Podcast ya dakika 10-45 ipo based on twitter ambapo kutafanyika interview kwa njia ya simu ya mkononi ambapo yataulizwa maswali tofauti tofauti kwa mmoja wa watu ambae atabahatika kuwepo kwenye kipindi kitakachokujia kila siku ya Ijumaa. Katika Phone call fotty ataongea na Influencers,wafanyabiashara,wasanii na watu wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii.
Kila mtu ana story yake kwenye maisha na haijalishi ni wakati mgumu kiasi gani unapitia kwenye maisha yako tambua kila mtu anapitia magumu yake. Lucas Malembo ni mwanzilishi wa "Malembo Farm" inayojishughulisha na maswala yote ya kilimo, Malembo ana amini kua kilimo kinaweza kutengeneza ajira kwa vijana wengi na vile vile kuikuza nchi yetu ki uchumi. Wengi tumemzoea Lucas Malembo akiongelea kilimo mara kwa mara ila kwenye episode hii amegusia mambo aliyopitia kwenye maisha yake kupelekea kuzaliwa kwa "Malembo Farm". Ni matumaini yangu utafurahia mahojiano haya na kujifunza mambo mengi
Kwenye maisha ya kila siku watu napitia mambo mengi ikiwemo kutafuta hela, stress za familia, stress za kazi n.k na mitandao inabidi iwe sehemu ya mtu kupata furaha hata kama siku yake ilikua mbaya kiasi gani. Kupitia mtandao wa twitter kuna kijana anaitwa "Big0047" yeye huwa anatengeneza memes kwa njia ya picha na watu wengi wamekua wakifurahishwa na ubunifu wake. Tumeongea kuhusu mtandao uliompa yeye umaarafu na story nyingine kibao kumuhusu yeye. Natumaini utaenjoy mahojiano haya.
Episode hii nimeifanya special kwa ajili ya valentine kilichonifanya niwachague Mr & Mrs Mrusi ni kwa sababu wapenzi hawa twitter ndo iliwakutanisha kwa mara ya kwanza na baada ya hapo kufikia maamuzi ya kuoana, kwenye Episode hii tumezungumza mambo mengi kuhusu mahusiano na ndoa vile vile tumegusia maisha ya wawili hawa ndani ya ndoa. #PHONECALLBYFOTTY
Geoffrey Lea ndio amehusika kwenye Episode hii ya 2 msimu wa 2 ni mchambuzi na mtangazaji wa michezo kutokea Efm, Kwenye Episode hii tumeongea mambo mengi kuhusu mpira wa miguu lakini vile vile mpira wa kikapu sababu yeye ni mpenzi wa kikapu pia vilevile ukiachana na hayo tuliongea kwa jinsi gani Mama ake (M/Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) amekua na mchango mkubwa sana katika safari yake hii. Kama wewe ni kijana ambae unajihusisha na jambo lolote lile katika Episode hii utajifunza kutokukata tamaa na kufanikisha lengo ulilokua nalo. #PHONECALLBYFOTTY
Baada ya mapokezi mazuri ya msimu wa kwanza uliokua na takribani Episodes 10 ambapo wahusika walikua...@MiriamMkanaka @mpambazi @abdulazackabdul @Mudimabiriani @princessfeona @mcnikawalamar @lusakowakwanza @georgeAmbangile @shamiraMshangama @fredKavishe. Tulichukua break ya week mbili na Tarehe 3/7/2020 tunarudi tena kwa Ajili ya msimu wa 2 Asante kwa Support yako kuanzia Episode ya kwanza msimu wa 1 mpaka sasa tunaelekea Msimu wa 2.
Fred Kavishe mmoja wa waanzilishi wa TOT BONANZA (Tanzania On Twitter) bonanza kubwa linalowakutanisha watumiaji wa twitter sehemu moja ili kuweza kujuana zaidi na kuenjoy, Kwenye Episode hii tumeongelea mambo mengi sana kuhusu Bonanza hili kuanzishwa kwake,Changamoto na mambo mengi sana. Vilevile tulipiga story na Fred juu ya safari yake ya Kupunguza uzito kutoka kilo 105 mpka kilo 65 ambayo ndo anamaintain sasa ivi. #PHONECALLBYFOTTY
Shamira Mshangama ni Mkurugenzi mtendaji na Muanzilishi wa Tasisi ya (Mwanamke na Uongozi) ni tasisi isiyokua ya kiserikali (NGO), yenye kazi ya kuhamasisha wasichana wenye Umri kuanzia miaka 12 kushiriki nafasi mbali mbali za uamuzi na kugombea Uongozi. Kwenye Episode hii tumeongea mambo mengi sana kuhusu Wanawake na changamoto gani wanazipata kwenye jamii yao. Vile vile nilipata nafasi ya kupiga story na Shamira kuhusu maisha yake binafsi.
