POPULARITY
Kwa zaidi ya karne mbili, maelezo ya Newton ndiyo yaliyotawala sayansi. Kisha mwaka 1915, Albert Einstein akaja na wazo lililobadilisha kila kitu: gravity si nguvu ya kuvutana — ni kupinda kwa nafasi na wakati (space-time).
"Patrzę na to z niedowierzeniem. Długopis prezydenta stał się przeszkodą w rządzeniu. Prezydent Nawrocki w ciągu dziesięciu miesięcy zawetował więcej ustaw niż prezydent Kwaśniewski w ciągu 10 lat. Czy to nie jest patologia? Na pewno rząd nie odpuści. Będą kolejne ustawy aż do skutku" – powiedział w Popołudniowej rozmowie w RMF FM minister cyfryzacji Krzysztof Gawkowski. Wicepremier skomentował też wizytę prezydenta w USA z okazji urodzin Donalda Trumpa, które odbędą się w najbliższy weekend. "Jeśli to ma służyć Polsce, to nie mam z tym problemu" – ocenił.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni kuboresha zao hilo na kuinua pato la mkulima.Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Lebanon amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa mapema leo Alhamisi baada ya makombora ya mizinga kulenga eneo lao la kazi karibu na Marjayoun kusini mashariki mwa nchi hiyo, imesema taarifa ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo muda wowote kuanzia sasa.Shirika la Umja wa Mataifa la afya Duniani, WHO, limesema chakula kisicho salama kinaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma duniani, kikisababisha takribani wagonjwa milioni 866 na vifo milioni 1.5 kila mwaka, huku watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari kubwa zaidi. Kwa mujibu wa ripoti mpya watoto hao wadogo, ambao ni asilimia 9 tu ya idadi ya watu duniani, wanachangia karibu theluthi moja ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula.Leo ni siku ya watoto wasio na hatia waathirika wa ukatili duniani, maadhimisho haya yanakuja wakati ambapo ripoti ya Mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Migogoro ya Silaha inaonesha kwamba ukatili dhidi ya watoto katika migogoro ya silaha ulifikia viwango visivyo vya kawaida mwaka 2024, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 25 la ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikilinganishwa na mwaka uliopita.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumoikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani. Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wito wa maeneo ya nyanda za malisho na jamii za wafugaji kutambuliwa.
Shirika la Afya Duniani limetangaza mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ni dharura ya afya ya umma inayotia wasiwasi kimataifa.WHO inasema mlipuko huo hauja fikia vigezo vya dharura ya janga, lakini nchi zinazo changia mipaka ya ardhi na DRC ziko katika hatari kubwa ya usambaaji zaidi.Kwa wakazi wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekuwa na mambo mengi ya kuhofia kutokana na uhasama ambao umekuwa ukiendelea kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji waasi.Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.
W nowym odcinku wideokastu „Temat tygodnia” Aleksander Kwaśniewski komentuje relacje USA–Polska, przyszłość NATO, zmieniającą się politykę Donalda Trumpa, zagrożenie ze strony Rosji. Ale też narastający konflikt wewnętrzny i to, jak wygląda polaryzacja w Polsce przed wyborami 2027. Czy relacje USA–Polska nadal mogą się opierać na strategicznym zaufaniu? Aleksander Kwaśniewski wywiad analizuje zmieniającą się sytuację międzynarodową i rolę Stanów Zjednoczonych. Czy Europa może nadal bezwarunkowo liczyć na amerykańskie gwarancje bezpieczeństwa? Rozmawiamy o tym, jak zmienia się polityka Donalda Trumpa i dlaczego – zdaniem Kwaśniewskiego – sam Trump przeminie, ale „trumpizm” pozostanie trwałym elementem amerykańskiej polityki. Analizujemy także, kim dziś jest amerykański elektorat i jak zmiany społeczne wpływają na przyszłość NATO. Czy NATO się rozpadnie? Czy NATO pomoże Polsce, gdyby Rosja upomniała się o kolejne terytoria? Punktem wyjścia dla naszej rozmowy jest kwestia obecności wojsk USA w Polsce i dyskusja wokół tematów takich jak ostatnie wycofanie wojsk USA z Polski. Jaką rolę odgrywają amerykańscy żołnierze w Polsce? Czy Polska ma się czego obawiać i na ile prawdziwe są obawy typu: USA nie pomogą Polsce? W rozmowie pojawia się również temat Rosji i bezpieczeństwa regionu. Zastanawiamy się, czy Rosja zaatakuje kolejne kraje. Czy możliwy jest scenariusz, że Rosja zaatakuje przesmyk suwalski? Aleksander Kwaśniewski podkreśla, że nie należy popadać w defetyzm, Sojusz Północnoatlantycki nadal ma zdolność reagowania. Druga część rozmowy dotyczy polskiej polityki: co Aleksander Kwaśniewski myśli o Karolu Nawrockim, jak trwała jest polaryzacja w Polsce, dlaczego konflikt Nawrocki kontra Tusk wpływa na relacje międzynarodowe Polski i dlaczego partnerzy zagraniczni coraz częściej nie wiedzą, kto realnie odpowiada za politykę państwa. W rozmowie poza tym: konflikt w PiS, rosnąca rola partii konkurencyjnych na prawicy (Konfederacja Korony Polskiej Grzegorza Brauna i Konfederacja Sławomira Mentzena), przyszłość polskiej sceny politycznej przed wyborami 2027. Z Aleksandrem Kwaśniewskim rozmawia Karolina Lewicka, tygodnik „Polityka”. Czego dowiesz się z odcinka? 1. Czy NATO i USA nadal są gwarantem bezpieczeństwa Polski 2. Dlaczego Aleksander Kwaśniewski uważa, że „trumpizm” przetrwa Donalda Trumpa? 3. Jak konflikt Nawrocki kontra Tusk wpływa na pozycję Polski za granicą?
