Podcasts about baada

An Aboriginal Australian people living in the Kimberley region of Western Australia

  • 69PODCASTS
  • 555EPISODES
  • 16mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Jul 14, 2026LATEST
baada

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about baada

Show all podcasts related to baada

Latest podcast episodes about baada

Habari za UN
14 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 14, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake. Baada ya ziara yake mjini Bunia, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO anayehusika na Programu ya Dharura za Afya, Dkt. Chikwe Ihekweazu, amewambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kwamba mlipuko wa sasa ni moto ambao kinachouchochea kiko katikati, huku ukiendelea kusambaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari (IMO) limesema lina wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya jana usiku yaliyolenga meli kwenye mlango wa bahari wa Hormuz na viunga vyake na kusababisha vifo vya takribani mabaharia wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kupitia taarifa yake iliyotolewa London, Uingereza, IMO imesema inafanya kazi kwa haraka na mamlaka husika ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.Na uungwaji mkono wa umma kwa wakimbizi unaendelea kuwa imara licha ya kuwepo kwa changamoto na kutokuweko kwa uhakika wa mustakabali duniani, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa na kampuni ya IPSOS na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Utafiti umebaini kuwa asilimia 66 ya washiriki katika nchi 29 wanakubaliana kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kuruhusiwa kusaka hifadhi katika nchi nyingine, ikiwa ni punguzo la asilimia moja tu ikilinganishwa na mwaka 2025.Utafiti huu umefanywa ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa Mkatab awa Kimataifa wa kulinda wakimbizi.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

iran kenya congo ebola hormuz imo sdgs drc ipsos unhcr unai umoja programu hii ituri afya mount kenya julai baada dkt bunia mataifa jamhuri marekani shirika kimataifa afrika mashariki uingereza kidemokrasia chuo kikuu
Habari za UN
01 JULAI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 1, 2026 9:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Ikiwa ni siku chache baada ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wasioona na viziwi inayoadhimishwa tarehe 27 Juni kila mwaka, Rashid Malekela wa Idhaa hii anakupeleka Mashariki ya Kati akimmulika mkazi mwenye ulemavu ambaye anakumbwa na changamoto katikati ya vita.Wakati harakati za uokozi na usaidizi zikiendelea nchini Venezuela baada ya matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1700 hadi sasa, leo hii ikiwa ni siku ya saba Emily Camargo akiwa kwenye kituo cha hifadhi kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jimboni La Guaira anaelezea alivyonusurika akisema, “kila kitu kilichonizunguka kiliporomoka na kunizingira, isipokuwa nilipokuweko. Nashukuru kwa sababu jengo la pembeni yetu halikuanguka. Hakuna kilichonipata. Hapa ndio tunalala, mimi, mume wangu , wifi yangu na mbwa wangu. Binadamu yangu na mpenzi wake hatujui waliko tumewatafuta hadi hospitalini, na kwenye orodha, hakuna dalili.”Jopo Huru la Kimataifa la Kisayansi la Umoja wa Mataifa kuhusu akili mnemba, limetoa ripoti leo inayoonesha kuwa teknolojia hiyo inaendelea kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi kuliko uwezo wa serikali kuandaa sera na kanuni zinazoendana nayo. Miaka michache iliyopita, akili mnemba ilikuwa ikitumika zaidi kujibu maswali au kuandika maandishi rahisi. Leo, teknolojia hii inaweza kutengeneza picha na video zenye uhalisia mkubwa na hata kufanya baadhi ya kazi bila usimamizi wa karibu wa binadamu lakini mifumo ya udhibiti na sheria za usalama haijafanikiwa kuendana na mabadiliko hayo.Baada ya miongo kadhaa hatimaye hii leo Umoja wa Mataifa umeondoa kanuni ya kifedha iliyokuwa ikiulazimisha kurejesha kwa nchi wanachama fedha ambazo hazikutumika  hata kama fedha hizo hazikuwa zimewasilishwa kabisa. Uamuzi huo uliofanywa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne unafuatia mapendekezo ya Kamati ya Tano, ya Baraza hilo ambayo inashughulikia masuala ya utawala na bajeti. Kanuni ilikwamisha ajira ndani ya Umoja wa Mataifa na operesheni za ulinzi wa amani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kuwa kanuni hiyo ilikuwa inahatarisha uthabiti wa Umoja wa Mataifa na kwa uamuzi huu, Baraza limeanzisha mbinu mpya itakayohakikisha kuwa fedha ambazo hazijatumika zinarejeshwa kwa nchi wanachama pale tu zinapokuwa zimewasilishwa taslimu na kupokelewa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGURU."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Wimbi la Siasa
Kwanini vita vinaendelea mwaka mmoja baada ya DRC na Rwanda kutia saini ya mkataba wa amani ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jul 1, 2026 9:57


Vita vimeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi na waasi wa M23/AFC wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Rwanda licha ya Kigali na Kinshasa, kutia saini mkataba wa kusitisha vita mwaka mmoja uliopita. Kwanini vita vinaendelea  licha ya kuwepo kwa mkataba huu ? Tunachambua.

