydney na kuchapishwa katika jarida la Nature Plants, umebaini kuwa miti katika aina zote za mifumo ya mazingira - kuanzia misitu ya mvua ya tropiki hadi misitu ya eucalypt - inapungua hali ya hewa inavyozidi kuwa ya joto.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia mradi wa kilimo cha mpunga ulivyoleta ustawi kwa jamii ya katikati mwa Sudan unaofanikishwa kwa msaada wa mafunzo wa walinda amani wa UN kutoka Korea Kusini wanaohudumu katika UNMISS kupitia wanasayansi na wakulima wa eneo la Bor katika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Mapigano makali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha watu zaidi ya 200,000, na kusitisha msaada wa chakula kwa maelfu. Umoja wa Mataifa unasema hali katika Kivu Kusini imezorota kwa kasi, huku msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP ukisimama na shule zaidi ya 30 zikigeuzwa makazi ya dharura. Katika taarifa yake, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema hali imefikia kiwango cha hatari, akionya: “Familia zinazoishi kwa njaa sasa zinagawana chakula chao cha mwisho na watu waliokimbia makazi. Hii ni dharura inayovuka mipaka.” UN inazitaka pande zote kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu misaada kufika kwa walio hatarini.Mkutano wa kikao cha 7 wa Baraza La Mazingira la Umoja wa Mataifa UNE-7 unaeelekea ukingoni jijini Nairobi Kenya na miongoni mwa washiriki ni kijana mwanaharakati wa mazingira kutoka asasi ya Umoja wa Mataifa YUNA nchini Tanzania Ally MwamzoraNa leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Milima, ukisisitiza umuhimu wa milima kama “kitovu cha maji ya dunia.” Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, takriban asilimia 70 ya maji safi ya Dunia yamehifadhiwa kama theluji au barafu, yakitoa mito inayosambaza maji ya kunywa, kilimo, viwanda, na umeme wa maji na takriban watu bilioni mbili, ikiwa ni pamoja na jamii nyingi za asili, wanategemea maji ya milima kwa mahitaji yao ya kila siku, maisha, na tamaduni zao. Wataalamu wanasisitiza kuwa kulinda mazingira ya milima ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa vizazi vijavyo.Katika kujifunza lugha Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "“MWENDAWAZIMU HAPEWI UPANGA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "“MWENDAWAZIMU HAPEWI UPANGA"
Hii leo jaridani tukiendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu siku 16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, leo tunaelekea Mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusikia hisia za wanawake kuhusu ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.Watu takribani 100,000 wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR likionya kuwa mashambulizi yanaongezeka na kuyakumba hata maeneo yaliyokuwa salama. Mwakilishi wa UNHCR, Xavier Creach, amesema mgogoro “unazidi kuzorota kwa kasi ya kutisha” huku familia zikikimbia usiku gizani wakati watu wenye silaha wakivamia vijiji vyao. UNHCR inasema linahitaji dola milioni 38.2 kukidhi mahitaji yanayoongezeka.Kaskazini mwa Asia, dhoruba za kitropiki na mvua zisizo za kawaida zimesababisha vifo vya mamia na watu wengi kukimbia makazi yao, imesema WMO. Clare Nullis, msemaji wa shirika hilo, alisema Indonesia, Ufilipino, Sri Lanka, Thailand na Vietnam ndizo zimeathirika zaidi. “Tunahitaji kuzingatia kuwa Asia iko hatarini sana kutokana na mafuriko,” amesema Nullis, akibainisha kuwa dhoruba karibu na Ekweta ni nadra na jamii hazina uzoefu wa kukabiliana nazo. Indonesia pekee, watu 604 wamefariki, 464 hawajulikani walipo, na 2,600 wamejeruhiwa, huku zaidi ya milioni 1.5 wakiathirika na 570,000 wakikimbia makazi yao.Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumwa leo Desemba 2 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani ILO limeonya kuhusu kuongezeka kwa utumwa wa kisasa wa binadamu, likionesha kuwa watu milioni 10 zaidi walikuwa wakiishi katika kazi za kulazimisha au ndoa za shuruti mwaka 2021 ikilinganishwa na mwaka 2016. Makadirio haya mapya yanaweka idadi ya walioathirika duniani kote kuwa watu milioni 50 huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wenye hatari kubwa zaidi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Daktari. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "CHA KIPOFU KI MKONONI MWAKE"
Leo mchambuzi ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya posta Duniani na tunakupeleka nchini Tanzania ambako huko Sabrina Said wa idhaa hii amefuatilia harakati za huduma hiyo kwenye shirika la Posta Tanzania lililoanzishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1993 na kuanza kutoa huduma Januari 1994.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha tangazo la makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka wote huko Gaza lililotolewa na Rais wa Marekani , akiyaita makubaliano hayo ni mafanikio yaliyohitajika sana baada ya miaka ya mzozo..Licha ya mzozo unaoendelea na changamoto za miundombinu nchini Sudan, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF leo limesema limefanikiwa kutoa chanjo kwa zaidi ya watoto 740,000 walio chini ya umri wa miaka mitano kati ya Januari na Juni 2025, na kutoa dozi zaidi ya milioni 16.Katika Siku ya Posta Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewashukuru wafanyakazi milioni 4.6 wa posta wanaounganisha jamii kote duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "FUNDI HANA CHOMBO"Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "FUNDI HANA CHOMBO"
