Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo. Flora Nducha na taarifa zaidi

Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha. Tuungane na Leah Mushi kupata tarifa zaidi.

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe katika siku ya Choo Duniani, simulizi za wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan, na usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR).Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo.Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha.Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UPUNGUFU"

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Brazil kwenye mkutano wa COP30, ambako Dkt. Richard Muyungi, Mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania anaeleza ni nini bara la Afrika linahitaji.Umoja wa Mataifa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio namba 2803 la Baraza la Usalama kuhusu Gaza hapo jana, ukilitaja kuwa hatua muhimu katika kuimarisha usitishaji mapigano. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anazitaka pande zote kuheshimu kikamilifu makubaliano hayo na kutafsiri kasi ya kidiplomasia kuwa hatua za dharura na za wazi kwa watu walioko katika eneo hilo. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Guterres, Stéphane Dujarric, amesema Umoja wa Mataifa umejizatiti kuongeza misaada ya kibinadamu na kuunga mkono jitihada zinazoelekezwa katika hatua inayofuata ya usitishaji mapigano.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali ya kibinadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini bado ni tete. Mkurugenzi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Kanda ya Afrika Patrick Youssef ambaye amerejea hivi karibuni kutoka DRC amewaleza waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi kwamba raia wa DRC wanaendelea kubeba mzigo mzito wa mapigano, hata wakati shughuli chache za kibiashara zikiendelea kurejea Goma. Ametoa tahadhari kuwa mgogoro huo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili, ukatili wa kingono unaongezeka, na zaidi ya asilimia 70 ya watu waliojeruhiwa kwa silaha mwaka huu ni raia.Kuanzia leo tarehe 18 inaanza Wiki ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usugu wa Vijiumbemaradhi dhidi ya dawa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa usugu wa vimelea yaani hali ambapo bakteria, virusi na vijidudu vingine havidhuriki tena kwa dawa tayari unatishia mifumo ya afya, uchumi na uhakika wa chakula. Kwa kaulimbiu “Chukua Hatua Sasa: Linda Leo Yetu, Linda Mustakabali Wetu,” WHO inatoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya, wakulima, wadau wa mazingira na umma kuchukua hatua madhubuti kutekeleza ahadi za kisiasa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi sugu ya dawa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UPUNGUFU"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Dunia inajiandaa kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa Novemba hadi tarehe 10 Disemba, kampeni inayolenga kuongeza uelewa na kutoa wito wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote. Na katika kuelekea maadhimisho hayo, Sabrina Saidi ameandaa taarifa kutokea huko nchini Ethiopia, akiangazia simulizi ya mwanamke ambaye ameamua kuvunja mzunguko wa mila zenye madhara kwa jamii yake.

Hii leo jaridani tunaangazia kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ukatili wa kijinsia na zoezi la mahakama tembezi nchini Sudan Kusini.Mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari (IRMCT) umeamua kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari, Félicien Kabuga, hana uwezo wa kiafya kusafiri kwenda Rwanda, uamuzi unaositisha mpango wa awali wa kumhamisha kwenda nchini Rwanda ili kuachiwa kwa muda kutokana na hali yake ya kiafya kuwa tete.Dunia inajiandaa kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa Novemba hadi tarehe 10 Disemba, kampeni inayolenga kuongeza uelewa na kutoa wito wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote. Na katika kuelekea maadhimisho hayo, Sabrina Saidi ameandaa taarifa kutokea huko nchini Ethiopia, akiangazia simulizi ya mwanamke ambaye ameamua kuvunja mzunguko wa mila zenye madhara kwa jamii yake.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudani Kusini UNMISS wakishirikiana na wizara ya haki na masuala ya katiba nchini humo wanaendeleza zoezi la mahakama tembezi nchini humo, mradi ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Norway ili kuhakikisha wananchi hususan wale walio na kesi mahakama wanapata haki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudani Kusini UNMISS wakishirikiana na wizara ya haki na masuala ya katiba nchini humo wanaendeleza zoezi la mahakama tembezi nchini humo, mradi ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Norway ili kuhakikisha wananchi hususan wale walio na kesi mahakama wanapata haki. Tuungane na Sheilah Jepngetich kwa taarifa zaidi.

Mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari (IRMCT) umeamua kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari, Félicien Kabuga, hana uwezo wa kiafya kusafiri kwenda Rwanda, uamuzi unaositisha mpango wa awali wa kumhamisha kwenda nchini Rwanda ili kuachiwa kwa muda kutokana na hali yake ya kiafya kuwa tete. Flora Nducha ameifuatilia taarifa hiyo kwa kina.

Tarehe 14 Novemba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kisukari na mwaka huu kauli mbiu ni “Kisukari katika hatua mbalimbali za maisha.” Je wafahamu ugonjwa huu unampata mtu gani na unawezaje kujikinga usiugue? Leah Mushi anatujuza zaidi.

Wiki ya kwanza ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP30, unaofanyika Belém Brazil, ikielekea ukingoni, viongozi wa dunia na wanaharakati wanakutana kujadili jinsi ya kushughulikia moja ya changamoto kubwa za wakati huu, ‘janga la mabadiliko ya tabianchi,” Na athari zake kwa wakimbizi hazikupewa kisogo. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii

Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa kisukari, chanjo ya polio katika ukanda wa Gaza na janga la mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa wakimbizi.Tarehe 14 Novemba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kisukari na mwaka huu kauli mbiu ni “Kisukari katika hatua mbalimbali za maisha.” Je wafahamu ugonjwa huu unampata mtu gani na unawezaje kujikinga usiugue? Leah Mushi anatujuza zaidi.Mashirika ya Umoja wa Mataifa WHO, UNICEF na UNRWA wameanzisha kampeni ya pamoja ya Uchanjaji watoto waliokosa huduma muhimu za kuokoa maisha kutokana na miaka miwili ya machafuko katika Ukanda wa Gaza umeanza kutekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la afya duniani, la kuhudumia watoto UNICEF na la kusaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.Wiki ya kwanza ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP30, unaofanyika Belém Brazil, ikielekea ukingoni, viongozi wa dunia na wanaharakati wanakutana kujadili jinsi ya kushughulikia moja ya changamoto kubwa za wakati huu, ‘janga la mabadiliko ya tabianchi,” Na athari zake kwa wakimbizi hazikupewa kisogo. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii.Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!

Mashirika ya Umoja wa Mataifa WHO, UNICEF na UNRWA wameanzisha kampeni ya pamoja ya Uchanjaji watoto waliokosa huduma muhimu za kuokoa maisha kutokana na miaka miwili ya machafuko katika Ukanda wa Gaza umeanza kutekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la afya duniani, la kuhudumia watoto UNICEF na la kusaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU".

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki mjini El Fasher, pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika maeneo ya Kordofan nchini Sudan. Guterres amesema “Mtiririko wa silaha na wapiganaji kutoka nje lazima ukatwe. Misaada ya kibinadamu lazima iweze kuwafikia haraka raia wanaohitaji, na mapigano lazima yakome,”.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano limemchagua Phoebe Okowa kutoka Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), baada ya duruu nne za upigaji kura. Upigaji kura huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini kwa utaratibu tofauti, kama inavyotakiwa na Katiba ya Mahakama hiyo ya Haki. Bi. Okowa amechaguliwa kwa wingi wa kura ambapo alipata kura 8 katika Baraza la Usalama na kura 106 katika Baraza Kuu.Kumekuwa na ongezeko la uraibu wa nikotini na bidhaa nyingine zinazozalishwa kwa kutumia tumbaku duniani hususani miongoni mwa vijana na tena wengi hivi sasa wanatumia sigara za kielektroniki, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO. Tarehe 17 mpaka 21 Novemba utafanyika mkutano mkubwa kujadili namna serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitakavyoweza kusaidia kupambana na janga la tumbaku duniani, linalosababisha vifo zaidi ya milioni saba kila mwaka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU"Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!

