POPULARITY
What are the rules around raising money and charities? How can you ensure you don't get scammed? Here is what you need to know if you're donating, raising money yourself or launching an online crowdfunding appeal. - Je, ni sheria gani zinazo husu kuchangisha pesa na mashirika ya kutoa misaada? Unawezaje hakikisha kuwa hutadanganywa? Haya ndiyo unastahili jua kama una toa mchango, unachangisha pesa mwenyewe au una zindua ombi la mchango mtandaoni.
Licha ya jitihada mbalimbali, bado watu wenye ualbino wanabaguliwa kwenye baadhi ya jamii na hata kuuawa kwa imani za kishirikina.
Licha ya jitihada mbalimbali, bado watu wenye ualbino wanabaguliwa kwenye baadhi ya jamii na hata kuuawa kwa imani za kishirikina.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD. Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za hatua za kupambana na UKIMWI, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hasa kwa watoto DRC, na ujumbe katika siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela.
Send us Fan MailMheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algiers tarehe 10 Juni, 2026. Balozi Mobhare Matinyi anayeiwakilisha Tanzania nchini Algeria, ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi kufaidika katika nyanja mbalimbali.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
Waziri Mkuu Anthony Albanese haja tupilia mbali uwezekano wa kuongeza muda wa kupunguzwa kwa ushuru wa mafuta kutokana na kufufuliwa upya kwa mapigano Mashariki ya Kati.
Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema zaidi ya watu 900 wanashukiwa kuwa wameambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Côte d'Ivoire ambako wakulima wameshuhudia kuimarika taratibu kwa uzalishaji wa kakao baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kusaidia wakulima nchini humo kurejesha ardhi katika ubora wake na kuongeza uzalishaji kupitia mbinu endelevu za kilimo mseto cha misitu, mazao na mifugo..Afrika imekuwa mstari wa mbele kushinikiza mfumo mpya wa kifedha unaozingatia usawa kwa nchi zinazoendelea. Na leo katika mkutano wa kuangazia mustakbali wa Afrika, Africa Forward huko Nairobi nchini Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezipongeza nchi za Afrika kwa kuongoza juhudi hizo za mageuzi ya mifumo ya fedha duniani. Kuhusu utajiri wa madini yanayopatikana Afrika kunufaisha nchi nyingine nje ya bara hilo Guterres amesema “Hakuna tena unyonyaji wala uporaji. Watu wa Afrika lazima wanufaike kwanza, na zaidi kutokana na rasilimali za Afrika.”.Taarifa mpya kuhusu virusi vya hanta ni kwamba hadi sasa wagonjwa walioripotiwa ni 11, na watu watatu wamefariki dunia. Kati ya wagonjwa hao, tisa wamethibitishwa kuwa na virusi vya Andes huku wawili wakihesabika kuwa wagonjwa wanaoshukiwa lilesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. WHO pia wameipongeza serikali ya Hispania kwa ushirikiano wake katika mchakato mzima wa kuwaondoa salama na kuwarejesha makwao abiria takriban 150 kutoka nchi 23 waliokuwa katika meli ya kitalii ya MV Hondius ambapo humo ndio mlipuko wa hanta ulipotokoea.ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hivi karibuni kuhusu Malengo ya Misitu Duniani, Global Forest Goals kwa mwaka 2026 ikieleza bayana kuwa misitu ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha uhakika wa chakula na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu duniani. Nchini Kenya mkazi mmoja ameeleza bayana jinsi wanavyonufaika na msitu asili wa Ngong ulioko takribani kilometa sita kutoka mji mkuu Nairobi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua maana ya neno “Payapaya''Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Haki ya afya kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni haki ya kila mtu bila kujali uko kwenye kundi au jamii gani. Huo ulikuwa ni msisitizo mwaka huu kwenye Jukwaa la jamii za watu wa asili lililokuja jamvi wiki iliyopita hapa New York Marekani. Na kandoni mwa kikao hicho Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili
Karibu usikilize Kipindi cha Utume wa Walei Mwezeshaji Bi Rose Gerrad Katibu Kamati ya Uinjilishaji Jimbo kuu Katoliki Dar es salaam Mada ni Kanzi ya Uongozi Tarehe 10 Aprili 2026 L'articolo Fahamu wajibu wakiongozi katika kuwaunganisha watu. proviene da Radio Maria.
Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?
Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo' iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita. Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa 14 alikamilisha ziara ya siku kumi barani Afrika juma hili; na katika mzozo wa Mashariki ya kati, Marekani yaongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran, hatua sawa ikichukuliwa kati ya Israeli na Lebanon.
Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefungua kikao chake cha ishirini na tano leo Aprili 20 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili. Kikao hiki kinafanyika katika muktadha wa changamoto zinazoendelea duniani, zikiwemo afya, migogoro na ukosefu wa usawa. Pia kinakuja wakati ambapo mfumo wa ushirikiano wa kimataifa, ndani ya mfumo wa mipango kama Mpango wa Mageuzi ya Umoja wa Mataifa, UN80 unakabiliwa na mahitaji yanayoongezeka ya ujumuishwaji, uhalali na ufanisi. Anold Kayanda amelifuatilia tukio hilo.
Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili hapa Makao Makuu, mafunzo Kenya ya "Social Media 4 Peace" yaani ya kuondoa habari potofu na deepfakes mtandaoni, na mlo shuleni shuleni nchini Tanzania.Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili (UNPFII) limefungua pazia leo Aprili 20 ikiwa ni kikao cha ishirini na tano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili. Maudhim aka huu yakimulika kuhakikisha afya ya watu wa jamii za asili ikiwemo kwenye mizozo.Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI'), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Karibu Rashid Malekela utujuze zaidi.Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Karibu katika Makala yetu ya leo changu chako chako changu jumapili hii, Makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parle francophone na Muziki ambapo leo nitakuletea utamaduni wa watu kutoka huko Embu kwenye maswala ya chakula, mazazi na uvhumba. Tutamaliza na vibwagizo kadhaa vya Muziki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu Kumbuka pia kutufuatilia @billy bilali
Baada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Leah Mushi na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea nchini Sudan, juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya, na kazi za wanafunzi katika utunzaji wa mazingira huko Zanzibar.Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan.Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko hayaBaada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospitali. Flora Nducha na Taarifa zaidi
Umoja wa Mataifa leo umekuwa na tukio la kumbukizi ya siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlanitiki ambapo nchi 123 wanachama wa Umoja huo wamepitisha azimio lililoandaliwa na mataifa 58 kutambua usafirishaji wa watu wa kiafrika na utumwa kwa misingi ya rangi ya waafrika kuwa uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu. Nchi hizo 123 ni pamoja na zile wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilhali nchi 3 zilizopinga azimio ni Marekani, Israeli na Argentina. Nchi 52 hazikuonesha msimamo wowote. Mwakilishi wa Marekani akizungumza baada ya