SBS Swahili - SBS Swahili
Australia Yafafanuliwa: Jinsi yakujiunga na soka jumuishi nchini Australia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 30, 2026 14:27


Sio kutia chumvi tunaposikia kwamba Kombe la Dunia la FIFA lina tarajiwa kuleta dunia pamoja katika mwezi wa Juni. Baada ya yote, mpira wa miguu unajulikana kama mchezo maarufu zaidi duniani.

SBS Swahili - SBS Swahili
Australia yatinga raundi ya 32 baada ya sare yakutofungana dhidi ya Paraguayi

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 26, 2026 4:39


Socceroos wamefanikiwa kufika hatua ya mchujo baada ya kupata sare yakutofungana katika Kundi D, wakati Ecuador ikiwaacha wajerumani vinywa wazi katika Kundi E na kufuzu kushiriki katika hatua ya timu bora 32.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Maelfu wahofiwa wamefariki baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika mji mkuu wa Venezuela

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 25, 2026 4:20


Hali ya dharura ime anza kutumika nchini Venezuela baada ya matetemeko mawili makubwa ya ardhi, yaliyotokea magharibi mwa mji mkuu wa Caracas, na kuua watu wasiopungua 32 pamoja nakuwajeruhi mamia.

Habari RFI-Ki
Kenya : Miaka miwili baada ya maandamano ya Gen Z

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jun 25, 2026 9:56


Shaba yetu leo inalenga nchini Kenya mbapo raia nchini humo wameadimisha miaka miwili tangu kutokea kwa maandamano ya mwaka 2024 ya vijana waliokuwa wapigigania mageuzi nchini humo. Skiza maoni ya mskilizaji.

Habari RFI-Ki
Kenya : Miaka miwili baada ya maandamano ya Gen Z

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jun 25, 2026 9:56


Shaba yetu leo inalenga nchini Kenya mbapo raia nchini humo wameadimisha miaka miwili tangu kutokea kwa maandamano ya mwaka 2024 ya vijana waliokuwa wapigigania mageuzi nchini humo. Skiza maoni ya mskilizaji.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari:Wanaume wawili wafunguliwa mashtaka baada ya Polisi kunasa tani 2.7 za kokeni nchini Australia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 22, 2026 5:16


Polisi wamekamata tani 2.7 za kokeni katika kile kinachoelezwa kuwa unyakuaji mkubwa zaidi wa kokeni kuwahi kutokea nchini Australia.

Habari za UN
18 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 18, 2026


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Katika mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliomalizika wiki iliyopita baadhi ya wahudhuriaji walikuja na wakalimani wao, kutoka Tanzania Mbunge Nassriya Nassir Ali mwenye ulemavu wa kusikia au Kiziwi aliambatana na mkalimani wake Tusajigwe Ernest. Baada ya mkutano huo Leah Mushi aliketi na Tusajigwe na hapa anaanza kwa kueleza kuhusu taaluma yake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Kauli za chuki zinaendelea kuhatarisha mshikamano wa jamii na amani duniani, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema mara nyingi ndizo chachu ya vurugu, migogoro na uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu. Katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Kauli za Chuki, leo Juni 18, Guterres amesema makundi kama wanawake, wahamiaji, wakimbizi, watu wenye ulemavu na jamii ya LGBTQIA+ mara nyingi hulengwa na ujumbe wa chuki. “Kauli za chuki ndio hatua ya kwanza katika njia ya kuwanyima watu utu wao, njia ambayo mara nyingi hupelekea vurugu, migogoro na uhalifu wa kutisha.” Pia ameonya kuwa mitandao ya kijamii imeongeza kasi ya kusambaa kwa chuki duniani.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, umetangaza kwa masikitiko hii leo kifo cha mfanyakazi wa kampuni iliyokuwa ikitoa huduma kwa ujumbe huo, aliyefariki dunia kutokana na Ebola mjini Bunia. MONUSCO imesema mfanyakazi huyo alikuwa ameacha kufanya kazi na ujumbe huo tangu Mei 22 mwaka huu na hakuwa amefika katika maeneo ya MONUSCO kwa zaidi ya siku 21 kabla ya ugonjwa huo kuthibitishwa. Ujumbe huo umetuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, marafiki na wafanyakazi wenzake na marehemu.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, limesema matukio mabaya ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi yaliathiri takriban watu milioni 13 barani Afrika mwaka 2025 na kusababisha vifo zaidi ya watu 3,000. Ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi inaeleza kuwa mafuriko yalikuwa janga lililoripotiwa zaidi, huku yakisababisha hasara kubwa za kiuchumi na kibinadamu. WMO pia imeonya kuwa barafu katika maeneo ya milima ya Afrika, ikiwemo Mlima Kilimanjaro, inaendelea kutoweka kwa kasi, wakati kina cha bahari katika baadhi ya maeneo ya pwani kikipanda kwa kiwango kikubwa kuliko wastani wa dunia. WMO imesisitiza kuwa Afrika bado ina pengo kubwa katika mifumo ya tahadhari za mapema, ingawa maendeleo yanaendelea kufanyika.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