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Hanta kwenye meli ya kifahari ya Hondius kutoka Argentina na kulazimika kutia nanga nchini Cabo Verde, hii leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliosababisha hadi sasa vifo vya watu 3 wakiwemo wanandoa wawili unaendelea.Tukisalia na mlipuko huo wa virusi vya Hanta, Mwakilishi wa WHO nchini Cabo Verde amesema hivi sasa meli hiyo Hondius iko njiani kuelekea visiwa vya Canary nchini Hispania, “na kwenye meli tuna daktari wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna madaktari wawili wa Kiholanzi ambao wameimarisha timu, na kuna mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mlipuko ambaye atasafiri na meli hadi bandari inayofuata ambayo ni visiwa vya Canary. Kwa sasa hakuna mtu mgonjwa kwenye meli, lakini iwapo mtu ataugua, basi kutakuwa na madaktari na vifaa vya matibabu vya kuwahudumia wakati wa safari.”Nchini Tanzania hivi karibuni ripoti ya uainishaji wa viwango vya upatikanaji wa chakula nchini humo iliyoandaliwa kwa pamoja na serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO ilieleza kuwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri za wilaya za Same, Maswa na Monduli yako katika kiwango cha tatu yaani (IPC 3).Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Karibu usikilize Kipindi cha Maswali ya Husuyo Imani. Mwezeshaji ni Shemasi Emmanuel mganga kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Mada ni Ni nani anaemchagua Papa? Tarehe 27 Februari 2026 L'articolo Kwa mfano mtu akikukosea na hataki kukuomba msamaha hapo inapaswa kumfanyeje? proviene da Radio Maria.
Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo' iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Rising fuel prices are putting pressure on household budgets across Australia, and for many people, it's changing the way they travel. So what can you do to reduce your fuel costs without giving up your daily routine? Here are some simple, practical ways to save money on petrol. - Kuongezeka kwa bei za mafuta kunaweka shinikizo kwenye bajeti za familia kote nchini Australia, na kwa watu wengi, kunabadilisha jinsi wanavyosafiri. Kwa hivyo unaweza fanya nini kupunguza gharama zako za mafuta bila kuacha utaratibu wako wa kila siku? Hapa kuna njia rahisi na za vitendo za kuokoa pesa kwa petroli.
Nchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani ya Shilingi za nchi hiyo Bilioni 125. Je, ripoti hii imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa kilichotokea nchini Tanzania ? Tunachambua.
Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Cochameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na wanadamu?
FAO nchini Kenya inasema mradi huo wa miaka mitano uitwao FARM, unalenga kuimarisha uwekezaji katika mbinu mbadala na usimamizi endelevu wa kemikali hatari na plastiki kwenye sekta ya kilimo barani Afrika na Amerika ya Kusini. Tweet URLUkifadhiliwa na Fuko la Mazingira Duniani, GEF, mradi unafanya kazi na vikundi vya wataalamu wa kitaifa kutoka taasisi mbalimbali, kuangazia vipaumbele na changamoto za ndani ili kutengeneza mitaala ya mafunzo inayolinda mazingira. Ripoti ya mradi imebainisha kuwa matumizi ya viuatilifu yamekuwa na madhara makubwa kwa viumbe wanaosaidia uchavushaji wa mimea. Aidha, mabaki ya sumu hizi yanaweza kukaa kwenye udongo kwa zaidi ya miaka 30, jambo ambalo ni hatari sio tu kwa mazao ya chakula bali pia kwa afya za wakulima. Madhara ya matumizi kupita kiasiMatumizi yaliyopitiliza yamehusishwa na magonjwa ya saratani na matatizo ya mfumo wa mishipa ya fahamu, huku yakipunguza uwezo wa nchi kuuza mazao yao kwenye masoko ya kimataifa kutokana na viwango vya sumu kuzidi mipaka ya usalama wa chakula. Afisa wa FAO, Oxana Perminova anasema, "plastiki na kemikali za kilimo ni jambo linalotia wasiwasi duniani kote. Suala hilo limekuwa katika ajenda za nchi nyingi. Kwa upande wa Kenya, tunaamini kuwa ushirikiano huu ambao umeanzishwa hapa na ambao kwa kweli unafanya kazi ya na unawaleta wadau wote pamoja utakuwa na manufaa makubwa kwa kanda hii. Hivyo nchi nyingine jirani zinaweza kuangalia mifano na bidhaa zitakazozalishwa ndani ya ushirikiano huu na kuzitumia mahususi kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na kemikali na plastiki za kilimo na kuwalinda wakulima, hasa katika maeneo haya." Fahamu kuhusu madhara ya plastiki za vifungashioKuhusu plastiki za vifungashio vya pembejeo za kilimo, takwimu zinaonesha kuwa takriban tani 330,000 za plastiki hutumika kila mwaka kama vifungashio vya viuatilifu duniani kote. Inakadiriwa kuwa asilimia 35 ya plastiki hizi hazidhibitiwi ipasavyo, ambapo asilimia 10 huishia baharini na nyingine nyingi kubaki kwenye udongo. Grace Muchemi, ni Meneja Mkuu wa bodi ya kudhibiti bidhaa za viuatilifu, PCPB, nchini Kenya, anaeleza hatua zinazochukuliwa kuwa ni "tunapotazamia njia mbadala salama zaidi, tumekuwa tukipitia upya viuatilifu ili kuhakikisha viuatilifu vyenye hatari ndogo vinatumika ndani ya nchi. Pia, utoaji wa uelewa umefanyika ndani ya kaunti, na tunafanya kazi pamoja na mashirika mengine ya serikali na pia wadau wa maendeleo kutoa uelewa juu ya matumizi salama ya viuatilifu ili kuhakikisha chakula salama na pia kuwezesha biashara na nchi nyingine." Katika hatua muhimu ya kuleta usawa, mradi huu umehakikisha uwiano sawa wa washiriki wanaume na wanawake katika mafunzo yote yatakayotolewa.
Tweet URLSuala hilo la mchango wa manusura katika kuepusha mauaji kama hayo hayajirudii tena, nililimulika wakati wa mazungumzo yangu ya hivi karibuni na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga ambaye bila kumung'unya maneno alinieleza kuwa, “ wanamchango mkubwa sana kwa sababu kwanza wanapambana na hali ambayo katika hali ya kawaida ya ubinadamu ni ngumu. Chukulia mfano wetu sisi Rwanda walionusurika mauaji na waliotekeleza wanaishi pamoja kwa sababu Rwanda hakuna mgawanyiko wa kikabila wa kwamba kuna baadhi wanaishi mkoa fulani. Wanaishi pamoja katika vijiji hivyo, hivyo wanaenda shule hizo hizo wanaenda hospitali pamoja na wanaishi pamoja. Kwa mtu ambaye amepoteza familia yake nzima na anawajua wauaji walioua familia yake na anaendelea kuishi nao kijijini, ni hali ambayo kwa kweli katika akili ya kawaida unaweza usielewe lakini imetokea Rwanda.”Mwaka huu wa 2026 ni miaka 32 tangu kutokea kwa mauaji hayo ya kimbari. Hivyo Balozi Ngoga ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa Rwanda kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu uliotokea Rwanda (ICTR) akafafanua kwamba, “Baadhi ambao walikuwa ni wadogo wakati huo ambao sasa ni watu wazima, wanaandika hata vitabu kueleza nini kilitokea. Lakini wamekubali kuingia katika mchakato wa maridhiano, kujenga upya taifa la Rwanda."Akaongeza kuwa, "na kama ambavyo aliwahi kusema kiongozi wetu Rais Paul Kagame wakati fulani kwamba wao walionusurika ndio wanacho cha kutoa. Wao ndio wanaombwa watoe zaidi katika kuchangia juhudi za kulijenga upya taifa kwa sababu muuaji unaenda kumuomba nini. Tunashukuru kwamba wamekubaliana na hiyo, hali ambayo katika mazingira ya kawaida ya kibinadamu ni ngumu sana. Lakini kwa miaka yote hii tunakwenda.”
Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea. Feissal Kirwa anasimulia.
Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano katika Mashariki ya kati, kilimo endelevu kinachowakwamua wakimbizi na wenyeji Kakuma nchini Kenya, na mafunzo ya UNDP ya uchimbaji salama wa madini ya ujenzi nchini Tanzania.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuongeza muda wa sitisho la mapigano kati ya Marekani na Iran, ukisema hiyo ni hatua muhimu kuelekea kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), kwa kushirikiana na Tume ya Madini nchini Tanzania katikati mwa wiki iliyopita yaani Aprili 16 na 17 wamefanya warsha ya mafunzo mkoani Singida katikati mwa nchi. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ujuzi wa uchimbaji salama, unaozingatia sheria, na wenye faida kwa wanawake na vijana wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya ujenzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda ambayo ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani na tutasikia simulizi za wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi wa haraka na uwajibikaji wa kimataifa kufuatia madai ya usafirishaji haramu wa wanawake na wasichana yaliyoibuliwa katika “faili za Epstein.” Wamesema madai hayo yanaonyesha mtandao mpana wa unyonyaji wa kingono uliodumu kwa miaka mingi na kuhusisha watu mashuhuri.mashambulizi makali ya anga ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon, yakilenga maeneo karibu na ngome ya Hezbollah ya Bint Jbeil, huku mashambulizi ya roketi kuelekea kaskazini mwa Israel nayo yakiendelea na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano. Katika hatua nyingine, jeshi la Marekani limesema limezuia meli 10 kupita katika Mlango Bahari wa Hormuz, likitekeleza zuio lake lililotangazwa dhidi ya bandari za Iran. Wakati huo huo, mvutano wa kidiplomasia unaongezeka katika Umoja wa Mataifa, ambapo Baraza Kuu linakutana leo kujadili matumizi ya kura ya turufu kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati lililoungwa mkono na wengi lakini kuzuiwa na China na Urusi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la watoto waliouawa au kujeruhiwa nchini Ukraine, ambapo watoto 89 wameathirika mwezi Machi 2026 pekee. Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na ripoti ya uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 65 ikilinganishwa na mwezi Februari, hali inayoonesha madhara makubwa ya mashambulizi yanayoendelea kwa familia na jamii. Mashambulizi mabaya ya usiku wa tarehe 15 Aprili yalipiga miji kadhaa mikubwa, ikiwemo Dnipro, Kharkiv, Kyiv na Odesa, yakionesha hatari kubwa inayowakabili watoto.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “AWALI KUWA HERI SI AJABU” asMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Australia, mwanamke ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Australia. Waziri Mkuu alitangaza uteuzi wa Luteni Jenerali Susan Coyle mjini Canberra.
Bronisław Komorowski o koalicji PSL z Mateuszem Morawieckim, niepokojących ruchach prezydenta Trumpa, po którym "przyjdzie nam sprzątać", o wyborach na Węgrzech, Ziobrze i Romanowskim i inicjatywie z prezydentem Kwaśniewskim
Jaridani tunaangazia sitisho la mapigano nchini Iran, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na elimu kwa watoto walioathiriwa na vita nchini Sudan.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano kwa wiki mbili, wakati huu ambapo vita hiyo iliyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran ikiingia siku ya 40. Kwa upande wa Lebanon hali bado ni tete kwani Israel inaendelea na mashambulizi katika mji wa Beirut.Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano kwa wiki mbili, wakati huu ambapo vita hivyo vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran ikiingia siku ya 40. Kwa upande wa Lebanon hali bado ni tete kwani Israel inaendelea na mashambulizi katika mji mkuu Beirut ikidai kukabili wapiganaji wa Hezbollah wanaopinga kushambuliwa kwa Iran. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS.Kwa muda mrefu kambi ya wakimbizi ya Makpandu imeonekana kuwa kimbilio, lakini sasa imegeuka kuwa eneo la mashaka, na hofu. Bekia Mahadi Ali, mama wa watoto wanane aliyekimbia vita nchini Sudan akitarajia kupata hifadhi, sasa amejikuta akiishi kwa wasiwasi mkubwa baada ya ghasia kuibuka upya katika eneo hili. Furaha ya kupata usalama imetoweka, ulinzi umepungua, Bekia anahofia maisha yake na ya familia yake."Hakuna usalama kabisa hapa kambini na tunaogopa, nilikimbia na wanangu bila baba yao. Watoto hawa ni jukumu langu, tulikuja hapa kutafuta kimbilio lakini hawawezi kwenda shule, sina cha kufanya. Ninachoomba tuhamishwe kutoka kambi hii,”Wakimbizi katika kambi ya Makpandu wanaripoti kuwa watu wenye silaha huingia ndani ya kambi mara kwa mara, wakifyatua risasi hovyo, kuwatishia watu, na kupora au kuchoma moto mali za raia. Omar Ibrahim, ni mkimbizi mwingine kutoka Sudan, anafunguka."Wakati mwingine tunawachukua wanawake na watoto wetu kwenda kulala vichakani kwa sababu hakuna uhakika wa usalama ndani ya kambi. Hatuwezi hata kwenda shambani kulima. Tunaiomba Serikali na Umoja wa Mataifa waingilie kati, tulikimbia risasi nchini Sudan, lakini tumekutana na risasi zilezile tena hapa."Kufuatia shambulio la hivi karibuni lililosababisha kifo cha mkimbizi mmoja wa Sudan, kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kimefanya doria katika kambi hiyo ya Makpandu ili kutathmini hali ya usalama. Thomas Bazawi, ni Afisa wa Ulinzi, Mpito na Urejeshwaji wa UNMISS, anafafnua jukumu lao.“Jukumu letu ni kusaidia kurejesha imani kwa kushirikiana na jamii, mamlaka za mitaa, vikosi vya usalama na wengineo. Tunafanya kazi na wadau wote kuimarisha usalama ili watu waweze kujiamini na kuendeleza maisha yao tena.”Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa uwekezaji katika amani kupitia mpango wa Hatua kwa Ajili ya Kulinda Amani (A4P) ni muhimu kwa usalama wa wakimbizi wanaokimbia migogoro ya silaha.
Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. FAO imekarabati zaidi ya kilomita 300 za mifereji ya umwagiliaji ili kurejesha upatikanaji wa maji katika mashamba na kwa jamii, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha ustahimilivu wa wakazi wa maeneo haya kame nchini Somalia. Wakulima wanasema wameanza kuona matumaini mapya kwani mradi huu wa CLIMB umeboresha maisha yao. Nuur Mukhtar Mohamed ni mmoja wao, anasema uhaba wa maji katika Mto Jordan ulikuwa umeathiri vibaya shughuli za kilimo.Akifafanua anasema, “hapo awali tulikumbana na changamoto kubwa kwa sababu Mto Juba uko chini kuliko mashamba yetu, hali iliyofanya umwagiliaji kuwa mgumu sana. Hata hivyo, mfereji mpya ulioinuliwa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha yetu.”Kwa mujibu wa wakulima wengine, maboresho hayo yameleta unafuu mkubwa katika shughuli za kilimo na maisha ya kila siku. Akiwa shambani, Sadiyo Sheikh Ali, mkulima kutoka kijiji cha Bulo Bartire, anaeleza kwamba,“Kabla ya mfereji huu, maji yalikuwa haba sana kiasi cha kusababisha migogoro baina ya wakulima. Sasa hali imeimarika na tuna matumaini mapya. Tumeanza kupata utulivu wa akili.”Mbali na ukarabati wa mifereji, FAO pia inawapatia wakulima mbegu bora na kuwawezesha kuanzisha vikundi vya Akiba na Mikopo vya Kijiji (VSLA), vinavyosaidia kukuza kipato na kuimarisha mshikamano wa kijamii.Akizungumzia umuhimu wa vikundi hivyo, Yusuf Abdisalam Yusuf, Mkuu wa Kikundi cha Midinimo kutoka Goobweyn, amesema “tumeunda kikundi hiki ili kushirikiana na kusaidiana katika shughuli za kilimo na maisha kwa ujumla, bila kujali ukubwa wa msaada.”Mifereji iliyokarabatiwa sasa inaendelea kufufua matumaini na kuleta fursa mpya za kipato katika eneo la Jubaland. Hata hivyo, wakulima wanasisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongezewa pembejeo, msaada wa kifedha na mafunzo endelevu ili kuhakikisha jamii zinaendelea kustawi.
Tangu kuanza kwa vita huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran mnamo tarehe 28 Februari na kisha Iran kujibu mashambulizi, wasiwasi umekuwa ukiongezeka kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa nyingine. Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD linafuatilia kwa karibu hali inayoendelea na kutoa takwimu na uchambuzi ili kuzisaidia serikali na wadau wengine waweze kujipanga na kuratibu vyema mambo yao hususan yanayohusiana na usafiri wa baharini.Katikati ya vita hii inayoendelea Mashariki ya Kati kuna suala la mlango bahari wa Hormuz, hili ni eneo muhimu sana lililopo Iran ambako takriban robo ya mafuta yote duniani, meli zake hupita hapo. Bidhaa nyingine muhimu zinazopita hapo ni gesi asilia na mbolea. Ingawa mlango bahari wa Hormuz haujafungwa rasmi, lakini umewekewa vikwazo vikali, huku kukiwa na mashambulizi mengi ya Iran dhidi ya meli tangu vita vilipozuka siku 26 zilizopita. Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD Frida Youssef anaanza kwa kutueleza hali ilivyokuwa kabla ya vita.“Kabla tu ya mzozo, tunapoangalia wastani wa idadi ya meli kwa siku zilizokuwa zikipitia Hormuz, ilikuwa karibu meli 129, 130 na katika wiki mbili zilizopita, ilikuwa karibu meli mbili hadi saba kwa siku.”Kwa lugha nyingine upungufu ni takriban asilimia 95. Je ni maeneo gani yameathirika zaidi? “Usafirishaji wa mbolea unaathirika pamoja na bei ya uzalishaji, kwa mfano, mbolea za nitrojeni ambazo hutegemea sana gesi. Kwa hivyo, hii inabadilisha tena kuwa ni athari kwenye kilimo ambayo baadaye itaonekana kwenye kupanda kwa bei ya chakula.” UN News/Daniel DickinsonKufungwa kwa mlangobahari wa Hormuz kunaathiri biashara kwa kiwango cha kimataifa.Akiendea na tathmini yake Mkuu huyo wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa UNCTAD anasema hivi sasa bei za mafuta zimepanda.“Tumeona bei ya mafuta yanayotumika katika vyombo vya usafiri baharini ikiongezeka maradufu. Hii pia inaathiri gharama ya usafiri, si tu kwasababu bei ya mafuta imepanda bali pia bei, kwa mfano, ya bima. Malipo ya bima ya vita yameongezeka, katika baadhi ya maeneo imeongezeka mara nne.”UNCTAD inaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kwa serikali na wadau kwani vita hii inayoendelea inaathari kwa kila mtu lakini nchi zenye uchumi mdogo ndio zitakazo athirika zaidi kwani zinauwezo mdogo zaidi wa kuvumilia mshtuko huu wa kiuchumi na ndio zitakazohisi athari zake kwa nguvu zaidi. “Inaathiri usafiri, inaathiri nishati, inaathiri chakula na pia inaongeza gharama na upatikanaji ni mgumu. Kwa hivyo, haya yote kwa pamoja yanakuwa na athari kwenye uchumi wa umma katika nchi, pamoja na gharama za maisha kwa kaya.”
Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiingia wiki ya nne tangu uanze tarehe 28 mwezi uliopita wa Februari, Umoja wa Mataifa leo umeonya kuwa athari mbaya za kibinadamu na uchumi wa kimataifa zinaongezeka wakati mzozo huo ukivuruga kabisa njia muhimu za usambazaji wa bidhaa ndani ya Mashariki ya Kati na kwingineko duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi.Asante Assumpta. Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati sasa umevuka mipaka ya eneo hilo, ukiathiri pia Asia na Afrika, hasa katika biashara na usafirishaji.Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Miradi na Huduma, UNOPS inaonya kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kutokana na athari za kibinadamu na kiuchumi. Mkuu wa shirika hilo, Jorge Moreira da Silva, amesema kuvurugika kwa usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz kumesababisha mshtuko mkubwa wa kiuchumi duniani.Amesema “Nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika zina uwezekano mkubwa wa kubeba gharama kubwa zaidi hali inayotishia usalama wa chakula,” na kuongeza kuwa njaa duniani inaweza kuongezeka kwa makumi ya mamilioni ya watu.Pia amesema mgogoro huu unazidisha hali mbaya iliyopo katika nchi kama Sudan, Sudan Kusini, Afghanistan, Yemen, na Somalia, ambapo mifumo ya chakula tayari ni dhaifuAmeonya pia kuwa mashambulizi dhidi ya meli na kuvunjika kwa minyororo ya usambazaji kunazuia upatikanaji wa dawa na misaada, hasa Gaza, huku vita vikienea vinaweza pia kuhatarisha fedha zinazotumwa nyumbani kwa familia, hasa Asia Kusini.Nchini Lebanon, kwa mujibu wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, zaidi ya watu 1,000 wameuawa na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, wakiwemo wahudumu wa afya, wanahabari na wafanyakazi wa misaada.Watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Naibu Mkurugenzi wa UNICEF, Ted Chaiban, anasema “Watoto wanaouawa au kujeruhiwa ni sawa na darasa moja kila siku.”UNICEF inaonya pia juu ya athari kubwa za kisaikolojia kwa watoto na wahudumu wa misaada.Katika Ukanda wa Gaza, hali inazidi kuwa mbaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestna UNRWA, limesema mamia ya watu wamepata ulemavu wa kudumu huku huduma za afya na misaada zikizidi kuwa finyu.Wakati huo huo, hofu ya usalama wa nyuklia inaongezeka kufuatia mashambulizi karibu kweny vituo nyeti nchini Iran na Israel. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA, Rafael Grossi, ameonya kuwa: “Hakuna hatua ya kijeshi inayopaswa kuhatarisha usalama wa vituo vya nyuklia.”Ingawa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa a Afya Duniani WHO, tayari linaanza maandalizi ya dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa bila hatua za haraka za kupunguza mzozo, dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu na kiuchumi.
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Furaha ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Machi, wakazi wa kata ya Luchelele, jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania, wameeleza maana ya furaha katika maisha yao ya kila siku, ambapo kwa wengi, furaha haitokani na anasa, bali inajengwa na afya njema, upendo wa familia, na uwezo wa kuitunza familia hiyo kwa mahitaji ya msingi. Wakizungumza na Rashid Malekela wa Idhaa hii, wanawake wa eneo hilo wameeleza kuwa furaha kwao ni chanzo kikuu cha amani ya moyo. Rehema James amesema kuwa furaha yake kubwa ni kuamka salama, wakati Regina Emmanuel amegusia uhusiano wa mzazi na mtoto kama nguzo ya furaha yake, "Furaha yangu kuu inatokana na mama yangu kuwa hai na mwenye afya."Faida Anthony, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, amefafanua kuwa kwake furaha ni matokeo ya jitihada za kutafuta riziki akisema,"Furaha ni kutafuta fedha, mboga, na kuijali familia yangu."Mitandao ya kijamii na changamoto za furahaLicha ya umuhimu wa afya na familia, matumizi ya teknolojia yameanza kuathiri jinsi watu wanavyopata au kupoteza furaha katika ulimwengu wa sasa. Duch Sababu, ambaye ni Afisa Usafirishaji maarufu ‘bodaboda', amebainisha kuwa mitandao ya kijamii ina sura mbili; inaweza kuleta kicheko kupitia maudhui ya ucheshi au kuleta huzuni kulingana na kile mtu anachokiona, huku akitoa angalizo kwa watumiaji wa mitandao,"Furaha ni afya njema, lakini pia mitandao inaweza kuleta furaha kupitia vichekesho au huzuni kulingana na kile unachokiona."Wito wa Umoja wa MataifaMwaka huu, Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa furaha ya kweli kwa binadamu wote itafikiwa endapo kutakuwa na usawa, haki, na ulinzi wa mazingira kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Ili kufikia malengo hayo duniani, kuna uhitaji wa kuendelea kuimarisha huduma za kijamii zinazogusa maisha ya watu wa hali ya chini moja kwa moja.Kwa vijana, wameshauriwa kutumia muda wao kwenye mitandao ya kijamii kutafuta mambo yatakayowajenga kifikra na kuwapa furaha badala ya mambo yanayoweza kuwaharibia amani yao ya moyo.
Tune in for a virtual Town Hall held on March 16, 2026: Our Common Health, Our Commonwealth: Who Decides What's Safe? hosted by Kentucky Waterways Alliance, Kentucky Resources Council, Kentucky Conservation Committee, and Sierra Club Kentucky Chapter. Connecting Legislation, Pollution, and Our Health. Environmental health, public health, and civic health are deeply intertwined. The condition of our air, water, and land shapes the wellbeing of our communities and the strength of our democracy. Who shows up, who speaks, and who votes determines whether decisions reflect the public's best interests or the priorities of corporate lobbyists. Kentucky Waterways Alliance, Kentucky Resources Council, Kentucky Conservation Committee, and Sierra Club Kentucky Chapter hosted this discussion on how environmental decisions affect public health and how current proposed legislation would prioritize polluter profits over the health and safety of every day Kentuckians — making it nearly impossible for communities to hold corporations accountable when our most basic necessities are at risk. Additionally, the League of Women Voters of Kentucky shared findings from their report How Can They Do That?, which examines how legislation can advance through the process with limited public visibility. The Town Hall starts out with testimony from Calvert City, Kentucky resident Joshua Tabor sharing his family's experience with angiosarcoma, a rare cancer linked to environmental exposures, and why these environmental protections are deeply personal for many Kentucky families. Together, we examined how decisions made in Frankfort affect Kentucky's natural resources and communities, and what Kentuckians can do to shape a healthier future. Speakers include: KWA's Michael Washburn, Joshua Tabor, KRC's Audrey Ernstberger, KWA's Nick Hart, KCC's Lane Boldman, LWA's Jeanie Lindel, and SC's Julia Finch. Watch full recording: https://vimeo.com/1174496139 Connect with the organizers: Kentucky Waterways Alliance: https://www.kwalliance.org/ Kentucky Resources Council: https://kyrc.org/ Kentucky Conservation Committee: https://kyconservation.org/ Sierra Club Kentucky Chapter: https://www.sierraclub.org/kentucky
