Podcasts about wazazi

  • 21PODCASTS
  • 121EPISODES
  • 19mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • May 22, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about wazazi

Latest podcast episodes about wazazi

Radio Maria Tanzania
Je, unafahamu madhara ya uraibu wa Wazazi kwa watoto?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 22, 2025 51:57


Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Uraibu, Mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha kutoka  Moshi, akitoa ufafanuzi wa madhara ya Uraibu wa wazazi kwa watoto.   L'articolo Je, unafahamu madhara ya uraibu wa Wazazi kwa watoto? proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Wazazi pelekeni watoto wenu kupata chanjo dhidi ya maradhi - Bi. Halfani

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 7, 2025 3:36


Katika Wiki ya Chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni  Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza. Je, ni mafanikio gani yamepatikana na kwa nini chanjo hizi ni muhimu? Ungana na Sharon Jebichii kwa makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini  Tanzania.

Radio Maria Tanzania
Wajibu wa Wazazi na Walezi katika Malezi ya Watoto wawapo Masomoni.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 42:59


Ungana nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Kutoka TEC , Mwezeshaji ni Sister Anagradness Mruma, Katibu wa Utoto Mtakatifu Taifa anayefanya Utume Balaza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC  akizungumzia juu ya Ufatiliaji wa Malezi kwa Watoto wawapo Masomoni? L'articolo Wajibu wa Wazazi na Walezi katika Malezi ya Watoto wawapo Masomoni. proviene da Radio Maria.

VOA Express - Voice of America
Vijana nchini Uganda inaripotiwa wanapata shida ya afya ya akili kutokana na wazazi au walezi kukosa muda wa kusikiliza mahitaji yao. - Februari 28, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 28, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Radio Maria Tanzania
Je, ni kwa namna gani Watoto wanapaswa kuwaheshimu Wazazi wao?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 11, 2025 27:13


Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tunaungana na Frateri Ayuto Kongo kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea, akijibu Swali hili Katika amri 10 za Mungu amri ya 4 inasema Waheshimu baba yako na mama yako upate miaka mingi na heri duniani,je? Hawa wazazi tulioamriwa Kuwaheshimu tuwaheshimu vipi? L'articolo Je, ni kwa namna gani Watoto wanapaswa kuwaheshimu Wazazi wao? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu historia ya Mtakatifu Josephine Bakhita.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 10, 2025 29:14


Ungana nami Patrick Tibanga katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akielezea juu ya Wajibu wa Wazazi kuwapeleka wa Watoto wao kwa Mungu. L'articolo Fahamu historia ya Mtakatifu Josephine Bakhita. proviene da Radio Maria.

SBS Swahili - SBS Swahili
Jinsi ya kupata Malipo ya Likizo ya Wazazi nchini Australia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Feb 7, 2025 12:48


Nchini Australia, baadhi ya wazazi wanaweza pokea malipo ya likizo ya wazazi kutoka serikali na waajiri wao. Ila si kila mtu ana stahiki.

Radio Maria Tanzania
Zifahamu mbinu za kuwalea Watotoa katika tabia njema

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 5, 2025 21:45


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo  mada,  juu ya ukosefu wa Maadili kwa Watoto, Je ni malezi dhaifu kwa Wazazi? L'articolo Zifahamu mbinu za kuwalea Watotoa katika tabia njema proviene da Radio Maria.

Bible Bard
swahili_BB-61 Maneno 10 Yanayoeleweka, Wazazi

Bible Bard

Play Episode Listen Later Feb 5, 2025 13:50


Amri ya tano inahusu jinsi watoto wanavyowatendea wazazi wao - Amri hii imejadiliwa katika kipindi hiki.

