POPULARITY
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Hali inazidi kuwa si hali huko Ukanda wa Gaza kwani sasa raia wanakwepa sio tu mashambulizi na magonjwa bali pia nyoka, panya na wadudu ambao wanasambaa kutokana na mazingira machafu. Watu wanajihifadhi kwenye maeneo ya wazi bila mifumo ya majitaka au ya kuondoa maji ya mvua. Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina imefika kupuliza dawa ili kulinda wananchi hao. Tuko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, video ya UNRWA inaonesha wafanyakazi wa shirika hilo wamefika kwenye makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani. Katika eneo hili majitaka yamezingira makazi ya wakimbizi kwani hakuna mifumo ya kuyaondoa.Kando kidogo, mama anaonekana akimsafisha mwanae kwa kutumia maji yaliyohifadhiwa kwenye dumu.Mama huyu ambaye jina lake halikupatikana anasema, nilifurushwa kutoka jiji la Gaza hadi hapa Khan Younis. Tumefika kwenye eneo lililokuwa wazi, kwa hiyo uwepo wa panya na wadudu unahatarisha maisha ya watoto wangu. Nina hofu kubwa ya afya ya watoto wangu kutokana na wadudu na panya.Sasa anaonekana afisa mmoja wa UNRWA akiwa na wenzake wakipita hema kwa hema wakigawa dawa za kuua wadudu hao.Afisa huyu anasema wamewapatia ushauri na mwongozo wa jinsi ya kutumia dawa hizo.Halikadhalika wamepuliza dawa za kuulia wadudu na pia kuondoa taka zilizokuweko karibu na makazi ya wakimbizi hao wa ndani.UNRWA inasema viwango vya juu vya joto, na uweko wa makazi hayo kwenye eneo la wazi ni mazingira rafiki kwa panya, nyoka na wadudu wengine.Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, tangu vita ianze Gaza, tarehe 7 Oktoba mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 1.9 wamefurushwa makwao.
Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa homa ya nyani au mpox barani Afrika na kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC huko Beni nchini DRC. Makala tanakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti.Makala inatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KiTiKi) unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa ufadhili wa Watu wa Jamhuri ya Korea.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani kanda ya Afrika, tunamsikia Shane Prigge mkuu wa mnyororo wa usambazaji, WFP Kenya akieleza jinsi UNHAS ambalo ni shirika la ndege la Umoja wa Mataifa la huduma za kibinadamu linavyowezesha mashirika ya kibinadamu kufanya kazi zao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti. Kupitia video ya Monusco iliyochapishwa mtandao wa X, John Matemuli, mwandishi wa habari wa kituo hicho cha Redio na Televisheni Beni, kilichositisha matangazo kwa karibu miaka mitano, anafafanua jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya kujengwa upya kwa kituo hicho.“Miaka mitano bila Radio na Televisheni ya kitaifa ya Kongo (RTNC) mjini Beni ilikuwa ya machafuko sana. Kulikuwa na wakati ambapo tulikuwa tukifanya kazi hata kutoka juu ya mti, unaweza kuamini! Tulihisi kwamba kulikuwa na hitaji, wananchi na hata baadhi ya viongozi walihisi vivyo hivyo.”Ezechiel Kambale, mkazi wa Beni naye pia anaeleza furaha yake.“Ulipita muda mrefu tangu redio hii kuwa hewani. Lakini sasa nashukuru kwamba wamerudi. Kuna tofauti kubwa ikilinganishwa na zamani, kwa sababu leo, hata kama niko mbali na mji, bado nayapata mawimbi ya redio kana kwamba nipo hapa mjini.”Tulimrudia John na kumuuliza kilichokuwa tofauti kuhusu kituo hicho hasa kabla ya msaada wa MONUSCO.“Kazi ilofanywa hapa imewaridhisha wananchi. Leo, tuna ofisi za usimamizi. Tuna studio za kisasa za televisheni. Tuna studio ya redio kwa ajili ya kutengeneza vipindi vyetu. Tuna chumba cha habari kilicho na vifaa vya kutosha. Tulikumbana na matatizo ambayo yalihitaji msaada katika ngazi zote, lakini MONUSCO ilitupatia vifaa, ambavyo sasa vinaturuhusu kufanya kazi katika hali bora.”
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa siku tatu, viongozi wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Chakula (WFP), Chakula na Kilimo (FAO) na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani, IFAD walikuwemo nchini Sudan Kusini kuona ni kwa jinsi gani miradi wanayotekeleza kwa pamoja ya kujenga mnepo na kuhakikisha lishe ya uhakika na bora imeleta mabadiliko. Wakazi wa Apada Boma jimboni Bahr el Ghazal Kaskazini nchini humo walikuwa taswira ya manufaa ya miradi hiyo ambayo wakuu hao walikagua kama inavyofafanua Makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi.
