POPULARITY
Uchafuzi wa taka za plastiki umekuwa kero kwa dunia, na kuhatarisha sayari yetu, vyanzo vya maji lakini pia afya ya binadamu na wanyama. Mataifa kukutana mwezi Agosti katika muendelezo wa majadiliano ya kutafuta mkataba wa kisheria wa kimataifa kukabili tatizo hili.
Jumatano ya Mei 28 2025, dunia itaadhimisha siku ya njaa ulimwenguni, siku hii ikilenga kutoa hamasa na kuchochea hatua kuchukuliwa ili kumaliza njaa duniani. Kulingana na ripoti ya kimtaifa ya 2025 kuhusu migogoro ya Chakula, zaidi ya watu milioni 295.3 katika nchi 53 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.
Jamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.
Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu huku wengine wakifanya safari za nenda rudi wakivuka mto uliosheheni viboko na mamba. Taarifa zaidi na Selina Jerobon.
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Msasani nchini Tanzania kusikia namna vijana na serikali wanavyolinda Mama Dunia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari ujumbe wa Katibu Mkuu, watoto kulinda mazingira DRC, na kifo cha Papa Francis.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa' kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka. Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.Kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kukumbuka mchango wake wa kutetea walio taabuni. Mathalani shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekumbuka wito wake wa kutaka kila mtu kukaribisha, kusindikiza na kujumuisha wale wote wanaobisha hodi kwenye milango yao.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Makala Anold Kayanda wa Idhaa hii baada ya kukamilika kwa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69 uliofikia tamati mwishoni mwa wiki amezungumza na Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake wa Vyombo vya Habari Tanzania (TAMWA) kuhusu tathimini yake ya hatua zilizopigwa katika miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke.Na katika mashinani fursa ni yake Imani Ramadhani kutoka wilaya ya Kilolo, Iringa nchini Tanzania akieleza jinsi ambavyo maisha ya familia yake ilivyobadilika kupitia mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF, uliofadhiliwa kwa ushirikiano na wadau wake unaolenga kuleta usafi enedelevu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na vyoo safi na salama ili kupunguza hatari za kila mara za magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Binadamu hutegemea rasilimali za wanyamapori na bayoanuwai ili kukidhi mahitaji yao. Tunahitaji chakula, mafuta, makazi, na hata mavazi. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kwamba mifumo ikolojia inaweza kustawi na mimea na wanyama wanaweza kuwepo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Machi 3 mwaka huu, ilikuwa ni fursa ya kutoa uhamasisho wa umuhimu wa wanyama na mimea pori, ili kuongeza ufahamu wa faida zao, na haja ya kuongeza mapambano ya uhalifu dhidi ya wanyamapori na kusababisha athari kubwa za kiuchumi, mazingira na kijamii.Skiliza ufahamu mengi zaidi.
Taka za kieletroniki zinajumuisha vitu vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira na utupaji ovyo ni chanzo kikuu cha madhara, dutu hizi hatari zikiwa na uwezo wa kuchafua udongo, maji, hewa na vyanzo vya chakula. Shirika la E-Waste Initiative Kenya linatoa suluhu ya taka za kieletroniki. Bonyeza hapa kufahamu zaidi.
Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Ayuto Kongwa Kulolwa Kutoka Seminari ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Katoliki Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Usitaje bure jina la Mungu na wale wanao apa wanalitumia vyema? L'articolo Fahamu Mazingira namna linavyo tumika Jina la Mungu? proviene da Radio Maria.
Mkaa wa Briketi hutengenezwa kutoka kwa vumbi la mkaa wa kawaida, taka za kilimo au mabaki ya mbao, na hutumiwa kimsingi kwa mapishi nyumbani, shuleni na hata katika makampuni. Mkaa huu una faida kwa kuwa unapunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza ukataji wa miti lakini pia huwaka kwa muda mrefu na kwa usawa zaidi kuliko mkaa wa kawaida, na kuufanya kuwa chaguo maarufu kwa kupikia.
Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana mwenye umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Makala haya yanazungumzia jinsi Wakulima wengi nchini Kenya wanakumbatia mbinu mpya za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea kwa kutumia madawa ya kiasili badala ya kemikali za viwandani. Kutokana na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kemikali,wakulima hawa sasa wanageukia madawa hayo asilia kuimarisha mazao na mazingira , Mimea kama vile ,pareto,kitunguu saumu,pilipili na hata mtunguja pori yaani sodom apple sasa inatumika kutengeneza madawa hayo.
Utunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo.Bustani hii hutumika kwa kilimo cha mboga, viungo vya upishi kama vitunguu, matunda, au mimea ya kitiba kwa matumizi.
Karibu nusu ya idadi ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wanategemea misitu kwa chakula, nishati, afya, riziki na huduma za mfumo wa ikolojia kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ambao ni takriban watu zaidi ya milioni 40. Kwa kulitambua hilo mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuai huku ukipambana na umasikini UNREDD unaleta nuru kwa raia hususani mashariki mwa nchi hiyo. Ungana na Flora Nducha kwa ufafanuzi zaidi katika makala hii.
Sekta ya mitumba inauwezo wa kuchangia mabilioni ya fedha katika mapato ya taifa, pamoja na kutoa maelfu ya ajira katika mataifa ya bara Afrika na ulaya. Kulinga na utafiti wa Oxford Econimics mwaka uliopita; 2024, sekta ya mitumba pekee ina dhamani ya dola bilioni 8 na imetoa ajiri ya idadi ya zaidi laki moja na elfu 60 kwa vijana nchini Msumbiji, Ghana na Kenya.Lakini hata hivyo wanaharakati wa mazingira wanasema baadhi ya nguo hizo za mitumba zinazoletwa Afrika zinachangia katika uchafuzi wa mazingira.Hili kufahamu Zaidi mwandishi wetu George Ajowi alizuru soko la Gikomba na kutuandalia makala yafuatayo .
Visa vya uchimbaji wa madini haramu vimeongezeka katika nchi mbalimbali barani Afrika .Afrika Kusini ikiwa mfano wa nchi hizo ambayo imeshuhudia miili ya wachimba midogo zaidi ya 70 ikipatikana katika mgodi wa dhahabu usiokuwa rasmi.Kwenye kipindi cha leo tumemuuliza msikilizaji anafkiri nchi za Afrika zimeshindwa kudhibiti uchimbaji haramu wa madini ? na nini kinaweza kufanyika kuzuia uchimbaji huo haramu ?
Visa vya uchimbaji wa madini haramu vimeongezeka katika nchi mbalimbali barani Afrika .Afrika Kusini ikiwa mfano wa nchi hizo ambayo imeshuhudia miili ya wachimba midogo zaidi ya 70 ikipatikana katika mgodi wa dhahabu usiokuwa rasmi.Kwenye kipindi cha leo tumemuuliza msikilizaji anafkiri nchi za Afrika zimeshindwa kudhibiti uchimbaji haramu wa madini ? na nini kinaweza kufanyika kuzuia uchimbaji huo haramu ?
Kijana Mtanzania Gibson Kawago hivi karibuni kupitia kampuni yake ya WAGA inayoshughulika na uvumbuzi wa teknolojia zinazolenga kupambana na uchafuzi wa mazingira ya ulimwengu, ametangaza kuanzisha vifaa vinavyotumika kuchaji magari ya umeme lengo likiwa ni kuwasaidia watu wa eneo lake, Afrika Mashariki kupata huduma ya kuchaji magari yao ili wahame kutoka katika matumizi ya mafuta ya kisukuku kama petroli na dizeli. Lakini je ana majibu gani kwa wale ambao bado hawaoni faida ya ya magari ya umeme kwa mazingira ikiwa bado vyanzo vya umeme ni chafuzi? Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Gibson anafafanua.