VOA Express - Voice of America
Wito watolewa kwa wazazi kutoiachia serikali mapambano na dawa za kulevya Tanzania - Januari 10, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 10, 2025 29:59


Wito watolewa kwa wazazi kutoiachia serikali mapambano na dawa za kulevya Tanzania

Radio Maria Tanzania
Ni, Kwanini Yesu alipelekwa Hekaluni na Wazazi wake akiwa mdogo?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jan 3, 2025 22:42


Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Benedict Lazaro Luvanga  Kutoka Parokia ya Bikira  Maria Mama wa Shauri Jema Nyabula, Jimbo Katoliki Iringa nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Kwanini Yesu alipelekwa Hekaluni na Wazazi wake akiwa mdogo? L'articolo Ni, Kwanini Yesu alipelekwa Hekaluni na Wazazi wake akiwa mdogo? proviene da Radio Maria.

SBS Swahili - SBS Swahili
Levi "Wazazi wasi harakishe kuwatuma watoto ng'ambo kabla hawaja komaa"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Dec 31, 2024 20:49


Wazazi wengi huwa na ndoto za kuwatuma watoto wao ng'ambo kufanya elimu ya juu.

VOA Express - Voice of America
Mmoja wa wazazi huko Tanzania anatoa maoni yake kufuatia tabia ya baadhi ya wazazi kuwaacha watoto peke yao majumbani au maeneo ya michezo. - Desemba 26, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 26, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 16, 2024 4:24


Tarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.

VOA Express - Voice of America
Dunia inaadhimisha siku ya walemavu huku walezi au wazazi wanaowahudumia walemavu wanaeleza changamoto zilizopo katika maisha ya kila siku. - Desemba 03, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 3, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Radio Maria Tanzania
Ifahamu Historia ya Wazazi wa Bikira Maria

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Nov 15, 2024 24:17


Ungana nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Tafakari nasi kutoka Studio za Radio Maria Tanzania, Mwezeshaji ni Padre Fabian Ngeleja Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Josephina Bakhita- Nyamanoro Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akielezea Familia ya Bikira Maria. L'articolo Ifahamu Historia ya Wazazi wa Bikira Maria proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Mradi wa UNICEF wa kuboresha lishe waleta tabasamu kwa wazazi na watoto Afar Ethiopia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 11, 2024 1:46


Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto. Video ya UNICEF Ethiopia inaanza ikimuonesha mtoto akitabasamu, na kisha akiwa na mama yake wakielekea kwenye kituo cha afya. Mama huyu anaitwa Fatuma Kebir na mwanae huyu aliyembeba anaitwa Abdu. Fatuma anasema..“Nilihofia kuwa angeendelea kuwa na utapiamlo. Kwa hiyo nilimpeleka kituo cha afya na mhudumu wa afya akanieleza kuwa mwanangu amepoteza uzito, kama ambavyo nilihisi. Akaniambia nimlishe zaidi, hasa uji uliochanganywa na mayai, maziwa, na mboga.”Video ikimuonesha Fatuma akiandaa uji akichanganya na mayai, mtaalam wa lishe wa UNICEF, Yetayesh Maru, anasema,“Kama sehemu ya mtambuka wa hatua na uratibu dhidi ya utapiamlo kwenye jamii, Fatuma ametambuliwa kuwa ni kaya iliyo hatarini, hivyo amenufaika na mradi wa kisekta wa kuboresha lishe kwa watoto.”Sasa Fatuma na mtoto wake Abdu wanapata tabasamu upya.“Nilimlisha kwa mwezi mmoja kama walivyoshauri na kisha nikarudi kituo cha afya. Mtoa huduma alisema kwamba sasa ana afya na amerudia uzito wake. Nilifurahi sana alipoanza kuongezeka uzito.”Tabasamu lao ni dhahiri hata kwa mtoa huduma Yetayesh, akisema “Sasa Abdul anakua vizuri, na nguvu kamilifu, huku akicheka na mama yake.”

VOA Express - Voice of America
Mmoja wa wazazi mwenye watoto wanaosoma shule za bweni nchini kenya anaeleza changamoto wanazopitia inapotokea visa vya mioto mashuleni. - Septemba 09, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

kenya visa watoto shule wazazi septemba
Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu Wazazi wa Bikira Maria?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 26:07


Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Maurus Zacharia Msigwa, kutoka Parokia ya Familia Takatifu Tunduma Jimbo Katoliki Sumbawanga nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Baba na Mama wa Bikira Maria ni nani? L'articolo Je, wafahamu Wazazi wa Bikira Maria? proviene da Radio Maria.

