Podcasts about hatimaye

  • 12PODCASTS
  • 34EPISODES
  • 12mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • May 5, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about hatimaye

Latest podcast episodes about hatimaye

Habari za UN
VoTAN sio tu mtandao wa kidijitali kusaidia manusura wa ugaidi bali pia ni familia - Manusura

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 5:02


Hatimaye kilio cha manusura wa ugaidi duniani cha kuwa na Mtandao wa Mashirika yao ili kuweza kupaza zaidi sauti zao kwa ajili ya sio tu kusaidiwa bali pia kuepusha matukio kama hayo, kimepata jawabu baada ya Mtandao huo au VoTAN kuzinduliwa kwenye Umoja wa Mataifa. Kwa msaada wa kifedha kutoka Hispania, Iraq na nchi nyingine wanachama, mtandao huu ulio chini ya Programu ya kusaidia manusura wa ugaidi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabilana na Ugaidi, UNOCT, unatarajiwa kuziba mapengo ya msaada na kuinua ushuhuda wa manusuta kutoka maeneo yaliyopuuzwa duniani. Assumpta Massoi amefuatilia uzinduzi huo na kuandaa makala hii.

Habari za UN
Ukraine: Mwakilishi wa UNFPA Ukraine Uller Muller na hali ya wanawake wajawazito nchini humo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 7, 2025 1:49


Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Ni Ulla Muller, Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini Ukraine, akieleza kuhusu changamoto zinazowakumba wanawake wajawazito wa Ukraine.Anasema, “ninaweza kukuambia hadithi nyingi ambazo zimebaki nami kwa sababu nakutana na wanawake hawa kila mara, na mapenzi yangu kwao hayana mipaka.”Uller Muller anasimulia kisa cha mwanamke mmoja akisema,"Kuna mwanamke anayeitwa Ira ana umri wa miaka 31, na tayari anamlea mtoto mvulana wa umri wa miaka sita. Hivi karibuni aligundua kuwa ni mjamzito tena na anatarajia mapacha watatu. Ni hali ya kutisha na kuchanganya."Bi. Muller anaendelea kueleza kuwa mwanamke huyo alikuwa njiapanda asijue abaki alee ujauzito katika hali hiyo ya mabomu kila mahali au andoke? Hatimaye aliamua kubaki na kwa usaidizi wa UNFPA akafanikiwa kujifungua lakini kabla ya wakati. Uller Muller, anaitathimini hali hiyo akisema,"Faraja yake ya kuweza kujifungua salama iliakisi uthabiti wa akina mama wengi wa Kiukraine ambao wanaamua kutoondoka. Wanaamua kuwa bado wanapaswa kujenga mustakabali wa maisha yao. Bado wanapaswa kuishi maisha yaliyo karibu na hali ya kawaida kadri wawezavyo. Na hilo linajumuisha kuleta uhai katika hali ya vita."

Habari za UN
Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 3:25


Kama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibindoni ujuzi wake mwingine. Ujuzi binafsi, ufundi wa kushona nguo.Celestin sasa anafundisha wanawake wadogo shughuli za kushona nguo.Hatimaye mwaka jana, 2024, kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali (RPL), uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO utaalamu wake wa kushona nguo ambao haukuwa na cheti, ukathibitishwa rasmi na akapata cheti, hali ambayo imemfungulia milango ya kuomba ajira rasmi.

Habari za UN
Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 2:01


Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto.  Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa  mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo  jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho  ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza  niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia changamoto zinazowazuia watoto wenye ulemavu na familia zao kupokea msaada muhimu wanaohitaji wakati wa majanga na dharura.Akiwa mwingi wa furaha, Eric anasema, “imechukua muda wa miaka sita ambapo nimekuwa nikizunguka tu kuhusu miwani. Mahali nilipoenda hapo awali, niliambiwa kulipia shilingi elfu arobaini ($313) lakini sikuweza kupata hiyo pesa. Nimefurahi kwamba leo nimepewa bila gharama yoyote.”Baada ya uchunguzi na mawaidha mbalimbali katika hii kambi, Eric na mwanaye Candy hawakuweza kuificha furaha yao kwa kupata suluhisho la tatizo ambalo limewaathiri kwa miaka sita.Hatimaye, Candy alipewa miwani yake maalum ili kumsaidia kuona vizuri zaidi.“Nimefurahia sana sina jukumu tena la  kutafuta pesa za kununua miwani. Na nimefurahi pia mtoto wangu atakuwa na wakati rahisi. Amefurahia kabisa na anaipenda sana miwani yake. Amesema anajihisi vizuri. Kwa sababu ana miwani, natumaini anaweza kucheza bila shida yoyote, bila kujali kuhusu jua kwa sababu miwani inamkinga.”

