Podcasts about elimu

  • 43PODCASTS
  • 525EPISODES
  • 18mAVG DURATION
  • 1WEEKLY EPISODE
  • Jun 18, 2026LATEST

POPULARITY

20192020202120222023202420252026


Best podcasts about elimu

Latest podcast episodes about elimu

MAELEZO PODCASTS
Kuelekea Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa, Paris - Ufaransa

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jun 18, 2026 34:12 Transcription Available


Send us Fan MailSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inatarajia kufanya Kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili kati ya Julai 4 - 7, 2026, jijini Paris, Ufaransa.Tumezungumza na Bw. Tito Lulandala, Afisa Utamaduni Mwandamizi, kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Maandalizi ya Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa kuhusu maendeleo ya Kiswahili, fursa zilizopo, ajenda muhimu kuelekea kongamano la pili la kimataifa la Kiswahili nchini Ufaransa, pamoja na mafanikio ya kongamano la kwanza lililofanyika Havanna, nchini Kuba, mwaka 2024.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali

tanzania kuba bw pili umoja havanna kiswahili julai elimu jamhuri mataifa serikali maendeleo ufaransa shirika kimataifa
Siha Njema
Shule ya Mali jijini Nairobi inavyowasaidia watoto wenye Austism pamoja na wazazi

Siha Njema

Play Episode Listen Later Jun 16, 2026 10:17


Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha  na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo

Habari za UN
10 JUNI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 10, 2026 10:28


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina maalum ambayo kama nilivyokujuza hapo awali inaangazia mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa chini ya kauli mbiu “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.”Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma. Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni Nassriya Nassir Ali mbunge wa watu wenye ulemavu kutoka nchini Tanzania, yeye anaulemavu wa kusikia au kiziwi. Leah Mushi amefanya mahojiano naye na hapa mkalimani wake wa lugha ya Alama Tusajigwe Ernest anajibu kwa sauti. Pia tunakuletea mhtasari wa habari tukimulika haki za elimu kwa watoto nchini Sudan, usalama wa mabaharia na judhibiti wa kusambaa kwa virusi vya Ebola hasa wakati huu wa michezo ya kimataifa ya kuwania kombe la dunia. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Wimbi la Siasa
Vijana nchini Kenya wanavyotumia teknolijia kuhamasisha elimu ya kisiasa

Wimbi la Siasa

Play Episode Listen Later Jun 10, 2026 9:39


Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vijana nchini humo, wanakumbatia teknolojia kuwafikia vijana wengi hasa  wale wa rika la Gen Z, kujiandikisha kama wapiga kura na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Je, hatua hii inaweza kuleta mwamko mpya wa kisiasa nchini Kenya ? Mwanahabari wetu Benson Wakoli alikutana na kuzungumza na vijana hao.

gen z kenya vijana elimu
Siha Njema
Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto

Siha Njema

Play Episode Listen Later Jun 6, 2026 9:43


Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha changamoto za afya ya akili anavyoeleza mwaandishi wetu Petronila Ogalo.

kenya afrika akili afya watoto elimu mataifa busia miongoni
Habari za UN
06 MEI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo' iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 6, 2026 2:34


Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?

new york tanzania unesco umoja haki kwa siku watu taifa tume wote elimu mataifa serikali marekani jukwaa
MAELEZO PODCASTS
Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Apr 25, 2026 38:36 Transcription Available


Pata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.Support the showIdara ya Habari MAELEZO 

pata seli mundu elimu dkt ugonjwa
Habari za UN
Watengeneza maudhui nchini Kenya waaswa kuwa walinzi wa amani na ukweli mtandaoni - UNESCO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 3:05


Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI'), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Rashid Malekela anaeleza zaidi.

Habari za UN
20 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 10:44


Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili hapa Makao Makuu, mafunzo Kenya ya "Social Media 4 Peace" yaani ya kuondoa habari potofu na deepfakes mtandaoni, na mlo shuleni shuleni nchini Tanzania.Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili (UNPFII) limefungua pazia leo Aprili 20 ikiwa ni kikao cha ishirini na tano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili.  Maudhim aka huu yakimulika kuhakikisha afya ya watu wa jamii za asili ikiwemo kwenye mizozo.Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI'), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Karibu Rashid Malekela utujuze zaidi.Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
Lishe yarejesha matumaini ya elimu Kigoma, Magdalena arejea shuleni na kuwa chanzo cha mabadiliko

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 20, 2026 3:02


Elimu imeanza kung'aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni. Feissal kirwa anasimulia.

