Podcasts about samaki

  • 26PODCASTS
  • 61EPISODES
  • 32mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • Nov 8, 2024LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about samaki

Latest podcast episodes about samaki

Reportage Afrique
Tanzanie: les pêcheurs d'Ukerewe quittent leur île par manque de poissons [2/3]

Reportage Afrique

Play Episode Listen Later Nov 8, 2024 2:03


C'est la plus grande île lacustre d'Afrique. Ukerewe, 500 km² de terre dans les eaux du lac Victoria, située à 50 kilomètres de la ville tanzanienne de Mwanza, est connue pour ses pêcheurs. Mais ces derniers voient leur quotidien menacé par une diminution des stocks de poissons dans le lac. En cause, des pratiques de pêche inadaptées, mais aussi les effets dévastateurs du changement climatique. « Samaki » (« le poisson » en swahili) est désormais bien difficile à trouver dans les eaux entourant Ukerewe. Pambano Boniface, pêcheur sur le lac Victoria depuis 15 ans, voit ses filets remonter de plus en plus vides : « Vous quittez la maison et naviguez pendant plus de six heures à la recherche de poissons. Vous partez trois ou quatre jours et il n'y a pas de garanties que vous trouverez du poisson. Vous pouvez partir pendant des heures et revenir avec seulement deux kilos de poissons, ou parfois rien du tout. »L'économie de l'île dépend principalement de la pêche. Alors, certains pêcheurs comme Damien Simon et ses collègues s'essaient à la pisciculture : « C'est quelque chose de nouveau, que nous ne faisions pas dans le passé, où on pêchait normalement dans le lac. Mais nous avons commencé à cause du manque de poissons. »Changer d'activité Tous ne peuvent se permettre ces techniques, car le coût de mise en place reste élevé et le gouvernement, même s'il promeut ces méthodes, n'offre pas d'aide au financement. Certains tentent donc de se tourner vers d'autres activités comme l'agriculture, mais ils font face à des défis similaires, comme l'explique Joyce Komanya de l'organisation Centre Juridique et des droits de l'Homme à Dar es Salam : « Ils pensent que de passer de la pêche à l'agriculture va les aider, mais en réalité, les agriculteurs ont, eux aussi, leurs propres problèmes liés au changement climatique. »Le changement climatique est l'une des causes majeures de ce manque de poissons. Les pluies sont de plus en plus rares, mais les épisodes pluvieux sont de plus en plus intenses, provoquant notamment une montée des eaux du lac. À cela s'ajoutent des techniques de pêche inadaptées avec des filets qui capturent même les plus petits poissons, qui n'ont pas le temps de se reproduire. Pour Pambano Boniface, le futur est incertain : « Je vois un avenir difficile. Si notre présent est rude, le futur le sera bien plus. »En 2024, le niveau des eaux du lac Victoria est supérieur à toutes les années records enregistrées depuis 1992.À lire aussiTanzanie: la montée des eaux du lac Victoria menace l'île d'Ukerewe [1/3]

The Bream Fishing Project
Episode 87: 2024 Samaki Queensland Open, Moreton Bay / Gold Coast, June 1-2

The Bream Fishing Project

Play Episode Listen Later Sep 2, 2024 69:39


Siha Njema
Wanawake wawafuga samaki kukwepa msambao hatari wa Ukimwi ziwa Victoria

Siha Njema

Play Episode Listen Later Aug 28, 2024 9:37


Mashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV

Radio Maria Tanzania
Je, ndege, mbuzi, ng’ombe na samaki waliomo baharini nao humuabudu Mungu?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Aug 20, 2024 25:12


Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Altho Hermes Mlelwa, wa parokia ya Makete Jimbo la Njombe nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Nasadiki ya kuwa vitu vyote vilivyomo ulimwenguni vimeumbwa na Mungu Je, ndege, mbuzi, ng'ombe na samaki waliomo baharini nao humuabudu Mungu. L'articolo Je, ndege, mbuzi, ng'ombe na samaki waliomo baharini nao humuabudu Mungu? proviene da Radio Maria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Kenya: Namna mabaki ya ngozi ya samaki yanavyotumiwa kuhifadhi mazingira

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Aug 5, 2024 9:20


Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Hata hivyo wenyeji sasa wengi wao vijana wameanza kutumia taka hizo kutengeza bayogesi na bidhaa zingine kama vile viatu,nguo,begi mifuko na kadhalika hivyo kubuni ajira na kuinua uchumi. Katika fuo za Dunga kando na ziwa Victoria kaunti ya kisumu nchini Kenya,wafanyabiashara hapa wanatumia bayogesi kukaanga samaki na  kuwauzia wateja wanaotalii êneo hili.Bayogesi hii inayotengenezwa kutokana na mabaki ya samaki ,imewafaidi wenyeji wa hapa kupunguza gharama ya matumizi vile vile kutunza mazingira. Caroline Achieng ni mfanyabiashara wa samaki.“Tunadumisha usafi kwa sababu wageni wanakuja hapa lazima tudumishe usafi ndio mazingira yetu yasiharibike,mradi huo umesaidia sana kwa sababu wametusaidia kuchukuwa hizi takataka za samaki kama matumbo,wanatengeneza nayo bayogasi hivyo kupunguza uchafu”alisema  Caroline Achieng mfanyabiashara wa samaki.Kwa mujibu wa Achieng, uwepo wa mradi huu umeimarisha biashara yake ukilinganisha wakati alipokuwa akitumia kuni kukaanga samaki.“Changamoto tuko nayo ni kama samaki haiko kwa sababu mazingira yameharibika,tudumishe usafi tutengeneze mazingira ili samaki ipate kuzalishana baharini.”AlisisitizaAchieng.Mita chache kutoka kwenye wafanyabiashara hawa wanaokaanga samaki,Mary Dede ni mwenye furaha,Kwa sasa anatumia kawi inayotokana na bayogesi vile vile kawi mbadala,kukausha samaki aina ya dagaa kwa minajili ya kuwahifadhi kwa mauzo ya baadaye.“Hapo tunaweka Omena kama tunataka kuikausha na inaweza chukuwa hata masaa tatu kukauka.”Alisema Mary Dede.Kwa miaka mingi taka inayotoka kwa samaki na viumbe vingine kwenye ziwa, imekuwa ikichafua mazingira na kusababisha samaki wengi kukosa hewa ya oxigeni hivyo kufariki na kusababisha hasara kubwa.Mradi huu wa kutengeneza gesi kutokana na taka hizi umeimarisha mazingira na biashara ya hapa. Charles Ochieng ni mtaalam wa kutengeneza bayogesi kwenye shirika flexy biogás, shirika ambalo linaendesha mradi huu wa gesi êneo hili.“Huwa tunachukuwa mabaki ya samaki ikifika jioni tunachukuwa tunaichunga maji yake tunamwaga kwa mtungi huu wa bayogesi, hiyo ndio inatengeneza bayogesi,uchafu mwingine tunatengeneza chakula ya kuku na nguruwe.” AlielezaCharles Ochieng ni mtaalam wa kutengeneza bayogesi.Kwa siku kilo 300 za mabaki ya samaki hukusanywa hapa na kisha kuchakatwa kwa kimombo recycle kisha kuzalisha gesi ambayo kwa mujibu wa Ochieng huuzwa kwenye soko hili na mikahawa karibu.“Bayogasi hii ,akina mama wanakuja hapa hapa wanapika githeri,omena na samaki na vyakula vingine ,wanalipa na inalingana na kiwacho cha chakula wanapika,ada ya juu zaidi ni shilingi 100 ,ada ya chini ni shilingi 50,tumsaidia eneo hili kutunza mazingira kwa vile uchafu huu sasa haurudishwi baharini.” AlisemaCharles Ochieng.Takwimu kutoka taasisi ya Utafiti wa Baharini na Uvuvi nchini Kenya zinaonyesha kuwa tani 150,000 za taka za samaki huzalishwa kila mwaka, ambapo asilimia 80 ya taka hizo hutupwa na kuharibu mazingira .Samuel Okoth ni mtaalam wa mazingira jimbo hili la Kisumu.“Ngozi hii na taka zingine zamani zilikuwa zinatupwa baharini na kuchafua mazingira,ndio tukagundua inaweza tengeneza bayogasi na bidhaa zingine kama viatu ,begi na vile vile kuunda uzi za kushona watu wakati wa upasuaji.”Alisimulia Samuel Okoth ni mtaalam wa mazingira jimbo hili la Kisumu.Okoth anasema kuwa Ufumbuzi wa teknojia umesaidia sana kutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na taka hizi, hivyo kuajiri vijana wengi eneo hili.“Bidhaa hizi kama begi hatuuzi hivi hivi tu tunauza katika masoko ya kimataifa kwa sababu dhamani yake ni ya juu mno,kwa sababu huo mchakato wa kuziunda ni ghali mno kama vile kulainisha hiyo ngozi ya samaki na kuifanya kuwa kubwa.”Kilomita 6 kutoka ufuo huu wa dunga ni ,kijiji cha kajulu kaskazini mwa mji wa Kisumu,,namkuta Sarah Adero akitumia ngozi na magamba  ya samaki kutengeza bidhaa kama vile nguo,viatu.magamba haya na ngozi ya samaki hukusanywa kutoka vituo mbalimbali jijini Kisumu .“Ngozi hizi tunazitoa maeneo kama vile ubunga,tunazileta hapa na kuzilainisha na kuzitumia kutengeneza bidhaa tofautitofauti,ngozi hii ikiachwa tu hivyo itachafua mazingira hata kule baharini kisha samaki wengine wataweza kufariki.”Mipango kama hii hata hivyo imeonekana kuchangia uchumi endelevu yaani circular economy hasa katika miji mbalimbali nchini Kenya, huku mashirika ya kaboni yakisema kuwa, fumbuzi hizi zitachangia Zaidi ya ajira millioni nane barani Afrika.“Inaleta mapato sana na nawaambia wenzangu,kila kitu ina kazi,kama hii ngozi ya samaki mtu hawezi jua eti inaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali,ingetupwa ingechafua mazingira na pia hatungepata mapato.”Uwepo wa hatua kama hizi za kutumia taka kutengeneza bidhaa mbalimbali ni moja wapo ya mataifa kama vile Kenya ,kuafikia malengo ya ruwaza ya maendeleo endelevu ya mwaka wa 2030 ,ambapo mataifa yanafaa kutumia uvumbuzi na teknolojia ili kutatua changamoto za mazingira,hivyo kubuni nafasi za kazi na kuimarisha mazingira.Victor Moturi,Kisumu RFI Kiswahili.