Habari za UN
26 AGOSTI 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 26, 2024 9:43


Hii leo jaridani tunamulika kupelekwa kwa chanjo dhidi ya polio huko Gaza; mkimbizi wa Burundi aliyerejea nyumbani kutoka Tanzania ainuliwa kiuchumi; makala ni mkimbizi wa Sudan aliyeko ugenini naye awezeshwa kijasiriamali na mashinani tunabisha hodi nchini Rwanda kumulika usawa wa kijinsia kwenye michezo.Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Kwa wakimbizi, kurejea nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha waliorejea nyumbani kujijenga upya na kwa tija. Miongoni mwao ni Emelyne Kabura kama anavyosimulia Bosco CosmasKatika makala Evarist Mapesa anatuletea simulizi ya mkimbizi wa Sudan ambaye sasa anaishi Sudan Kusini. Baada ya kupitia madhila lukuki amewezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na sasa anajishughulisha na ujasiriamali.Na sasa ni mashinani  Christelle Umuhoza, Mkurugenzi wa Programu wa Rwanda katika shirika la Shooting Touch, kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO nchini humo, anaeleza umuhimu wa michezo katika kuondoa vikwazo vya kijinsia.

Habari za UN
Dozi za chanjo dhidi ya polio zapelekwa Gaza - UNICEF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 26, 2024 1:22


Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, UNICEF inasema dozi hizo milioni 1.2 za chanjo dhidi ya polio zitatumiwa kwa watoto zaidi ya 640,000.Chanjo hizo zinapelekwa wakati wiki iliyopita shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO lilithibitisha kuwa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 10 huko  Deir al-Balah aliugua polio hiyo aina ya 2 na amepooza sehemu ya chini ya mguu wake. Ingawa hivyo hivi sasa hali yake inaendelea vizuri.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, nalo kupitia mtandao wa X linasema kwa kuzingatia hatari kubwa ya kusambaa kwa ugonjwa huo hatari huko Gaza kutokana na ukosefu wa huduma za kujisafi na maji safi, kwa kushirikiana na UNICEF na WHO siku zijazo watazindua kampeni ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya laki sita wenye umri wa chini ya miaka 10.Kwa mujibu wa UNRWA, operesheni za jeshi la Israeli huko Deir Al Balah zimeharibu miundombini ya maji na kwamba ni visima vya maji 3 tu kati ya 18 ndio vinafanya kazi na kwa mantiki hiyo uhaba wa maji ni asilimia 85. 

Alfajiri - Voice of America
Hatimaye Hungary yaidhinisha Sweden kujiunga na NATO - Februari 27, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 27, 2024 29:59


Sweden inatarajiwa kujiunga rasmi na NATO katika siku au wiki zijazo, baada ya Hungary hatimaye kutoa idhini yake siku ya Jumatatu – mwanachama wa mwisho kufanya hivyo.

Habari za UN
25 JULAI 2023

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 25, 2023 0:11


Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Burundi wanaopata hifadhi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamepata matumaini mapya ya maisha baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika lisilo la kiserikali ya AIDES kuwawezesha kuanzisha mradi wa kazi za Sanaa ambao unawasidia kujikimu kimaisha pamoja na familia zao. Ashinani tutaelekea Bahari ya Shamu au Red Sea, kulikoni? Hatimaye operesheni kubwa imeanza leo huko Yemen ya kupakua mapipa ya mafuta ghafi kutoka meli ya FSO Safer iliyoanza kuoza kwenda meli ya  Nautica au Yemen katika pwani  ya bahari ya Shamu.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia watu kuzama majini, shirika la Umoja wa MAtaifa la chakula na kilimo, FAO limesema linatumia siku hii kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kuelimisha umma juu ya kuzama majini hasa katika sekta ya uvuvi.Nchini Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linaendesha semina kuhusu ukatili wa kijinsia na kingono ili kusaidia manusura ambao wanakabiliwa na vitendo hivyo wakati wakirejea nyumbani kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan.Mashinani tutamsikia Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNEP hatua iliyoanza asubuhi ya leo kwa saa za Yemen ya kuhamisha mafuta yaliyokuwa yanahatarisha usalama kwenye Bahari ya Shamu au Red Sea.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
UNICEF linahofia kwamba zaidi ya watoto 11,000 wameuawa au kujeruhiwa Yemen