George Ambangile ni mchambuzi wa mpira na mtangazaji wa michezo wa WASAFI TV kipindi cha (Sports Arena & Sports Court) kwenye episode hii tumeongelea kuhusu safari yake ya uchambuzi na changamoto gani alizopitia mpaka kufika hapo alipofikia leo ukiachana na hayo tumeongea juu ya support aliyopata kutoka kwa familia yake wakati anapambania ndoto yake hii. Ana followers wasiopungua Elfu 14 kwenye mtandao wa twitter.
Lusako Wa Kwanza ni Ambassador wa TZnaVijana ambapo ni taasisi ambayo DIRA yao ni "Kuwa na Vijana wenye uwezo wa kujisimamia na kukabiliana na changamoto mbalimbali" Tumeongea mambo mengi sana kwenye Episode hii kuhusu scandal zake za kutuma Ujumbe kwenye DM za wakina dada na pia tumeongelea maisha ya kijana wa kitanzania kwenye mambo ya Mahusiano. Ana followers wasiopungua Elfu 80 kwenye mtandao wa Twitter.
Mcnika wa Lamar mimi napenda kumuita "SOCIAL MEDIA GURU" huyu jamaa nimeanza kuzijua kazi zake kabla ya kupata nafasi ya kumjua yeye. Anandaa memes ambazo kama hujawai kuweka kwenye status yako basi umeona kwenye status ya ndgu au rafiki ako, Tumeongea kuhusu uandaaji wake wa memes na pia kuhusu dili za matangazo mitandaoni sababu ana followers zaidi ya laki 2 instagram na Zaidi ya laki 1 Twitter.
Princess Feona ni Model,Fashionista na muanzilishi wa THE NEW FACE SERVICES Ni moja ya watu ambae alizua gumzo sana Twitter Tanzania baada ya kuweka picha ambazo zilileata sintofahamu na maswali mengi kwa watu, tumelizungumzia hili lakini pia kuhusu mambo ya Modeling na changamoto anazozipata na Je Corona imeathiri kiasi gani shughuli zake. Kwenye akaunti yake ya Twitter ana Followers wasiopungua Elfu 35
Mpishi maarufu wa biriani anaejulikana kama Mudi Mabiriani ndo nilipata nafasi ya kufanya nae interview na kupiga nae stori hususani kuhusu biashara yake ya chakula aina ya Biriani. Kama ww ni mfanyabiashara au ni kijana tu mpambanaji basi amini una mengi ya kujifunza kupitia hii Episode. Tumeongelea juu ya Marketing anayoifanya ya biashara yake na pia kwa nini aliamua kujiajiri hali ya kuwa alikua ameajiriwa. Kwenye mtandao wa twitter ana Followers wasiopungua Elfu 20
Katika Episode hii nipo na mtaalam wa kupigia promo Samaki aina ya Dagaa na pia ni mtu wa kuweka wazi Maparody kwenye mtandao wa twitter yani watu wanaotumia Identity ambazo sio zao ili kuweza kujipatia Follows, Nimepiga nae story kibao bila kuhasau scandal yake ya kuzusha msiba na kula pesa za rambirambi. Kwenye mtandao wa twitter ana followers wasiopungua Elfu 60.
Interview na mtumiaji wa twitter anaejulikana kwa jina la Mpambazi moja ya vijana ambae ndo alikua kama Special Apearance (T.O.T bonanza 2020) tanzania on Twitter na watu wengi walikua wanatamani kumuona baada ya kuwa anainteract na mambo aliyokua akiyafanya kumpa umaarufu twitter, Ana followers wasiopungua Elfu 10 na account yake inazidi kukua kadiri siku zinavokwenda tumeongea kuhusu safari yake ya Dubai ambayo ilileta Gumzo kubwa ambapo aliendakutembea na pia mambo mengi juu ya mapokezi aliyoyapata twitter.
Miriam Mkanaka anajulikana twitter kama @miriammkanaka ni mwandishi,Motivational speaker na moja ya wakina dada wenye ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa twitter ana followers zaidi ya elfu 90 na wanazidi kadri siku zinavozidi kwenda. Kwenye Episode hii tumezungumzia jinsi gani Account yake ya Twitter imekua ikimuingizia pesa kwa matangazo anayokua akiyatweet na pia mambo kadhaa kuhusu mtandao wa twitter. Na uhakika utafurahia Mahojiano haya...ASANTE