POPULARITY
Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu, Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."
Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au kwingineko. Mkiwa mbali na familia zenu, mbali na nchi yenu, katika mazingira yenye changamoto, na wakati mwingine katika hali hatarishi.”Anawapa moyo zaidi askari lakini akiwakumbusha kuwa wao ni kioo cha ulimwengu wazingatie maadili“Na tunathamini sana kujitolea kwenu. Tunathamini sana kwamba mnaenda kuwasaidia ndugu zenu katika nchi nyingine, iwe ni nchi jirani au sehemu iliyo mbali. Mnapokwenda, mnaliwakilisha dunia. Mnawakilisha watu wa dunia.”Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang'are akamthibitishia mgeni kwamba askari hawa wameiva na hakuna kisingizio chochote cha kutozingatia maadili huko wameandako, kisha akawahoji, Nao wanajibu, “twende pamoja, turudi pamoja.”
Tanzania inaingia kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu kuanzia Agosti 28, kuelekea kufanyika kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba, 29 2025. Rais Samia Suluhu Hassan, kutoka chama tawala CCM, anawania uongozi wa nchi hiyo. Mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anaendelea kuzuiwa jela, kwa tuhma za uchochezi na uhaini.
Timu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali
Timu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.
Mada ya leo ni kuhuus michuano ya CHAN inapoendelea kushika kasi kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, nchini Kenya baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani bila ya tiketi, hatua ambayo shirikisho la soka la Afrika CAF, limelazimika kupunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani kwa sababu za kiusalama.,,tumemuuliza nini kifanyike kudhibiti usalama wa mashabiki na viwanja? na Kwenye nchi yako wakati wa mechi kubwa hali huwaje?
Mada ya leo ni kuhuus michuano ya CHAN inapoendelea kushika kasi kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, nchini Kenya baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani bila ya tiketi, hatua ambayo shirikisho la soka la Afrika CAF, limelazimika kupunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani kwa sababu za kiusalama.,,tumemuuliza nini kifanyike kudhibiti usalama wa mashabiki na viwanja? na Kwenye nchi yako wakati wa mechi kubwa hali huwaje?
mada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
mada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
Leo tumeangazia fainali ya Kombe la Mataifa ya Wanawake kati ya Nigeria na Morocco, maandalizi ya CHAN yapamba moto, kamati ya Olimpiki nchini Kenya yapata viongozi wapya, kurejea kwa soka nchini Sudan licha ya vita, chama cha wachezaji Fifpro kikidai wachezaji wanahofia kulalamikia mrundiko wa mechi kwenye kalenda ya soka, uhamisho wa wachezaji ulaya, Verstappen ashinda mashindano ya mazoezi ya Belgian GP, Tour de France yafikia hatua ya 20 na fainali ya Kombe la EURO kwa wanawake.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.
Kutoka Dar es Salaam hadi Geneva, na sasa New York. Ni safari ya kujifunza, kujaribu na kufanikiwa. Kwa vijana wengi barani Afrika, Umoja wa Mataifa huonekana kuwa ndoto isiyowezekana. Lakini kijana huyu kutoka Tanzania anathibitisha kuwa kwa nia thabiti na bidii, ndoto hiyo inaweza kuwa kweli. Kupitia programu ya mafunzo kwa vitendo ya Umoja wa Mataifa, amejifunza mengi kuhusu utawala, maendeleo na kujenga ujasiri wa kushiriki katika kazi za kimataifa. Sarah Nshoka alipata fursa kuzungumza na Shraon Jebichii katika makala hii.