Jioni - Voice of America
Mgomo wa waalimu Kenya bado unaendelea huku baadhi ya wazazi wakiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo. - Agosti 30, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Aug 30, 2024 59:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 22 Agosti 2024

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 22, 2024 6:07


Wazazi wapya hivi karibuni wataweza anza pokea malipo yao ya uzeeni juu ya malipo ya likizo ya wazazi yanayo wekezwa na serikali, sheria ziki tarajiwa kuwasilishwa ndani ya bunge la shirikisho hii leo Alhamis 22 Agosti.

agosti habari wazazi alhamis
Radio Maria Tanzania
Fahamu mbinu za kuwalea Watoto katika Makuzi mema katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 31, 2024 59:47


Ungana nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Familia bora katika Nyumba aminifu, Wawezeshaji ni Bwana Paschal Maziku, Bi. Federika Bayaga, Bi. Ester Kinyonga, Katekista Vicent Nathanael na Katekista Gabriel Mgala, Wakufunzi wa Familia bora na Nyumba aminifu, wanaendelea kutufundisha juu ya Chanagamoto wapatazo Wazazi na Walezi katika Makuzi ya Watoto. L'articolo Fahamu mbinu za kuwalea Watoto katika Makuzi mema katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu changamoto wapatazo Wazazi na Walezi katika Malezi bora ya Watoto?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 22, 2024 48:07


Ungana nami Mtangazaji wako Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Familia bora na Nyumba aminifu leo tupo na Wakufunzi kutoka Familia bora katika Nyumba aminifu, wakiendelea na mada isemayo changamoto wapatazo wazazi na walezi katika malezi bora ya watoto.   L'articolo Je, wafahamu changamoto wapatazo Wazazi na Walezi katika Malezi bora ya Watoto? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, Watoto waliotolewa mimba na Wazazi wao siku ya mwisho watafufuliwa?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 10, 2024 29:18


Ungana na Happiness Mlewa katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani pamoja na Frateri Franco Abeli Ubamba kutoka Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni,  Jimbo Katoliki Mafinga, mada ya leo ni Watoto walio tolewa mimba na Wazazi wao siku ya mwisho watafufuliwa. L'articolo Je, Watoto waliotolewa mimba na Wazazi wao siku ya mwisho watafufuliwa? proviene da Radio Maria.

radio maria siku watoto ungana wazazi maswali
Alfajiri - Voice of America
Wazazi watakiwa kutambua umuhimu wa malezi ya mtoto kwa pamoja - Juni 17, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jun 17, 2024 29:59


SBS Swahili - SBS Swahili
Iyanii "fahari yangu imekuwa kubadilisha maisha ya wazazi wangu"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 13, 2024 15:19


Iyanii ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kenya, anaye zidi kuwa maarufu kila kukicha.

Radio Maria Tanzania
Fahamu wajibu wa Wazazi na Walezi juu ya Uraibu wa Mitandao kwa Watoto.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 17, 2024


Karibu Ungane na Mtangazaji Happiness Mlewa, katika kipindi cha Uraibu na Padri Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, leo tunaangazia Wajibu wa Wazazi na Walezi juu ya Uraibu wa Mitandao kwa Watoto. L'articolo Fahamu wajibu wa Wazazi na Walezi juu ya Uraibu wa Mitandao kwa Watoto. proviene da Radio Maria.

