POPULARITY
Karibu katika kipindi cha Huruma ya Mungu kwa Ulimwengu, Mwezeshaji ni Padre Wojceich Adam, Paroko wa Parokia ya Kiabakari na Mhifadhi wa kituo cha kitaifa cha hija cha Huruma ya Mungu, akizungumzia Dominika ya Huruma ya Mungu. L'articolo Je, unafahamu asili ya dominika ya Huruma ya Mungu? proviene da Radio Maria.
Je, umewahi kufikiria jinsi ulimwengu ulivyo mkubwa?
Je, unajua kwa nini wanasayansi hutumia mwaka wa mwanga badala ya kilomita kupima umbali wa nyota na miili mingine ya anga?
Je, umewahi kufikiria jinsi ulimwengu ulivyo mkubwa?
Ungana nami John Samky katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu, Wawezeshaji ni Melania Maziku, George Mapunda, Benedict Kessy, Monica Kessy, Katekista Gabriel Jimua na Katekista Castory Matimla, wakitufundisha juu ya changamoto za malezi ya Watoto na Vijana katika Ulimwengu wa leo. L'articolo Fahamu changamoto za malezi ya Watoto na Vijana katika Ulimwengu wa leo. proviene da Radio Maria.
Ungana nami Martin Joseph, katika Kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu Wawezeshaji ni Wakufunzi kutoka Familia bora katika Nyumba Aminifu, wakiendelea kutufundisha Changamoto za Malezi ya Watoto na Vijana katika Ulimwengu wa leo. L'articolo Fahamu mambo muhimu ya kumlea kijana katika njia bora. proviene da Radio Maria.
Makala hii imeangazia namna ambavyo nchi zetu zilivyoukaribisha mwaka wa 2025 kwa shamrashamra za kila aina huku wakisema kwaheri kwa mwaka 2024 ulioshuhudia michezo mikubwa zaidi ulimwenguni ya Olimpiki, vita ya Ukraine na kule Gaza, usalama mashariki mwa DRC, Sudan pamoja na kurejea madarakani kwa aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump.
Katika makala ya leo, Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS.
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambako mkutano wa Zama Zijazo umen'goa nanga leo kwa siku mbili za kuchua hatua kabla ya kikao cha ngazi ya juu siku ya Jumapili na Jumatatu. Leo Vijana wanapata fursa ya kupaza sauti zao kuhusu dunia na mustakbali wautakao. Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na kijana mwenye ulemavu kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa wazungumzaji wa mkutao wa leo. Anaanza kwa kujitambulisha.
Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani vijana kutoka kila kona ya dunia wanakutana kuanza kujadili kuhusu mstakabali wao katika zama zijazo. Miongoni mwao ni Jerop Limo kutoka Kenya anayetumia uzoefu wake wa kuishi na Virusi Vya Ukimwi kwa miaka 24 ya umri wake kuhakikisha ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu ambao tayari wanaishi na virusi hivyo. Anold Kayanda amezungumza naye na hapa Jerop Limo anaanza kwa kueleza yale ambayo atawaeleza viongozi wa ulimwengu.
VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Karibu katika Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Emilian Samson Mahinya, kutoka Parokia ya Uyole Jimbo Kuu Katoliki Mbeya nikijibu swali la Msikilizaji linalosema naomba kufahamu miongozo inayotolewa na Mama Kanisa kama sehemu ya kusaidia malezi ya watoto wetu, ili kuwaepusha na upotovu wa Ulimwengu wa leo . L'articolo Je, wafahamu miongozo ya Kanisa juu ya Malezi ya Watoto? proviene da Radio Maria.
Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia na Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu la Mwanza, akiendelea kutuelimisha juu ya hoja ya laana. L'articolo Je, kuna laana katika ulimwengu huu? proviene da Radio Maria.
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, sasa linataka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kuwasaka watuhumiwa zaidi wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, ambapo mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30.
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Ulimwengu umeanza kukumbatia matumizi ya akili mnemba au AI kuboresha huduma muhimu licha ya kuwa bado kukamilika mchakato wa kudhibiti matumizi ya teknolojia hiyo. Katika sekta ya afya mfumo wa AI umeanza kutumika kwenye ubainishaji wa magonjwa na ufuatiliaji wa matibabu.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Jaridani hii leo tunakuletea mahojiano kuhusu masuala ya vijana, na pi tunaangazia kazi ya walinda amani TANBAT 6 nchini DRC. Makala tunaangazia maafuriko Kalehe nchini DRC, na mashinani tunaakuletea ujumbe kuhusu watoto wanaozaliwa njiti.Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 6 cha kutoka Tanzania TANBAT 06 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wamepokea ugeni na salamu kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia ujumbe uliongozwa na Brigedia Jenerali George Mwita Itang'are aliyewakilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kutokana na sifa nzuri anazozipokea kutoka MINUSCA kuhusu kikosi hicho.Katika Mkala, George Musubao mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa huko nchini Jamhuri akizungumza na msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA nchini humo, Yvon Edoumou kuhusu mafuriko ya maji yaliyokumba eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini hivi karibuni.Katika masshinani tutasikia ujumbe wa Muuguzi, ambaye alilazimika kuacha kazi yake kwa muda ili aweze kuwalea watoto wake ambao walizaliwa njiti.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu. Wakati wa mkutano huu wa juu kabisa katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa, vijana pia hushiriki katika mikutano ya kando ili kuchangia mawazo yao katika mstakabali wa ulimwengu. Vijana wawili kutoka Tanzania Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew watawakilisha vijana wenzao wakati wa Baraza hili. Ili kufahamu mipango yao, Stell Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na mmoja wao.
