Ni jukwaa la kila wiki la kuzungumzia mapenzi miongoni mwa vijana; mahusiano, kuchumbiana na mengi yaliyowakaa mioyoni.
Mitandao ya kijamii siku hizi imeanza kutumiwa na watu wengi kuwatafuta wachumba. Je, ni muda upi unaostahili kuchukua kabla ya kukutana ana kwa ana na mchumba wa mtandaoni? Tumewashirikisha wananchi katika gumzo hili wakiwamo vijana waliojaribu mapenzi ya mtandaoni vilevile mshauri kulihusu suala hili.
Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika. Tumezungumza na wananchi.
Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika. Tumezungumza na wananchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, jamii imekuwa ikiyafanya kipaumbele maslahi ya mtoto wa kike baada ya kukandamizwa kwa miaka mingi. Wengi sasa wamepata nafasi ya kusoma na hata kuajiriwa. Lakini kuna wanaoamini kwamba mwanamke anapopata kazi na kuwa na cheo katika jamii, mara nyingi hujawa kiburi. Suala hili tunaliangazia kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile kupata ushauri kuhusu masuala ya ndoa.
Ulimwengu huu wa utandawazi umewapa wengi fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kuweka picha zao kujifurahisha na hata kuwafurahisha wengine. Kuna wale huweka picha wakiwa wamevalia nadhifu, wengine kujianika nusu uchi na kadhalika. Je, mwonekano wa mtu katika picha anazoweka mitandaoni unaweza kuchangia apate mchumba ama akose, hasa kwa wanaolenga kuwapata wachumba? Tumezunguma na wananchi kuihusu mada hii vilevile kupata wosia wa mshauri Bi. Rachel Mahungu.
Washauri wa masuala ya mapenzi watakweleza kwamba huwa ni kibarua kumtafuta mchumba na hasa mtu mtakayefaana maishani. Ili kumpata mpenzi ni lazima kwanza umtafute. Lakini je, ni mbinu zipi ambazo hutumiwa katika kutongoza? Msichana naye anaweza kufanya nini ili kumvutia mwanamume ambaye anampenda bila kutoa taswira kwamba ndiye anayemfukuzia mwanamume? Vijana na washauri wanatoa kauli zao kuihusu mada hii.
Katika siku za hivi karibuni yamekuwapo majaribio ya dawa za upangaji uzazi ambazo pia zinaweza kutumika miongoni mwa wanaume. Iwapo dawa hizo zitaanza kutumika, je, wanaume wanaweza kuaminika katika kuzimeza dawa hizo ama utakuwa mchezo wa paka na panya kati yao na wake zao? Tumezungumza na wananchi vilevile mshauri kulihusu suala hili.
Mwanamume anapokuwa mtu mzima, wengi hutarajia kwamba awe mwenye kujitegemea kimawazo na hata kuweza kujifanyia maamuzi ya busara. Hata hivyo, kuna wanaume ambao huitwa 'mamas boy' ambao hushtumiwa kwa kutojitegemea kimawazo na kuwasikiliza zaidi wazazi kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Je, ni sawa kwa mume kuzingatia zaidi ushauri wa mzazi badala ya mkewe?
Mwanamke anapopata mtoto nje ya ndoa ama kumzaa mtoto katika ndoa kisha kutengana na mumewe, wapo wanaojipata katika njia panda anapotafuta mchumba. Baadhi huhofia kuwa katika mapenzi kwa hofu ya kulaghaiwa tena na hofu ya kupata mwanamume atakayempenda pamoja na mwanawe. Je, mwanamke huyu afanye nini ili ampate mchumba wa kumwamini?Tunaliangazia suala hili kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Description. Wapenzi wanapokuwa katika mahusiano, mara nyingine huibuka hali za kutokuwa waaminifu. Katika kipindi hiki tuaangazia namna ya kumtambua mtu ambaye si mwaminifu kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile mshauri.
Wapenzi huoneshana upendo wao kwa njia mbalimbali mfano kushikana mikono katika maeneo ya umma, kupigana pambaja na wengine kupigana mabusu hadharani. Lakini je, ni sawa kwa wapenzi kuandamana mara kwa mara mfano kwenye saloon, kinyozi na kadhalika ama hali hiyo huenda ikachangia kuzoeana sana kiasi cha kusambaratisha uhusiano? Tumewashirikisha wananchi kulihusu suala hili vilevile kupata kauli ya mshauri.
