POPULARITY
Wakati raia wa Haiti Giovanni Rotschild alipowasili Mexico mwaka 2022 baada ya safari ndefu isiyo na uhakika kutoka nchi mwake kulikosheheni ghasia, hakufahamu mtu yeyote wala hakuzungumza kabisa lugha ya kispanyola. Lakini msaada alipata msaada kumwezesha kujenga upya maisha na kupata jamii mpya. Flora Nducha na maelezo zaidi.
Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.
Walipoanza Men Men Men The Podcast mwishoni mwa mwaka 2019, Michael na Nadia walikuwa wawili tu – na maikrofoni. Hakukuwa na studio ya kitaalamu, wala mpango mkubwa. Kulikuwa tu na wazo moja: kuanzisha mazungumzo ya kweli kuhusu afya ya akili ya wanaume.Hawakujua kama kuna mtu atawasikiliza. Hawakujua kama kuna yeyote atajali kuhusu maongezi haya. Lakini leo hii, baada ya miaka mitano na episodes 100, imekuwa wazi kuwa podcast hii imekuwa zaidi ya wao wawili. Imebeba sauti za uchungu, ushindi, maswali magumu, na ukweli ambao mara nyingi husalia kimya.Katika episode hii ya kipekee, Michael na Nadia wanarudi walipoanzia – si kwa kurudia, bali kwa kutafakari. Wanazungumza kwa uhalisia kuhusu safari yao, changamoto walizokumbana nazo, na yale ambayo bado ni vita ambayo wanapigana nayo hadi leo. Wanajiuliza: Je, bado wana kiu ya mabadiliko kama siku ya kwanza? Je, bado wanaamini kuwa mazungumzo haya ni muhimu katika jamii?Jibu lao ni NDIO. Na kama wewe pia bado unaamini hivyo, basi episode hii ni kwa ajili yako pia.
Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi, UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.
Katika jamii inayomtazama mwanaume kama mhimili wa familia na mtafutaji mkuu wa riziki, changamoto za kiuchumi zimewasukuma wengi kutafuta njia mbadala za kujikimu. Moja ya njia hizo ni kamari.Lakini je, kamari ni suluhisho la kweli kwa changamoto za kiuchumi, au ni mtego mwingine unaozidi kudidimiza maisha ya wanaume wengi?Katika episode hii, tunachambua kwa kina ongezeko la michezo ya kubahatisha miongoni mwa wanaume wa Kitanzania. Tunaangazia sababu, athari, na uhalisia wa maisha yao baada ya kuingia katika mzunguko wa kamari.Tupo na Tumaini Maligana, mshauri wa michezo ya kubahatisha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10, ambaye anatuongoza katika mjadala huu kwa maarifa, ushuhuda, na maonyo yenye msingi wa uhalisia wa maisha. Karibu usikilize, tafakari, na shiriki. #MenMenMenPodcast #KamariNaMaisha #ChangamotoZaMwanaume #UkweliWaKamari
Wanasema ndoa ni ndoto, lakini vipi ikiwa inageuka kuwa ndoto mbaya... na unaamka mahakamani?
Rekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi imefanyika.” Anasema Mkrugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA.Kwake, mwandishi wa habari nguli, anaona moja ya maeneo ambayo ni muhimu yafanyiwe kazi ni kuzipa nafasi taarifa zinazohusu shughuli kubwa zinazofanywa na wanawake katika jamii kote duniani kwani licha ya wanawake kuwa na michango mikubwa katika mustakabali wa ulimwengu, taarifa zao hazipewi kipaumbele cha kutosha.“Mimi kwa mtazamo wangu naona wanawake wamefanya kazi nyingi lakini hazijarekodiwa. Rekodi ni chache sana.” Anasisitiza na kuongeza, “kwa hiyo tunatakiwa kuanza kurekodi vile vitu ambavyo vilifanywa na wanawake wale wa miaka 30 iliyopita lakini hata na hawa wanaokuja kizazi kipya.”Dkt. Rose Reuben anahamasisha pia vyombo vya habari kuangazia masuala mengine ambayo kwa namna moja amba nyingine yanaigusa jamii moja kwa moja na hiyo ni kusema yanamgusa mwanamke moja kwa moja kama vile mabadiliko ya tabianchi, tekonolojia, “na vitu vingine ambavyo vinaweza kuathiri usawa wa kijinsia na hali ya mwanamke duniani.”Aidha kiongozi huyo wa TAMWA anatoa wito kwa wanawake popote walipo kutumia nyenzo zinazopatikana katika jamii yao kuhakikisha wanapata taarifa, wanasambaza taarifa na kujipatia maarifa.
Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.
Mwaka 1995 huko Beijing, China kwenye mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake lilipitishwa Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji, ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kusongesha haki za wanawake. Mwaka huu wa 2025 ikiwa ni miaka 30 baadaye, tathmini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa nchi zimesonga mbele katika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake, kuanzia kuharamaisha ubaguzi kwenye ajira hadi mipango ya kuhimili tabianchi inayozingatia jinsia. Lakini bado kuna vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisiasa na ndio maana wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu wa 2025 kipaumbele ni kusongesha uwezeshaji, haki na usawa. Ni katika kumulika harakati hizo, Assumpta Massoi anakupeleka Singida nchini Tanzania kwenye maadhimisho yaliyoambatana na ujengeaji uwezo.
Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia ambapo wamemchagua kiongozi wa tume ya Umoja wa Afrika AU kati ya wagombea watatu, lakini pia mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda dhidi ya jeshi la serikali FARDC na ambao sasa wameudhibiti mji wa Bukavu huko Kivu kusini mashariki mwa DRC, mapigano ya nchini Sudan, siasa za Uganda na pia kwenye nchi za Afrika Magharibi. Lakini pia zoezi la ubadirishanaji wa mateka huko Gaza
Kutana na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi. Kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu imekuwa mtihani mkubwa kwa wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi. Kupitia video ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Flora Nducha anafafanua zaidi katika Makala hii.
