Podcasts about hatua

  • 42PODCASTS
  • 360EPISODES
  • 14mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • Feb 9, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about hatua

Latest podcast episodes about hatua

Habari RFI-Ki
Afrika Kusini yatangaza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kwa monusco nchini DRC

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Feb 9, 2026 10:00


Mwishoni mwa juma Afrika Kusini ilitangaza kuondoa wanajeshi wake kutoka kwa tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC (MONUSCO) baada ya kikosi hicho kuhudumu kwa miaka 27.Pretoria inasema hatua hiyo ni kutokana na mipango yake ya kurekebisha na kuimarisha raslimali ya jeshi lake.Tumemuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Afrika kusini,Hatua hii ni kumaanisha Monusco imepoteza nguvu DRC na Nini kifanyike kuleta usalama wa kudumu nchini DRC?

Habari RFI-Ki
Afrika Kusini yatangaza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kwa monusco nchini DRC

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Feb 9, 2026 10:00


Mwishoni mwa juma Afrika Kusini ilitangaza kuondoa wanajeshi wake kutoka kwa tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC (MONUSCO) baada ya kikosi hicho kuhudumu kwa miaka 27.Pretoria inasema hatua hiyo ni kutokana na mipango yake ya kurekebisha na kuimarisha raslimali ya jeshi lake.Tumemuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Afrika kusini,Hatua hii ni kumaanisha Monusco imepoteza nguvu DRC na Nini kifanyike kuleta usalama wa kudumu nchini DRC?

Habari za UN
27 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2026 12:40


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za vijana katika kuchagiza maisha wayatakayo kuanzia kujiondoa kwenye umasikini, ukosefu wa usawa hadi kwenye upatikanaji mdogo wa elimu bora na kazi zenye staha.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika pamoja na manusura wa mauaji ya kimbari ya holokosti hususan yale yaliyofanywa na manazi wa kijerumani, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Baraza Kuu kumefanyika kumbukizi ikileta pamoja manusura waliotoa shuhuda za waliyopitia wakikimbia maeneo kadhaa ikiwemo Austria baada ya kutwaliwa na wajerumani.Huko Geneva, Uswisi ambako inaelezwa kuwa kurejesha mfumo wa elimu uliosambaratika huko Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni jambo la kuokoa maisha, na kuwarudisha watoto shuleni lazima kiwe kipaumbele cha haraka, amesema James Elder Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Umoja wa Mataifa umezindua Mpango wa Mahitaji na Hatua za Kibinadamu wa dola milioni 852 kwa ajili ya Somalia, huku ukionya kuwa ukosefu mkubwa wa ufadhili utaacha mamilioni ya watu walio katika mazingira magumu bila msaada wa kuokoa maisha, huku hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "TWINGA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari RFI-Ki
Marekani kujiondoa rasmi kwenye WHO, hatua hatari kwa sekta ya afya dunaini

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jan 27, 2026 9:53


Wiki iliopita, ilijiondoa kwenye shirika la afya duniani licha ya onyo kuwa hatua hiyo itaathiri ufadhili kwenye sekta ya afya duniani. Wiki chache zilizopita, rais Donald Trump alitangaza pia kuwa Marekani itajiondoa kwenye mashirika 66 ya kimataifa, yakiwemo yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa

Habari RFI-Ki
Marekani kujiondoa rasmi kwenye WHO, hatua hatari kwa sekta ya afya dunaini

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jan 27, 2026 9:53


Wiki iliopita, ilijiondoa kwenye shirika la afya duniani licha ya onyo kuwa hatua hiyo itaathiri ufadhili kwenye sekta ya afya duniani. Wiki chache zilizopita, rais Donald Trump alitangaza pia kuwa Marekani itajiondoa kwenye mashirika 66 ya kimataifa, yakiwemo yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa

Habari za UN
Guterres: Hatua kuelekea nishati safi hazitoshi, kasi lazima iongezwe

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 26, 2026 2:39


Katika Siku hii ya Kimataifa ya Nishati Safi mwaka huu iliyobeba maudhui “Nishati safi kwa wote”, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia inaelekea kubadilika lakini ameonya kuwa kasi ya mabadiliko hayo kuelekea nishati safi haitoshi na ni lazima iongezwe. Flora Nducha na taarifa zaidi

Habari za UN
Türk aeleza aliyoyashuhudia katika ziara yake Sudan, aitaka dunia ichukue hatua za haraka

