Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathir…
Juhudi za serikali za Afrika kuja na mikakati ya kutoa huduma za afya kwa raia kupitia mipango ya bima ya afya ya kitaifa zimekabiliwa na changamoto za utekelezaji,ufisadi na mifumo isiyo thabiti. Watalaam wa afya sasa wanapendekeza mipango hiyo ya afya iwe kwenye mipango ya kitaifa ya kila mwaka,ikiwa na mwongozi kamili kuhusu huduma gani serikali itatoa kwa raia na kwa kiasi gani. Aidha watalaam wanashauri mipango hiyo iwe inaendana na mahitaji ya kila jamii kwa kuwa serikali nyingi kwa sasa hazina uwezo wa kutoa huduma zote kwa raia Isitoshe,mifumo inyopunguza uvujaji wa raslimali za umma ni muhimu
Wanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekundu nchini ,KRC,katika kujaribu kukabili hali hiyo ,zinatekeleza mpango wa kujaribu kurejesha mawasiliano na uhusiano wa familia za wakimbizi. Kwa kuwatafuta namna ambao wakimbizi hao wanaweza kuwasiliana kupitia ujumbe wa kuandikiwa au kwa njia ya simu,mashirika hayo wanasema wamefanikiwa kuwarejeshea tabasamu wachache wenye bahati na wanaendelea kuwasaka wanafamilia zaidi kila mwaka. Matunda ya mpango huo yameonekana miongoni mwa wakimbizi wanaozungumza na jamaa zao na pia kwa wahudumu wa kujitolea wanaotangamana karibu kila siku na wakimbizi hao kwenye kambi.
Hivi karibuni watalaam wa afya pamoja kwa ushirikiano na shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini. Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi hudhani kuwa Pneumonia husababishwa na baridi kuingia kwenye kifua lakini watalaam wanasema chanzo cha Pneumonia ni vimelea kushambulia mapafu na mfumo wa kupumulia Watalaam wa afya wanasema ndani ya wiki moja, mtu aliye na Pneumonia hugundulika kwa kuwa anapata ugumu wa kupumua au hata kukosa hewa.
Hali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla. Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu. Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu. Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo kwa wakati mwingi huwekeza kwenye miradi inayozingatia matakwa yao. Aidha ili kuhakikisha kuwa huduma za afya kama uchomaji chanjo zinawafikia wanajamii wote ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kuimarisha huduma za wahudumu wa afya wa jamii ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawafikia watoto walengwa baadala ya wazazi kupata ugumu wa kwenda kusaka huduma hizo.
H pylori isipotibiwa inaweza kugeuka kuwa saratani ya tumbo ,watalaam wameonya Katika makala haya,tunaangazia sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kupata maambukizo ya H pylori na matibabu yake. Matibabu yake kwa mujibu wa daktari Alex Mungala anayehudumu jijini Nairobi yanaweza kukabiliwa na usugu wa vimelea ,ni ghali na si rahisi kupatikana katika vituo vya afya vya daraja la kwanza.
Utafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na kupoteza kumbu kumbu Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya. Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu. Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku. Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi. Wapo waliokuwa na wanatumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu na sasa wameachana nazo. Aidha wengine wameeleza matembezi kuwaondolea maumivu ya viungo na pia kupata marafiki wazuri.
Kukaa kwa zaidi ya saa sita mfululizi kila siku inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya uti wa mgongo,kisukari,shinikizo la damu na kifo cha mapema
Katika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema polisi wenye changamoto za afya ya akili hawatafukuzwa kazi bali watapewa matibabu stahiki Kumeshuhudiwa hivi karibuni visa vya polisi kutumia silaha zao visivyo na utendakazi wao kukosolewa na raia pamoja na wanaharakati wa haki
Hivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila kushinikizwa .