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 12, 2022 0:03


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto zaidi ya 11,000 nchini Yemn wameuawa au kujeruhiwa hadi kufikia sasa ikiwa ni sawa na wastani wa watoto 4 kwa siku tangu kushika kasi kwa machafuko nchini humo mwaka 2015. Shirika hilo limesema linahofia kwamba idadi kamili ni kubwa zaidi kwani hizi ni takwimu tu za matukio yaliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa.Kwa mujibu wa UNICEF wakati usuluhishi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa ulisaidia kupungua kwa kasi kwa mzozo huo, watoto wengine 62 wameuawa au kujeruhiwa kati ya mwisho wa kumalizika kwa makubaliano ya usitishaji uhasama mwanzoni mwa mwezi Oktoba na mwisho wa Novemba.  Takriban watoto 74 walikuwa miongoni mwa watu 164 waliouawa au kujeruhiwa na mabomu ya kutegwa ardhini na risasi zisizolipuka kati ya mwezi Julai na Septemba 2022 pekee. Takriban miaka minane tangu kuongezeka kwa mzozo huo Yemen UNICEF inasema zaidi ya watu milioni 23.4, wakiwemo watoto milioni 12.9, wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi ikiwa ni sawa na karibu robo tatu ya wakazi wote wa taifa hilo.  Shirika hilo limeongeza kuwa  watoto wapatao milioni 2.2 nchini Yemen wana utapiamlo mkali, wakiwemo karibu watoto 540,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wanaokabiliwa na unyafuzi na wanahaha kuishi. Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Catherine Russell, ambaye alizindua ombi la hatua za kibinadamu kwa ajili ya watoto akiwa Yemen wiki iliyopita amesema  "Ili watoto wa Yemen waweze kuwa na nafasi yoyote ya mustakabali mzuri, basi wahusika katika mzozo, jumuiya ya kimataifa na wale wote wenye ushawishi lazima wahakikishe wanalindwa na kuungwa mkono. Hiyo inajumuisha watoto kama Mansour, ambaye nilikutana naye katika kituo cha urekebishaji na viungo bandia kinachoungwa mkono na UNICEF. Mguu wake ulikatwa kwenye goti baada ya kupigwa risasi. Hakuna mtoto anayepaswa kuteseka hivyo. Urejeaji upya na wa haraka wa usitishaji vita itakuwa hatua chanya ya kwanza ambayo ingeruhusu ufikiaji muhimu wa msaada wa kibinadamu. Hatimaye, ni amani endelevu pekee ndioyo itaruhusu familia kujenga upya maisha yao yaliyosambaratika na kuanza kujipanga kwa ajili ya siku zijazo.” Takwimu za UNICEF zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 17.8, wakiwemo watoto milioni 9.2, wanakosa huduma za maji salama, usafi wa mazingira na kujiusafi (WASH).  Na zaidi ya hapo shirika hilo la kuhudumia watoto limesema kwa miaka mingi, mfumo wa afya nchini humo umekuwa dhaifu sana, ni asilimia 50 tu ya vituo vya afya ndivyo vinavyofanya kazi, na kuwaacha karibu watu milioni 22 ikiwa ni pamoja na karibu watoto milioni 10 bila upatikanaji wa kutosha wa huduma za afya. Kwa mujibu wa UNICEF utoaji wa chanjo umedorora kitaifa, huku asilimia 28 ya watoto walio chini ya mwaka 1 wakikosa chanjo za kawaida.  Sambamba na ukosefu wa maji salama, na hii inawaweka watoto katika hatari kubwa huku kukiwa na milipuko ya mara kwa mara ya kipindupindu, surua, diphtheria na magonjwa mengine yanayozuilika kwa chanjo limeonya shirika hilo. Wakati huo huo, limeongeza kuwa Yemen inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa elimu, unaosababisha madhara makubwa ya muda mrefu kwa watoto.  Kwani watoto milioni mbili hawako shuleni, na idadi hii inaweza kuongezeka hadi watoto milioni 6 wanaopata changamoto ya elimu yao kwani angalau shule moja kati ya nne nchini Yemen imesambaratishwa au kuharibiwa kiasi. 

Habari za UN
Mama akutanishwa na watoto wake baada ya kutenganishwa kufuatia mashambulizi: UNICEF/CAJED