japan tanzania umoja kuwa elimu mataifa serikali
Habari za UN
10 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 10, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea nchini Sudan, juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya, na kazi za wanafunzi katika utunzaji wa mazingira huko Zanzibar.Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan.Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko hayaBaada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
Mwanafunzi Ahmad Omar aongoza mabadiliko ya kijani shule ya Kisiwandui Zanzibar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 10, 2026 2:35


Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko haya.

tanzania unicef rota zanzibar umoja wakfu shule elimu mataifa shirika mazingira
Habari za UN
08 APRILI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 8, 2026 11:00


Jaridani tunaangazia sitisho la mapigano nchini Iran, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na elimu kwa watoto walioathiriwa na vita nchini Sudan.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano kwa wiki mbili, wakati huu ambapo vita hiyo iliyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran ikiingia siku ya 40. Kwa upande wa Lebanon hali bado ni tete kwani Israel inaendelea na mashambulizi katika mji wa Beirut.Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!

Habari za UN
UNICEF na Benki ya Dunia warejesha matumaini ya elimu kwa watoto nchini Sudan kupitia programu mbadala za kujifunza

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 8, 2026 2:41


Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.

Habari za UN
Elimu ya haki za kisheria inapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii - Wakili Mengo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 31, 2026 5:29


Wiki iliyopita Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kilikunja jamvi baada ya wiki mbili za kujadili mada ya haki, haki za kisheria na kuchukua hatua kuhakikisha haki za wanawake na wasichana zinapatikana. Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya  ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.

kenya wiki haki makala jamii mengo wanawake elimu
Habari za UN
13 MACHI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 13, 2026 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ujumbe wa kijana kutoka Uganda anayehudhuria mkutano wa CSW70, na mradi wa intaneti kwa wanafunzi nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa taifa hilo la Mashariki ya Kati lililotumbukizwa kwenye vita isiyowahusu.Mikutano hii inayokutanisha Umoja wa Mataifa watetezi wa haki za wanawake dunia inawapa ujasiri vijana wa kuona kuwa nao wana uwezo na fursa ya kusaka majawabu katika jamii zao. Ni kauli ya kijana wa kike kutoka nchini Uganda anayeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani (CSW70 ) unaoendelea hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity'. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Habari za UN
UNICEF: Mradi wa intaneti shuleni waleta mapinduzi ya kidijitali nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 13, 2026 2:52


Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity'. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa. Rashid Malekela amefuatilia maendeleo ya mradi huo katika shule za Enkasiti na Moipei, na hii hapa ni taarifa yake.

Habari za UN
Mpango wa MEMKWA Tanzania wampa fursa ya elimu mtoto Sanita

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 9, 2026 2:40


UNICEF: Mradi wa Elimu Kwa Waliokosa warejesha matumaini kwa mtoto wa kikeNchini Tanzania Mpango wa Elimu Kwa Waliokosa au MEMKWA umemwezesha msichana mmoja kuweza kupata haki yake ya msingi ya elimu na kisha kuwa na matumiani ya kutimiza ndoto yake ya kuwa nesi au muuguzi. Simulizi ya Assumpta Massoi inafafanua kisa hicho kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Nats.. 00'00 – 00'14” (Kwa majina naitwa…. Wanaenda shule)Tupo wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania Sanita huyo alishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule.(Sauti ya Sanita)Amerejea shuleni kupitia mradi wa MEMKWA uliotambua kuwa zaidi ya watoto milioni 2 wenye umri wa kuwa shule ya msingi nchini Tanzania hawako shuleni hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau UNICEF na serikali ya Qatar wakafanikisha MEMKWA.Tangu mwaka 2022 zaidi ya watoto elfu 98 katika mikoa 3 ya Tanzania ikiwemo Kigoma, wamenufaika na MEMKWA.Nats…(Darasani) 0'30-0'36” (Shikamoo mwalimu…….la mstatili)Sasa tumo darasani na Sanita ni miongoni mwa wanafunzi. Rashid, mwalimu wa Sanita anaelezea.(Sauti ya Rashid- Mwalimu wa Sanita)Sanita anakwenda ubaoni kujibu swali. Mwalimu anauliza..Nats.. 1'00” – 1'03” (Ameweza, haya tumpigie makofi….fx makofi)Sanita anafunguka..(Sauti ya Sanita)Kitendo cha Sanita kupata haki ya elimu kinamwezesha hata Rhoedesia ambaye ni mama mzazi wa Sanita kuwaza mustakabali wa binti yake.(Sauti ya Rhoedesia) 1'11” -1'20” (NInavyomuona mwanangu anaenda…. ili apate kazi)Mwalimu Rashid anatamatisha na tathmini ya mradi wa MEMKWA na ombi mahsusi.(Sauti ya Mwalimu Rashid)