Jukwaa la Michezo
Arsenal yashinda ubingwa wa Uingereza baada ya miaka 22, Fainali za BAL zikianza

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later May 23, 2026 23:50


Leo tumeangazia Arsenal kushinda ubingwa wa Ligi Kuu baada ya miaka 22, kocha wa Uingereza Tuchel azomewa kuwaacha nje wachezaji kadhaa, kocha wa DRC Desabre ataja kikosi cha Kombe la Dunia, Aston Villa yashinda Kombe la Europa, Droo ya kufuzu michuano ya AFCON 2027 yakamilika huku AFCON U17 ikiendelea, fainali za BAL zaanza Kigali, Kipchoge kukimbia marathon ya kwanza Afrika, Motsengo Omba ashinda urais wa Fecofa, raundi ya pili kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17 yaanza.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala Leo: WHO yatangaza dharura ya afya duniani baada ya mlipuko wa Ebola DR Congo na Uganda

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 22, 2026 9:02


Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ni dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi kimataifa.WHO inasema mlipuko huo hauja fikia vigezo vya dharura ya janga, lakini nchi zinazo changia mipaka ya ardhi na DRC ziko katika hatari kubwa ya usambaaji zaidi.Kwa wakazi wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekuwa na mambo mengi ya kuhofia kutokana na uhasama ambao umekuwa ukiendelea kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji waasi.Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Habari RFI-Ki
Wakenya walazimika kutembea baada ya magari ya uchukuzi wa umma kugoma.

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later May 20, 2026 9:58


Siku ya Jumatatu uchukuzi ulitatizwa nchini Kenya kufuatia mgomo wa wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kupinga ongezeko la bei ya mafuta. Hii ni baada ya serikali kupandisha Lita moja ya Petroli kufikia Shilingi za nchi hiyo 214 huku ile ya Dizeli ikifikia Shilingi 242. Tumemuuliza mskilizaji wetu anzungumziaaje kilichotokea nchini Kenya na nchini mwake hali iko je kuhusu bei ya mafuta.

Habari RFI-Ki
Wakenya walazimika kutembea baada ya magari ya uchukuzi wa umma kugoma.

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later May 20, 2026 9:58


Siku ya Jumatatu uchukuzi ulitatizwa nchini Kenya kufuatia mgomo wa wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kupinga ongezeko la bei ya mafuta. Hii ni baada ya serikali kupandisha Lita moja ya Petroli kufikia Shilingi za nchi hiyo 214 huku ile ya Dizeli ikifikia Shilingi 242. Tumemuuliza mskilizaji wetu anzungumziaaje kilichotokea nchini Kenya na nchini mwake hali iko je kuhusu bei ya mafuta.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Maamuzi magumu kuhusu kupunguzwa kwa NDIS yatawala baada ya kutolewa kwa bajeti ya shirikisho

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 15, 2026 11:00


Upunguzaji wa fedha katika Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu ndio chanzo kikubwa zaidi cha uokoaji wa fedha katika bajeti ya serikali shirikisho, jambo linalowaacha watu wengi katika jamii ya wenye ulemavu wakiwa na hasira na wasiwasi juu ya kile kinachokuja.

Habari za UN
14 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 14, 2026 12:13


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme iliyoko kaunti ya Samburu nchini Kenya, ambaye katika mahojiano na Flora Nducha ameelezea jinsi mila na desturi kwa wanawake na wasichana kutorithi chochote kwenye jamii yao zinavyoanza kuyoyoma. Pia tunamsikia kutoka Salome Gatakaa Araka wa FODDAJ ambalo ni Jukwaa la Maendeleo ya Wanawake, Demokrasia na Haki, nchini Kenya ni shirika la kiraia ambalo mwaka huu kwa mara nyingine lilishiriki mkutano huo wa CSW70. Baada ya kushriki vikao mmoja wa viongozi wa shirika hilo amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na ndio msingi wa mahojiano haya.Tunakuletea pia muhtasari wa habari zikiwemo za hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na Sudan, pamoja na masuala ya afya tukimulika yanaoendelea kuhusu virusi vya Hanta au Hantavirus.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

kenya congo sudan drc hantavirus ipc machi umoja hii haki kiswahili samburu baada wanawake mataifa jamhuri maendeleo mkutano kidemokrasia miongoni jukwaa
Radio Maria Tanzania
Kwanini mapapa wanabadili majina baada yakupata wadhifa huo?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 19:33


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Benedict Luvanga, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Kwanini mapapa wanabadili majina baada yakupata wadhifa huo? Tarehe 17 Machi 2026   L'articolo Kwanini mapapa wanabadili majina baada yakupata wadhifa huo? proviene da Radio Maria.

