POPULARITY
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya maendeleo tangu Januari 2025 kumesababisha takribani wanawake na wasichana milioni moja duniani kupoteza huduma muhimu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro. Ikitolewa leo Geneva, Uswisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo iliyopatiwa jina ‘Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika' miongoni mwa changamoto ilizozitaja ni pamoja na kuwa asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi na kwamba mashirika mawili kati ya matano yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.Huko Sudan, nchi inayoumia kwa vita kwa miaka minne sasa, kumetangazwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu hali inayozidisha wasiwasi kuhusu usalama wa jamii zilizo hatarini, hususan katika mji wa El-Obeid uliozingirwa, ambako mashambulizi ya kila siku ya ndege zisizo na rubani yanaendelea kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Dkt. Shible Sahbani, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan akizungumza kwa njia ya video na waandishi wa habari leo mjini Geneva, uswisi amesema, “tumerekodi zaidi ya wagonjwa 1,330 wa kipindupindu, huku watu 114 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Hii inaonesha kiwango cha vifo miongoni mwa wagonjwa wa kipindupindu cha asilimia 13.7, ambacho ni cha juu sana. Na bila shaka, msimu wa mvua unaotarajiwa utaifanya hali kuwa mbaya zaidi.”Na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu Ufuatiliaji wa Elimu Duniani, umeonesha kuwa misaada ya kimataifa kwa sekta ya elimu imeendelea kupungua na nchi 113 duniani zinatumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko pesa wanazoziwekeza kwenye elimu. Matokeo ya utafiti huo yamewekwa wazi leo mbele ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Mageuzi ya Elimu TES+4 unaofanyika Paris, Ufaransa ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mageuzi ya Elimu uliofanyika mwaka 2022 na pia ili kusongesha zaidi ufikiaji wa Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu Elimu Bora.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako miongo ya vita imeacha maelfu ya watoto bila familia, elimu au usalama, Lydie Mbusa Mwenge ameweka maisha yake katika mstari wa mbele wa kupigania haki za wasichana walioathiriwa na vita. Mwenge ni mwanzilishi na mratibu wa shirika la Action Intervention des Femmes Entrepreneurs pour le Développement, linalojikita katika kulinda na kuwawezesha wasichana walio chini ya umri wa miaka 18, hususan wale manusura wa ubakaji, kupoteza familia zao au kulazimika kuishi mitaani. Bi. Lydie Mwenge amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii, ungana nao.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa kingono.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea na harakati za kutoa msaada wa dharura kwa Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo jana Jumatano Juni 24, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 164 pamoja na uharibifu mkubwa katika mji mkuu, Caracas, na maeneo ya jirani. Matetemeko hayo mawili yenye ukubwa wa 7.2 na 7.5 katika kipimo cha Richter yametokea ndani ya muda wa chini ya dakika moja, yakiharibu nyumba, hospitali, barabara na miundombinu mingine muhimu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi wa mabaharia duniani, akionya kuwa ongezeko la migogoro na mivutano ya kisiasa linaweka maelfu ya wafanyakazi wa baharini katika hatari wakati wakiendelea kuhakikisha biashara na usafirishaji wa bidhaa duniani vinaendelea. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mabaharia, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Juni, Katibu Mkuu amesema karibu asilimia 90 ya bidhaa na mahitaji muhimu duniani, ikiwemo chakula, dawa na nishati, husafirishwa kwa njia ya bahari.Na maandalizi ya Mkutano wa 15 wa Afrika Kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, AfIGF utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Ghana yameanza ambapo maoni ya wadau yatakusanywa ili kuweka mazingira salama ya matumizi ya intaneti barani Afrika na hatimaye duniani. Vijana na watoto kutoka nchi mbalimbali wamekutana jijini Nairobi Kenya kuandaa mawazo yao na mmoja wao ni Sheryl Christine Adhiambo kutoka taasisi ya Legal Sisters ya nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Je, maisha yangekuwaje kama kila manusura wa ukatili wa kijinsia angejua mahali pa kupata msaada kwa wakati? Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linaimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, hususan katika maeneo ya pembezoni. Kupitia mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana Zanzibar na Kuimarisha Uongozi wa Wanawake, manusura wanapata habari muhimu, ushauri nasaha na msaada wa kisheria wakati wowote. Feissal Kirwa na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia wito wa UN wa kulinda mamilioni wa wakimbizi kote duniani, masuala ya kijinsia Zanzibar nchini Tanzania, na ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani.Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi kesho Juni 20, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na hatua za kimataifa za kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao kote duniani kutokana na vita, vurugu na mateso.Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani. Takribani watoto 24,174 waliuawa, kujeruhiwa, kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha, kubakwa au kuathiriwa kwa namna nyingine na ukiukwaji mkubwa wa haki katika maeneo yenye mizozo mwaka 2025.Je, maisha yangekuwaje kama kila manusura wa ukatili wa kijinsia angejua mahali pa kupata msaada kwa wakati? Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linaimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, hususan katika maeneo ya pembezoni. Kupitia mradi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana Zanzibar na Kuimarisha Uongozi wa Wanawake, manusura wanapata habari muhimu, ushauri nasaha na msaada wa kisheria wakati wowote.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Leo tunakupeleka Zimbabwe kwa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia ya “Unlimited Hope Alliance”. Kandoni mwa moja ya mikutano ya Zama Zijazo ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani alipata fursa ya kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akipaza sauti kwa viongozi wa dunia kuhakikisha wanawake na wasichana wa vijijini hawapewi kisogo katika ajenda za maendeleo, elimu na teknolojia. Flora Nducha anafafanua zaidi alichomueleza katika taarifa hii
Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula barani Afrika, utumikishaji wa watoto jeshini Sudan Kusini, na ujumbe wa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia nchini Zimbabwe.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na Mpango wa Chakula Duniani, WFP, yametoa onyo kali kuwa hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kwa mamilioni ya watu katika nchi 13 zilizotajwa kuwa maeneo hatari ya njaa kati ya mwezi Juni na Novemba mwaka huu wa 2026.Watoto tisa waliokuwa wakihusishwa na vikosi vya ulinzi katika Jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wameanza safari mpya ya maisha baada ya kutambuliwa, kuachiliwa na kukabidhiwa kwa ajili ya kurejeshwa katika familia na jamii zao.Leo tunakupeleka Zimbabwe kwa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia ya “Unlimited Hope Alliance”. Kandoni mwa moja ya mikutano ya Zama Zijazo ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani alipata fursa ya kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akipaza sauti kwa viongozi wa dunia kuhakikisha wanawake na wasichana wa vijijini hawapewi kisogo katika ajenda za maendeleo, elimu na teknolojia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Baadhi ya wanawake wenye miaka 40 na zaidi, hujipata wana koma kupata hedhi. Hali hii huja na changamoto mbali mbali kwa wahusika.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waaandishi wa habari kuwa “Kuna zaidi ya washukiwa 500 na vifo 130 vinavyohisiwa kutokana na ugonjwa wa Ebola, na maabara zimethibitisha watu 30 wanaugua ugonjwa huo.” Mbali ya DRC, wagonjwa wawili wamegundulika huko Kampala Uganda na mwingine raia wa Marekani ambaye amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi, wakati huu ambapo WHO bado inakumbwa na sintofahamu kuhusu chanzo cha mlipuko wa sasa wa Ebola DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD, limetoa ripoti ukionesha uchumi wa dunia unakabiliwa na mtihani mpya kutokana na mishtuko ya biashara, chakula na fedha inayosambaa kimataifa. Ripoti hiyo inaonya kuwa licha ya kuanza kwa mwaka kwa matumaini mazuri, hali ya kijiografia, vita na changamoto za masoko sasa zinatishia ukuaji wa uchumi duniani. UNCTAD inaeleza kuwa nchi zinazoendelea ndizo zilizo hatarini zaidi, zikikabiliwa na mtikisiko wa mitaji, mzigo wa madeni na hofu ya uhaba wa chakula. Shirika hilo linashauri mataifa kuchukua hatua za kuimarisha sera za uchumi, biashara na uwekezaji ili kujikinga na madhara ya mishtuko hiyo.Na panya wanazua balaa huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Wananchi wanasema kuwa panya wanaingia kwenye mahema kila siku, wanachafua akiba ya chakula, na kushambulia watoto wadogo nyakati za usiku. Ikumbukwe baada ya vita kusitishwa wananchi walirejea katika maeneo yao lakini kwakuwa nyumba zililipuliwa wengi wanaishi kwenye mahema huku mazingira yakiwa machafu na mifumo ya maji ikiwa haifanyi kazi na hayo ni mazingira mazuri kwa panya kuzaliana.