kupiga kura ya kupinga azimio hilo amesema, "tunalaani makosa yoyote yaliyofanyika kuhusiana na utumwa kuvuka bahari ya Atlantiki, jangwa la Sahara na kwingineko, lakini tumepinga azimio kwa sababu hatuoni msingi wa kulipatia kiwango cha juu hivyo cha hadhi tukio hilo. Na zaidi ya yote kama ni fidia, fidia hiyo atalipwa nani,?" amehoji.Rais wa Ghana aliwasilisha rasimu ya azimio mbele ya Baraza KuuUN/Manuel EliasRais John Mahama wa Ghana akihutubia Baraza Kuu wakati wa siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Rais wa Ghana John Mahama ambaye ni Balozi wa Muungano wa Afrika wa Kuendeleza Hali ya Haki na Fidia. Azimio hilo namba A/80/L.48 limepatiwa jina kutambua usafirishaji wa watu waliokuwa watumwa kutoka Afrika na utumwa kwa msingi wa rangi ya watu wa kiafrika kama mojawapo ya uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu. Azimio hilo lililoandaliwa na mataifa 58 yakiwemo mataifa ya Afrika Mashariki, lina vipengele 16 vya utekelezaji ikiwemo kutambua usafirishaji huo wa watumwa kutoka Afrika kuwa uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu, kurejeshwa kwa mali za kitamaduni kutoka Afrika na zaidi ya yote kulipwa fidia.Kauli ya Rais wa Baraza KuuTukio la kumbukizi lilianza kwa Annalena Baerbock Rais wa Baraza Kuu kuitisha kikao na kisha kuelekea kwenye mimbari kutoa hotuba yake akirejelea simulizi ya mtumwa Oladuk Ekwano kutoka Nigeria ya sasa akielezea machungu ya safari ndani ya meli iliyowabeba.UN/Manuel EliasRais wa Baraza Kuu la UN Annalena Baerbock akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Anasema Makumi ya mamilioni ya wengine kama Egvano walinyang'anywa kutoka kwa familia zao, nchi zao na tamaduni zao, wakafanywa watumwa na kupelekwa kufanya kazi katika nchi za kigeni—kwenye mashamba ya pamba hapa Marekani, na kwenye mashamba ya miwa na kahawa katika makoloni yaliyodhibitiwa na Ulaya. Katika maeneo ambayo leo yanajulikana kama Brazili, Barbados, Jamaica, na maeneo mengine mengi. Wote wakiwa mbali na nyumbani, mbali na familia, mbali na maisha yao.Tunatambua nchi zinazoomba radhi lakini hatua zaidi zahitajikaKwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amerejelea mateso waliyopata mamilioni ya waafrika waliotekwa nyara na kusafirishwa katika hali dhalili na kugeuzwa watumwa barani Amerika. Amesema kumbukumbu pekee haitoshi.Amebainisha kuwa mfumo huo haukuwa tu ukatili wa zamani bali pia ulikuwa msingi wa miundo ya uchumi wa dunia ambayo madhara yake yanaendelea hadi leo katika mfumo wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo na ukosefu wa usawa.UN/Manuel EliasKatibu Mkuu António Guterres akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Hotuba hiyo imesisitiza kuwa kumbukumbu pekee haitoshi. Badala yake, nchi lazima zikabiliane na dhuluma za muda mrefu zinazoendelea kuwaathiri watu wenye asili ya Kiafrika. “Kiini cha juhudi hizo, alisema, ni kutafuta ukweli, haki, na marekebisho, ikiwa ni pamoja na mijadala yenye maana na hatua kuhusu fidia,” amesema Katibu Mkuu. Guterres anasema, “Ndiyo maana Muongo wa Pili wa Kimataifa kwa Watu wenye Asili ya Kiafrika na Muongo wa Fidia wa Muungano wa…