Hii leo jaridani tunaangazia Afya na malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Rwanda, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi..Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria. Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. .Mashinani tutaelekea nchini Rwanda kusikia ni kwa jinsi gani programu ya remedial ambayo imewafikia watoto zaidi ya 10,000 katika shule 200 na vituo 10 vya vijana imeboresha masomo kwa wanafunzi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. Mwandishi wetu wa nchini DRC, George Musubao amefuatilia na kuandaa makala hii.
Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau imeeleza bayana jinsi utalii kwenye maeneo ya milimani unaweza kuwa na manufaa sio tu kwa baiyonuwai bali pia kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo.Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO mjini Roma, Italia hii leo imesema chapisho hilo limetolewa ili kwenda sambamba na hitimisho la mwaka wa kimataifa wa maendeleo endelevu ya milima ulioanza mwaka jana wa 2022. Chapisho hilo linasema utalii wa milimani iwapo utasimamiwa kwa uendelevu, una nafasi kubwa ya kuinua vipato vya jamii zinazozingira maeneo hayo na kusaidia kulinda maliasili na utamaduni. Hata hivyo imebainika kuwa ukosefu wa data na ufahamu kuhusu fursa za kiuchumi na mazingira zitokanazo na utalii wa milimani umezuia jamii nyingi kunufaika na fursa hizo. FAO kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la utalii duniani, UNWTO na shirika la Mountain Partnership, MP, wametoa ripoti hiyo kama njia ya kuondoa pengo ili hatimaye jamii za maeneo ya milimani zipate kunufaika na fursa zilizoko. Mathalani chapisho linataka kusongesha upatikanaji wa takwimu za utalii wa milimani ambako ni makazi ya watu wapatao bilioni 1.1, baadhi yao wakiwa ni wale hohehahe zaidi na waliotengwa. Milima ina maeneo ambako watalii wanaweza kutembea, kupanda na kufanya michezo nyakati za majira ya baridi kali. Maeneo hayo yanaweza pia kuvutia wageni kutokana na taswira zake, utajiri wa baiyonuai na tamaduni za kipekee. Hata hivyo takwimu za karibuni zaidi za mwaka 2019 zinaonesha nchi 10 zenye milima zaidi duniani zilipokea asilimia 8 pekee ya watalii wa kimataifa duniani kote. Mkurugenzi Mkuu wa FAO QU Dongyu na Katibu Mkuu wa UNWTO Zurab Pololikashvili kupitia utangulizi wa ripoti hiyo wamesema kupata takwimmu za watalii wa milimani ni hatua ya kwanza muhimu tunayopaswa kuchukua. Uwepo wa takwimu sahihi utawezesha kufuatilia mienendo ya utalii kwenye maeneo hayo na kisha kutumia takwimu kusaidia mipango na kuandaa bidhaa endelevu kulingana na mahitaji ya watalii kwenye kila eneo husika na hatimaye sera za kuchochea utalii wenye manufaa kwa jamii.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga umeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu.wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.Video ya Benki ya Dunia inaanzia kwenye msitu wa bonde la Mto Congo ambako yaelezwa ekari nusu milioni ya misitu ya asili hutoweka kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa ajili ya shughuli za kilimo, kuni na kuchoma mkaa.Tunalima ardhi na kila siku nakata matawi ya miti na kuchanja ndoo moja ya kuni,” anasema Nzaka Ilanga akiwa porini akikata kuni akiendelea kusema zikiisha kesho tena narudi nakata nyingine kupikia chakula kwa ajili ya watoto.”Kwingineko anaoneka Guysha Izemengwe akichoma mkaa akisema anatumia miti midogo midogo kuchoma mkaa akisema anapata magunia 22 ya mkaa na kila moja anauza faranga 7,000 za DRC sawa na dola 3 na senti 50 na hiyo ndio chanzo cha kipato kwa familia yake.Kwa mujibu wa Benki ya Dunia ni asilimia 3.7 tu ya wananchi wa DRC ndio wanapata nishati ya kisasa ya kupikia.Shinikizo la ukataji miti holela linaweka mashakani wale wanaotegemea zaidi kwa chakula kama vile watu wa asili jimboni Mai- Ndombe ambapo Deko Louis akiwa anatembea msituni anasema…mitego yangu iko porini. Nawinda wanyama kwa ajili ya familia yangu. Siku hizi ni vigumu sana kupatawanyama. Si unaona leo nzima hatujapata mnyama. Zamani tungalikuwa tumepata hata Kobe.”Benki ya Dunia ikaja na mradi wa kupanda misitu mipya kwa kutumia miti ya migunga. Wakulima awali walikuwa na wasiwasi lakini sasa ndani ya misitu hiyo wamepanda na mihogo.Mayasa Mpime mkulima huyu akiwa kwenye msitu huo wa kupanda anasema uyoga ambao awali ilikuwa vigumu kupata sasa inachipuka tena. Na hata tunaweza kuwinda swala ndani ya msitu huu. Hivyo tunakula vizuri. Pia tunarina asali ambayo tunatumia na pia tunauza.”