Ni msimu mwingine wa sherehe ya siku ya wapendanao tarehe 14 Februari. Siku hiyo hutumiwa na wapenzi wengi kuoneshana upendo. Baadhi hununuliana zawadi na hata kujitengea muda wa kufurahia mapenzi yao. Hata hivyo kwa wengine ni siku ya kawaida tu. Tunaangazia umuhimu wa siku hii na iwapo kuna ulazima wa kumpa zawadi umpendaye.
Mtu anapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi, mara nyingine hujipata katika hali ambapo analazimika kutengana na mpenzi wake. Kuna wale ambao husitisha kabisa mawasiliano kati yao huku wengine wakiyaendeleza licha ya kutengana. Je, ni sawa kuwasiliana na uliyetengana naye? Wananchi wanatoa kauli zao wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga. Aidha, washauri wawili, Rachel Mahungu na Malkia wa Vijembe wanatupambia podcast hii kwa ushauri nasaha.
Katika jamii, uhuru wa kutangamana huwafanya watu kuwa na marafiki, washirika wa kibiashara, kisiasa na kadhalika. Lakini je, inawezekana kwa mwanamume na mwanamke kuwa marafiki tu bila kuhusika kimapenzi, kwa kimombo inaitwa platonic friendship. Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili. Vilevile tuna hoja za mshauri.
Awamu hii ya Vijana na Mapenzi inaangazia kisa cha mwanadada ambaye licha ya kuolewa, hataki kwenda kuishi na mumewe na kupendelea aishi tu alikozoea kabla ya kuolewa. Anasema kwamba anakoishi, maisha ni rahisi kulinganisha na kwa mumewe. Tunaliangazia suala hili kwa kushirikisha kauli za wananchi na wataalam.
Kuna msemo kwamba pesa ni sabuni ya roho. Hata hivyo kuna wapenzi ambao hutengana licha ya kuwa na pesa nyingi na mtu kuamua kumwendea asiyekuwa nazo. Je, ni kipi kinachoweza kuchangia hali hii? Wananchi vilevile washauri wa masuala ya ndoa wanatoa kauli zao.
Kwa nini baadhi ya wanaume huwachumbia wake za watu wakijua fika kuwa wameolewa? Je, wa kulaumiwa ni nani? Wananchi wanatoa kauli zao kulihusu suala hili vilevile ushauri wa mtaalam.
[09:19, 11/4/2021] Mungou: Mara nyingi watu wanapochumbiana, huwa kuna rafiki wa karibu anayeufahamu uhusiano huo. Hali hii huwafanya wengine kujipata katika hali ya kuanza kutongozwa na wapenzi wa marafiki zao. Iwapo utajipata katika hali hii, ni sawa kumfahamisha rafiki yako kwamba amdhaniaye ndiye kumbe siye?
Mara nyingi wapenzi hupenda kutia ladha katika mahusiano yao kwa kufanyiana mambo ambayo mtu hakutarajia. Kuna wale huenda kiasi cha kuwatembelea wapenzi wao bila kuwajulisha. Je, hatua hiyo inafaa ama ni lazima umjulishe mpenzi wako kwanza? Tumepata hisia za wananchi vilevile mtaalam wa masuala ya mahusiano kulihusu suala hili.
Ni jambo la kawaida wakati msichana anapoolewa aende kuishi na mumewe. Hata hivyo, kuna msichana anayesema yeye atabaki kwao kwani ni karibu na anakofanyia kazi na kukodi nyumba ya kuishi na mumewe ni gharama kwani anakofanyia kazi mume huyo ni mbali. Vijana wanatoa kauli zao huku mshauri, Rachel Mahungu akitumia utaalam wake kutoa ushauri kwa vijana
Baadhi ya wasichana siku hizi wamejaliwa na ajira tofauti na miaka ya nyuma ambapo kazi ya mwanamke ilikuwa jikoni. Wengine wanaofanya kazi hupata mapato ya kujisetiri na hata kujiendeleza kimaisha. Lakini ni sawa kwa msichana kujinunulia mali mfano magari, nyumba na kadhalika kabla hajaolewa ama anastahili kusubiri aolewe ili ajiendeleze pamoja na mumewe? Vijana wanalichangamkia suala hili katika makala haya. Vilevile tumemhusisha mshauri anayetoa wosia kuhusu suala hili.