Ulimwengu huadhimisha siku ya malaria kila tarehe 25 mwezi wa nne. Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaenezwa na mbu wa jenasi anayefahamika kama Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya Plasmodium. Kulingana na shirika la afya duniani Nigeria inasajili visa hivyo kwa asilimia 31.3, DRC asilimia 12.3,Tanzania kwa asilimia 4.1 na Niger kwa asilimia 3.9.Vilevile Kulingana na ripoti ya shirika la maendeleo ya Ufaransa nchini Kenya AFD ni kwamba Kisumu inaongoza kwa visa vya malaria kwa hadi asilimia 40.Na Kwenye makala haya tunazungumzia ugonjwa huu na jinsi ya kupambana nao. Nimezungumza nae Peris Oloo ambae anaugua malaria na anaelezea baadhi ya dalili alizokua nazo.kisha Daktari anaezungumzia Ugonjwa huu kwa kina na jinsi mtu anaeza uepuka.
Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Jukwaa la kudumu la watu wa asili limeanza rasmi ambapo katika ufunguzi wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na majukumu muhimu ya jamii za asili hususan katika kulinda mazingira na mbinu nyingine mbadala za maisha, watu hawa wanazidi kuwa masikini na kuzitaka nchi zote duniani zihakikishe zinawasaidia kuondokana na umasikiniAkizungumza katika jukwaa hilo la 22 Guterres amesema jamii za watu wa asili zinawasilisha utofauti mzuri na mkubwa duniani kwani kuna tamaduni tofauti zaidi ya 5000 zinazo zungumza zaidi ya lugha 4000 tofauti.Hata hivyo pamoja utajiri huu wa mila na destuli duniani lakini bado watu hawa wanakabiliwa na changamoto lukuki tena zinazo fanana.Ametaja changamoto hizo kuwa ni kutengwa, kukandamizwa, kunyimwa haki za binadamu, unyonywaji, kuchukua kiharamu maeneo yao yenye rasilimali nyingi, kuondolewa kwenye ardhi zao za asili na hata mashambulizi ya kimwili na kufanyiwa vurugu.Kwa bahati mbaya zaidi pamoja na wanawake wa jamii ya asili kuwa ndio watunzaji wa urithi tajiri sana wa asili zao lakini wao ndio mara nyingi huteseka zaidi.Guterres amesema “Udhalimu wa vizazi kwa vizazi vya ubaguzi unajidhihirisha katika ukosefu wa usawa ambao unashangaza. Jamii za watu wa asili ni takribani asilimia tano ya idadi ya watu duniani, pamoja na uchache wao lakini wao ni asilimia 15 ya watu maskini zaidi duniani.”Guterres amesema ujumbe wake uko wazi kabisa, Umoja wa Mataifa unasimama nao katika kudai haki zao na ametaka washirikishwe kwenye kutafuta suluhu za changamoto za ulimwengu kwenye masuala mbalimbali akitolea mfano afya na mabadiliko ya tabianchi ambapo dunia sasa inahamasishwa kujikita kwenye uchumi wa kijani.Amesema “Hii dhana ya uchumi wa kijani sio mpya kwa watu wa asili wamekuwa wakiitumia kwa zaidi ya milenia. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye hekima, ujuzi, uongozi, uzoefu, na mifano yao.”Amezipongeza pia jamii za asili kwa ushiriki wao kwenye masuala kadhaa kama vile Mkataba wa Anuwai za Kibiolojia na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote kuiga mfano wa UN na kufanyakazi pamoja na jamii za watu wa asili katika kutokomeza changamoto za uhaba wa chakula na kupunguza pengo la kidijitali kwa kuhakikisha huduma zinawafikia.Pia ametaka washirikishwe kwenye utungaji wa sera na utekelezaji wa programu mbalimbali katika ngazi zote huku wakitoa fursa kwa watu wa asili kupaza sauti zao.
Mashirika manne ya kimataifa yakiwemo matatu ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza mpango wa kimataifa wa ‘Afya Moja' au ‘One Health', hii leo yametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa ili kujenga mifumo imara ya afya kufanikisha kukabiliana na changamoto ngumu za kiafya zinazoukabili ulimwengu. Taarifa iliyotolewa hii leo mjini Roma-Italia, Paris-Ufaransa, Geneva-Uswisi na Nairobi-Kenya imeeleza kuwa katika mkutano wao wa kila mwaka uliofanyika kwa mara ya kwanza ana kwa ana, wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo (FAO), la Mpango wa Mazingira (UNEP), la Afya Ulimwenguni (WHO) pamoja na mdau wao Shirika la Afya ya Wanyama Ulimwenguni (WOAH) wameeleza kuwa changamoto za kiafya zinazoukabili ulimwengu zimeonesha hitaji la mifumo thabiti ya afya na hatua za haraka za kimataifa. Kwa pamoja mashirika hayo manne yanalenga kufanikisha kwa pamoja kile ambacho sekta moja haiwezi kukifanikisha peke yake yaani mpango wa Afya Moja ambao unaonekana kuwa njia kuu ya kukabiliana na changamoto ngumu zinazokabili ulimwengu kama vile dharura za kiafya kimataifa za hivi hivi karibuni kama vile janga la COVID-19, Mpox, milipuko ya Ebola, na kuendelea kwa vitisho vya magonjwa mengine yanayotokana na Wanyama, uhakika wa chakula, usugu wa vijiumbe maradhi, uharibifu wa mfumo wa ikolojia na mabadiliko ya tabianchi. Wakisisitiza haja ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa na kujitolea kutafsiri mbinu ya Afya Moja katika utekelezaji wa sera katika nchi zote, viongozi wa Mashirika hayo manne yanayoshirikiana wanahimiza nchi zote na wadau wakuu kuendeleza na kuchukua hatua saba za kipaumbele: Mosi, kuupa mpango wa Afya Moja katika ajenda ya kimataifa ya kisiasa, kuongeza ufahamu na kuhamasisha kupitishwa na kukuza utawala bora wa afya kati ya sekta mbalimbali.Pili, kuimarisha sera, mikakati na mipango ya kitaifa ya Afya Moja. Tatu, kuharakisha utekelezaji wa mipango ya Afya Moja. Nne, kujenga nguvu kazi za Afya Moja zinayoshirikisha sekta mbalimbali. Tano, kuimarisha na kudumisha uzuiaji wa magonjwa ya milipuko na matishio ya kiafya katika chanzo. Sita, kuhimiza na kuimarisha maarifa ya kisayansi ya Afya Moja na uundaji na ubadilishanaji wa ushahidi. Na saba, kuongeza uwekezaji na ufadhili wa mikakati na mipango ya Afya Moja. Afya Moja ni mbinu jumuishi iliyoundwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa ambapo wadau mbalimbali wanashirikiana katika kutatua changamoto za kiafya kwa wanadamu, wanyama na mazingira.