Jioni - Voice of America
Wazazi wenye watoto wa Autism pamoja na wataalamu wa Afya wanaelezea ugonjwa wa Usonji au Autism na changamoto zake katika maisha - Aprili 12, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Apr 12, 2024 59:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Jioni - Voice of America
Dunia inaadhimisha siku ya Usonji au Autism huku wazazi wanaoishi na watoto wenye tatizo hilo wanaelezea changamoto zilizopo katika matibabu - Aprili 02, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Apr 2, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Alfajiri - Voice of America
Mamia ya watoto hawajulikani walipo baada ya kutenganishwa na wazazi wao, kufuatia mapigano makali kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 - Februari 07, 2024

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 7, 2024 30:00


Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

VOA Express - Voice of America
Karo za shule changamoto kwa wazazi Uganda - Februari 07, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 7, 2024 30:00


Karo za shule changamoto kwa wazazi Uganda

VOA Express - Voice of America
Mtaalam wa afya ya akili ashauri wazazi kutoweka shinikizo kwa watoto wao wanapojianda kufanya mitihani ya taifa - Januari 31, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 31, 2024 29:59


SBS Swahili - SBS Swahili
Wazazi wanaweza msaidiaje mtoto kupona kiwewe?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 18, 2024 12:15


Iwapo mtoto wako amepata kiwewe ng'ambo au nchini Australia, iwapo ilitokea hivi karibuni au katika siku za nyuma, pakiwa msaada unao faa, mtoto anaweza pona.

australia wazazi
SBS Swahili - SBS Swahili
Australia ya elezewa: Wazazi wanaweza msaidiaje mtoto kupona kiwewe?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 28, 2023 12:09


Ikiwa mtoto wako amepata kiwewe ng'ambo au nchini Australia, ikiwa ilifanyika hivi karibuni au katika siku za nyuma, pakiwa msaada unao faa, mtoto anaweza pona.

australia wazazi ikiwa
Nyumba ya Sanaa
Wazazi chanzo cha Wasichana kutofanya Muziki Tanzania

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later Oct 21, 2023 20:08


Wazazi chanzo cha Wasichana kutofanya Muziki Tanzania, Steven Mumbi anazungumza na Zulfa Mohamed maarufu Xoul

tanzania eac muziki wazazi steven mumbi
SBS Swahili - SBS Swahili
Kudhibiti ugonjwa wa vituo vya malezi ya watoto: Vidokezo kwa wahamiaji wapya na wazazi wa mara ya kwanza

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 22, 2023 9:41


Kuanza kupeleka mtoto katika huduma ya malezi ya watoto mapema, inaweza kuwa suluhisho la vitendo kwa kusawazisha matarajio ya kazi na wajibu wa uzazi.

kwanza watoto wazazi ugonjwa
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari 14 Agosti 2023

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 15, 2023 6:49


Wazazi wa mwomba hifadhi kutoka Iran aliye uawa wakati wa mgomo katika kisiwa cha Manus mnamo 2014, wamefikia suluhu ya siri na serikali ya shirikisho pamoja na kampuni ya ulinzi ya G4S.

Habari za UN
Hospitali Sudan zaomba usaidizi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 26, 2023 0:02


Vita nchini Sudan ambayo sasa imedumu kwa zaidi ya siku 100 imeshuhudia zaidi ya watu milioni 3 wakiyakimbaia makazi yao kwenda kusaka hifadhi katika miji mingine pamoja na nchi Jirani. Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA inaanza kwa kuonesha chupa cha upasuaji ambako mjamzito amefanyiwa upasuaji na kujifungua salama huko katika mji Port Sudan jimboni Red Sea mashariki mwa nchi ya Sudan.Hapo awali, hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wajawazito 300 mpaka 450 wanaojifungua kwa njia ya kawaida na wale wanaohitaji upasuaji walikuwa takriban 300 kwa mwezi. Daktari Randa Osman ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo ya Wazazi ya Port Sudan anasema “Idadi ya sasa ni kubwa zaidi kwa sababu ya ongezeko la watu wanaokimbilia katika jimbo hili.” Dokta Randa anaendelea kwa kusema wajawazito na watoto wachanga wanakabiliwa na ufikiaji finyu wa huduma muhimu za afya. “Hospitali hii ya kujifungulia ndio pekee iliyopo katika mji huu na inatoa huduma za dharura za uzazi, uangalizi baada ya kujifungua na upasuaji. Hospitali imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wagonjwa na mzigo wa kazi umeongezeka mara mbili. Watendaji wetu wanafanya kazi bila kuchoka kuwahudumia wakimbizi wanaokaa katika makazi ya muda ya wakimbizi.” Daktari huyu anahitimisha kwa kueleza kile wanachohitaji? “Tunahitaji vifaa tiba zaidi kwakuwa idadi ya wagonjwa ni zaidi ya mara mbili. Na pia tunahitaji kuongeza juhudi ili kukabiliana na hitaji hili kubwa linalozidi kuongezeka.”Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linafanya kila juhudi kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau kuhakikisha wanawasaidia watu wote wenye uhitaji.