Mara nyingi msichana anapovunja ungo ama tayari kuwa katika mahusiano, hutarajia ampate mtu ambaye hajaoa ili wafunge pingu za maisha. Hata hivyo kuna wale ambao huishia kuchumbiwa zaidi na mabwana wa wenyewe. Je, ni kipi ambacho huchangia zaidi msichana kukumbana na wanaume walio katika ndoa? Ni yeye anayejitangaza kwao ama ni ukosefu wa maadili kwa wanaume walio katika ndoa kutaka kuwa na wapenzi wengi? Vijana na washauri wanatoa hoja zao.
Visa vya wapenzi kuuana baada ya kurudiana vimekithiri nchini Kenya. Mara nyingi, mauaji hutokea baada ya mpenzi mmoja kushawishiwa na mwingine warudiane. Suala hili linatufanya kujiuliza je, ni sawa kurudiana na mtu uliyetengana naye? Aidha ni vigezo vipi ambavyo mtu anastahili kuzingatia kabla ya kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake? Tumewashirikisha wananchi wanaotoa kauli zao vilevile kupata ushauri wa mtaalam wa masuala ya mapenzi.
Ili kumpata mtu wa kuoa, ni lazima mpatane mahali. Kuna wale ambao hupatana vilabuni, mitandaoni, vyuoni na kadhalika. Hata hivyo kuna wale ambao huelekeza juhudi za kuwatafuta wachumba katika maeneo ya kuabudu. Tumewashirikisha vijana vilevile washauri ili kupata kauli zao kuhusu suala hili. Je, maeneo ya kuabudu ndiyo bora ya kuwatafutia wachumba?
Wakati mtu anapokuwa katika harakati za kumtafuta mchumba, mara nyingine utampata akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja kabla ya kumchangua anayempenda. Je, ni sawa kuwa katika mahusiano na watu kadhaa kabla ya kufanya uamuzi kuhusu anayefaa? Vijana wanatoa kauli zao vilevile mshauri wa masuala ya mahusiano ambaye anatoa mwelekeo kuhusu suala hili.
Baadhi ya wasichana walio katika mahusiano wana mazoea ya kuomba hela, bundles na hata credit kutoka kwa wapenzi wao. Je, tabia hii inafaa? Vijana wanasema nini? Washauri Rachel Mahungu na Alex Munyere wanasema ni lazima kuwe na vipimo katika ombaomba mnapochumbiana.
Mara nyingi mwanamke anapovishwa pete ya uchumba, hutarajia kwamba aliyemvisha pete hiyo atamwoa. Hata hivyo, kijana mmoja amejipata kwenye njia-panda kwani hata baada ya kumvisha mpenziwe pete ya uchumba, hana hakika kama atamwoa au la kwani kijana huyo anasisitiza kwamba ni lazima waishi kwenye eneo moja na mchumba wake atakapomwoa ilhali mchumba huyo anaishi katika kaunti nyingine anakofanyia kazi. Je, msichana huyo aache kazi ili aishi na mpenziwe? Tunalidadavua suala hili.
Mara nyingi watu wawili wanapochumbiana, huwa kuna msukumo wa kuichokora simu ya mwenzako mfano kuangalia jumbe, kuona picha alizo nazo katika simu, mawasiliano anayofanya na kadhalika. Lakini je, ni sawa kuwa na uhuru wa kuichokora simu ya mpenzi wako ama huenda hali hiyo ikazua mgogoro? Beatrice Maganga amelizamia suala hili akizihusisha kauli za wananchi vilevile hoja za Mwanasosholojia, Alex Munyere.
Si jambo geni kusikia wanafunzi hasa wa vyuo wakiwa katika mahusiano na watu wanaowazidi umri. Utawapata vijana wa kike wakijihusisha kimapenzi na wanaume wanaowazidi umri ambao huitwa sponsors huku vijana wa kiume nao wakijihusisha na 'sugar mummies'. Mienendo hii bila shaka imekithiri katika jamii na si jambo la kufumbia macho. Katika awamu hii ya kipindi cha Vijana na Mapenzi, Beatrice Maganga amezungumza na wanafunzi wa vyuo kupata uhalisia kuhusu suala la 'sponsors' na 'sugar mummies' ili kubaini hasa kichocheo cha mahusiano hayo.
