POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapema kwa Wote katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika kwenye jukwaa la kimataifa la Akili Mnemba na Tabianchi jijini Shanghai na kutoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mifumo ya tahadhari za mapema inayotumia akili mnemba ili kuzuia majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo amesema "tahadhari lazima zifikie kila mtu aliyeko hatarini kwa lugha wanazoelewa na mifumo ya mawasiliano wanayoweza kuiamini."Kesho Julai 18 ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, huko Geneva, Uswisi hii leo mashindano ya 18 ya Nelson Mandela ya Mahakama ya Kimataifa ya Kuigiza yamefikia kilele kwa timu ya Chuo Kikuu cha Midlands State kutoka Zimbabwe kuibuka mshindi ilihali Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya kimeshika nafasi ya pili.Hii leo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na marafiki wa mpira wa miguu au kabumbu, wamezindua kampeni ya mwaka mmoja ya Dunia Moja, Mchezo Mmoja, Lengo Moja kwa lengo la kutumia mpira wa miguu kama kichochea cha kuimarisha afya ya akili kwa vijana, tukio linalofanyika siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanaume. Akizungumza mapema kabla ya tukio hilo Sahira Al Nahari, ambaye ni Kiongozi kijana mchechemuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs amesema, "kwa hiyo, mpira wa miguu una mengi ya kutufundisha. Tunapokabiliwa na janga la kimataifa, hebu tuzielekeze fikra zetu kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Tunapotazama kinachotokea viwanjani, tunajifunza nidhamu, ustahimilivu, na jinsi ya kuinuka tena baada ya kupoteza jambo muhimu sana."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana tunamulika jinsi gani vijana waliojiendeleza katika stadi ya akili mnemba au wengine wanaita akili unde, kwa kiingereza Artificial Intelligence au AI, wanarahisisha maisha ya jamii. Na tunamuangazia kijana Kalebu Gwalugano kutoka Tanzania, Muasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Neurotech iliyoanzishwa mwaka 2022. Kijana huyu ni Mhandisi wa AI na akiwa Dar Es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki, amezungumza na mwenzetu Japhael Jambo. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Stadi za Vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema kuwezesha vijana kufikia uwezo wao kamili kunahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu na mafunzo jumuishi yenye ubora. Ametambua mchango wa vijana kote duniani kwamba wanaendelea kutoa mchango mkubwa kama wabunifu, viongozi na mawakala wa mabadiliko katika kujenga jamii zenye usawa, ustahimilivu na maendeleo endelevu hata hivyo mabadiliko ambayo dunia inapitia sasa yakichochewa na maendeleo ya teknolojia za kidijitali, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na pengo la usawa yanahitaji vijana kuwa na ujuzi mpya unaowawezesha kushindana na kunufaika na fursa zinazojitokeza.Ingawa mwaka 2025 duniani kiwango cha chanjo kwa watoto kiliongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, kiwango cha chanjo bado kiko asilimia moja chini ya kiwango cha mwaka 2019, kikiwa kimeendelea kubaki ndani ya kiwango finyu tangu mwaka 2009. Hayo ni kwa mujibu wa makadirio ya kila mwaka ya mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO na la kuhudumia watoto, UNICEF kuhusu viwango vya kitaifa vya chanjo.Na ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR inazitaka pande zinazohusika katika vita nchini Sudan, pamoja na serikali na kampuni zinazofanya biashara ya Gum Arabic, gundi inayotokana na aina fulani ya miti ya Acacia kuhakikisha shughuli zao zinaendana na sheria za kimataifa na hazichangii kuendeleza mzozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendelo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo limeendesha midahalo ya amani na utatuzi wa migogoro kwa vijana, lengo, ni kuimarisha amani kwa Maendeleo Endelevu.Siku nne tu baada ya shambulio kubwa la Urusi dhidi ya Ukraine, usiku wa kuamkia leo kwa saa za Ukraine wakazi wa Mji Mkuu, Kyiv kwa mara nyingine tena wamekumbana mashambulizi yaliyofanywa na Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Matthias Schmale, amesisitiza akisema, "haiwezi