Ripoti mpya ya pamoja kutoka mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonya kwamba uhaba mkubwa wa chakula unazidi kuongezeka katika maeneo 16 yenye njaa duniani, hali inayoweza kusababisha mamilioni zaidi ya watu kukumbwa na njaa kali au hatari ya kufikia kiwango cha baa la njaa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Kituo cha utafiti wa kusaka Suluhu kuhusu mafuriko kinachoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Uganda kimetumia maarifa ya pamoja kukabiliana na changamoto za mafuriko katika eneo la Makerere Kavule, makazi yasiyo rasmi yaliyo pembezoni mwa mji wa Kampala, mji mkuu wa Uganda. Kituo hicho kimeunganisha juhudi za jamii, maarifa asilia, na teknolojia ya kisasa kubuni mfumo wa mifereji ya maji unaoendana na Mpango Mkuu wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan). Mfumo huu unalenga kupunguza mafuriko si tu katika jamii hiyo, bali pia katika eneo la katikati ya jiji. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya FAO ya uhaba wa chakula, Mwanaharakati kijana kutoka Kenya katika mkutano wa pili wa WSSD Doha, na mradi wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan) inayosaidia kupunguza mafuriko Uganda.Ripoti mpya ya pamoja kutoka mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonya kwamba uhaba mkubwa wa chakula unazidi kuongezeka katika maeneo 16 yenye njaa duniani, hali inayoweza kusababisha mamilioni zaidi ya watu kukumbwa na njaa kali au hatari ya kufikia kiwango cha baa la njaa.Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka.Kituo cha utafiti wa kusaka Suluhu kuhusu mafuriko kinachoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Uganda kimetumia maarifa ya pamoja kukabiliana na changamoto za mafuriko katika eneo la Makerere Kavule, makazi yasiyo rasmi yaliyo pembezoni mwa mji wa Kampala, mji mkuu wa Uganda. Kituo hicho kimeunganisha juhudi za jamii, maarifa asilia, na teknolojia ya kisasa kubuni mfumo wa mifereji ya maji unaoendana na Mpango Mkuu wa Mifereji ya Maji wa Jiji la Kampala (Kampala Capital City Drainage Master Plan). Mfumo huu unalenga kupunguza mafuriko si tu katika jamii hiyo, bali pia katika eneo la katikati ya jiji.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka. Flora Nducha na taarifa zaidi

Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Daktari. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "CHA KIPOFU KI MKONONI MWAKE"





Na sasa ni wakati wa kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "JAMALA na BULBUL"

Jarida hii leo tunamulika harakati za kuzuia mauaji ya kimbari El Fasher, Sudan, hakuna dalili za kumalizika kwa janga la njaa mashariki mwa DRC na furaha kwa watoto waliopatiwa mabegi ya kwenda shule huko Tigray, Ethiopia.Unapokabiliana na ukatili na mauaji ya kimbari ni vema kuhakikisha wanaotekeleza wanafahamu kuwa wanafuatiliwa na kutazamwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao, amesema Chaloka Beyani Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari.Mgogoro katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unaendelea kuwa mbaya huku mapigano yakizidi, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuzidisha njaa kali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeeleza leo.Nchini Ethiopia, Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Tigray watoto wamefurahia kupatiwa vifaa kwa ajili ya kurejea upya shuleni baada ya vita ya muda mrefu, shukrani kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.


Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock ametembelea wakimbizi wa kipalestina huko Doha nchini Qatar kuwajulia hali na kujionea maisha yao baada ya kuondolewa wakati wa vita kali huko Ukanda wa Gaza eneo la wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel na kuletwa nchini Qatar kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Leah Mushi anatupa taswira ya ziara yake hiyo.Wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar nchi hiyo ilitenga eneo maalum na kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya makazi kwa wale walioenda kutazama mechi za kombe la Dunia, eneo hilo pia lilikuwa na kiwanja cha mpira, eneo hilo ni Al-Thumama maarufu kama Al-Thumama complex katika mji wa Doha.Mtoto na simulizi kupitia pichaEneo hilo sasa limegeuzwa makazi ya dharura kwa zaidi ya wakimbizi 1,700 wa Kipalestina ambao waliondolewa nchini mwao wakati wa vita Kali kati ya majeshi ya Israel na wanamgambo wa Hamas vita ambayo imesitishwa hivi sasa. Wakimbizi hao wa kipalestina wakiwa katika eneo la Al-Thumama wanapatiwa matibabu ya kawaida, ya viungo na usaidizi wa kijamii.Rais wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amefika katika eneo hilo ili kuwajulia hali.Kwanza alikutana na watoto, video inamuonesha akizungumza na mtoto wa kiume ambaye ameandika kitabu kwa njia ya picha na ndoto yake ni kitafsiriwe kutoka kiarabu kwenda lugha mbalimbali. toto huyo akatia saini nakala ya kitabu chake na kumpa Rais wa Baraza Kuu.Watoto licha ya majeraha bado wana matumainiKisha, Rais Baerbock anaonekana akizungumza na familia nyingine, pembeni mtoto mmoja mwenye umri kama wa miaka mwili hivi mkono wake wa kulia unaonekana umekatwa chini kidogo ya bega. Mtoto huyo anarukaruka kwenye kochi huku wanafamilia yake wakizungumza na mgeni.Anatoka akitembea kwenda eneo jingine lakini ndani ya eneo hilo hilo la Al-Thumama kwenye chuo cha ufundi stadi na kujionea namna wanawake wanavyojishughulisha na kazi za mikono ikiwemo ufumaji kwa kutumia mashine za kisasa za mkono.Akitoka huko akiwa na wanawake kadhaa akawa anaelekea eneo lenye hospitali … njiani akakutana na mwanamke akiwa kwenye kiti mwendo, wakasimama na mwanamke huyo akawapa vitafunywa wakala na kufurahia huku Rais wa Baraza Kuu akisifu kwa utamu wa vitafunio hivyo.Baada ya hapo safari ya kwenda hospitali ikaendelea, na huko akakutana na madaktari na kujionea mashine mbalimbali za kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina.Ziara hiyo aliyoianza tangu mchana kweupe alihitimisha giza likiwa limeshatanda nje na akatoa ujumbe kwa dunia kile alichojionea.Amesema, “nimeona yale hawa watoto walipitia, nyuso zao ziliungua kwa moto, wamepoteza mikono, wazazi, familia nzima, lakini bado wanaonesha ujasiri na wanamatumaini na maisha yao ya baadae, wakijaribu kurejea shuleni na hii inaweka mkazo wa jukumu letu ni lipi kama jumuiya ya kimataifa. Tunapaswa kukomesha kabisa mgogoro huu uliodumu kwa muongo mmoja, mzozo wa muda mrefu na kwamba amani ya kudumu haita hakikishwa kwa kupitia vita, ugaidi wala kukalia eneo kimabavu bali kwa makubaliano ya amani ya kuwa na mataifa mawili yanayojitegemea, kupelekea kwa taifa huru la Kipalestina ambapo kizazi kijacho kinaweza kuishi kwa heshima pia.”