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kwa Chama cha Wanawake Majaji, (TAWJA) ambacho kimetambua pengo la upatikanaji wa haki hususan kwa wanawake na wasichana na tunasikia hatua zinazochukuliwa kuziba pengo hilo kutoka kwa mwenyekiti wake, Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia tunakuletea mhtasari wa habari kama zifuatazo..Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangazwa kwa mara nyingine kugundulika kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC katika jimbo la Ituri lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya 17 kwa mlipuko wa Ebola kutokea DRC tangu kugunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976. Wagonjwa 13 vimethibitishwa na taasisi ya utafiti wa tiba ya INRB mjini Kinshasa. Dkt. Tedros amesema tayari wametuma wataalamu, vifaa tiba na ameruhusu kutolewa kwa dola laki tano kusaidia kudhibiti mlipuko huo na kuwahudumia wagonjwa.Hali ya kibinadamu nchini Somalia inazidi kuwa mbaya kuliko ilivyotarajiwa hapo awali. Akuzungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi afisa mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia George Conway amesema “Hivi sasa Takriban watu milioni sita nchini Somalia amba ni sawa na mtu mmoja kati ya sita anakabiliwa na njaa ikimaanisha kuwa anaruka muda wa kula chakula, au anaenda siku kadhaa bila chakula cha kutosha. Watoto ndio wanaolipa gharama kubwa zaidi. Karibu watoto milioni mbili wana utapiamlo mkali, ikimaanisha kuwa wana utapiamlo mbaya na dhaifu kimwili, na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kuugua au kufa.”.Na leo ni siku ya Kimataifa ya Familia, Umoja wa Mataifa unasema maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia jinsi umaskini, ukosefu wa huduma muhimu na msaada mdogo wa malezi vinavyoathiri familia na kudhoofisha maendeleo bora ya watoto. Maadhimisho ya mwaka huu yanaweka mkazo maalum kwenye hatua jumuishi za ulinzi wa kijamii kama vile ruzuku za watoto, likizo za uzazi zenye malipo, huduma nafuu za malezi ya watoto na elimu ya awali kwa watoto wadogo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW70 uliofanyika mwezi Machi mwaka huu hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo tulipata fursa ya kuzungumza na washiriki wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya wanawake. Miongoni mwao ni Severina Lemachokoti kutoka asasi ya kiraia ya Naretu Girls and Women Empowerment Programme iliyoko kaunti ya Samburu nchini Kenya, ambaye katika mahojiano na Flora Nducha ameelezea jinsi mila na desturi kwa wanawake na wasichana kutorithi chochote kwenye jamii yao zinavyoanza kuyoyoma. Pia tunamsikia kutoka Salome Gatakaa Araka wa FODDAJ ambalo ni Jukwaa la Maendeleo ya Wanawake, Demokrasia na Haki, nchini Kenya ni shirika la kiraia ambalo mwaka huu kwa mara nyingine lilishiriki mkutano huo wa CSW70. Baada ya kushriki vikao mmoja wa viongozi wa shirika hilo amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na ndio msingi wa mahojiano haya.Tunakuletea pia muhtasari wa habari zikiwemo za hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na Sudan, pamoja na masuala ya afya tukimulika yanaoendelea kuhusu virusi vya Hanta au Hantavirus.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar.Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia..Mwenyeji wako ni Anold Kayandai, karibu!
Je Akili mnemba AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake. Tuungane na Leah Mushi kusikia wamesema nini kuhusu AI.
Wanawake wanao ishi katika maeneo ya jiji la Melbourne wame andaliwa tukio maalum Jumapili 10 May, ambayo huadhimishwa kama siku ya kina mama.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Wanawake watatu wa Australia wenye uhusiano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (ISIS) wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya utumwa, uhalifu dhidi ya binadamu, na mashtaka ya ugaidi, baada ya kurejea nyumbani kutoka miaka kadhaa ya kuzuiliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Syria.
Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka sasa watu watatu wamepoteza maisha.Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Zaidi ya wanawake na wasichana 100 wanakimbia makazi yao kila saa nchini Sudan Kusini huku kuongezeka kwa mapigano na njaa kukichochea kuongezeka kwa janga la kibinadamu, Anna Mutavati, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women) ameeleza leo baada ya ziara ya siku tano nchini humo.Kupitia taarifa ya UN Women iliyosambazwa leo kwa vyombo vya habari katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba na katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva, Uswisi, Anna Mutavati amenukuliwa akisema, “takribani asilimia 60 ya watu 223,641 ya waliokimbia makazi yao tangu mwanzo wa mwaka huu nchini Sudan Kusini ni wanawake na wasichana, wastani wa wanawake 104 kila saa,” na akaongeza kuwa baadhi ya wanawake na wasichana “wanakula mimea ya porini ili kuishi,” huku wengine wakikaa siku kadhaa bila kula. Amefafanua zaidi kuwa sehemu kubwa ya watu waliokimbia makazi yao ni kutoka Jimbo la Jonglei, ambako takribani wanawake na wasichana 174,197 wameathiriwa na mapigano. Bi. Mutavati amesema wanawake na wasichana ni miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi ya kulengwa, ikiwemo shambulio la Machi katika Eneo la Utawala la Ruweng lililosababisha vifo vya watu wasiopungua 169 akionya kuwa ghasia zinazidi kuongeza hatari kwa wale waliokwishakimbia makazi yao. Pia ameeleza wasiwasi kuhusu kusambaratika kwa huduma muhimu, akisema uporaji na uharibifu wa vituo vya afya umeacha wanawake bila huduma muhimu za matibabu. “Wanawake wanajifungua bila huduma yoyote ya kitabibu kwa hatari kubwa ya kupoteza maisha,” amesema. UN Women inakadiria wanawake na wasichana milioni 5 nchini Sudan Kusini wanahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu, wakiwemo milioni 2.5 wanaohitaji huduma zinazohusiana na ukatili wa kijinsia.Akitoa wito wa hatua za haraka, Bi. Mutavati amesema uongozi wa wanawake lazima ubaki kuwa kiini cha juhudi za amani na ametoa wito wa kuheshimiwa kwa kiwango cha asilimia 35 cha uwakilishi wa wanawake serikalini chini ya makubaliano ya amani. “Hakuna njia ya amani ya kudumu iliyothibitika zaidi kuliko uongozi wa wanawake,” amesema, huku pia akitaka ufadhili kwa mashirika yanayoongozwa na wanawake na msaada kwa kaya zinazoongozwa na wanawake. Wakati Sudan Kusini ikielekea katika uchaguzi wa mwaka huu 2026, Mkurugenzi huyo wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika wa UN Women ametoa wito wa kuwepo kwa mchakato wa uchaguzi unaoaminika, jumuishi na wa uwazi unaohakikisha ushiriki wa wanawake katika kila hatua. Amenukuliwa akisema, “tunatoa wito wa utekelezaji kamili na wa haraka” wa makubaliano ya amani, na akasisitiza kuwa kulinda wanawake na wasichana na kuhakikisha wanashiriki katika uamuzi ni msingi wa kufikia amani ya kudumu.
Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mauaji wa wanawake na wasichana Gaza, ukatili wa kijinsia na wa kingono unaotumiwa kama silaha ya vita Sudan, na msaada wa dawa na matibabu ya bure nchini DRC yanyoendeshwa na walinda amani wa MONUSCO kutoka Tanzania.Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Ukatili wa kijinsia na wa kingono unatumiwa kama silaha ya vita nchini Sudan, jambo ambalo limesahaulika huku migogoro ikiendelea katika maeneo mengi mengi kote duniani amesema Tonderai Chikuhwa, Mshauri Mwandamizi wa Sera katika Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Ukatili wa kijinsia katika Migogoro, katika mahojiano na Khaled Mohamed wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa.Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mji wa Oicha wiki hii.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika kuunga mkono lengo namba 9 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kuhusu miundombinu na ujenzi wenye mnepo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania, limeingia makubaliano ya kimkakati na Taasisi ya wanawake wasanifu Majenzi, TAWAH, kwa ajili ya kuboresha sekta ya ujenzi. Makubaliano hayo yaliyowekwa saini Aprili 8, 2026, yanalenga kutambua madini ya ujenzi na viwandani yaliyosahaulika, kukuza ujenzi usioharibu mazingira na kuwawezesha wanawake kiuchumi. Rashid Malekela na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za Umoja wa Mataifa za kutafuta suluhu ya vita nchini Sudan pamoja na simulizi za wakimbizi ikiwa leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini humo, na miundombinu na ujenzi wenye mnepo nchini Tanzania.Wakati vita nchini Sudan ikiingia mwaka wa nne tangu kuvuka kwa mapigano baina ya jeshi la Sudan na kikosi vya msaada wa haraka RSF, hii leo huko Berlin nchini Ujerumani unafanyika mkutano wa Kimataifa ukilenga kurejesha mgogoro wa Sudan katika ajenda ya juu ya kidiplomasia duniani.Leo ni miaka mitatu kamili tangu vita vilipoanza nchini Sudan 15 Aprili 2023, mgogoro ambao umegeuka kuwa moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani. Mamilioni ya watu wamekwama katikati ya mapigano, kuwa wakimbizi wa ndani na nje, njaa na ukosefu wa makazi, huku mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yakionya kuwa mateso yanaendelea kuongezeka kila uchao.Katika kuunga mkono lengo namba 9 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kuhusu miundombinu na ujenzi wenye mnepo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania, limeingia makubaliano ya kimkakati na Taasisi ya wanawake wasanifu Majenzi, TAWAH, kwa ajili ya kuboresha sekta ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ubaguzi katika sehemu za kazi, unyanyasaji wa kijinsia na ukosefu wa usawa wa kifedha—hizi ni baadhi ya sababu, zinazowafanya wanawake wahitaji huduma maalum za kisheria.