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 7, 2022 0:02


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa kushirikiana na wadau wake kama shirika lisilo la kiserikali la CAJED (CONCERT D'ACTIONS POUR JEUNES ET ENFANTS DÉFAVORISÉS), wanaendelea na huduma kadhaa muhimu za ulinzi kwa watoto ambazo ni pamoja na utambulisho, matunzo na kuwaunganisha watoto na familia zao.  T‘'Mapigano yalikuwa yameanza tukiwa shambani. Binti yangu na wengine walikimbia. Walipofika Goma, walipotea njia.” Anafahamika kwa jina moja, Mukonge, mama wa watoto sita aliyefurushwa na mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sasa anaishi katika Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kanyarutshinya.   Mama huyu japo naye yuko katika kambi hii ambayo imejaa nyumba za mahema na msongamano wa watu, amejawa na furaha kuunganishwa tena na watoto wake wawili ambao walitenganishwa naye wakati wa mapigano ya hivi karibuni huko Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Watoto hao wawili walitenganishwa na wazazi wao wakati kijiji chao kiliposhambuliwa kwa silaha mwezi Oktoba mwaka huu na kuwalazimu kutembea tarkribani kilomita 60 au Maili 37 kwa muda wa saa 14 kutoka nyumbani kwao Rugari hadi Goma bila usimamizi. Marie mwenye umri wa miaka 12 na kaka yake Justin mwenye umri wa miaka mitatu waaliachwa kujilinda wenyewe baada ya shambulio hilo kwa sababu wazazi wao walikuwa mbali na kijiji wakifanya kazi mashambani. Watoto hao wawili iliwalazimu kutembea mwendo huo mrefu wa takribani kilomita 60 peke yao kutoka nyumbani kwao Rugari hadi Goma kuepuka ghasia. Hatimaye kupitia usaidizi wa CAJED, shirika lisilo la kiserikali linalofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, watoto hao wameunganishwa na familia yao baada ya zaidi ya wiki mbili za kutengana.  “Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu sikuweza kuwaona tena. Baadaye, CAJED iliwapata. Ili kujua walikuwa wapi, nilienda kuona picha za watoto waliopotea zilipowekwa, na nikasoma majina yao. Nilipowapata, niliguswa na furaha kwa sababu nilifikiri wamekufa, na sitawaona tena. Tulipoonana watoto walinijia kwa furaha na kuniambia wanakula na kulala vizuri. Ninaota kwamba mtoto wangu atakuwa daktari siku moja ili kutibu watu katika kijiji chake. Vita lazima iishe ili aende shule na kutimiza ndoto yake.'' Anasema kwa matumaini Mukonge.  

Habari za UN
Misingi ya kuanzisha UN miaka 77 iliyopita inakumbwa na mtikisiko, tuchukue hatua- Katibu Mkuu UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 24, 2022 0:02


Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni wakati muhimu wa kurejesha tena matumaini na imani katika kile ambacho ubinadamu unaweza kufanikiwa pindi jamii yote ya kimataifa itakapofanya kazi kama kitu kimoja na kwa mshikamano wa kimataifa. Thelma Mwadzaya na taarifa kamili.Siku ya Umoja wa Mataifa huadhimishwa tarehe 24 ya mwezi Oktoba kila mwaka kukumbuka tarehe kama hiyo mwaka 1945 wakati Chata ya kuanzisha Umoja huo ilipoanza kutumika baada ya kutiwa saini na kuridhiwa na nchi waanzilishi 51 zikiwemo tano zenye ujumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama ambazo ni China, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Marekani.,Katibu Mkuu Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anasema Umoja wa Mataifa ni tunda la matumaini. Matumaini na azma baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ya kwamba kusonga kutoka mizozo na kuelekea katika ushirikiano wa kimataifa.Guterres amesema “leo hii shirika letu linakumbwa na majaribu kuliko wakati wowote ule. Lakini Umoja wa Mataifa uliundwa kwa ajili ya nyakati kama hizi. Sasa kuliko wakati wowote ule tunahitaji kurejesha tena uhai wa misingi ya Chata ya Umoja wa Mataifa katika pembe zote za dunia.”Misingi mikuu saba ya Umoja wa Mataifa  ambao sasa una wanachama 193 ni pamoja na kila nchi mwanachama ni sawa na mwingine na migogoro yote inapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani.Katibu Mkuu anasema hilo lifanyike kwa kupatia fursa amani na kwa kumaliza migogoro ambayo inavuruga maisha, mustakabali na maendeleo ya dunia.Halikadhalika kwa kufanya kazi kutokomeza lindi la  umaskini, kupunguza ukosefu wa usawa na kunusuru malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Ametaja pia kulinda sayari dunia, ikiwemo kuondokana na uraibu wa matumizi ya nishati kisukuku na kuanza kutekeleza mapinduzi ya nishati jadidifu isiyoharibu mazingira.Hatimaye kuweka mizania ya fursa na uhuru kwa wanawake na wasichana na kuhakiksha haki zao kibinadamu zinazingatiwa.Wakati Chata ya Umoja wa Mataifa ina misingi saba, kwa upande wa malengo  yake ni manne ambayo ni kulinda amani na Usalama duniani, kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa katika kutatua matatizo ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni au kiutu na kuwa kitovu cha kuweka utangamano wa vitendo vya nchi katika kufanikisha malengo hayo. 