Habari za UN
Komesha FGM SASA: Mradi wa kupambana na ukeketaji waleta nuru nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 4, 2026 4:15


Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA nchini Kenya kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya wanatekeleza mradi wa kukomesha ukeketaji ambapo waathirika wanatumika kutoa elimu kwa mabinti na jamii ili kuondokana na mila hiyo potofu. Kaunti ya Marsabit , iliyoko Kaskazini mwa nchi ya Kenya, iko mpakani na nchi ya Ethiopia. Kaunti hii ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya ile ya Turkana wakazi wake wengi ni wafugaji, na mbali na changamoto za mabadiliko ya tabianchi wanawake wa hapa wamepitia masahibu ya ukeketaji au kwa lugha ya kiingerza Female genital mutilation (FGM). Audio fileShirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) chini ya Ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya nchini Kenya wanatekeleza mradi uitwao Komesha FGM SASA Kila muathirika wa ukeketaji anayo hadithi ya kusimulia na ndio maana kwa namna ya kipekee mradi huu unawatumia waathirika hao, kuwaelimisha wanajamii wenzao ili kuondokana na tamaduni ya ukeketaji. Prisca Lekuraki ni mmoja wao. “Mimi nilipitia magumu sana, baada ya kukeketwa nilipata shida sana, ni Mungu ndio amenisaidia mpaka nimefika hapa. Nilipoenda kujifungua mtoto wangu wa kwanza nilipata shida sana, kila nikienda kuzaa nikawa napitia shida sana, sasa hivi nina watoto watatu na nikajifunga nisizae tena. Niliona vile nimeumia nikasema siwezi kukubali binti yangu naye aumie hivyo. Na hiyo ndio ilinifanya niamke niungane na wengine kuhamasisha kukataa ukeketaji.”Ameongeza kuwa katika tamaduni zao wanamila nyingi nzuri sana na wanaweza kuziendeleza na kuachana na hii mila moja ya ukeketaji kwani ni mbaya na inamadhara. Prisca amepongeza mradi wa Komesha FGM SASA wa UNFPA kwa kuwasaidia kuwafikia wale ambao awali ilikuwa ni vigumu kuzungumza nao.“Kuna mahali wametufikisha na tumeona mafanikio, hapo awali tulikuwa tunaweza kwenda kwa wamama, vijana na watoto ila wale watu ambao ilikuwa inatushinda kuwafikia ilikuwa ni wazee. Lakini hii kukutana na wazee, wamama na wanakijiji kwa ujumla imesaidia, kwasababu nilikutana na wakina mama wakaniambia ile kitu mlikuwa mnasema tumeona ni uhalisia na tumeona inaweza kufanyika.”Mwingine aliyeathirika na ukeketaji ni Nasarai Learo anasema ukeketaji umechukua nguvu zake.“Mimi sina nguvu kama yule mama ambaye hajakeketwa, nilienda kuwaambia wamama wasikekete watoto wao, lakini wakaniambia wananifahamu na nilipoolewa nilkuwa mdogo sana na wao ndio walionishika nikatetetwe nikiwa mdogo. Lakini mimi niliwaeleza mimi sikuwa najua hiki kitu ni kibaya lakini sasa hivi nimekuwa na elimu na nimejua ubaya wake.”Nasarai anaamini kuwa iwapo jamii itapata elimu basi itabadilika“Jamii yetu sanasana haina elimu, tukiona jamii yetu watu wachache ndio wamesoma na wengi wakisoma watapata hiyo elimu zaidi na watakuja kuikomesha FGM. Mimi naamini kwamba miaka 10 inayokuja mambo ya kukeketa wasichana hatutasikia tena.” Elimu ya kutokomeza ukeketaji inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni, katika vikao vya jumuiya na mashuleni. 