machi radio maria karibu baada kipindi maswali majina
Radio Maria Tanzania
Fahamu Maisha ya Mitume wa Yesu na vifo vyao baada ya yesu kupaa?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 27:34


Karibu usikilize Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani. Mwezeshaji ni Frateri Desderius Mwambaluka, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali ni Naomba kujua Maisha ya Mitume wa Yesu na vifo vyao baada ya yesu kupaa. Tarehe 22 Machi 2026   L'articolo Fahamu Maisha ya Mitume wa Yesu na vifo vyao baada ya yesu kupaa? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu Hatua za ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 7, 2026 51:04


Karibu usikilize Kipindi  cha Pro_life Utetezi wa Uhai Wawezeshaji kutoka Prolife Tanzania Bw. Godfrey Mkaikuta, Anthon Liepa,  Janet Akkaro na Bi Grace Shayo Mada ni Hatua za ukuaji wa mtoto Tarehe 21 Aprili 2026 L'articolo Fahamu Hatua za ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa. proviene da Radio Maria.

radio maria karibu baada hatua aprili kipindi fahamu
Habari za UN
Nimesahau yaliyopita na naganga yajayo baada ya kuuawa kwa baba yangu - Rwibutso

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 29, 2026 2:51


Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliuawa katika mauaji hayo ya kimbari. Jina la baba huyo ni Emmanuel Turatsinze

Habari za UN
Balozi Ngoga: Manusura wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Rwanda baada ya mauaji ya kimbari

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 27, 2026 2:20


Tweet URLSuala hilo la mchango wa manusura katika kuepusha mauaji kama hayo hayajirudii tena, nililimulika wakati wa mazungumzo yangu ya hivi karibuni na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga ambaye bila kumung'unya maneno alinieleza kuwa, “ wanamchango mkubwa sana kwa sababu kwanza wanapambana na hali ambayo katika hali ya kawaida ya ubinadamu ni ngumu. Chukulia mfano wetu sisi Rwanda walionusurika mauaji na waliotekeleza wanaishi pamoja kwa sababu Rwanda hakuna mgawanyiko wa kikabila wa kwamba kuna baadhi wanaishi mkoa fulani. Wanaishi pamoja katika vijiji hivyo, hivyo wanaenda shule hizo hizo wanaenda hospitali pamoja na wanaishi pamoja. Kwa mtu ambaye amepoteza familia yake nzima na anawajua wauaji walioua familia yake na anaendelea kuishi nao kijijini, ni hali ambayo kwa kweli katika akili ya kawaida unaweza usielewe lakini imetokea Rwanda.”Mwaka huu wa 2026 ni miaka 32 tangu kutokea kwa mauaji hayo ya kimbari. Hivyo Balozi Ngoga ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa Rwanda kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu uliotokea Rwanda (ICTR) akafafanua kwamba, “Baadhi ambao walikuwa ni wadogo wakati huo ambao sasa ni watu wazima, wanaandika hata vitabu kueleza nini kilitokea. Lakini wamekubali kuingia katika mchakato wa maridhiano, kujenga upya taifa la Rwanda."Akaongeza kuwa, "na kama ambavyo aliwahi kusema kiongozi wetu Rais Paul Kagame wakati fulani kwamba wao walionusurika ndio wanacho cha kutoa. Wao ndio wanaombwa watoe zaidi katika kuchangia juhudi za kulijenga upya taifa kwa sababu muuaji unaenda kumuomba nini. Tunashukuru kwamba wamekubaliana na hiyo, hali ambayo katika mazingira ya kawaida ya kibinadamu ni ngumu sana. Lakini kwa miaka yote hii tunakwenda.”

rwanda umoja wana kwa katika wao baada mwaka lakini baadhi kimataifa uhalifu
Habari za UN
Epukeni kutumia droni, asema Mwakilishi wa Katibu Mkuu DR Congo baada ya kuwasili Goma

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 24, 2026 2:55


James Swan, ambaye ni Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, leo Ijumaa amewasili huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza ya kuendeleza juhudi za amani kwenye eneo hilo la mashariki mwa nchi lililogubikwa na vita. Assumpta Massoi na taarifa kamili

congo drc goma umoja droni drcongo baada asema mataifa jamhuri mkuu kidemokrasia
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Waombolezaji wa Kitaalamu wa Kenya walipwa kulia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 21, 2026 8:37


Unawezaje hakikisha kwamba msiba uta hudhuriwa na watu wengi? Baada ya yote, jambo la mwisho unalotaka kutokea unapo aga dunia... ni kuondoka bila shamra shamra yoyote.

SBS Swahili - SBS Swahili
Wiki Hii Afrika: CHADEMA chafungua ofisi zake tena Tanzania baada yakupigwa marufuku

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 7:29


Mahakama ya rufaa ime ondoa marufuku dhidi ya viongozi wa CHADEMA kushiriki katika maswala ya siasa Tanzania.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Historia ya tengezwa baada ya mwanamke kuteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Australia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 14, 2026 14:32


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Australia, mwanamke ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Australia. Waziri Mkuu alitangaza uteuzi wa Luteni Jenerali Susan Coyle mjini Canberra.