Serikali ya shirikisho ime wasilisha sheria mpya ya kuweka marufuku ya muda, kwa baadhi ya nchi kutumia viza fulani kuja Australia.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA nchini Kenya kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya wanatekeleza mradi wa kukomesha ukeketaji ambapo waathirika wanatumika kutoa elimu kwa mabinti na jamii ili kuondokana na mila hiyo potofu. Kaunti ya Marsabit , iliyoko Kaskazini mwa nchi ya Kenya, iko mpakani na nchi ya Ethiopia. Kaunti hii ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya ile ya Turkana wakazi wake wengi ni wafugaji, na mbali na changamoto za mabadiliko ya tabianchi wanawake wa hapa wamepitia masahibu ya ukeketaji au kwa lugha ya kiingerza Female genital mutilation (FGM). Audio fileShirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) chini ya Ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya nchini Kenya wanatekeleza mradi uitwao Komesha FGM SASA Kila muathirika wa ukeketaji anayo hadithi ya kusimulia na ndio maana kwa namna ya kipekee mradi huu unawatumia waathirika hao, kuwaelimisha wanajamii wenzao ili kuondokana na tamaduni ya ukeketaji. Prisca Lekuraki ni mmoja wao. “Mimi nilipitia magumu sana, baada ya kukeketwa nilipata shida sana, ni Mungu ndio amenisaidia mpaka nimefika hapa. Nilipoenda kujifungua mtoto wangu wa kwanza nilipata shida sana, kila nikienda kuzaa nikawa napitia shida sana, sasa hivi nina watoto watatu na nikajifunga nisizae tena. Niliona vile nimeumia nikasema siwezi kukubali binti yangu naye aumie hivyo. Na hiyo ndio ilinifanya niamke niungane na wengine kuhamasisha kukataa ukeketaji.”Ameongeza kuwa katika tamaduni zao wanamila nyingi nzuri sana na wanaweza kuziendeleza na kuachana na hii mila moja ya ukeketaji kwani ni mbaya na inamadhara. Prisca amepongeza mradi wa Komesha FGM SASA wa UNFPA kwa kuwasaidia kuwafikia wale ambao awali ilikuwa ni vigumu kuzungumza nao.“Kuna mahali wametufikisha na tumeona mafanikio, hapo awali tulikuwa tunaweza kwenda kwa wamama, vijana na watoto ila wale watu ambao ilikuwa inatushinda kuwafikia ilikuwa ni wazee. Lakini hii kukutana na wazee, wamama na wanakijiji kwa ujumla imesaidia, kwasababu nilikutana na wakina mama wakaniambia ile kitu mlikuwa mnasema tumeona ni uhalisia na tumeona inaweza kufanyika.”Mwingine aliyeathirika na ukeketaji ni Nasarai Learo anasema ukeketaji umechukua nguvu zake.“Mimi sina nguvu kama yule mama ambaye hajakeketwa, nilienda kuwaambia wamama wasikekete watoto wao, lakini wakaniambia wananifahamu na nilipoolewa nilkuwa mdogo sana na wao ndio walionishika nikatetetwe nikiwa mdogo. Lakini mimi niliwaeleza mimi sikuwa najua hiki kitu ni kibaya lakini sasa hivi nimekuwa na elimu na nimejua ubaya wake.”Nasarai anaamini kuwa iwapo jamii itapata elimu basi itabadilika“Jamii yetu sanasana haina elimu, tukiona jamii yetu watu wachache ndio wamesoma na wengi wakisoma watapata hiyo elimu zaidi na watakuja kuikomesha FGM. Mimi naamini kwamba miaka 10 inayokuja mambo ya kukeketa wasichana hatutasikia tena.” Elimu ya kutokomeza ukeketaji inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni, katika vikao vya jumuiya na mashuleni.
Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia huku vita vikiendelea kushika kasi nchini Iran, masuala ya afya ya wanawake na watoto nchini Burundi, na maisha ya baadaye ya watoto katika ukanda wa Gaza.Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo.Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa.Hakuna maisha ya baadaye! Siyaoni maisha ya baadaye kwani sioni wanaoshikamana nasi! Hayo ni sehemu tu ya maoni ya watoto walioko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima, mustakabali wao uko mashakani, na wanachohitaji kama inawezekana ni amani na ujenzi mpya wa makazi ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nyumba zao na kuacha kuishi kama wakimbizi katika ardhi yao wenyewe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Tathimini mpya iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imeonya kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa duniani mwaka 2025, ikisema kuwa idadi ndogo ya nchi ndiyo inachochea mwenendo huu unaotia wasiwasi kubwa wa haki za binadamu. Flora Nducha ameisoma tathimini hiyo na hapa anafafanua zaidi
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 - 2025/26 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (2021/22 - 2025/26), Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050 na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063. Taarifa hizi zitaipima Tanzania katika hatua iliyofikia kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu; Mpango ambao unalenga kuleta usawa na kutokomeza umaskini wa aina zote ukiwemo umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma.Idara ya Habari MAELEZO
Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Venezuela operesheni ya kijeshi ya Marekani, afya ya uzazi Tana River nchini Kenya, na wanawake wakimbizi wa DR Congo wanaopitia ukatili wa kijinsia wakikimbia machafuko. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo katika kikao cha dharura baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela tarehe 3 Januari mwaka huu, hatua iliyozua hofu ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu nchini humo na katika eneo zima.Huko nchini Kenya katika kaunti ya Tana River, hali mbaya ya hewa na migogoro imesababisha takriban watu 140,000 kuyahama makazi yao. Upatikanaji wa huduma za afya nao umekuwa mgumu na kuongeza magumu hususani kwa wanawake na watoto. Katika kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya nchini humo inashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO katika kutoa huduma za afya kipaumbele kikielekezwa kwenye masuala ya uzazi salama.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), nchini Burundi, linaongeza juhudi zake kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wanaokimbia mapigano yanayoendelea mashariki taifa hilo la Maziwa Makuu ili kulinda afya, usalama na utu wao na wa jamii zinazowapokea.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), nchini Burundi, linaongeza juhudi zake kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wanaokimbia mapigano yanayoendelea mashariki taifa hilo la Maziwa Makuu ili kulinda afya, usalama na utu wao na wa jamii zinazowapokea. Sheilah Jepng'etich na taarifa zaidi
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO linaendelea na mfululizo wa programu ya kuiunganisha jamii au Social Connection ikiwa na lengo la kusaidia watu kutojitenga na kujihisi wapweke, mmoja kati ya walionufaika wa programu hiyo ni Roz, binti mwenye umri wa miaka 21 raia wa India, aliyehisi upweke mkubwa wakati baba yake alipokuwa akipambana na ulevi. Nini kilitokea na aliwezaje kuishinda hali hiyo??? Tuungane na Leah Mushi katika simulizi hii.
Polisi wametangaza shambulio la risasi nyingi huko Bondi Beach Jumapili kama shambulio la kigaidi, baada ya wanaume wawili kufyatua risasi kwa mamia ya watu waliokusanyika kwa ajili ya sherehe ya Hanukkah. Watu wasiopungua 16 wameuawa, pamoja na mtoto, katika shambulio la risasi nyingi lililosababisha vifo vingi zaidi nchini Australia tangu mauaji ya Port Arthur ya mwaka 1996. Tukio hilo limezua shutuma za kimataifa, limeongeza usalama kwenye maeneo ya Kiyahudi, limeleta hofu miongoni mwa jamii na kuzusha tena wito kutoka kwa viongozi kukemea chuki na kusimama pamoja kwa mshikamano na jamii ya Kiyahudi.
Nairobi's ride-hailing sector hits 40% electric motorcycles as Bolt logs 4.8 million EV rides. Financing from M-KOPA and Watu helps riders switch to cheaper, cleaner bikes, and local companies like Roam and Ampersand expand assembly and charging. Norway agrees to study its post-oil future after a deal with the Greens to pass the 2026 budget. EV incentives begin to scale back as adoption goals are met: https://www.ctvnews.ca/world/article/norway-to-examine-scenarios-for-post-oil-economy/. Thermostats Part 2 with Brian and James reviews the McVeggie. He wonders if it's actually just a mayo sandwich. They react to CNN's Bill Weir covering Trump's MPG rollback (full clip on Patreon: https://patreon.com/cleanenergypod) and look back at The Price Is Right giving away a $112,000 Tesla Roadster in 2010 and other EVs over the years: https://www.youtube.com/watch?v=IPq_I_L2UL4. A drone strike damages the protective shelter over the Chernobyl reactor. UN inspectors say repairs are needed, though experts caution against panic. BBC link: https://www.bbc.com/news/articles/c98nldr06l2o James wakes up to hazardous air quality as Environment Canada issues a 10+ AQHI alert. LA becomes officially coal-free after the Intermountain Power Project shuts down, ending decades of coal power for the city. More from Electrek: https://electrek.co/2025/12/08/los-angeles-power-supply-is-now-officially-coal-free/. Contact Us cleanenergyshow@gmail.com or leave us an online voicemail: http://speakpipe.com/clean Support The Clean Energy Show Join the Clean Club on our Patreon Page to receive perks for supporting the podcast and our planet! Our PayPal Donate Page offers one-time or regular donations. Store Visit The Clean Energy Show Store for T-shirts, hats, and more!. Copyright 2025 Sneeze Media.