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 19, 2026 3:20


Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, baada ya ziara yake ya siku tano nchini Sudan, ametahadharisha kuhusu kuongezeka kwa hali mbaya zaidi ya ukikukwaji wa haki za binadamu na ongezeko la janga la kibinadamu nchini humo.Rashid Malekela na taarifa zaidi.

sudan dunia umoja haki katika yake hatua mataifa volker turk ziara
Habari RFI-Ki
Maoni: Hatua ya Marekani kutangaza kujiondoa katika mashirika 66 yakiwemo yale ya Umoja wa Mataifa

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jan 15, 2026 10:01


Agizo la kiutendaji lililosainiwa na rais wa Marekani linaagiza Marekani kujiondoa kutoka kwa jumla ya mashirika 66, karibu nusu yake ambayo yana uhusiano na Umoja wa Mataifa, Ikulu ya White House ilisema wiki iliyopita. Miongoni mwa hayo ni Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC), mkataba wa msingi wa mikataba mingine yote ya kimataifa ya hali ya hewa, uliohitimishwa mwaka wa 1992 katika Mkutano wa Rio Earth.

white house kenya yale uganda tanzania burundi drc umoja katika hatua mataifa marekani mkutano miongoni mashirika
Habari RFI-Ki
Maoni: Hatua ya Marekani kutangaza kujiondoa katika mashirika 66 yakiwemo yale ya Umoja wa Mataifa

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Jan 15, 2026 10:01


Agizo la kiutendaji lililosainiwa na rais wa Marekani linaagiza Marekani kujiondoa kutoka kwa jumla ya mashirika 66, karibu nusu yake ambayo yana uhusiano na Umoja wa Mataifa, Ikulu ya White House ilisema wiki iliyopita. Miongoni mwa hayo ni Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC), mkataba wa msingi wa mikataba mingine yote ya kimataifa ya hali ya hewa, uliohitimishwa mwaka wa 1992 katika Mkutano wa Rio Earth.

white house kenya yale uganda tanzania burundi drc umoja katika hatua mataifa marekani mkutano miongoni mashirika
Habari za UN
UN yaonya hatari ya kuongezeka kwa mvutano nchini Venezuela kufuatia hatua ya kijeshi ya Marekani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 3:15


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo katika kikao cha dharura baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Venezuela tarehe 3 Januari mwaka huu, hatua iliyozua hofu ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu nchini humo na katika eneo zima. Leah Mushi anatufahamisha zaidi.

venezuela umoja hatari baraza hatua mataifa marekani
SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya habari:Marekani yavamia Venezuela na kumkamata rais Maduro na mkewe

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 9:13


Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru shambulio kubwa dhidi ya Venezuela kuwakamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mke wake. Wametuhumiwa na makosa ya dawa za kulevya na silaha huko New York. Hatua hiyo imepongezwa na washirika wa Bw. Trump, lakini imelaaniwa sana na mataifa mengi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Yaliyojiri Afrika:Hatua ya Israel kuitambua Somali Land yazua utata

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jan 5, 2026 6:24


Mwanahabari Jason Nyakundi atujuza yaliyojiri Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa mitandao yetu ya kijamii au tovuti yetu sbs.com.au/swahili

Jukwaa la Michezo
Uchambuzi wa Mada: Je, AFCON 2025 inatoa msisimko kama mashindano yaliyopita?

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later Jan 4, 2026 24:34


Leo tunajadili kwa undani kauli ya kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos kuwa michuano ya mwaka huu haina mvuto na msisimko kama Afcon zilizopita. Uchambuzi wa mechi za jana na leo kwenye hatua ya 16 bora - Tanzania vs Morocco, Afrika Kusini vs Cameroon, DRC vs Algeria. Hatua ya serikali ya Gabon kuvunjilia mbali timu ya Gabon huku marais wa Msumbiji na Benin wakitoa ahadi za pesa kwa timu zao. Morocco kuandaa michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu 2029 nayo Ethiopia ikiwania kuandaa Afcon ya 2028.