Habari za UN
Ukatili wa Kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya waibua wadau, viongozi - UNFPA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 10, 2026 2:55


Baada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Leah Mushi na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Serikali yachukua hatua yakupunguza bei ya mafuta nchini baada ya siku kadhaa za shinikizo

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 13:35


Waziri Mkuu amesema serikali yake imechukua hatua ya kupunguza bei ya mafuta kote nchini, kwa sababu hata kama vita vitaisha mara moja, madhara ya kiuchumi yataendelea.

siku baada habari hatua serikali waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Afueni kwa madereva wanaokabiliwa na matatizo baada ya serikali kupunguza ushuru wa mafuta

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 10:34


Baada ya wiki kadhaa za shinikizo kuhusu kupanda kwa bei ya petroli, serikali ya shirikisho imepunguza kodi ya mafuta kwa nusu.

makala baada serikali
Habari za UN
Kunusuru wanawake wenzangu na jamii Gaza inanipa faraja: Alya Abu Shawish

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 9, 2026 2:57


Alya Abu Shawish, mwanamke aliyeko mstari wa mbele kuondoa hatari ya mabomu Gaza  (OVERNIGHT)Hii leo pia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, imefanyika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo duniani kote iliadhimishwa jana Jumapili. Katika muktadha huo huo ninamualika Anold Kayanda atupeleke Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kumwangazia Alya Abu Shawish, Mwanamke anayefanya kazi katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma ya kutegua mabomu, UNMASakisaidia kuwaweka salama wenzake katika mojawapo ya mazingira hatari zaidi duniani. Karibu Anold.(Taarifa ya Anold)Asante Flora,Hakika Gaza ni moja ya mazingira hatari duniani kwa sasa. Alya Abu Shawish anaposhuka kwenye gari kabla ya kuingia ofis iza UNMAS zilizoko Deir al-Balah katikatimwa Gaza, anavaa jaketi la kujikinga na risasi.Ndani ya ofisi amesimama mbele ya ramani ya kidijitali, akifuatilia mienendo ya timu za wafanyakazi walioko mitaani zilizosambazwa kote katika ukanda huo wa Gaza ili kufanya kazi za kuondoa mabaki ya vilipuzi vya vita katika eneo hilo.Baada ya mipango yote kukamilika ofisini, sasa Alya Abu anaendesha gari akiwa na wenzake kuelekea kazini nje ya ofisi. Anaeleza akisema,(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kazi yangu kama mwanamke katika eneo hili inaonyesha kwamba wanawake wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha usalama na kuleta mabadiliko yanayoonekana, hata katika mazingira hatari na yenye changamoto kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza.”Alya Abu Shawish anaonekana na wenzake mitaani wakifanya kazi. Watoto wanafuata, kwa vyovyote wakitambua kazi muhimu inayofanywa na UNMAS kufanya mazingira yawe salama dhidi ya vilipuzi.Hata hivyo, nyuma ya dhamira hii ya kitaaluma kuna hadithi binafsi inaloakisi hali halisi ya maelfu ya wanawake huko Gaza.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kama mwanamke na mama, nimepitia changamoto nyingi ambazo wanawake wa Kipalestina huko Gaza hukabiliana nazo wakati wa vita hofu, kuhama makazi, uhaba wa mahitaji muhimu, na hali ya kutokuwa na uhakika kila wakati. Kama wanawake wengi hapa, nimelazimika kuilinda familia yangu huku nikikabiliana na hali hizi ngumu.”Licha ya changamoto hizi, Alya Abu Shawish anasema uzoefu wake umeimarisha azma yake ya kuwasaidia wengine na kumhamasisha kufanya kazi katika uwanja ambao mara nyingi huonekana kutawaliwa na wanaume.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Uzoefu huu haukunidhoofisha; uliimarisha azma yangu ya kuwasaidia wengine. Ulinitia moyo kufanya kazi katika masuala ya kuondoa mabomu na usalama na UNMAS uwanja ambao mara nyingi huonekana kuwa wa wanaume. Katika jukumu hili, ninachangia kupunguza hatari zinazosababishwa na mabaki ya vilipuzi vya vita na kusaidia jamii kuishi kwa usalama zaidi.”Wanawake wengine katika timu za UNMAS pia hushiriki katika shughuli za kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabaki ya vilipuzi, ambayo sasa yamekuwa moja ya changamoto kubwa zaidi za kibinadamu huko Gaza kadri uharibifu unavyoendelea kuenea. Kwa Abu Shawish, juhudi hizi hubeba ujumbe unaokwenda mbali zaidi ya kazi kwani inaonesha uimara na mnepo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Wairani-Waaustralia waomba demokrasia baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 3, 2026 11:14


