POPULARITY
Kesho kutwa Ijumaa huko nchini India, Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itakutana nchini India kutathmini vitisho vipya duniani vitokanavyo na teknolojia mpya. Mkutano huo wa siku mbili ni wa kwanza kufanyika nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tangu mwaka 2015. Happiness Pallangyo wa Redio washirika Uhai FM kutoka Tabora Tanzania anafafanua zaidi.Mjadala utajikita kwenye maeneo matatu makuu ambayo ni mosi; Intaneti na mitandao ya kijamii; Pili, Ufadhili wa mitandao ya kigaidi duniani na tatu; kuenea kwa matumizi ya mifumo ya angani isiyo na rubani kama vile droni.Umoja wa Mataifa unasema teknolojia hizo mpya zinakua kwa kasi kubwa na zinatumika mara kwa mara katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo kwenye usalama wa taifa na kukabili ugaidi.Hata hivyo teknolojia hizo zinatumiwa vibaya na vikundi vya kigaidi kwa manufaa yao binafsi yasio na nia njema.Mkutano pia utakuwa ni jukwaa la kubadilishana mawazo ya jinsi teknolojia inaweza kusaidia kukabili kusambaa kwa maudhui ya kigaidi mtandaoni na kukabili pia simulizi za kigaidi.Hofu nyingine iliyoko na itakayomulikwa ni matumizi kwa nia mbaya ya uchapishaji wa chapa tatu au 3D, maroboti, akili bandia na mifumo ya angani isiyo na usimamizi.Kwa sasa India ndio inashikilia kiti cha Uenyekiti wa Kamati hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Mwakilishi wa Kudumu wa India Kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ruchira Kamboj ambaye ndiye Mwenyekiti amesema,(Sauti ya Ruchira Kamboj)“Ugaidi katika aina zote zile, katika muonekano wowote ule ni moja ya vitisho vikubwa zaidi vya amani na usalama duniani. Kitendo chochote cha kigaidi hakiwezi kuhalalishwa kwa misingi ya nia yoyote ile, wakati uliofanyika, pahali ilipofanyika na ni nani aliyetekeleza. Kamati imejizatiti kupambana na janga hili katika ngazi ya kimataifa.”Kutokana na ugumu wa suala zima, na kasi ya mapinduzi yake, matarajio ni kwamba wajumbe watakuwa na nyaraka ya mwisho ambayo itatoa mwelekeo wa jinsi magaidi wanatumia teknolojia, kwa lengo la kufunga simulizi zao na matumizi ya teknolojia.Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la UN iliundwa kwa kauli moja tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2001, kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani tarehe 11 Septemba 2001 na wanachama ni wajumbe wote 15 wa Baraza la Usalama.
Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Nepal Sangya Malla anayehudumu katika ujumbe wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC, MONUSCO ameshinda tuzo ya Afisa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2021. Leah Mushi ana taarifa zaidi. Ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres “ kwa heshima kubwa napenda kutunuku tuzo ya 11 ya Afisa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa Mrakibu wa Polisi Sangya Malla wa Nepal. Malla umeifanya nchi yako, pamoja na MONUSCO na familia nzima ya Umoja wa Mataifa kujivunia.” Katibu Mkuu amesema hayo kupitia ujumbe wake kwa njia ya video kwa mkutano wa kuadhimisha kuanza kwa wiki ya Polisi wa Umoja wa Mataifa, mkutano unaofanyika kwa njia ya mtandao. Mrakibu Malla mbali ya kuwa polisi pia ana taaluma ya utabibu ambapo kwa kutumia taaluma hizo yeye na timu anaoiongoza wameweza kuhakikisha wanasimamia na kuhamasisha masuala ya afya na mazingira huku wakiendelea na shughuli za kulinda amani nchini DRC. Miongoni mwa yale aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kuandaa semina zaidi ya 300 kwa mwaka huu pekee kuelimisha wananchi wa DRC kuhusu ugonjwa wa Corona au COVID-19 na majanga mengine ikiwemo Ebola. Halikadhalika wakati wa mlipuko wa volkano ya mlima Nyiragongo huko Goma mwezi Mei mwaka huu 2021, Mrakibu wa Polisi Malla na kitengo chake ndio haswa walitahadharisha wakazi wa eneo hilo na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatua za tahadhari na watu wakafanikiwa kuondoka kwenye enoe hatari na kuelekea maeneo salama ikiwemo nchi jirani ili kuokoa maisha yao. “Alisaidia kuanzisha na sasa anaongoza Kitengo cha Afya na Mazingia cha MONUSCO, akiimarisha usalama na ustawi wa walinda amani wetu kwa kupunguza hatari za COVID-19 na vitisho vingine. Anawakilisha kitu kikubwa zaidi, michango mingi ya maafisa wa polisi wanawake katika kuendeleza amani na usalama duniani kote. Kupitia kazi yake, Mrakibu wa polisi Malla anaonesha kazi bora inayofanywa na Umoja wa Mataifa” Akipokea tuzo hiyo Mrakibu Malla ameshukuru na kusema "Nimefurahi kupokea tuzo hii, na ninatumai itawapa moyo wanawake vijana zaidi katika nchi yangu na kote ulimwenguni kufuata taaluma ya polisi, ambayo bado inatazamwa kama kazi ya wanaume". Naye Mshauri wa Polisi wa Umoja wa Mataifa Luis Carrilho amesema “kama walinda amani wengi wakati huu wa changamoto za usalama huku kukiwa na janga hili la Corona, Mrakibu Malla amevuka wito wa kuhudumia jamii, pamoja na timu yake, juhudi zake za kuongeza ufahamu kuhusu afya ya umma na hatari za asili hatimaye zimewafanya wafanyakazi wenzake na watu wa DRC kuwa salama zaidi ambayo ni kazi kuu ya polisi." Kitendo cha polisi wa Umoja wa Mataifa kimefikia lengo la usawa kijinsia katika ngazi zote za wafanyakazi.