Habari za UN
24 FEBRUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 24, 2026 11:41


Tuliyokuandalia katika Jarifada la Habari hii leoNi miaka miine tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, Umoja wa Mataifa wataka vita vikome mara moja kuwapunguzia madhila raiaHuko Gaza Shirika la UNICEF limezindua mpango wa Gaza we want au Gaza tuitakayo ili kukusanya maoni ya watoto baada ya miaka miwili ya vitaHuko The Hague Uholanzi kikao cha majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, (ICC) cha kuthibitisha iwapo kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakama aliyekuwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kinaendeleaMada yetu kwa kina inajikita Tanzania kuangazia juhudi za kuhakikisha wasichana na wanawake hawaachwi nyuma katika sayansiNa katika jifunze Kiswahili utasikia maana na neno "PEMBUA"

Habari za UN
18 FEBRUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 18, 2026 12:01


Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya Akili Mnemba na wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha, waumini wa dini ya kiislamu wakati huu wa Ramadhani katika ukanda wa Gaza, na matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho huko Mwanza nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesema wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha ya kiingereza content creators wanakabiliwa na hatari ya kupoteza hadi asilimia 24 ya mapato yao ifikapo mwaka 2028 kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba, au AI.Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kipindi kinachoambatana na sio tu ibada bali pia mlo kama vile futari na daku. Hata hivyo kwa wakazi wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na kimabavu na Israeli hali si hali kwani mlo na mengine yanayoambatana na kipindi hiki vinasalia kuwa ndoto.Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kupitia Ushirikiano wa Upatikanaji na Ufikishaji wa Huduma (ADP), inaendesha mpango wa majaribio wa kihistoria katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, na Kigoma ili kutoa matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho yaliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!

Habari za UN
Watengeneza maudhui kupoteza mapato kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 18, 2026 3:43


Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesema wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha ya kiingereza content creators wanakabiliwa na hatari ya kupoteza hadi asilimia 24 ya mapato yao ifikapo mwaka 2028 kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba, au AI. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

ai unesco kasi umoja akili elimu mataifa maendeleo shirika teknolojia
Habari za UN
CAMFED yaendelea kujengea uwezo wanafunzi wa kike nchini Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 28, 2026 2:42


Nchini Tanzania shirika la kiraia la kusongesha elimu kwa watoto wa kike, CAMFED limeendelea kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kuwezesha wanafunzi wa kike kuimarika sio tu kimasomo darasani bali pia stadi za maisha na hatimaye wawajengee uwezo wenzao. Katika taarifa hii, John Kabambala wa Redio washirika Kids Time FM amezfuatilia kinachofanyika. 

tanzania sdgs katika vijana elimu camfed redio
Habari za UN
27 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2026 12:40


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za vijana katika kuchagiza maisha wayatakayo kuanzia kujiondoa kwenye umasikini, ukosefu wa usawa hadi kwenye upatikanaji mdogo wa elimu bora na kazi zenye staha.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika pamoja na manusura wa mauaji ya kimbari ya holokosti hususan yale yaliyofanywa na manazi wa kijerumani, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa Baraza Kuu kumefanyika kumbukizi ikileta pamoja manusura waliotoa shuhuda za waliyopitia wakikimbia maeneo kadhaa ikiwemo Austria baada ya kutwaliwa na wajerumani.Huko Geneva, Uswisi ambako inaelezwa kuwa kurejesha mfumo wa elimu uliosambaratika huko Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ni jambo la kuokoa maisha, na kuwarudisha watoto shuleni lazima kiwe kipaumbele cha haraka, amesema James Elder Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Umoja wa Mataifa umezindua Mpango wa Mahitaji na Hatua za Kibinadamu wa dola milioni 852 kwa ajili ya Somalia, huku ukionya kuwa ukosefu mkubwa wa ufadhili utaacha mamilioni ya watu walio katika mazingira magumu bila msaada wa kuokoa maisha, huku hali ya kibinadamu kuendelea kuzorota.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "TWINGA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
23 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 23, 2026 11:40


Hii leo jaridani tunaangazia miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, AI katika elimu na juhudi za kuhakikisha wananchi wamepata huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi nchini Niger.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hii leo historia na dharura vilikutana chini ya paa moja. Ni miaka themanini tangu Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC lifanye kikao chake cha kwanza tarehe 23 Januari 1946 na linaadhimisha hatua hii muhimu wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni wa maamuzi kwa mustakabali wa ushirikiano wa kimataifa.Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Huko Afrika Magharibi taifa la Niger linaongeza uwezo wa wananchi wake walio maeneo hatarishi na ya pembezoni kufikia huduma bora za afya kupitia kliniki tembezi. Kwa usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, kliniki hizo tembezi zinaziba pengo la wale wanaoishi mbali na vituo vya afya, na wakati huo huo kuhakikisha umbali sio tena kikwazo cha mtu kupata huduma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
UNESCO yataja dhana potofu, na hatari ya kutumia AI mashuleni

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 23, 2026 3:09


Wakati dunia ikijiandaa kusherehekea Siku ya Elimu Duniani hapo kesho tarehe 24 Januari, 2026 embu sasa tuangazie mjadala unaozidi kushika kasi duniani kote kuhusu matumizi ya Akili Mnemba - AI katika elimu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO linasisitiza kuwa si kila kilicho cha kisasa ni suluhisho la changamoto za elimu duniani.Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Habari za UN
22 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 22, 2026 11:26