VOA Express - Voice of America
Vijana wanaovua samaki kutoka ziwa Victoria walalamikia kuzorota kwa biashara kutokana na mafuriko - Mei 13, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later May 13, 2024 29:59


Vijana wanaovua samaki kutoka ziwa Victoria walalamikia kuzorota kwa biashara kutokana na mafuriko

Radio Maria Tanzania
Je,wafahumu alama ya Samaki kwenywe Mavazi ya Mapadre?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 2, 2024 22:05


  Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani Leo tupo Frateri Oscar Mwamoto, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramihio, Jimbo kuu la Songea  swali  la msikilizaji linalojibiwa linasema  Ivi alama ya samaki kwenywe Mavazi ya Padri na vyombo vya Kanisa inamaana gani?    L'articolo Je,wafahumu alama ya Samaki kwenywe Mavazi ya Mapadre? proviene da Radio Maria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ukulima wa baharini na ukuzaji wa nzi wa Black Soldier katika utengenezaji wa chakula cha samaki

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Jul 18, 2023 9:59


Ili kuwa na kilimo endelevu cha samaki, wakulima pwani ya Kenya wakumbatia ukuzaji wa nzi wa Black Soldier katika utengenezaji wa chakula cha samaki.

The Bream Fishing Project
Episode 26: 2023 Samaki Bream Queensland Open, June 24-25

The Bream Fishing Project

Play Episode Listen Later Jul 10, 2023 72:35


In this episode we take a deep dive into the Queensland Open. Leading up to this event there was some talk around whether Steve Morgan could take the the two Bream opens and the Bass open. By his own admission, Steve said he typically didn't place highly up there in QLD. I did have a brief conversation with Steve about why out of state anglers sometimes perform really well. This small part of Steve's interview was brilliant and definitely worth listening to before we got into the nitty gritty of his competition. I then spoke with second place Cain Waller who also had a great story to tell. One of my favourite parts of the interview was when Cain spoke about having motor issues, getting towed back and then running like an athlete to put his key tag back on the board. Finally in first place was Chris Lonne, who also had a great story. Chris caught a whole bunch of fish off one location. I have not heard a story quite like this before. For anyone heading to the Hobie round this weekend on the Gold Coast,  this is a must listen!

Habari za UN
Jamii ya Wavuvi Sudan Kusini wawezeshwa na FAO kutengeneza mnyororo wa thamani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 16, 2023 0:03


Mkuu wa Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amefanya ziara maalum ya kutembelea visiwa vilivyopo katika kaunti ya Terekeka na kujionea utekelezaji wa miradi ya stadi za maisha inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO. Katika ziara hiyo maalum, Mkuu wa UNMISS aliambatana na wawakilishi wa FAO pamoja na Benki ya Dunia ambao ni miongoni mwa wahusika wa moja kwa moja wa kuendesha Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Jamii ya Wavuvi -FICREP ambao unawajengea uwezo wananchi wa visiwani ambao kwa kiasi kikubwa wanajishughulisha na biashara ya Samaki. Mwakilishi wa FAO nchini Sudan Kusini Meshack Malo anasema malengo ya miradi yao ni kuziwezesha jumuiya za wavuvi kutengeneza mnyororo wa thamani na kuwa na biashara stahimilivu kwakutumia vyema uwepo wao katika ukanda wa mto Nile, “Unakuta kwamba changamoto walizonazo Wasudan Kusini na wakazi wa Terekeka ni kuongeza muda wa kuhifadhi samaki. Hapo awali walikuwa wakipata samaki asubuhi na ikifika jioni chochote kile ambacho hakijauzwa wanatupa. Kwa hivyo, tumeanzisha ukaushaji wa Samaki ili waweze kuchukua hadi miezi minane.  Kwa teknolojia ya usindikaji tunatumai kuwa wananchi hawa wanaweza kupata thamani ya pesa.”Mbali na kuwapatia vifaa vya kuvulia pamoja na kusindika samaki, FAO inaendesha mafunzo ya kutunza na kuhifadhi Samaki, kutafuta masoko na kutengeneza uhusiano mwema. Vijana nao wanafundishwa kutengeneza mitumbwi ya kuvulia samaki ambayo inadumu na haiingizi maji.Miradi hii tayari imeanza kuwa na matokeo chanya, mfano wanawake wamewezeshwa kujenga mtandao wa kimataifa na kujikwamua kiuchumi, wamepelekwa katika ziara za kimasomo kwenye nchi za Kenya, Uganda na Ghana, ambako wamejifunza njia za gharama nafuu na zenye afya za kuendesha biashara zao suala lililo mfurahisha mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom, “Nimepata uzoefu muhimu san,a sio tu kwa kutoka nje ya mji wa Juba na kuja kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaida wa Sudani Kusini, lakini kujionea mradi huu wenye mafanikio makubwa yamradi huu unaotekelezwa na Wasudan Kusini wa kawaida. Nadhani kuna utambuzi mpana kwamba huko Sudan Kusini hakuwezi kuwa na amani bila maendeleo, lakini tunajua kuwa hakuwezi kuwa na maendeleo bila amani. Kwa maana hii, kaunti hii inawakilisha jaribio la kweli, la kusitawisha amani, lakini pia mradi ambao matunda ya amani yanaweza kuhisiwa na watu wote.”Mkuu huyo wa UNMISS amehitimisha ziara yake kwakusema jumuiya zinazofanya maamuzi na kuyasimamia zinafanikiwa na kuwa mfano bora kwa jamii zote za nchini Sudan Kusini. 

Alfajiri - Voice of America
Baadhi wa wakazi wa mataifa ya Afrika magharibi walalamikia upungufu wa samaki kwenye bahari kutokana wavuvi haramu kutoka China. - Desemba 27, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 27, 2022 29:59


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Zambia: FISH4ACP kusaidia uvuvi endelevu wa dagaa Kapenta na samaki buka

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 21, 2022 0:03


Nchini Zambia, wafanyabiashara ya samaki kandokando ya Ziwa Tanganyika wameanza kuwa na wasiwasi kuwa uvuvi usizingatia kanuni za uvuvi bora unaweza kuhatarisha ustawi wao ambao unategemea biashara ya dagaa aina wafahamikao nchini humo kama Kapenta na samaki aina ya Buka.Ili kuondokana na hali hiyo, hapo ndipo unapoingia Mradi wa FISH4ACP ambao ni mkakati wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Afrika, AU na ule wa nchi za Karibea na Pasifiki OACPS, kuhakikisha minyororo ya thamani ya uvuvi na ufugaji wa samaki barani Afrika, Karibea na Pasifiki kuwa endelevu zaidi. Anold Kayanda na maelezo zaidi kupitia makala hii.