Leo ni siku ya afya duniani ujumbe ukiwa ni Afya kwa Wote ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, wametumia siku hii kuwapima magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs, wakazi wa Beni-Mavivi jimboni Kivu. Taarifa zaidi na Afisa habari wa kikundi hich cha tatu cha kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZ-QRF-3 ndani ya MONUSCO, Luteni Abubakar Muna.Mganga Mkuu wa TANZQRF-3 Luteni Hussen Sinda amesema “tumeona tuadhimishe siku hii kwa kuwapima afya ndugu zetu wa Nzuma na kuwashauri kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari na saratani mbalimbali. Magonjwa haya hayaambukizi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine, lakini ni magonjwa tunayapata kulingana na namna tunavyoishi maisha yetu.” Tunawashukuru waliobuni siku hii Jusue Kapisa ambaye ni Chifu wa Kata ya Nzuma eneo la Beni-Mavivi anasema ushirikiano kati ya walinda amani wa UN kutoka Tanzania na eneo lao umekuwa ni mzuri tangu kuanza kuweko kwa walinda amani hao. Na zaidi ya yote, tunashukuru viongozi wa afya ulimwenguni kwa kuwazia na kupanga siku ya leo ya kuzungumzia siku ya afya. Sasa hawa viongozi wa afya duniani waone jinsi ya kuendelea kufanya utafiti ili magonjwa yaliyoko duniani na hayana tiba, yapate tiba na wakazi wa dunia waone mambo ya afya yanasonga mbele.” Upatikanaji wa dawa ni shida, waasi wanatukwamisha Alphonsine Muhindi, mkazi wa kata ya Nzuma ameshiriki pia huduma hii ya kupima afya na baada ya kupata huduma hiyo anafunguka kuhusu changamoto akisema, “tunapitia shida ya afya hapa Nzuma kwa sababu kwenye afya hatuna dawa kwa kuwa hatuna fedha. Ukisema ulime ili upate fedha, sasa ukiwa shambani unasikia waasi wamefika shambani. Hii inaleta dhiki kwa jamaa kwanza, njaa na magonjwa yanazidi kusambaa kwa kuwa hatuna dawa.” Ameshukuru kuweko kwa huduma hii kwa sababu angalau akishapima atajua hali ya afya yao inakuwa ni rahisi kwenda kupata dawa kwani tayari wanafahamu hali yao ya afya na pia kushughulikia watoto. Hoja ya wananchi yajibiwa na TANZ-QRF-3 Kwa Luteni Martha Mapunda, mtaalamu wa masuala ya saikolojia ndani ya TANZ -QRF -3 ombi lake ni kwa MONUSCO kuongeza idadi ya maafisa wa Jinsia zote wenye taaluma ya saikolojia ili waweze kuwasaidia wakazi wa Beni jimboni Kivu kaskazini. Hoja ya uhaba wa dawa unaokabili wakazi wa kata ya Nzuma ikajibiwa na Kapteni Damasi Khaza, Afisa Uhusiano wa TANZ-QRF -3 kwa niaba ya kamanda kikosi Luteni Kanali Adson Mwashifungwe ambapo amesema, utaratibu wa ugawaji dawa utafanyika kwa kuzipeleka kwenye vituo vya afya na hospitali ili zipatiwe wakazi hao. Taarifa hii imeandaliwa kwa pamoja na Luteni Abubakar Muna Afisa Habari TANZ-QRF -3 na George Musubao
Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumi. Mwandishi wetu wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wa kwanza kuzungumza mjini Beni ambako vikundi vya waasi vimekuwa vikishabulia raia, ni Vakekya Kaswera mama huyu wa watoto 7 akiwa shambani anasema furaha kwake yeye ni shamba lake analolima mihogo. Shambani anapata sombe au kwa kiswahili kisamvu na pia anapata unga wa muhogo. Hata hivyo anasema “furaha yangu inapotea pale mbuzi wanapokuja na kuharibu mazao yangu. Napenda kazi ya kilimo kwa sababu ndio kazi yangu tangu mdogo na inaniweza kutunza familia. Wazazi walitufundisha kulima na pia walitupeleka shuleni.” Mkazi mwingine Serge Kyamundu kwake yeye furaha ni pale enzi hizo ilikuwa inawezekana kupata starehe mjini Beni. “Kwangu ni furaha ni pale ninaona mji wangu uko katika starehe. Miaka iliyopita katika mji wetu wa Beni muziki ulipigwa ilikuwa furaha hakika. Lakini leo hii wakati usalama umemalizika katika mji wetu furaha kwangu imekwisha.” Ametoa wito kwa watu wengine wa nje na serikali za mbali zisaidie kurejesha usalama ili furaha irejee Beni kwani katika siku ya leo ya furaha“watoto wa Beni hatuna hakika furaha kwani tunakosa usalama katika mji wetu.” Naye Sylvie Mbakania, mkulima amesema “furaha yangu ni kutazama mazingira yakiwa mazuri. Ninapoona mbegu zimechipuka hunipatia furaha.” Hata hivyo hivi sasa furaha yake si kamilifu “kwa sababu ya vita katika nchi yetu. Natoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi zaidi kurejesha amani ili kukamilisha furaha yangu kama vile mahali pengine wanasherehekea siku hii.” Tarehe 12 mwezi Julai mwaka 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha tarehe 20 ya kila mwaka kuwa siku ya furaha duniani kwa kutambua mchango wake furaha na ustawi kama malengo ya kimataifa na matamanio ya kila binadamu.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Mashirika matatu makubwa ya kiraia yasimamisha shughuli zake baada ya Taliban kukataza wafanyakazi wanawake. Wakazi wa kambi za wakimbizi Goma walalamika kutaabika katika kipindi hiki cha sikukuu.
