POPULARITY
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Katika ujumbe wake wa mwaka mpya 2026 Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ameitaka dunia kushikamana kwa ajili ya amani, maendeleo, na usalama badala ya kuongeza mateso-Huko Somalia kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wakaazi wa Laascanood waboreshewa huduma za afya baada ya kuvurugika kwa miaka miwili-Na Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO amesema mwaka 2025 ulighubikwa na changamoto lukuki za afya ya umma duniani ikiwemo ukata wa ufadhili, lakini kuna matumaini hasa katika suala la utipwatipwa
Huko kaskazini mashariki mwa Somalia, eneo la Laascaanood linaendelea kushuhudia maboresho ya huduma muhimu za afya baada ya miaka miwili ya kuvurugika kwa huduma hizo kutokana na mizozo, maboresho haya yanaleta huduma za afya karibu zaidi na akina mama na watoto shukran kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na washirika wake. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.(Taarifa ya Leah)Kwa mujibu wa UNICEF nchini Somalia, mamilioni ya watoto wanakua katika kivuli au mazingira ya ukimya na dharura zilizosahaulika, takribani watoto milioni 1.8 wanahitaji matibabu ya utapiamlo mwaka huu wa 2025. Kila mwaka watoto wapatao 75,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hufariki dunia kutokana na magonjwa yanayozuilika na yanayoweza kutibiwa.Miaka miwili ya migogoro imesababisha kusambaratika kwa huduma muhimu huko Laascaanood. Kurejea kwa hali ya utulivu kumeanza kushuhudia urejeshwaji wa taratibu wa huduma hizi muhimu zinazookoa maisha. UNICEF, kwa msaada wa KSRelief na Saudi Esports Federation, inachangia kwenye kutoa huduma jumuishi za afya ya msingi, huku huduma hizo zote zikitolewa chini ya paa moja.Mpaka sasa maelfu ya watu wamefikiwa huku ukisaidia vituo 13 vya afya kama anavyoeleza Dayid Said Ismail Afisa Lishe (Sauti ya Dayid Said Ismail – Evarist)“Mradi huu unasaidia vituo 13 vya afya na unahudumia zaidi ya watu 150,000. Huduma zake zinajumuisha chanjo za watoto, matibabu ya magonjwa kama nimonia na kuhara, pamoja na huduma za magonjwa mengine ya kawaida ya utotoni.”Katika huduma za matibabu tumsikilize Saida Ali Elmi ambaye ni mhudumu wa Afya(Sauti ya Saida Ali Elmi- Sheilah)“Kama mnavyoona, akina mama wengi wamekuwa kwenye foleni tangu saa moja asubuhi na sasa ni saa 5:30 asubuhi. Kwa hiyo wapo hapa kwa ajili ya chanjo za kinga, ikiwemo chanjo za kifua kikuu, surua, polio, pepopunda, kifaduro, pamoja na chanjo mpya iitwayo PCV ya nimonia.”Juhudi hizi zinazofanywa na mashirika haya, tayari zimeanza kuleta matumaini mapya kwa Ayan Hassan Abdi mama mzazi wa Maryam “Nimemleta Maryam kwa sababu alikuwa na homa. Amepatiwa matibabu na pia chanjo. Alifanyiwa vipimo vya homa na kuharisha, na akatibiwa vizuri, Masha'Allah.”
Mwaka 2025 umeelezwa kuwa mwaka wa kihistoria kwa sekta ya afya duniani. Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe uliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO,Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, wakati akitoa tathmini yake ya mwisho ya mwaka 2025. Taarifa zaidi na Sabrina Saidi. Karibu Sabrina..(TAARIFA YA SABRINA SAIDI) Asante Flora,Akizungumza kutokea makao makuu ya WHO mjini Geneva, Uswisi, Dkt. Tedros amesema mwaka 2025 umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na changamoto nzito kwa afya ya dunia, huku akisisitiza kwamba dunia bado inahitaji uwepo wa WHO. (Clip 1-Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Kweli mwaka 2025 umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa na changamoto nyingi kwa afya ya dunia na kwa WHO. Mafanikio makubwa zaidi yalikuwa kupitishwa kwa Mkataba wa WHO wa kukabiliana na milipuko ya magonjwa, ambao ni mfano wa nguvu ya ushirikiano wa kimataifa pale nchi zinapochagua kushirikiana badala ya kugawanyika. Pia, mwaka huu WHO imethibitisha nchi 13 kufanikiwa kutokomeza magonjwa, ikatoa miongozo kuhusu tiba mpya kama Lenacapavir kwa kinga dhidi ya VVU na matibabu ya GLP-1 kwa utipwatipwa,na ikachukua hatua dhidi ya majanga 48 katika nchi na maeneo 79, ikiwemo Gaza, Sudan na Ukraine.”Akizungumzia changamoto, Dkt. Tedros amesema kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa na bajeti kumeathiri sekta ya afya duniani, lakini ameeleza kuwa hali hiyo pia inaleta fursa mpya.(Clip 2- Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Lakini ndani ya changamoto hizi pia kuna fursa. Ni fursa kwa nchi kuondokana na utegemezi wa misaada na kujenga mifumo ya afya inayojitegemea, na ni fursa kwa WHO kuwa taasisi imara zaidi na inayojipanga kwa siku zijazo. Dunia bado inahitaji WHO, na WHO itaendelea kushikilia maono yake ya msingi kuhakikisha kiwango cha juu kabisa cha afya kinapatikana kwa wote, si kama upendeleo wa wachache, bali kama haki ya kila mtu.”Dkt. Tedros amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa WHO itaendelea kushirikiana na nchi wanachama ili kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo za afya duniani.