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaeleza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka, mathalan huko Lebanon watu 816,000 sawa na asilimia 14 ya watu wote wamekimbia makazi yao. Na huko Iran watu milioni 3.2 wanakadiriwa kukimbilia maeneo ya Kaskazini mwa taifa hilo na vijijini wakikimbia machafuko. Namba ya dharura ya msaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UHCHR inapokea zaidi ya simu 1,000 kwa siku za watu wakiomba msaada.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya kuwa njaa duniani inaweza kufikia viwango vya juu mwaka huu iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea na bei ya mafuta itabaki kuwa juu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Carl Skau amesema “Ongezeko la gharama za chakula na mafuta duniani zinaweza kuacha mamilioni ya familia zikiwa nje ya uwezo wa kununua vyakula, hasa katika nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa kama vile Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Kwa hakika, uchambuzi wetu unakadiria kwamba, kama mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea hadi mwezi Juni, watu zaidi ya milioni 45 wanaweza kuingizwa kwenye njaa kali kutokana na bei kuwa juu na hii itaweka rekodi ya juu ya njaa duniani kote. Na haya ni matarajio mabaya.".Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo moja ya matukio ya kando ya Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 ni Kushughulikia vikwazo vya haki ya kijinsia kupitia mfumo wa Mahakama ya Mtandao nchini Tanzania kwa lengo la kufanikisha haki kwa wanawake na wasichana. Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania anasema mashinani mfumo unatumia simu zisizo janja na akisema mobile app ni apu ya kwenye simu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia yaliyojiri katika mkutano wa CSW70, ambapo kandoni mwa mkutano huo Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza na Lucy Kabyemera, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Makazi nchini Tanzania aliyeongoza kikao hicho na kumpatia ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mabadiliko ya sera.Idadi ya watu waliokimbia makazi yao nchini Iran imeongezeka kwa kasi na kufikia takriban watu milioni 3.2 kutokana na mashambulizi makali yanayozidi kushika kasi nchini humo kutoka jeshi la Marekani na Israeli huku nayo Iran ikijibu mashambulizi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kupitia taarifa yake iliyotolewa leo jijini Geneva, Uswisi, limebainisha kuwa kaya kati ya 600,000 na milioni 1 zimepoteza makazi yao, huku wengi wakikimbia miji mikubwa kama Tehran kuelekea maeneo ya vijijini na mikoa ya kaskazini kutafuta usalama. “Hali hii imeleta hofu kubwa ya kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu kadiri uhasama unavyozidi kusambaa katika maeneo mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelezea kuhusu matumizi makubwa ya fedha kwenye silaha za kivita wakati huu ambapo dunia ina uhitaji mkubwa wa msaada wa chakula na maeneo kadhaa kuwa na hali mbaya ya chakula huku mgao wa chakula ukitolewa mara moja au mbili badala ya mara tatu sababu ya ufinyu wa ufadhili. Dkt Tedros amesema matumizi ya kijeshi duniani yamefikia $ trilioni 2.7 - katika mwaka mmoja. Na kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, kukomesha njaa duniani ifikapo mwaka wa 2030 kutahitaji $ bilioni 93 kila mwaka. “Hiyo ina maana kwamba tunatumia karibu mara 30 zaidi kila mwaka kuuana kuliko kuhakikisha kila mtu anakula.”Leo ni Siku ya Mlo shuleni. Mamilioni ya watoto duniani kote huenda shuleni kila siku bila kutia chochote tumboni. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP, zaidi ya watoto milioni 100 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati hukabiliwa na njaa kila siku. Hali hii huathiri uwezo wao wa kuzingatia masomo, kujifunza na kufaulu darasani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, WFP inaunga mkono serikali mbalimbali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapata milo shuleni ili wawe na afya njema na wawe tayari kujifunza.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
CSW70 yang'oa nanga ikisistiza haki, haki ya kisheria na hatua kwa wanawake na wasichanaKikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kimefungu pazia hii leo jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”. Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750. Leah Mushi amefuatilia ufunguzi huo na hii hapa taarifa yake.(TAARIFA YA LEAH MUSHI)Natts……Katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani …. huu ni ufunguzi wa Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 Mgeni rasmi ni Katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye ameeleza…. Nats.. (SG cut 1 play under 00:06 I am so pleased to be in a…. )furaha yake kuwa katika ukumbi uliojaa viongozi waliokataa kukubali ukosefu wa usawa kama jambo lisiloepukikaKatika hotuba yake Guterres amesema dunia bado inaongozwa zaidi na mfumo dume unaowapa wanaume nafasi kubwa ya mamlaka. (SG Cut 1 – Fiesal )“Tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume, na utamaduni unaotawaliwa na wanaume. Usawa wa kijinsia ni suala la mamlaka. Hakuna hatua hata moja mbele kwa haki za wanawake ambayo imewahi kutolewa. Bali imeshinda. Wameshinda vizazi vya wanawake na wasichana, watetezi na wanaharakati, viongozi wa jamii na watafuta haki. Umeshinda wewe na kabla ya kitu chochote napenda kusema Asante.”Amesema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa katika jitihada za kufikia usawa wa kijinsia katika taasisi nyingi duniani. Hata hivyo, ndani ya UN kumekuwa na maendeleo muhimu katika kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wakati alipoanza uongozi wake, alijiwekea lengo la kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume katika ngazi za juu za uongozi wa Umoja wa Mataifa. Leo, amesema lengo hilo limefikiwa.