kurudiwa mara nyingi vya kutosha kwamba sheria za kimataifa za kibinadamu zinataka hatua zote zinazowezekana zichukuliwe ili kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia." Mbali na mji mkuu, mwishoni mwa wiki mashambulizi ya mabomu katika mji wa Sumy yaliwaua raia kadhaa na kuwajeruhi makumi ya wengine, wakiwemo watoto. Miji mingine kama Dnipro, Kherson, Kyiv, Zaporizhzhia na mingine pia ilikumbwa na vifo na majeruhi wengi miongoni mwa raia pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia, hali iliyokatiza upatikanaji wa huduma za msingiHakuna dawa au mwanasesere anayefikia mtoto bila kufanyiwa kwanza uchunguzi au majaribio ya kina kuthibitishwa ni salama, lakini akili mnemba au AI imefikia watoto kupitia kusoma, urafiki au maswali binafsi ya msingi bila hata mtu mmoja kujiuliza athari mbaya za mfumo huo kwa watoto, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa siku mbili kuhusu usimamizi wa akili mnemba ulioanza leo huko Geneva, Uswisi. Hivyo amesema, “hakuna mtoto anayepaswa kugeuzwa majaribio ya akili mnemba isiyodhibitiwa. Kwa kuendeleza kazi inayofanywa na Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na wadau wengine, leo ninatoa wito wa kupitishwa kwa Ahadi ya Usalama wa Watoto katika Matumizi ya akili mnemba, yenye kanuni tatu rahisi kwa mfumo wowote wa AI unaoweza kufikiwa na watoto.”.Na taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salama. Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tunaangazia fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo au kwa lugha ya kiingereza Internship hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Rashid Malekela kutoka Mwanza Tanzania, ambaye aliomba na kupata fursa hiyo anazungumzia na Leah Mushi wa Idhaa hii kueleza ni nini faida yake.Mashirika ya misaada nchini Ukraine leo Alhamisi Julai 2 yameongeza juhudi za kutoa msaada kufuatia ongezeko kubwa la mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Urusi usiku wa jana, yakiwemo yale yaliyolenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kuwa miongoni mwa mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa dhidi ya mji huo.Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa zama za sasa Ashwini K.P ameonya kuwa ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, ubaguzi dhidi ya jamii za pembezoni, na aina nyingine za kutovumiliana zinazohusiana na misingi hiyo bado vimejikita kwa kina katika ngazi zote za michezo duniani. Kwenye ripoti yake kwa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu, mtaalamu amesema michezo ina uwezo wa kukuza ujumuishi, usawa na mshikamano wa kijamii, lakini bado inaendelea kuakisi na kuendeleza mifumo ya ubaguzi wa rangi na kimaeneo unaoshuhudiwa katika jamii kwa ujumla.Na huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania kumeanza mdahalo wa siku mbili wa vijana na amani ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na mmoja wa washiriki anatoa maoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa kingono.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea na harakati za kutoa msaada wa dharura kwa Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo jana Jumatano Juni 24, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 164 pamoja na uharibifu mkubwa katika mji mkuu, Caracas, na maeneo ya jirani. Matetemeko hayo mawili yenye ukubwa wa 7.2 na 7.5 katika kipimo cha Richter yametokea ndani ya muda wa chini ya dakika moja, yakiharibu nyumba, hospitali, barabara na miundombinu mingine muhimu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi wa mabaharia duniani, akionya kuwa ongezeko la migogoro na mivutano ya kisiasa linaweka maelfu ya wafanyakazi wa baharini katika hatari wakati wakiendelea kuhakikisha biashara na usafirishaji wa bidhaa duniani vinaendelea. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mabaharia, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Juni, Katibu Mkuu amesema karibu asilimia 90 ya bidhaa na mahitaji muhimu duniani, ikiwemo chakula, dawa na nishati, husafirishwa kwa njia ya bahari.Na maandalizi ya Mkutano wa 15 wa Afrika Kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, AfIGF utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Ghana yameanza ambapo maoni ya wadau yatakusanywa ili kuweka mazingira salama ya matumizi ya intaneti barani Afrika na hatimaye duniani. Vijana na watoto kutoka nchi mbalimbali wamekutana jijini Nairobi Kenya kuandaa mawazo yao na mmoja wao ni Sheryl Christine Adhiambo kutoka taasisi ya Legal Sisters ya nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hivi karibuni Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI, UNAIDS kupitia ripoti yake mpya limeonya kuwa kupungua kwa ufadhili wa kimataifa na uwekezaji mdogo katika huduma za kinga dhidi ya Virusi vya UKIMWI, VVU kunaweza kufuta mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI duniani.Katika hatua za mwitikio wa kitaifa, wiki iliyopita, Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania, TACAIDS kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo imeendesha warsha ya siku tano kuanzia Juni 15 hadi 19 kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wa asasi za vijana na wawakilishi wa vijana katika utetezi wa masuala ya VVU na Afya ya Uzazi. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Leo katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, viongozi wa dunia wanakutana katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Virusi vya UKIMWI VVU, na UKIMWI kujadili mafanikio na changamoto za mapambano dhidi ya janga hilo tangu mwaka 2021. Mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka mitano unalenga kupitisha Azimio jipya la Kisiasa litakaloelekeza hatua za dunia katika kukabiliana na UKIMWI kwa miaka mitano ijayo.Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women, limeonya kuwa matumizi ya akili mnemba au AI yanaongeza hatari ya ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana duniani. Utafiti wa mifumo 133 ya AI umebaini kwamba asilimia 44 ilikuwa na upendeleo wa kijinsia, huku asilimia 26 ikiwa na ubaguzi wa kijinsia na rangi kwa pamoja.Na Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hatua za kujikinga dhidi ya Ebola zimeimarishwa katika Gereza Kuu la Bunia ambako zaidi ya wafungwa 2,000 wanaishi katika mazingira ya msongamano mkubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO kanda ya Afrika, kwa ushirikiano na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamejenga kituo maalum cha muda cha kutenga wagonjwa wa Ebola.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Wakati dunia ikikabiliwa na ongezeko la uhalifu wa kupangwa, biashara haramu ya binadamu na matumizi ya dawa za kulevya, mwanamke kutoka Afrika Mashariki amepewa jukumu kubwa la kusaidia kuongoza mapambano ya kimataifa dhidi ya changamoto hizo. Monica Juma, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), anavunja rekodi kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kusini mwa dunia kushika nafasi hiyo ya juu katika taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa. Pata mahojiano maalum na ya kina baina ya Flora Nducha wa Idhaa hii na Mkuu huyu mpya wa ofisi ya UNODC.
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vijana nchini humo, wanakumbatia teknolojia kuwafikia vijana wengi hasa wale wa rika la Gen Z, kujiandikisha kama wapiga kura na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Je, hatua hii inaweza kuleta mwamko mpya wa kisiasa nchini Kenya ? Mwanahabari wetu Benson Wakoli alikutana na kuzungumza na vijana hao.
Nyota wa mchezo wa raga ama rugby, Kevin Wekesa kutoka nchini Kenya ambaye alishiriki Michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa mwaka 2024, ameeleza nia yake ya kufanya vizuri uwanjani huku akitumia umaarufu wake kuhifadhi mazingira na kuhamasisha hatua endelevu kupitia michezo ili kujenga dunia yenye mnepo. Rashid Wekesa na taarifa zaidi.
Licha ya kuwa na Shahada ya Utafiti wa Binadamu,Sanaa ya Uchoraji imempa fursa ya kumudu Maisha, Kutana na Cletus Kenedy.
Mkutano wa Afrika forward unaoongozwa na Ufaransa umeanza leo jijini Nairobi ambapo karibia marais 30 ,kutoka barani Afrika wanatarajiwa kuudhuria ili kujadili ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu, mazingira ,afya na kilimo. Mkutano huu umetoa kipaumbele ka ajenda zinazowahusu vijana, na hasa matumizi ya teknolojia, akili unde au AI na namna vijana wanaweza kukumbatia fursa katika sekta hizo.