Ukeketaji wa wasichana bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Kenya, licha ya marufuku ya kitaifa na juhudi za uhamasishaji zinazoendelea. Takwimu za Kitaifa KNBS na zile Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 83 ya wanawake na wasichana wa Marsabit na 66 wa Isiolo tayari wamekeketwa—ikiziweka kaunti hizi miongoni mwa maeneo yenye viwango vya juu zaidi nchini.Sasa wazee maeneo hayo wameanza mchakato kukabiliana na ukeketaji huo
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema tiba asilia na tiba jadidifu zina nafasi muhimu katika mifumo ya afya duniani, hasa katika kinga, huduma za usaidizi wa magonjwa na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Tiba Asilia, Jadidifu na Jumuishi cha WHO, Dkt. Sung Chol Kim, katika mahojiano maalum kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Tiba Asilia unaoendelea huko New Delhi, India. Sabrina Saidi na taarifa zaidi..
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa dawa za asili. Flora Nducha na taarifa zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia tiba asili, machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ubakaji unaotumika kama silaha ya vita nchini humo humo.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa tiba za asili.Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hofadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka.Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili, akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
A Dra. Tayne Miranda, médica psiquiatra e editora de Psiquiatria da Afya, analisa o conceito de hiperfoco à luz das evidências científicas e esclarece mitos comuns sobre sua relação com o TDAH e outros transtornos mentais.Temas abordados no episódio:• O que é hiperfoco e por que o termo se popularizou• Diferença entre hiperfoco e flow• O que a ciência diz sobre hiperfoco e TDAH• Influência de motivação, contexto e funções executivas• Hiperfoco no autismo e na esquizofrenia• Limites e desafios conceituais do tema
Watalaam wa wanyama wanasisitiza wanyama wote wanaochinjwa ni sharti kutimiza viwango vya juu ikiwemo mwonekano ,afya na usafi. Na kabla kuchinjwa wanyama hao kwa mfano ngombe ,hukaguliwa na kutengwa ili kubainisha nyama yao ni salama. Kwa mlaji unashauriwa kununua nyama iliyo na muhuri ambayo ni alama ya kuonesha nyama hiyo imekaguliwa na kuthibitishwa ni salama. Kwa wale wanaochinjia nyumbani bado unatakiwa kumpata mtalaam wa wanyama kumkagua mnyama wako na kutoa kibali cha kuchinjwa.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kwake Afisa Habari wa UN Stella Vuzo ambaye kandoni mwa mkutano wa UNEA-7 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki, alizungumza na Frida Amani, Mchechemuzi wa UNEP wa masuala ya mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema aina mpya ya virusi vya mafua inaenea kwa kasi duniani, ikiwa imeripotiwa katika zaidi ya nchi 30. WHO wanasema licha ya aina hiyo kutosababisha ugonjwa mkali zaidi wa mafua, chanjo bado ni kinga bora zaidi dhidi ya madhara makubwa na kulazwa hospitalini na inawahimiza wananchi, hasa makundi yaliyo hatarini, kupata chanjo mapema huku ikionya kuwa msimu huu wa likizo unaweza kuongeza maambukizi ya magonjwa ya njia ya hewa.Tuelekee Bujumbura Burundi ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo wamepatiwa hifadhi baada ya kukimbia machafuko nchini mwao. Innocent Chubaka kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR aliyeko katika kambi ya muda ya Mugara katika jimbo la Rumonge nchini Burundi anasema “tumepokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Congo ambao wamefika kupitia njia ya ziwa wakiwa na mitumbwi kuu kuu.Na kwa mara nyingine tena Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amezisihi pande zote katika mzozo nchini Sudan na Mataifa yenye ushawishi kuhakikisha mapigano yanasitishwa mara moja na kuzuia ukatili. Turk amelaani vikali mauaji ya raia zaidi ya watu 104 pia mauaji ya walinda amani sita wa Umoja wa Mataifa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Kaduguli, Kordofan Kusini, mnamo Desemba 13.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi. Nini kilitokea na aliwezaje kuishinda hali hiyo??? Tuungane na Leah Mushi katika simulizi hii.