Tunaangazia ikiwa tunaweza kuwa na mazingira tulivu bila kelele chafuzi katika maeneo tunayoishi lakini pia sehemu tunazofanya kazi. Tunaangazia ikiwa tunaweza kuwa na mazingira tulivu bila kelele chafuzi katika maeneo tunayoishi lakini pia sehemu tunazofanya kazi.
Makala haya yanazungumzia jinsi dampo la Taka la Nkumba nchini Uganda limekuwa tishio la kimazingira kwa ziwa victoria ambalo ndilo chanzo kuu cha mto Nile.Baada ya dampo la Kiteezi jijini Uganda kuporomoka Agosti 9 mwaka wa 2024 na kuwauwa watu kadhaa,serikali nchini humo ilitoa amri taka zote kutoka Kampala ielekezwe Nkumba karibu na ziwa ,hatua hiyo ikiongeza uchafuzi zaidi wa mazingira .
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher mashariki wa kati, na uwezeshaji wa vijana katika sekta ya kilimo nchini humo. Makala inatupeleka nchini Zimbabwe na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete.Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Zimbabwe kumulika nuru iliyofikia wakulima baada ya Umoja wa Mataifa kuona jinsi mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri shughuli za kilimo.Mashinani fursa ni yake Rukia, kijana wa kike kutoka Tana River nchini Kenya ambaye kupitia mafunzo na uwezeshaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, yeye hasiti kutoa tahadhari za mapema na kuwahamasisha jamii kujiepusha na madhara panapotokea majanga ya mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hivi karibuni mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kuenea kwa jangwa, ulikunja jamvi huko Riyadh, Saudi Arabia ambapo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ulitumia fursa hiyo kuelezea harakati zake za kusaidia wakulima barani Afrika walioathiriwa vibaya na kuenea kwa jangwa. Miongoni mwa mataifa hayo ni Zimbabwe ambako IFAD imeshaanza kuchukua hatua na kuleta nuru kwa wakulima kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
Katika miji ya pwani ya Kenya, vita dhidi ya uraibu vimepata mwelekeo mpya wa kusisimua. Kupitia miradi ya kimazingira, vijana kutoka vituo vya kuwarekebisha tabia hawajizuia tu na mihadarati, bali wanabadili jamii zao pia kupitia miradi hiyo. Mwanahabari wetu Victor Moturi alitembelea Mtopanga, Kaunti ya Mombasa, ambako vijana wamepata matumaini kutokana na utunzaji wa mazingira huku wakipata riziki.
Mkutano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulikamilika mwanzoni mwa Disemba 2024 bila mwafaka kufikiwa, wataalam wa mazingira wakisema pendekezo la kuchakata plastiki wakati nchi nyingine zikiendelea kuzalisha sio suluhu la tatizo hilo. Kwenye makala hii leo tunaangazia athari za plastiki kwa afya na mazingira, suluhu zinazopendekezwa lakini pia kupata ufafanuzi zaidi kilichokwamisha kupatikana kwa mkataba wa kumaliza tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa plastiki.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kuhakikisha wafugaji kuku wasiotumia dawa kiholela wananufaika kiuchumi baada ya kupatiwa mafunzo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani ya Timor-Leste.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe mahususi kwa siku hii, ameueleza ulimwengu kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanawakumbusha kwamba ulimwengu unahitaji uongozi wa watu wenye ulemavu zaidi kuliko hapo awali. Guterres ameeleza kuwa Watu wenye ulemavu tayari wanabeba mzigo mkubwa wa majanga yanayoumiza ulimwengu lakini mara nyingi wananyimwa haki yao ya kuchangia katika suluhu za majanga haya.Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Syria hii leo imezitaka pande zinazopigana nchini Syria zifuate kikamilifu sheria za kimataifa na kuwalinda raia. Hii inatokana na ongezeko kubwa la mapigano tangu tarehe 27 mwezi uliopita ambayo yanatishia kuenea katika maeneo mengine ya nchi.Mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika umeanza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mada ya mkutano huo wa siku tatu ni "Nguvu, Haki, na Watu: Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria kwa Mabadiliko ya Afrika." Mkutano huo wa kila mwaka unalenga kuongeza uwakilishi wa Waafrika katika ufadhili wa kimaendeleo wa kimataifa, ili kuchagiza mustakabali bora wa Afrika.