Takwimu zinaonesha watu wengi kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kuishi bila kufanya mazoezi na kula vibaya Sera hii itatoa mwongozo wa taasisi za serikali na binafsi kuweka mikakati ya kuruhusu mazoezi ya kila mara wakati wa kazi au nje ya kazi
Kila siku mwili wako hukuzungumzia na ni jukumu lako kusoma mwili wako na kuelewa unasema nini au unakuonya kuhusu nini Baadhi ya matatizo ambayo unaweza kujiepusha nayo ni matatizo ya afya ya akili ,kufeli viungo muhimu au mifumo yako ya afya. Na ili kuhakikisha mwili wako unazungumza na kutoa taarifa iliyo sahihi kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kwa mfano kupata muda wa kutosha kulala,kupata lishe bora na kufanya mazoezi
Matatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid Disease Awareness Kenya Foundation ,TDAK, Sarah Katulle anaelezea umuhimu wa wagonjwa kuwa kwenye kundi ambapo wanaweza kushirikishana kuhusu mbinu mbadala ya kuishi na matatizo hayo kando na matibabu. Kundi hilo linawasaidia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa ,mahabara maalum na dawa sahihi. Aidha TDAK ili kuwasaidia wagonjwa hao kuishi maisha ya kawaida wakiwa kazini ,inawaandikia barua ambazo zinawasilishwa kwa maajiri kutambua hali halisi ya wagonjwa na mahitaji yao.
Misri ipo kwenye njia panda kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho la pili sheria zake za kutoza ushuru bidhaa za tumbaku iwapo lengo ni kuleta mapato kwa serikali ,kuwafaidi wazalishaji au kwa maslahi ya afya ya wengi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani,WHO, asilimia 20-25% ya watu wazima nchini Misri huvuta sigara.
Kabla mgonjwa yeyote kuanzishwa kwenye matibabu, awe ana tatizo la tezi koo kuzalisha homoni kupitiliza au kushindwa kuzalisha, ni sharti vipimo maalum kufanyika Kipimo cha kwanzo ni inaangazia homoni tofauti inayozalishwa na tezi koo na hii mtu yeyote anaweza kufanya katika wakati wa kufanya vipimo kujua hali yake ya afya ,hapa mtu si lazima awe ameonesha dalili za tezi koo kuwa na tatizo.Kipimo cha pili ambacho ni muhimu huzingatia zaidi viwango vya homoni tatu muhimu zinazozalishwa na tezi koo ambayo ni (TSH), thyroxine (T4), na triiodothyronine (T3) .Matokeo yataamua ni mpango gani wa matibabu mgonjwa atapewa dawa,kudhibiti homoni au kuzalisha homoni mbadala tezi koo inaposhindza kazi yake.Kando na dawa kama mpango wa matibabu ,wagonjwa wenye uvimbe wanaweza kushauriwa kufanya upasuaji kuondoa tezi koo ,sehemu yake au yote.Kuna pia mpango wa kutumia mianzi na madini ya Iodine maarufu kama Radioiodine mpango ambao ni sharti kufanywa kwa ueledi mkubwa na kwenye vituo vya afya vilivyo na vifaa vya viwango vya juu.
Matatizo ya tezi ya koo ,kwa kawaida yananaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland). Homoni inapokuwa kidogo hali ambayo inafahamika kama Hypothyroidism, hii inaashiria kwamba tezi inafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo .Mtu aliye na hali hii ,anakuwa hana nguvu ,nywele kudondoka na hata mzunguko wake wa mwezi wa damu huvurugika.Madini hayo yanapokuwa mengi inamanisha tezi inafanya kazi kupitliza kuzalisha homoni iliyozidi kwenye mzunguko wa damu na kuchanganyika na vitu vingene ambavyo husababisha kutengeneza kama sumu fulani ambayo huchoma mafuta yaliyo kwenye hifadhi mwilini, mishipa ya fahamu huathirika kiasi kidogo.Mtu ambaye ameathiriwa na aina hii ya pili, huanza kupunga uzito na umbo la mwili taratibu baadaye madhara yanapoongezeka mtu anaanza kupoteza kumbukumbu, anakuwa na hasira, anakula sana, nywele zinanyonyoka mpaka anapata upara, magoti yanakosa nguvu na mtu anashindwa kutembea.Moyo kwenda mbio , macho yanavimba sehemu ya juu kope na jicho lenyewe linatoka nje kama vile linadondoka.Ni vizuri kuwahi hosipitali ili kupata vipimo ambavyo vinaangazia utendakazi wa tezi ,kwa jina la kiingereza ,Thyroid Function ,ili kubaini iwapo una tatizo la kwanzo au la pili.Na si lazima mtu kuwa na uvimbe ili kubainika kuwa ana tatizo la tezi koo. Kuna wale ambao uvimbe unakuwa upande wa ndani ,wale wenye uvimbe unaonokena nje ya koo ya wale ambao hawana uvimbe wowote.