Rais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa. Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa.Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.
Akili Mnemba au AI inakuja kwa kasi kubwa sana na kubadilisha mwenendo wa walimu na wanafunzi darasani. Inaleta fursa za kipekee kama kufundisha kwa njia ya kibinafsi na upangaji wa masomo wenye ufanisi zaidi. Lakini pamoja na zana hizi, changamoto zimeibuka: kutegemea sana teknolojia hii, masuala ya kimaadili, na kupungua kwa ujuzi wa kusoma kwa kina. Walimu wanajifunza jinsi ya kuendesha mabadiliko haya, wakiwaonesha wanafunzi jinsi ya kutumia AI kama mshirika wa kufikiri badala ya njia ya mkato ya kuuliza na kunakili. Ubunifu na kufikiri kwa kina vinabaki kuwa ujuzi muhimu zaidi, ambao hakuna teknolojia inayoweza kuchukua nafasi yake. Je, walimu wana mawazo gani? Assumpta Massoi anakupeleka Paris, Ufaransa kusikia mazungumzo ya walimu wawili wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba kwenye ufundishaji.
Sekta ya mitumba inauwezo wa kuchangia mabilioni ya fedha katika mapato ya taifa, pamoja na kutoa maelfu ya ajira katika mataifa ya bara Afrika na ulaya. Kulinga na utafiti wa Oxford Econimics mwaka uliopita; 2024, sekta ya mitumba pekee ina dhamani ya dola bilioni 8 na imetoa ajiri ya idadi ya zaidi laki moja na elfu 60 kwa vijana nchini Msumbiji, Ghana na Kenya.Lakini hata hivyo wanaharakati wa mazingira wanasema baadhi ya nguo hizo za mitumba zinazoletwa Afrika zinachangia katika uchafuzi wa mazingira.Hili kufahamu Zaidi mwandishi wetu George Ajowi alizuru soko la Gikomba na kutuandalia makala yafuatayo .
Nchini Liberia, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD umejengea uwezo watu wenye ulemavu wa kuona na kuwawezesha kuongeza vipato na vile vile uhakika wa kupata chakula. Simulizi ya Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM mkoani Mwanza nchini Tanzania, inaelezea zaidi.Tuko kaunti ya Lofa, kaskazini kabisa mwa Liberia, magharibi mwa Afrika, tunakutana na Hawa Kamara, yeye ni mlemavu wa kutoona. Yeye pamoja na wenzake wa chama cha watu wenye ulemavu wa kutoona hapa Lofa, wanathibitisha kuwa unapoamua kufanya kitu, hakuna kinachokuzuia.Kupitia mradi wa Mabadiliko ya kilimo kwa wakulima wadogo na uchechemuzi wa kilimo biashara au STAR-P, mavuno ya mpunga kwenye shamba la kikundi hicho, yameongezeka kwa asilimia 300.Hawa anasema, “Mwanzoni hatukuwa na kitu kabisa. Tulihangaika sana kulima mpunga. Lakini baada ya IFAD kutufikia katika maisha yetu na kutusaidia, mambo yalianza kubadilika. Walitupatia pembejeo na mbegu za ubora wa juu kuanzisha mashamba. Tulitumia mbegu hizo kupanda kwenye mashamba yetu Bakadu.”Awali walilima ekari 1.2 tu, lakini baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa vya kilimo wameweza kulima hadi ekari 4.3.Mavuno ya mpunga yameongezeka. Wanasagisha mashine, kiasi cham chele wanauza na ziada ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Hawa akiwa kwenye shamba lake la mpunga anasema,“Kabla ya STAR-P nilijihisi nimepotea na mpweke. Lakini sasa ninaweza kulima mwenyewe shambani, na ninaweza kujihudumia mimi na pia familia yangu. Zamani niliacha shule. Lakini baada ya kuanza mradi huu, nimerejea shuleni na ninataka kuwa mhasibu mkubwa duniani.”
Karibu katika Kipindi cha Maswali ya Imani ukiwa nami Frateri Samson Peter Tibianus, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Katoliki Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Nini maana ya maneno Ee Bwana Sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na Roho yangu itapona? L'articolo Fahamu maana ya Maneno Ee Bwana Sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na Roho yangu itapona. proviene da Radio Maria.
Teknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaendelea kusambaza msaada wa kibinadamu ili kurejesha matumaini ya waathirika wa kimbunga Chido kilichotokea tarehe 15 Desemba mwaka jana nchini Msumbiji na kuziacha taabani jamii za majimbo ya Cabo Delgado, Nampula na Niassa. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba duniani kote kuna vijana bilioni 1.2 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24. Idadi hii ni saw ana asilimia 16 ya wakazi wote wa dunia. Kama hiyo haitoshi, idadi hiyo ya vijana inatarajiwa kufikia bilioni 1.3 ifikapo mwaka 2030, yaani miaka mitano ijayo. Lakini changamoto ni kwamba bado serikali nyingi hazijaweza kutumia wingi wa idadi hii kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Kwa hali hiyo baadhi ya vijana wameamua kutumia fursa na kujiongeza ili vijana wenzao waweze kufahamu wanachopaswa kufanya ili SDGs zifanikiwe ifikapo 2030. Miongoni mwao ni Paul Siniga, kijana kutoka Tanzania ambaye mwezi Oktoba mwaka huu alikuweko kwenye makao makuu ya UN jijini New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu. Assumpta Massoi alitaka kufahamu kwa kina ni hatua zipi alichukua hadi kufika aliko sasa.
Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox's Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza kuhusu vifaa mbalimbali ikiwemo msumeno wa mabomba, spana na kadhalika.ILOMradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox's Bazaar nchini Bangladesh.Na ndoto yake ni kwamba nikihitimu masomo nitakwenda kuungana na kaka yangu kwenye duka lake linalounza vifaa vya ujenzi. Nataka niwe mjasiriamali kama yeye, nijitegemee na nisaidie familia yangu. Siku hizi kwenye nyingi zilizoendelea na hata hapa Bangladesh wasichana wanafanya aina zote za kazi.Wanaweza kufanya kazi ngumu kama wanaume, nami nataka kuwa hivyo.Video ya ILO inamalizika mnufaika huyu amekamilisha kufunga bomba na sasa maji yanatoka, na mkufunzi anatumia maji hayo kunawa mikono.Malengo namba 4, 5, na 8 ya SDGs yanatekelezwaMradi huu ulizinduliwa mwezi Septemba mwaka 2023 ukifadhiliwa na…
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa kituo cha afya kiko karibu na sisi kwa hiyo si lazima tena kulipa nauli kwa ajili ya mashahidi. Sasa ni rahisi kwetu kusajili watoto wetu baada tu ya kuzaliwa. Hata mume wangu hajui kama niko naandikisha hapa wakati huu. Anadhani nitapata tu chanjo ya mtoto lakini nitakapomuonesha cheti cha kuzaliwa cha mtoto wetu, atafurahi sana. Hatalazimika tena kwenye ofisi za serikali na kulipa faranga za Burundi 10,000 kwa ajili ya usafiri. Ni faida kwetu.” UNICEF pia inasaidia katika kuandikisha watoto ambao walichelewa kusajiliwa katika umri mdogo na hiyo imesaidia sana watoto walio katika mazingira magumu kupata huduma za msingi za kijamii ambazo hapo awali walikuwa nazikosa kwa kuwa hawana utambulisho wowote unaotambuliwa kiserikali. Katika mkoa wa Bugabira jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, tunakutana na Jean Baptiste Mutaniyonka baba wa mtoto mwanafunzi Karerwa Olivier anaeleza changamoto walizokuwa wanakumbana nazo hapo awali kabla ya huduma ya usajili kuletwa karibu. “Mara ya kwanza nilipoenda kwenye ofisi za mkoa kusajili ilikuwa imefungwa kwa sababu ya sikukuu. Mara ya pili, mashahidi walitutaka kuwapatia faranga za Burundi elfu kumi nila mmoja. Sikuwa na fedha hiyo kwa hiyo ilibidi tuahirishe hiyo miadi ili tutafute pesa.” Mzazi huyu ili kuonesha namna cheti cha kuzaliwa kilivyo na umuhimu mkubwa katika maisha ya mtoto nchini Burundi anasema, “bila cheti cha kuzaliwa mtoto hana haki ya kupata kupata huduma ya bure katika hospitali. Tulikuwa tunaondoka bila bila kupata matibabu. Na katika hali kama hiyo tuligeukia katika tiba za asili au katika maduka ya dawa. Ilikuwa hivyo hivyo katika shule. Watoto wangu walikuwa wanarejeshwa nyumbani kwa kukosa cheti cha kuzaliwa.” Huyo ni Olivier Karerwa mwenyewe, mtoto wa Jean Mutaniyonka. Olivier amesajiliwa kupitia mradi huu wa UNICEF na anasema anataka kuwa mwalimu atakapohitimu masomo yake. Anne Rwasa ni bibi anazungumzia ilivyo rahisi sasa kumuhudumia mjukuu wake akisema, lakini leo mtoto awe na homa au kuumwa tumbo tunakimbia katika kituo cha afya ambako anapata huduma ya bure ya afya.” Mradi huu wa UNICEF Burundi wa kuunganisha taarifa za watoto za serikali ili ziweze kusomeka pia katika taasisi nyingine kama vile vituo vya afya umepata pia usaidizi kutoka kwa kamati ya UNICEF ya Uingereza.
Kijana Mtanzania Gibson Kawago hivi karibuni kupitia kampuni yake ya WAGA inayoshughulika na uvumbuzi wa teknolojia zinazolenga kupambana na uchafuzi wa mazingira ya ulimwengu, ametangaza kuanzisha vifaa vinavyotumika kuchaji magari ya umeme lengo likiwa ni kuwasaidia watu wa eneo lake, Afrika Mashariki kupata huduma ya kuchaji magari yao ili wahame kutoka katika matumizi ya mafuta ya kisukuku kama petroli na dizeli. Lakini je ana majibu gani kwa wale ambao bado hawaoni faida ya ya magari ya umeme kwa mazingira ikiwa bado vyanzo vya umeme ni chafuzi? Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Gibson anafafanua.
Dr. Lwidiko Mhamilawa ameibuka kwenye studio zetu siyo kwa ajili ya kutuambia jinsi maisha ni magumu (tulishajua hiyo), bali kutufundisha jinsi ya kufurahia safari ya maisha – hata pale unapotaka kutupa lapa na kusema, “Inatosha!” Unajua, kuwa mwanaume ni kama kuwa kocha wa timu isiyoelewa mchezo: kila mtu anakutegemea wewe, lakini hakuna anayekuelewa!
Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto. Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa wameathirika kisaikolojia.Zavadi Mbambu ni miongoni mwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto lukuki ikiwemo mapigano. Akisema stress, anamaanisha msongo.“Unakuwa na wanafunzi wanaokuwa na msongo wa mawazo kutokana na jambo ambalo wanaishi, na hata mauaji. Kuna wale ambao hata wameua wazazi wao , hata familia yao yote. Na kwa hao wanafunzi wanapoingia shuleni , wanakuwa kama hawako ndani, fikra zao zinakuwa mbali . Lakini kupitia mafunzo nimewaelewa , na tumejua namna gani ya kuishi nao. Na tayari mabadiliko yameanza kuonekana.”Pacifique Kyakimwa, mmoja wa wanafunzi anasimulia mkasa mmoja.“Kuna mwenzetu aliyekuwa na tatizo, yaani tukiwa ndani ya shule, alikuwa anacheka, yaani anatusumbua hadi hatumwelewi mwalimu. Lakini tangu wameanza kufundisha hili somo, wameanza kuelewa . Ameanza kuwa na akili inayotumika vizuri. Mafunzo haya yamefika wakati tunahitaji , na imetusaidia sana.”
Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao. Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na migogoro na tatu teknolojiaUNICEF inasema yote haya ni changamoto na fursa ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo katika zama zijazo.Rafif mtoto mkimbizi wa ndani ameandika barua kutoka Palestina ambako vita imetamalaki, anasema“Ninatoka mjini Gaza na sasa nimefurushwa hadi Kusini mwa Gaza. kama watoto Ni haki yetu kuishi kwa usalama na kujenga mustakbali bora”Kutoka mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki kwa Steven akimulika afya“Na nianaandika kwenu kutoka Tanzania. Kwenye jamii yangu watoto wanaugua kila wakati , kwa nini? Huu ndio mustakbali wangu je unasikiliza?”Nako Congo DRC mitihani ni mingi, Andrea anasema“Nataka kushuhudia dunia ambayo kila mtoto anapendwa, dunia ambayo amani inashamiri ni raha na faraja. Napenda kuona hasira zinageuka na kuwa mazungumzo”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono suti hizo za watoto katika ujumbe wake amesema Katika Siku ya Watoto Duniani tunasherehekea washiriki wachanga zaidi wa familia yetu ya kibinadamu. Lakini leo pia ni wakati wa kutambua changamoto kubwa zinazowakabili watoto katika ulimwengu wetu uliogawanyika sana, wenye misukosuko na mara nyingi ulioshamiri ukatili.”Ripoti ya UNICEF imetoa wito wa kuwekeza katika elimu, miji endelevu na yenye mnepo kwa watoto, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, huduma muhimu na mifumo ya msaada wa kijamii na pia teknolojia iliyo salama kwa watoto ili kupambana na mzigo wa changamoto zinazowakabili.
Sadick Ali ni mchekeshaji, muigizaji, mfanyabiashara... na zaidi ya yote—ni baba. Sasa, kama wanaume wengi duniani, wazo la kuwa baba kwa mara ya kwanza lilimjia kama mshangao wa mitihani ya darasa la saba: hauko tayari, lakini unajidanganya kuwa utaweza! Na kama ulivyotegemea, Sadick alijikuta akikabiliana na mchanganyiko wa hisia—uoga, shauku, na sintofahamu isiyokuwa na GPS. Lakini kubwa zaidi, aligundua ukweli mchungu: hata uki-google kila kitu, hakuna njia ya kujiandaa kikamilifu kwa "daddy duties." Na ukifikiri unajua, mtoto wako atakutengenezea changamoto mpya—au diapers zitakutengenezea! Karibu katika Men Men Men The Podcast, ambapo Michael, Sadick, na Nadia wanazama kwa kina (na kwa vicheko) kwenye changamoto na baraka za kuwa baba kwa mara ya kwanza. Hii ni safari inayochanganya furaha, machungu, na maswali kama: “Mbona mtoto hajalala bado?”
Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 , kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti. Katika hotuba yake mbele ya washiriki wa mkutano huo ulioanza leo huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan hadi tarehe 22 mwezi huu wa Novemba, Bwana Stiell amesema kwa kadri madhara ya mabadiliko ya tabianchi yalivyo dhahiri ni lazima kukubaliana mwelekeo mpya wa ufadhili kwa miradi ya kukabili na kuhimili.Amehoji, mnataka bei za vyakula na nishati iongezeke zaidi? Je mnataka nchi zenu ziendele kushindwa kushindana kiuchumi? Je mnataka dunia yetu iendelee kukosa utulivu na kugharimu maisha adhimu?Amekumbusha kuwa janga la tabianchi linaathiri kila mkazi wa dunia kwa njia moja au nyingine.Bwana Stiell amesema nimekanganyikiwa kama mtu mwigine yeyote kwamba mkutano mmoja wa COP hauwezi kuleta marekebisho abayo kila taifa linahitaki. Lakini iwapo majibu yenu kwenye maswali hayo ni HAPANA, basi ni hapa pande zote zinahitaji kukubaliana jinsi ya kuondokana na zahma hii.Hivyo amesema, “katika nyakati ngumu, kukiwa na majukumu mazito, sitegemei matumaini na ndoto. Kinachonihamasisha ni stadi na azma ya binadamu. Uwezo wetu wa kuanguka na kuinuka tena na tena, hadi tunapotimiza malengo yetu.”Amekumbusha kuwa mkataba wa tabianchi ndio mchakato pekee ambapo wanaweza kupatia majawabu janga la tabianchi na kuwajibishana kwa wale wanaokwenda kinyume.Ametaka washirika kuonesha stadi zao kwenye COP29 na pande zote zishinikize makubaliano ya ufadhili kwa tabianchi la sivyo kila nchi itagharimika.
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kinachotupeleka jijini Havana Cubaambapo kongamano la kimataifa la Kiswahili limeng'oa nanga likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu.Miongoni mwa habari kubwa Umoja wa Mataifa hii leo ni uwajibikaji unasakwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wapalestina na waisraeli, na pia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeweka bayana gharama za kiuchumi na hata kiafya zilizofichika zitokanazo na mifumo ya uzalishaji, usafirishaji na ulaji wa chakula. Lakini kubwa zaidi nakupeleka Havana, Cuba kupata kwa mahtasari mazungumzo ya Flora Nducha na mmoja wa washiriki.Mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba na fursa ni yake Profesa Juan (Huani) Jacomino (Hakumino) raia wa Cuba ambaye ni Mwalimu wa Kiswahii katia chuo kikuu cha Havana Cuba anayeshiriki Kongamano la Kiswahili lililofunguliwa leo akitoa wito kwa raia wa Cuba na wa nchi zingine kuhusu umuhimu wa kukumbatia Kiswahili. Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana.Katika video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ombeni anasimulia jinsi waasi wa FDLR mashariki mwa DRC walivyowakamata msituni."Tulikuwa vijana watanoFDLR walitukamata na kutupeleka msituni. Maisha ilikuwa ngumu sana na hatukuweza kutoroka"Kazi wanatumikishwa bila mshahara na zaidi ya yote."Kila saa ni mateso, kazi mingi bila malipo."Alitumikishwa msituni kwa miaka minane, akionesha makovu ya vipigo alivyopatiwa."Tuliteseka sana, tulitumikishwa kwa muda wa miaka minane, tukachapwa viboko, tuliumizwa sana na kubaki na majeraha"Lakini siku moj aliweza kutoroka. Akiwa Kibirizi akamweleza mkubwa wake ya kwamba.." Siku moja nikamwambia mkubwa wangu naenda kusalamia rafiki yangu, wakati huo tukapata nafasi ya kutoroka."Katika harakati hizo akakutana na MONUSCO. Anasema kwamba, "Njiani nikakutana na wanajeshi wa MONUSCO, nikainua bunduki juu na kujisalimisha, nikisindikizwa na mkubwa wao nikaeleza kile tulichopitia"Sasa Ombeni anashiriki programu za kumjumuisha tena kwenye jamii, DDR-S inayondeshwa na MONUSCO huko Beni, jimboni Kivu Kaskazini.
Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika. Tuko Adale, mji wa ndani zaidi wa jimbo la kati mwa Somalia, Galmudug. Hapa zaidi ya kaya 2,000 sasa zina huduma ya maji safi na salama, kufuatia ukarabati wa kisima cha maji.Salada Mohammed Omar, yeye ni mfugaji na ni shuhuda wa mradi huu uliotekelezwa na serikali ya jimbo la Galmudug kwa ufadhili wa shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na UNICEF.“Tulisafiri muda mrefu kuteka maji, lakini sasa kisima kiko karibu na makazi yetu, tunapata kwa urahisi maji ya kupikia, kufulia na kufanyia usafi.”Video ya UNICEF inaonesha raia na ngamia wakiwa kisimani. Mohammed Yusuf Dirshe ambaye ni kiongozi wa kijamii hapa Adale anasema “awali hakukuwa na tanki la maji wala pampu. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kupata maji kwa ajili ya mifugo. Lakini sasa unaona hawa ngamia wanatoka umbali wa hadi wa kilometa 35.”Issack Mohammed, kutoka Kituo cha Amani na Demokrasia mdau wa mradi huu anaeleza kilichofanyika.“Ukarabati ulihusisha kujengea juu matanki, kuweka pampu inayotumia nishati ya jua, na kioski cha maji ili wavulana, wasichana na wanawake waweze kuteka maji kwa urahisi.UNICEF inasema mradi huu unarejesha uhai hapa Adale, kwa kuhakikisha watoto wanakua wakiwa na afya njema, jamii zinastawi na mbinu za kujipatia kipato zinakuwa endelevu.
Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng'oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili. COP16 kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye pia anategemewa kuhudhuria siku za mwishomwisho za mkutano huu, amewaeleza wajumbe akisema, “mkakati wa Kimataifa wa Bioanuwai unaahidi kurekebisha uhusiano na dunia na mifumo yake ya ikolojia. Lakini hatuko kwenye mstari. Jukumu lenu katika COP hii ni kubadilisha maneno kuwa vitendo.”
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka mmoja wa vita nchini Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji.Katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike tunaelekea nchini Tanzania kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo, kujifunza kutoka mtoto mmoja wa kike kuhusu haki za watoto.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mwaka mmoja wa vita katika ukanda wa Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji na ndio makala yetu ya leo ikisimuliwa na Assumpta Massoi.
Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani. Tunasherehekea miaka 150 ya shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU, tunatambua umuhimu wa moja ya mifano ya mapema zaidi ya ushirikiano wa kimataifa. Ni Masahiko Metoki, Mkurugenzi Mkuu wa UPU katika ujumbe wake wa siku hii adhimu akiongeza kuwa..“Kile kilichoanza na wanachama 22 sasa inajumuisha nchi 192, kikionesha uthabiti wa ushirikiano wa kimataifa.”Miaka 150 wamekumbana na changamoto, vita, majanga mabadiliko ya kasi ya teknolojia ya kidijitali. Lakini wanafanya nini?“Leo hii UPU inaongoza juhudi za kufanya huduma za posta kuwa za kisasa na bora. Inatoa fursa kwa nchi kushirikishana ufahamu, kusaka majawabu na kukabili changamoto za sasa. Moyo wetu wa ushirikiano ndio umetusaidia kugeuza vikwazo kuwa fursa na kufanya huduma za posta kuendana na dunia inayobadilika.”Na zaidi ya yote…“Awali tuliona ongezeko la mawasiliano ya kidijitali kuwa ni tishio kwani kiwango cha utumaji wa barua kwa njia ya posta kilipungua. Lakini sasa tunaona fursa za utajiri. Mtandao mkubwa wa UPU umesaidia kupanuka kwa huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao, huduma za kifedha, kijamii na kidijitali, ikihakikisha ufikiaji wa kila mtu duniani hata wale walio ndani zaidi hawaachwi nyuma.”Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, UPU imehimili changamoto kwa kuwa bunifu, jumuishi na kusongesha ushirikiano wa kimataifa.“Katika siku hii muhimu, hebu na tusherehekee na tupongeze kazi ya shirika la Posta duniani ya kuondoa umbali na kuunganisha dunia.”
Mnamo mwaka wa 2020, Umoja wa Mataifa ulipotimiza miaka 75 tangu kuanzishwa, pamoja na maadhimisho wakati huo ulimwengu ulianzisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu matarajio na hofu kuhusu zama zijazo. Huo ndio ukawa mwanzo wa mchakato ambao hatimaye, miaka minne baadaye, hivi majuzi umefanyika Mkutano wa Zama Zijazo. Lakini kwa kuwa mikutano na mipango mingine ilishafanyika katika siku za nyuma, je huu nao unaweza kuwa ni mvinyo wa zamani katika chupa mpya kwa hiyo hautakuwa na mchango mkubwa chanya kwa dunia? Kuyajadili haya na mengine mara baada ya mkutano huo wa zama zijazo kukamilika jijini New York, Marekani, Anold Kayanda wa Idhaa hii aliketi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva aliyeshiriki mkutano huo.