Mkutano wa Afrika forward unaoongozwa na Ufaransa umeanza leo jijini Nairobi ambapo karibia marais 30 ,kutoka barani Afrika wanatarajiwa kuudhuria ili kujadili ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu, mazingira ,afya na kilimo. Mkutano huu umetoa kipaumbele ka ajenda zinazowahusu vijana, na hasa matumizi ya teknolojia, akili unde au AI na namna vijana wanaweza kukumbatia fursa katika sekta hizo.
Rais Samia Suluhu Hassan, anataka Kenya na nchi yake ya Tanzania kushirikiana ili kukabili uanaharakati wa 'kuvuka mipaka' kutoka kwa vijana wa Gen Z ambao ameelezea unatishia amani na usalama wa nchi nchi za Afrika Mashariki. Unazungumziaje kauli hii ya rais Samia? Unadhani ni sahihi kwa vijana kuadhibiwa kwa kushinikiza mabadiliko kwenye nchi zao?
Rais Samia Suluhu Hassan, anataka Kenya na nchi yake ya Tanzania kushirikiana ili kukabili uanaharakati wa 'kuvuka mipaka' kutoka kwa vijana wa Gen Z ambao ameelezea unatishia amani na usalama wa nchi nchi za Afrika Mashariki. Unazungumziaje kauli hii ya rais Samia? Unadhani ni sahihi kwa vijana kuadhibiwa kwa kushinikiza mabadiliko kwenye nchi zao?
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hali ngumu ya kiuchumi inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel imewafanya vijana waliokuwa wakisoma vyuo vikuu na wahitimu kuhangaika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu baada ya ndoto zao za masomo na taaluma kuvurugwa na vita iliyodumu kwa miaka mitatu. Leah Mushi anatuletea simulizi za baadhi ya vijana hao na shuhuli wanazozifanya hivi sasa.
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye anatumia AI kuunda suluhisho zinazolenga mazingira halisi ya Afrika.
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye anatumia AI kuunda suluhisho zinazolenga mazingira halisi ya Afrika.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kupata ujumbe wa Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana amabye kwa kuwa mwaka huu 2026 ameshiriki tena katika mkutano wa CSW70 anatueleza ni kwa kiasi gani wameweza kulitekeleza malengo ya mikutano haya katika nchini humo.Vita Mashariki ya Kati vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia mwezi wa pili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hapa makao makuu ya UN jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari akisisitiza sio tu vita hivyo vikome bali pia anaendeleza diplomasia za kusaka suluhu. Guterres amesema, Ninamtuma Mjumbe wangu Maalum Jean Arnault. Lengo ni kuunga mkono jitihada za kikanda. Lazima tupate njia ya amani ya kutoka katika hali hii. Ujumbe wangu uko wazi. Kwa Marekani na Israeli, ni wakati muafaka kusitisha vita vinavyosababisha mateso makubwa ya kibinadamu na tayari vinaanzisha athari mbaya za kiuchumi. Kwa Iran, isitishe kushambulia majirani zake.. Ripoti mpya ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika, (ECA) imependekeza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa deni la umma barani Afrika, ikionya kwamba uendelevu hautegemei tu kiwango cha kukopa bali pia ubora wa taasisi, mifumo ya kisheria, na uwazi. Ikitolewa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, ripoti hiyo inataja udhaifu kama vile uwezo mdogo wa kufanya uchambuzi wa hatari, na ushawishi wa mashinikizo ya kisiasa katika maamuzi ya kukopa ikisema kuwa kuboresha usimamizi ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa deni la umma linachangia ukuaji wa uchumi endelevu badala ya kuwa chanzo cha kuyumba kifedha.Wakati dunia hii leo ikiadhimisha Siku ya Uelewa wa Usonji, familia katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka katika kuwahudumia watoto usonji katikati ya mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu. Katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Jiji la Gaza, Layan Abu Qousa mwenye umri wa miaka 16, ambaye ana usonji, anaishi na familia yake katika magofu ya nyumba yao. Familia yake inasema hali ngumu ya maisha imeongeza changamoto zinazohusiana na hali yake, huku ukosefu wa utulivu na mkwamo wa kupata huduma za kitaalamu ukiendelea kudhoofisha ustawi wake.Na katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujielez tangu mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, mabomu ya kutegwa ardhini na ujumbe wa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka Kenya.Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk.Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba' kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini.Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao. Feissal Kirwa wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyo.
Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana. Flora Nducha amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa vijana washiriki kutoka Ghana na kutuandalia taarifa hii
Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali. Feissal Kirwa anaangazia simulizi ya kijana mmoja mnufaika wa mradi huo.
Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana. Flora Nducha amekutana na baadhi yao kusikia maoni yao
Nchini Tanzania shirika la kiraia la kusongesha elimu kwa watoto wa kike, CAMFED limeendelea kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kuwezesha wanafunzi wa kike kuimarika sio tu kimasomo darasani bali pia stadi za maisha na hatimaye wawajengee uwezo wenzao. Katika taarifa hii, John Kabambala wa Redio washirika Kids Time FM amezfuatilia kinachofanyika.
Hii leo jaridani tunaangazia….mafunzo ya usalama katika Ziwa Victoria, na harakati za Shirika la kiraia la kusongesha elimu kwa watoto wa kike, CAMFED za kuwawezesha wanafunzi wa kike nchini Tanzania.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika pamoja na manusura wa mauaji ya kimbari ya holokosti hususan yale yaliyofanywa na manazi wa kijerumani, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Baraza Kuu kumefanyika kumbukizi ikileta pamoja manusura waliotoa shuhuda za waliyopitia wakikimbia maeneo kadhaa ikiwemo Austria baada ya kutwaliwa na wajerumani.Ziwa Viktoria barani Afrika, licha ya kuwa mhimili muhimu wa maisha kwa zaidi ya watu milioni 40 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, bado linakabiliwa na vitisho vihusianavyo na biashara haramu za magendo, usafirishaji haramu binadamu na uvuvi haramu. Ili kupatia suluhu changamoto hiyo Ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria (INL) ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM), na walinzi wa pwani wa Kenya wamechukua hatua.Nchini Tanzania shirika la kiraia la kuendeleza elimu kwa watoto wa kike, CAMFED limeendelea kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kuwezesha wanafunzi wa kike kuimarika sio tu kimasomo darasani bali pia stadi za maisha na hatimaye wawajengee uwezo wenzao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za vijana katika kuchagiza maisha wayatakayo kuanzia kujiondoa kwenye umasikini, ukosefu wa usawa hadi kwenye upatikanaji mdogo wa elimu bora na kazi zenye staha.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika pamoja na manusura wa mauaji ya kimbari ya holokosti hususan yale yaliyofanywa na manazi wa kijerumani, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Baraza Kuu kumefanyika kumbukizi ikileta pamoja manusura waliotoa shuhuda za waliyopitia wakikimbia maeneo kadhaa ikiwemo Austria baada ya kutwaliwa na wajerumani.Huko Geneva, Uswisi ambako inaelezwa kuwa kurejesha mfumo wa elimu uliosambaratika huko Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni jambo la kuokoa maisha, na kuwarudisha watoto shuleni lazima kiwe kipaumbele cha haraka, amesema James Elder Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Umoja wa Mataifa umezindua Mpango wa Mahitaji na Hatua za Kibinadamu wa dola milioni 852 kwa ajili ya Somalia, huku ukionya kuwa ukosefu mkubwa wa ufadhili utaacha mamilioni ya watu walio katika mazingira magumu bila msaada wa kuokoa maisha, huku hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "TWINGA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo Duniani FAO, kupitia mradi wake wa masuala ya biashara HASTEN limeendesha warsha maalum ya kuanzisha biashara kwa vijana na wanawake, mjini Kigali Rwanda, lengo likiwa ni kuwapa miradi 10 mipya ya biashara itakayofanyika kwa msaada maalum kutoka kwa wakufunzi wa kitaifa na kimataifa juu ya mbinu za kupanua biashara, kuongeza ufanisi na kuchangia katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Sheilah Jepng'etich na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako wasichana juhudi za kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) zimewezesha vijana wa kike kushiriki masomo ya Teknolojia ya Habari na Maewasiliano, TEHAMA na kujifunza stadi za teknolojia ili waweze kuedeleza biashara ya mtandaoni pamoja na matumizi mengine.Zaidi ya watu nusu milioni wameathiriwa na mafuriko makubwa katika mikoa ya kusini na kati ya Msumbiji, huku mvua kubwa ikiendelea kuvuruga usafiri, huduma za afya na njia za ugavi. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA nchini humo, Paola Emerson, amewaambia waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi kuwa majimbo ya Gaza, Sofala na Maputo ndiyo yaliyoathirika vibaya zaidi.Huko Mashariki ya Kati mapema leo Jumanne, vikosi vya Israel vimebomoa kwa tingatinga makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, huko Yerusalemu Mashariki eneo linalokaliwa kimabavu na Israel. Mkuu wa UNRWA, Philippe Lazzarini, amelieleza tukio hilo kama “shambulio lisilo na kifani dhidi ya Umoja wa Mataifa,”.Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, leo imesema imeanza kutekeleza mpango wa kurejesha kwa hatua mamlaka ya dola katika mji wa Uvira, mashariki mwa nchi hiyo, kufuatia kuondoka kwa kundi lenye silaha la AFC/M23. Serikali inasema vikosi vya usalama, polisi na huduma nyingine za serikali vinarejea ili kulinda raia, kulinda mali na kuleta utulivu katika eneo hilo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu ONNI SIGALA Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana ya neno “ KING'ANI”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Licha ya uchumi wa dunia kuendelea kukua, maendeleo katika kupata kazi zenye ubora na staha yamekwama, huku mamilioni ya wafanyakazi wakisalia katika lindi la umaskini na ajira zisizo rasmi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani (ILO)iliyotolewa hii leo huko Geneva Uswisi. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Mnapofikiria kutazama ndege, labda mnawazia wastaafu. Lakini kizazi kipya kinaanza kutumia darubini na kujihusisha na burudani hii. Kile kilichokuwa kimbilio kutoka ulimwengu wa mtandaoni sasa kinafufuka tena mtandaoni.
Haki ni msingi wa Kila siku, hiyo ndio ilikuwa kaulimbiu ya siku ya Haki za binadamu mwaka huu iliyoadhimishwa wiki iliyopita. Lakini kila uchao haki za binadamu zinaendelea kukiukwa kuanzia nyumbani hadi kwenye mtandao. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha vijana katika kupambana na ukiukwaji wa haki hasa mtandaoni, Ofisi ya Umoja wa Maataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) jijini Nairobi Kenya umewakusanya vijana kujadiliana nao na kuwapa mafunzo ya kumakinika hasa mtandaoni.
Hii leo jaridani tunaangazia kilichojiri katika Mkutano wa COSP11 kuhusu ufisadi mjini Doha Qatar, haki za kibinadamu na vijana nchini Kenya, afya ya akili ikimulika upweke na jinsi unavyoweza kuepukana nayo.Mkutano mkubwa zaidi duniani wa kupambana na rushwa au ufisadi umeanza leo Desemba 15 mjini Doha nchini Qatar kwa wito wa kutumia teknolojia zinazoibuka katika mapambano dhidi ya rushwa na kushughulikia uhusiano wake na uhalifu wa kupangwa na makosa mengine ya kifedha.Haki ni msingi wa Kila siku, hiyo ndio ilikuwa kaulimbiu ya siku ya Haki za binadamu mwaka huu iliyoadhimishwa wiki iliyopita. Lakini kila uchao haki za binadamu zinaendelea kukiukwa kuanzia nyumbani hadi kwenye mtandao. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha vijana katika kupambana na ukiukwaji wa haki hasa mtandaoni, Ofisi ya Umoja wa Maataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) jijini Nairobi Kenya umewakusanya vijana kujadiliana nao na kuwapa mafunzo ya kumakinika hasa mtandaoni.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan, mkutano unaomulika hatua za tabianchi barani Afrika UNEA7, na juhudi za vijana nchini Kenya za kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo endelevu.Nchini Sudan, barani Afrika, wasiwasi mkubwa unaendelea kuhusu makumi ya maelfu ya watu wanaoaminika kuwa bado wamenaswa mjini El Fasher katika eneo la Darfur,magharibi mwa nchi lakini mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanaamini kwamba huenda yakaruhusiwa kufika katika mji huo uliogubikwa na mapigano.Leo Dunia inapoadhimisha miaka kumi tangu Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya Tabianchi kupitishwa, wataalamu wa masuala ya tabianchi barani Afrika wanasema maadhimisho haya ni wakati wa kupima hatua zilizofikiwa lakini pia kukabili pengo linalopanuka kati ya sera na utekelezaji wa hatua za tabianchi.Kutoka mashambani hadi