Ukame wa zaidi ya miongo minne na mafuriko vimekuwa ‘mwiba' kwa wananchi wa Somalia na hivyo kutishia uhakika wa kupata chakula halikadhalika mbinu za kujipatia kipato. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kwa msaada kutoka serikali ya Sweden imewezesha mradi wa kusaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia pembejeo na msaada wa fedha na sasa kuna nafuu hasa kwenye jimbo la Hirshabelle nchini humo. Mradi huo uko kwenye maeneo ya Johwar na Beledweyne na manufaa yameanza kuonekana huku wakulima wakilinganisha kabla na baada ya kupata usaidizi. Kwa kina basi kuhusu kilichofanyika ungana na Thelma Mwadzaya kwenye Makala hii iliyofanikishwa na FAO.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema iwapo halitapokea fedha za nyongeza, litalazimika kusitisha msaada muhimu wa kibinadamu kwa wakazi milioni moja wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ifikapo kilele cha msimu wa njaa mwezi Februari mwakani kutokana na ukata unaokabili. Leah Mushi na taarifa zaidi.Antonella D'Aprile ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Msumbiji amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo ya kwamba Cabo Delgado ni jimbo la Msumbiji lisilo na uhakika wa chakula na uhakika wa chakula unadorora kila uchao, huku takribani watu milioni 1.15 jimboni humo wakiwa kwenye janga au udharura wa njaa, huku takwimu mpya zaidi zikionesha hali inaweza kuwa mbaya zaidi.Ghasia zimeshamiri miezi ya karibuni, mashambulizi karibu na Pemba, mji mkuu wa Cabo Delgado pamoja na jimbo Jirani la Nampula, yamelazimu watu wengi zaidi kukimbia vijiji vyao, idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka mara nne na kufikia milioni moja katika miaka miwili iliyopita.Licha ya ghasia hizo, Bi. D'Aprile amesema WFP imeendelea kusambaza misaada ya dharura, vyakula vyenye lishe kwa wajawazito na watoto, pamoja na miradi ya kujengea mnepo jamii zilizo hatarini, wakiwemo watu 44,000 kupata ardhi yao huko Cabo DelgadoHalikadhalika WFP inaendesha shirika la huduma za ndege la Umoja wa Matiafa, UNHAS ambalo ndilo pekee linalosafirisha wahudumu wa kibinadamu kuelekea maeneo yasiyofikika kwa barabara.Mkuu huyo wa WFP nchini Msumbiji amesema katika maeneo ya ndani kabisa, UNHAS ndio huduma pekee ya anga kwa wahudumu wa misaada na kwamba “mwezi Desemba mwaka 2020, kufuatia kushamiri kwa mapigano na janga la COVID-19, WFP ilifungua njia ya anga ya kuunganisha maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji yasiyofikika. Huduma hii ya anga imesafirisha zaidi ya watumishi wa kibinadamu 10,000, na kilo 70,000 za misaada ya kibinadamu sambamba na huduma 330 za kiusalama.”Amesema kutokana na ukata huduma zote hizo zinaweza kusitishwa iwapo hawatopata dola milioni 51.Amesisitiza kuwa wakati wanatoa ombi la usaidizi huo, wataendelea kujitahidi kusambaza huduma kwa mak undi yaliyo hatarini zaidi kama wenye utapiamlo uliokithiri, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha watoto, lakini kuna baadhi ambao itabidi washindwe kuwahudumua labda kupatikane fedha za ziada.
Wakazi wengi ukanda wa Pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.
Wakazi wengi ukanda wa pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.