Hii leo jaridani tunaangazia kilichojiri katika Mkutano wa COSP11 kuhusu ufisadi mjini Doha Qatar, haki za kibinadamu na vijana nchini Kenya, afya ya akili ikimulika upweke na jinsi unavyoweza kuepukana nayo.Mkutano mkubwa zaidi duniani wa kupambana na rushwa au ufisadi umeanza leo Desemba 15 mjini Doha nchini Qatar kwa wito wa kutumia teknolojia zinazoibuka katika mapambano dhidi ya rushwa na kushughulikia uhusiano wake na uhalifu wa kupangwa na makosa mengine ya kifedha.Haki ni msingi wa Kila siku, hiyo ndio ilikuwa kaulimbiu ya siku ya Haki za binadamu mwaka huu iliyoadhimishwa wiki iliyopita. Lakini kila uchao haki za binadamu zinaendelea kukiukwa kuanzia nyumbani hadi kwenye mtandao. Kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha vijana katika kupambana na ukiukwaji wa haki hasa mtandaoni, Ofisi ya Umoja wa Maataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) jijini Nairobi Kenya umewakusanya vijana kujadiliana nao na kuwapa mafunzo ya kumakinika hasa mtandaoni.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Matibabu mengi licha ya kupendekezwa au kuorodheshwa sahihi ,yanakabiliwa na usugu wa vimelea tatizo linalofanya dawa hizo kushindwa kutibu inavyotakikana Dawa za kutibu Malaria ,TB na Kipindu Pindu zimetajwa kuathirika sana ,haswa dawa aina ya antibiotics ambazo hutumika kuwa matibabu ya kwanza ya kuua vimelea.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kwa mwanariadha na mchchemuzi wa masuala ya wanawake, akieleza hatua zinazochukuliwa kutokomeza dhulma wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze lugha ya Kiswahili.Huku mapigano yakizidi kushika kasi katika eneo la Kordofan nchini Sudan, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya hii leo kuhusu hatari ya mashambulizi mapya dhidi ya raia, baada ya kuripotiwa vifo zaidi ya watu 269 kutokana na mashambulizi ya angani, mabomu na mauaji ya kiholela tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba. Ofisi yake imeeleza kupokea taarifa za ulipizaji kisasi, utekaji, ukatili wa kingono na ulazimishaji wa watoto kujiunga na makundi ya kivita, huku miji kama Kadugli, Dilling na El Obeid ikikabiliwa na njaa, kuzingirwa na kukwama kwa misaada ya kibinadamu.Malaria, ugonjwa ambao takriban asilimia 95 ya vifo vinavyoripotiwa duniani ni kutoka nchi za Afrika tena kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5. Ulionekana kuweza kudhibitiwa lakini sasa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, anasema unaelekea kubaya kutokana na kuongezeka kwa usugu wa dawa, hali inayotishia kuyafuta mafanikio yaliyookoa maisha ya watu milioni moja mwaka 2024 kupitia chanjo na vyandarua vipya vyenye dawa ya kukabiliana na mbu waenezao Malaria.Na tuhitimishie nchini Msumbiji ambako Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Amy Pope amefanya ziara ya siku tatu na kujionea athari zilizoletwa na Mafuriko, vimbunga na kuzorota kwa usalama huko Kaskazini mwa nchi hiyo hali iliyosababisha zaidi ya 100,000 wameyakimbia makazi yao, na zaidi ya 600,000 wakihitaji msaada.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MADHALI"Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, simulizi ya Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona na huduma za afya ya uzazi kwa wasichana vigori nchini Kenya.Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli.Ili kuyajadili baadhi ya masuala aliyoyagusia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, basi Diana Katabarwa wa redio washirika wetu Uhai FM amezungumza na Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona, Bahati Sanga, Katibu wa Chama Cha Wasioona, Mkoa wa Tabora.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Ripoti nyingi huonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ni akina mama au watoto Hii ni kutokana na wao kutangamana moja kwa moja na mazingira ambayo huwa makazi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa mbali mbali. Vimelea hao hukaa mchangani,kwenye maji au hupatikana kwenye kinyesi .
Kama tulivyokujuza le oni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU. Flora Nducha na taarifa zaidi
Tafiti zimeonesha kuwa magonjwa mengi ya milipuko haswa barani Afrika yanachochewa na mabadiliko ya tabia nchi Mafuriko ,ukame au kupanda joto yanaweza kusababisha kusambaa kwa haraka kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa au kuzaana kwa haraka.
Karibu mmoja kati ya Waustralia wanne hawatafuti msaada wanapopata matatizo ya afya ya akili wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua. Wataalamu wanasema kwamba taarifa zilizotolewa na Gidget Foundation zinaonyesha ukosefu wa kuelewa dalili na ishara, pamoja na unyanyapaa unaoendelea kuhusu suala hili.