Jukwaa la Michezo
AFCON 2025: Mtazamo wa hatua ya mtoano, timu 16 zitawania tiketi ya fainali

Jukwaa la Michezo

Play Episode Listen Later Jan 3, 2026 23:48


Leo tumeangazia kwa undani matokeo na matukio ya hatua ya makundi iliyokamilika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea Morocco, uchambuzi wa hatua ya 16 bora - nani atafuzu robo fainali?, tathmini ya hatua ya serikali ya Gabon kuvunja kabisa timu ya taifa ya Gabon, ahadi za pesa kutoka kwa marais kadhaa Afrika kwa timu zao kuelekea robo fainali, usajili wa Rayon Sport, kwa nini Maresca aliondoka Chelsea?, dereva wa Anthony Joshua afunguliwa mashtaka baada ya ajali Nigeria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Dec 19, 2025 10:03


Wakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa,  Wataalamu wa lugha,,  walimu pamoja na  wanafunzi waaendeleza  mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

dunia umoja kiswahili katika wakati hatua mataifa mazingira
Habari RFI-Ki
Marekani yapiga marufuku kwa raia kutoka mataifa kadhaa kuingia ardhi yake

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Dec 18, 2025 10:01


Makala hii imeangazia hatua ya hivi karibuni ya rais wa marekani Donald Trump ya kuongeza orodha mpya ya mataifa zaidi yakiwemo ya Afrika ikiwemo Tanzania,  ambayo raia wake wanazuiwa kuingia Marekani, tumekuuliza Je? hatua hii ni ya kibaguzi ama inalenga kuulinda usalama wa Marekani? Na kwa mtazamo wako Hatua hii Ina maana gani? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata maoni ya wasikilizaji

Habari RFI-Ki
Marekani yapiga marufuku kwa raia kutoka mataifa kadhaa kuingia ardhi yake

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Dec 18, 2025 10:01


Makala hii imeangazia hatua ya hivi karibuni ya rais wa marekani Donald Trump ya kuongeza orodha mpya ya mataifa zaidi yakiwemo ya Afrika ikiwemo Tanzania,  ambayo raia wake wanazuiwa kuingia Marekani, tumekuuliza Je? hatua hii ni ya kibaguzi ama inalenga kuulinda usalama wa Marekani? Na kwa mtazamo wako Hatua hii Ina maana gani? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata maoni ya wasikilizaji

Habari za UN
Miaka 10 ya Mkataba wa Paris ni kupima hatua zilizopigwa na kukabili mapengo - UNEA-7

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 12, 2025 3:04


Leo Dunia inapoadhimisha miaka kumi tangu Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya Tabianchi kupitishwa, wataalamu wa masuala ya tabianchi barani Afrika wanasema maadhimisho haya ni wakati wa kupima hatua zilizofikiwa lakini pia kukabili pengo linalopanuka kati ya sera na utekelezaji wa hatua za tabianchi. Flora Nducha na taarifa zaidi

afrika nairobi miaka hatua unea
Habari RFI-Ki
Upinzani barani Afrika waendelea kunyanyaswa na polisi wakati wa kampeni

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Dec 9, 2025 10:01


Mada ya leo ni kuhusu kinara wa upinzani  nchini Uganda Bob Wine pamoja na baadhi ya wagombea wengine wa upinzani wameendelea kunyanyaswa na vyombo vya usalama wanapoendelea na kampeni zao, tume ya uchaguzi ikilaani vitendo hivyo.Yanayofanyika Uganda yanashuhudiwa pia kwenye mataifa kadhaa ya Afrika .Tumemuuliza msikilizaji  Hatua hii ya vyombo vya usalama inaathiri vipi demokrasia na nini kifanyike kujenga mazingira sawa ..Karibu

Habari RFI-Ki
Upinzani barani Afrika waendelea kunyanyaswa na polisi wakati wa kampeni

Habari RFI-Ki

Play Episode Listen Later Dec 9, 2025 10:01


Mada ya leo ni kuhusu kinara wa upinzani  nchini Uganda Bob Wine pamoja na baadhi ya wagombea wengine wa upinzani wameendelea kunyanyaswa na vyombo vya usalama wanapoendelea na kampeni zao, tume ya uchaguzi ikilaani vitendo hivyo.Yanayofanyika Uganda yanashuhudiwa pia kwenye mataifa kadhaa ya Afrika .Tumemuuliza msikilizaji  Hatua hii ya vyombo vya usalama inaathiri vipi demokrasia na nini kifanyike kujenga mazingira sawa ..Karibu

Habari za UN
Kuchukua hatua ya mpango wa uzazi kama msichana haimanishi unajihusisha na vitendo vya ngono kiholelaholela - Lucy

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 3, 2025 3:01


Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya  Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi

kenya kama umoja afya watu hatua mataifa shirika vitendo
Habari za UN
20 NOVEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 20, 2025 10:45