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya watu wenye ulemavu duniani tunakupeleka Timor-Leste, kusini-mashariki mwa Asia kuona jinsi mradi uliofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP umemwezesha Antonio Ornai mwenye ulemavu wa kutoona kushiriki zoezi la kuitikia maonyo ya taarifa za majanga kwenye taifa hilo ambalo hugubikwa na majanga ya asili mara kwa mara kama vimbunga na mafuriko.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 unaoendelea huko Baku Azerbaijan umeleta pia watoto na vijana wanaharakati wa mazingiria kutoka kote ulimwenguni na kuwapatia fursa kuketi katika meza moja na viongozi ili kuhakikisha mustakabali wao umewekwa katika ajenda ya mkataba huo. Jukumu lao kama wachechemuzi wa mabadiliko chanya na hitaji la mazungumzo na ushirikiano kati ya vizazi lilitambuliwa rasmi katika matokeo ya Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF mnamo Septemba 2024.Georgina Magesa, msichana mwenye umri wa miaka tisa na mwanaharakati wa mazingira, ambaye amewakilisha watoto wenzake kutoka Tanzania katika Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan. Anatoa ujumbe mahsusi akianza kwa kusistiza kuwa watoto pia wana mchango katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.“Watoto wenzangu duniani kote, nyie pia mnaweza kuleta mabadiliko chanya. Anza na hatua ndogo pia muwe na ndoto kubwa. Panda miti. Hifadhi maji. Jifunze kuhusu mazingira yetu. Kwa Pamoja vitendo vyetu vidogo vitageuka mabadiliko makubwa”Katika mwaka huu wa 2024 ambao viwango vya joto duniani vimevunja rekodi duniani, watoto na vijana wanaendelea kupaza sauti zao wakihimiza viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka zinazohitajika ili kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Georgina anasema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF liko mstari wa mbele, lakini sasa ni wakati wa mshikamano kwa ajili ya mazingira bora kwa watoto wa leo, na wa zama zijazo..“Kwa viongozi wa dunia walioko hapa leo, hii si kazi ya UNICEF pekee. UNICEF inafanya kazi nzuri na sisi watoto, lakini tunahitaji msaada wako ili kujenga ulimwengu wa kesho ambapo hakuna mtoto anayepaswa kuchagua kati ya afya na elimu yake; ambapo hakuna mtoto anayekunywa maji yasiyo salama; hakuna mtoto anayekosa shule kwa sababu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi; na ambapo kila mtoto ana nafasi ya kuwa na afya bora na elimu bora.”Georgina anatamatisha kwa kusisitiza kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi limenyima watoto haki zao hivyo kwa kila mtu...“Kumbuka unapolinda mazingira unalinda afya, elimu na ndoto za watoto. Mtoto mwenye afya bora na elimu bora anaweza kubadilisha ulimwengu.”Ama kweli watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku nchini Azerbaijan kwenye mkutano wa COP29. Miongoni mwa mambo yanayopigiwa chepuo ni madini ya kimkakati yanayoelezwa kuwa ni jawabu la nishati chafuzi kwa mazingira na tunapata ufafanuzi kutoka kwa Adam Anthony, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasihi viongozi wa kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 wanaokutana huko Rio De Janeiro, Brazil kuwaagiza mawaziri na washawishi wao huko COP29 wahakikishe wanakubaliana juu ya lengo jipya na kubwa la mwaka huu la ufadhili kwa tabianchi nchi. Guterres amesema sambamba na hilo ni vema kukabiliana na taarifa potofu kuhusu tabianchi.Huko Kusini mwa Lebanon, walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha Mpito nchini humo, UNIFIL, wameshuhudia uharibifu mkubwa wa kutisha kwenye vijiji vilivyoko sambamba na eneo la kati ya Israeli na Lebanon lisilopaswa kuwa na mapigano, huku hali ya watoto nchini humo ikizidi kuwa mbaya.Hii leo ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.Mashinani tunasalia huko huko Baku, kwenye COP29 ambapo nampisha msichana mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania, akieleza ni nini anafanya na nini atakachoondoka nacho kwenye mkutano huo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. FKulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane MARS, ambayo ni sehemu ya UNEP ya uangalizi wa kimataifa wa uzalishaji wa methane IMEO ambayo