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe katika siku ya Choo Duniani, simulizi za wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan, na usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR).Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo.Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha.Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
A inteligência artificial está transformando profundamente a medicina. De diagnósticos mais rápidos e precisos a sistemas capazes de prever riscos e personalizar tratamentos, a tecnologia vem ampliando o alcance e a eficiência dos cuidados com a saúde. Mas surgem também grandes desafios: como preparar os novos profissionais e atualizar os que já atuam há décadas para acompanhar esse ritmo acelerado da inovação? A formação médica precisa se reinventar, incorporando habilidades digitais, pensamento crítico e ética no uso da IA. O futuro da medicina já começou — e ele exige uma nova forma de aprender, de atender e de cuidar. Para falar disso, e como a cultura da inovação e da IA vem se incorporando à formação profissional, o apresentador Daniel Gonzales recebe, no Start Eldorado, o radiologista Gustavo Meireles, vice-presidente médico da Afya, o maior hub de educação e soluções para a prática médica do Brasil. O Start vai ao ar todas as quartas-feiras, às 21h, na Rádio Eldorado FM (107,3 para toda a Grande SP), app, site e assistentes de vozSee omnystudio.com/listener for privacy information.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki mjini El Fasher, pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika maeneo ya Kordofan nchini Sudan. Guterres amesema “Mtiririko wa silaha na wapiganaji kutoka nje lazima ukatwe. Misaada ya kibinadamu lazima iweze kuwafikia haraka raia wanaohitaji, na mapigano lazima yakome,”.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano limemchagua Phoebe Okowa kutoka Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), baada ya duruu nne za upigaji kura. Upigaji kura huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini kwa utaratibu tofauti, kama inavyotakiwa na Katiba ya Mahakama hiyo ya Haki. Bi. Okowa amechaguliwa kwa wingi wa kura ambapo alipata kura 8 katika Baraza la Usalama na kura 106 katika Baraza Kuu.Kumekuwa na ongezeko la uraibu wa nikotini na bidhaa nyingine zinazozalishwa kwa kutumia tumbaku duniani hususani miongoni mwa vijana na tena wengi hivi sasa wanatumia sigara za kielektroniki, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO. Tarehe 17 mpaka 21 Novemba utafanyika mkutano mkubwa kujadili namna serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitakavyoweza kusaidia kupambana na janga la tumbaku duniani, linalosababisha vifo zaidi ya milioni saba kila mwaka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU"Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!
Wahamiaji wengi wanakumbana na matatizo tofauti wanapojaribu kupata msaada wa afya ya akili. Umoja wa Mataifa unasema kwamba upatikanaji wa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi kwa kila mtu , ikiwemo wahamiaji na wakimbizi. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wahamiaji mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, huzuni, kiwewe na ata upweke kutokana na mazingira mapya. Mtaalamu wa Afya ya Akili Terry Kiguru anatueleza jinsi ya kupata msaada huo na kwanini.
No terceiro episódio da série Tomada de Decisão, o diretor médico da Afya e editor-chefe do Whitebook, Dr. Ronaldo Gismondi, recebe a Dra. Dayanna Quintanilha, médica formada pela Universidade Federal Fluminense (UFF), com residência em Clínica Médica pelo HUAP e doutoranda em Ciências Médicas pela UFF.Ronaldo e Dayanna discutem um caso real de infecção urinária febril em uma mulher jovem com histórico de ITU de repetição. A partir de uma apresentação com febre, dor lombar e sinais de gravidade, eles analisam o raciocínio clínico necessário para responder às grandes perguntas: internar ou tratar ambulatorialmente? Qual antibiótico escolher? Quais exames realmente importam? Quando solicitar imagem?Um episódio prático e direto, ideal para estudantes e médicos em formação que querem entender o pensamento clínico aplicado à beira do leito.