Habari za UN
Shehena ya nafaka kutoka Ukraine yawasili Djibouti

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 31, 2022 2:08


Hatimaye meli iliyokodiwa na Umoja wa Mataifa iliyokuwa imepakia tani 23,000 za ngano kutoka Ukraine inayopeleka kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula nchini Ethiopia ilitia nanga katika nchi jirani ya Djibouti. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi Ukame mkali kwa zaidi ya misimu minne mfululizo umewaacha watu milioni 22 kutoka nchi za pembe ya Afrika ambazo ni Ethiopia, Kenya na Somalia katika uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu.  Vita ya Ukraine na Urusi ilifanya hali kuwa mbaya zaidi kwa mataifa haya kwakuwa wanategemea nafaka kutoka Ukraine kwa ajili ya msaada wa chakula. Lakini sasa Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kanda ya Afrika Mashariki Mike Dunford anasema meli yenye shehena ya tani 23,000 za ngano imetia nanga katika bandari ya nchi jirani ya Djibouti tayari kusafirishwa kuingia Ethiopia. Dunford anasema “Chakula kilicholetwa na meli hii ya kamanda shujaa kitalisha watu milioni 1.5 kwa mwezi mmoja nchini Ethiopia. Hii italeta utofauti mkubwa sana kwa watu ambao kwa sasa hawana chochote. Na sasa WFP itaweza kuwapatia mahitaji yao ya kimsingi.” Tangu Umoja wa Mataifa kufanikisha kusainiwa makubaliano ya Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi ulioruhusu meli ya Ukraine kusafirisha nafaka, tayari meli takriban 114 zilizobeba shehena ya tani milioni 1.2 za chakula zimesafirishwa katika soko la kimataifa na maeneo ya misaada kama hii ilitoleta nafaka Ethiopia na Mkuu huyo wa Kanda wa WFP anasema...  "Tayari tumeona bei ya ngano imepungua kwa asilimia 15 duniani kote tangu mpango wa Bahari Nyeusi kuanza. Tunachotaka kuona ni chakula kinatiririka zaidi. Tunahitaji, kwa mtazamo wa WFP, mamilioni ya tani katika eneo hili. Nchini Ethiopia pekee, robo tatu ya kila kitu tulichokuwa tukisambaza kilitoka Ukraine na Urusi.”

Habari za UN
Ukraine na Urusi zatia saini makubaliano ya kuruhusu usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia bahari nyeusi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 22, 2022 3:19


Hatimaye makubaliano ya kuruhusu meli zilizojaa shehena za nafaka kutoka nchini Ukraine zipite kwenye baharí nyeusi yamefikiwa hii leo huko Instanbul Uturuki baina ya Ukraine na Urusi yakishuhudiwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amesema makubaliano hayo yameleta nuru kwa ulimwengu kupata ahueni kwenye be iza mazao ya chakula katika soko la kimataifa. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi  Makubaliano haya ni nuru,nuru ya matumaini, nuru ya unafuu ambao ulimwengu unahitaji kuliko zaidi hivi sasa kuliko hapo awali. Napenda kuwatambua na kuwashukuru wote waliohusika mpaka kufanikisha hatua hii. Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko Instanbul Uturuki baada ya kushuhudia utiaji saini baina ya Ukraine na Urusi kuruhusu meli zenye shehena ya mazao na nafaka zilizokuwa zimekwama katika mandari za Odessa, Chernomorsk na Yuzhny huko bahari nyeusi upande wa Ukraine. Guterres amesema bila shaka haya ni makubaliano ya ulimwengu “Yataleta ahueni kwa nchi zinazoendelea ambazo zipo kwenye makali ya kufilisika na watu walio hatarini zaidi wanaokabiliwa na njaa Kali.  Na yatasaidia kuleta utulivu wa bei za vyakula duiani ambazo tayari zilikuwa katika viwango vya rekodi mbaya hata kabla ya vita. Hili lilikuwa jinamizi la kweli kwa nchi zinazoendelea.” Mbali na kuzishukuru nchi hizo mbili, Guterres amemshukuru Rais wa Uturuki Recep Erdogan kwa kuwa mwenyeji wa makubaliano hayo ambaye pia nchi yake itakuwa na jukumu muhimu la kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kufanya ukaguzi wa meli hizo za Ukraine ili zisibebe silaha za magendo wakati wa usafirishaji wa nafaka kwenda na zinaporejea kutoka katika soko la kimataifa. Mashirika mengine ya UN yaliyohusika na mchakato huo ni lile la Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya kibinadamu OCHA na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kibiashara na maendeleo UNCTAD. “Nipo hapa kuweka ahadi kamili kuwa Umoja wa Mataifa tutabakia kuwa wahusika wa karibu katika kufanyia kazi na kuhakikisha kuna mafanikio ya makubaliano haya. Tutaendelea kuongeza juhudi ili kuhakikisha UN iko katika nafasi nzuri ya kutekeleza ahadi zake. Ninavishukuru vikosi kazi vyote viwili vya Umoja wa Mataifa ambavyo vimetengeneza mkataba huu sawia, kwa uratibu thabiti.” Wakati huo huo Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametangaza kikosi kazi cha kuwezesha utekelezaji wa mpango wa baharí nyeusi kikiongozwa ma Katibu Mkuu wa UNCTAD Rebecca Grynspan kikijikita katika kuwezesha upatikanaji usiozuiliwa wa chakula na mbolea zinazotoka nchini Urusi kwenda kwenye soko la kimataifa ikiwa pia ni utekelezaji wa moja ya vifungu vya makubaliano wa mkataba huo uliosainiwa hii leo. “Nawaomba pande zote zisiache kipengele chochote na juhudi zozote za utelekezaji wa ahadi zao. Hatupaswi pia kuacha juhudi zozote kwa ajili ya amani, haya ni makubaliano ambayo hayajawahi kutokea kati ya pande mbili zinazohusika katika mzozo wa umwagaji damu” Katibu Mkuu Guterres alihitimisha hotuba yake kwakusema nuru ya matumaini imeng'aa katika baharí nyeusi ni matokeo chanya ya kuhudi za pamoja za washirika wengi na kuhimiza katika nyakati za misukosuko ya dunia, nuru hii itaangaza njia ya kuelekea katika kupunguza mateso yanayowasibu wanadamu na kupatikana kwa amani.