kwenye majukwaa ya kidijitali, vijana wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wanaongoza enzi mpya ya kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabianchi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Watoto UNICEF limeunga mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya vitendo na zana muhimu ili kukuza biashara zao za kilimo, kuimarisha mifumo ya chakula ya ndani, na kujenga jamii zinazohimili mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kutoka mashambani hadi kwenye majukwaa ya kidijitali, vijana wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wanaongoza enzi mpya ya kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabianchi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Watoto UNICEF limeunga mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya vitendo na zana muhimu ili kukuza biashara zao za kilimo, kuimarisha mifumo ya chakula ya ndani, na kujenga jamii zinazohimili mabadiliko ya tabianchi. SheilaH Jepngetich na taarifa zaidi
Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui“Kila Mchango Una Umuhimu.” Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania Sabrina Saidi amezungumza na kijana ambaye anajitolea katika Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania YUNA Je kasema nini?.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU.Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya amani na usalama nchini Guinea-Bissau, utapiamlo nchini Sudan na juhudi za UNICEF za kuwawezesha vijana ili waweze kujikwamua kimaisha nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba.Zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita nchini Sudan imewaacha watu milioni 21 karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakikabili njaa kali, huku maeneo mawili yakithibitishwa kukumbwa na baa la njaa. Mapigano yamepungua kwa sasa katika baadhi ya sehemu za Khartoum, na masoko yanaanza kufunguliwa tena., Lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaonya kuwa hali bado ni tete.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama, inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoniMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama , inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoni. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi.
Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga, elimu kuhusu uraia nchini Sudan kusini, na kilimo endelevu na vijana nchini Rwanda.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali.Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi. Leah Mushi anatuletea taarifa ikiangazia namna Sudan Kusini inavyojiandaa na uchaguzi wake mkuu mwakani 2026.
Katika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana wa Uingereza na Ghana, Dkt. Khadija Owusu ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili.Owusu, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Akaya inayowakilisha wasichana wa zama hizi, anasema vijana hawapaswi kuzungumziwa tu, bali wajumuishwe moja kwa moja katika kuandaa Suluhu za changamoto zinazoihusu dunia wakiwemo na wao "Mara nyingi tunazungumza kuwa tunataka ushiriki zaidi wa vijana wakati umefika wa kuacha kuzungumza tu kuhusu kuhitaji vijana wengi, bali tuwe na vijana wengi."Niko hapa kuwakilisha maelfu ya wasichanaAnasema ushiriki wake katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa vijana si wa kibinafsi tu, bali unaakisi sauti za wasichana na vijana wengi wanaosaidiwa na taasisi yake ya Akaya."Niko hapa kuwakilisha si mimi peke yangu, si Uingereza tu, na si Ghana tu, bali Taasisi ya Akaya, na wasichana na vijana wengi tunaowahudumia nchini kote."Owusu anaamini vijana wa Kiafrika, hususan wasichana, wanapaswa kupata nafasi kubwa zaidi katika jmaukwaa ya kimataifa kama Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kupaza sauti zao."Bado tunahitaji kuona vijana zaidi kama sisi kwenye vyumba vya mikutano, Waafrika zaidi, vijana zaidi wa Kiafrika na wasichana wa Kiafrika kwenye vyumba vya mijadala, wakishiriki majadiliano kwa sababu tunaleta mabadiliko halisi."Owusu anasema ujumbe wake kwa vijana barani Afrika ni kubeba vipaji vyao, wajiamini, na kuendeleza ndoto zao kwani kila kitu kinawezekana.