Habari za UN
Tusaidieni huko DRC ili nasi tuwe na furaha, Wakazi Beni waomba Umoja wa Mataifa

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2023 0:03


Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumi. Mwandishi wetu  wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wa kwanza kuzungumza mjini Beni ambako vikundi vya waasi vimekuwa vikishabulia raia, ni Vakekya Kaswera mama huyu wa watoto 7 akiwa shambani anasema furaha kwake yeye ni shamba lake analolima mihogo. Shambani anapata sombe au kwa kiswahili kisamvu na pia anapata unga wa muhogo. Hata hivyo anasema “furaha yangu inapotea pale mbuzi wanapokuja na kuharibu mazao yangu. Napenda kazi ya kilimo kwa sababu ndio kazi yangu tangu mdogo na inaniweza kutunza familia. Wazazi walitufundisha kulima na pia walitupeleka shuleni.” Mkazi mwingine Serge Kyamundu kwake yeye furaha ni pale enzi hizo ilikuwa inawezekana kupata starehe mjini Beni. “Kwangu ni furaha ni pale ninaona mji wangu uko katika starehe. Miaka iliyopita katika mji wetu wa Beni muziki ulipigwa ilikuwa furaha hakika. Lakini leo hii wakati usalama umemalizika katika mji wetu furaha kwangu imekwisha.” Ametoa wito kwa watu wengine wa nje na serikali za mbali zisaidie kurejesha usalama ili furaha irejee Beni kwani katika siku ya leo ya furaha“watoto wa Beni hatuna hakika furaha kwani tunakosa usalama katika mji wetu.” Naye Sylvie Mbakania, mkulima amesema “furaha yangu ni kutazama mazingira yakiwa mazuri. Ninapoona mbegu zimechipuka hunipatia furaha.” Hata hivyo hivi sasa furaha yake si kamilifu “kwa sababu ya vita katika nchi yetu.  Natoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi zaidi kurejesha amani ili kukamilisha furaha yangu kama vile mahali pengine wanasherehekea siku hii.” Tarehe 12 mwezi Julai mwaka 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha tarehe 20 ya kila mwaka kuwa siku ya furaha duniani kwa kutambua mchango wake furaha na ustawi kama malengo ya kimataifa na matamanio ya kila binadamu. 

VOA Express - Voice of America
Mmoja wa wazazi kutoka mkoa wa Arusha huko Tanzania anaiomba serikali kuchunguza kwa kina suala la watoto kufundishwa kulawitiana shuleni - Januari 18, 2023

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 18, 2023 29:59


Shutuma za watoto wanafundishwa kulawitiana shuleni zimeripotiwa na moja ya magazeti yanayoaminika nchini Tanzania jambo lililozusha taharuki kwa wazazi, jamii na wakati huo huo serikali inasema inafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hili