Alfajiri - Voice of America
Baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi yalalamikia upungufu wa samaki kutokana na kile wanasema ni uvuvi haramu unaofanywa na meli za China. - Desemba 13, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 13, 2022 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

Habari za UN
Sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa chakula: FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 21, 2022 0:02


Ikiwa leo ni siku ya uvuvi duniani imeelezwa kuwa sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa chakula na inasaidia mtu 1 kati ya 10 duniani kote. Kwa kutambua mchango wake wito umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuboresha miasha ya mamilioni ya wanawake kwa wanaume wanaofanyakazi katika sekta hii kwa kuhakikisha haki zao za binadamu zinatimizwa.  Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa FAO Dkt. QU Dongyu, amesema kwa muda mrefu FAO imekuwa ikiwasaidia mamilioni ya wanawake na wanaume wanaofanyakazi katika sekta ya uvuvi na watu wa jamii za asili kote duniani kwa sababu ni sekta muhimu katika mfumo wa chakula na mnyororo wa thamani  ambayo inatoa fursa kubwa ya ajira hususan kwa nchi zinazoendelea. Pia inasaidia kujenga jamii imara za watu wa Pwani na kuhakikisha uhakika wa chakula la lishe kwa mamilioni ya watu.  Bwana Dongyou ameongeza kuwa “Samaki na bidhaa za Samaki ni miongoni mwa bidhaa za chakula zinazouzwa sana duniani kote na mwaka 2019 pekee iliingiza takriban dola bilioni 163 za mapato ya usafirishaji nje huku nchi zilizoendelea zikiongeza kiwango chake cha thamani ya biashara ya kimataifa ya bidhaa za Samaki kwa zaidi ya asilimia 54.” Mkuu huyo wa FAO amesema pamoja na mchango huo mkubwa kwa lishe na maendeleo “Kwa bahati mbaya sekta hiyo inayotoa fursa kubwa kwa wavuvi na wafanyakazi wa uvuvi inaweza pia kuwaathiri  wasiojiweza kupitia ukiukwaji wa haki za wafanyakazi ambazo zinajumuisha mfumo usio wazi wa ajira ambao hauhakikishi malipo bora kwa wafanyakazi, kufanyakazi kwa saa nyingi zisizoendana na malipo, ajira ya shuruti, ajira kwa watoto na mambo mengine.”  Kwa mantiki hiyo Dongyou amesisitiza “Tunahitaji kuwapa sauti wanafanyakazi ha wa na kushikamana nao katika vita vya kuwa na ajira yenye staha kwa kupitia kuongeza ushirikiano miongoni mwa wadau wote zikiwemo nchi, mashirika ya kimataifa, vyama au jumuiya za wavuvi, sekta binafsi, jumuiya za wafanyakazi, mashirika ya asasi za kiraia na walaji.” Pamoja na mikataba mingine iliyopo FAO imesema inazindua mwongozi mpya kuhusu wajibu wa kijamii kwa makampuni yaliyoko kwenye sekta ya uvuvi na pia itaendelea kusfanyakazi kwa karibu na wadau wengine kama shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO kusaidia kuboresha mazingira ya kazi na maisha ya jamii za wavuvi kote duniani ikiwemo haki zao za masingi za binadamu. Siku ya uvuvi duniani huadhimishwa kila mwaka Novemba 21 na mwaka huu imebeba maudhui "Kuzuia wimbi: Kwa pamoja tunaweza kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu baharini!". 

RadioRahma
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part One

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 7:53


Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

RadioRahma
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 9:57


Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

RadioRahma
Chupa zageuzwa kuwa mazalia ya Samaki baharini.

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 10, 2022 11:33


Mirundiko ya takataka sio tu katika nchi kavu bali pia baharini kwa miaka mingi imekuwa shida kubwa kuthibiti, taka za baharini zikichangia kuharibika kwa miamba ya matumbawe. Lakini katika Kijiji cha Mkwiro kaunti ya Kwale Ukanda wa pwani, baadhi ya taka za baharini na zile za nchi kavu zimegeuzwa kuwa thamani kwa kutumia mchakato mbadala wa kutengeneza chupa za matumbawe. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Habari za UN
Mradi wa FAO Thailand warejesha si tu vibua bali pia ufugaji wa kamba wadogo umeimarika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 5, 2022 2:19


Nchini Thailand, neema imerejea tena kwa wafugaji wa Kamba wadogo baada ya mradi wa FAO wa teknolojia mpya ya kuchuja maji na kulisha viumbe hao kusaidia kuondoa changamoto waliyopata awali ya milipuko ya magonjwa kutokana na uchafu wa maji kwenye mabwawa wanayofugia. Taarifa iliyoandaliwa na FAO ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO inasomwa na Ibrahim Rojalla wa televisheni washirika Mamlaka TV inafafanua zaidi. Mradi unatekelezwa kwenye jimbo la Khiri Khan nchini Thailand kwenye mabwawa ya kisasa ya ufugaji samaki, mfugaji akitembea kwenda kuvua samaki kwa kutumia wavu unaonin'ginizwa kwenye njia anamopita, iliyojengwa kwa wavu juu ya mabwawa hayo. Samaki wamenasa nyavuni na kando ni mashine maalumu yenye magurudumu ya chuma na mfumo wa kutumia hewa inayopuliza maji . Inapita juu ya maji kwa lengo la kuchuja uchafu. Awali kabla ya teknolojia hii, walitumia siku hadi 10 kusafisha maji ambayo yanachafuliwa si tu na mabaki ya vyakula vya kamba hawa wadogo bali pia uchafu wa haja zao kubwa. Uchujaji usiokuwa fanisi hapo awali ulisababisha milipuko ya magonjwa na mabwawa kufungwa. Kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo wamepatiwa mashine hii ya kuchuja uchafu, halikadhalika mfumo wa kisasa wa kupatia samaki chakula badala ya kumwaga kwenye bwawa. Kirana Leesakulpran, mama wa watoto wawili na ambaye amekuwa akifuga samaki aina ya Kamba kwa zaidi ya miaka 30 anasema, “tangu tuanze kutumia teknolojia hii, tunapata kamba wengi zaidi, faida imeongezeka na maisha ya ukulima ni endelevu zaidi.” Nchini Thailand zaidi ya watu milioni 23, takribani asilimia 34 ya watu wote hawana uhakika wa kupata chakulia na FAO kupitia mradi wa kusaidia uchumi utokanao na shughuli za baharini na majini, inasaidia Thailand kuongeza tija kwenye ufugaji samaki kwa kudhibiti pia uvuvi wa kibiashara. Theerapong Thammasara ni mvuvi mdogo ambaye anaona mabadiliko ya kiwango cha uvuvi kabla na baada ya mradi. (Sauti ya Theerapong Thammasara) “Nadhani ni kwa sababu ya kanuni zote zinazotekelezwa. Meli kubwa za uvuvi haziruhusiwi kufika maili tatu kutoka pwani. Na kuna sheria kuhusu ukubwa wa nanga. Hizi ni sababu ya kurejea tena kwa vibua.” Ama hakika katika soko tuliloingia kupitia video ya FAO, vibua ni wakubwa na wengi na bila shaka lengo la kutokomeza uhaba wa chakula na lishe bora litafikiwa.  

NQ Fishing Show Podcast
NQ Fishing Show 16th July Catch Up Show

NQ Fishing Show Podcast

Play Episode Listen Later Jul 17, 2022 183:11


Sit back and enjoy NQ Fishing Show 16th July catch up show , plenty of fishing business to discuss. How to keep your live bait fresh , Marty,s harbour barra trip plus plenty of other tips and tricks , so grab a coldie and enjoy everything North Queensland has to offer. The NQ Fishing Show is Proudly supported by Humminbird/Minn Kota , Mako Eyewear , Samaki , Tacspo , Yozuri , Rid insect Repellant , Eagle Claw , Hooked Apparel , Crabba , Ironman 4x4 , Ecooda and Bladerunner knives  

NQ Fishing Show Podcast
NQ FISHING SHOW 2nd JULY PODCAST

NQ Fishing Show Podcast

Play Episode Listen Later Jul 2, 2022 180:31


We have a great show today Jason Masters joins us in the studio , Jase cut his teeth fishing Hinchinbrook Channel and shares his knowledge with us. We also have our usual guests , tips tricks and lots of laughs , so sit back grab a coldie and enjoy 3 hours of Aussie larrikinism  Proudly Supported By Mako Eyewear , Samaki , Tacspo , Yozuri , Eagle Claw , Rid insect repellant , Humminbird/Minn Kota , Bladerunner knives

Habari za UN
Ripoti ya FAO yaonesha mchango wa uvuvi na ufugaji wa samaki katika kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa chakula