Wasiwasi mkubwa umeshuhudiwa katika Mji wa Rutshururu huko Kivu kaskaskazini mashariki mwa DRC kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo la karibu na kijiji cha Matebe .
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini. Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu. Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Wakazi wa Beni, Kivu kaskazini, na Ituri wameiomba serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kutangaza mauaji ya mara kwa mara katika eneo lao kuwa ya kimbari.
Wakazi waliokimbia vijiji vyao kutoka mji wa Irumu, wilaya ya Djugu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao wanaishi katika kambi za muda, wanaiomba serikali y kurejesha amani na usalama kwenye vijiji vyao kwa haraka, ili kupunguza changamoto zinazoendelea kuongezeka kila uchao.
Wakazi hao wanadai kwamba boti za kisasa na salama zinahitajika kwenye usafiri kwenye ziwa Tanganyika ili kuzuia ajali za boti za mara kwa mara.
Wakazi wa mji wa Pwani ya Kenya wanatarajia kuwa rais mteule William Ruto ataleta maendeleo katika mji wa Mombasa, ambao wanasema ulitengwa kwa muda mrefu na serikali zilizotangulia.
Wakazi wa mkoa wa Kivu Kusini wanajiuliza kipi kitafuata baada kikosi cha wanajeshi wa Burundi kuruhusiwa kuingia kwenye ardhi ya Congo mapema wiki hii, chini ya mpango wa Jumuia ya Afrika mashariki kupambana na makundi ya kigeni yenye silaha mashariki mwa DRC.
Kenya ni moja ya nchi zilizoathirika sana na ukame uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika Pembe ya Afrika, lakini sasa baadhi ya wakulima wa nchi hiyo kwa msaada wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD wameamua kuchukua hatua kulinda mazingira, maisha yao na kujenga mnepo kwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Katika kaunti ya Embu wakulima wamepanda msitu mpya ambao unawapa sio tu jukumu jipya la kuulinda lakini pia kuwa chanzo cha kuwapatia kipato.
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBATT-5 kwenye ujumbe wa umoja huo unaolinda amani nchini humo MINUSCA, kando mwa jukumu lao la ulinzi wa raia wamechukua jukumu la kusambaza huduma za maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo ambako wanalinda amani kama njia mojawapo ya kuimarisha ulinzi wa raia. Kwa kina basi kuhusu taarifa hii tuungane na Meja Asia Hussein, Afisa habari wa kikosi cha 5 cha Tanzania nchini CAR, TANBATT-5. Ulinzi wa amani kwa raia na mali zao huenda sambamba na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kwa raia wanaolindwa. Upatikanaji wa maji safi na salama ni moja ya changamoto kwa wananchi wengi wa mijini na vijijini. TANBATT – 5 kwa kulitambua hilo imeamua kuwapunguzia machungu wanakijiji huko Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï kwa kuwapelekea maji safi na salama katika eneo lao. Wakazi wa Kijiji hicho akiwemo Bi Ruth aliishukuru TANBATT 5 kwa huduma hiyo na kuwataka waendelee kuwakumbuka kila inapowezekana. Utoaji wa huduma ya maji ni moja ya utekelezaji wa majukumu yao kwa jamii wanayoihudumia na hufanya hivyo kila hali inaporuhusu.
Tumeishi hapa tangu miaka ya 1950 na katu hatujawahi kushuhudia mafuriko kama haya, amesema mkazi wa jimbo la White Nile nchini Sudan ambako mafuriko makubwa yamesababisha wakimbizi wa ndani kusaka hifadhi kwa wenyeji wao huku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wakiendelea kusambaza misaada ya kibinadamu. John Kibego na maelezo zaidi. Nats.. Kukurukakara za wakimbizi wa kambi ya Alganaa jimboni White Nile nchini Sudan za kupokea misaada kama vile mablanketi, vyakula na madumu ya kubebea maji. Wakimbizi hawa wanawake, wanaume na watoto wamejikuta hawana makazi baada ya mafuriko kuzingira makazi yao na kuathiri watu 80,000 wakiwemo wakimbizi 30,000. Sasa wanaishi kwa wenyeji ambao nao hawajui la kufanya kwa kuwa hawajashuhudia mafuriko kama haya yaliyotokana na mvua kubwa katika jimbo la Upper nile nchini Sudan Kusini. Yahia Ahmed, ni mmoja wa wenyeji ambaye anapatia hifadhi wakimbizi wa ndani. “Tumekuwa tunaishi eneo hili tangu miaka ya 1950 na tunachoona hivi sasa si hali ya kawaida. Mara chache tumekuwa tukipata mafuriko ya ghafla lakini si kama hivi. Hii ni mara ya kwanza hii inatokea.” Mafuriko haya yamekumba kambi ya wakimbizi ya Alganaa miezi michache tu tangu ianzishwe na sasa imetwama na kimbilio la wakimbizi ni katika kambi zingine sambamba na kwa wenyeji ambao nao hawana kinyongo. Sunday Rock, naye ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini lakini amekubali kuhifadhi wakimbizi wenzake akisema, “Tunajivunia kwamba wakimbizi wa ndani walipofika, tulikubaliana kuwasaidia kwa sababu sote ni ndugu na tumetoka nchi moja. Tunatumia pamoja chochote kile tulichonacho.” UNHCR inasema msaada zaidi unahitajika ili kuweza kusaidia wakimbizi hao waliofurushwa kutoka kambini kutokana na mafuriko.