(SG cut2 – Fiesal )“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa, wanawake sasa wanaunda nusu kamili ya nguvu kazi ya Umoja wa Mataifa katika vitengo vya kitaaluma na vya juu zaidi. Na kwa mara ya kwanza, tulifikia usawa katika uongozi mkuu. Tumefanya hivyo ikiwa ni miaka miwili kabla ya ratiba - lakini pia natambua imekuwa ni miaka 80 imechelewa.”Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa António Guterres amesisitiza kuwa kufikia usawa wa kijinsia si suala la haki kwa wanawake pekee, bali ni hatua muhimu kwa maendeleo ya dunia nzima. Amesema jamii ambazo wanawake wanapata haki na fursa sawa huwa na maendeleo ya haraka zaidi, uchumi imara na taasisi zenye uwajibikaji zaidi, akisisitiza kuwa kuimarisha usawa wa kijinsia ni msingi muhimu wa kufikia maendeleo endelevu duniani.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanawake wanapata haki na fursa sawa katika jamii duniani.Ametaja maeneo matano muhimu ya kuharakisha haki na usawa kwa wanawake ambayo ni kuhakikisha haki sawa za kiuchumi kwa wanawake, kuimarisha uwakilishi wao katika maamuzi ya kisiasa, kupanua upatikanaji wa elimu na fursa za kazi, kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, pamoja na kulinda haki za wanawake katika dunia ya kidijitali.Kwa upande wake mwenyekiti wa Kikao hicho cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 Maritza Chan Valverde amezungumzia maudhui ya mwaka huu ambayo ni “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote nakusema kila mtu anajukumu la kufanya (Maritza cut )“Ondo vikwazo na uhakikishe kwamba haki inakuwa ukweli halisi kwa…
UNICEF: Mradi wa Elimu Kwa Waliokosa warejesha matumaini kwa mtoto wa kikeNchini Tanzania Mpango wa Elimu Kwa Waliokosa au MEMKWA umemwezesha msichana mmoja kuweza kupata haki yake ya msingi ya elimu na kisha kuwa na matumiani ya kutimiza ndoto yake ya kuwa nesi au muuguzi. Simulizi ya Assumpta Massoi inafafanua kisa hicho kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Nats.. 00'00 – 00'14” (Kwa majina naitwa…. Wanaenda shule)Tupo wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania Sanita huyo alishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule.(Sauti ya Sanita)Amerejea shuleni kupitia mradi wa MEMKWA uliotambua kuwa zaidi ya watoto milioni 2 wenye umri wa kuwa shule ya msingi nchini Tanzania hawako shuleni hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau UNICEF na serikali ya Qatar wakafanikisha MEMKWA.Tangu mwaka 2022 zaidi ya watoto elfu 98 katika mikoa 3 ya Tanzania ikiwemo Kigoma, wamenufaika na MEMKWA.Nats…(Darasani) 0'30-0'36” (Shikamoo mwalimu…….la mstatili)Sasa tumo darasani na Sanita ni miongoni mwa wanafunzi. Rashid, mwalimu wa Sanita anaelezea.(Sauti ya Rashid- Mwalimu wa Sanita)Sanita anakwenda ubaoni kujibu swali. Mwalimu anauliza..Nats.. 1'00” – 1'03” (Ameweza, haya tumpigie makofi….fx makofi)Sanita anafunguka..(Sauti ya Sanita)Kitendo cha Sanita kupata haki ya elimu kinamwezesha hata Rhoedesia ambaye ni mama mzazi wa Sanita kuwaza mustakabali wa binti yake.(Sauti ya Rhoedesia) 1'11” -1'20” (NInavyomuona mwanangu anaenda…. ili apate kazi)Mwalimu Rashid anatamatisha na tathmini ya mradi wa MEMKWA na ombi mahsusi.(Sauti ya Mwalimu Rashid)
Ikiwa hujakuwa ukifuatilia vita vya Marekani pamoja na Israeli dhidi ya Iran, huwenda usijue matukio ya kipekee ambayo yametokea kwenye vita hivi. Kwa mara ya kwanza, akili unde ambayo tunaitumia kila kuchao, ilitumika kufanya mashambulizi dhidi ya Iran. Tazama video hii ujue mengi
Kwa wanafunzi wa kimataifa wanaosomea nchini Australia, kupata huduma ya afya mara nyingi huonekana kama swala ghali sana... au la kutatanisha sana kuweza kuipitia.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimsikia Barbara Batte Guevara, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Havana nchini Cuba. Kwa kushirikiana na Tanzania chuo hicho ambacho mwezi uliopita kimetimiza miaka 298 tangu kuanzishwa kwake, hivi karibuni kimetoa fursa kwa Wacuba kujifunza lugha ya Kiswahili.Anold Kayanda wa Idhaa hii amemtembelea Profesa Barbara Batte katika jiji la Havana nchini Cuba ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kama zifuatazo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Kimataifa wa Akili Mnemba au AI wenye thamani ya dola bilioni 3, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inawanufaisha watu wote duniani, badala ya kuwa mali ya mataifa machache au kampuni chache zenye nguvu. Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa kujadili Athari za AI huko New Delhi nchini India, Guterres amesema mustakabali wa AI unapaswa kujengwa kwa ushirikiano wa kimataifa”.Mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi ambayo inakalia kimabavu yanatia hofu ya uwezekano wa utokomezaji wa kabila, imesema Ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR), ya kuanzia Novemba 1 2024 hadi Desemba 31 2025. Ripoti inasema mashambulizi ya Israeli yameweka mazingira ambamo kwamo wapalestina kama kundi watashindwa kuendelea kuishi Gaza huku Ajith Sunghay, Mkuu wa Ofisi ya OHCHR Palestina akisema, “ripoti inachambua mwenendo wa mapigano ya jeshi la Israeli, linaloendelea kuua idadi kubwa ya raia, kusababisha njaa, kuwahamisha takribani wakazi wote wa Gaza, tena zaidi ya mara moja — na kuharibu miundombinu iliyosalia ya kiraia ya Gaza.”wanamgambo wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan walitekeleza kampeni iliyoratibiwa ya uharibifu dhidi ya jamii zisizo za kiarabu ndani ya mji wa El-Fasher na viunga vyake, kampeni yenye viashiria vya mauaji ya kimbari, imeeleza ripoti mpya iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan. Ripoti imetaja vitendo hivyo ni pamoja na kuua wanachama wa kundi la kikabila linalolindwa; kusababisha madhara makubwa ya kimwili na kiakili; ambavyo ni vipengele muhimu vya kosa la mauaji ya kimbari chini ya sheria za kimataifa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunawasikiliza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Havana wanaojifunza lughaya Kiswahili. Tuanze na Yibran Nunez Batte.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Leo ni siku ya redio duniani ambayo msingi wake unatokana na kuanzishwa kwa redio ya Umoja wa Mataifa tarehe 13 Februari mwaka 1946 jijini New York, Marekani. Kwa mantiki hiyo ikiwa mwaka huu redio hiyo ya Umoja wa Mataifa inatimiza miaka 80 tumeangazia mchango wa vipingi vyake vilivyokuwa vinarushwa na redio zingine ikiwemo iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) nchini Tanzania wakati huo. Assumpta Massoi amemulika suala hilo.