Salama Na
SE7EP30 - SALAMA NA BRENDA | MY DEAR…

Salama Na

Play Episode Listen Later Jan 5, 2023 66:17


Ushawahi kumuangalia mtu kwa mbali na kujiuliza maswali mengi juu yake? Maswali kama siku yake ikoje, amewezaje? Kama ana familia? Ki kawaida huwa anaamka saa ngapi? Amesoma wapi? Siku yake anaipangaje? Ana watoto? Mtoto? Huwa anawaandaa kwenda shule? Muda je wa kukaa nao? Elimu yake ameipatia wapi? Kwenye familia aliyotoka je? Wazazi wake wapo? Na je wanajivunia yeye kwa kiasi gani? Sasa ili kupata majibu ya maswali hayo yote ilibidi tumtafute Bi Brenda Msangi-Kinemo ambaye ndo nilikua namzungumzia hapo juu. Kama wewe utakua mtu wa kujua ambayo yanaendelea nchini, na pia kama ni mkazi wa Dar es Salaam basi lazima utakua unajua kuhusu hospitali ya CCBRT ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia na inaendelea kutoa huduma za macho, mifupa na magonjwa mengine kwa watu wengi kwenye nchi yetu. Sasa Bi Brenda yeye ndo Mkurugenzi pale. Na amekua kwenye cheo hicho kwa zaidi ya miaka minne sasa na hiyo ukiachilia mbali miaka ambayo alikua akifanya kazi pale wakati bado hakua Mkurugenzi. Yeye ni mtaalamu wa masuala ya afya, hicho ndo ambacho aliendea skuli huko nchini Uingereza na kwa mujibu wa baadhi ya majarida ambayo nimesoma maisha yake kama yalikua yanataka kubaki huko baada ya kuhutimu ila aliporudi nyumbani na kupata nafasi pale hospitali mambo mengi yalibadilika. Kwenye kipindi hiki anatusimulia jinsi ambavyo hayo yalitokea. Na aina ya maamuzi ambayo ilibidi ayachukue ili mambo yatuwame. Kwa wasichana wengi hasa wale ambao wanakua na kuanza kujitafuta Brenda ni role model wao sana na ni nafasi ambayo kwake yeye ilikuja baada ya kuwa anaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu kupambana na kuweza kuvaa kofia zaidi ya moja kwenye maisha ukiwa kama mwanamke. Humu pia ananiambia jinsi ambavyo hizo nondo za ku inspire zilivyoanza, ananiambia jinsi ambavyo alikua akisoma na kufanya kazi na wakati mwengine jinsi ambavyo majukumu yalikua yakimzidi mpaka anakaribia kukata tamaa ila msukumo ambao alikua akiupata kutoka ndani yake ndo ambao ulimfikisha alipo. Aliamini kwamba kuna wanawake na wasichana wengi ambao wanapitia kwenye mitihani ambayo yeye alikua nayo na kama yeye aliweza kushinda basi aliona atumie sauti yake na busara zake kuwaambia wengine kama hakuna kinacho shindikana kama nia inakuwepo. Binafsi nilijichotea mengi sana kutoka kwenye kisima chake cha busara na uthubutu na bado darasa naendelea kulipata kwasababu nafuatilia yale anayo yafanya na ambayo anayaandika ili kusaidia wengine wasijione wako peke yao. Mungu amueke na aendelee kumsimamia kwenye kazi zake na maono yake ambayo yanasaidia watu wengi wengine kuanzia ofisini kwake mpaka kanisani na nyumbani. Yangu matumaini nawe uta enjoy na kupata faida kwenye episode hii kama ilivyo nia yetu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

VOA Express - Voice of America
Wazazi waaswa wajihusishe zaidi katika maisha ya watoto wao. - Januari 05, 2023

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 5, 2023 29:59


Huko Tanzania matokeo ya kitaifa ya mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili kwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2022 yameshuka ikilinganishwa na 2021 Wadau wamewataka wazazi wajihusishe zaidi katika maisha ya watoto wao.