Jaridani leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake na utamsikia maoni ya Balozi Gertrude Mongella kutoka Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza Jumatatu ijayo, Rais wa Mkutano huo Annalena Baerbock amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa “jukumu letu ni Umoja wa Mataifa uwe thabiti kwa miaka 80 ijayo. Michakato ya kuhakikisha hilo ndio itakuwa jukumu letu mwaka huu, ikiwemo kusongesha ajenda ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tukitaka Umoja wa Mataifa thabiti, basi tunahitaji ahadi kutoka serikali zote duniani.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotolewa kila mwaka kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu inasema Umoja wa Mataifa umeendelea kusimama imara, ukifanya kazi ya kuendeleza amani, kuchochea maendeleo endelevu, na kupunguza mateso ya kibinadamu licha ya majaribu makubwa. Katika ripoti hiyo Antonio Guterres amesisitiza uimara wa watumishi wa Umoja wa Mataifa, ambao wamejitolea kuleta matumaini na msaada kwa wale wanaohitaji licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.ripoti ya Hali ya Rasilimali za Maji Duniani iliyotolewa leo inasema ni takriban theluthi moja tu ya mabonde ya mito duniani yaliyokuwa na hali ya “kawaida” mwaka 2024 ilhali mengine yote yalikuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji au chini ya kiwango cha kawaida — ikiwa ni mwaka wa sita mfululizo wa kutokuwepo kwa uwiano wa wazi. Ikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO, ripoti inasema mwaka 2024 uliokuwa mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa ulianza na tukio la El Niño ambalo liliathiri vibaya mabonde makubwa ya mito na kusababisha ukame katika maeneo kadhaa ikiwemo kusini mwa Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"
Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu, Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT lataka wakusanyaji na wachakataji wa taka watambuliwe kwani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha mazingira safi na salama mijini-Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza Papua New Guinea kwa kuwa kisima cha kuvuna hewa ukaa na kuzitaka nchi za G-20 kuwajibika katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi-Nchini Mali, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya juu ya kuzorota zaidi kwa hali ya haki za binadamu. -Na leo katika jifunze Kiswahili Je wafahamu maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"? basi msikilize mtaalam wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani
Leo katika jifinze Kiswahili mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"
Jaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpango mpya wa kuonesha faida za nchi hizo kwa muunganiko wao kwa njia ya ardhi amesema…. hii leo LLDCs zinatumia vema uwepo wao kimkakati, katikati ya Afrika na muunganiko wa kikanda kuwa vitovu muhimu vya kuunganisha nchi kiuchumi , biashara na ubunifu. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu leo wamesema ili kuzuia vifo zaidi na mateso kutokana na njaa huko Gaza, Israel inapaswa kurejesha mara moja ruhusa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu kuingia bila vikwazo vyovyote eneo la Palestina inalokalia kimabavu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."
Hii leo jaridani utasikia muhtasari wa habari utakaoangazia hali ya uhaba wa chakula Gaza, mkutano wa maspika wa bunge duniani na mkutano wa tabianchi na afya. Katika jarida pia utasikia mada kwa kina inayoangazia siku ya kimataifa ya marafiki duniani ambayo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2011 ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Julai. Vijana kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino nchini Tanzania - SAUT wanajadili umuhimu wa siku hii.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika utapiamlo kwa watoto na madhila yasiyo fikirika kwa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Kati, Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli. Pata pia muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana jinsi mitandao ya kihalifu duniani inavyoingiza kwenye masoko dawa za binadamu zenye viwango vya juu vya kemikali za sumu ambazo zimesababisha vifo na kuathiri afya ya wagonjwa wengi hasa watoto kwenye nchi za kipato cha chini.Tunasalia na afya ambapo hii leo WHO imethibitisha kwamba Timor-Leste imetokomeza ugonjwa wa malaria, hatua ya kipekee kwa nchi ambayo ilipatia kipaumbele malaria na kuanzisha juhudi za kitaifa na zilizoratibiwa mara tu baada ya kupata uhuru wake mwaka 2002. Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Volker Türk, amesema maoni ya ushauri yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi ni ushindi mkubwa kwa wote wanaopigania kulinda hali salama ya tabianchi na sayari kwa ajili ya binadamu wote. Halikadhalika ni uthibitisho usio na shaka kuhusu madhara mapana ya mabadiliko ya tabianchi na wajibu mkubwa wa Mataifa, chini ya sheria za haki za binadamu na zaidi ya hapo, kuchukua hatua za haraka ili kuzuia uharibifu.Na katika kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali "UKIONA KIVULI CHA MTU MFUPI KIMEANZA KUREFUKA JUA KUMEKUCHA AU NI MACHWEO."