#TomadaDeDecisão #CasosClínicos #InfecçãoUrinária #ITU #Pielonefrite #RaciocínioClínico #ClínicaMédica #Afya #Whitebook #MedStudent #ResidênciaMédica #SaúdeDaMulher #MedicinaInterna #DiagnósticoDiferencial #Antibioticoterapia #EmergênciaMédica #DiscussãoDeCasos #PráticaMédica #FormaçãoMédica #MedicinaBaseadaEmEvidências #DayannaQuintanilha #RonaldoGismondi #HealthTech #IAnaSaúde #MachineLearning
Leo jaridani tunamulika kimbunga Melissa huko Karibea, uhamishaji wagonjwa kutoka Gaza kwenda nchi za nje kupata huduma za kigeni na hali tete kwa watoto nchini Sudan. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaAntonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha athari kubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, limeongoza uhamishwaji wa kwanza wagonjwa kutoka Gaza tangu awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano. Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura. Flora Nducha na taarifa zaidi.Nchini Sudan hususani katika eneo la El Faher kusinimagharibi mwa nchi, hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya kila siku, huku ghasia, njaa, na vizuizi vya utoaji misaada vikiendelea kuathiri mamilioni ya watu wakiwemo watoto waliokwama katika maeneo ya vita. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, limeongoza uhamishwaji wa wagonjwa kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano kwenye ukanda huo.Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, kuelekea Afrika Kusini, Uswisi na kwingineko, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura.Katika hospital iliyojengwa kwa mahema katika eneo la AL-MAWASI, RAFAH kwenye Ukanda wa Gaza wagonjwa wakihudumiwa kila kona watoto kwa wakubwa Miongoni mwao ni Ibrahim Abu Ashiba, mkurugenzi wa filamu ambaye maisha yake yamebadilika ghafla. Anakumbuka wakati alipojeruhiwa. Anasema, "Nilipigwa risasi mara kadhaa, mara moja kwenye kifua, mara moja kwenye bega, mara mbili mkononi. Risasi hizo mbili zilikata mishipa ya neva ya mkono wangu. Sasa siwezi kushika kamera wala kunyoosha mkono wangu kawaida. Ghafla, maisha yangu yote yalisimama."Safari ya kupona kwa Ibrahim inaanzia Afrika Kusini, ambapo amekubaliwa kwenda kupokea matibabu maalum ambapo anasema "Maisha yangu yote yalikuwa yamesimama baada ya kujeruhiwa hadi waliponipigia simu na kunijulishakwamba nitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu. Ilionekana kama nimezaliwa upya."Mgonjwa mwingine katika hospitali hii ni, Maria Al-Shaer, alijeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyokuwa yakiendelea Gaza, huku akipoteza ndugu zake. Mama yake, Raghda Ahmed Al Shaer, anaelezea mateso hayo. "Maria amepoteza baba yake na ndugu zake wote. Alijeruhiwa na kuvunjika mguu, mifupa na kupoteza nyama. Anahitaji upasuaji wa kuwekewa viungo bandia. Maisha yake yamegeuka, hawezi kutembea, na hali yake ya kisaikolojia imeathirika sana."Uhamishwaji huu umeratibiwa na Shirikisho la Chama cha Msalaba Mwekundu Palestina, kwa msaada wa WHO. Dkt. Luca Pigozzi, Mratibu wa Timu ya Dharura ya WHO, anafafanua umuhimu wake."Huu ni uhamishaji wa kwanza wa matibabu tangu kusitishwa kwa mapigano Oktoba 10. Tumejizatiti kuongeza uwezo wetu kusaidia na kuratibu uhamishaji kwa ajili ya matibabu, kwa ushirikiano wa karibu na Shirikisho la chama cha Msalaba Mwekundu la Palestina."Raghda anaeleza matumaini kwa ajili ya binti yake wanapohama kwenda Uswisi. "Wametupigia kutuarifu kwamba Maria amekubaliwa kusafiri kwenda Uswisi kwa matibabu. Tumefurahi sana kwamba atatembea tena, na hali yake ya kisaikolojia itaboreka. Atarudi kuwa Maria wa kawaida kama tuliyemjua."WHO inasisitiza kuwa wagonjwa takriban 15,000 bado wanangojea idhini ya kupata matibabu nje ya Gaza na inatoa wito kwa nchi zote kufungua milango yote za dharura kwa ajili ya uokoaji wa wagonjwa.