Kaunti ya Kirinyaga, iliyoko katikati mwa nchi ya Kenya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, inashuhudia mageuzi mapya katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa kuwahusisha vijana katika kilimo na lishe unaojulikana kama EKYAN. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na wadau nchini humo. Karibu Sabrina Saidi utupe taarifa zaidi.....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Mradi wa EKYAN ni mfano wa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, ukiwa na lengo la kutengeneza fursa za ajira, kuwanufaisha na kubadilisha maisha ya vijana walioko vijijini, kupitia mbinu bora za kilimo na lishe, ukitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, serikali ya kaunti ya Kirinyaga na shirika linalotoa mafunzo, elimu ya biashara ndogo ndogo na uwezeshaji barani Afrika KUZA Biashara.Felista Nyakio Mutungi kijana mkulima wa kaunti ya Kirinyaga, ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kupitia mradi huo. Na hapa anasema....CUT 2- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Kabla ya kuanza kilimo, nilikuwa nauza barabarani viazi vya kukaanga au chipsi, na mihogo, pamoja na nafaka. Haikuwa vizuri sana, lakini ndiyo nafasi pekee niliyokuwa nayo wakati huo. Kupitia serikali ya kaunti ya Kirinyaga, tulisajiliwa kama vijana wanaopenda kilimo na tukapata mafunzo kupitia KUZA na UNICEF. Sasa mimi ni mkulima na mjasiriamali.”Felista anasema awali alikuwa akilima robo ekari ya mpunga na kuvuna magunia manne hadi matano pekee. Lakini baada ya mradi wa EKYAN, kwa robo ekari hiyo hiyo sasa anapata hadi magunia saba. Aidha, shamba lake limepanuka hadi ekari nne katika eneo la 'mradi wa umwagiliaji wa Bura.Felista hakutaka kuwa mchoyo wa manufaa aliyopata, hivyo ameamua kueneza ujuzi wa kilimo cha kibiashara kwa kuwafundisha baadhi ya wakulima wengine mbinu na maarifa ya kilimo hiki.CUT- Sauti ya Felista Nyakio Mutungi“Sasa si tu kwamba nalima, bali pia nawafundisha wakulima wengine kuongeza thamani katika mazao yao. Wanapata ujuzi wa kufanya biashara kupitia kilimo. Na kwa kweli tunawashukuru wahisani na UNICEF kwa kutuwezesha. Bila mpango huu, nisingekuwa hapa nilipo leo.”Kwa upande wake mtaalamu wa ubunifu wa UNICEF nchini Kenya Lilian Njoro, anaeleza kwa nini mradi huo ni muhimu kwa vijana.CUT- Sauti ya Lilian Njoro."Ni asilimia 10 pekee ya vijana wanaojihusisha na sekta ya kilimo. Kwa hivyo, kupitia mradi wa EKYAN, tulitaka kuona jinsi ya kuwahusisha vijana wengi zaidi katika kilimo na kuwavutia ili waweze kuanza kupata maisha yenye utulivu na ajira bora kupitia sekta hii.”Njoro anasisitiza kuwa teknolojia mpya zinafungua njia kwa kilimo cha kisasa tofauti na enzi za wazazi na mababu zao.Namna kilimo kinavyofanyika nyakati hizi ni tofauti na zamani,hii ni kwa sababu ya uwepo wa teknolojia bunifu, majukwaa ya kidijitali, na fursa nyingi.Kwa sasa, mradi wa EKYAN umeendelea kuwajengea vijana ujuzi, kuwapatia nafasi ya ajira, na kubadilisha mtazamo wao kuhusu kilimo, kutoka shughuli ya kizamani hadi kuwa biashara yenye faida.Link: https://youtu.be/hv17nk-2l5kTAGS:UNICEF Kenya/Kilimo/Biashara na ujasiriamali
Jaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Na katika mashinani nampisha Mchanga Omari Kombo kutoka Pemba Zanzibar ambaye ni mnufaika wa mpango mpya wa afya ya uzazi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF na wadau wake umewasaidia wanawake wajawazito kama kuondokana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya njema.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!