Jasusi
Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha Magufuli... kilichofuata sintokisahau maishani

Jasusi

Play Episode Listen Later Mar 11, 2022 8:10


Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Kabla ya tangazo langu hilo, tayari kulikuwa na tetesi kadhaa kwamba afya ya kiongozi huyo ilikuwa tete. Hata hivyo, kwa kupitia vyanzo vyangu vya kuaminika, nilikuwa mtu wa kwanza kutangaza kifo hicho. Lakini madhila yaliyonikumba baada ya kuweka taarifa hiyo hadharani, sintoyasahau. Nilitukanwa, nililaaniwa, nilitishwa, na kwa hakika laiti hao waliokerwa wangeweza kunifikia, bila shaka muda huu ningekuwa marehemu. Hatimaye, siku tano baadaye, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa kweli Magufuli amefariki. Nami ikawa ahueni kwangu. Baadhi ya walionitukana, walikuja kuniomba msamaha japo haikusaidia kitu. Hata hivyo nafarijika kwa kuwatumikia Watanzania ipasavyo na kuwa chanzo cha kuaminika cha habari mbalimbali.

Changu Chako, Chako Changu
Francophonie na mshindi wa tuzo ya RFI prix decouverte

Changu Chako, Chako Changu

Play Episode Listen Later Mar 7, 2022 19:47


Makala hii imeanzia nchini Kenya ambako wanamuziki kutoka kabila la luo walikusanyika katika bustani ya Alliance Francaise Jijini Nairobi kuadhimisha miaka minne ya kifo cha mwanamuziki Job Seda, kwa jina maarufu kama Ayub Ogada. Kwa kuwa Machi ni mwezi wa La Francophonie ulimwenguni, RFI Kiswahili ilikuwepo hapo Alliance kurekodi vipindi mbali mbali mbele ya wanafunzi wa lugha ya kifaransa. Hatimaye, tutarejelea sehemu ya pili mahojiano ya mshindi wa tuzo ya RFI Prix Découverte 2021, Alesh pamoja na vijisehemu vya tamasha lake huko Paris february 28 2022.

Jukwaa la Michezo
Soka Afrika: Hatimaye michuano ya AFCON kuanza nchini Cameroon

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later Jan 8, 2022 23:54


Maandalizi yamekamilika kuelekea michuano ya soka kwa mataifa ya Afrika nchini Cameroon, iliyoahirishwa kutoka mwaka 2021 kwa sababu ya janga la Covid 19.

Habari za UN
Mashirika ya misaada yaingia Tigray Ethiopia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 10, 2021 1:15


Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake wamepata tena uwezo wa kuingia katika kambi za wakimbizi za Mai Aini na  Adi Harush zinazohifadhi wakimbii wa Eritrea nchini Ethiopia. Hatua ya sasa inakuja baada ya kushindwa kuingia kambini huko tangu tarehe 13  mwezi uliopita wa Julai kutokana na mapigano jimboni humo. (Taarifa ya John Kibego)

Habari za UN
Senegal na Brazil kuzalisha vipimo vya COVID-19

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 15, 2021 2:01


Hatimaye makubaliano yamefikiwa ya kuwezesha uzalishaji wa vifaa vya upimaji haraka wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa nchi za kipato cha chini na kati ambapo sasa uzalishaji utafanyika Brazil kwa nchi za Amerika ya Kusini na Senega kwa nchi za Afrika.