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 29, 2022 2:26


Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiwa katika siku ya tatu hii leo huko Lisbon nchini Ureno Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ongezeko kubwa la ufugaji wa samaki sambamba na uvuvi wa kimataifa umesababisha mazao ya vyakula vya majini kuwa kwenye rekodi ya juu katika kuchangia kwa kiasi uhakika wa chakula na lishe katika karne hii ya Ishirini na moja. Taarifa ya Leah Mushi. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya FAO iliyotolewa leo kwenye miji ya Lisbon Ureno na Roma Italia ikinukuu Ripoti ya mwaka huu wa 2022 kuhusu Hali ya uvuvi na mazao ya majini au SOFIA.  Akizungumzia ripoti hiyo Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu amesema jumla ya uvuvi na ufugaji wa samaki ulifikia kiwango cha juu cha tani milioni 214 mwaka 2020 ikijumuisha tani milioni 178 za wanyama wa majini na tani 36 za mwani.  Uvuvi na ufugaji wa samaki huchangia katika ajira, biashara na maendeleo ya kiuchumi. Jumla ya mauzo ya kwanza ya thamani ya uvuvi na ufugaji wa samaki na wanyama wa majini kwa mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa dola bilioni 406, ambapo dola bilioni 265 zilitokana na uzalishaji wa ufugaji wa samaki.  FAO imesema ukuaji wa uvuvi na ufugaji wa samaki ni muhimu duniani kote katika jitihada za pamoja za kumaliza njaa na utapiamlo lakini kunatakiwa kufanyika mabadiliko ili kukabiliana na changamoto zilizopo.  Dongyu amesema wakati sekta hiyo ikizidi kukuwa “kunahitajika mabadiliko ili kuwa na sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu zaidi, yenye ushirikishaji na usawa kwakuwa biashara ya kutumia vyakula vya majini ni muhimu ikiwa tunataka kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa”.  “Lazima tubadili mifumo ya chakula kitokanacho na kilimo ili kuhakikisha vyakula vya majini vinavunwa kwa uendelevu, maisha yanalindwa na makazi ya majini na viumbe hai vinalindwa”  Na ili kupata suluhisho la changamoto za uzalishaji huo Mkurugenzi Mkuu wa FAO anayehusika na Idara ya Uvuvi na Ufugaji wa samaki Manuel Barange amesema kunahitajika  mabadiliko ya bulu “Ni mchakato unaoendeshwa na malengo ambapo wanachama na washirika wa FAO wanaweza kuongeza mchango wa mifumo ya chakula cha majini ili kuimarisha uhakika wa chakula , lishe bora na lishe kwa gharama nafuu huku ikibaki ndani ya mipaka ya ikolojia” 

NQ Fishing Show Podcast
NQ Fishing Show June 25th

NQ Fishing Show Podcast

Play Episode Listen Later Jun 26, 2022 183:11


Tune in to NQ Fishing Show June 25th catch up show , I have been away on holidays so have missed a couple of weeks so sit back grab a coldie and tune in. Graham from G & T fishing school and charters joins us for a chat plus I let you all know how cool my NTH/Western Queensland holiday was. The NQ Fishing Show is proudly supported by Humminbird/Minn Kota , Yozuri Lures , Mako Eyewear , Samaki , RID insect repellent , Tacspo Distributing , ironman 4x4 , eagleclaw hooks and Ecooda

NQ Fishing Show Podcast
NQ Fishing Show 30th April Catch Up

NQ Fishing Show Podcast

Play Episode Listen Later May 1, 2022 189:59


Tune in to our 30th of April show , Mal the create man joins us to talk about his whiting adventures plus all the other chit chat , So sit back grab a coldie try not to fall asleep :) and enjoy 3 hours of fun Proudly brought to you by Lucinda Fishing Lodge ,Humminbird/Minn Kota ,Samaki ,Tacspo Eagle claw ,Yozuri Lures ,Bladerunner knives

JACKPOT 919
JACKPOT 56

JACKPOT 919

Play Episode Listen Later Apr 5, 2022 56:47


Boys' Shorts - New Era (Vocal Radio Mix); Marc Brauner & Jimbo Mack - Birkenstocks & Crocs; Casual Connection - The Mission (Casual Connection Boogie Funk Rework); Dance System - Filter Funk; Kush Jones - Raver Type Stab; Nikki Nair - 1overf; Slackin Beats - With Me; Harvey Sutherland - Feeling Of Love (India Jordan Remix); Physical Therapy - 2 Tears (Ladies Night Dub); Smokey Bubblin' B - FTC; FlexFab & Ziller Bas - Haha! Haha!; DJ Sugar C - I'm Lost; DJ Smilez - Can't Stop (Smilez remix); Chance de la Soul - You, Me; SBTRKT - The light; Samaki - hartsfield

SNACK 919
JACKPOT 56

SNACK 919

Play Episode Listen Later Apr 5, 2022 56:47


Boys' Shorts - New Era (Vocal Radio Mix); Marc Brauner & Jimbo Mack - Birkenstocks & Crocs; Casual Connection - The Mission (Casual Connection Boogie Funk Rework); Dance System - Filter Funk; Kush Jones - Raver Type Stab; Nikki Nair - 1overf; Slackin Beats - With Me; Harvey Sutherland - Feeling Of Love (India Jordan Remix); Physical Therapy - 2 Tears (Ladies Night Dub); Smokey Bubblin' B - FTC; FlexFab & Ziller Bas - Haha! Haha!; DJ Sugar C - I'm Lost; DJ Smilez - Can't Stop (Smilez remix); Chance de la Soul - You, Me; SBTRKT - The light; Samaki - hartsfield

RadioRahma
Takataka Za Plastiki Zinavyotumiwa Kuimarisha Mazingira.

RadioRahma

Play Episode Listen Later Mar 21, 2022 12:06


Idadi ya uchafu wa plastiki baharini imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni, Likiwa ni tatizo kubwa linalokabili mazingira duniani. Jambo ambalo limeathiri sana upatikanaji wa Samaki kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya bahari eneo la pwani, Lakini kikundi cha Gazi Women Magrove Boardwalk kimejitolea kulinda msitu wa mikoko katika eneo hilo la Gazi ili mbali na kulinda mazingira, pia wapate kipato cha kujikidhi kimaisha. Kama anavyotueleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Habari za UN
FAO yawapigia chepuo wavuvi wadogo na wafugaji wa samaki

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 1, 2022 3:06


Mkutano wa siku nne wa wakuu wa nchi zenye bahari duniani, umeanza leo huko Roma Italia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo -FAO limetoa wito kwa wasomi, serikali, mashirika ya kiraia na sekta binafsi kutambua umuhimu wa wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki, ambao ni sehemu muhimu ya uvuvi. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Happiness Palangyo wa Redio washirika Kids Time FM ya Morogoro Tanzania (Taarifa ya Hapiness Palangyo ) Bahari, inachukua jumla ya  asilimia 70 ya uso wa dunia na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Lakini bahari inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uvuvi wa kupita kiasi, uchafuzi wa bahari na mabadiliko ya tabianchi na hivyo vyote vinatishia uwezo wa bahari kuendelea kutoa huduma muhimu za mfumo wa ikolojia na rasilimali muhimu za chakula. Wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki ni sehemu muhimu ya mifumo ya chakula duniani na inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kulinda bahari, hata hivyo, hawatambuliwi au kueleweka vyema kama anavyoeleza mvuvi José Tejeda Dumé kutoka Santo Domino, DOMINICAN REPUBLIC. “Sekta fulani zinatupuuza. Hawaoni kwamba mvuvi huamka saa 10 alfajiri na kukumbana na dhoruba na mvua. Ni lazima aende baharini ili kuwapatia rizki watoto wake.” FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP imejitolea kuimarisha shughuli za uvuvi wa kisanaa, kuhakikisha kuwa watu wanaohusika katika sekta hii wanapata usaidizi na kutambuliwa ipasavyo kama anavyoeleza  Vera Agostini, Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uvuvi na Ufugaji wa samaki cha FAO "Uvuvi mdogo mdogo na ufugaji wa samaki hautambuliki kuwa ni muhimu sana. Tukiangalia tu baadhi ya takwimu zinaweza kukusaidia kuelewa, zinaweza kutusaidia sote kuelewa kwamba asilimia 90 ya wanaojihusisha na uvuvi ni wale ambao ni wavuvi wadogo, watu milioni 60 na asilimia 40 ya hao ni wanawake. Kwa hivyo, kwa kweli ni sehemu muhimu ya uvuvi, lakini hazitambuliki na hazithaminiwi. Tunahitaji kupata neno kuhusu umuhimu wao, na tunahitaji kuwasaidia watoa maamuzi kutambua hilo na kuchukua hatua”. Agostini ameongeza kuwa FAO inaamini mifumo ya chakula cha majini ni sehemu muhimu ya mifumo ya chakula duniani. Kwa nini? ( Sauti ya Vera Agostini, Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uvuvi na Ufugaji wa samaki cha FAO) “Kwa sababu wao huboresha lishe, haswa kwa walio hatarini zaidi, ni sehemu muhimu ya ukuaji wa uchumi, na hutoa suluhisho ambazo hupunguza kiwango cha uharibifu wa mazingira cha mifumo ya chakula. Kwa hivyo, mkutano huu wa kilele ni fursa muhimu sana kuleta ajenda hiyo ya mabadiliko ya bluu na kushiriki katika mazungumzo na kundi tofauti la wadau watakaokuwepo”. FAO imejidhatiti kuimarisha shughuli za uvuvi wa kisanaa, kuhakikisha kuwa watu wanaohusika katika sekta hii wanapata usaidizi na kutambuliwa ipasavyo.