Wairani-Waaustralia wanaelezea hisia mseto kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran, pamoja na mauaji ya Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari: Kiongozi mpya wa Iran kuteuliwa baada ya Ayatollah Ali Khamenei kuuawa

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Mar 2, 2026 5:02


Mchakato unaendelea kuamua ni nani atakaye iongoza Iran, baada ya kuuawa kwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

Habari za UN
“Nitaachia ngazi” WFP baada ya miezi mitatu: Cindy McCain

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 27, 2026 3:05


Kiongozi wa shirika kubwa zaidi la msaada wa chakula duniani ametangaza kujiuzulu. Bi. Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP amesema atajiuzulu wadhifa wake huo  baada ya miezi mitatu ili kuzingatia afya yake, akisema bado hajapona kikamilifu baada ya kupata kiharusi mwaka jana 2025. Flora Nducha na taarifa zaidi

bi umoja cindy mccain afya baada mataifa kiongozi shirika
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: 'Punguza uchochezi' Waziri Mkuu asema baada ya ongezeko ya vitisho dhidi ya wabunge

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 27, 2026 9:08


Kuondolewa kwa dharura kwa Waziri Mkuu kutoka nyumbani kwake mjini Canberra kwa sababu ya tisho la bomu lililolengwa, kumesababisha maonyo ya kuongezeka kwa mazingira ya usalama, ambapo uadui mtandaoni unazidi kujitokeza kama vitisho vya kimwili vyenye madhara makubwa.

canberra makala baada asema waziri mkuu
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo: Wito wa mabadiliko makubwa watolewa baada ya wagonjwa wa afya ya akili kutoroka Sydney

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 21, 2026 11:53


Serikali ya New South Wales inachunguza mazingira yaliyozunguka kutoroka kwa wagonjwa wawili kutoka hospitali moja, ambao siku chache baadaye walidaiwa kuhusika katika matukio tofauti ambapo watu watatu walifariki.

Habari za UN
WHO yaunga mkono kampeni ya dharura ya kutoa chanjo ya polio nchini Malawi baada ya kubainika kwa mgonjwa wa polio

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 20, 2026 3:22


Takribani watoto milioni 1.3 nchini Malawi wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni maalum ya siku nne, kufuatia kugunduliwa kwa mgonjwa mpya wa polio mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Huyu ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa tangu mwaka 2022, wakati virusi vya polio pori vilivyokuwa na uhusiano wa kijenetiki na mlipuko ulioripotiwa nchini Pakistan vilipobainika. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

Habari za UN
MONUSCO yaishukuru Afrika Kusini baada ya kutangaza uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wake nchini DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 9, 2026 2:06


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) umetoa taarifa kwamba umefahamishwa na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa kuwa Afrika Kusini itaondoa vikosi na wanajeshi wake waliobaki ndani ya MONUSCO. Rashid Malekela ameifuatilia kwa kina taarifa hiyo na anaeleza zaidi.

wake congo afrika drc umoja monusco baada mataifa jamhuri ujumbe kidemokrasia
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo:viwango vya riba vyaongezeka baada ya kusitishwa kwa miaka miwili

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 6, 2026 6:36


Benki ya Hifadhi ya Australia imehitimisha mapumziko ya miaka miwili kwa kuongeza viwango vya riba hadi asilimia 15, jambo ambalo limeanzisha mjadala mkali wa kisiasa juu ya kama matumizi ya serikali au mahitaji ya watu binafsi ndiyo yanayosababisha mfumuko wa bei kuendelea. Wakati Mweka Hazina anatetea bajeti na kuashiria mashinikizo ya nje, Upinzani na Kijani wanadai kuwa sera za sasa zinawaadhibu Waustralia wa kawaida na zinaacha mbali njia zingine za kiuchumi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika:Marekani kutathmini upya ushirikiano wake na Uganda baada ya uchaguzi

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 2, 2026 8:44


Kwa maelezo ama habari zaidi elekea kwenye tovuti yetu ya sbs.com.au/swahili.

SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo:Maelfu wanadai fidia baada ya Huduma za Australia kutumia sheria za msaada wa watoto visivyo

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 29, 2026 7:30


Ripoti muhimu imefichua kuwa Service Australia ilikwepa kwa makusudi sheria za malezi ya watoto kwa muda wa miaka sita, ikiwa imezuia ndani kwa ndani malipo kwa zaidi ya wazazi 16,000 ambao walitoa chini ya asilimia 35 ya huduma kwa watoto wao. Wakati shirika hilo lilipinga kuwa sheria ilileta "matokeo yasiyotarajiwa" kwa kuulazimisha walezi wakuu kulipa wale wenye majukumu kidogo ya huduma, Ombudsman aliamua kwamba kupuuza sheria si chaguo kwa watumishi wa umma.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika:Watanzania bado wanakabiliwa na athari za baada ya uchaguzi wa hivi karibuni