SIRI ZA BIBLIA
SIRI ZA BIBLIA: NUHU NA GHARIKA YA MAJI/DUNIA NZIMA WATU 8 TU WALIOPONA

SIRI ZA BIBLIA

Play Episode Listen Later Apr 18, 2021 23:00


Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao agano thabiti (Eb 11:7). Kadiri ya Mtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya ubatizo (1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni Kanisa, ambalo kadiri ya Agano Jipya ni la lazima kwa wokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake. Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la mzeituni unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta. Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa Yesu ambapo alipakwa Roho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu (Mk 1:9-11; Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa binadamu. Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu sadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili. Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika ekaristi, ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu (Math 24:37-41). --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message

Jasusi
Hatimaye Serikali Yathibitisha Kifo Cha Rais Magufuli Nilichoripoti 12.03.2021

Jasusi

Play Episode Listen Later Mar 18, 2021 15:04


Hatimaye Serikali Yathibitisha Kifo Cha Rais Magufuli Nilichoripoti 12.03.2021 Get full access to Barua Ya Chahali at www.baruayachahali.com/subscribe

Jasusi
Hatimaye Serikali Yathibitisha Kifo Cha Rais Magufuli Nilichoripoti 12.03.2021

Jasusi

Play Episode Listen Later Mar 18, 2021 15:04


Hatimaye Serikali Yathibitisha Kifo Cha Rais Magufuli Nilichoripoti 12.03.2021

Cleaning The Airwaves
3. Musical Growth Is Necessary - Atemi Oyungu - The Play House

Cleaning The Airwaves

Play Episode Listen Later Jan 3, 2021 74:54


Carol Atemi Oyungu is a Kenyan singer, songwriter and entertainer. She first made her mark by being in the girl band Intu until 2007 when they each decided to go solo. In 2003, she joined Eric Wainaina, as an assistant vocal harmony provider for his band. Atemi released her first single "Happy" in 2004 and her debut album Hatimaye in 2008, and her second studio album Manzili in 2013. She hosted the sixth series of Africa Rising, a programme showcasing Africa's musical talent. She has worked with various Kenyan musicians such as Nikki, Lady Jaydee, Chris Adwar and Delvin Mudigi.

Cleaning The Airwaves
2. Being A Woman In The Kenya Music Industry - Atemi Oyungu - The Play House

Cleaning The Airwaves

Play Episode Listen Later Jan 3, 2021 54:56


Carol Atemi Oyungu is a Kenyan singer, songwriter and entertainer. She first made her mark by being in the girl band Intu until 2007 when they each decided to go solo. In 2003, she joined Eric Wainaina, as an assistant vocal harmony provider for his band. Atemi released her first single "Happy" in 2004 and her debut album Hatimaye in 2008, and her second studio album Manzili in 2013. She hosted the sixth series of Africa Rising, a programme showcasing Africa's musical talent. She has worked with various Kenyan musicians such as Nikki, Lady Jaydee, Chris Adwar and Delvin Mudigi.

Cleaning The Airwaves
1. My Musical Beginning - Atemi Oyungu - The Play House

Cleaning The Airwaves

Play Episode Listen Later Jan 3, 2021 44:46


Carol Atemi Oyungu is a Kenyan singer, songwriter and entertainer. She first made her mark by being in the girl band Intu until 2007 when they each decided to go solo. In 2003, she joined Eric Wainaina, as an assistant vocal harmony provider for his band. Atemi released her first single "Happy" in 2004 and her debut album Hatimaye in 2008, and her second studio album Manzili in 2013. She hosted the sixth series of Africa Rising, a programme showcasing Africa's musical talent. She has worked with various Kenyan musicians such as Nikki, Lady Jaydee, Chris Adwar and Delvin Mudigi.

Habari za UN
Miaka 10 baadaye, hatimaye misaada ya UN yawafikia katika milima ya Jebel Marra, Sudan. 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 21, 2020 2:51


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limepeleka misaada katika eneo la Jebel Marra, Darfur, Sudan ili kuokoa maisha ya watu waliokimbilia katika maeneo hayo ya milima kuyakimbia mapigano katika maeneo yao. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.  Ngamia waliobeba misaada mbalimbali kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wanakatiza polepole katika mabonde na vilima vya mawe.   

Habari za UN
UNHCR yajenga mahema kunusuru wakimbizi baada ya kambi ya Moria kuteketea kwa moto,

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 15, 2020 2:10


Hatimaye mamia ya wasaka hifadhi kwenye kambi ya Moria iliyoteketetea kwa moto katika kisiwa cha Lesvos nchini Ugiriki wiki iliyopita, sasa wamepata makazi kwenye mahema yaliyosimikwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Ahimidiwe Olotu na taarifa kwa kina. UNHCR inasema kuwa takribani wasaka hifadhi 2,200 wamepatiwa malazi kwenye eneo la dharura ambapo shirika hilo limesimika mahema 280.