Habari za UN
Nchini Zimbabwe FAO kuhakikisha ufugaji samaki una tija shambani hadi mezani 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 2, 2022 2:13


Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa teknolojia ya ufugaji wa Samaki nchini Zimbabwe imekua bado lengo la kufanikisha uhakika wa chakula kwa kuhakikisha Samaki anafika mezani bado linakabiliwa na changamoto kwa kuwa gharama ya ufugaji ni ya juu halikadhalika gharama ya kitoweo hicho. Kariba nchini Zimbabwe katika mabwawa ya ufugaji Samaki yanayomiliwa na Lake Harvest Farm, teknolojia ni ya kisasa kuanzia shambani hadi kiwandani ikiwemo uchambuzi wa samaki aina ya sato.  Kutoka Kariba tunaingia Karoi, shamba lingine lingine la ufugaji samaki likimilikiwa na kampuni ya ufugaji samaki ya Edeni, na mmiliki wake Hafra Nanhanga, naye anafuga sato na anasema, “nilipoingia kwenye ufugaji wa sato, nilidhani ni rahisi, hasa tulipoanza kujenga mabwawa tulijua tunaweza kuchimba tu mashimo yetu na kujenga kuta, kumbe tunahitaji mashine za kuchimba.”  Tariro Chari, Meneja Mkuu wa shamba la Lake Harvest  anasema samaki anafugwa majini kwa kati ya miezi sita hadi tisa kulingana na uzito anaotaka mnunuzi wa kati ya gramu 300 hadi 900 na “suala kubwa kwa mfugaji yoyote wa sato ni lishe ya Samaki, kwa sababu chakula kinagharimu asilimia 60 ya gharama zote za uendeshaji.”  Kwa kutambua kuwa Zimbabwe ni nchi isiyo na baharí, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO lilianzisha mradi wa kusaidia wafugaji wa Samaki ili kuongeza kipato na kuimarisha afya kupitia kitoweo cha Samaki, mradi unaoitwa FISH4ACP uliobuniwa na shirika la nchi za Afrika, Karibea na PAsifiki, na kutekelezwa na FAO.  Mradi unawekeza kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji wa Samaki kuanzia shambani hadi mezani lakini bado ulaji samaki nchini Zimbabwe ni wastani wa kilo 2.6 kwa mtu mmoja kwa mwaka ilhali katika nchi za ukanda huo wastani wa ulaji ni kilo 6.   Gilles Van De Walle wa kitengo cha ufugaji Samaki FAO anasema, “tunataka kufanya kazi kuanzia kwenye boti au kwenye nyavu hadi kwa walaji. Tunataka huu mnyororo uwe na manufaa kama inavyotakiwa.”  FAO imetangaza mwaka 2022 kuwa mwaka wa kimataifa wa uvuvi wa kienyeji na ufugaji wa Samaki. 

Habari za UN
Jarida 01 Februari 2022

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 1, 2022 13:03


Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa  Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya inayoonesha kuwa mifumo ya usimamizi wa taka za afya duniani kote hivi sasa imezidiwa uwezo kutokana na maelfu ya tani za taka zinazotokana na vifaa vilivyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la COVID-19 na hivyo kutishia afya ya binadamu na mazingira na wakati huo huo kufichua hitaji kubwa la kuboresha udhibiti wa taka zinazozalishwa kutokana na huduma ya tiba.  Tathmini mpya ya uhakika wa upatikanaji wa chakula iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Januari 2022 na Shirika la Umoja wa Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP, inaonesha takriban asilimia 40 ya wakazi wa Tigray Ethiopia wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula ikiwa ni miezi 15 ya migogoro kaskazini mwa Ethiopia.  Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa teknolojia ya ufugaji wa Samaki nchini Zimbabwe imekua bado lengo la kufanikisha uhakika wa chakula kwa kuhakikisha Samaki anafika mezani bado linakabiliwa na changamoto kwa kuwa gharama ya ufugaji ni ya juu halikadhalika gharama ya kitoweo hicho.  Na leo mashinani tunakwenda nchini Bangladesh ambako mradi wa ILO umemgeuza mtoro wa shule kuanza kupata kipato ambacho hakutarajia. Karibu! 

Habari za UN
IFAD yasaidia wanawake wa kisiwani Sumar Ufilipino kujikomboa kiuchumi 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 18, 2022 3:33


Mradi wa samaki unaofadhiliwa na Mfuko wa  Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo duniani FAO na Serikali ya Ufilipino, umekuwa mkombozi kwa wakina mama ambao hapo awali walikuwa hawana shughuli ya kuwaingizia kipato na sasa wanawake hao, wamejiinua kiuchumi kwa kutumia mbinu walizojifunza enzi za utotoni pamoja na utaalamu wa kisasa waliopatiwa.   Asubuhi ya kupendeza yenye pilika pilika kwa wafanyabiashara wa soko la Guiyang nchini Ufilipino, katika kisiwa cha Sumar kilichoko mashariki mwa nchi hiyo. Ruperta Gagarin akiuza samaki aliowakausha kwa bei nzuri ya kumpatia faida, lakini hali haikuwa hivi hapo awali anasema, “Sasa naweza kununua chakula, nguo za watoto wangu na vifaa vya shule. Lakini hapo awali hali haikuwa hivi, nilikuwa napata msongo wa mawazo, nilikuwa tu mama wa nyumbani, haikuwa rahisi, kuwanunulia wanangu maziwa ilikuwa kitu kigumu, nilijihisi mnyonge sababu sikuweza kumsaidia mume wangu. Akiwa hana kitu chochote maana yake siwezi hata kuwanunlia watoto maziwa au chakula chetu.“ Ruperta alijifunza kukausha samaki akiwa na umri wa miaka 13 lakini ni miaka michache tu iliyopita ndio aliamua kuubadili utaalamu wake huu kuwa biashara na kuweza kupata faida. Mradi wa samaki wa kwenye matumbawe unaofadhiliwa na IFAD na serikali ya Ufilipino, umewapatia mafunzo Ruperta na wanawake wengine namna ya kuongeza kipato kwenye samaki wao. Anasema, “kipindi cha nyuma tulikuwa tunajua tuu kupaa samaki, kuwaweka chumvi na kuwaanika, lakini sasa tunatumia teknolojia bora na njia nzuri zaidi za kutengeneza bidhaa zenye ubora. Mradi wa Samaki wa Matumbawe umetupa vikaushio vya kutumia umeme wa jua, meza za chuma kisichoingia kutu, mizani ya kupimia, visu, ubao wa kukatia samaki na mabox ambayo ndio tunaweka bidhaa zetu na kisha tunatoa upepo nakuzifunga , na pia wametupa share zetu tunazovaa. “ Na sasa wanawake hawa wanaweza kuzalisha samaki iwe jua au mvua na hii imesaidia kuwa na uhakiki wa kuwa na uzalishaji endelevu usioathiriwa na msimu wa hali ya hewa. Mradi huu wa IFAD umesaidia kuhamasisha wanawake kufanya kazi kwa pamoja na kubadilishana uzoefu wao na kutumia kwa pamoja rasilimali chache walizonazo na Ruperta anasema wanafuraha wakati wote hata wakiwa na changamoto. Wanakikundi hawa wa Taytay wamepatiwa mafunzo ya kutafuta masoko na huduma kwa wateja na sasa wanauza bidhaa zao kwenye maonesho ya biashara pamoja na masoko ya maeneo wanayoishi. “Kwa usaidizi wote tuliopata, kwakweli sasa tuna maendeleo makubwa, hapo awali wanawake wote hawa walikaa nyumbani wakisubiri kuletewa na waume zao, lakini sasa tumeelimika na kuwezeshwa kujitegemea. Sisi wanawake tuna uwezo wetu, uimara wetu na mawazo yetu, hata kwenye kuuza na kufanya mipango mingine yakujipatia fedha, tuifanyie kazi.” Hivi sasa Ruperta na wanakikundi wenzake wana mipango mikubwa ya kuuza samaki wao katika mikoa mingine na kuwahamasisha wanawake wengine kufuata nyayo zao.  