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kajiado iliyoko Kusini na Kusini magharibi mwa jiji la Nairobi nchini Kenya kumulika upatikanaji wa huduma za choo na hasa choo safi na salama ambazo bado ni kizungumkuti kote dunianini.Katibu Mkuu wa Umoja wa, António Guterres,akizungumza na waandishi wa habari hii leo ametoa onyo kali COP30 huko Belém, Brazil, akisisitiza dharura ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Amesema “Jamii zilizo mstari wa mbele zinaangalia zikiesabu nyumba zao zilizozamishwa na mafuriko mavuno yaliyoshindikana, vyanzo vya maisha vilivyopotea na kuuliza kwa kiasi gani zaidi wateseke . Wamesikia visingizio vya kutosha, sasa wanatakahatua”.Leo ni Siku ya mtoto Duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Sikilizeni watoto, simameni kwa ajili ya haki za kila mtoto, kila siku.” Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo ya Hali ya Watoto Duniani 2025 sanjari na maadhimisho haya  inaonya kwamba zaidi ya watoto milioni 417, sawa na mtoto 1 kati ya 5 katika nchi za kipato cha chini na cha kati, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu angalau katika maeneo mawili ya msingi ya maisha.Mkutano wa wanaharakati vijana wavumbuzi kutoka kila pembe ya dunia umeaanza leo mjini Geneva Uswisi ukibeba mafda kuu “Kutoka Hashtag hadi Hatua”, ukisherehekea vijana wanaobadilisha maisha ya jamii zao kupitia zana za kidijitali na majukwaa ya mtandaoni. Mwaka huu, washindi wa uvumbuzi huo wanatoka nchi mbalimbali, ikiwemo Côte d'Ivoire, India, Lebanon, Japan, na Brazil, wakitambuliwa kwa kazi zao zenye athari kubwa chanya. Waandaaji wa Jukwaa hilo amba oni Umoja wa Mataifa wanasema tukio hili lina lengo la kuhamasisha vijana wengi zaidi kubadilisha ushiriki wao wa mtandaoni kuwa hatua halisi zinazoboresha jamii, kuthibitisha kuwa uanaharakati wa kidijitali unaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Na katka kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MTAWALIA.”Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!

japan brazil kenya lebanon ant tanzania nairobi guterres umoja hii kiswahili siku mwaka hatua mataifa novemba mkutano shirika ripoti kaunti jukwaa
Habari za UN
Hatua ndizo zinazohitajika baada ya mkutano wa dunia wa Maendeleo ya Kijamii - Diana Pasha

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 12, 2025 2:18


Mkutano wa Pili wa Dunia wa Maendeleo ya Kijamii umefunga pazia mjini Doha, Qatar, mwishoni mwa wiki hii, ukiwaleta pamoja viongozi wa dunia, mashirika ya kiraia na vijana wakitoka na wito wa pamoja dhidi ya umasikini, ukosefu wa usawa na kutengwa kijamii. Kutoka Kenya, mwanaharakati kijana amesema mkutano huo umekuwa wa kuhamasisha akitoa wito wa hatua za haraka. Flora Nducha na taarifa zaidi

SBS Swahili - SBS Swahili
Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Nov 11, 2025 7:35


Australia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu lake kwa ukimbizi mkubwa wa dunia nzima.

Habari za UN
UNICEF yachukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 3:02


Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi

kenya wash unicef mpox mombasa umoja katika mastercard foundation hatua mataifa serikali shirika kaunti
Habari za UN
Guterres: ASEAN chukueni hatua kukomesha ukatili Myanmar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 27, 2025 2:47


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN kuchukua hatua za haraka kumaliza machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, akisisitiza kuwa mgogoro huo si tishio kwa watu wa Myanmar pekee bali pia kwa amani na usalama wa kanda nzima ya Asia ya Kusini Mashariki.  Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Rais W.Ruto amtunuku hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi, hali mashariki ya DRC

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Play Episode Listen Later Oct 25, 2025 20:03


Hatua ya rais wa Kenya William Ruto kumtunuku aliyewahi kuwa waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi nchini, kukamatwa kwa makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania, John Heche, DRC na Rwanda zakubaliana juu ya mchakato wa upatikanaji wa amani chini ya upatanisho wa Marekani, uchaguzi wa urais nchini Cote D'Ivoire, na rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarcozy wiki hii alianza kukitumikia kifungo cha miaka mitano.

israel kenya uganda rwanda tanzania drc rais zaidi ruto raila odinga hayati hatua mkuu marekani ufaransa mashariki kenya william ruto
Habari za UN
14 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 14, 2025 11:27


Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Mwalimu Nyerere na tunakupeleka nchini Tanzania ambako kunaendelea juhudi za kuimarisha matumimizi ya lugha ya Kiswahili na utangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashairki, manufaa ya kiuchumi na kijami na kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba Gaza itahitaji karibu dola bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi upya baada ya miaka miwili ya mzozo, huku dola bilioni 20 zikitakiwa katika miaka mitatu ijayo. Makadirio haya yanatokana na, tathmini ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Benki ya Dunia. Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina Jaco Cilliers,amesema “Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92.”Umoja wa Mataifa umeongeza hatua zake za dharura huko Gaza kwa kutoa dola milioni 11 kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) kukidhi mahitaji ya haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Mgao huu, uliozinduliwa na Mratibu wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher, utaunga mkono utoaji wa chakula, maji, huduma za afya na makazi kwa raia walioathiriwa na mzozo wa miaka miwili. Hatua hii inafuatia mgao wa dola milioni 9 wiki iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa hospitali na huduma muhimu, na kufanya jumla ya msaada wa hivi karibuni kufikia dola milioni 20.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa ya neva duniani, ambayo sasa yanachangia zaidi ya vifo milioni 11 kila mwaka. Ripoti mpya ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva inaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni 3 sawa na zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani  wanaishi na magonjwa yanayoathiri ubongo, ikiwemo kiharusi, ugonjwa wa kusahau, kifafa, na maumivu ya kichwa ya muda mrefu. Kwa mujibu wa ripoti nchi maskini ndizo zinazoathirika zaidi, zikiwa na upungufu mara 80 wa idadi ya wataalamu wa magonjwa ya neva ikilinganishwa na nchi tajiri. WHO inazitaka serikali kutoa kipaumbele kwa afya ya ubongo, kuongeza fedha na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE!Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Wimbi la Siasa
Uchambuzi: Kwanini waasi wa AFC/M23 waendelea kujiimarisha zaidi mashariki mwa DRC ?

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Oct 8, 2025 10:09


Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa waasi wa AFC/M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi,  katika maeneo wanayodhibiti, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa Washington uliokubaliwa kati ya DRC na Rwanda kuhusu namna ya kupata mwafaka wa kudumu. Hatua hii inamaanisha nini ? Tunachambua. 

Habari za UN
16 SEPTEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 16, 2025 10:31


Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa  Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Kengele ya amani yagongwa UN kuikumbusha dunia wakati wa kuchua hatua kuidumisha ni sasa: Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 12, 2025 3:18


Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia. Flora Nducha amefuatilia hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii. Karibu Flora(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Natts --bellLeo, mlio mzito wa Kengele ya Amani umesikika kwenye Makao Makuu ya Umoja wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na na burudani ya muziki wa allaNatts........Kisha Katibu Mkuu Guterres akawageukia washiriki na kusema “miaka ni themanini iliyopita Umoja wa Mataifa kuzaliwakutoka kwenye majivu ya vita ili kusaka amani”, akatoa ujumbe ulio wazi,sasa  jukumu la amani duniani ni la dharura kuliko wakati mwingine wowote.Wakati migogoro ikienea na mamilioni ya raia wakiendelea kunaswa kwenye mzunguko wa ghasia, Katibu Mkuu ametahadharisha kwa onyo kali “Amani imo hatarini.”Amesema haki za binadamu na sheria za kimataifa zinakanyagwa, na kuacha nyuma kile alichokiita “mandhari yanayodhalilisha ubinadamu wetu wa pamoja.”Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu  ya siku ya Amani “Tuchukue Hatua Sasa kwa Dunia yenye Amanisi maneno ya kupita tu, bali ni wito wa dhati wa kuchukua hatua. Guterres amewakumbusha wanachama wa Umoja wa Mataifa na raia kila mahali kwamba amani haiji kwa bahati. Inajengwa hatua kwa hatua, kwa maelewano, ujasiri, na vitendo.“Ni lazima tuchukue hatua kunyamazisha bunduki na kukuza diplomasia. Ni lazima tuchukue hatua kuwalinda raia na kutetea Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ni lazima tuchukue hatua kushughulikia chanzo cha migogoro kuanzia ukosefu wa usawa na kutengwa, hadi kauli za chuki, na janga la tabianchi.”Katibu Mkuu amesisitiza kwamba amani bado iko ndani ya uwezo wa binadamu lakini ni iwapo tu tutaichagua. Ameiitaja kama nguvu kubwa zaidi kwa mustakabali bora, na kuwataka watu wote kuwaunga mkono wale wanaojenga amani, hususan wanawake na vijana walioko mstari wa mbele wa matumaini.Natts kengele.....muzukiKengele ya Amani ilipopigwa  iliyotengenezwa miongo kadhaa iliyopita kutokana na sarafu na medali zilizotolewa na watu wa kawaida kote duniani Guterres amewakumbusha hwashiriki wa hafla hiyo ishara yake “Hata katika dunia iliyogawanyika, bado tunaweza kuungana na kuiacha amani ishike hatamu.”Amehitimisha kwa kusema Katika Siku ya Kimataifa ya Amani, mlio wa kengele unatoa si tu wito wa kimya cha tafakuri, bali pia wito wa kuchukua hatua kwa viongozi, kwa raia, na kwa vizazi vijavyo.Natts muziki..