Wanawake na wasichana wanaokimbia vita vya Sudan wanaelezea ubakaji, mateso na unyanyasaji, huku wafanyakazi wa misaada wakionya kwamba mateso yanazidi kuwa makubwa kuliko visa vinavyofikia huduma ya matibabu.
Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujielez tangu mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, mabomu ya kutegwa ardhini na ujumbe wa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka Kenya.Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk.Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba' kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini.Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao. Feissal Kirwa wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyo.
Wiki iliyopita Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kilikunja jamvi baada ya wiki mbili za kujadili mada ya haki, haki za kisheria na kuchukua hatua kuhakikisha haki za wanawake na wasichana zinapatikana. Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.
Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW70, Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo DRC, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaeleza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka, mathalan huko Lebanon watu 816,000 sawa na asilimia 14 ya watu wote wamekimbia makazi yao. Na huko Iran watu milioni 3.2 wanakadiriwa kukimbilia maeneo ya Kaskazini mwa taifa hilo na vijijini wakikimbia machafuko. Namba ya dharura ya msaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UHCHR inapokea zaidi ya simu 1,000 kwa siku za watu wakiomba msaada.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya kuwa njaa duniani inaweza kufikia viwango vya juu mwaka huu iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea na bei ya mafuta itabaki kuwa juu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Carl Skau amesema “Ongezeko la gharama za chakula na mafuta duniani zinaweza kuacha mamilioni ya familia zikiwa nje ya uwezo wa kununua vyakula, hasa katika nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa kama vile Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Kwa hakika, uchambuzi wetu unakadiria kwamba, kama mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea hadi mwezi Juni, watu zaidi ya milioni 45 wanaweza kuingizwa kwenye njaa kali kutokana na bei kuwa juu na hii itaweka rekodi ya juu ya njaa duniani kote. Na haya ni matarajio mabaya.".Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo moja ya matukio ya kando ya Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 ni Kushughulikia vikwazo vya haki ya kijinsia kupitia mfumo wa Mahakama ya Mtandao nchini Tanzania kwa lengo la kufanikisha haki kwa wanawake na wasichana. Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania anasema mashinani mfumo unatumia simu zisizo janja na akisema mobile app ni apu ya kwenye simu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana. Flora Nducha amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa vijana washiriki kutoka Ghana na kutuandalia taarifa hii
Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Wanawake kutoka jumuiya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wana jiandaa kwa sherehe maalum ya siku ya wanawake.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia yaliyojiri katika mkutano wa CSW70, ambapo kandoni mwa mkutano huo Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza na Lucy Kabyemera, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Makazi nchini Tanzania aliyeongoza kikao hicho na kumpatia ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mabadiliko ya sera.Idadi ya watu waliokimbia makazi yao nchini Iran imeongezeka kwa kasi na kufikia takriban watu milioni 3.2 kutokana na mashambulizi makali yanayozidi kushika kasi nchini humo kutoka jeshi la Marekani na Israeli huku nayo Iran ikijibu mashambulizi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kupitia taarifa yake iliyotolewa leo jijini Geneva, Uswisi, limebainisha kuwa kaya kati ya 600,000 na milioni 1 zimepoteza makazi yao, huku wengi wakikimbia miji mikubwa kama Tehran kuelekea maeneo ya vijijini na mikoa ya kaskazini kutafuta usalama. “Hali hii imeleta hofu kubwa ya kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu kadiri uhasama unavyozidi kusambaa katika maeneo mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelezea kuhusu matumizi makubwa ya fedha kwenye silaha za kivita wakati huu ambapo dunia ina uhitaji mkubwa wa msaada wa chakula na maeneo kadhaa kuwa na hali mbaya ya chakula huku mgao wa chakula ukitolewa mara moja au mbili badala ya mara tatu sababu ya ufinyu wa ufadhili. Dkt Tedros amesema matumizi ya kijeshi duniani yamefikia $ trilioni 2.7 - katika mwaka mmoja. Na kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, kukomesha njaa duniani ifikapo mwaka wa 2030 kutahitaji $ bilioni 93 kila mwaka. “Hiyo ina maana kwamba tunatumia karibu mara 30 zaidi kila mwaka kuuana kuliko kuhakikisha kila mtu anakula.”Leo ni Siku ya Mlo shuleni. Mamilioni ya watoto duniani kote huenda shuleni kila siku bila kutia chochote tumboni. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP, zaidi ya watoto milioni 100 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati hukabiliwa na njaa kila siku. Hali hii huathiri uwezo wao wa kuzingatia masomo, kujifunza na kufaulu darasani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, WFP inaunga mkono serikali mbalimbali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapata milo shuleni ili wawe na afya njema na wawe tayari kujifunza.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia habari ya kusikitisha ya kifo cha mfanyakazi wa UNICEF nchini DRC, na ujumbe wa washiriki wa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.Shirika la UNICEF limesema limesikitishwa na kushtushwa na kifo cha mfanyakazi wake Karine Buisset kilichotokea katika shambulio linaloripotiwa kufanywa na droni katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhriy a Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo ambalo kwa muda mrefu limekumbwa na mapigano na hali mbaya ya kibinadamu. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, amesema shirika hilo pamoja na wafanyakazi wake duniani wameumizwa sana na tukio hilo.Oluwaseun Ayodeji Osowobi, mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Nigeria amezungumzia umuhimu wa kushirikisha wanaume katika harakati za kupigania haki za wanawake duniani wasichana.Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Oluwaseun Ayodeji Osowobi, mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Nigeria amezungumzia umuhimu wa kushirikisha wanaume katika harakati za kupigania haki za wanawake duniani wasichana. Rashid Malekela na maelezo zaidi.
Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana. Flora Nducha amekutana na baadhi yao kusikia maoni yao
Waziri Mkuu wa Australia amesema serikali itamsaidia yeyote kati ya timu ya soka ya wanawake ya Iran ambaye bado hajaomba hifadhi hapa.
Wanawake kote duniani walijitokeza mitaani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, wakitaka kukomeshwa kwa ukosefu wa usawa na ubaguzi.
CSW70 yang'oa nanga ikisistiza haki, haki ya kisheria na hatua kwa wanawake na wasichanaKikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kimefungu pazia hii leo jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”. Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750. Leah Mushi amefuatilia ufunguzi huo na hii hapa taarifa yake.(TAARIFA YA LEAH MUSHI)Natts……Katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani …. huu ni ufunguzi wa Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 Mgeni rasmi ni Katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye ameeleza…. Nats.. (SG cut 1 play under 00:06 I am so pleased to be in a…. )furaha yake kuwa katika ukumbi uliojaa viongozi waliokataa kukubali ukosefu wa usawa kama jambo lisiloepukikaKatika hotuba yake Guterres amesema dunia bado inaongozwa zaidi na mfumo dume unaowapa wanaume nafasi kubwa ya mamlaka. (SG Cut 1 – Fiesal )“Tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume, na utamaduni unaotawaliwa na wanaume. Usawa wa kijinsia ni suala la mamlaka. Hakuna hatua hata moja mbele kwa haki za wanawake ambayo imewahi kutolewa. Bali imeshinda. Wameshinda vizazi vya wanawake na wasichana, watetezi na wanaharakati, viongozi wa jamii na watafuta haki. Umeshinda wewe na kabla ya kitu chochote napenda kusema Asante.”Amesema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa katika jitihada za kufikia usawa wa kijinsia katika taasisi nyingi duniani. Hata hivyo, ndani ya UN kumekuwa na maendeleo muhimu katika kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wakati alipoanza uongozi wake, alijiwekea lengo la kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume katika ngazi za juu za uongozi wa Umoja wa Mataifa. Leo, amesema lengo hilo limefikiwa.(SG cut2 – Fiesal )“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa, wanawake sasa wanaunda nusu kamili ya nguvu kazi ya Umoja wa Mataifa katika vitengo vya kitaaluma na vya juu zaidi. Na kwa mara ya kwanza, tulifikia usawa katika uongozi mkuu. Tumefanya hivyo ikiwa ni miaka miwili kabla ya ratiba - lakini pia natambua imekuwa ni miaka 80 imechelewa.”Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa António Guterres amesisitiza kuwa kufikia usawa wa kijinsia si suala la haki kwa wanawake pekee, bali ni hatua muhimu kwa maendeleo ya dunia nzima. Amesema jamii ambazo wanawake wanapata haki na fursa sawa huwa na maendeleo ya haraka zaidi, uchumi imara na taasisi zenye uwajibikaji zaidi, akisisitiza kuwa kuimarisha usawa wa kijinsia ni msingi muhimu wa kufikia maendeleo endelevu duniani.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanawake wanapata haki na fursa sawa katika jamii duniani.Ametaja maeneo matano muhimu ya kuharakisha haki na usawa kwa wanawake ambayo ni kuhakikisha haki sawa za kiuchumi kwa wanawake, kuimarisha uwakilishi wao katika maamuzi ya kisiasa, kupanua upatikanaji wa elimu na fursa za kazi, kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, pamoja na kulinda haki za wanawake katika dunia ya kidijitali.Kwa upande wake mwenyekiti wa Kikao hicho cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 Maritza Chan Valverde amezungumzia maudhui ya mwaka huu ambayo ni “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote nakusema kila mtu anajukumu la kufanya (Maritza cut )“Ondo vikwazo na uhakikishe kwamba haki inakuwa ukweli halisi kwa…
Alya Abu Shawish, mwanamke aliyeko mstari wa mbele kuondoa hatari ya mabomu Gaza (OVERNIGHT)Hii leo pia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, imefanyika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo duniani kote iliadhimishwa jana Jumapili. Katika muktadha huo huo ninamualika Anold Kayanda atupeleke Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kumwangazia Alya Abu Shawish, Mwanamke anayefanya kazi katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma ya kutegua mabomu, UNMASakisaidia kuwaweka salama wenzake katika mojawapo ya mazingira hatari zaidi duniani. Karibu Anold.(Taarifa ya Anold)Asante Flora,Hakika Gaza ni moja ya mazingira hatari duniani kwa sasa. Alya Abu Shawish anaposhuka kwenye gari kabla ya kuingia ofis iza UNMAS zilizoko Deir al-Balah katikatimwa Gaza, anavaa jaketi la kujikinga na risasi.Ndani ya ofisi amesimama mbele ya ramani ya kidijitali, akifuatilia mienendo ya timu za wafanyakazi walioko mitaani zilizosambazwa kote katika ukanda huo wa Gaza ili kufanya kazi za kuondoa mabaki ya vilipuzi vya vita katika eneo hilo.Baada ya mipango yote kukamilika ofisini, sasa Alya Abu anaendesha gari akiwa na wenzake kuelekea kazini nje ya ofisi. Anaeleza akisema,(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kazi yangu kama mwanamke katika eneo hili inaonyesha kwamba wanawake wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha usalama na kuleta mabadiliko yanayoonekana, hata katika mazingira hatari na yenye changamoto kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza.”Alya Abu Shawish anaonekana na wenzake mitaani wakifanya kazi. Watoto wanafuata, kwa vyovyote wakitambua kazi muhimu inayofanywa na UNMAS kufanya mazingira yawe salama dhidi ya vilipuzi.Hata hivyo, nyuma ya dhamira hii ya kitaaluma kuna hadithi binafsi inaloakisi hali halisi ya maelfu ya wanawake huko Gaza.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kama mwanamke na mama, nimepitia changamoto nyingi ambazo wanawake wa Kipalestina huko Gaza hukabiliana nazo wakati wa vita hofu, kuhama makazi, uhaba wa mahitaji muhimu, na hali ya kutokuwa na uhakika kila wakati. Kama wanawake wengi hapa, nimelazimika kuilinda familia yangu huku nikikabiliana na hali hizi ngumu.”Licha ya changamoto hizi, Alya Abu Shawish anasema uzoefu wake umeimarisha azma yake ya kuwasaidia wengine na kumhamasisha kufanya kazi katika uwanja ambao mara nyingi huonekana kutawaliwa na wanaume.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Uzoefu huu haukunidhoofisha; uliimarisha azma yangu ya kuwasaidia wengine. Ulinitia moyo kufanya kazi katika masuala ya kuondoa mabomu na usalama na UNMAS uwanja ambao mara nyingi huonekana kuwa wa wanaume. Katika jukumu hili, ninachangia kupunguza hatari zinazosababishwa na mabaki ya vilipuzi vya vita na kusaidia jamii kuishi kwa usalama zaidi.”Wanawake wengine katika timu za UNMAS pia hushiriki katika shughuli za kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabaki ya vilipuzi, ambayo sasa yamekuwa moja ya changamoto kubwa zaidi za kibinadamu huko Gaza kadri uharibifu unavyoendelea kuenea. Kwa Abu Shawish, juhudi hizi hubeba ujumbe unaokwenda mbali zaidi ya kazi kwani inaonesha uimara na mnepo.