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Redio Duniani likitupeleka nchini Tanzania kusikia jinsi ambavyo redio inavyochochea maendeleo ya kijamii, nchini Uganda kumsikia mkimbizi kutoka DRC, na katika ukanda wa Gaza ambako redio inaunganisha tena jamii ndani ya vifusi.Leo ni siku ya redio duniani ambayo msingi wake unatokana na kuanzishwa kwa redio ya Umoja wa Mataifa tarehe 13 Februari mwaka 1946 jijini New York, Marekani. Kwa mantiki hiyo ikiwa mwaka huu redio hiyo ya Umoja wa Mataifa inatimiza miaka 80 tumeangazia mchango wa vipingi vyake vilivyokuwa vinarushwa na redio zingine ikiwemo iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) nchini Tanzania wakati huo. Assumpta Massoi amemulika suala hilo.Katika maeneo ya migogoro, duniani redio huwa nguzo ya utulivu na wakati mwingine daraja la kuokoa maisha. Na ndivyo ilivyokuwa kwa mkimbizi Bahati Yohane kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwani kwake, redio haikuwa tu combo cha habari ilikuwa dira ya kuokoa maisha yake.Kabla ya vita vya sasa kuanza katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina lilalokaliwa kimabavu na Israel, Redio ilikuwa chombo muhimu kwa umma na kwa hakika umuhimu wake haujakoma isipokuwa huduma ya matangazo ya redio ndio iliyokuwa imekoma kutokana na vituo vya redio kusambaratishwa kwa makombora, lakini sasa juhudi zinafanyika kuirejesha huduma hiyo muhimu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Kwa habari na melezo zaidi, tembelea tovuti ya sbs.com.au.
Kwa wengi katika kusini-mashariki mwa Australia, siku baada ya Siku ya Australia ilileta hali ya joto kali na rekodi za viwango vya joto. Katika Mildura, jimboni Victoria, kaskazini-magharibi zaidi, joto lilifikia nyuzi 48.6. Na wakati maeneo ya pwani yalifurahia kupungua kwa joto, maeneo ya bara yalilazimika kukabiliana na joto kali lililodumu kwa wiki moja. Wataalamu wanasema aina hizi za matukio zitaendelea kuongezeka kwa wakati kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi - lakini wakati kumejaa habari nyingi kuhusu jinsi hiyo inaathiri vituo vya mijini, maeneo ya vijijini nchini Australia hayajapata umakini sawa. SBS ilitembelea Mildura kuona jinsi eneo hilo lilivyohisi joto, na wanavyofanya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi ya eneo hilo.
Kwa maelezo ama habari zaidi elekea kwenye tovuti yetu ya sbs.com.au/swahili.
Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, AI katika elimu na juhudi za kuhakikisha wananchi wamepata huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi nchini Niger.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hii leo historia na dharura vilikutana chini ya paa moja. Ni miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC lifanye kikao chake cha kwanza tarehe 23 Januari 1946 na linaadhimisha hatua hii muhimu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni wa maamuzi kwa mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa.Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.
Katika wakati wa mgogoro wa makazi na gharama za maisha, serikali ya Victoria iko katika mchakato wa kubomoa minara yote 44 ya makazi ya umma ya Melbourne. Licha ya upinzani mkubwa na uchunguzi wa bunge unaotaka kusitishwa kwa haraka kwa kazi hizo, serikali ya Victoria inaendelea na mipango hiyo. Kuhama nyumba huchukuliwa kuwa moja ya matukio yenye msongo mkubwa zaidi katika maisha ya mtu. Kwa hivyo, mwaka 2023, wakati maelfu ya wakaazi wa Victoria walipokea taarifa kwamba nyumba zao zitabomolewa wakati fulani kati ya mwaka huo na 2051, msongo ulikuwa dhahiri. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au kwa taarifa ama maelezo zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumsikia kijana Baraka Ayubu ambaye amekuwa kielelezo cha jinsi teknolojia inavyoweza kuleta mageuzi katika mifumo ya ujifunzaji na ustawi wa wanafunzi.Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa uchunguzi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaohusishwa na vita kati ya Hamas na Israel huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel utaendelea, licha ya kuanzishwa kwa Bodi ya Amani ya Gaza ambayo imezinduliwa hii leo na Rais wa Marekani Donald Trump.Tuelekee nchini Kenya ambako zaidi ya watu milioni mbili wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa uhakika wa kupata chakula kufuatia msimu wa mvua fupi za mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2025 kuwa mkavu zaidi kuwahi kurekodiwa. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, uhaba wa maji unalazimu familia kutegemea vyanzo visivyo salama, jambo linaloongeza hatari ya kipindupindu, homa ya matumbo, na magonjwa ya kuhara.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani, WHO, la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na la Makazi, UN-Habitat, kwa pamoja wamezindua mwongozo mpya unaozitaka serikali na viongozi wa miji kuweka kipaumbele kwa watoto katika upangaji wa miji ili kurejesha maeneo ya michezo yanayozidi kutoweka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya "SIKU ZA MUAMBO" katika muktadha wa uchumi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji, ripoti inayomulika kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, na mradi unaolenga kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.Kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbiji kutokana na mvua zinazoendelea, serikali ya nchi hiyo ya kusinimashariki mwa Afrika imetangaza kuwa hadi kufikia sasa imerekodi vifo vya watu 120 na maelfu ya nyumba zimeharibiwa huku kiwango kikubwa cha fecha kikihitajika.Katika muktadha wa kupungua kwa muda mrefu kwa maji ya chini ya ardhi, matumizi kupita kiasi ya rasilimali za maji, uharibifu wa ardhi na udongo, ukataji miti, pamoja na uchafuzi wa mazingira, Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa UNU leo kimetoa ripoti ikitangaza kuingia kwa “enzi ya kufilisika kwa maji duniani” na kutoa wito kwa viongozi wa dunia kuendana na uhalisia huu mpya kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Kwa muongo mmoja kuanzia mwaka wa 2016 hadi mwaka wa 2025, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa ushirikiano na serikali ya Canada limechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan likilenga kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika kushinda changamoto za muda mrefu za uzalishaji, masoko na mnepo wa maisha. Sheilah Jepngetich na taaarifa zaidi.
Mwanahabari Jason Nyakundi anatujuza yanayoendelea Afrika. Kwa habari ama maelezo zaidi tembelea tovuti yetu sbs.com.au/swahili.
Tangu kuanza kwa kiangazi, watu 33 wamepoteza maisha yao kutokana na kuzama maji huko Australia. Kwa kuwa kuzama maji kunatokea zaidi tangu Janga la COVID-19, Baraza la Usalama wa Maji la Australia limetoa Mkakati Mpya wa Usalama wa Maji wa Australia 2030, ambao unalenga kuimarisha juhudi za kitaifa kupunguza vifo vya kuzama maji kwa asilimia 50 kufikia mwisho wa muongo huu.