Baada ya Jumanne, Taliban kutangaza kuunda serikali isiyo na wanawake, Naibu Mwakilishi wa shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa, UN Women nchini Afghanistan amesema "kukosekana kwa uwazi wa msimamo wa Taliban kuhusu haki za wanawake kumezua hofu ya ajabu" ambayo ni "inayoonekana kote nchini Afghanistan. (Taarifa ya John Kibego) Alison Davidian akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani kwa njia ya video akiwa mjini Kabul, Afghanistan siku moja baada ya Taliban kutangaza kuunda serikali bila ushiriki wa wanawake amesema UN Women wamekatishwa tamaa na uamuzi wa Taliban na kwamba "kuheshimu haki za wanawake ni kipimo kwa mamlaka yoyote ya serikali, na ambayo mamlaka yoyote ya uongozi inapaswa kuhukumiwa kwayo. Kwa tangazo Taliban imekosa nafasi muhimu kuonesha ulimwengu kwamba kweli wana nia ya kujenga jamii inayojumuisha na yenye mafanikio. " Aidha Bi Davidian ameongeza kusema, “Ukosefu wa uwazi wa msimamo wa Taliban kuhusu haki za wanawake umesababisha hofu ya ajabu. Hofu hii inaonekana kote nchini. Kumbukumbu ni wazi juu ya jukumu la Taliban katika miaka ya 1990 ambapo kulikuwa na kizuizi kikali juu ya haki za wanawake na wanawake na wasichana wanaogopa. Na hofu hizi zinatokana na ukweli kwamba Taliban bado haijaelezea kikamilifu msimamo wake wa haki za wanawake. " Akieleza hali halisi wanayokumbana nayo wanawake wa Afghanistan, Bi Davidian anasema, “Kila siku tunapokea ripoti za kurejea nyuma kwa haki za wanawake. Wanawake wamekatazwa kutoka nyumbani bila mahram yaani msimamizi wa kiume. Katika maeneo mengine wameacha kwenda kazini. Vituo vya ulinzi wa wanawake ambavyo vinatoa huduma muhimu kwa wanawake wanaokimbia unyanyasaji vimeshambuliwa na nyumba salama kwa watetezi wa haki za binadamu wanawake wakiwemo waandishi wa habari na wanaharakati zimejaa.” Kwa mujibu wa Naibu Mwakilishi huyo wa UN Women nchini Afghanistan, UN Women wamesema watasalia Afghanistan na kufanya kazi kusaidia wanawake wa nchi hiyo.
Katika mahojiano kati ya Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa na Aneth Gerana Isaya, msichana kiziwi ambaye ushauri wake alioutoa alipojiunga katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umeendelea kuwasaidia viziwi wote wanaojiunga kwa masomo katika Chuo hicho kikongwev cha elimu ya juu nchini Tanzania. Aneth pia ni Mwanzilishi wa shirika la Furaha kwa Wanawake Viziwi Tanzania FUWAVITA. Aneth Isaya anaanza kwa kueleza hatua ambazo wameshapiga katika harakati za kupigania usawa wa kijinsia hususani kwa wanawake wenye ulemavu.
Mpira wa jana uliishangaza dunia baada ya barca kufungwa goli 8 ndani ya dakika 90, wakati wao wakifunga goli 2 tu. Kitendo hicho kimetafsiriwa kama ni udhalilisha mkubwa sana kwa timu kubwa ya barca. Walichofanyiwa katika mchezo wa jana hakikuwa kitu kizuri katika historia ya mpira duniani. --- Send in a voice message: https://anchor.fm/ayubu-chewale/message
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Herr Meier ametoweka – zumari lake tu limebakia chumbani hotelini... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu mögen
Deutsch – warum nicht? Fungu 1| Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Wasi wasi hotelini – Herr Meier ametoweka... Muhtasari wa sarufi: Kitendo haben
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mvutano kuhusu mchezo upi wa kuingiza unafaa... Muhtasari wa sarufi: Kielezi cha pahali wo. Kitendo cha utaratibu sollen
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mama yake Andreas anataka kujua mengi... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu wollen
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Kwenye mapokezi ya hoteli: Mgeni mmoja ana haraka... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu dürfen
Deutsch – warum nicht? Fungu 2 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Mabwana wageni na mabibi wa makamo – Andreas akiwa kazini kwenye mapokezi ya hoteli... Muhtasari wa sarufi: Kitendo cha utaratibu können
Deutsch – warum nicht? Fungu 4 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle
Msichana anahadithia juu ya maisha katika Ujerumani ya Mashariki... Muhtasari wa sarufi: Kitendo chenye hali ya sharti (würde + kitenzi jina)