Katika Jarida la Habari Hii leo Kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea-Mashirika ya UN yatahadharisha kuongezeka kwa vurugu Mashariki ya Kati.-Mafunzo ya haki ya kumiliki ardhi yanayotolewa na Kituo cha Msaada wa Kisehria kwa Wanawake WLAC yamebadilisha maisha ya familia ikiwemo ya Jovita Provius: WLAC-Mpango wa Jamii Rafiki kwa Mtoto wazinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika Kaunti ya Samburu
Hii leo jaridani tunaangazia hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia huku vita vikiendelea kushika kasi nchini Iran, masuala ya afya ya wanawake na watoto nchini Burundi, na maisha ya baadaye ya watoto katika ukanda wa Gaza.Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo.Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa.Hakuna maisha ya baadaye! Siyaoni maisha ya baadaye kwani sioni wanaoshikamana nasi! Hayo ni sehemu tu ya maoni ya watoto walioko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima, mustakabali wao uko mashakani, na wanachohitaji kama inawezekana ni amani na ujenzi mpya wa makazi ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nyumba zao na kuacha kuishi kama wakimbizi katika ardhi yao wenyewe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk ameonya kuwa shinikizo linaongezeka duniani kote dhidi ya haki za wanawake, uhuru wa kiraia na taasisi za kimataifa akitoa wito kwa serikali kujitolea upya katika ushirikiano, uwajibikaji na utawala wa sheria. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Fundi wa magari mwanamke kutoka nchini Ethiopia anayehudumu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, Meja Tigist Ferede ametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, kwa kusimamia jukumu muhimu la wanawake katika operesheni za kulinda amani nje ya kushika bunduki. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Rashid Malekela.
Hii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake, na uhuru wa kiraia, ujumbe wa Bi Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, na ripoti ya IPC kuhusu njaa nchini Somalia.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk ameonya kuwa shinikizo linaongezeka duniani kote dhidi ya haki za wanawake, uhuru wa kiraia na taasisi za kimataifa akitoa wito kwa serikali kujitolea upya katika ushirikiano, uwajibikaji na utawala wa sheria.Kiongozi wa shirika kubwa zaidi la msaada wa chakula duniani ametangaza kujiuzulu. Bi. Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP amesema atajiuzulu wadhifa wake huo baada ya miezi mitatu ili kuzingatia afya yake, akisema bado hajapona kikamilifu baada ya kupata kiharusi mwaka jana 2025.Fundi wa magari mwanamke kutoka nchini Ethiopia anayehudumu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, Meja Tigist Ferede ametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, kwa kusimamia jukumu muhimu la wanawake katika operesheni za kulinda amani nje ya kushika bunduki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya IPU kuhusu uhasama wa wabunge, siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, na yalitojiri katika Jukwaa la akili unde au AI lililofanyika kwa siku mbili huko Nairobi, nchini Kenya.Wabunge kote ulimwenguni wanakabiliwa na viwango vinavyoongezeka vya vitisho, unyanyasaji na vurugu kutoka kwa umma imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Muungano wa Mabunge Duniani (IPU). Rashid Malekela na taarifa zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi mwaka huu mauadhui yakihimiza “Sayansi kwa Mustakabali Jumuishi kwa Wanawake na Wasichana” Kwamujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO leo hii , wanawake wanachangia chini ya theluthi moja ya watafiti duniani, kulingana hivyo kuziba pengo hili la kijinsia si suala la haki pekee ni muhimu kwa ubora, uhalisia na mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu.Jukwaa la akili unde au AI lililofanyika kwa siku mbili huko Nairobi, nchini Kenya limekunja jamvi ambapo mmoja wa washiriki amesema wanaodai kuwa bara la Afrika liko nyuma kwenye teknolojia hiyo, ni dhahiri shairi hawalifahamu vema bara hilo lenye mataifa 54.