unawakilisha fursa ambazo haijatumiwa kwa hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Akizindua ripoti hiyo Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, amesema ili kuwa na nafasi yoyote ya kudhibiti ongezeko la joto duniani, uzalishaji wa methane lazima ushuke, na ushuke haraka."Tunapozingatia kuwa ni asilimia 1 tu ya taarifa 1200 ambazo tulitoa ndizo zilisababisha hatua kuchukuliwa, basi hauitaji kuwa mtaalamu wa hesabu ili kuhesabu ushindi mkubwa unaowezekana hapa. Tuna mifumo iliyothibitishwa ya kutambua uvujaji Mkubwa wa gesi ya methane ili uweze kukomeshwa haraka, mara nyingi kwa ukarabati rahisi na wakati mwingine tunazungumza juu ya kukaza mipira au kubadilisha vichungi.”Ameongeza, kuwa "Serikali na makampuni ya mafuta na gesi ambayo sehemu kubwa ya uchumi wa dunia bado inawategemea lazima waache kupiga domo kwa changamoto hii wakati majawabu yanawatazama usoni. Badala yake, wanapaswa kutambua fursa muhimu ambayo mfumo huu unatoa na kuanza kuchukua hatua kutokana na taarifa kwa kuziba uvujaji ambao unamwaga gesi ya methane ya joto kwenye angahewa.”Amehitimisha kwa kusema, "Serikali na sekta binafsi lazima zizuie uzalishaji wa methane, na lazima zifanye hivyo sasa."Gesi ya Methane kwenye angahewa ni kichocheo cha pili kikubwa cha ongezeko la joto duniani baada ya hewa ya ukaa au CO2 na ina nguvu zaidi ya mara 80 kuliko hewa ya ukaa katika kusambaa kwa muda mfupi.UNEP imesisitiza kuwa utoaji wa gesi ya methane duniani lazima upunguzwe kwa asilimia 40 hadi 45 ifikapo 2030 ili kufikia njia za gharama nafuu zinazopunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5°C.Bado taarifa za sayansi za hivi karibuni zinaonyesha viwango vya angahewa vya methane vimepanda kwa kasi iliyovunja rekodi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Vijana wanataka wasiachwe nyuma katika kulinda mazingira
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Havana Cuba kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili kusikia kutoka kwa waziziri Zanzibar kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kuhusu Kiswahili.Fedha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni jambo lililopatiwa kipaumbele katika ripoti mpya ya leo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP wakati huu ambapo kiwango cha joto kinazidi kuongezeka kila uchao na kuleta zahma duniani kote.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hii leo watoto 6 wa kipalestina, wamesafirishwa kutoka Gaza kwenye Romania kwa matibabu mahsusi ; watatu wakiwa wanaugua saratani, wawili magonjwa ya damu na mmoja majeraha. Wameambatana na jumla ya waangalizi 15.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umezindua mfumo wa uthibitishaji, kama sehemu ya mchakato wa Luanda wenye lengo la kufuatilia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Rwanda na DRC yaliyoanza kutekelezwa tarehe 4 mwezi Agosti mwaka huu mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunasalia huko huko Havana Cuba, kwenye kongamano la Kiswahili la Kimataifa ambako Dkt. Kisembo Ronex Tendo mshiriki kutoka taasisi ya vijana ya Afrika Mashriki Fest Uganda anaeleza cha kufanya kusongesha Kiswahili nchini Uganda.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
It's another week of storytelling tune in to our latest episode, 'Tutunze Mazingira' as we commemorate Mazingira Day in Kenya. This wonderful narration focuses on the importance of preserving our environment. What can you do to keep the environment safe? Listen to the story to find out. This story is published by the African Storybook Initiative. You can find an openly licensed PDF version of the book here. Author: Fatma Maleta Illustration: Magriet Brink, Offei Tettey Eugene, Rob Owen, Salim Kasamba Narrator: Magdalene Chorongo Host and Editor: Magdalene Chorongo You can reach us via info@edutab.africa or through our social media channels to find out how you can get involved in this project:-) Twitter Facebook LinkedIn Instagram
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, mada ni Mama Bikira Maria katika ndani ya Mazingira yetu. L'articolo Kwanini tunajifungamanisha Maisha yetu na Mama Bikira Maria?. proviene da Radio Maria.