No segundo episódio da série Tomada de Decisão, o diretor médico da Afya e editor-chefe do Whitebook, Dr. Ronaldo Gismondi, recebe o Dr. Yuri Albuquerque — médico do Hospital Sírio-Libanês, intensivista e doutorando pela USP, com formação em Clínica Médica pela UERJ e R3 pela UFRJ — para discutir um caso real de pneumonia comunitária grave.A partir de um paciente idoso com febre, dispneia e rebaixamento do nível de consciência, eles exploram o raciocínio clínico necessário para definir exames prioritários, critérios de gravidade, momento ideal para iniciar antibiótico e suporte ventilatório adequado.Com uma conversa dinâmica e didática, o episódio mostra como pensar de forma estruturada diante de uma emergência respiratória, ajudando estudantes e médicos em início de carreira a aprimorar sua tomada de decisão à beira do leito.#TomadaDeDecisão #CasosClínicos #PneumoniaComunitária #RaciocínioClínico #ClínicaMédica #Afya #Whitebook #Medicina #MedicinaInterna #TerapiaIntensiva #EmergênciaMédica #DiagnósticoDiferencial #PneumoniaGrave #DoençasRespiratórias #ExameFísico #Antibioticoterapia #SuporteVentilatório #CuidarÉCiência #FormaçãoMédica #DiscussãoDeCasos #MedStudent #ResidênciaMédica #Hospital #AprendizadoClínico #RonaldoGismondi #YuriAlbuquerque #MedicinaBaseadaEmEvidências #PráticaMédica
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Umoja wa Mataifa na tutasikia kutoka mashinani wananchi na asasi za kiraia zina yapi ya kusema kuhusu shirika hili kubwa na la kipekee linalounganisha nchi wanachama 193 duniani.Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa dharura kwa dunia kuchukua hatua mara moja kukabiliana na janga la kibinadamu linaloongezeka nchini Sudan. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, nchini humo wakiwemo watoto milioni 15 na wakimbizi karibu milioni moja.Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Oktoba 22 ilisema Israeli lazima itimize majukumu yake kama “anayekalia kimabavu” kwa kuhakikisha kuwa msaada unaweza kupita bila vizuizi na kwa kuheshimu haki za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu yanayofanya kazi katika Ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa Mabavu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea maoni hayo ya ICJ kuwa “muhimu sana,” akiongeza kuwa yametolewa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unafanya kila juhudi kuongeza kasi ya misaada kuingia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.Nchini Kenya, wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri hadi siku 15 kupata malipo sasa wanapokea pesa ndani ya saa 72 pekee, shukrani kwa mfumo mpya wa malipo ya kidijitali uliotolewa na Shirika la Sfya la Umoja wa Mataifa WHO na Wizara ya Afya ya nchi hiyo. Mfumo huu unapeleka fedha moja kwa moja kwenye pochi za simu za wafanyakazi, ukipunguza ucheleweshaji, gharama na kuongeza motisha. Wafanyakazi zaidi ya 120,000 sasa wanafaidika, kuboresha ufanisi wa kampeni za chanjo na juhudi za kudhibiti polio.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Mwalimu Nyerere na tunakupeleka nchini Tanzania ambako kunaendelea juhudi za kuimarisha matumimizi ya lugha ya Kiswahili na utangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashairki, manufaa ya kiuchumi na kijami na kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba Gaza itahitaji karibu dola bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi upya baada ya miaka miwili ya mzozo, huku dola bilioni 20 zikitakiwa katika miaka mitatu ijayo. Makadirio haya yanatokana na, tathmini ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Benki ya Dunia. Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina Jaco Cilliers,amesema “Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92.”Umoja wa Mataifa umeongeza hatua zake za dharura huko Gaza kwa kutoa dola milioni 11 kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) kukidhi mahitaji ya haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Mgao huu, uliozinduliwa na Mratibu wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher, utaunga mkono utoaji wa chakula, maji, huduma za afya na makazi kwa raia walioathiriwa na mzozo wa miaka miwili. Hatua hii inafuatia mgao wa dola milioni 9 wiki iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa hospitali na huduma muhimu, na kufanya jumla ya msaada wa hivi karibuni kufikia dola milioni 20.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa ya neva duniani, ambayo sasa yanachangia zaidi ya vifo milioni 11 kila mwaka. Ripoti mpya ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva inaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni 3 sawa na zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani wanaishi na magonjwa yanayoathiri ubongo, ikiwemo kiharusi, ugonjwa wa kusahau, kifafa, na maumivu ya kichwa ya muda mrefu. Kwa mujibu wa ripoti nchi maskini ndizo zinazoathirika zaidi, zikiwa na upungufu mara 80 wa idadi ya wataalamu wa magonjwa ya neva ikilinganishwa na nchi tajiri. WHO inazitaka serikali kutoa kipaumbele kwa afya ya ubongo, kuongeza fedha na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE!Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
No episódio de estreia da série Tomada de Decisão, o diretor médico da Afya e editor-chefe do Whitebook e Portal Afya, Dr. Ronaldo Gismondi, conversa com a Dra. Larissa Wermelinger sobre um caso real de confusão mental em paciente idosa.Eles analisam o raciocínio clínico passo a passo — da avaliação inicial aos diagnósticos diferenciais, exames e condutas — destacando os principais aprendizados sobre delirium e distúrbios metabólicos em idosos.Um bate-papo direto e prático, feito para estudantes e médicos em início de carreira que querem aprimorar sua tomada de decisão à beira do leito.#Medicina #CasosClínicos #Delirium #RaciocínioClínico #TomadaDeDecisão #Afya #Whitebook