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..
Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni. “Niliacha shule darasa la nne ilikuwa mwaka 2022, kwasababu shuleni walikuwa wananirejesha nyumbani nikalete ada. Sasa nikifika nyumbani wazazi wanasema hawana”Huyo ni David Tumaini kijana mwenye umri wa miaka hivi sasa 16 mmoja wa wanafunzi waliolazimiika kukatiza masomo miaka miwili iliyopita katika shule ya msingi ya Soyosoyo kutokana na umasikini. Kwa miezi kadhaa alihaha kusaka njia ya kuendelea na masomo."Nilikaa nyumbani kwa muda wa miezi mitano, wakati wenzangu wanakwenda shule na ni siku za masomo na wewe uko nyumbani. Hii inakufanya ujihisi kama wewe si mtu muhimu.”Hisia kama hizo na mustakbali wa watoto hao ndio kilicholisukuma shirika la UNICEF kuanzisha mradi wa “Elimisha mtoto” likishirikisha wizara ya elimu ya kenya na wadau wengine ili kuhakikisha watoto kama David wanarejea shuleni. Elizabeth Waitha ni afisa elimu wa UNICEF.“Tuliweza kubaini Kaunti 16 ambazo zilikuwa na watoto zaidi ya 10,000 ambao wanaendi shuleni, na hii ilikuwa ni kwa shule za msingi tu. Na tukaangalia ni jinsi gani ya kuhakikisha mazingira bora ya kusoma kwa watoto waliosajiliwa kwenye mradi. Na tumeweza kuwasaidia zaidi ya wanafunzi milioni kwa vifaa vya shule na pia kwa waalimu vifaa vya kuandikia kama chaki, kalamu na vingine.”Na ndipo David akasikia kuhusu mradi huo,“Nilipata taarifa kutoka kwa walimu ya kwamba kuna mradi ambao unawasaidia watoto walioacha shule ili warehjee shuleni kuendelea na masomo. Sasa nilipokuja shuleni nikaambiwa wewe tutakusajili katika huu mradi wa msaada , ndipo nikaweza kurejea masomoni, hadi sasa nipo shuleni kwa sababu ya msaada huu. Vitu ambavyo nilipewa ni pamoja na mkoba wa madaftari, vitabu, kalamu na vifutio.”Hii imemrejeshea David matumaini ya ndoto yake“Mimi nikimaliza kusoma nataka kuwa Daktari ili kusaidia wagonjwa. Na katika kusaidia wagonjwa mshahara nitakaolipwa ntajisaidia mwenyewe na pia kusaidia familia yangu”Kupitia mradi huu mbali ya vifaa umewezesha zaidi ya watoto 256,000 kurejea shuleni na bado wanaendelea na masomo.
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama nchini DRC, na suala la elimu katika malengo ya maendeleo endelevu tukimulika wanafunzi Kilifi nchini Kenya. Makala tunasalia na mada hiyo hiyo ya elimu na mashiani inamulika sheria za kibnadamu.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wameelezwa jinsi ushindani wa uchimbaji kupita kiasi na biashara ya maliasili huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unavyozidi kuchochea mapigano kwenye eneo hilo, madini kama vile dhahabu na Koltani.Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni.Makala leo inatupeleka Paris Ufaransa katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kuzungmzia juhudi za shirika hili katika kuhakikisha kwamba wanafunzi walio katika maeneo ya migogoro wanaendelea na masomo yao na wenzao waliohamishwa wanapata ufikiaji wa elimu juu katika nchi zilizowapokea.Katika mashinani fursa ni yake Mirjana Spoljaric Egger, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya chama cha Msalaba Mwekundu ICRC akitoa wito wa kutafakari machungu yanayowakumba waathirika wa mizozo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum. Leo mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia siku ya nne, miongoni mwa wahutubiaji ni Tanzania. Kabla ya kupanda katika mimbari ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuketi na mwakilishi wa taifa hilo katika mjadala huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuzungumza naye masuala kadhaa ikiwemo mzigo wa madeni kwa nchi zinazoendelea na pia nafasi ya wanawake katika nyanja ya kimataifa. Lakini kwanza alitaka kufahamu Waziri Mkuu Majaliwa amekuja na ujumbe gani kutoka Tanzania kwenye mjadala huu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu nchini Lebanon, Imran Riza, akizungumza kutoka mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kwa njia ya video amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo kwamba katika Lebanon kipaumbele kwa sasa ni kuhakikisha usitishaji mapigano wa haraka ili kukomesha mateso zaidi ya raia na uharibifu. Bwana Riza amesisitiza tena wito kwa jamii ya wahudumu wa kibinadamu kwa nchi zote kutumia ushawishi wao kusaidia katika kupunguza machafuko kwa dharura.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women inaangazia athari kubwa za janga la kibinadamu linaloongezeka kwa wanawake na wasichana wa Sudan, wakiwemo milioni 5.8 ambao ni wakimbizi wa ndani.Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi imetoa wito kwa mamlaka ya Haiti na jumuiya ya kimataifa kufanya zaidi kulinda watu na kuzuia mateso zaidi na kwamba hicho ndicho kinapaswa kuwa kipaumbele. Takwimu za hivi karibuni kutoka Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa takribani watu 3,661 wameuawa nchini Haiti tangu Januari mwaka huu.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa hii leo Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa UNGA79 umeng'oa nanga hii na tunakutana na mdau anayepigia chepuo malengo ya maendeleo endelevu hasa haki katika lengo namba 4 la Elimu Bora.Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 umeanza leo New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Antonio Guterres amesema anashawishika kwamba kuna kweli mbili chungu katika zahma zinazokumba dunia hivi sasa: Mosi-Hali ya dunia si endelevu na hatuwezi kuendelea kama ilivyo na pili; changamoto zilizozoko zinatatulika. Kinachohitajika ni kuweko kwa mfumo wa kimataifa wenye uwezo wa kutatua changamoto hizo.Rais Joe Biden wa Marekani ambaye amesema ni hotuba yake ya mwisho mbele ya Baraza hilo kama Rais wa Marekani na kwamba anatambua changamoto zinazokabili dunia ikiwemo vita, tabianchi na demokrasia. Lakini ana matumaini kuna suluhu kwa kuzingatia yote waliyofanya pamoja kwa miongo iliyopita.Huko Lebanon shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaomboleza vifo vya watumishi wake wawili waliouawa huko Bekaa Mashariki baada ya kombora lililorushwa na Israeli kuangukia makazi yao jana Septemba 23. UNHCR imerejelea wito wa Katibu Mkuu wa UN ya kwamba mashambulizi yakome.Na katika mashinani tunamsikia kijana mmoja aliyefika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa Zama Zijazo uliofunga pazia lake jana, ana wito wa kuwapa viongozi wa ulimwengu ambao wanashiriki katika Mjadala Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa ambao wenyewe umefungua pazialake leo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti. Kupitia video ya Monusco iliyochapishwa mtandao wa X, John Matemuli, mwandishi wa habari wa kituo hicho cha Redio na Televisheni Beni, kilichositisha matangazo kwa karibu miaka mitano, anafafanua jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya kujengwa upya kwa kituo hicho.“Miaka mitano bila Radio na Televisheni ya kitaifa ya Kongo (RTNC) mjini Beni ilikuwa ya machafuko sana. Kulikuwa na wakati ambapo tulikuwa tukifanya kazi hata kutoka juu ya mti, unaweza kuamini! Tulihisi kwamba kulikuwa na hitaji, wananchi na hata baadhi ya viongozi walihisi vivyo hivyo.”Ezechiel Kambale, mkazi wa Beni naye pia anaeleza furaha yake.“Ulipita muda mrefu tangu redio hii kuwa hewani. Lakini sasa nashukuru kwamba wamerudi. Kuna tofauti kubwa ikilinganishwa na zamani, kwa sababu leo, hata kama niko mbali na mji, bado nayapata mawimbi ya redio kana kwamba nipo hapa mjini.”Tulimrudia John na kumuuliza kilichokuwa tofauti kuhusu kituo hicho hasa kabla ya msaada wa MONUSCO.“Kazi ilofanywa hapa imewaridhisha wananchi. Leo, tuna ofisi za usimamizi. Tuna studio za kisasa za televisheni. Tuna studio ya redio kwa ajili ya kutengeneza vipindi vyetu. Tuna chumba cha habari kilicho na vifaa vya kutosha. Tulikumbana na matatizo ambayo yalihitaji msaada katika ngazi zote, lakini MONUSCO ilitupatia vifaa, ambavyo sasa vinaturuhusu kufanya kazi katika hali bora.”
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
Huko Paris, Ufaransa kumekamilika mkutano wa wiki moja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ukipatiwa jina Wiki ya Kujifunza Masuala ya Kidijitali au Digital Learning Week ambapo hoja ya Akili Mnemba kudhibiti habari potofu na za uongo imepatiwa kipaumbele.Mkutano huo ulimulika mchango wa teknolojia ya kidijitali katika elimu inayolenga maendeleo badala ya kuyadumaza. Mathalani ni kwa jinsi gani mifumo ya kidijitali inaweza kukabiliana na taarifa potofu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Simon Wanda, Afisa Programu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni amefafanua nafasi ya teknolojia kwenye kukabili taarifa hizo.“Mifumo hii inaweza kuchambua na kutathmini yale yanayowekwa kwenye matandao na kutambua taarifa za uongo au za kupotosha.”Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Doris Mwikali, Mwanasheria na mtetezi wa elimu kutoka Kenya. Tukamuuliza maoni yake kuhusu nafasi ya teknolojia za kidijitali kwa vijana."Ninafahamu kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi kampuni za mitandao ya kijamii zinavyopambana na habari potofu na za uongo. Lakini nadhani kuna zana mpya za akili mnemba zinazotumika na baadhi ya kampuni, kuhakiki taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa haitakuwa na mchango mkubwa ikilinganishwa na kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua jukumu la kudhibiti habari potofu kwenye majukwaa yao, Bado kuna jukumu kubwa kwa akili mnemba katika uhakiki wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, na hiyo imefanywa na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali."Nikarejea kwa Bwana Wanda na kumuuliza maoni yake kuhusu maendeleo ya akili mnemba au AI na ujumuishaji wa sauti kutoka pande zote wakati wa kusongesha AI.“Zipo jamii nyingi zetu za kiafrika kama wamaasai wa Kenya na Tanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na elimu ya asili kuhusu kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni elimu inayofaa kutopuuzwa katika makuzi haya ya teknolojia. Hivyo, hili ni suala la kuhoji sana hasa tunapozingatia kwamba maendeleo katika teknolojia yasiegemee eneo moja la elimu tu, ambayo ni elimu ya magharibi, na kupuuza elimu ya kiasili, ambayo ni tunu.”
Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) nchini Tanzania unawapatia vijana wakulima wadogo ujuzi na rasilimali zinazohitajika ili kuboresha uzalishaji wa chakula na kujenga uchumi endelevu wakati huu ambao madhara ya El niño [EL NINYO] yanayosabisha ukame na mafuriko yamekuwa dhahiri. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Hali ya El Nino huwa changamoto kwa wakulima kwani hawana uhakika wa mavuno ya kile walichopanda. Hali ni tofauti kwa mkulima kijana Coletha Kiwenge anayeendesha kilimo biashara kupitia mradi huo wa WFP wa Vijana Kilimo Biashara (VKB) nchini Tanzania. Yeye amefanikiwa kuvuna mazao mwaka mzima, licha ya changamoto za hali ya hewa zinazotokana na El Niño.“Pamoja na mradi huu wa Vijana Kilimo Biashara, unaofadhiliwa na Shirika la mpango wa chakula duniani na mtekelezaji ‘Farm Afrika', tumejifunza yafuatayo: - Moja, matumizi ya mbegu bora, na kwa msimu huu tumetumia mbegu bora au mbegu chotara za alizeti Pamoja na mtama Pamoja na kufadhiliwa hizo mbegu ambazo zina mazao mengi.”Kutokana na madhara ya hali ya hewa na tabianchi, WFP imeelekeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima hao.“Lakini pia tumechimbiwa kisima na Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP, kisima hiko ni lengo na madhumuni kwaajili ya kilimo cha bustani, na kwasasa kwenye bustani yetu tumeanza na nyanya na ziko shambani. Lakini kwenye kikundi cha KAPATA, tunaendelea na upando mbalimbali.”
Mgonjwa wa kwanza wa polio kubainika Gaza huko Mashariki ya Kati baada ya miaka 25 ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi 10. Mtoto huyo na mama yake pamoja na familia nzima wamekuwa wakihamahama na hivyo akakosa chanjo dhidi ya polio. Amri za Israeli za kutaka wapalestina wahame mara kwa mara sasa zinaleta madhara kwa asilimia 90 ya wakazi wa Gaza. Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Afya, WHO, la kuhudumia watoto, UNICEF na la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA wamejipanga kupatia chanjo watoto 640,000 huko Gaza wiki chache zijazo. Lakini mipango hiyo ikiendelea, Assumpta Massoi kupitia mahojiano yaliyofanywa na Ziad Tarib wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Ukanda wa Gaza, anakuletea makala inayojikita kwenye simulizi ya mama wa mtoto aliyepooza, changamoto na ndoto zake.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, umeboresha huduma za afya kwenye Gereza Kuu la Beni, jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika kwa kujenga zahanati iliyoboresha sit u mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya bali pia huduma za matibabu kwa wafungwa. Cecily Kariuki anasimulia zaidi(Taarifa ya Cecily Kariuki)Video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, zamani Twitter inaonesha jengo la zahanati hiyo likiwa la rangi nyeupe na buluu, wahudumu wa afya wakiwa na makoti meupe, masafi kabisa, halikadhalika mazingira ya kituo hiki.Miongoni mwao ni Dkt. Michel Muhindo ambaye hawezi kuficha furaha yake.(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Msaada huu wa zahanati ni ahueni kubwa kwetu sisi tunaofanya kazi hapa, na hata kwa wafungwa, kwa sababu wanapatiwa huduma nzuri ya uchunguzi, na tunafanikiwa kutoa majibu mazuri na tunawatibu ipasavyo. Tunakadiria kwamba kweli ilikuwa inahitajika.”Je, hali ilikuwa vipi kabla ya maboresho haya?(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Kabla ya kupata huduma hii ya matibabu, yaani zahanati hii, kulikuwa tu na vyumba ambavyo tulikuwa tunawaweka wagonjwa kwa ajili ya uchunguzi. Lakini hakukuwa na maabara, wala ofisi nzuri za ushauri. Tulikuwa na wakati mgumu sana, kulikuwa na kelele. Ilibidi kuwa makini sana ili kuweza kusikiliza wafungwa wagonjwa.”Sasa wafungwa wanapata huduma kwa nafasi kabisa..(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Hii inapunguza muda wa huduma kwa wafungwa katika zahanati hii. Sasa kuna maeneo maalumu yaliobainishwa vizuri. Tunaweza kusema: hiyo ni maabara, hicho ni chumba cha uchunguzi wa wagonjwa, hicho ni chumba cha daktari, kwa wauguzi, pamoja na mapokezi ambapo tunaweza kuwakaribisha wafungwa wanaokuja kwa ushauri wa matibabu.”
Kwa wakimbizi, kurudi nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha wakimbizi kujenga upya na kuanza maisha yenye tija. Mmoja wa wakimbizi hao ni KABURA Emelyne, ambaye sasa anamiliki nyumba na ni mfanyabiashara. Bosco Cosmas anatupa habari kamili…Tangu mwaka 2017, takriban wakimbizi 250,000 wa Burundi wamepewa msaada wa kurejea nyumbani kutoka nchi jirani ya Tanzania. Wengi kama Emelyne hawakuwa na chaguo jingine ila kuanza maisha upya. Lakini kwa ufadhili wa (UNHCR) kwa ushirikiano na (KOICA) sasa wanaishi kwa tija.Emelyne anasema, “nilifurahi sana kuvuka mpaka wa Manyovu na kurejea nchini mwangu Burundi. Ninapoona maendeleo mapya na miji inayostawi, najihisi nimeridhika. Nilikimbilia Tanzania mwaka 2015 na nikarejea mwaka 2021.”Sasa Emelyne ameanza kujishughulisha na kilimo na kuuza mihogo, kutengeneza mafuta ya mawese, na kufuga sungura kwa ajili ya nyama na mbolea. “Najisikia furaha ninapowalisha sungura wangu kwa sababu wananiwezesha kupata mbolea. Nashukuru kwamba kupitia mauzo ya sungura nilikodi kipande cha ardhi kwa ajili ya kulima na nikapata fedha za kuanzisha biashara yangu ya mihogo na mafuta ya mawese.”Msaada kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) unawawezesha waliorejea kujenga upya na kuanza maisha mapya. Kwa mujibu wa Emelyne, "UNHCR walitukaribisha na kutusaidia. Kwa msaada wa kifedha tuliopewa, tulinunua ardhi hii, tukatengeneza matofali na kujenga kuta za nyumba yetu. Kisha tukapokea mabati, nguzo, madirisha, na milango ili kukamilisha nyumba. Kama ningalikuwa bado kwenye kambi, nisingeweza kupiga hatua kubwa kiasi hiki.”