RadioRahma
Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 2

RadioRahma

Play Episode Listen Later Nov 8, 2022 8:47


Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo, Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi. Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Habari za UN
Mradi wa UN Zambia warejesha watoto wa kike shuleni, wazazi wafurahia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 0:04


Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA na la kuhudumia watoto, UNICEF  huko nchini Zambia unatekeleza mradi wa kuchochea kasi ya kutokomeza ndoa za utotoni, GPECM. Mradi unalenga kulinda na kuendeleza watoto wa kike na barubaru ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni na hatimaye wafikie malengo ya juu ya ustawi kielimu, kiuchumi na kijamii. Barani Afrika pekee, mradi huo umewezesha wasichana milioni 7.9 katika mataifa 12 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 na bado unaendelea kuleta nuru kama ilivyo huko Zambia ambako matunda yanaanza kuonekana. Ni kwa vipi basi? Ungana na Happiness Pallangyo wa Radio washirika UHAI FM kutoka Tabora nchini Tanzania katika Makala hii iliyoandaliwa na UNICEF nchini Zambia.

Habari za UN
Huduma ya RapidPro iliyoletwa na UNICEF imeokoa watoto wetu Turkana nchini Kenya – Wazazi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 16, 2022 3:45


Kaunti ya Turkana nchini Kenya inakabiliwa na ukame wa muda mrefu. Ili kusaidia kuimarisha mifumo ya lishe, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, nchini Kenya limeanzisha mfumo wa simu za mkononi uitwao RapidPro. Huduma hii huwezesha vituo vya afya kushirikishana ujumbe wa lishe na wafanyakazi wa kujitolea wa afya ya jamii, ambao huripoti taarifa na takwimu mbalimbali za kiafya kuhusu jamii zao. 

Habari za UN
Mazingira haya bora kwa watoto Molteno ni asante kwa wazazi na jamii:Mkuu wa shule