Misri imepambana kwa karibu miaka 100 kabla kupata cheti cha WHO cha kufaulu kutokomeza Malaria Oktoba 2024 Katika mkakati ambao umetumia Misri kuangamiza Malaria ni udhibiti wa Mbu,ambapo serikali iliwekeza kwenye kupiga dawa kwenye maeneo yanayoweza kuwa makazi ya mbu .Ufuatiliaji na ubainishaji wa haraka umechangia pia pakubwa kuushinda ugonjwa wa Malaria ,mkakati ambao pia jamii ilibidi kushirikishwa.Kitengo cha afya ya umma kimekuwa kikifanya hamasisho kwa wanajamii kukumbatia mbinu za kuzuia mbu kwa kutumia vyandarua na pia kupata matibabu ya haraka mtu anapoonesha dalili za Malaria.
Ongezeko la magonjwa ya milipuko linaibua swala la kwa nini watalaam wa wanyama hawahusishwi kikamilifu katika mifumo ya afya ya binadaam Mpango wa one Health Approach unaonadiwa kwa sasa kwa mataifa ,unahimiza kuipa kipau mbele afya ya wanyama ,ili kuchangia siha njema ,usalama wa chakula na maendeleo endelevu .
Kumekuwa na malalamishi ya maziwa yaliyo kwenye soko kusababisha madhara ya kiafya Watalaam wa afya ,bodi inayosimamia bidhaa za maziwa nchini Kenya na wanavetirinari wanasema matatizo hayo huenda yanatokana na uzembe wakati wa uchakataji maziwa ,uhifadhi na pia wafanyabiashara wenye pupa.
Baadhi ya changamoto zinazokumba sekta ya tiba asilia ni mwitiko na ukosefu wa sheria za kuisimamia katika nchi mbali mbali
Waganga wa tiba asilia wana mchango katika ulimwengu wa uzalishaji dawa
Kuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa kupata maji salama kwa matumizi ya nyumbani ,hospitali na hata mashamba Uhaba wa maji unaorodheshwa kuwa sababu kubwa ya watu kukosa chakula, kujikimu katika nchi zinazoshuhudia migogoro.Katika nchi kama Sudan na DRC kuna ripoti za hospitali ,kambi za wakimbizi kukosa moja hivyo mashirika ya kimsaada yanapata changamoto kuwahudumia wakimbizi
Ukosefu wa lishe bora huathiri afya na elimu nchini Kenya Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la linalowahudumia Watoto (UNICEF) imeonesha kuwa takriban watoto milioni mbili nchini Kenya wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na utapiamlo. Mipango ya lishe bora shuleni eneo la Nyanza na maghari mwa Kenya umeonekana kuwa suluhu huku wanafunzi wakipata vyakula vilivyo na virutubishi bora vinavyosaidia kuboresha kinga ya mwili,hivyo kuimarisha afya .
WHO imetaja ukosefu wa huduma za kuokoa maisha wakati wa kujifungua huchangia vifo vingi vya wanawake waja wazito Huduma hizo za wanawake hata hivyo zina bei kubwa
Serikali za Afrika zitalazimika kuchangia ufadhili wa mipango ya kupambana na Malaria kufidia pengo kubwa la ufadhili Muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria ,Africa Leaders Malaria Alliance unasema Afrika inahitaji dola bilioni 5 nukta nane mwaka huu wa kifedha hadi 2026.Hali hii pia imechangiwa na Marekani kukata ufadhili wa misaada kwa nchi za kigeni
Mamia ya wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa kilomita chache na msitu wa Boni ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi na kujificha .