dunia guterres hata sasa umoja siku wakati hatua mataifa kimataifa septemba
Habari za UN
28 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 28, 2025 9:59


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipaka ya Ukraine kama inavyotambuliwa kimataifa.Kuhusu Mashariki ya Kati Katibu Mkuu António Guterres akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa      ameonya kuwa operesheni za kijeshi mjini Gaza zitakuwa na zahma kubwa na amesisitiza “hili lazima likome.” Amesema njaa si tishio tena bali janga la sasa, huku raia, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wakiuawa  wakati “macho ya dunia yakitazama.” Guterres ameikumbusha Israel wajibu wake wa kisheria kulinda raia na kuruhusu msaada wa kibinadamu bila vikwazo akisema “Hakuna visingizio tena. Hakuna vizuizi tena. Hakuna uongo tena,”  akitoa wito wa usitishaji mapigano haraka na kuachiliwa kwa mateka wote.Kikosi cha 11 cha Tanzania TANZBATT 11 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kimetoa msaada wa magodoro kwa raia walioathirika na machafuko ya karibuni katika kijiji Oicha  jimboni Kivu Kaskazini. Miongoni mwao ni Bi Masika Jistine na Mzee Bahati Paluku ambao hawakusita kuonesha furaha yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Maji ni Uti wa mgongo kwa jamii kote duniani - Stephen Tai

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 28, 2025 5:09


Wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mtendaji huyo anayeanza kwa kujitambulisha, anazungumza na Kelvin Keitany wa radio washirika Radio Domus nchini Kenya.

Kiswahili, Lugha Ya Afrika
AI, AGI na ASI zinamaanisha nini?

Kiswahili, Lugha Ya Afrika

Play Episode Listen Later Aug 9, 2025 8:22


Katika makala haya ya kipekee, tunafichua siri kuhusu Akili Bandia—kuanzia AI ya kawaida, hadi AGI (Artificial General Intelligence), na hatimaye ASI (Artificial Super Intelligence)!Tunakufafanulia kwa Kiswahili sanifu na kwa lugha rahisi:✅ AI ni nini na kwa nini iko kila mahali sasa?✅ AGI inatishia kazi zako—ina uwezo sawa na binadamu!✅ ASI ni hatua ya hatari sana—inaweza kuwa mwisho au mwanzo mpya kwa wanadamu.✅ Faida na hasara za kila hatua ya maendeleo ya akili unde.✅ Hatua za kuchukua ili kulinda jamii kutokana na madhara ya AI.

ai asi agi nini kiswahili katika agi artificial general intelligence hatua
Habari za UN
IOM yachukua hatua za dharura baada ya wahamiaji kufa maji katika pwani ya Djibouti

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 11, 2025 1:52


Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

djibouti iom umoja maji katika kufa baada hatua mataifa shirika
Habari za UN
Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 4, 2025 3:23


Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.

SBS Swahili - SBS Swahili
Wito watolewa kwa hatua ya ziada kuchukuliwa kushughulikia gharama ya janga yaki asili

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jun 3, 2025 10:14


Uchambuzi mpya wa hazina ume onesha gharama ya Kimbunga Alfred na mafuriko mengine katika majimbo ya New South Wales na Queensland imefika takriban $2.2 bilioni dollars.

Habari za UN
Malawi inachukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto za makazi - Mercy Bety Dube

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 30, 2025 2:16


Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji. Flora Nducha na taarifa zaidi.