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Mwezi Juni mwaka 2025, Tume ya Ulaya iliorodhesha Kenya miongoni mwa nchi zenye changamoto ya utakatishaji wa fedha, huku Uganda ikipata afueni kwa kuondolewa kwenye orodha hiyo. Hatua hii ina maana kuwa mashirika ya kifedha – ikiwemo benki – zinalazimika kuzingatia kwa makini uhusiano wa kibiashara na miamala yoyote inayohusiana na nchi zilizo kwenye orodha hiyo, na kuchukua hatua kali za udhibiti wa fedha. Nchi nyingine katika orodha hiyo ni pamoja na Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, na zingine. Katika Makala haya, Gurudumu la Uchumi, tunachambua hatua hii na athari zake kwa uchumi, lakini pia nini mamlaka katika nchi hizo zinaweza kufanya hili kujiondoa kwenye orodha hiyo.
Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.
Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika, Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Assumpta Massoi anamulika moja ya familia zilizonufaika.
Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na na majukwaa ya kidijitali. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili namna teknolojia inaweza kutumika katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa. Tumezungumza na Mhandisi Octavian Lasway, mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na umwagiliaji.
Wiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili namna teknolojia inaweza kutumika katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa. Tumezungumza na Mhandisi Octavian Lasway, mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na umwagiliaji.
Nchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi, kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.
Shukran sana kwake maulana kutukutanisha tena jumapili ya leo, ambapo nakuletea historia na namna tamasha la filamu maharugu duniani lijulikanalo kama Festival de cannes ambalo hufanyika mwezi Mei ya kila mwaka, kwenye Palais du festival huko Cannes. Kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba ya shughuli mbalimbali kwenye vituo vya Alliance Francaise za ukanda na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Ali Kiba,
Kwenye makala haya tunajadili kilichotokea nchini DRC ambapo bunge la seneti lilimuondolea kinga ya kutoshtakiwa rais wa zamani, Joseph Kabila, hatua ambayo sasa inatoa nafasi kwa mahakama ya kijeshi kumshtaki kiongozi huyo kwa tuhuma za uhaini. Unazungumziaje hatua hii ya seneti, unadhani ilikuwa sahihi?Ndio swali tumekuuliza?skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
Kwenye makala haya tunajadili kilichotokea nchini DRC ambapo bunge la seneti lilimuondolea kinga ya kutoshtakiwa rais wa zamani, Joseph Kabila, hatua ambayo sasa inatoa nafasi kwa mahakama ya kijeshi kumshtaki kiongozi huyo kwa tuhuma za uhaini. Unazungumziaje hatua hii ya seneti, unadhani ilikuwa sahihi?Ndio swali tumekuuliza?skiza maoni ya baadhi ya waskilizaji.
Wabunge wa upinzani hata hivyo walisusia kikao kilichopitisha mswada huo kwa haraka. Wanasiasa wa upinzani wanadai mswada huo unawalenga wakosoaji wa rais Yoweri Museveni
Wabunge wa upinzani hata hivyo walisusia kikao kilichopitisha mswada huo kwa haraka. Wanasiasa wa upinzani wanadai mswada huo unawalenga wakosoaji wa rais Yoweri Museveni
Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO. Flora Nducha anakutaarifu kwa muhtasari.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.
Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk amesisitiza haja ya kudumisha usitishaji mapiganona kutoa wito wa mchakato wa amani unaozingatia haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya kujitawala na uwajibikaji. Ametaka kuachiliwa kwa mateka, kukomeshwa kwa vizuizi vya kiholela, na kuanza tena kwa msaada wa kibinadamu mara moja ndani ya Gaza.Kuhujsu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine amersema bado ni suala la kutia wasiwasi, huku raia wakiishi kwa hofu ya mara kwa mara kutokana na mashambulizi yasiyokoma.Türk amekemea vikali vikwazo vya Shirikisho la Urusi juu ya haki za msingi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kuelezea masikitiko yake kuhusu ripoti za mauaji ya kiholela na mateso ya kimfumo ya wafungwa wa vita wa Kiukraine.Almeihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kuelekea amani endelevu inayoheshimu haki na matarajio ya watu wa Ukraine.Türk pia ameelekeza mawazo kwenye maeneo mengine yenye migogoro, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Myanmar, Haiti, na Sudan.Alielezea jinsi watawala wa kiimla, wanasiasa wahubiri wa chuki, na walanguzi wanavyotumia machafuko kwa faida zao binafsi.Amesema Athari za migogoro huenea zaidi ya mstari wa mbele, zikiathiri minyororo ya usambazaji duniani na nafasi za kidijitali.Ametoa wito kwa watu binafsi kutambua jukumu lao la pamoja kwa kufanya maamuzi ya kimaadili ya ununuzi, kushiriki kisiasa, na kuunga mkono uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.Hata hivyo amesema demokrasia zilizoimarika haziko salama dhidi ya kudorora kwa haki za binadamu. Türk ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mwelekeo nchini Marekani, ambako maendeleo kuhusu usawa wa kijinsia na sera za kupinga ubaguzi yanarudi nyuma.Pia amekosoa Shirikisho la Urusi kwa ukandamizaji wake wa jamii za kiraia na vyombo vya habari huru, ambapo wapinzani wanakabiliwa na unyanyasaji, kukamatwa, au kufurushwa.Kudhoofika kwa haki za binadamu katika mataifa yenye nguvu, Türk alionya kwamba kunaweka mfano hatari kwa ulimwengu mzima, akisisitiza hitaji la dharura la mshikamano wa kimataifa na uwajibikaji kuhusu haki za binadamu.
Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeeleza mshtuko mkubwa na wasiwasi wake kufuatia kugunduliwa kwa makaburi mawili nchini Libya walimozikwa wahamiaji kadhaa, baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi. Flora Nducha na taarifa zaidi
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Wasyria wana matarajio makubwa kwa nchi yao, na hamu kubwa ya watu kutoka katika kila nyanja ya jamii kuja pamoja na kuunda katiba mpya, ambayo lazima ianze na mazungumzo ya kitaifa yaliyo jumuishi. Hayo ni kwa mujibu wa Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, ambaye amekuwa Damascus kukutana na wajumbe kadhaa wa mamlaka ya mpito ili kuhakikisha Wasyria wote wana uwezo wa kushiriki katika mustakbali wa nchi hiyo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa. Flora Nducha amefuatilia kampeni hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo..
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 tunamsikia Nasra Abdallah, mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao. Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na migogoro na tatu teknolojiaUNICEF inasema yote haya ni changamoto na fursa ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo katika zama zijazo.Rafif mtoto mkimbizi wa ndani ameandika barua kutoka Palestina ambako vita imetamalaki, anasema“Ninatoka mjini Gaza na sasa nimefurushwa hadi Kusini mwa Gaza. kama watoto Ni haki yetu kuishi kwa usalama na kujenga mustakbali bora”Kutoka mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki kwa Steven akimulika afya“Na nianaandika kwenu kutoka Tanzania. Kwenye jamii yangu watoto wanaugua kila wakati , kwa nini? Huu ndio mustakbali wangu je unasikiliza?”Nako Congo DRC mitihani ni mingi, Andrea anasema“Nataka kushuhudia dunia ambayo kila mtoto anapendwa, dunia ambayo amani inashamiri ni raha na faraja. Napenda kuona hasira zinageuka na kuwa mazungumzo”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono suti hizo za watoto katika ujumbe wake amesema Katika Siku ya Watoto Duniani tunasherehekea washiriki wachanga zaidi wa familia yetu ya kibinadamu. Lakini leo pia ni wakati wa kutambua changamoto kubwa zinazowakabili watoto katika ulimwengu wetu uliogawanyika sana, wenye misukosuko na mara nyingi ulioshamiri ukatili.”Ripoti ya UNICEF imetoa wito wa kuwekeza katika elimu, miji endelevu na yenye mnepo kwa watoto, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, huduma muhimu na mifumo ya msaada wa kijamii na pia teknolojia iliyo salama kwa watoto ili kupambana na mzigo wa changamoto zinazowakabili.