Habari za UN
Chanjo ya bei dozi ya ‘Numonia’ yapungua kwa asilimia 43 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 17, 2020 2:25


Hatimaye bei ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya vichomi au Numonia, PVC,  imeshuka kwa asilimia 43 na kufikia dola 2 za kimarekani kwa dozi moja na hivyo kuwa ni nafuu kubwa kwa nchi za kipato cha chini duniani kote.

pvc hatimaye
Habari za UN
Ndoto ya mkimbizi wa Syria kuwa fundi umeme yatimia huko Ujerumani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 1, 2020 2:08


Hatimaye ndoto za mkimbizi kutoka Syria za kutaka kutumia ujuzi wake katika hisabati na fizikia zimetimia huko Ujerumani baada ya kupata kazi katika kampuni ambamo kwayo anatumia stadi zake. Loise Wairimu na ripoti kamili. Mjini Hamburg,nchini Ujerumani, katika karakana ya treni ya kampuni ya Deutche Bahn.Tunakutana na Mohammad Alkalaf, mkimbizi kutoka Syira mwenye umri wa miaka 28 ambaye hatimaye ametimiza ndoto yake baada ya kuajiriwa kwa nafasi ya uanagezi kwenye kampuni hii ya treni ya kijerumani.

syria fundi kuwa huko ujerumani hatimaye
Mjadala wa Wiki
Mjadala wa Wiki - DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano

Mjadala wa Wiki

Play Episode Listen Later May 23, 2019 12:12


Hatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?

Wimbi la Siasa
Wimbi la Siasa - Tume ya Uchaguzi yahairisha Uchaguzi katika baadhi ya maeneo, Mashariki mwa DRC

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Dec 28, 2018 9:57


Hatimaye, Uchaguzi Mkuu wa DRC utafanyika siku ya Jumapili, lakini Tume ya Uchaguzi imeahirisha zoezi hilo katika maeneo ya Butembo, Beni na Yumbi kwa sababu za kiusalama na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

ebola drc beni katika tume baadhi butembo mashariki uchaguzi jumapili uchaguzi mkuu hatimaye
Talisman Brise
Talisman Brisé - Hatimaye Profesa awa huru,Kwame apongezwa

Talisman Brise

Play Episode Listen Later Jun 23, 2012 2:42


Hatimaye Prosefa Omar aokolewa,watekaji nyara watiwa nguvuni  na Kwame apongezwa na kila mtu kwa ushujaa wake wa kufatilia hadi kufanikisha Profesa Omar anapatikana.

Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Tukio 19 – Kuingilia Jambo kwa Kina

Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Play Episode Listen Later Aug 25, 2009 15:00


Ingawa maduara ya mimea yalitengezwa na Wakulima, Eulalia bado anaamini kuna madude yanayoanguka kutoka angani. Katika kuchunguza ulaghai huo, Philipp na Paula wanakwenda baa ya mahali ambako wanazungumza na wanakijiji. Paula na Philipp wametengua kitendawili cha maduara ya mimea lakini bado wana shaka kuhusu kuweko kwa madude yanayoanguka kutoka angani. Madude hayo ni nini? Eulalia anasisitiza amewahi kuliona moja. Hatimaye waandishi habari hao wanawauliza wateja kwenye baa maoni yao kuhusu maduara bandia ya mimea. Ziara ya baa ni fursa nzuri ya kutanguliza wakati uliopita, hasa kitenzi kisichotabirika "sein" (kuwa). Kitenzi cha utaratibu "können" (kuweza) pia kimeangaziwa katika tukio hili. Zingatia jinsi irabu zinavyobadilika wakati wa kunyambua kitenzi.

Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Tukio 18 – Uchunguzi wa Usiku

Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Play Episode Listen Later Aug 25, 2009 14:08


Paula na Philipp wanataka kujua mbivu na mbichi kuhusu maumbo ya duara ya mimea na wanakwenda usiku kuchunguza. Lakini wanachokumbana nacho hakihusu viumbe kutoka angani. Mwenye shamba lenye maumbo ya duara yasiyoeleweka anawatoza watalii ada ya Yuro 5 kila mmoja ili wapige picha maumbo hayo. Wakati huo huo Philip na Paula wamepiga kambi mwituni kusubiri madude yanayoanguka kutoka angani. Badala yake, wanaume wawili wanajitokeza wakiwa na mtambo. Je wao ndio waliotayarisha hayo maduara ya mimea kuwavutia watalii? Hatimaye, dude kutoka angani linaonekana na hivyo kuzidisha kizungumkuti. Kitenzi "machen" kinaeleweka kwa urahisi. Katika tukio hili mwalimu anakufunza namna tofauti za kutumia neno hili.