SBS Swahili - SBS Swahili
Tafakari, na wito wakuchukua hatua, katika siku ya Kitaifa yakusema Pole

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 27, 2025 9:22


Matukio yame fanyika kote nchini Kuadhimisha Siku ya Kitaifa yakuomba msamaha 26 Mei, hatua ambayo ni kukiri kuondolewa kwa lazima kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza kutoka kwa familia na tamaduni zao.

Habari za UN
Kampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 28, 2025 3:32


Huko mashariki mwa Indonesia, kampuni za usindikaji samaki za PT Chen Woo Fisheries na PT Harta Samudra zimeongeza motisha wa kazi miongoni mwa wafanyakazi wake baada ya kuchukua hatua za kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi. Hatua hizo ambazo zimeweka mazingira ya staha pahala pa kazi zinafuatia mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO na Umoja wa Kampuni za Uvuvi na Usindikaji Samaki nchini Indonesia, AP2H1. Je nini kilifanyika na hali sasa iko vipi? Assumpta Massoi anafafanua zaidi katika makala hii inayoletwa leo hii ikiwa ni siku ya kimataifa ya usalama na afya pahala pa kazi.

Habari za UN
Nzi, panya watapakaa Gaza, UNRWA yahaha kuchukua hatua

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 23, 2025 1:42


Hali si hali huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambako wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari za kiafya ambako panya na wadudu kama vile viroboto na  nzi wamesambaa kutokana na mlundikano wa taka na  ukosefu wa huduma muhimu kama vile maji safi na salama. Assumpta Massoi anaelezea zaidi.

Habari za UN
Wanachama wa WHO wachukua hatua za kujenga uwezo dhidi ya majanga yajayo ya afya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2025 1:50


Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.  "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.

covid-19 umoja afya baada hatua dkt mataifa katiba mkutano shirika mamlaka
Habari za UN
Lazima hatua madhubuti zichukuliwe kukomesha mzunguko wa watu kutoweka nchini Sudan - Radhouane Nouicer

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 9, 2025 3:22


Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi.

Habari za UN
Hatua za haraka zinahitajika sasa kuzuia vifo na kulinda afya ya wanawake na wasichana: UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 7, 2025 2:40


Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua  kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.

sasa umoja siku afya wanawake hatua mataifa shirika
Habari za UN
Getrude Mongella: Ukilinganisha na tulikotoka tumepiga hatua lakini safari bad oni ndefu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 14, 2025 1:57


Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini  tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo. 

beijing safari umoja lakini wanawake hatua mataifa getrude mkutano
Habari za UN
Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 4:58


Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii

kenya umoja makala baraza jamii nchi hatua maendeleo ungana
Habari za UN
Redio imetusaidia kufikisha elimu kwa umma kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 12, 2025 3:12


Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

kenya nairobi umma makala siku hatua elimu kimataifa redio ikiwa
Habari za UN
Mabaya zaidi nchini DRC yanakuja iwapo hatutauchukua hatua, aonya Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 7, 2025 2:18


Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa. Flora Nducha na taarifa zaidi.

drc goma zaidi umoja congo drc haki baraza hatua jamhuri mataifa volker turk mkuu kidemokrasia
Habari za UN
Huu ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na AI-Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 22, 2025 3:20