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa wanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu ambao wamekuja hapa makao makuu ya umoja wa mataifa kuwa sehemu ya utatuzi katika mijadala mikuu ya UNGA79. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda DRC.Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí kutokana na kina cha baharí.Mjadala mkuu wa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79 umeingia siku ya pili hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nasi tunaendelea kuzungumza na washhiriki mbalimbali wakiwemo kutoka asasi za kiraia kusikia maoni yao kuhusu mkutano huu. Flora Nducha amebahatika kuongea na mmoja wao kutoka nchini Zimbabwe.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS.Na mashinani fursa ni yake mwananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini akiwasilisha ujumbe wake kwa viongozi wanaoshiriki mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataiafa, UNGA79 hapa New York, Marekani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí kutokana na kina cha baharí. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia viongozi wa dunia amewataka wachukue hatua za kijasiri kunusuru maisha na mbinu za kujipatia vipato kwa watu zaidi ya milioni 900 wanaoishi uwanda wa chini wa pwani ulio hatarini kuzama kutokana na kina cha baharí kuongezeka.Kwa Tanzania Umoja wa Mataifa umeanza kuchukua hatua kama unavyosikia kutoka kwa Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la UN la Mataifa la Mazingira, UNEP nchini humo huku tukipata ufafanuzi wa madhara ya ongezeko la kina cha baharí kwenye eneo lao kutoka kwa Segule Segule, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Maji Pangani
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Hii leo jaridani tunaangazia jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kwa kifupi HLPF ambalo linakaribia kufikia ukingoni na pia ukame nchini Kenya. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Yemen, kulikoni? Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu. Mwandishi wetu wa DRC George Musubao amefika huko na kutuandalia makala ifuatayo. Kwako George.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Kenya kuangazia awamu ya pili ya mradi wa PLEAD unaoendesha na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za msaada kwa wakulima nchini Ukraine, ripoti ya UNICEF kuhusu watoto katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi na hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa Paris. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"TATABISI", salía hapo hapo!Zaidi ya watoto bilioni moja wako katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu Hatari za Tabianchi kwa Watoto iliyofanywa na Muungano wa Mpango wa Haki za Mazingira za Watoto (CERI) ambao unahisisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF, Plan International na Save the Children. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo mjini Paris, Ufaransa kupitia hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa amerelea ombi lake la mageuzi makubwa ya muundo wa fedha wa kimataifa na kuwasilisha mapendekezo yake ikiwa ni pamoja na kichocheo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDG) ili kusaidia nchi zinazoendelea na zinazoibukia kiuchumi ili kuurudisha ulimwengu kwenye mstari wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua mpango wa pamoja kwa ushirikiano na shirika la FSD (Fondation Suisse de Déminage) kusaidia wakulima wadogo na familia za vijijini zilizoathiriwa zaidi na vita huko nchini Ukraine.Na leo katika jifunze Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "TATABISI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa imetoa wito kwa kila mtu kusaidia vita