Wakazi wa Jimbo la NSW hasa mji wa Syndey wameendelea kufungiwa ndani kwa kile kilichoelezewa na wananchi hao kuwa ni sheria ngumu ndefu kutokea nchini humu.SBS ilizungumza na mmoja wa wafanyabiashara Bw Hamisi Babu Kumbuka ambaye alidodosa kuhusiana na kufungiwa huko kunavyoathiri wafanyabiashara.Gonga hapa kusikiliza zaidi.
Kila siku wananchi watano katika kijiji cha Pazhaki jimboni Kabul nchini Afghanisan walikuwa wanajukumu la kufungulia maji katika mfereji uliokuwa unategemewa na wanakijiji hao kwa shughuli za kilimo. Lakini Ramazan Ibrahimkil, mwenyekiti wa Kijiji cha Pazhak anasema alikuwa anapokea kesi kila uchwao kwamba wananchi wanaokaa milimani wakilalamikiwa kufungulia maji kwa wingi na hivyo wale wa mabondeni kukosa maji ya kutosha kwenye kilimo chao na hivyo kupata mazao machache na kipato kidogo.
Wakazi wa jimbo la Magharibi Australia wameishi, kwa muda mrefu bila vizuizi vyovyote vya Coronavirus tofauti na wenzao kote nchini Australia.
Jasusi Apiga Stori Na WAKAZI: Ubunge 2020, Hali Ya Bongofleva, Kifo cha JPM, Urais wa Mama SAMIA, nk Get full access to Barua Ya Chahali at www.baruayachahali.com/subscribe
Jasusi Apiga Stori Na WAKAZI: Ubunge 2020, Hali Ya Bongofleva, Kifo cha JPM, Urais wa Mama SAMIA, nk
Wakazi katika jimbo la magharibi Australia wanahama nakupata makazi, wakati kimbunga chakitropiki Seroja kina karibia pwani ya kati ya magharibi jimboni humo.
Wakazi wa jimbo la Victoria wame anza kuishi chini ya masharti makali ya vizuizi kwa muda wa siku tano, wakati mamlaka wanafanya kazi kuzuia usambaaji wa aina ambukizi ya COVID-19 kutoka Uingereza.
Salama jamah mussikiliza noticiAudio. Karibuni habar za lelo kamba ezi: ▪Presidenti Felipe Nhusi lazima apeleleziwe kuhusu kupokelela rushuwa ya milhão modja za dólar ncaty ya deny saidjiwanikana- keleza Adriano Nuvunga. ▪Hali ya kupima Moçambiqui kuhusu hali ya uwongozi mwema yukolata kamba wankutumika uwongozi wa kimabavu na iwapo rushuwa nhingui. ▪Hali ya hewa yolota ikamba manhumba adjenguiwe para wanu walipo Chinde siyo amana. ▪Wakazi wa sirikali wakwamba aipo nafassi ya kuludila kutenda kazi Palma, ndandu ya hali ya kutowa kuwepo usalama wakutosha. Landikisse uzuji wa Podcast ema ukurassa wa Telegram na WhatsApp pamodja na ukurassa wa Facebook wa NoticiAudio ili uphathe habazi za mana za inty ya Moçambique, kwa Kila sumana. Leia o script em Português aqui Assante Sana, mphaka nafassi Nhenguine!
Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto, UNICEF na mpango wa chakula duniani , WFP yamefika eneo la kati la Msumbiji ili kutoa msaada kwa manusura wa kimbunga Eloise kilichopiga Msumbiji mwishoni mwa juma wakati bado wananchi hawasahau madhila ya vimbunga Kenneth na Idai. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu na kuongezeka kwa ghasia katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.
Wakazi wa eneo pana la Brisbane kupata afueni baada ya vizuizi kuregezwa, na wakazi wa maeneo ya milipuko ya COVID-19 jimboni NSW waombwa kuendelea kufanya tahadhari.
Wakazi katika jimbo la New South Wales kitongoji cha Murwillumbah wameamriwa kuhama baada ya Mto Tweed kupasuka kingo zake.