Baadhi ya habari zinazojumuisha taarifa yetu leo, *Victoria inatarajiwa kutoa msamaha kwa watu wa mataifa ya kwanza leo *Serikali ya Northern territory imepinga ziara ya umoja wa mataifa *Australia na marekani waanza mazungumzo kuhusu usalama na pia AUKUS *idadi ya vifo vinaendelea kuongezeka sudan baada ya mashambulio wiki iliyopita Kwa habari na maelezo zaidi tembelea tovuti yetu kwa sbs.com.au/swahili.
Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui“Kila Mchango Una Umuhimu.” Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania Sabrina Saidi amezungumza na kijana ambaye anajitolea katika Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania YUNA Je kasema nini?.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, simulizi ya Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona na huduma za afya ya uzazi kwa wasichana vigori nchini Kenya.Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli.Ili kuyajadili baadhi ya masuala aliyoyagusia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, basi Diana Katabarwa wa redio washirika wetu Uhai FM amezungumza na Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona, Bahati Sanga, Katibu wa Chama Cha Wasioona, Mkoa wa Tabora.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli. Flora Nducha na taarifa zaidi
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi
Hii leo jaridani tukiendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu siku 16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, leo tunaelekea Mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusikia hisia za wanawake kuhusu ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.Watu takribani 100,000 wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR likionya kuwa mashambulizi yanaongezeka na kuyakumba hata maeneo yaliyokuwa salama. Mwakilishi wa UNHCR, Xavier Creach, amesema mgogoro “unazidi kuzorota kwa kasi ya kutisha” huku familia zikikimbia usiku gizani wakati watu wenye silaha wakivamia vijiji vyao. UNHCR inasema linahitaji dola milioni 38.2 kukidhi mahitaji yanayoongezeka.Kaskazini mwa Asia, dhoruba za kitropiki na mvua zisizo za kawaida zimesababisha vifo vya mamia na watu wengi kukimbia makazi yao, imesema WMO. Clare Nullis, msemaji wa shirika hilo, alisema Indonesia, Ufilipino, Sri Lanka, Thailand na Vietnam ndizo zimeathirika zaidi. “Tunahitaji kuzingatia kuwa Asia iko hatarini sana kutokana na mafuriko,” amesema Nullis, akibainisha kuwa dhoruba karibu na Ekweta ni nadra na jamii hazina uzoefu wa kukabiliana nazo. Indonesia pekee, watu 604 wamefariki, 464 hawajulikani walipo, na 2,600 wamejeruhiwa, huku zaidi ya milioni 1.5 wakiathirika na 570,000 wakikimbia makazi yao.Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Utumwa leo Desemba 2 Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani ILO limeonya kuhusu kuongezeka kwa utumwa wa kisasa wa binadamu, likionesha kuwa watu milioni 10 zaidi walikuwa wakiishi katika kazi za kulazimisha au ndoa za shuruti mwaka 2021 ikilinganishwa na mwaka 2016. Makadirio haya mapya yanaweka idadi ya walioathirika duniani kote kuwa watu milioni 50 huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wenye hatari kubwa zaidi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU.Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.