Wahisani wa kimataifa wanakutana leo mjini Geneva UswisI kwa ajili kutanabaisha kuhusu zahma ya kibinadamu inayoendelea nchini Yemen na kuchangisha fedha za kufadhili operesheni za kibinadamu nchini humo. Mkutano huo wa ngazi ya juu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Yemen umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na serikali za Sweden na Uswis. Flora Nducha na taarifa kamili Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Yemen inasalia kuwa moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani , na baada ya miaka mingi ya vita inaendelea kuwa na dharura kubwa kibinadamu kwani watu zaidi ya milioni 21 au theluthi mbili ya watu wote katika taifa hilo la Mashariki ya Kati watahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi mwaka huu 2023. Sababu kubwa za kuendelea kwa mgogoro wa kibinadamu mbali ya vita ni kudorora kwa uchumi na kusambaratika kwa huduma za msingi. Umoja wa mataifa pia umesema Yemen iko katika kitovu cha mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi ikikabiliwa na majanga ya asili ya mara kwa mara kama ukame wa kupindukia na mafuri yanayotishia maisha ya watu, usalama na ustawi wao. Mashirika ya misaada ya kibinadamu “Yanahitaji dola bilioni 4.3 mwaka huu 2023 ili kusaidia watu milioni 17.3 kote nchini kwani bila msaada endelevu kwa operesheni ya misaada nchini Yemen, maisha ya mamilioni ya Wayemen yatabaki hatarini na juhudi za kumaliza mzozo huo mara moja zitakuwa ngumu zaidi.” Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kuongeza kuwa "Jumuiya ya kimataifa ina uwezo na mbinu za kumaliza mgogoro huu. Na huanza kwa kufadhili ombi letu kikamilifu na kuahidi kutoa fedha haraka. Kwa pamoja, hebu hatimaye tugeuze wimbi hili la mateso. Tuwape matumaini watu wa Yemen.” Kwa upande wake, mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Martin Griffiths, amesema: "Ulimwengu unakutana tena leo kudhihirisha dhamira yake ya kuwasaidia watu wa Yemen kujinasua kutoka katika mgogoro huu mbaya. Hiyo ina maanisha ni kuendelea, na kwa kweli kuongeza maradufu, juhudi za kutafuta suluhu ya amani. Inamaanisha kufadhili operesheni za misaada ili programu za kuokoa maisha ziweze kuendelea kuzuia hali mbaya zaidi. Na inamaanisha kusaidia mashirika ya misaada yanapofanya kazi kuchukua hatua za kukabiliana na mgogoro huo nchini kote.” Mwaka 2022 wahisani walitoa dola zaidi ya bilioni 2.2 ambazo ziliwezesha mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwafikia karibu watu milioni 11 nchini humo kila mwezi kwa misaada ya kuokoa maisha ikiwemo chakula, maji safi, malazi, ulinzi na elimu.
Ulimwengu uliukaribisha mwaka mpya kwa sherehe iliyojaa watu huko Times Square New York na fataki zilizotanda anga katika miji mikuu ya Ulaya, huku kukiwa na matarajio ya kumalizika kwa vita nchini Ukraine na kurejea kwa hali ya kawaida ya baada ya COVID-19 huko Asia.