Katika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
Guinea itakuwa ni taifa la nane la Afrika kuthibitishwa kuangamiza ugonjwa wa malale Guinea imekuwa ilishiriki katika majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa malale ambayo yalifanyiwa utafiti mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoTimu ya madaktari kutoka DRC na Guinea walishirikishwa kwenye majaribio hayo na kwenye makala haya tumezungumza na Dkt Chirac Bulanga kutoka DRC
DRC imeripoti maambukizi ya Ukoma mwisho wa mwaka jana na pia mwaka huu Ukoma ni ugonjwa unaoathiri sana ngozi na unaweza kuharibu baadhi ya viungo kama vile mikono ,miguu na hufanya mtu kutengwa na jamii
Kumeendelea kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya watu wanaougua mafua au magonjwa yanayoathiri mfumu wa kupumua mwezi Januari ambao una joto jingi na vumbi. Hii inajiri wakati China ikiwa imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Human metapneumovirus ,HPMV unaofanana na COVID 19 .Daktari Juma Maleve kutoka Hospitali ya rufaa ya Mombasa ,Pwani ya Kenya anafafanua.
Kwa kitaalam mtindio wa ubongo unaitwa Cerebral Palsy kwa kifupi CP..ugonjwa huu unatokana na jereha kwenye ubongo ambao huwa linafanya mtoto kushindwa kudhibiti misuli ya mwili wake hali inayoweza kusababisha viungo vya mtoto kulegea au kukamaa muda wote. Mtoto anaweza kupata majeraha kwenye ubongo akiwa bado yuko tumboni, wakati wa kuzaliwa au baadae maishani.CP husababisha ulemavu wa kudumu katika maisha yote ya mtoto.
Vasectomy ni njia ya kupanga uzazi ambayo inahusisha upasuaji wa mshipa unaopitisha mbegu za kiume, ili mme asiweze kumpachika mke mimba. Ni njia ya upangaji uzazi ya milele.Na pengine unajiuliza hili linafanyiikaje na ina athari gani kwenyen afya ya mwanaume ?Sikiliza makala haya
Kwenye awamu yetu ya Kwanza tuliangazia njia za asilia walizokuwa wanatumia nyanya zetu kabla ya sayansi kuingia.Tukataja njia ya Kalenda,mipira ya kondomu na kumwaga mbegu za kiume nje ya njia ya uzazi almaarufu Withdrawal.Hivyo basi kwenye sehemu hii ya pili tutaangazia njia za homoni na zisizo za homoni na ambazo asilimia kubwa ya wanawake wanatumia.Kama vile vidonge, vipandikizi ,sindano, na IUD.
Makala haya yanaangazia upangaji kupanga uzazi, na jinsi linavyohusiana na afya ya mwanamke. Kupanga uzazi ni sehemu muhimu ya afya, kwani husaidia wanawake kudhibiti idadi ya watoto wanapokuwa nayo, na pia ina athari kubwa katika afya yao ya kimwili na kihisia.
Idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya katika umri mdogo imeongezeka
Katika makala haya, tutazungumza na watu muhimu kama vile mgonjwa wa UKIMWI, daktari, na mkunga anayeelimisha kuhusu jinsi ya kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wanapozaliwa. Pamoja, tutafahamu changamoto, mafanikio na hatua zinazochukuliwa katika vita hivi.
Umoja wa mataifa umeorodhesha mwaka 2024 kama mwaka hatari zaidi kwa wafanyikazi wa mashirika ya kimsaada Katika takwimu za UN ,wafanyakazi zaidi ya 200 wamewauwa katika mzoz wa Gaza na wengine zaidi ya 20 katika mzozo wa Sudan
Idadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.
Makala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari nyepesi.Ni safari yenye changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.