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 29, 2026 8:52


Watanzania bado wanakabiliwa na athari za baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, huku wanahabari wakizuiwa kuripoti usimulizi mbele ya tume ya uchunguzi. Makubaliano kati ya Congo na Marekani kuhusu madini yana dosari kubwa.

congo afrika baada hivi marekani uchaguzi
Habari za UN
15 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 15, 2026 11:58


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkataba wa Kimataifa wa kulinda viumbe hai wa baharini kwenye Bahari Kuu na ujumbe wa Mzee Ali Haji, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Katiba na Sheria katika Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nchini Tanzania kuhus umuhimu wa mkataba huu.Kesi inaendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ mjini The Hague, kuhusu madai kwamba Myanmar ilitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Rohingya. Mawakili wa Gambia wameiambia mahakama hiyo kuwa jeshi la Myanmar lilichochea ghasia kupitia kauli za chuki, likiwaita Warohingya “mbwa Waislamu”kabla ya mashambulizi ya mwaka 2017.Baada ya zaidi ya siku 1,000 za mzozo, Sudan inakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa njaa na uhamaji wa watu duniani. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, leo linaonya kuwa operesheni zake za kuokoa maisha ziko hatarini kutokana na uhaba mkubwa wa ufadhili.Mamilioni ya raia wa Uganda leo walipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na serikali za mitaa huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR likisisitiza umuhimu wa wakimbizi zaidi ya milioni moja nchini humo kubaki bila kuegemea upande wowote wa kisiasa. Shirika hilo limeonya kuwa kushiriki katika siasa kunaweza kuwakosesha wakimbizi usalama, kupelekea mateso kutoka nchi zao za asili, au kuathiri ulinzi na hali yao ya hifadhi nchini Uganda.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na ya neno "MLOWIMA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
14 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 14, 2026 9:50


Hii leo jaridani tnaangazia uchumi wa dunia unaoendelea kukua ila maendeleo katika kupata kazi zenye ubora na staha yamekwama, pia tunaangazia afya ya uzazi nchini Uganda na homa ya bonde la ufa (RVF) kwa mifugo nchini Tanzania. Licha ya uchumi wa dunia kuendelea kukua, maendeleo katika kupata kazi zenye ubora na staha yamekwama, huku mamilioni ya wafanyakazi wakisalia katika lindi la umaskini na ajira zisizo rasmi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani (ILO)iliyotolewa hii leo huko Geneva Uswisi.Baada ya kuhitimu shahada ya udaktari nchini mwake Uganda, huko Afrika Mashariki, Daktari mmoja alibaini kuwa hiyo haitoshi, bali alienda mbali zaidi kubuni kifaa kinachosaidia wajawazito hasa wale wanaoishi maeneo ya ndani zaidi kufahamu hali ya afya ya watoto wao tumboni, na hivi sasa kifaa hicho kinaelekea kupata hakibunifu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Hakibunifu, WIPO.Mfumo wa kubaini mapema homa ya bonde la ufa (RVF) iliyobuniwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania imewezesha wizara, wakulima, na madaktari wa mifugo kuchukua hatua za mapema, hivyo kulinda maisha na mali dhidi ya ugonjwa huo unaoshambulia mifugo na binadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

uganda tanzania fao ilo kazi umoja hayo hii wipo afya baada wanawake mataifa ajira shirika afrika mashariki rvf
Habari za UN
Mscan yawezesha wajawazito vijijini Uganda kupata huduma za uchunguzi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 14, 2026 2:33


Baada ya kuhitimu shahada ya udaktari nchini mwake Uganda, huko Afrika Mashariki, Daktari mmoja alibaini kuwa hiyo haitoshi, bali alienda mbali zaidi kubuni kifaa kinachosaidia wajawazito hasa wale wanaoishi maeneo ya ndani zaidi kufahamu hali ya afya ya watoto wao tumboni, na hivi sasa kifaa hicho kinaelekea kupata hakibunifu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Hakibunifu, WIPO. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.

uganda umoja wipo baada wanawake mataifa afrika mashariki
SBS Swahili - SBS Swahili
Makala leo:wazazi wapata afueni baada ya serikali kupunguza gharama za vituo vya malezi ya watoto

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 8, 2026 5:45


Wazazi wanaopeleka watoto kwenye vituo vya malezi wana uhakika wa kupata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu za wiki, bila kupitia mchakato wowote wa uthibitishaji. Ruzuku hii itagharimu karibu dola milioni 430 kwa kipindi cha miaka minne ijayo, lakini serikali inasema mamia ya maelfu ya familia zitafaidika.

makala watoto baada serikali wazazi
SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika:Wanafunzi 300 waachiliwa baada ya kutekwa nyara shuleni Nigeria

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 8:41


Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

SBS Swahili - SBS Swahili
Australia yafafanuliwa:Afya ya akili katika ujauzito na baada ya kujifungua

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 24, 2025 9:51


Karibu mmoja kati ya Waustralia wanne hawatafuti msaada wanapopata matatizo ya afya ya akili wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua. Wataalamu wanasema kwamba taarifa zilizotolewa na Gidget Foundation zinaonyesha ukosefu wa kuelewa dalili na ishara, pamoja na unyanyapaa unaoendelea kuhusu suala hili.

Habari za UN
Mradi wa FAO wajenga mnepo baada ya mafuriko nchini Rwanda

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 3:16


Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo,kwa wakati wmingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii. Kufahamu zaidi kuhusu mradi huo ungana na Sheilah Jepngetich

japan rwanda umoja maji baada mataifa serikali ajira lengo shirika
Habari za UN
21 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2025 12:02


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mbinu bunifu za kilimo cha kakao nchini Peru, na mradi wa miundombinu wa kupunguza athari ya mafuriko na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii nchini Rwanda.Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi.Katika msitu wa Amazon upande wa nchi ya Peru, jamii za watu wa asilizimeonesha namna mbinu bunifu za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Yote haya yanakuja wakati dunia ikiendelea kujadili mustakabali wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa COP30 unaoendelea huko Belém, Brazil.Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo, kwa wakati mwingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

amazon japan brazil peru rwanda drc kakao umoja congo drc hii maji katika monusco baada mataifa jamhuri serikali ajira lengo shirika novemba kidemokrasia
Habari za UN
Hatua ndizo zinazohitajika baada ya mkutano wa dunia wa Maendeleo ya Kijamii - Diana Pasha

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 12, 2025 2:18


Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka. Flora Nducha na taarifa zaidi

Habari za UN
Nashukuru FODDAJ imenirejeshea matumaini ya maisha - Mnufaika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2025 3:16


Nchini Kenya, shirika la kiraia la FODDAJ  au la Forum for Women Development, Democracy and Justice linatekeleza kivitendo lengo namba 3 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la afya bora na ustawi ambalo pamoja na mambo mengine linataka manusura wa ukatili wa kijinsia wapatiwe huduma sio tu za afya bali pia za kijamii. Je linafanya nini, Sheilah Jepngetich amezungumza na mwakilishi wa shirika hilo.Ni Salome Gatakaa Araka, Mwakilishi wa FODDAJ ambaye katika mazungumzo nami anaanza kwa kuelezea walianzia wapi harakati zao.  Akisema Policy and Advocacy anamaanisha Sera na Uchechemuzi.“FODAJ ilianza na uundaji wa ufahamu yaani policy and advocacy kumaanisha kwamba kuwe  kutengwa kwa fedha za kutengeneza mahali pa waathiriwa kuishi, na pia kusisitiza ufahamu wa kutetea wale ambao wametengwa. Katika kata ya Kajiado, tumesukuma sera za GBV ili kuimarisha juhudi za kuzuia waathiriwa kuumia zaidi.”Pamoja na kukabili ukatili wa kijinsia, nikataka kufahamu iwapo wanawejengea wanawake uwezo wa kujitegemea.“FODDAJ imekuwa mstari wa mbele katika katika kupaza sauti za wanawake na wasichana, na pia kuhimiza akina mama kuweka akiba za vikundi, kushirikiana na kusaidiana ili kujikimu kiuchumi. Tumehimiza akina mama kuweka akiba kwa vikundi vya maendeleo, kushirirki mafunzo ya ujasiriamali na kushirikiana na wengine kwa pamoja. Na pia wanafundishwa mambo tofauti kama vile kutengeneza nywele , kusoma na kuandika na pia na kuhesabu.”Maneno ya Bi. Araka si matupu kwani Geraldine Ndayisenga mkazi wa Kitengela ambaye ni manusura wa ukatili na mnufaika wa miradi ya FODDAJ anafunguka.“Mimi ni mmoja wa wale waliopitia dhuluma. Nilijua kuhusu FODDAJ kupitia rafiki yangu. Nikasaidiwa, nilipata matibabu, nikapata ushauri (counselling) kwa mwezi mmoja. Baada ya hapo nikajiunga na mafunzo ya kutengeneza nywele, makucha na ushonaji. Mafunzo hayo yamenisaidia sana, sasa najisikia niko huru na nina furaha kuwa sehemu ya jamii tena. Fodaj Foundation imenishika mkono na kunionesha namna bora ya kuishi hapa Kitengela. Wamenisaidia kwa mambo mengi, na kwa kweli maisha yangu yamebadilika kwa njia chanya sana.”Nikarejea kwa Bi. Araka, kufahamu iwapo wana ushirikiano na serikali na mashirika ya kiraia. Akisema Post Traumatic anamaanisha kiwewe baada ya dhuluma.“Kwa kushirikiana na serikali na mashirika mengine ya kiraia, waathirika wanapatiwa msaada kwa ajili ya huduma za afya. Mfano wale waliobakwa au kupigwa, hupata matibabu kwa vipimo au dawa. Aidha, waathirika wa kimawazo wanapewa msaada wa kisaikolojia ili iwasaidie kuondokana na madhara ya post trauma ambayo wamepitia.