ya kutokomeza plastiki kwa faida ya mustakbali wa mazingira ya dunia na viumbe vyake.Maudhui ya siku ya mazingira mwaka huu ni “tokomeza taka za plastiki” utajiuliza kwa nini? Jibu analo Inger Anderson mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP kupitia ujumbe wake wa siku hii anasema ni, “Kwa sababu taka za plastiki Kwa sababu zinasonga mifumo yetu ya ikolojia, zinapasha joto hali ya hewa yetu na kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu afya zetu. Urejelezaji sio mazingaombwe. Mifumo yetu haiwezi kuhimili. Mabadiliko lazima yafanyike katika mzunguko mzima wa maisha wa plastiki. Ni lazima kukataa vitu visivyo vya lazima vya matumizi ya mara moja. Tupange upya bidhaa na vifungashio ili kutumia plastiki kidogo, tutumie tena, turejeleze, tuelekeze upya na tubadilishe mifumo yetu.”Amesema kwa njia hiyo ndio Dunia itaweza kuengua plastiki katika mifumo ya ikolojia na uchumi na hilo amsisitiza ni jukumu la kila mtu, “ Kila mtu lazima atimize wajibu wake. Serikali zinaweza kutoa matokeo madhubuti kwenye mpango huo wa kukomesha uchafuzi wa plastiki kwa majadiliano. Biashara zinaweza kuchukua mtazamo mpya, sekta ya fedha inaweza kuweka mtaji wake katika kusongesha mabadiliko, na wananchi wanaweza kutumia sauti, kura na pochi zao kuleta mabadiliko.Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono wito huo amesema, “Kila mwaka, zaidi ya tani milioni 400 za plastiki huzalishwa duniani kote - theluthi moja ambayo hutumiwa mara moja tu. Kila siku, zaidi ya lori 2000 za takataka zilizojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito na maziwa yetu. Matokeo yake ni janga. Chembechembe za plastiki huishia kwenye chakula tunachokula, maji tunayokunywa, na hewa tunayopumua.”Ameongeza kuwa plastiki imetengenezwa kutokana na nishati ya kisukuku na kadiri tunavyozalisha plastiki zaidi, ndivyo mafuta ya kisukuku tunavyoyachoma, na ndivyo tunavyofanya mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi kuwa mbaya zaidi.Hata hivyo amesema kuna suluhu “Mwaka jana, jumuiya ya kimataifa ilianza kujadili makubaliano ya kisheria ya kukomesha uchafuzi wa taka za plastiki. Hii ni hatua ya kwanza ya matumainii, lakini tunahitaji kila hatua kutekelezwa.”Ameongeza kuwa ripoti mpya ya UNEP inaonyesha, “tunaweza kupunguza uchafuzi wa taka za plastiki kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2040 ikiwa tutachukua hatua sasa kurejeleza, kuchakata tena, kuelekeza upya, na kutenganisha plastiki.”Kwa mantiki hiyo amesisitiza “Ni lazima tufanye kazi kama kitu kimoja, serikali, kampuni na watumiaji kwa pamoja ili kuondokana na uraibu wetu wa matumizi ya plastiki, kuchagiza kutokuwa na taka za plastiki na kujenga uchumi wa kweli. Kwa pamoja, tutengeneze maisha safi, yenye afya na endelevu zaidi kwa wote.”Siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila mwaka Juni 5.
Tathmini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, inaashiria kuwa fani ya mitindo huchangia asimilia kati ya 2 hadi 8 ya gesi ya ukaa kwenye mazingira.Shughuli ya kutia rangi vitambaa ina mchango mkubwa kwenye vyanzo vya uchafuzi wa mifumo ya maji kote ulimwenguni. Na ni kwa mantiki hiyo ,mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya Thelma Mwadzaya amefuatilia harakati za kuepusha uchafuzi wa mazingira kwa kutumia nguo tena na tena huko nchini Kenya.
Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.Kutoka jijini Mwanza kaskazini-magharibi mwa Tanzania, Evarist Mapesa alikutana na Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Sayansi wa Maji na Mazingira yake na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bahati Mayoma, akitaka kufahamu athari za taka za plastiki kwa viumbe hai waishio kwenye maji na hapa mhadhiri huyo anaeleza.