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
Habari za UN
Sophie afurahia mradi wa UNHCR ulivyomnusuru kiuchumi ukimbizini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 28, 2021 2:39


Nchini Cote d'Ivoire  shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta tabasamu na nuru kwa wakimbizi ambao biashara zao zilivurugika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambalo limetikisa dunia kuanzia mwaka jana wa 2020. Kwa sasa wakimbizi hao wakiwemo wa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wana imani ya kujiinua tena kiuchumi kama anavyosimulia Happiness Pallangyo wa Radio washirika Radio Uhai FM ya Tabora Tanzania katika taarifa hii iliyoandaliwa na UNHCR. “Mimi ni mtaalamu wa kusafisha Samaki,” ndivyo asemavyo Sophie Lilombi Mwika, mkimbizi kutoka DRC ambaye sasa anaishi kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Cote d'Ivore, Abidjan.  Katika video ya UNHCR, Sophie akiwa nyumbani kwake akiandaa Samaki anaokausha kwa chumvi anasema “naipenda kazi hii kwa sababu kupitia biashara ya samaki nimeondokana na umaskini.” Sophie alikimbia DRC kutokana na ghasia na hapa Cote D'Ivoire akaanza biashara ya samaki wakavu. Akiwa anakagua vitabu vyake vya mahesabu ya biashara anasema, “COVID-19 imeniumiza sana. Ni kama vile imenichapa kiboko kama tusemavyo nchini mwetu DRC. Biashara ilipungua.” Sophie alikuwa anauza Samaki wakavu siyo tu nchini Cote D'Ivoire bali pia nchi jiran ikiwemo ya Mali. Fedha alizopata aliweza pia kutuma nyumbani DRC kwa familia yake na hata alikuwa amepanga kupanua eneo la kuhifadhi samaki. Hata hivyo ujio wa COVID-19 ukalazimu nchi kufunga mipaka ambapo mauzo yalipungua kwa theluthi tatu na hivyo akasitisha mpango wa kupanua ujenzi wa eneo la kuhifadhi samaki. Mungu si Athumani, wahenga wamenena! UNHCR ikaingilia kati na kumpatia Sophie na wakimbizi wengine 80 mafunzo ya kuinua upya biashara zao sambamba na fedha taslimu za mtaji. Leonidas Nkurunzinza ni Naibu Mwakilishi wa UNHCR nchini Côte d'Ivoire: “Idadi kubwa ya watu tunaowasaidia wameathirika zaidi kuliko wengine. Hii ni kwasababu wako kwenye sekta isiyo rasmi, wakifanya biashara ndogo za kujikimu.” Na sasa kwa Sophie mambo ni mazuri akisema “mimi ni mwanamke thabiti hii leo kwa sababu ya biashara yangu ya Samaki wakavu. Ninajivunia na ninajivunia kile nilichoanzisha. Tuko huru kufurahia maisha.“ Ama hakika furaha hadi kuimba na kucheza!  

Habari za UN
CHOMBO KILICHOPIKIWA SAMAKI HAKIACHI KUNUKA VUMBA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2021 0:39


Katika kujifunza Kiswahili leo tunapata ufafanuzi wa Methali “CHOMBO KILICHOPIKIWA SAMAKI HAKIACHI KUNUKA VUMBA” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA 

Uchumi na Biashara
Uchumi na Biashara Podcast; Uuzaji wa Samaki, kipato tosha

Uchumi na Biashara

Play Episode Listen Later Nov 4, 2021 28:05


Nelson Babu ana taaluma ya uhasibu. Alifutwa kazi wakati korona iliporipotiwa nchini. Hata hivyo hakukata tamaa; amezamia biashara ya samaki mtaani Pipeline, Nairobi. Biashara yake licha ya kuanza ikiwa ndogo, amefanikiwa kufungua tawi jingine mtaani Umoja na anatazamia kufungua matawi zaidi, mbali na kuwapa vijana ajira. Esther Kirong' amezungumza naye

Habari za UN
FISH4ACP kunasua wavuvi na wachuuzi wa samaki Katavi nchini Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 6, 2021 4:27


Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limetambulisha mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika mkoani Katavi baada ya mradi huo unaohusisha nchi 12 za Afrika, Karibea na Pasifiki kuwa na matokeo chanya kwa wavuvi mkoani Kigoma. Devotha Songorwa wa Radio washirika KidsTime FM anafafanua zaidi katika ripoti hii. Mkoani Katavi, kusini magharibi mwa Tanzania shughuli mahsusi ni utambulishaji wa mradi wa FISH4ACP ( Fish for ACP) unaolenga kuboresha mazao ya baharini kwa lengo la kulinda mazingira na kuinua kipato cha wananchi. Walengwa ni wavuvi na mmoja wao akanieleza Akizungumza na UN News, Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvivu na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin amesema mradi huu ulioanza kutekelezwa nwezi Septemba mwaka jana wa 2020 unagharimu zaidi ya dola milioni  46. Na vipi ujio wa mradi huu mkoa wa Katavi? Naye Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Donald Kusekwa amebainisha kuwa kwa sasa hali ya uvuvi Wilayani Tanganyika  siyo ya kuridhisha kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kusababisha kupungua kwa dagaa na samaki hivyo kufanya wakazi wa maeneo hao kukosa kitoweo hicho na ujio wa mradi wa FISH4ACP ni mkombozi kwao na umewafika kwa wakati sahihi. Nao baadhi ya wavuvi na wafanya biashara wakazungunzia ujio wa mradio huo na namna utakavyowanufaisha kufanya shughuli zao kuondokana na Uvuvi wa mazoea hatimaye kuvua kisasa.  

Habari za UN
Kupiga makasia na kula samaki mwarobaini wa unene uliopiliza nchini Tonga

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 30, 2021 2:27


Nchini Tonga, moja ya mataifa ya visiwa vidogo lililoko katika bahari ya Pasifiki, vijana wanafundishwa stadi ya utengenezaji mitumbwi kama njia mojawapo ya kujipatia kipato, kulinda mazingira na kupunguza unene uliopitiliza au utipwatipwa. Kwa vipi?  (Taarifa ya Leah Mushi) Katika karakana ya utengenezaji wa mitumbwi nchini Tonga, taifa lenye visiwa vidogo 170 na ambako chakula si mazao yalimwayo nchini humo bali kwa kiasi kikubwa vilivyosindikwa na hivyo kusababisha kuwa moja ya nchi yenye watu wengi tipwatipwa duniani. Tawfiq El-Zabri ni Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD na anafafanua.  "Tonga inakabiliwa na viwango vya juu kabisa vya lishe duni na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama unene kupita kiasi na mengi ambayo yanahusiana na ukosefu wa lishe bora. Eneo la ardhi ni dogo na limeathiriwa na maji ya chumvi, mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la idadi ya watu na kwa hivyo ni muhimu watu hapa kupata nafasi ya kwenda baharini kuvua samaki. " Ili kunusuru vijana wa Tonga, IFAD ikaamua kuanzisha mradi kwa kushirikiana na serikali pamoja na taasisi ya MORDI TONGA ili kutoa mafunzo stadi ya kutengeneza mitumbwi, wakufunzi wakiwa ni wazee. Kupitia mafunzo mosi, vijana wanapata nyenzo za uvuvi, pili stadi za kupiga makasia zitawaweka kwenye afya njema kwani ni mazoezi, na tatu samaki watakaovua baharini watawasaidia si tu kupata kipato bali lishe bora kama anavyoeleza Alipate Sailosi mkufunzi na kiongozi wa jamii ya Eua. “Kwa sasa watu lazima walipe fedha ili waweze kwenda baharini kwa kutumia boti. Lakini ukiwa na mtumbwi, kisha ukapata kifungua kinywa kizuri, hapo kijana atapata nguvu ya kutosha kupiga makasia siku nzima ” Vijana walioanza kunufaika na mradi huu wa IFAD wanashukuru kama anavyosema Okusi Lama “Nimejifunza vitu vingi wakati wa mafunzo. Ningependa kuwahimiza vijana wahudhurie kwa sababu hii inaweza kuwa njia ya kuwanufaisha sio tu kama wavuvi, bali pia kama mafundi. ” Mradi huo pia unakusudia kuwa hakikisho la upatikanaji wa chakula na kuwa chanzo cha kipato cha ziada kwa familia za Tonga.

Habari za UN
Watoto wenye  umri wa chini ya miaka 2 hawapatiwi chakula au virutubisho wanavyohitaij : UNICEF

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 22, 2021 2:48


Watoto wenye  umri wa chini ya miaka 2 hawapatiwi chakula au virutubisho wanavyohitaij ili waweze kukua vyema na hivyo kukwamisha makuzi yao, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF hii leo. Taarifa zaidi na John Kibego. Video ya UNICEF inatupatia taswira ya lishe kwa watoto ikianzia Indonesia mama na mwanae mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja akichagua matunda sokoni na kisha mlo kamiliifu wa wali, mboga na kitoweo akipatiwa mtoto. Kisha ni Sudan Kusini katika kituo cha afya cha afya ya mama na mtoto kazi ikiwa ni upimaji wa viwango vya utapiamlo. Ripoti ya UNICEF ikipatiwa jina la Wamelishwa ili Wakwame? Janga la mlo watoto wakiwa wachanga, imetolewa leo wakati kunafanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo endelevu ya chakula. Ripoti inaonya kuwa ongezeko la umaskini, ukosefu wa usawa, mizozo, majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi, na dharura za afya kama vile janga la COVID-19 vinasababisha janga la lishe miongoni mwa watoto na hakuna dalili zozote za mabadiliko katika miaka 10 iliyopita. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore anasema, “Matokeo ya ripoti hiyo ni dhahiri kwamba hali inapokuwa mbaya, mamilioni ya watoto wanalishwa mlo waporomoke. Lishe duni katika miaka miwili ya mwanzo ya mtoto inaweza kukwamisha ukuaji wa viungo na ubongo na hivyo kuwa na madhara yasiyorekebishika kielimu, ajira na mustakabali wake. Wakati tumebaini hilo kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwepo na maendeleo kidogo katika kuwapatia watoto lishe bora na salama. Na COVID-19 inaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.” Uchambuzi uliofanyika katika nchi 91 umebaini kuwa ni nusu tu ya watoto wenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi 23 ndio wanapatiwa idadi ya milo inayotakiwa kwa siku, huku theluthi moja wanapatiwa kiwango kidogo cha mlo ili waweze kuishi. Janga la COVID-19 limefanya hali kuwa mbayá zaidi kwa kuwa baadhi ya familia zimelazimika kupunguza ununuzi wa vyakula vyenye lishe kutokana na ukata. Ripoti inapendekeza kuwa ili watoto wapate lishe bora, serikali, wahisani, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo washirikiane kubadili mifumo ya vyakula, afya, hifadhi ya jamii kwa kuchukua hatua kama vile kuongeza fursa ya kupata na kumudu vyakula vyenye lishe yakiwemo matunda, mboga za majani, mayai, nyama, Samaki na vile vilivyoongezewa virutubisho kwa kuwekea motisha uzalishaji, usambazaji na uuzaji wake. Halikadhalika kutekeleza sheria na kanuni za kitaifa za kulinda watoto dhidi ya vyakula visivyo na lishe na kutokomeza mbinu hatarishi za kibiashara zinazolenga watoto na familia zao. Mbinu mbalimbali za mawasiliano zitumike kuhamasisha matumizi ya vyakula salama na vyenye lishe ili wazazi na watoto waweze kutambua umuhimu wa vyakula hivyo. Ripoti inasema hilo linawezekana kwa kuwekeza.