Nchini Tanzania, mradi wa lishe endelevu unaoendeshwa na shirika la watoto la Save the Children kwa ufadhili wa USAID umekabidhi vifaranga vya kuku pamoja na vyakula vyake kwa serikali ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ili visambazwe kwa wananchi.
Makala by Ruth Keah
Timu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumia Sudan Kusini wanatafuta njia za ubunifu za kutafuta pesa za kulipia ada ya watoto yatima na watoto katika familia zenye mzazi mmoja, kutoa chakula, vitabu na kuboresha vyumba vya madarasa vya shule ambayo inahudumia jamii maskni katika mji mkuu Juba.
Katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji, mafuriko yaliyokumba eneo hilo mwishoni mwa mwaka jana na mashambulizi kutoka kwa watu wenye silaha, vimesababisha hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi na Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha linaepusha majanga zaidi ikiwemo kusambaa kwa ugonjwa wa Corona au
Wakazi wa jimbo la Victoria waregezewa vizuizi kwa jiji la Melbourne na maeneo yakanda.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema mafuriko yanayoendelea katika majimbo 17 kati ya 18 ya nchini Sudan ni janga juu ya janga na kuichagiza jumuiya ya kimataifa kupeleka msaada wa haraka kunusuru maisha ya maelfu ya watu.
Wakazi wa Melburne wata amka kesho asubuhi jumatatu, nakupata baadhi ya vizuizi vya COVID-19 vimeregezwa kabla ya ratiba.
Umoja wa Mataifa ukitimiza miaka 75, wakazi wa sayari ya dunia kutoka nchi maskini hadi tajiri, wanawake hadi wanaume, vijana hadi watoto wametoa maoni yao kuhusu Umoja wa Mataifa wautakao, ikiwa ni matokeo ya utafiti uliofanyika kuanzia mwezi Januari mwaka huu kufuatia wito wa Katibu Mkuu Antonio Guterres.
Zahanati 15 zinazo toa huduma maalum ya afya ya akili, zimefunguliwa kwa umma jimboni Victoria kuanzia Jumatatu 14 Septemba, kama sehemu ya mfuko waku wasaidia wakazi wa Victoria wakati huu wa janga.
Umra Omar ambaye ni miongoni mwa mashujaa watano wa kiutu kwa mwaka huu wa 2020 ameelezea jinsi janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 limesaidia kusongesha kazi yao ya kupatia tiba wakazi wa kaunti ya Lamu nchini Kenya kupitia shirika la kiraia la Safari Doctors ambalo yeye ni muasisi na pia mkurugenzi. Kutoka Kenya, Jason Nyakundi ana maelezo zaidi.
Mkoa wa Morogogoro ulioko katika eneo la mashariki la Tanzania ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka mingi yametambulika kuwa maeneo yenye hali nzuri ya hewa kutokana na mazingira yake kuwa yenye misitu, nyika, na milima yenye kutiririsha maji safi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanaharakati wa kutunza mazingira wanaona kuwa ni muhimu kuchukua hatua za kuilinda hali hiyo kwani iko katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli za binadamu kama vile uchomaji mkaa.
Ongezeko ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 ime ilazimisha serikali ya jimbo la Victoria kuchukua hatua kali kulinda jamii.
Mamlaka wamechukua hatua kali zakuzuia usambaaji wa virusi vya COVID-19 katika jamii kote nchini Australia.
Afisa mkuu wa afya wa Victoria anawahamasisha watu wavae barakoa wakiwa nje, wakati jimbo hilo limerekodi visa vipya 288 vya COVID-19.
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo: - Nchini Kenya Wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 kutibiwa nyumbani - Wakazi wa Mathare nchini Kenya washukuru UNICEF kwa kuwawekea tenki za maji - UNICEF yachukua hatua kukabiliana na ukatili wa kingono Sierra Leone
Maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, yakiendelea kuripotiwa nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo limeanzisha zaidi ya vituo 1000 vya kunawa mikono katika eneo la makazi duni la Mathare kwenye mji mkuu Nairobi, kama njia mojawapo ya kukabiliana na maambukizi mapya.