Ulimwengu umeendelea kuomboleza kwa masikitiko kifo cha mcheza soka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento, almaarufu Pelé. Kwa Umoja wa Mataifa Pelé alikuwa mshambuliaji muhimu katika kufanikisha ushindi wa malengo ya Umoja wa Mataifa. Kwa nyakati tofauti akiteuliwa kuwa Balozi Mwema wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na kuhudumia watoto UNICEF. UN News kupitia Idhaa ya Kireno imepata fursa ya kuzungumza na mtoto wake wa kiume na mkewe kuhusu Pelé nje ya uwanja.....Ni Monica Grayley wa Idhaa ya Kireno ya Umoja wa Mataifa akimkaribisha Joshua Nascimento mmoja wa watoto wa kiume wa Pelé. Na baada ya mazungumzo kuhusu namna Pelé alivyowalea kwa adabu japo bila kuwaadhibu sana, swali likawa…ni kwa namna gani ungependa baba yako akumbukwe kwa vizazi vingi vijavyo?Joshua Nascimento anajibu kuwa angependa baba yake kwanza akumbukwe kama mchezaji bora kama alivyokuwa wakati wake na mafanikio yote aliyokuwa nayo kwa mchezo huo lakini pia mambo aliyoyafanya nje ya mchezo, mambo aliyoyafanya kwa nchi yake ya Brazil na hasa kwa watoto hata pale alipofunga goli lake la 1000 alisema ni kwa ajili ya kuwajali watoto.Kijana Joshua alikuwa akiyasema haya akiwa ameketi na mama yake mzazi, Assiria Lemos, mke wa zamani wa Pele naye anajibu swali kama hilo la Je, angependa Pelé akumbukwe vipi? Anasema ukiacha kile ambacho kila mtu anakifahamu kuwa Pele alikuwa mcheza mpira wa miguu wa kiwango cha juu, lakini pia kama mtu tu binafsi alikuwa,(Sauti ya Assiria Lemos)“mstahimilivu, mnyenyekevu, mkarimu, mwenye roho nzuri, mtu wa familia anayejali watu wa familia yake na watu wenye uhitaji. Roho nzuri.”
Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 30 mwezi Desemba mwaka 2022 tunakuletea habari za maombolezo na pia ya uteuzi wa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa UNEP. Makala tunaelekea nchini Kenya katika makazi ya wakimbizi ya Kalobeyei na mashinani tunaangazia haki za wanawake na wasichana Afghanistan.Ulimwengu umeendelea kuomboleza kwa masikitiko kifo cha mcheza soka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento, almaarufu Pelé. Kwa Umoja wa Mataifa Pelé alikuwa mshambuliaji muhimu katika kufanikisha ushindi wa malengo ya Umoja wa Mataifa. Kwa nyakati tofauti akiteuliwa kuwa Balozi Mwema wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na kuhudumia watoto UNICEF.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumanne wiki hii alimtangaza Elizabeth Maruma Mrema kutoka nchini Tanzania kuwa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEPMakala tunaelekea nchini Kenya katika makazi ya wakimbizi ya Kalobeyei kuangazia mradi unaotumia michezo kulinda vijana hasa wa kike dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.Na mashinani tuungane na Ramiz Alakbarov, naibu mwakilishi na mratibu mkazi na wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan akisistiza umuhimu wa haki za wanawake kuheshimiwa.
Pelé alikuwa mmoja wa wachezaji mahiri wa mpira wa miguu na muda wote alitikisa michuano ya Kombe la Dunia kwa Brazil katika michezo ya klabu pamoja na ziara za kimataifa na timu yake ya Santos kabla ya kuleta msisimko wa mchezo wa soka kwa klabu ya soka ya kulipwa ya Marekani, New York Cosmos
Ulimwengu waendeleza kampeni ya siku 16 za kutokomeza dhulma dhidi ya wanawake na wasichana, huku utafiti uliofanywa nchini Rwanda ukieleza wanawake 6 kati ya 10, walioko kwenye ndoa wanapigwa na waume zao.
Ulimwengu waendeleza kampeni ya siku 16 za kutokomeza dhulma dhidi ya wanawake na wasichana, huku utafiti uliofanywa nchini Rwanda ukieleza wanawake 6 kati ya 10, walioko kwenye ndoa wanapigwa na waume zao.
Ushirikiano kati ya Rwanda na Umoja wa Mataifa ambao umedumu kwa miaka 60 sasa tangu taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga uanachama kwenye Umoja wa Mataifa ni wa manufaa kwa pande zote amesema Josephine Ulimwengu ambaye ni mratibu na mkuu wa miapango wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda . Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini Kigali Rwanda ambako leo kumefanyika maadhimisho ya miaka 60 ya uanachama wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa yaliyoandaliwa kwa pampoja na serikali ya Rwanda na Umoja wa Mataifa nchini humo yakibeba maudhui "Ushirikiano kwa ajuli ya mustakbali wa pamoja kwa wote" anafafanua baadhi ya mafanikio hayo
Baadhi ya changamoto zilizoangaziwa ,ambazo mtoto wa kike anapitia ni pamoja na ndoa za mapema, ukeketaji, na ukosefu wa usawa wa kijamii miongoni wa nyingine.
Baadhi ya walimu kutoka mataifa ya Afrika mashariki watoa maoni yao kuhusu siku hii, wakati kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni 'Uimarishwaji wa elimu unaanzia kwa walimu.'
Kuanzia wiki hii viongozi wa ulimwengu wanamiminika jijini New York Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kushiriki Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mambo kadhaa yatajadiliwa ikiwemo amani, haki za binadamu, uchumi na kuilinda sayari dunia dhidi ya uharibifu unaochochea majanga. Ulimwengu tayari umebaini kuwa changamoto zimefungana na hivyo majawabu yanapaswa kutafutwa kwa kushirikiana. Katika maeneo ambayo ushirikiano umefanyika ili kutafuta ufumbuzi wa jambo, matunda yameonekana. Mathalani nchini Tanzania, shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wananchi wa wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wanaendelea na mradi wa kutatua changamoto ya umeme na maji, masuala mtambuka ambayo yanagusa sekta nyingine kama elimu, afya, uchumi na mazingira. Mradi wa umeme wa nishati ya jua kupitia ufadhili wa shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF umeanza kuzaa matunda kwa wananchi kama anavyosimulia Jongo Sudi wa redio washirika Ruangwa FM.
Uingereza na Ulimwengu wanaomboleza kifo cha Malkia Elizabeth wa pili ambaye alifariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 96. Elizabeth atakumbukwa kama kiongozi aliyedumisha umoja na upendo kati ya raia wa Uingereza.
Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI. Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake. Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa. Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung'amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani. Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake. Yangu matumaini uta enjoy sana. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Ulimwengu huu wa utandawazi umewapa wengi fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kuweka picha zao kujifurahisha na hata kuwafurahisha wengine. Kuna wale huweka picha wakiwa wamevalia nadhifu, wengine kujianika nusu uchi na kadhalika. Je, mwonekano wa mtu katika picha anazoweka mitandaoni unaweza kuchangia apate mchumba ama akose, hasa kwa wanaolenga kuwapata wachumba? Tumezunguma na wananchi kuihusu mada hii vilevile kupata wosia wa mshauri Bi. Rachel Mahungu.
World News in 7 minutes. Monday 11th July 2022.SURVEY FINISHES TOMORROW: https://s.surveyplanet.com/9wij432s or send7.orgToday: Japan Abe murder. Sri Lanka palace stormed. Rajapaksa resigns. US Biden abortion order. Twitter sues Musk. South Africa shootings. Mexico, Angola ex presidents die. Ukraine updates. UK Wimbledon done.Start Up Rad.io: https://startuprad.io/Support us and read the transcripts at send7.org/transcriptsPlease leave a rating on Apple podcasts or Spotify.With Stephen Devincenzi.Contact us at podcast@send7.org or send an audio message at speakpipe.com/send7If you enjoy the podcast please help to support us at send7.org/supportSEND7 (Simple English News Daily in 7 minutes) tells the most important world news stories in intermediate English. Every day, listen to the most important stories from every part of the world in slow, clear English. Whether you are an intermediate learner trying to improve your advanced, technical and business English, or if you are a native speaker who just wants to hear a summary of world news as fast as possible, join Stephen Devincenzi and Namitha Ragunath every morning. Transcripts can be found at send7.org/transcripts. Simple English News Daily is the perfect way to start your day, by practising your listening skills and understanding complicated stories in a simple way. It is also highly valuable for IELTS and TOEFL students. Students, teachers, and people with English as a second language, tell us that they listen to SEND7 because they can learn English through hard topics, but simple grammar. We believe that the best way to improve your spoken English is to immerse yourself in real-life content, such as what our podcast provides. SEND7 covers all news including politics, business, natural events and human rights. Whether it is happening in Europe, Africa, Asia, the Americas or Oceania, you will hear it on SEND7, and you will understand it. For more information visit send7.org/contact
Makala ya wiki hii imeangazia kwa kiasi kikubwa tahadhari inayoshuhudiwa hivi sasa kote ulimwenguni baada ya kuenea sehemu mbali mbali ya dunia kwa taarifa kuhusu maambukizi ya kirusi kilichogunduliwa huko Afrika kusini, pamoja na mambo mengine mengi. Karibu kujiunga na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 leo umeng'oa nanga rasmi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani ukifanyika moja kwa moja na pia kupitia mtandaoni ukiwaleta pamoja nchi 193 wanachama wa Umoja huo. Flora Nducha na taarifa zaidi Abdullah Shahid Rais wa Baraza Kuu akifungua mjadala huo ambao umebeba mada ya “Kujenga mnepo kupitia tumaini la kujikwamua kutoka kwa janga la COVID-19, kushughulikia mahitaji ya sayari dunia, kuheshimu haki za watu, na kuufufua Umoja wa Mataifa. " Hii ni mara ya pili mjadala huu unafanyika wakati janga la COVID-19 likiendelea tofauti na mwaka jana ambapo kwa asilimia kubwa ulifanyika kwa njia ya mtandao mwaka wakuu wa nchi za serikali wachache wanashiriki kupitia mtandao na wengine takriban 100 wako moja kwa moja kwenye ukumbi wa Baraza Kuu akiwemo Katibu Mkuu Antonio Guterres ambaye amesema. “Niko hapa kupiga kengele ulimwengu lazima uamke. Tuko ukingoni mwa dimbwi na tunaenda katika mwelekeo mbaya. Ulimwengu wetu haujawahi kupata tisho zaidi ya hili au kugawanywa zaidiya sasa. Tunakabiliwa na mtafaruku mkubwa katika maisha yetu. Janga la COVID-19 limezidisha pengo la usawa, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi unaipiga dunia, machafuko kutoka Afghanistan hadi Ethiopia hadi Yemen na kwingineko yamezuia upatikanaji wa amani.” Ametaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa hali ya kutoanimiana duniani, kuendelea kubinywa kwa haki za binadamu, kushanmbuliwa kwa sayansi na migongano ya kiuchumi. Kwa upande wa janga la COVID-19 amesema hakuna mshikamano kwa vitendo, wakati huu ambao unahitajika kuliko wakati mwingine wowote, kwani ubinafsi umetawala na utu umetoweka "Taswira tuliyoiona katika baadhi ya nchi kuhusu chanjo ya COVID-19 , ziko majalalani, muda wake umekwisha na hazijatumika. Na kwa upande mwingine tunashuhudia chanjo zikizalishwa kwa kasi isiyo ya kawaida, ambao ni ushindi wa kisayansi na ujuzi wa kibinadamu.. Lakini kwa upande mwingine tunaona ushindi huu ukisambaratishwa na janga la kutokuwa na utashi wa kisiasa, ubinafsi na kutoaminiana. Kuna ziada katika baadhji ya nchi , wakati kwingineko hawana chochote, watu wengi katika nchi Tajiri wamechanjwa, lakini zaidi ya asilimia 90 ya Waafrika bado wanasubiri dozi ya kwanza. Haya ni mashtaka ya kimaadili ya hali ya ya dunia yetu. Ni uchafu, tumefaulu mtihani wa sayansi, Lakini tunapata F katika maadili.” Amesisitiza kwamba huu ni wakati wa kutambua mbivu na mbichi, wakati wa kutekeleza kwa vitendo, wakati wa kurejesha uaminifu , wakati wa kuchagiza matumaini, kwani yeye anayo matumaini . Ametaja mambo sita ya kuzingania ambayo mosi ni kuhakikisha kuna amani, pili lazima kupata kushikimana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tatu lazima kuziba pengo la baina walionacho na wasio nacho, nne lazima kumaziba pengo la usawa wa kijinsia, tano kurejesha uaminifu na kuchagiza matumaini na sita lazima kuziba pengo baina ya vizazi. Naye Rais wa Baraza Kuu Abdulla Shahid katika hotuba yake ametaja mambo matano muhimu kuweza kukabiliana na changamoto zote zinazoikabili dunia kwa hivi sasa akisema Kama ulivyo utaratibu wa kila mwaka katika mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amekuwa mjumbe wa kwanza kuwasilisha taarifa yake akifuatia na Rais Joe Biden wa Marekani , lakini nchi zote wanachama zinatarajiwa kuzungumza katika mjadala huo utakaojikita pia katika masuala ya kumbukumbu ya miaka 20 ya azimio la Durban, mifumo ya chakula, nishati, mabadiliko ya tabianchi na kumuenzi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO iliyotolewa hii mjini Geneva, Uswisi yenye jina 'Hali ya ulimwengu kuhusu hatua za afya ya umma dhidi ya tatizo la kusahau', inasema ni robo tu ya nchi zote ulimwenguni ambazo zina sera, mkakati au mpango wa kitaifa wa kusaidia watu walio na ugonjwa wa shida ya akili unaosababisha kupoteza kumbukumbu na hali nyingine kama kushindwa kufikiria vizuri. (Taarifa ya Jason Nyakundi) Ripoti hiyo kifafanua zaidi imeeleza kuwa nusu ya nchi hizi ziko katika Kanda ya Ulaya ya WHO, na sehemu iliyobaki imegawanyika kati ya maeneo mengine ya ulimwengu. Wakati huo huo barani Ulaya mipango mingi iliyokuwepo kushughulikia tatizo hili la kupoteza kumbukumbu au dementia, imekwisha muda wake na hivyo ikionesha hitaji la serikali kujitolea upya kuweka mipango madhubuti ya kupambana na hali hii. Mkurugenzi wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amenukuliwa akisema, "ugonjwa wa kusahau unawaibia mamilioni ya watu kumbukumbu zao, uhuru na utu, lakini pia unatuibia sisi watu tunaowajua na tunaowapenda. Ulimwengu unawaangusha watu walio na shida ya akili, na hiyo inatuumiza sisi sote. Miaka minne iliyopita, serikali zilikubaliana malengo ya wazi ya kuboresha huduma za dementia. Lakini malengo pekee hayatoshi. Tunahitaji hatua za pamoja ili kuhakikisha kuwa watu wote walio na shida ya akili na kupoteza kumbukumbu wanaishi na msaada na hadhi inayostahili.” Aidha, WHO inaeleza kuwa idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa shida ya akili na hivyo kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri, inaongezeka ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 55, ikiwa asilimia 8.1 ya wanawake na 5.4% ya wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 65 wanaishi na shida ya dementia. Idadi hii inakadiriwa kuongezeka watu milioni 139 ifikapo mwaka 2050. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na WHO, Ugonjwa wa kusahau husababishwa na magonjwa tofautitofauti na majeraha ambayo huathiri ubongo, kama ugonjwa wa Alzheimers au hata kiharusi. Ugonjwa huu unathiri kumbukumbu na kazi nyingine za utambuzi, pamoja na uwezo wa kufanya kazi za kila siku.
Ukosefu wa ajira ni moja ya matatizo yanayoendelea kuukumba ulimwengu na hasa ikizingatiwa kuwa wahitimu katika ngazi mbalimbali ni wengi, lakini nafasi za ajira haziongezeki na pia kwa namna fulani kutokana na maendeleo ya teknolojia, nafasi hizo zinazidi kupungua. Nchini Tanzania, kijana Underay Mtaki ameligundua hilo na sasa anatumia ubunifu wake, ujuzi na elimu ya darasani kujiajiri kwenye sanaa ya uchoraji ili kuondokana na changamoto ya kukosa ajira na kujishughulisha na kazi zenye staha kama lisemavyo lengo namba nane katika malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Lucy Igogo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania amezungumza na kijana huyo na kuandaa makala ifuatayo.
Fainali ya michuano ya riadha ya mita 100 katika michezo ya Olimpiki mjini Tokyo, Japan ilikuwa yakipekee.
MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU Mungu wa madhabahu Kuhani wa madhabahu Washirika wa madhabahu Kafara ya madhabahu Nguvu ya madhabahu --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Ndoto kwa kawaida ya wanaadamu katika ulimwengu wa mwili ni mambo unaunayoyaona wakati umelala mara nyingi ndoto utaota wakati umelala Aina za ndoto kwa tafsiri za ulimwengu wa kimwili - Ndoto unaota kwa sababu umechoka sana mara nyingi ukiota hivyo watu na wewe mwenyewe unasema kua ni ndoto tu kwa sababu ni uchovu - Ndoto unaota kwa sababu una mawazo kwa kitu kinakufanya ukifikirie sana mfano ajira au mke au mume ukiota mara nyingi unasema ni ndoto tu kwa sababu namuwaza sana au unawaza sana - Ndoto unaota kwa sababu umehadithiwa au kuambiwa kitu Fulani kabla haujalala harafu unaota hivyo hivyo. Sasa hayo yote ni katika Ulimwengu wa kimwili tuangalie katika ulimwengu war oho ndoto ni nini? - Ndoto maana yake ni ( Hesabu 12:6) BWANA akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa BWANA miongoni mwenu, ninajifunua kwake kwa maono, ninanena naye katika ndoto. Maana yake kwamba Mungu anaongea na watu wake kwa kupitia ndoto na maono ila watu wengi ukiota unasema ni ndoto tu Kila ndoto unayoota inawezekana ikawa inakuhusu wewe au ndugu,jirani,mwenza,rafiki au mtu yeyote ambaye Mungu anakuonesha kitu juu yake na ukiwa unafatilia ulichokiota kwa makini unatakiwa uishi katika ndoto au maono yako anayokunesha Mungu @siri za biblia www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Mashirika ya kimataifa yamekutana kuzindua Jopo jipya la kitaalam la ngazi ya juu kuhusu afya ili kuboresha uelewa wa jinsi magonjwa yenye uwezo wa kusababisha magonjwa ya milipuko, yanavyoibuka na kuenea. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.
Mitungi milioni 4 ya oksijeni yahitajika duniani kote kila siku kwa wagonjwa wa COVID-19. Ulimwengu wajipanga kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoanzia kwa wanyama.
CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Ulimwengu ukiwa katika muongo wa kuelekea kufikia utimizaji wa malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030, shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania, Restless Development, lina imani kubwa kwa vijana kuwa wamekuwa na wanaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha malengo hayo hivyo uwekezaji mkubwa inabidi uendelee kuelekezwa kwa kundi hili hasa katika kuwajengea uwezo wa uongozi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake wa kuadhimisha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Tafakari kuhusu Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 Dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.alioutoa kwa njia ya video, amesema wakati huu dunia inapojiunga katika mshikamano na watu wa Rwanda, ni lazima kuangalia sana ulimwengu wa leo na kuhakikisha kwamba tunazingatia masomo ambayo wanadamu waliyapata kutokana na tukio hilo la miaka 27 iliyopita ambapo zaidi ya watu milion
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akihutubia Kikao cha 65 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW65 mjini New York Marekani, amesema "hali ya wanawake ni hadhi ya demokrasia," akiongeza kwamba Marekani imedhamiria kutekeleza maadili ya kidemokrasia yaliyoko katika Azimio la Ulimwengu haki za binadamu.
Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. (Ufunuo 13:1-9). Tumeona kuwa kila atakayekataa kupigwa ile chapa ya utawala, atafuatiliwa, atatengwa, atateswa na hata kuuawa. Lakini kwa wale ambao watakuwa wamekubali kupokea chapa ya utawala huo, wataonekana kana kwamba wana raha, maana watapewa mahitaji yao ya kila siku na serikali. Lakini baada ya utawala huo kufikia mwisho, watakutana sasa na Mfalme wa wafalme, Yesu Kristo. Biblia inasema: Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. (Ufunuo 14:9-10). --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Naamini watu wengi wameshasikia juu ya kile kinachojulikana kama Mpango Mpya wa Ulimwengu (New World Order). Hata hivyo, wapo pia wengine wengi ambao hawana habari juu ya kile kinachoendelea kuhusiana na mpango huu. Mpango Mpya wa Ulimwengu ni mpango wenye nia ya kuusuka ulimwengu upya ili uweze kuwa tofauti na ulivyo sasa; ili uweze kuendana na malengo ya hao wanaoutaka. Mpango huu ni mkakati kabambe unaosimamiwa na watu wenye nguvu duniani, yaani wenye nguvu za kiuchumi, kisiasa, na hata kiroho. Malengo ya mpango huu ni mengi. Kati yake ni haya yafuatayo: Kuwa na serikali moja inayotawala dunia yote. Kuwa na mfumo mmoja wa fedha duniani kote. Kuwa na uchumi mmoja duniani kote. Kuwa na dini moja duniani kote. Kuwa na jeshi moja linalosimamia ‘amani' duniani kote. Kuwa na dunia yenye watu wasiozidi bilioni moja tu. Kuwa na makundi mawili tu ya watu, yaani watawala na watumishi. Utawala utakuwa ni wa kurithi; si wa kuchaguliwa. Yaani unakuwa mikononi mwa kundi lilelile. Kutokuwapo kwa mipaka iliyopo leo ambayo inatenganisha mataifa. Kuwa na udhibiti kikamilifu juu ya kila mwanadamu ambaye atakuwapo duniani wakati huo. --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Kipindi hiki nilikibuni makusudi kutusaidia sisi binadamu kujua maana ya mtazamo na amani na kisha kuziunganisha kwa manufaa ya Ulimwengu na walimwengu wake☺️ --- Send in a voice message: https://anchor.fm/unityradio254/message