Nchini Kenya, shirika la kiraia la FODDAJ au la Forum for Women Development, Democracy and Justice linatekeleza kivitendo lengo namba 3 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la afya bora na ustawi ambalo pamoja na mambo mengine linataka manusura wa ukatili wa kijinsia wapatiwe huduma sio tu za afya bali pia za kijamii. Je linafanya nini, Sheilah Jepngetich amezungumza na mwakilishi wa shirika hilo.Ni Salome Gatakaa Araka, Mwakilishi wa FODDAJ ambaye katika mazungumzo nami anaanza kwa kuelezea walianzia wapi harakati zao. Akisema Policy and Advocacy anamaanisha Sera na Uchechemuzi.“FODAJ ilianza na uundaji wa ufahamu yaani policy and advocacy kumaanisha kwamba kuwe kutengwa kwa fedha za kutengeneza mahali pa waathiriwa kuishi, na pia kusisitiza ufahamu wa kutetea wale ambao wametengwa. Katika kata ya Kajiado, tumesukuma sera za GBV ili kuimarisha juhudi za kuzuia waathiriwa kuumia zaidi.”Pamoja na kukabili ukatili wa kijinsia, nikataka kufahamu iwapo wanawejengea wanawake uwezo wa kujitegemea.“FODDAJ imekuwa mstari wa mbele katika katika kupaza sauti za wanawake na wasichana, na pia kuhimiza akina mama kuweka akiba za vikundi, kushirikiana na kusaidiana ili kujikimu kiuchumi. Tumehimiza akina mama kuweka akiba kwa vikundi vya maendeleo, kushirirki mafunzo ya ujasiriamali na kushirikiana na wengine kwa pamoja. Na pia wanafundishwa mambo tofauti kama vile kutengeneza nywele , kusoma na kuandika na pia na kuhesabu.”Maneno ya Bi. Araka si matupu kwani Geraldine Ndayisenga mkazi wa Kitengela ambaye ni manusura wa ukatili na mnufaika wa miradi ya FODDAJ anafunguka.“Mimi ni mmoja wa wale waliopitia dhuluma. Nilijua kuhusu FODDAJ kupitia rafiki yangu. Nikasaidiwa, nilipata matibabu, nikapata ushauri (counselling) kwa mwezi mmoja. Baada ya hapo nikajiunga na mafunzo ya kutengeneza nywele, makucha na ushonaji. Mafunzo hayo yamenisaidia sana, sasa najisikia niko huru na nina furaha kuwa sehemu ya jamii tena. Fodaj Foundation imenishika mkono na kunionesha namna bora ya kuishi hapa Kitengela. Wamenisaidia kwa mambo mengi, na kwa kweli maisha yangu yamebadilika kwa njia chanya sana.”Nikarejea kwa Bi. Araka, kufahamu iwapo wana ushirikiano na serikali na mashirika ya kiraia. Akisema Post Traumatic anamaanisha kiwewe baada ya dhuluma.“Kwa kushirikiana na serikali na mashirika mengine ya kiraia, waathirika wanapatiwa msaada kwa ajili ya huduma za afya. Mfano wale waliobakwa au kupigwa, hupata matibabu kwa vipimo au dawa. Aidha, waathirika wa kimawazo wanapewa msaada wa kisaikolojia ili iwasaidie kuondokana na madhara ya post trauma ambayo wamepitia.

leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu Tsunami Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kujiandaa dhidi ya mawimbi hayo makubwa ya bahari yanayotokana na tetemeko chini ya bahari. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Asante Assumpta,Katika ujumbe wake, Guterres amesema maandalizi hayo yanahusisha kuweka mifumo ya kutoa maonyo ya mapema au tahadhari kwenye kila ufukwe, jamii na kokote kule.Bwana Guterres amefafanua kuwa tsunami si matokeo ya mara kwa mara lakini pindi yanapotokea madhara yake yanaweza kuwa makubwa na hata kusababisha vifo.“Husababisha vifo vya maelfu na hata mamia ya maelfu ya watu. Lakini kuna mbinu za kuweka watu salama,” anasema Guterres.Ametolea mfano janga la tsunami kwenye bahari ya Hindi mwaka 2004, janga ambalo lilisababisha dunia kuamua kuwekeza katika mifumo ya kutoa maonyo mapema.“Miongo kadhaa baadaye, uamuzi huo umelipa,” amesema Katibu Mkuu akitolea mfano tetemeko kubwa la ardhi lililokumba pwani ya Urusi mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu akisema, “lilisababisha tahadhari kwa mamilioni ya watu kuanzia pwani za Japani hadi visiwa vilivyoko bahari ya Pasifiki hadi California.”Ingawa hivyo amesema madhara ya janga hilo la tsunami yanaendelea kubadilika kutokana na mabadiliko kadhaa ikiwemo yale ya tabianchi.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akieleza kuwa kuheshimu baharí ni kutambua nguvu yake anasema, “kiwango cha maji ya bahari kikiongezeka, na idadi ya watu wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari ikiongezeka, mifumo ya kutoa maonyo mapema nayo inahitaji uwekezaji zaidi na kuboreshwa,”Ni kwa mantiki hiyo amesema hilo ndio lengo la mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mfumo wa Tahadhari kwa Wote ulioanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mpango wa utoaji onyo mapema dhidi ya tsunami ifikapo mwaka 2027.Maadhimisho ya mwaka huu ni ya 10, ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha siku hii kupitia azimio namba 70/203 la mwaka 2005.

Katika jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo utasikia kuhusu wito wa mataifa yote kuwekeza kwenye mifumo ya tahadhari za mapema ikiwa leo dunia inaadhimisha Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu Tsunami. Utasikia pia ziara ya Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa nchini Qatar ambapo amewatembelea wakimbizi wa kipalestina walioko nchini humo. Kutoka nchini Kenya utasikia juhudi za taasisi ya FODDAJ kusaidia jamii nchini Kenya kupambana na ukatili wa kijinsia.