Serikali ya Kenya imeombwa kuwa wakati huu wa janga la COVID-19 isiwafurushe wakazi wa maeneo yasiyo rasmi ya Kariobangi na Ruai na ilinde usalama wa watetezi wa haki za binadamu ambao wanatishiwa usalama wao kutokana na kutetea haki za wakazi hao. Assumpta Massoi na taarifa zaidi Wataalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za makazi na haki za watetezi wa haki za binadamu wamesema hayo leo kupitia taarifa yao iliyotolewa mjini Geneva, Uswisi na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Salama djamah piya, karibuni kussikiliza NoticiAudio, habar za Maana mu inty ya Moçambiqui zilaviwa kwa kwavyana na Habar za Kissiassa zitangaziwa na Centro ya Integridade Pública-CIP. Nafassi ya lelo, tukwanza kuhussu muadja vya zili kuka kazi za kulebelana votu, ncaty ya mpango wa kitondola tcha muezi wa 10 Namuaka. Kwa nassafi ya pili Habari ulu ndizi: ▪️Empresa itiwa VALE na ufalume wa inty ya Moçambiqui wankufissa kubadilika ka Hali ya heewa mu Distrito ya Moatize. ▪️Wakazi wa Empresa EMATUM weleza na kudanizila kuthenda mandamano. ▪️Biashara za zeleweka ncaty ya wizara ishugulikila kazi za Mapulicia Wakaty wa uphatikane Nzuluco muingui mu inty ya Moçambiqui. Landikisse uzuji wa Podcast ema ukurassa wa Telegram na WhatsApp pamodja na ukurassa wa Facebook wa NoticiAudio ili uphathe habazi za mana za inty ya Moçambique, kwa Kila sumana. Assante Sana, mphaka nafassi Nhenguine
New South Wales residents will go to the polls on Saturday to decide who will lead their state for the next four years. - Wakazi wa NSW wata ingia katika vituo vyakupiga kura jumamosi 23machi2019, kuamua atakaye ongoza jimbo hilo kwa muda wa miaka minne ijayo.
As residents of flood affected parts of Townsville estimate the potential costs to their properties and businesses, SBS Swahili spoke with members of the Swahili speaking community who live in neighboring suburbs to the flood affected areas. - Wakazi wa maeneo ambayo yame athiriwa kwa mafuriko mjini Townsville wanapo endelea kuhesabu gharama ya uharibifu kwa nyumba na biashara zao, SBS Swahili ilizungumza na wanachama wa jamii wanao zungumza Kiswahili, ambao wana ishi katika vitongoji jirani vya maeneo ambayo yame athiriwa kwa mafuriko hayo.
Wakazi is a bilingual Tanzanian hip hop artist. He grew up in Dar es Salaam, but spent several years in the United States, where he was active in the Chicago hip hop scene. Like many MCs who spend several years abroad, when he returned to Tanzania he had to prove himself on the local scene. He was able to craft his brand, largely by harnessing the power of social media. In this interview, Wakazi talks about his experiences in Chicago, with the local hip hop scene and how his experiences there have impacted his career. He discusses his return to Tanzania, the reception he faced on his return, and how has managed to build his career. Wakazi, who is fluent in English and Swahili, also talks about multilingualism, and the use of other Tanzanian languages in hip hop. Wakazi also reflects on some of the struggles within the hip hop community, some of which he feels is largely due to a lack of mentorship by the first generation of Tanzanian hip hop artists. He also discusses perceptions & understandings of African American culture in Tanzania. Wakazi’s music can be purchased on iTunes at https://itunes.apple.com/us/artist/wakazi/928220403 Nomadic Wax Super MC: https://nomadicwax.bandcamp.com/track/super-mc-v2 Wakazi is online at Twitter @Wakazi: https://twitter.com/Wakazi Facebook @wakazimusic: https://www.facebook.com/wakazimusic/ Instagram @wakazimusic: https://www.instagram.com/wakazimusic/ Youtube @wakazimusic: https://www.youtube.com/user/WakaziMusic Continue reading
Victorians go to the polls on 24 November 2018 - Wakazi wa Victoria, watafanya uchaguzi tarehe 24 mwezi wa kumi na moja mwaka huu wa 2018.
Makala ya Siha njema inaangazia ugonjwa wa kipindupindu uliopiga nchini DRC hivi karibuni na kuathiri idadi kubwa ya wakazi.Waziri wa afya jimboni kivu kaskazini na daktari mtafiti wanaangazia namna jami hiyo inavyokabiliana na maradhi hayo.
Paula na Philipp wanakwenda kuchunguza wakati maumbo ya duara yanapogunduliwa kwenye shamba la mahindi. Je kuna dude lililoanguka kutoka angani au kuna mtu anawacheza watu shere? Wakati Ayhna anapowasili katika afisi ya Radio D, nao Paula na Philipp wamo njiani kutoka afisini. Maumbo ya duara yamegunduliwa katika shamba la mahindi na hakuna anayeweza kueleza jinsi yalivyojitokeza. Si waandishi habari hao wawili pekee walio na hamu ya kushuhudia jambo hilo; watalii wengi wanakuja kushuhudia pia. Wakazi wa kijiji hicho wanapata namna ya kujifaidi kutokana na tukio hilo la ajabu. Katika zogo hilo, watu wenye nia tofauti wanajumuika. Watalii wana hamu ya kujionea wenyewe, waandishi habari wanataka kuagua kitendawili hicho na wakulima wanataka kufaidika kifedha. Zingatia vitenzi vya utaratibu katika tukio hili.