Mashirika ya afya duniani yametoa miongozo mipya yenye lengo la kuokoa maisha ya maelfu ya wanawake wanaopoteza maisha kutokana na kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua hali inayojulikana kama postpartum haemorrhage au PPH. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya katika hospital Gaza, mradi wa PLEAD nchini Kenya na mafanikio yako katika kesi za mashinani, na kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP.Kufuatia kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani, halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu. Tuungane na Leah anayetujuza zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 tukimulika hotuba za viongozi na mikutano mingine ya pepmbezoni kuhusu malengo ya maendeleo enedelevu, SDGs.Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha.Tukisalia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masula mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masuala mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza tena na Dkt. Kapologwe mara tu baada ya mkutano huo
Makubaliano yaliyosimamiwa na mashirika ya kimataifa, likiwemo UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, halikadhalika Mpango wa afya wa Clinton (CHAI), Wits RHI na Maabara ya Dkt. Reddy, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa Lenacapavir kwa gharama nafuu.Dawa hii, inayodungwa mara mbili pekee kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, jambo muhimu hasa kwa wale wanaopata changamoto kutumia dawa za kila siku.Video ya UNITAID inaonesha maabara yenye teknolojia ya hali ya juu, ambamo wanasayansi wanaandaa dawa hiyo inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID, Tenu Avafia, anasema hatua hii ni ushindi mkubwa kwa jamii zinazohitaji kinga ya muda mrefu dhidi ya VVU."Tumeitikia wito kutoka kwa jamii na nchi tunazohudumia kwa kuhakikisha dawa hii inapatikana kwa gharama nafuu. Tunatarajia usambazaji wa toleo la bei nafuu la dawa hii kuanza kufikia mwaka 2027, chini ya miaka miwili tu tangu idhini kutolewa katika nchi za kipato cha juu — kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa."Akizungumza kuhusu hatua hii muhimu, Carmen Pérez Casas, Mkuu wa Mikakati Mwandamizi wa UNITAID, anasema:"Kwa kushirikiana na watengenezaji wa dawa mbadala, tumefanikisha bei nafuu mapema zaidi. Lakini bado tunahitaji kusaidia nchi na jamii kwa kuongeza upatikanaji."UNITAID inasema kwa msaada wa mashirika kama PEPFAR ambao ni mfuko wa Rais wa MArekani wa usaidizi wa dharura dhidi ya UKIMWI, pamoja na mfuko wa kimataifa na wakfu wa Gates, hatua hii inaleta matumaini ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU duniani.
Mada hii kwa kina inamulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wazungumzaji wa Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi
No episódio especial do Afya Podcasts, "Bora se Cuidar", o cardiologista Dr. Ricardo Moraes conversa com a médica psiquiatra Dra. Lorena Del Sant sobre a importância da saúde mental e o papel do humor nesse processo. Será que rir realmente é o melhor remédio? Embora o riso possa trazer um alívio temporário, ele não substitui o cuidado profissional. Juntos, eles discutem como o humor pode ser uma válvula de escape, mas sempre com a necessidade de uma abordagem cuidadosa e profissional. E para quem quer dar o primeiro passo, a Afya oferece um espaço digital seguro e gratuito, com acolhimento psicológico e psiquiátrico. Bora se cuidar? Confira os recursos disponíveis e comece hoje mesmo: https://www.afya.com.br/bora-se-cuidar
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi' chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.”Kando ya hotuba za viongozi, kunafanyika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa Programu ya Dunia kwa ajili ya vijana. Je vijana kutoka Malawi wana ujumbe gani? Mwakilishi wao kwenye mkutano huu Rachel Mganga Wanangwa anasema, “Ujumbe kutoka vijana wa Malawi ni wekezeni kwetu, tusaidieni, shirikianeni nasi, na wanashiriki kwenye meza za mazungumzo ili kuhakikisha kuwa sauti zao zinawakilishiwa.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika siku ya pili ya mjadala mkuu wa UNG80, na ujumbe wa washiriki wa mkutano huu kutoka Nigeria na Tanzania.Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia.Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19.Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando. Leo, sauti kutoka pande zote za dunia zinaitaka haki ya kijamii katika moja ya mikutano ya kando na miongoni mwa sauti hizo ni ya mwanaharakati na mhamasishaji wa masuaa ya wasichana kutoka Nigeria ambaye anasema wasichana vigori hawapaswi kusahaulika.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ametaja wanachotarajia kwenye mkutano huo..
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum na mada yetu inamulika maoni kuhusu miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Pia tunakuetea muhtasari wa habari unaofuatilia ujumbe wa viongozi katika mjadala mkuu wa UNG80.viongozi wa dunia wamekutana leo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiwa ni siku ya kwanza ya Mjadala Mkuu wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiambatana na vikao vya kando vya ngazi ya juu. Katika hotuba yake ya UNGA 80 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufanya maamuzi “ni aina gani ya dunia tunataka kujenga pamoja.”Kuanza kwa UNGA maana yake idadi kubwa ya wageni, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN anayeshughulikia habari na teknolojia, Bernardo Mariano, amesema wamejipanga kutoa huduma ya internet (Wi Fi) kwa watu 40,000 huku wakihakikisha hotuba za viongozi zinapeperushwa bila hitilafu za kiufundi wala kuvurugwa na mashambulizi ya mtandaoni.Na Hapo kesho Jumatano viongozi wa jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, ESCA watakutana kumulika Diplomasia ya kisayansi na afya ili kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe ameeleza kulikoni?.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete kama anavyosimulia Flora Nducha kwa taarifa hii.