Je wafahamu maana ya neno Mhanga ambalo wingi wake ni Wahanga? Basi ambatana na Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA akikupatia ufafanuzi huo.

Hii leo Jaridani, Anold Kayanda anakupeleka nchini Kenya kusikia usaidizi wa FAO kwenye harakati za kuondokana na njaa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupitia uimarishaji wa sekta ya kilimo. Lakini pia kuna Muhtasari kutoka kwa Leah Mushi akimulika:Baa la Njaa kuthibitishwa huko El Fasher na Kadugli nchini SudanAzimio la Doha lenye lengo la kuimarisha maendeleo ya jamii dunianiKauli ya Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa OCHA akiwa huko Doha, Qatar kufuatia kupitishwa kwa azimio hilo.Na kipengele cha Jifunze Kiswahili leo kinaelezea matumizi ya neno Mhanga na Wahanga.Karibu!

Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadu umewezesha biashara kukwamuka nchini Tanzania baada ya janga la COVID-19, hatua ambayo imeinua pia jamii nzima na si wajasiriamali wanawake peke yao. Simulizi hii ya Assumpta Massoi inamulika mjasiriamali mwanamke Haika Lawere anayemiliki hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar Es Salaam ambako ni jiji kuu la biashara la taifa hilo la Afrika.

Kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria, kikiajiri zaidi ya theluthi moja ya watu wote nchini humo. Lakini hali ya hewa isiyotabirika imefanya kilimo kuwa shughuli yenye mashaka makubwa — ukame, mafuriko na mvua zisizo na mpangilio zimekuwa tishio kubwa kwa wakulima, ambapo kilio chao kimesikiwa na Benki ya Dunia iliyokuja na suluhisho kwa kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Selina Jerobon ana taarifa zaidi.

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Sudan, Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) nchini Tanzania, na kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria.Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikieleza kuwepo kwa mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).Mpango wa Ufadhili Wajasiriamali Wanawake, (We-Fi) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadu umewezesha biashara kukwamuka nchini Tanzania baada ya janga la COVID-19, hatua ambayo imeinua pia jamii nzima na si wajasiriamali wanawake peke yao. Simulizi hii ya Assumpta Massoi inamulika mjasiriamali mwanamke Haika Lawere anayemiliki hoteli ya Mbezi Garden jijini Dar Es Salaam ambako ni jiji kuu la biashara la taifa hilo la Afrika.Kilimo ni moja ya sekta muhimu za kiuchumi nchini Nigeria, kikiajiri zaidi ya theluthi moja ya watu wote nchini humo. Lakini hali ya hewa isiyotabirika imefanya kilimo kuwa shughuli yenye mashaka makubwa — ukame, mafuriko na mvua zisizo na mpangilio zimekuwa tishio kubwa kwa wakulima, ambapo kilio chao kimesikiwa na Benki ya Dunia iliyokuja na suluhisho kwa kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikieleza kuwepo kwa mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF). Taarifa zaidi na Sheilah Jepngetich.

Dunia leo ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majiji, majiji ya kisasa pamoja na kukumbatia teknolojia yametakiwa kuhakikisha yanazingatia zaidi watu ili wengine wasiachwe nyuma au kutengwa na maendeleo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi.

Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Majiji, vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania na uwezeshaji wa wanawake nchini huko huko Tanzania.Dunia leo ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majiji, majiji ya kisasa pamoja na kukumbatia teknolojia yametakiwa kuhakikisha yanazingatia zaidi watu ili wengine wasiachwe nyuma au kutengwa na maendeleo hayo.Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba.Mpango wa “Chaguo Langu, Haki Yangu” nchini Tanzania ni jitihada thabiti zinazolenga kuwawezesha wanawake na wasichana kuishi maisha huru dhidi ya ukatili na vitendo hatarishi. Kwa ufadhili wa Serikali ya Finland, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la IPS, linafanya mabadiliko halisi katika jamii.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu imeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia vifo na majeruhi vilivyotokea katika maandamano yanayohusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi huu wa Oktoba. Selina Jerobon na maelezo zaidi.