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Shamba la Samaki

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Shamba la Samaki

Habari za UN
Kijana msomi ageukia ufugaji wa nzi ili kunusuru wafugaji wa samaki 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 17, 2021 4:36


Vijana katika sehemu mbalimbali duniani wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kubonga bongo na kusongesha maendeleo yao pale walipo kwa kubaini suluhisho la changamoto zinazokabili jamii inayowazunguka. Miongoni mwao ni Dayana Olembe kutoka Tanzania ambaye baada ya kubaini kuwa wafugaji wa kuku na samaki wanapata shida kupata protini ya kile wanachofuga, akaamua kuingia katika biashara ya ufugaji wa nzi. Ni kweli utashangaa nzi? Ndio! Anafuga nzi, kulikoni?Ungana basi na Devotha Songorwa wa radio washirika Kids Time FM ya nchini Tanzania ambaye alizungumza naye na kuandaa makala ifuatayo.

Habari za UN
Ninatumia nishati ya jua katika ufugaji wa samaki - George Muga

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 13, 2021 3:21


Moja ya masuala yaliyojadiliwa kandoni mwa Mkutano wa ngazi ya juu ya siasa kuhusu maendeleo endelevu unaoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ni pamoja na namna waafrika wengi wanavyopambana na njia za zamani za nishati na hivyo kutafuta njia mbadala kama vile matumizi ya nishati ya jua.  Mfano halisi ni huko nchini Kenya ambako mfugaji wa Samaki amepata mafanikio makubwa baada kuwekeza  kwenye vifaa vya nishati ya jua. George Muga anaelezea manufaa yaliyotokana na hatua aliyoichukua na pia kuwashauri wale walio na miradi inayotumia umeme.

Banh Mi Podcast
#10 – Dara, de Evaan Market et Samaki Kohn Khmer, l'artisanat, la culture, et la solidarité cambodgienne

Banh Mi Podcast

Play Episode Listen Later Apr 15, 2021 64:50


« Je suis parti faire mes propres recherches, j'ai étudié l'histoire du Cambodge. Je me suis réapproprié mon identité, mes racines, et ça m'a rendu fier. » Dans ce 10ème épisode, Linda rencontre Dara, créateur d'Evaan market, et co-fondateur de l'association Samaki Kohn Khmer. Dara est entrepreneur, il a créé en 2019 une plateforme en ligne de créations et produits authentiques en provenance de l'Asie du Sud Est, Evaan Market, il a aussi co fondé l'association Samaki Kohn Khmer qui met en lumière la richesse culturelle cambodgienne. Dara retrace son enfance dans un quartier populaire de St Cyr l'école où il était le seul asiatique, il arrête tôt ses études et commence à travailler pour subvenir à ses besoins. Il se confie sur sa quête identitaire qui commence à la vingtaine et ce désir de comprendre son histoire, ses racines, l'histoire du Cambodge. On parle des traumatismes que nos parents ont pu vivre lors du génocide des khmers rouges de 1975 à 1979, du livre auto biographique de Loung Ung « D'abord ils ont tué mon père » , et de la difficultés à parler de ses sujets avec nos parents. Dara me parle de sa fierté de renouer avec son identité et de son envie de partager autour de lui la richesse de la culture Khmère en co-fondant en 2013 avec Samara l'association Samaki Kohn Khmer (Jeunesse solidaire cambodgienne). Ils organisent de nombreux évènements qui réunissent toutes les générations, des concerts, font venir des artistes cambodgiens en France et on parle de cette connexion qu'il est nécessaire de maintenir entre la diaspora cambodgienne en France et dans le monde avec le Cambodge. On discute de son premier voyage au Cambodge qui le bouscule et se rend compte de la chance qu'il a d'avoir grandi en France, il réunit alors des personnes et mènent des projets collectifs en réunissant des fonds pour venir en aide à des personnes au Cambodge : en commençant par vendre des bracelets à 2euros, puis en organisant des forums associatifs lors d'un des plus grand évènements pour la communauté cambodgienne, tous les ans en avril pour le Nouvel an khmer à la pagode de Vincennes. Cet élan de solidarité prend une proportion encore plus grande lors des inondations d'octobre 2020. Par la force des réseaux sociaux et la solidarité de la communauté asiatique, il récolte plus de 7000 dollars qui aide plus de 200 familles au Cambodge. Dara lance en 2019, sa plateforme en ligne de vente de produits venus d'Asie du sud est, Evaan market. A travers ses produits, c'est un héritage culturel, des traditions qu'il veut mettre en avant. On finit l'épisode par le partage des festivités de nouvel an cambodgien, ses meilleures adresses de restaurant et une musique qui symbolise la fusion des traditions et de la modernité Cambodgienne. Pose toi avec moi et Dara et écoute ce qu'on t'a préparé. Pour donner de la force au podcast, mettez lui des étoiles et commentaires sur vos plateformes de podcast préférées. Pour suivre Dara, Evaan market et Samaki kohn khmer: @sabaydara @evaanmarket @samakikohnkhmer Pour suivre Banh Mi podcast: @banhmi.podcast/ banhmiculture.com/ Musique Intro: Benjamin Pham Références citées dans l'émission Restaurants: En lai, Bamboo d'or, Basilic and spy, Siem reap Paris Time to Rise, Vannda ft. Master Kong Nai Partagez cet épisode à ceux que vous aimez.

Uchumi na Biashara
BIASHARA YA SAMAKI

Uchumi na Biashara

Play Episode Listen Later Mar 20, 2021 12:49


Katika Ushauri wa Kibiashara na Fedha, mwanahabari wetu Moses K. Kiraese anazungumza na Julius Okello, mfanyabiashara wa samaki katika Soko la Kacheliba, Kaunti ya Pokot Magharibi.

Habari za UN
Uvuvi uko njiapanda licha ya umuhimu wake katika kukabiliana na umasikini-FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 23, 2020 1:59


Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema uvuvi uko njiapanda hususani katika nchi maskini ingawa ni wazi kuwa samaki ni muhimu katika kupambana na umaskini.

Habari za UN
Mafunzo kupima watoto utapiamlo Niger ni hali ya kumfundisha mtu kuvua ili apata samaki kila wakati

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 16, 2020 2:05


Wahenga wanasema usimpe mtu samaki bali mfundishe kuvua ilia pate samaki kila wakati, na hivyo ndivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Niger limefanya kwa kuwapatia wazazi ujuzi wa kupimia watoto wao utapiamlo nyumbani badala ya kusubiri kwenda vituo vya afya kama njia mojawapo ya kutokomeza janga hilo linalokumba takribani watoto 400,000 kila mwaka.  

KIDDCAST SHOW
KIDDCAST EPISODE 25 - THE FINAL RECAP - OFF THE SHELF TAPES + ANDREW KIBE & BOBO SAMAKI LOST TAPE

KIDDCAST SHOW

Play Episode Listen Later Oct 3, 2020 23:04


The Final Recap is a mash up of select sections of our conversation from our Off The Shelf Tapes, plus a bonus lost tape of a conversation with Andrew Kibe and Muthoni Mwangi a.k.a Bobo Samaki.

Weltverbesserer
55 Samaki - ein Aquaponik-Konzept

Weltverbesserer

Play Episode Listen Later Sep 14, 2020 22:05


Heute habe ich wieder einen Weltverbesserer vom Enactus Verein hier bei mir sitzen, - es ist Mark Mehler, Student aus Aachen. Er möchte uns das Projekt Samaki vorstellen. Als allererstes, lieber Mark, erklär mal bitte wofür der Name Samaki steht.