Jaridani leo jaridani tunaangazia haki ya elimu kwa wasichana na wanawake nchini Afghanistan, na kuzorota kwa huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Pia tunakwenda nchini Zambia kumulika mradi wa wakulima wadogo.Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete.Kupitia mradi wa SCRALA uliowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP, wakulima wadogo nchini Zambia sasa wanaweza kulima mwaka mzima kwa kutumia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi kama vile mifumo ya umwagiliaji na vituo vya ukusanyaji mazao, jambo linalochangia kuongezeka kwa tija na upatikanaji wa masoko.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limefanya mabadiliko muhimu katika orodha yake ya dawa muhimu duniani au Essential Medicines List – EML na orodha ya dawa muhimu kwa watoto (EMLc) ikijumuisha dawa za kisasa za saratani, kisukari, unene uliopitiliza na magonjwa mengine sugu.Orodha za WHO za dawa muhimu ni nyenzo za mwongozo zinazotumiwa na zaidi ya nchi 150 kupanga ununuzi, bima za afya na upatikanaji wa dawa. Kwa lugha rahisi, dawa zinazoorodheshwa hapa huwa na nafasi kubwa zaidi ya kununuliwa na kutolewa kwa wagonjwa kupitia huduma za umma kwani wanachama wa WHO wanaziweka dawa hizi kama kipaumbele cha kiafya kwa mamilioni ya watu duniani.WHO wakati wakitangaza orodha hiyo mpya waliweka bayana kuwa dawa hizi mpya si za majaribio, bali ni zile ambazo zimethibitishwa kitabibu kuwa zinaokoa maisha, kupunguza madhara ya magonjwa na kuboresha maisha ya wagonjwa.Nini maana yake?Kuongezwa kwa dawa hizi ni hatua ya mbele katika safari ya kuhakikisha afya bora kwa wote. Inamaanisha wagonjwa zaidi wa saratani, kisukari na magonjwa mengine sugu wanaweza kuwa na matumaini ya maisha marefu na bora. Pia ni wito kwa mataifa kuchukua hatua ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa haki na usawa, bila kumwacha mtu yeyote nyuma.Changamoto ya bei na usawa wa kiafyaChangamoto kubwa sasa ni bei kubwa ya dawa hizi mpya, ambazo zinaweza kufanya wagonjwa wengi kushindwa kuzipata.WHO inapendekeza mikakati ya kupunguza gharama na kuhakikisha dawa hizi zinapatikana kwenye ngazi ya huduma za msingi za afya.Deusdedit Mubangizi, Mkurugenzi wa Sera na Viwango vya Dawa WHO, anasema “Sehemu kubwa ya matumizi ya nje ya mfuko wa magonjwa yasiyoambukiza yanaelekezwa kwenye dawa, ikiwa ni pamoja na zile zinazoainishwa kama muhimu na ambazo kimsingi, zinapaswa kupatikana kwabei rahisi kwa kila mtu. Ili kufikia upatikanaji sawa wa dawa muhimu kunahitajika mwitikio madhubuti wa mfumo wa afya unaoungwa mkono na dhamira dhabiti ya kisiasa, ushirikiano wa sekta nyingi na programu zinazozingatia watu ambazo hazimwachi mtu nyuma.”Kwa maneno mengine, dawa hizi haziwezi kuwa za matajiri pekee lazima mifumo ya afya, serikali na sekta binafsi zishirikiane kuhakikisha kila mtu anayehitaji anapata dawa kwa gharama nafuu.© UNOCHA/Ali Haj SuleimanDaktari akimpatia matibabu mgonjwa wa Saratani huko nchini SyriaSaratani, kisukari na unene uliopitiliza ni changamotoSaratani na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu kwa mamilioni ya watu duniani kila mwaka. Kwa mfano, saratani pekee inaua karibu watu milioni 10 kila mwaka.Kuongeza dawa mpya za saratani kama pembrolizumab na atezolizumab, ambazo zinasaidia kinga ya mwili kushambulia chembe chembe za saratani, kunaleta matumaini mapya hasa kwa wagonjwa katika nchi zenye rasilimali chache.Kwa upande mwingine, dawa za kundi la GLP-1 receptor agonists kama semaglutide na tirzepatide zimeingizwa kwenye orodha ili kusaidia wagonjwa wa kisukari cha aina ya pili wanaoishi pia na unene uliopitiliza au matatizo ya moyo na figo. Dawa hizi husaidia kudhibiti sukari, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na figo, na pia kusaidia kupunguza uzito.