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 12, 2022 2:05


Salama Na
SE7EP13 - SALAMA NA MARDHIYA | HIARI…

Salama Na

Play Episode Listen Later Sep 8, 2022 50:57


Salum Mardhiya ni mmoja ya watu maarufu sana kwenye visiwa vya marashi ya karafuu yaani kule kwetu Zanzibar. Ni mmoja ya waalimu hodari anayeongoza kwa kutoa Da'wa kwa watu ambao wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali. Kwenye nyumba karibu zote wanamfahamu maana huonekana mara kwa mara kwenye maeneo mbali mbali ili kusaidia wale ambao wanahitaji kisomo chake. Binafsi nilifahamiana nae kupitia rafiki ambae alinitambulisha kwake mapema mwaka huu, tena haikua imepangwa wala, alikuja sehemu ambayo mie nilikuwepo kuja kupata chai na mimi bahati nzuri nilikua maeneo hayo so mtu akatutambulisha, na akaambiwa kama Mama yangu ni mgonjwa yuko hospitali na yeye akasema basi atakuja baadae kwaajili ya kumuombea dua, na jioni akatokea. Oh kama angependa kujua hali ya Mama yangu Alhamdulillah yuko vizuri. Tunamshkuru Mungu. Kwa mujibu wa story za hapa na pale niliambiwa nilikua na bahati sana kumpata maana ratiba yake ya kutoa Da'wa ni tight sana na watu ni wengi wanaohitaji huduma zake ila muda anakua hautoshi wa kumtilia Dua kila mtu ingawa angependa kufanya hivyo, kwahiyo ilikua kama bahati sisi kukutana na kuanzia hapo tukaanza kuwa tunaonana kwa kiasi. Nikaona si vibaya kama nitamleta kwenye meza yetu ili na sisi tuweze kumfahamu zaidi. Wakati namuambia kuhusu mualiko wa kuja kwenye kiti chetu chakavu hakua na hiyana, aliangalia ratiba yake na akaniambia hiyo tarehe atakuwepo nchini. Sheikh Mardhiya yeye huwa anasafiri sana, Da'wa zake huzitoa sehemu tofauti tofauti duniani, mara nyingi anakua zake Arabuni, mitaa ya Oman na Dubai na Abu Dhabi huwepo sana, kashatibu watu wa aina tele kwenye maisha yake. Kuanzia marajiri mpaka maskini, ambao walikua na imani na anachofanya na ambao hawakua na imani nae. Simu yake huita mara kwa mara na hiyo ni moja ya sababu za yeye kuwa na namba zaidi ya moja na kuwa na wasaidizi kadhaa. So huku kwenye kutoa Da'wa alifikaje? Hii ilikua ndo mwanzo wa maongezi yetu haya. Akiwa kama kijana ambaye angeweza pengine kufanya kazi ya aina yoyote na kujipatia rizki yake, kwanini alichagua hii? Kaniambia tokea akiwa na umri wa miaka sita, alianza kupata upeo huo, bila hata yeye mwenyewe kujua ni nini hasa kilikua kinaendelea katika maisha yake, anakumbuka pia jinsi alivyokua anazimia na kupata uwezo wa kuwasomea walokua wanahitaji kisomo chake na wanakua poa kabisa, anasema hata hakumbuki alikua anawasomea nini baadhi yao ila sasa baada ya kuwa mtu mzima na kupata kuijua vizuri Quran Tukufu ndo anang'amua nini alikua anawasomea watu ule. Mwanzo nilisema Mardhiya ni kijana kwahiyo kwa kiasi kikubwa ana style ya maisha ambayo vijana wengi wangependa kuwa nayo ila uwezo nayo hawana. Kama kuwa na maisha ya kifahari, magari mazuri na mke zaidi ya mmoja, pesa nyingi na nyumba nzuri zaidi ya moja na kusafiri mara kwa mara. Hii kwa ki aina flani imekua ikileta maneno na maswali kuhusu uhalali wa ambacho anafanya au ambacho amekua akifanya. Je maneno hayo yanamzui yeye kufanya ambacho anafanya kwa watu wenye uhitaji? Au kubadilisha aina ya maisha ambayo anaishi? Tumeongea kuhusu masuala ya Husda na wivu, usafi na mmoja kuamua kujipenda zaidi. Je kuna makosa kwenye baadhi ya matamanio ya nafsi zetu? Vipi kuhusu Sadaka? Inatakiwa itolewe ki namna gani? Ipi ni sawa na ipi si sawa? Ipi ni dhambi na ipi ni nzuri ili kuweza kuwafanya na wengine watamani kutoa? Vipi kuhusu Heshima kwa kila mmoja? Wazazi? Nafasi ya Wanawake? Kuhusu imani na uchawi kwa ambacho yeye anafanya? Mmoja anaweza kujuaje kama hii ni kufuru na hii ni sawa? Maswali yalikua mengi na majibu pia yalikua yanatoka kutokana na swali lilivyo ulizwa, yangu matumaini elimu ambayo Mimi nimeipata na kwako itakua vivyo hivyo. Tafadhali Enjoy, Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Habari za UN
Mradi wa UNICEF Rwanda wahakikisha wazazi wanafanya kazi bila wasiwasi wa hali ya wanao

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 1, 2022 3:10


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Rwanda kwa kushirikiana na Bodi ya Madini nchini humo wamefanikiwa kuanzisha vituo viwili vya kulea watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0 mpaka 6 kwa ajili ya kusaidia wazazi wanaofanya kazi migodini waweze kuwa na uhakika wa sehemu wanapowaacha watoto pindi waendapo kujitafutia kipato.

Alfajiri - Voice of America
Jaji Mkuu Kenya aonya wazazi wanaozishtaki shule - Mei 24, 2022

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later May 24, 2022 30:00


Muungano wa wazazi nchini Kenya umesema haujaridhishwa na kauli ya Jaji Mkuu Martha Koome kuwaonya wazazi wenye tabia ya kuwashtaki walimu pamoja na shule baada ya watoto wao kufukuzwa shuleni kwa utovu wa nidhamu na uvunjaji wa sheria za shule

Habari za UN
Wazazi wasione aibu kuwaelimisha watoto kuhusu afya ya uzazi - Tumaini Community Services Mbeya Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 26, 2022 2:50


Nchini Tanzania, Shirika la Tumaini Community Services linatekeleza mradi wa ‘Dreams' yaani ‘Ndoto' katika wilaya ya Mbeya mjini, Kyela na Mbarari mkoani Mbeya kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa kuwawezesha vijana balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu ya kiuchumi ili kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.