Baadhi ya wanaume wamekuwa wakilalamikia 'kuliwa' kwa nauli wanazowatumia wasichana ili wapatane katika date kauli maarufu ikiwa 'kula fare'. Katika awamu hii ya kipindi cha Vijana na Mapenzi tunauliza swali je, ni sawa kwa mvulana kumtumia msichana 'fare' ili wapatane kwa 'date'? Tumepata hisia za wananchi kulihusu suala hili, vilevile ushauri wa Mwanasosholojia, Alex Munyere.
Siku hizi, mitandao ya kijamii imekuwa ikitumiwa na wengi kujitafutia wachumba, wengine wamefaulu na wengine wakikosa. Kijana mmoja amewasilisha malalamiko yake kupitia podcast hii akisema hamwamini tena mpenziwe wanayechumbiana mtandaoni akihisi kwamba anamchezea shere. Je, aendelee na uhusiano huo na mwanadada ambaye hajawahi kukutana naye ana kwa ana ama aukatize?
Podcast hii inamwangazia jamaa mwenye umri wa miaka 30 ambaye hajui la kufanya baada ya mkewe kumtoroka. Kijana huyo anayefanya kazi katika Kaunti ya Isiolo anasema kwamba siku moja mkewe alimwomba ruhusa ya kwenda kuwaona wazazi wake na hadi sasa hajarejea. Mwanamke huyo aliondoka pamoja na mtoto wao wa umri wa miaka 3 na anapopigiwa simu na mumewe anasema kwamba aliolewa kwingine. Kijana huyu yuko katika njia-panda asijue la kufanya. Mshauri wa masuala ya kijamii, Rachel Mahungu anampa ushauri katika podcast hii.
Suala la fedha katika mahusiano ya kimapenzi, bila shaka limechangia kuvunjika kwa mahusiano mengi kutokana na ukosefu wa uwazi. Mada hii inalenga kuangazia namna ya kulijadili mnapochumbiana. Washauri wa masuala ya kijamii, Alex Munyere na Rachel Mahungu wanalichanganua katika podcast hii.
Mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, WhatsApp, Twitter, Instagram na kadhalika imerahisisha pakubwa njia za mawasiliano katika karne hii. Ni hali ambayo imechangia kubadilika kwa mbinu za watu kuchumbiana ambapo wengine hutumia mitandao kuwatafuta wachumba. Lakini je, hili linafaa? Tumehusisha kauli za wananchi kuhusu mapenzi ya mitandaoni vilevile kushiriki mazungumzo na vijana na washauri wa masuala ya kijamii kuihusu mada hii.
Katika awamu hii ya pili ya kipindi cha Vijana na Mapenzi, tunaangazia ishara mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kutambua iwapo uhusiano wa kimapenzi hauendi popote na ni wakati wa kutengana. Wananchi wametoa kauli zao kuihusu mada hii huku washauri, Alex Munyere na Rachael Mahungu Mboya wakitoa ushauri kuhusu mada hii. Mtayarishi ni Beatrice Maganga.
Awamu ya kwanza ya Vijana na Mapenzi inaangazia suala la miadi yaani dating, Je ni kipi ambacho huzungumziwa wakati wa date? Tumewashirikisha vijana kujadili suala hili, vilevile kupata kauli za washauri wa masuala ya mahusiano.
Wasichana wa Kenya wanaeleza sababu za kuwapenda wanaume wa Nigeria au Wazungu; kwamba wanajua mapenzi, kutumia pesa, kuvinjari na kuwapa raha za peponi. Kwamba wanaume wa Kenya hawajui kupenda, wana mikono birika. Ni gumegume tu...si wanaume kamili. Nao wanaume wa Kenya wanahofia ushindani na kusalimu amri; wanasema kwamba ni sawa tu...acha wapendane.
Ni msimu wa mapenzi, Je ni lazima mpenziwe akupe zawadi siku ya Valentines, na asipo kupa ina maana kwamba hakupendi? Wakenya wanalizungumzia suala hili vilevile washauri wa masuala ya mahusiano ambayo wana mtazamo wao kulihusu.
Katika awamu hii tunaangazia utumiaji wa mitandao katika kuchumbiana. Je, inafaa ama haifai? Vijana wamelizungumzia suala hili katika kipindi hiki vilevile kuna ushauri wa mjuzi wa masuala ya mahusianio, Rachel Mahungu.
Episode 2 is about the red flags during dating
Episode 1 is about what to be discussed during a date