Kumekuwa na mikakati maksudi katika nchi za Afrika kuwekeza katika utafiti kuhusu nyoka na matibabu ya simu yake Baadhi ya mikakati hiyo ni utafiti wa kuwa na aina moja ya dawa ambayo inaweza kutumika katika nchi za Afrika Mashariki vile vile kuelimisha jamii kuhusu huduma za kwanza sahihi kuwasaidia wagonjwa na namna ya kuzuia madhara zaidi kutokana na sumu ya nyoka.
Kungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC mara nyingi hubidi kuhudumu katika maeneo yenye mizozo kutoa huduma za dharura ,msaada wa kibinadaam ikiwemo afya Ili kukabiliana na changamoto za kuafikia malengo yake ya kutoa huduma za afya za dharura katika uwanja wa vita ,maeneo yenye majanga ,imebidi kufumbua mbinu ya kuwa na hospitali za muda ambazo zinajengwa kutumia hema na zinaweza kufanya kazi ndani ya saa 96ICRC inaendelea na mafunzo ya kuwaandaa wahudumu wa afya wanaohudumu katika mazingira hatarishi ,ili wapate kuhudumu ipasavyoMafunzo hayo yanatolewa kwenye hospitali halisi ambazo hutumika katika maeneo ya mizozo ,ambapo wahudumu hao hutakiwa kushughulikia mazingira tofauti ya dharuraMafunzo hayo yamefanyika nchini Kenya mara mbili ambapo wahudumu hao kutoka maeneo tofauti wanawekwa kwenye makundi na kutakiwa kutangamana na kushughulikia dharura tofauti kabla kuanza kutumwa kwenye maeneo ya mizozo
Mashirika ya nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali za kaunti ,yamezindua mfumo mpya na wa kisasa wa vyoo bunifu visivyotumia maji wala kuunganishwa na mabomba ya maji taka Hatua Ambayo imeonekana kupunguza msambao wa magonjwa kama vile kipindupindu.
Raia wengi bado hawawezi kufurahia haki zao za afya ya uzazi kutokana na ukosefu wa ufahamu Haki hizo ni pamoja na haki ya kuwa mzazi au la,kupata habari kuhusu afya ya uzazi ,kupata huduma bora za uzazi ,kushiriki mapenzi kwa njia stahiki na kuhudumiwa katika vituo vya afya kwa heshima
Ripoti nyingi zinaonesha wanawake pamoja na wanaume wanakabiliwa na changamoto za uzazi Wanandoa nyingi wanalazimika kukaa miaka mingi kabla kupata watoto ,kitu ambacho bado kinazingatiwa na jamii za Afrika kuwa ukamilifu katika kila ndoa au familia.Daktari bingwa wa uzazi dkt Dennis Miskella anaeleza juhudi za kutafuta mtoto zinastahili kuwa ushirikiano kati ya mke na mumeweBaadhi ya sababu zinazohusishwa na hali hii ni kushiriki tendo la ndoa visivyo ,athari za baadhi ya mbinu za kupanga uzazi ,uvutaji sigara na pia unene wa kupitiliza
Mashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV
Mikakati ambayo WHO inahimiza nchi za Afrika kukumbatia ni ubadilishanaji wa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mpox ,ubainishaji sahihi na kampeni za chanjo Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,kuna hofu ya msambao hatari wa MPox unaohuishwa na vitendo vya ngonoWatalaam wa afya nchini DRC pia wanahimiza uhamasisho zaidi kuhusu ugonjwa huo ambao umesababisha vifo zaidi ya 500
Shirika la afya duniani ,WHO na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya umoja wa Afrika ,CDC zililazimika kuchukua uamuzi mzito wa kutangangaza MPOX dharura ya kiafya Mataifa 16 ya Afrika kati ya 55 yameripoti visa vya MPOX mwaka huu ,CDC ikisema maambukizo yamepanda hadi asilimia 160 mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2023Virusi vya MPOX vimeripotiwa kujibadilisha na kwa sasa msambao hatari wa virusi sugu zaidi unahusishwa na ngono
Kuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .