POPULARITY
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akiwa barani Afrika; na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani. Makala tunakwenda nchini Burundi na mashinanitunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani barani Afrika ambapo juzi tarehe 7 aliingia nchini Gambia, kwa njia ya mtandao wa X ameonesha namna ziara yake ilivyokuwa ya mafanikio kwa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali nchini humo katika harakati za kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani, (WSIS) ukiingia siku ya 3 hii leo huko Geneva, Uswisi, washiriki wanapazia sauti umuhimu wa kila mtu kokote pale aliko afikiwe na teknolojia inayomwezesha kupokea taarifa kwa urahisi, usahihi na kwa haraka.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.Na katika mashinani fursa ni yake Dkt. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambaye katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa kila msichana anahitaji huduma muhimu za afya uzazi ili waweze kuendelea na elimu, akitaja mfano wa kazi zao nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Viongozi kuhusu Upashanaji wa Taarifa duniani, (WSIS) ukiingia siku ya 3 hii leo huko Geneva, Uswisi, washiriki wanapazia sauti umuhimu wa kila mtu kokote pale aliko afikiwe na teknolojia inayomwezesha kupokea taarifa kwa urahisi, usahihi na kwa haraka.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini Uganda katika Mbuga ya Wanyama inayofahamika kwa jina Murchison Falls National Park kuangazia namna washiriki wa Kongamano la kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika mapema mwaka huu jijini Kampala walivyofurahia mazigira asili nchini Uganda na namna yanavyounufaisha ulimwengu.Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa maendeleo umemalizika leo huko Sevilla, Hispania ambapo mashirika ya kiraia yametaka utekelezaji kwa vitendo kwa yale yaliyomo katika nyaraka iliyopitishwa iliyopatiwa jina Makubaliano ya Sevilla.Mmoja wa wawakilishi wa mashirika ya kiraia, Paula Sevilla amesema kinachohitajika ni uongozi kutoka nchi tajiri ambako ndiko zilizko kampuni kubwa zinazokwepa kodi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kuhusu vijana na mifumo ya uzalishaij chakula na kilimo inaonesha kuwa karibu asilimia 85 ya vijana duniani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati, ambako mifumo hiyo ni muhimu kwa ajira na maisha yao. Ripoti inasema kuwajumuisha vyema vijana katika mifumo hiyo kunaweza kuleta mchango wa hadi trilioni moja ya dola kwa uchumi wa dunia..Na mwezi uliopita wa Juni umeshuhudia ongezeko kubwa la familia za raia wa Afghanistan zikirejeshwa nyumbani kutoka Iran, tofauti na awali ambapo waliokuwa wakirejeshwa walikuwa ni wanaume peke yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchabuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA nchini Tanzania, anachambua neno KUTOHOA.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, juhudi za kuhakikisha nchi zinajitegemea kifedha kupitia vyanzo jumuishi na vya ubunifu zimezidi kupewa kipaumbele. Katika hafla ya kufungua mafunzo ya Muongozo wa Upatikanaji wa Fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, au Intergrated Local Financing Framework (ILFF) yaliyofanyika katika Manispaa ya Morogoro kaskazini-mashariki mwa Tanzania hivi majuzi , Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP umetoa mafunzo ya namna halmashauri zinaweza kuandaa mikakati madhubuti ya kuhimiza maendeleo ya ndani kupitia ushirikiano kati ya sekta binafsi, mashirika ya kiraia, benki na jamii. Lengo ni kuendelea kuunga mkono serikali na wadau mbalimbali barani Afrika katika kutafuta mbinu mbadala za kufadhili maendeleo.Sharon Jebichii na maelezon zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika ukame na uhakika wa upatikanaji wa maji na kusikia jinsi taifa la Chile, linatumia sera kushawishi mabadiliko yanayoweza kukabiliana na tatizo hilo. Pia tunakuletea muhtasari na mashinani.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iran, Stefan Priesner amesema wanachofanya hivi sasa ni kupanga upya programu za Umoja wa Mataifa nchini humo wakimulika vipaumbele vipya kufuatia mashambulizi yaliyoanza tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu na kubadili mwelekeo wa kazi zao. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea Tehran mji mkuu wa Iran, Bwana Priesner amesema sasa tuko kwenye mazugumzo ya serikali kuona ni vipi tutapanga upya programu zetu kukidhi mahitaji mapya yanayoanza kuwa dhahiri, ikiwa ni siku chache tu tangu mashambulizi yakome baada ya sitisho la mapigano kuridhiwa.Huko huko Geneva, Uswisi lakini akizungumza kutoka Nairobi Kenya, Shaun Hughes, ambaye ni Mratibu wa Dharura kwa mzozo wa Sudan katika shirika la Umoja wa MAtaifa la Mpango wa Chakula, WFP amewaambia waandishi wa habari kuwa hali ni tete kwa mamilioni ya raia wa Sudan waliokimbilia nchi jirani kuepuka mapigano nchini mwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linapotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, limesema dunia imeshuhudia maendeleo muhimu katika usawa wa kijinsia ambayo yamebadilisha maisha ya wanawake na wasichana kote duniani. Licha ya ya kusherehekea, juhudi za kusukuma usawa wa kijinsia zinaonekana kurudi nyuma.Na mashinani, Mkutano wa 4 wa Ufadhili wa Maendeleo (FFD4) ukiendelea huko Sevilla Hispania, Natalia Toschi, Mkuu wa kitengo cha uwekezaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD annasema ni wakati wa kufikiria upya jinsi maendeleo yanavyofadhiliwa kwa kuzingatia mifumo ya kilimo cha mazao ya chakula ili kukuza ukuaji wa kiuchumi vijijini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 huko Sevilla Hispania, na siku ya Mabunge tukizungumza na mmoja wao kutoka Tanzania. Makala inatupeleka nchi Kenya na mashinani tunarejea huko huko Tanzania, kulikoni?Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng'oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti..Katika makala tanatupeleka kaunti ya Kajiado, Kenya, katika eneo la EMbulbul, kukutana na vijana wanaotumia maarifa ya kilimo cha kisasa kubadilisha maisha yao na ya jamii, wakisema teknolojia imefungua njia mpya ya kuinua maisha ya wakulima wadogo, hasa kwa kutumia ukulima wa kisasa unaotumia maarifa na Teknolojia.Na mashinani, fursa ni yake Sandra Aloyce, Msichana mwenye umri wa miaka 12 kutoka Tanzania ambaye kupitia Mpango wa Vijana unaofadhiliwa na shirika la UNICEF uitwao “Furaha” unaotoa mafunzo kwa wazazi kuhusu umuhimu wa uwepo wa wazazi wote katika ukuaji wa mtoto ana ujumbe.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng'oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa. Anold Kayanda amefuatilia na anatupasha zaidi
Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.
Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kutekeleza lengo nambari 14 la Maendeleo Endelevu, ulifanyika kule Nice, Ufaransa, kujadili mbinu mwafaka za kuhifadhi na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake, washikadau wakiunda uhusiano mpya kati ya wanadamu na mazingira ya baharini. Mkutano wa kilele ulikamilika Ijumaa tarehe 13 Juni, 2025 wakati huu mataifa yakitarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili sheria za uchimbaji madini kwenye kina kirefu cha maji baharini.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 18 COSP18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki kwenye Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa ulijadili ajenda mbalimbali za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuisha, kushirikishwa na kutoachwa nyumba. Amon Anastaz Mpanju Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo na aliketi chini na kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye alitaka kufahamu ni nini kikubwa anachoondoka nacho kwenye mkutano huo kitakachofanyiwa kazi Tanzania na kuleta tija kwa watu wenye ulemavu.
Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa, na masuala ya baharini ikiwa ni pamoja na uvuvi nchini Sao Tome, umuhimu wa kutunza mazingira nchini Kenya na uondoaji wa taka za plastiki Tanzania.Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung'unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika.Makala, tunasalia na mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3, tunakuletea sehemu ya mwisho ya mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.Na katika mashinani fursa ni yake Kaara Waithaka, Mwanamazingira kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus anatoa wito kwa vijana kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 ukiendelea mjini Nice, Ufaranzsa, tunakuletea mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung'unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
Mataifa yametakiwa kuchukua misimamo mikali kuhusu uvuvi wa kupindukia, uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini.
Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.
Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki.
Hii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika kuelekea mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3) utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa, kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025 ukijikita na maudhui "Kuharakisha hatua na kuhamasisha wadau wote kuhifadhi na kutumia bahari kwa njia endelevu", tunaelekea nchini Tanzania kwa Clara Makenya Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia, akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam anaeeleza nini kinapaswa kufanywa na jamii ya kitaifa na kimataifa ili kutekeleza azma ya mkutano huo.Na katika mashinani Debora, mkazi wa Sake jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, aliyekimbilia mji wa Goma jimboni humo humo kutokana na machafuko sasa amerejea tena Sake ambako wanapatiwa msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP. Akisema PAM anamaanisha WFP.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya elimu kwa watoto mashariki mwa DRC na Mkutano wa pili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT unaofunga pazia leo jijini Nairobi Kenya. Makala inaturejesha nchini DRC na mashinani inatupeleka katika bonde la Ziwa Victoria, kulikoni?Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi.Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji.Makala inakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi kuwasikia walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania,kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani.Na katika fursa ni yake Mhandisi Coletha Ruhamya, Naibu Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Mradi unaofanikishwa na Benki ya Dunia ambao unakabiliana na masuala ya usafi wa mazingira katika ziwa hilo. Anaeleza umuhimu wa usimamizi endelevu wa bonde hilo kote nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika wafugaji wa nyuki nchini Tanzania leo ikiwa ni siku ya nyuki duniani iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 Desemba mwaka 2017 kupitia azimio namba A/72/211.Baada ya miaka mitatu ya majadiliano, leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya unaoendelea Geneva, Uswisi, nchi zimepitisha rasmi makubaliano ya kihistoria ya kuzuia, kujiandaa, na kukabiliana vyema na majanga ya magonjwa kwa siku zijazo. Taratibu zote zitakapopitishwa na angalau nchi 60, mkataba utaanza kutumika rasmi mwakani.Kutokana na mamlaka za Israeli kulegeza kwa muda mzingiro uliodumu kwa wiki 11, angalau sasa matumaini kidogo yamerejea Gaza, yameeleza leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya dharura, OCHA, Jens Laerke amesema tayari wamepata ruhusa ya kuyavusha malori matano yaliyokuwa yamezuiliwa jana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetahadharisha leo kwamba bila ufadhili zaidi, huenda katika muda wa wiki chache zijazo likalazimika kusitisha msaada wa chakula kwa takribani nusu ya watu linaowahudumia kwa sasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Na katika mashinani, fursa ni yake Hanan Al-Dayya, Mkimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, akisimulia madhara ya mashambulizi yanayoendelea kutoka Israeli.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Ulimwengu Mmoja kwa Afya” inaakisi dhamira ya pamoja ya kujenga mfumo wa afya wa kimataifa ulio imara, jumuishi na thabiti. Flora Nducha amefuatilia na hapa anatupasha zaidi
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya, na wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao. Makala tukwenda nchini Kenya kumulika ufukaji wa nyuki, na mashinani tunakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa IMO kuhusu Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia.Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu.Tangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.Katika makala tunaelekea Kajiado nchini Kenya, ambako juhudi za utunzaji mazingira kupitia mradi wa ufugaji wa nyuki unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa kushirikiana na idara ya misitu ya Kenya KFS hazichangii tu katika kukuza uchumi wa jamii, bali pia kulinda mazingira. Kupitia Makala hii iliyoandaliwa na Sharon Jebichii, Bwana Mureithi mmoja wa wanufaika wa mradi huo anaanza kwa kueleza mafanikio yao.Nakatika mashinani, fursa ni yake Arsenio Dominguez, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafirishaji Majini, IMO akitoa ujumbe wa ujumuishaji na usawa wa kijinsia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia ambayo huadhimishwa tarehe 18 mwezi Mei kila mwaka.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.
Mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Anaanza kwa kujitambulisha
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi. "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano hii.Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.
Hii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assumpta Massoi amezungumza na Rosemary Mwaipopo, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kiraia la DaySpring Foundation nchini Tanzania. Yeye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 uliofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita wa Machi.Na mashinanileo ikiwa leo ni siku ya afya duniani, kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus, fursa ni yake Padri Thaddeus Mukaya wa kanisa la katoliki la Parokia ya Embulbul ambalo pamoja na wadau wengine waliandaa huduma za bure za matibabu kwa wenyeji wa eneo hilo ili kusaidia jamii ambazo haziwezi kujimudu kimaisha.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki takriban milioni 1.9.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa ya Bahari ya Atlantiki, ikiwakumbuka mamilioni ya Waafrika walioteswa, kunyanyaswa, na kunyimwa utu wao. Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kwa zaidi ya karne nne, mamilioni ya Waafrika walitekwa kwa nguvu, kusafirishwa kwa meli hadi mataifa ya kigeni, na kufanyishwa kazi katika hali mbaya za kikatili.”Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Lea mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa amekimbilia Burundi na familia anasilimua hali ilivyokuwa wakati wa kukimbia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Makala Anold Kayanda wa Idhaa hii baada ya kukamilika kwa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69 uliofikia tamati mwishoni mwa wiki amezungumza na Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake wa Vyombo vya Habari Tanzania (TAMWA) kuhusu tathimini yake ya hatua zilizopigwa katika miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke.Na katika mashinani fursa ni yake Imani Ramadhani kutoka wilaya ya Kilolo, Iringa nchini Tanzania akieleza jinsi ambavyo maisha ya familia yake ilivyobadilika kupitia mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF, uliofadhiliwa kwa ushirikiano na wadau wake unaolenga kuleta usafi enedelevu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na vyoo safi na salama ili kupunguza hatari za kila mara za magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Rekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi imefanyika.” Anasema Mkrugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA.Kwake, mwandishi wa habari nguli, anaona moja ya maeneo ambayo ni muhimu yafanyiwe kazi ni kuzipa nafasi taarifa zinazohusu shughuli kubwa zinazofanywa na wanawake katika jamii kote duniani kwani licha ya wanawake kuwa na michango mikubwa katika mustakabali wa ulimwengu, taarifa zao hazipewi kipaumbele cha kutosha.“Mimi kwa mtazamo wangu naona wanawake wamefanya kazi nyingi lakini hazijarekodiwa. Rekodi ni chache sana.” Anasisitiza na kuongeza, “kwa hiyo tunatakiwa kuanza kurekodi vile vitu ambavyo vilifanywa na wanawake wale wa miaka 30 iliyopita lakini hata na hawa wanaokuja kizazi kipya.”Dkt. Rose Reuben anahamasisha pia vyombo vya habari kuangazia masuala mengine ambayo kwa namna moja amba nyingine yanaigusa jamii moja kwa moja na hiyo ni kusema yanamgusa mwanamke moja kwa moja kama vile mabadiliko ya tabianchi, tekonolojia, “na vitu vingine ambavyo vinaweza kuathiri usawa wa kijinsia na hali ya mwanamke duniani.”Aidha kiongozi huyo wa TAMWA anatoa wito kwa wanawake popote walipo kutumia nyenzo zinazopatikana katika jamii yao kuhakikisha wanapata taarifa, wanasambaza taarifa na kujipatia maarifa.
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Nilipokutana naye nimemuuliza swali hili la kichokozi.Mazungumzo zaidi kati yangu na Mama Gertrude Mongella yatakujia katika vipindi vyetu vijavyo hivi karibuni.
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu, na wakulima wanawake nchini Senegal. Mashinani inatupeleka nchini Tanzania kumulika mradi wa maji.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Tukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na utengenezaji video za mtandaoni kuelimisha jamii kuhusu kilimo chenye tijaMakala inayoturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unaokunja jamvi hii leo Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania.Na katika mashinani fursa ni yake Janeth Zakaria kutoka kijiji cha Kaguruka mkoani Kigoma nchini Tanzania ambaye kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF anasema alikuwa anatembea umbali wa kilomita 10 kupata maji safi na salama lakini sasa ni hatua chache tu kutoka nyumbani kwake”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unakunja jamvi leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya mjadala wa wiki mbili kutathimini hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia miaka 30 baada ya azimio la Beijing la usawa wa kijinsia nah atua za utekelezaji. Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wakishiri wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania
Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani ni Finland na ya mwisho kabisa ni Afghanistani. Katika 10 bora zenye furaha hakuna hata moja ya Afrika, ilihali kwenye 10 za mwisho nchi za Afrika ni 7 ambazo ni Lesotho, Comoro, Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Malawi na Sierra Leone.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukikaribia ukingoni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tumemuuliza mshiriki Wakili Rosemary Mwaipopo kutoka Tanzania mkutano umekidhi kiu yake ya kusongesha usawa wa kijinsia?Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake.
Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi
Hii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69. Ili kufanikisha lengo la usawa wa kijinsia Umoja wa Mataifa unasisitiza ushiriki wa wanaume katika mchakato hasa kwa kuzingatia kuwa mfumo dume miaka nenda miaka rudi umekuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo, Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wanaume wanaoshiriki mkutano huo kusikia maoni yake.Na katika mashinani baadhi ya washiriki wa mkutano wa CSW69 wakizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo, wametoa wito wa mshikamano na msichana na mwanamke yeyote anayepitia changamoto kote duniani hususani wale wanaorejea shuleni baada ya kusitisha masomo kutokana na ujauzito kabla ya wakati. Mshiriki wa kwanza ni Nasra Kibukila anayewakilisha Mtandao wa Elimu Tanzania, TEN/Met.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox's Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini kwanza ni makala ambapo Assumpta Massoi anazungumza na mshiriki wa CSW69 kutoka Cote D'Ivoire.Na katika mashinani Felicite Djoukouo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Maendeleo nchini Cameroon ambaye anashiriki mkutano wa CSW69 hapa Umoja wa Mataifa anaelezea matarajio yake ya mkutano huu utakaomalizika tarehe 21 mwezi huu wa Machi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80, na yaliyojiri katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa..Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.Makala tukisalia hapa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani ambako Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu, nimezungumza na Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.Na Katika mashinani fursa ni yake Janet Zebedayo Mbene kutoka Tanzania aliyehududhuria mkutano huu hapa makao makuu, kama mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa uwezeshaji wa wanawake Tanzania na angependa kuwashauri wanawake na wasichana wanaopitia changamoto wajikite katika fursa mbalimbali. Kila kitu kina changamoto. Wajitie moyo na waondoe uoga, na kwa kile kidogo walicho nacho wanaweza kujiinua na kuinua jamii kwa ujumla.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.
Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa kina inayomulika mkutano wa CSW69 ulioanza Jana Jumatatu hapa New York, Marekani, ikiwa ni miaka 30 tangu mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995, ukiweka msingi wa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ya usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari na sauti za vijana kutoka mashinani.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekutana na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wanaoshiriki Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69. Bwana Guterres amezitaka Asasi za Kiraia kuendelea kuzisukuma nchi kuweka mazingira bora kwa ajili ya usawa wa wanawake na wasichana na pia akakumbushia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwaunga mkono katika kulitimiza lengo hilo.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk kupitia Msemaji wake, ameripoti ukatili unaoendelea katika pwani ya Syria tangu Machi 6, ambapo anasema takriban raia 111 wameuawa, wengi wao kwa misingi ya kiimani. Hospitali pia zimeshambuliwa na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa uchunguzi huru na uwajibikaji kwa wahusika.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Malawi limeongeza wigo wa mpango wake wa Mlo Shuleni unaopatikana kwa kununua vyakula vinavyolimwa na wananchi wa karibu katika maeneo hayo. Mradi huo unaotekelezwa wilayani Nkhotakota, unanufaisha wanafunzi 10,000 na kusaidia wakulima wadogo 1,200, hivyo kuimarisha upatikanaji wa chakula na uchumi wa ndani.Na Katika mashinani huku mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukiendelea hapa makao makuu, tutakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe wa vijana kuhusu usawa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000. Selina Jeroboni na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji chakula mwezi Julai mwaka huu huko Addis Ababa, Ethiopia, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amezungumza hivi karibuni akiwa Nairobi, Kenya kwenye kikao cha maandalizi ambako alitembelea jiko la Giga, mpango wa Chakula kwa ajili ya Elimu, unaoendeshwa na Wawira Njiru, mshindi wa tuzo ya Mtu Maarufu Kenya mwaka 2021.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu. Selina Jerobon na taarifa kamili..
Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya lugha mama, tunakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kushuhudia matumizi ya nishati safi na ya gharama nafuu kupika mlo shuleni jijini Nairobi linaloofanikishwa na Shirika la Food4Education. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani inatupeleka Ethiopia.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema hali ya usalama mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inazidi kuwa mbayá kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali, FARDC na waasi wa M23. Saa 24 zilizopita zimekuwa ni mbayá.Naye Dkt. Adelheid Marschang, Mratibu wa masuala ya dharura wa shirika la Umoja wa MAtaifa la afya duniani, WHO nchini DRC amesema tumesikia ripoti za wahudumu wa afya kupigwa risasi huku wagonjwa pamoja na watoto wakinaswa kwenye mapigano. “WHO inakumbusha kila mtu kuwa mashambulizi dhidi ya huduma za afya ni kinyume na kanuni za vita. Vituo vya afya lazima vilindwe wakati wote.”Mkutano wa viongozi wa Afrika kuhusu nishati ukipatiwa jina Mission 300 umekunja jamvi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa kuzindua Mikataba ya Nishati ya Kitaifa kutoka nchi 12 za barani Afrika, ikiwemo Tanzania, hatua ambayo ni msingi wa uwekezaji mkubwa na mageuzi ya será za nishati. Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema, “kwa kusongesha mipango ya muda mrefu ya kupata nishati na kuisimamia, tunaweza kuimarisha amani, na kuunda ajira zisizoharibu mazingira, na kujenga mnepo wa mbinu za kujipatia kipato, na hivyo kufungua njia ya utulivu na ustawi wa bara letu.”.Na mashinani fursa ni yake mwalimu Beray kutoka eneo la Tigray nchini Ethiopia ambaye amezungumza na maafisa wa msaada wa mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri (ECW) akieleza matumaini yake kwa wanafunzi wake iwapo watawezeshwa.Mwenyeji wako niAnold Kayanda karibu!
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza. Aidha Mjumbe huyo maalum amesisitiza azma ya Umoja wa Mataifa ya kutoa usaidizi wa kina kwa watu wa Syria.Taarifa imedokeza kuwa Bwana Pedersen ana shughuli nyingi zilizopangwa siku zijazo katika harakati za kusaka suluhu ya amani nchini Syria.