Viongozi wa kimataifa wa masuala ya kisiasa na biashara wanaokutana Davos Uswisi kwa ajili ya jukwaa la kiuchumi duniani WEF, leo wamekabiliwa na ukweli mchungu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akilaani ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokosa mwelekeo, ikikabiliwa na hatari mbili kubwa ambazo ni mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiyodhibitiwa. Flora Nducha na taarifa zaidiAkizungumza katika Jukwaa hilo la kila mwaka la Kiuchumi Duniani Katibu Mkuu amewaonya viongozi wa dunia na wakuu wa biashara kuhusu vitisho viwili vinavyoongezeka kwa ubinadamu mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiodhibitiwa amesema “Kunapokuja suala la tishio la kimataifa nyuklia sio tishio pekee. Leo hii tunakabiliwa na matishio mawili makubwa ambayo yanahitaji kupewa uziti Mkubwa wa kimataifa na hatua kwa sababu yanatishia kubadili kabisa maisha tunayoyajua, janga la mabadiliko ya tabianchi na upanuzi wa kasi wa wigo wa akili mnemba.”Akikosoa ukosefu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hizi kubwa, Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja haraka ili kushughulikia dunia aliyoiita  dunia inayokosa mwelekeo “Hebu tukabili ukweli , leo hii watu wengi wanapoitazama dunia hawaoni ushirikiano mkubwa wala maarifa ya kutosha . Licha yah atua zilizopigwa uwekezaji katika nishati jadidifu , teknolojia na masuala ya  kiafya ni dunia na matatizo yetu mengi yanazidi kuwa mbaya”Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Guterres amelinganisha uraibu wa dunia kwa nishati ya mafuta na mnyama wa Frankenstein, akisisitiza madhara yake makubwa.Amebainisha kuwa baadhi ya bandari kuu za mafuta duniani ziko hatarini kutokana na viwango vya bahari kuongezeka, jambo linalosababishwa na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi asilia.Katibu Mkuu amekemea viwanda na taasisi za kifedha zinazosuasua kwenye ahadi zao za tabianchi, akisema hii ni kukosa maono na usaliti wa sayansi na watumiaji wanaotafuta uendelevu.Akizungumzia hatari na fursa za AI, Guterres ameelezea kama upanga wa makali mawili. Ingawa inatoa matumaini katika kubadilisha sekta za afya, kilimo, na elimu, ameonya kuhusu hatari kubwa ikiwa haitadhibitiwa.Amesema AI isiyodhibitiwa inaweza kuvuruga uchumi, kudhoofisha imani kwa taasisi, na kuongeza ukosefu wa usawa.Guterres amehitimisha kwa kutoa wito wa mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto hizi muhimu akisema “kubadili mwelekeo wa taasisi kunahitaji kubadili fikra kwa sababu tunakabiliwa na changamoto kubwa zinazoweza kuiangamiza dunia na sishawishiki kwamba viongozi wanalielewa hili.”Amesisitiza umuhimu wa kurekebisha mifumo ya utawala wa kimataifa ili kukabiliana ipasavyo na migogoro ya kisasa, akionya kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu lakini bado haupo katika kiwango cha kutosha.Ujumbe wake ni bayana kwamba sasa ni wakati wa kuchukua hatua za pamoja na za haraka.

Habari za UN
UNEP: Licha ya taarifa za ongezeko la gesi ya methane hatua zinazochukuliwa ni kidogo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 15, 2024 2:05


Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. FKulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina  “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane MARS, ambayo ni sehemu ya UNEP ya uangalizi wa kimataifa wa uzalishaji wa methane IMEO  ambayo unawakilisha fursa ambazo haijatumiwa kwa hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Akizindua ripoti hiyo Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, amesema ili kuwa na nafasi yoyote ya kudhibiti ongezeko la joto duniani, uzalishaji wa methane lazima ushuke, na ushuke haraka."Tunapozingatia kuwa ni asilimia 1 tu ya taarifa 1200 ambazo tulitoa ndizo zilisababisha hatua kuchukuliwa, basi hauitaji kuwa mtaalamu wa hesabu ili kuhesabu ushindi mkubwa unaowezekana hapa. Tuna mifumo iliyothibitishwa ya kutambua uvujaji Mkubwa wa gesi ya methane ili uweze kukomeshwa haraka, mara nyingi kwa ukarabati rahisi na wakati mwingine tunazungumza juu ya kukaza mipira au kubadilisha vichungi.”Ameongeza, kuwa "Serikali na makampuni ya mafuta na gesi ambayo sehemu kubwa ya uchumi wa dunia bado inawategemea lazima waache kupiga domo kwa changamoto hii wakati majawabu yanawatazama usoni. Badala yake, wanapaswa kutambua fursa muhimu ambayo mfumo huu unatoa na kuanza kuchukua hatua kutokana na taarifa kwa kuziba uvujaji ambao unamwaga gesi ya methane ya joto kwenye angahewa.”Amehitimisha kwa kusema, "Serikali na sekta binafsi lazima zizuie uzalishaji wa methane, na lazima zifanye hivyo sasa."Gesi ya Methane kwenye angahewa ni kichocheo cha pili kikubwa cha ongezeko la joto duniani baada ya hewa ya ukaa au CO2 na ina nguvu zaidi ya mara 80 kuliko hewa ya ukaa katika kusambaa kwa muda mfupi.UNEP imesisitiza kuwa utoaji wa gesi ya methane duniani lazima upunguzwe kwa asilimia 40 hadi 45 ifikapo 2030 ili kufikia njia za gharama nafuu zinazopunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5°C.Bado taarifa za sayansi za hivi karibuni zinaonyesha viwango vya angahewa vya methane vimepanda kwa kasi iliyovunja rekodi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

co2 tuna methane unep umoja joto gesi hatua mataifa serikali mkutano ripoti mazingira