Mmoja kati ya Waaustralia watano, au takriban watu wazima milioni tatu, wana kiwango cha chini cha ujuzi wa kusoma na kuandika au hesabu - na hii inaweza kuwa na athari kubwa katika jinsi watu wanavyoweza kushiriki maisha ya kila siku. Programu zimewekwa kote nchini kusaidia watu kuboresha ujuzi wao na kufikia malengo yao ya maisha. Ikiwemo moja huko Tasmania, ikiwasaidia watu wazima kuwa tayari kwa kazi.
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo. Flora Nducha na taarifa zaidi
Shirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.
Dunia leo ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majiji, majiji ya kisasa pamoja na kukumbatia teknolojia yametakiwa kuhakikisha yanazingatia zaidi watu ili wengine wasiachwe nyuma au kutengwa na maendeleo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete kama anavyosimulia Flora Nducha kwa taarifa hii.
Je, unajua jinsi ya kuwapa watu mwaliko rasmi na usio rasmi?
Juhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko.Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ambao walikuwa wa kwanza kupeleka msaada kwenye eneo la tukio, Bwana John Aylieff, akiwa mjini Kabul amesema, “WFP inaweza tu kumudu kuwalisha waathirika wa tetemeko la ardhi kwa wiki chache zijazo kabla ya ufadhili kuisha.”Kwa upande wake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linapeleka msaada muhimu wa dharura kutoka maghala yake yaliyopo Kabul, ikiwemo mahema, blanketi na taa za sola. Pia maelfu ya wanajamii wa eneo hilo wameelekea eneo lililoathirika kusaidia juhudi za uokoaji, wakiwa na maji na chakula.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwaka 2016, wamekuwa wakitoa huduma muhimu ikiwemo kufunga mifumo ya maji, kujenga vyoo, na kusambaza sabuni na mahitaji mengine ya usafi.Miongoni mwa wanaofanya mabadiliko kupitia msaada huo ni Ahunga Msama, mkimbizi mwenye umri wa miaka 55 kutoka DR Congo, ambaye ni afisa msimamizii wa huduma za maji, usafi, kujisafi na usafi wa mazingiira WASH katika kambi ya Nyarugusu.(AHUNGA CLIP 1)“Ninasaidia jamii yetu ya kambi ya Nyarugusu ili wawe wanapata maji safi na salama”Ahunga anasema jamii yake iliteseka sana iliteseka sana kwa magonjwa yanayosababishwa na maji machafu ndio maana aliamua kuchukua hatua kulinda afya zao. Kila siku ahakikisha watu wanapata maji safi na huduma za usafi salama.Akiwa pamoja na wakimbizi wenzake, Ahunga anapita nyumba kwa nyumba kufundisha familia jinsi ya kuzuia magonjwa kupitia usafi kwani anaamini elimu ni ufunguo(AHUNGA CLIP 2)“Tunasaidia kuelimisha jamii yetu ili wawe wasafi. Wawe na vyoo, wawe na mabafu, wawe na vichanja na wawe na mashimo ya takataka.”Watu wakielewa, wanaweza kujilinda.Anasema watu wakieelewa ni rahisi kujilinda na juhudi zake zinaokoa maisha na kuhamasisha wengine, zikionyesha kwamba hata katika mazingira magumu, wakimbizi wanaweza kuongoza mabadiliko katika jamii zao na anasema hilo ni la muhimu sana kwani(AHUNGA CLIP 3)“Tunasaidia jamii yetu ili wajilinde na magonjwa ya milipuko”Kwa msaada wa UNHCR na Baraza la Wakimbizi la Norway, maelfu ya wakimbizi katika kambi za wakimbizi za Kigoma sasa wana maji salama, usafi wa mazingira ni bora, na wana matumaini mapya ya maisha.