SEMINA YA NENO LA MUNGU FEBRUARY 2021 DAR ES SALAAM,VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Wengi wamehusishwa kurithi ufalme wa Lionel Messi na Christiano Ronaldo lakini hawakuweza kufikia kiwango chao. Je, Kylian Mbappé na Erling Braut Haaland wataweza kufikia kiwango cha Messi na Ronaldo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili namna makinda hawa wanavyotengeneza ulimwengu wao wa soka. Tunaangazia zaidi takwimu za mchezo na namna wanavyosaidia timu zao kuweza kupata matokeo. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa mtumishi wake Mwalimu Christopher Mwakasege mwezi wa pili jijini Dar Es Salaam.akifundisha kuhusu MSAADA WA MUNGU KWA ULIMWENGU KATIKA MABADILIKO YA MSIMU HUU MPYA.jifunze maarifa haya muhimu kwa maisha yako kiroho --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
FUATILIA ZAIDI MAFUNDISHO MBALIMBALI KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU KUPITIA PODCAST YA SIRI ZA BIBLIA NA MITANDAO YOTE YA KIJAMII. LEO TUPO NA MTUMISHI WA MUNGU,MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE WA MANA MINISTRY KUTOKA NCHINI TANZANIA.SEMINA HII IMEFUNDISHWA JIJINI DAR ES SALAAM FEBRUARI 2021 "MSAADA WA MUNGU KWA ULIMWENGU KATIKA MABADILIKO YA MSIMU HUU MPYA" --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Zab 46:1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Msaada wa Mungu kwa ulimwengu katika mabadiliko ya msimu huu mpya --- Send in a voice message: https://anchor.fm/siri-za-biblia/message
Ulimwengu ukiwa katika siku 16 za kuhamasisha kupinga ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na wasichana, takwimu zinaonesha kuwa wakati huu wa janga la COVID-19, wanawake wengi zaidi wamedhulumiwa kwa namna moja au nyingine.
Ulimwengu ukiwa katika siku 16 za uhamasishaji wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, pamoja na mengine, jamii inakumbushwa kuhusu lengo namba 5 la malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendelepo endelevu, SDGs, lengo ambalo linahamasisha kuhusu usawa wa kijinsia. Lakini jamii za ulimwengu zilifikaje katika kuwa na pengo la usawa wa kijinsia kwa kiasi hiki cha kuwa na uhitaji wa kukumbushwa? Bi.
Ulimwengu uko katika muongo wa kuelekea utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu. Lengo namba 8 linaongelea kazi bora au zenye hadhi pampja na ukuaji wa uchumi. Lengo hilo ni vigumu kulifikia iwapo hakuna maandalizi ya kutosha kwa wale wanaoandaliwa kufanya kazi na hivyo hali hiyo itasababisha sehemu ya pili yaani ukuaji wa uchumi nayo kutokufikiwa. Kwa msingi huo, ndipo asasi ya Umoja wa Mataifa ya vijana, YUNA Tanzania imeamua kuendesha mradi wa kuwapa nafasi vijana waliohitimu masomo na hata walioko masomoni bado ili wapate mafunzo kwa vitendo.
Ulimwengu unaadhimisha miaka 30 ya Siku ya Wazee duniani tunapotathimi athari mbaya na kali ambazo janga la COVID-19 limesababisha kwa wazee ulimwenguni kote, sio tu kwa afya zao, bali pia juu ya haki zao na ustawi wao, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa hii leo kuhusu Siku ya leo ya Kimataifa ya wazee duniani na kisha akashau
Fikra za baadhi ya watu kuwa maelfu kwa maelfu ya watu barani Afrika watapukutika kutokana na janga la ugonjwa wa Corona, au COVID-19 zimekuwa ndivyo sivyo baada ya bara hilo kuchukua hatua kitaifa na kikanda na hatimaye hadi sasa kudhihirisha umuhimu wa mshikamano katika kukabili adui.
Maneno yaletayo faraja
Maneno yaletayo faraja
Maneno yaletayo faraja
Makala ya wiki hii imeangazia ulimwengu wa wakristo ulivyoikaribisha sikukuu ya krismas mwaka 2019, mwendelezo wa mauaji katika baadhi ya vijiji wilayani Beni mashariki mwa DRC, mazungumzo kuhusu upatikanaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Sudan kusini, kurejelewa mwezi february mwakani, pia kuendelea kwa mgomo wa kitaifa nchini Ufaransa kufwatia mpango wa marekebisho ya mfumo wa pensheni
Ulimwengu unaadhimisha siku ya kisukari duniani huku idadi ya watu wanaougua maradhi hayo ikiongezeka kutoka milioni 108 mwaka 1980 hadi milioni 420 mwaka 2014. Mtindo wa maisha unatajwa kuwa mojawapo ya sababu. Je kubadili mtindo wa maisha kunaweza kusaidia kukabiliana na maradhi haya? Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji.
Ulimwengu leo unaadhimisha siku ya wafanyakazi huku wafanyakazi wakikabiliwa na changamoto mbalimbali. Je serikali za Afrika zinatia juhudi katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu.
Ulimwengu wa Muziki wa Rock and Roll wamlilia mwanamuziki wa miondoko hiyo kutoka Ufaransa Johnny Hallyday ambae alifariki usiku wa Desemba 5 kuamkia Desemba 6. Kufahamu zaidi kuhusu mwanamuziki huyo ambatana naye Ali Bilali katika makala haya Muziki Ijumaa unaweza pia kumfollow kwa instagram @billy_bilali/