Radio Uhai Broadcast
Unampa Taulo Samaki Ajifute Maji (Swahili)

Radio Uhai Broadcast

Play Episode Listen Later Aug 4, 2020 27:00


The Social Kick Podcast
The Social Kick Podcast #049 - Jason Dunford

The Social Kick Podcast

Play Episode Listen Later Jul 31, 2020 76:20


In this episode of The Social Kick, Jason Dunford joins the show to discuss his careers as an Olympic swimmer, tech startup co-founder, reporter, and rapper. A true renaissance man, this conversation explores Jason’s evolution from a young swimmer in Kenya to one of the best butterfliers in the world, his transition into business and an MBA at Stanford GSB, to his life now as Samaki Mkuu (rap star) including special guest Jabali Afrika. For a special treat, Samaki and Jabali perform live!      

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
PHONE CALL
S01E03 with DR.Zack

PHONE CALL

Play Episode Listen Later Apr 17, 2020 16:05


Katika Episode hii nipo na mtaalam wa kupigia promo Samaki aina ya Dagaa na pia ni mtu wa kuweka wazi Maparody kwenye mtandao wa twitter yani watu wanaotumia Identity ambazo sio zao ili kuweza kujipatia Follows, Nimepiga nae story kibao bila kuhasau scandal yake ya kuzusha msiba na kula pesa za rambirambi. Kwenye mtandao wa twitter ana followers wasiopungua Elfu 60.

The Player's Perspective: Uncensored with Larry O'Bannon
13. Roles & Egos of The NBA w/ Samaki Walker: Shaq & Kobe; The 3 J's in Dallas (Pt. 2 of 2)

The Player's Perspective: Uncensored with Larry O'Bannon

Play Episode Listen Later Apr 4, 2020 29:26


This week, in the second part of a two part interview, Samaki talks about the friction between Kobe and Shaq being the alpha dawg in LA, the Tony Braxton saga with the three J's in Dallas, the infamous playoff series Lakers vs Kings and we finish off with our Barrel Proof Segment of rapid fire questions. Tune in to see what our bourbon of the day is for this episode.

The Player's Perspective: Uncensored with Larry O'Bannon
13. Roles & Egos of The NBA w/ Samaki Walker: Shaq & Kobe; The 3 J's in Dallas (Pt. 1 of 2)

The Player's Perspective: Uncensored with Larry O'Bannon

Play Episode Listen Later Apr 3, 2020 29:17


On today's episode, we're joined by former NBA lottery pick and World Champion Samaki Walker. We talk about Samaki's collegiate career and early times I'm the NBA after being drafted as a 20 year old to the Dallas Mavericks. He discusses his playing experience with two of the NBA's top organizations (San Antonio Spurs & Los Angeles Lakers), learning from some of the all-time great players and playing for two of the all-time great coaches in Grep Popovich and Phil Jackson.

No Referees Podcast
Samaki Walker (Part 2)

No Referees Podcast

Play Episode Listen Later Mar 26, 2020 60:15


In this episode, Evarist speaks with 10-year NBA veteran, NBA champion and 1996 NBA Draft Lottery pick, Samaki Walker. Samaki compares and contrasts the coaching styles between the Zen Master and Coach Pop. He also shares some hilarious stories about his Lakers teammates, how he would fair in today's game, advice he gives to his children about going through the recruitment process and much more from second part of his NBA career

No Referees Podcast
Samaki Walker (Part 1)

No Referees Podcast

Play Episode Listen Later Mar 19, 2020 52:40


In this episode, Evarist speaks with 10-year NBA veteran, NBA champion and 1996 NBA Draft Lottery pick, Samaki Walker. Samaki talks about his upbringing in Columbus, schools us on the difference between Kicker and JBL subwoofers, his infamous draft day suit, a hilarious story about Suge Knight and much more from his first five years of his NBA career.

Forgotten Lakers
Episode 29: Samaki Walker

Forgotten Lakers

Play Episode Listen Later Oct 15, 2018 42:36


Former Los Angeles Laker Samaki Walker came on the podcast to discuss his two years in LA. After coming to the Lakers via free-agency before the 2001-2002 season, Samaki entrenched himself as a starter, using his size and strength to play alongside Shaquille O'Neal and helped the team to their third-straight title.

Hoopchalk - AAU Youth Basketball Podcast
Top Secret Training That Nobody Uses!

Hoopchalk - AAU Youth Basketball Podcast

Play Episode Listen Later Sep 4, 2017 24:36


About 4 Years ago Moses had the privilege of training with 10 year NBA veteran Samaki Walker. For him it was what's supposed to happen when you are 8 years old and training to be in the NBA, but for me it was kind of surreal. After about a month or two of training with him I felt comfortable enough to ask him some for some sage advice about the basketball world and what he told me those many years ago led me on a search that has forever changed our basketball lives. Our conversation went a little something like this: Me: Samaki what is the difference between the great players and the good players in the NBA. Samaki: What do you mean? Me: I mean at the NBA level every guy was the star of his college team or high school team or Euroleague team, but only a few become the best of the best. What would you say is the difference? Samaki looked at me and without any hesitation he said: Metal toughness. Of course being the "Any edge is a good for my kid" kind of dad. I thought "Hey! Let me look for mental toughness training. That will give us an edge on top of the physical part." I looked high and low and couldn't find anything that really spoke to helping kids with mental toughness. I mean, when the biggest challenge of your day is losing in Overwatch or getting fewer likes on instagram  than you would like, how do you develop true mental toughness? I read sports psychology book after sports psychology book and looked up every article I could find, but I couldn't find anything for young basketball players. So... I kind of forgot about it and just stuck to the physical training and then IT happened! MY KID STOPPED PERFORMING IN GAMES! In practice he would be a monster and then on game day he would clam up. I tried it all, rewards for performance, money, angry talks on the way home, happy talks on the way home. NOTHING WAS WORKING! It was then that my conversation with Samaki's came back to me. The difference is mental toughness! I dug out all of the books that I had read before and started using their knowledge and suggestions. However, I couldn't use them exactly as they were written because they were written for grown men and women. So I altered them a little and like magic my kid came back! He was scoring at will and easily. He was BACK! I then added more from the books and articles and he became even more relaxed and comfortable during on game day! It was awesome! I saw other dad's struggling with the same thing and not trying to be one to give out all of our secrets I quietly thought. Man, if he only knew X,Y, and Z! I kept my secrets to myself for a little while, but my conscious got the best of me and GAME READY was born. I created GAME READY for those parents that have kids that are awesome during practice but struggle during games. It's kind of my way of making it available for anyone who wants it without giving everyone our secret sauce. If you are reading this you are one of the few that are going to get the secret information that I wold have killed for when our kid was struggling. So buckle up and take notes. Your life and your young athletes life is about to change for the better. What is the Hoopchalk Basketball Podcast? The Hoopchalk Basketball Podcast is the best Youth Basketball podcast for young AAU basketball players and their families. Our motto is - NO MORE GUESS WORK! Our mission is to help young basketball players and their families successfully navigate the ever-changing world of youth basketball. In this podcast we will unlock all of the locked doors that have become road blocks for youth basketball players. We will also help those who dream, but have no idea how to move towards their basketball dreams. Figuring it out alone is a pretty daunting task. I was in your shoes. My son Moses and I invite you to learn from our wins and our losses. We hope it will help someone else in their journey toward their dreams. In this podcast, we will cover everything about youth basketball - from what to look for when joining a team, to college recruiting, to social media, and even how to develop the mental toughness that will allow your young athlete to soar in games. "There I was with this kid who wanted to follow his dream of playing pro basketball and, as a non-basketball parent, I had no idea how to make it happen. When I asked others, I constantly heard things like - 'You just have to be good and people will find you.' I knew that waiting for the phone to ring couldn't be the key to success. So I started digging and I found out that, like every career, there is an actual path that you MUST take to even have a chance. I am excited to share my findings with you. Let's work together to make this happen for our little and not-so-little ballers!" - Troy Horne See you inside episode 19! Troy and Moses Horne hoopchalk.com

Deborah Kobylt LIVE
Samaki Walker - Former NBA Champion

Deborah Kobylt LIVE

Play Episode Listen Later Aug 30, 2017 30:38


Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 13, 2016 9:18


Ufugaji wa samaki wa kisasakwenye visima au mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani na Ufugaj huu wa samaki ni sawa kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Katika makala haya ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa juma hili itangazia kwa ujumla kwa juu ya ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki wa kisasa 

dunia katika yako fahamu samaki mazingira kesho ufugaji
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Sehemu ya Pili:Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 13, 2016 9:59


Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani kote inchi kama .Niwazi tumeona baadhi ya inchi nyingi zikizidi kuzalisha nafasi nyingi za ajira kwa shughuli hizi pamoja na kukuza kipato cha mhusika mmoja mmoja, jamii flani na taifa kwa ujumla. Katika kuiangalia fursa hii katika sehemu yetu ya pili na ya mwisho ya makala yetu ya Mazingira Leo Dunia Yako Kesho kwa juma hili tutaangalia juu ya mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki wa kisasa