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumsikia kijana Baraka Ayubu ambaye amekuwa kielelezo cha jinsi teknolojia inavyoweza kuleta mageuzi katika mifumo ya ujifunzaji na ustawi wa wanafunzi.Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa uchunguzi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaohusishwa na vita kati ya Hamas na Israel huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel utaendelea, licha ya kuanzishwa kwa Bodi ya Amani ya Gaza ambayo imezinduliwa hii leo na Rais wa Marekani Donald Trump.Tuelekee nchini Kenya ambako zaidi ya watu milioni mbili wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa uhakika wa kupata chakula kufuatia msimu wa mvua fupi za mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2025 kuwa mkavu zaidi kuwahi kurekodiwa. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, uhaba wa maji unalazimu familia kutegemea vyanzo visivyo salama, jambo linaloongeza hatari ya kipindupindu, homa ya matumbo, na magonjwa ya kuhara.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani, WHO, la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na la Makazi, UN-Habitat, kwa pamoja wamezindua mwongozo mpya unaozitaka serikali na viongozi wa miji kuweka kipaumbele kwa watoto katika upangaji wa miji ili kurejesha maeneo ya michezo yanayozidi kutoweka.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya "SIKU ZA MUAMBO" katika muktadha wa uchumi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

MAELEZO PODCASTS
Elimu kwa umma kuhusu zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI (2022)

MAELEZO PODCASTS

Play Episode Listen Later Jan 15, 2026 2:02


Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 - 2025/26 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (2021/22 - 2025/26), Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050 na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063. Taarifa hizi zitaipima Tanzania katika hatua iliyofikia kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu; Mpango ambao unalenga kuleta usawa na kutokomeza umaskini wa aina zote ukiwemo umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma.Idara ya Habari MAELEZO

tanzania afrika zanzibar sensa tatu umma dira watu taifa mwaka elimu serikali maendeleo afrika mashariki
Habari za UN
09 JANUARI 2026

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 9, 2026 11:17


Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Uganda, elimu kwa watoto nchini Sudan leo ikitimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini humo, na juhudi za wanawake za kuhifadhi misitu huko Narok nchini Kenya.Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa na ukandamizaji, vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, na waandishi wa habari.Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani yanchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP), nchini Kenya, kupitia mradi wa kuhimili tabianchi au Climate Promise Guarantee, limewawezesha wanawake wa jamii ya asili katika Kaunti ya Narok, nchini humo kuongoza juhudi za uhifadhi wa misitu huku wakilinda urithi wao wa kitamaduni na kuboresha maisha ya familia zao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

kenya uganda sudan unicef undp umoja hii elimu jeshi mataifa maendeleo shirika ikiwa kaunti uchaguzi mkuu
Habari za UN
UNICEF yaonya uhaba wa fedha wawaweka na watoto hatarini nchini Sudan

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 9, 2026 3:21


Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani ya nchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita. Tuungane na Rashid Malekela kwa taarifa zaidi

sudan unicef rsf umoja watoto elimu jeshi mataifa shirika fedha
Habari za UN
UNICEF na KISE wawapiga jeki watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir nchini Kenya

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 1, 2025 3:05


Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizi kama anavyofafanua Sheilah Jepngetich  katika taarifa hii

kenya unicef umoja katika watoto elimu mataifa shirika kaunti
Habari za UN
01 DESEMBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 1, 2025 11:33


Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU.Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!

kenya pooja arv umoja hii katika siku watu vijana elimu mataifa shirika anshu sharma desemba
Habari za UN
Guterres atumia siku ya elimu kuhusu tsunami kukumbusha mkakati wa kujikinga

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2025 1:51


leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu Tsunami Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kujiandaa dhidi ya mawimbi hayo makubwa ya bahari yanayotokana na tetemeko chini ya bahari. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Asante Assumpta,Katika ujumbe wake, Guterres amesema maandalizi hayo yanahusisha kuweka mifumo ya kutoa maonyo ya mapema au tahadhari kwenye kila ufukwe, jamii na kokote kule.Bwana Guterres amefafanua kuwa tsunami si matokeo ya mara kwa mara lakini pindi yanapotokea madhara yake yanaweza kuwa makubwa na hata kusababisha vifo.“Husababisha vifo vya maelfu na hata mamia ya maelfu ya watu. Lakini kuna mbinu za kuweka watu salama,” anasema Guterres.Ametolea mfano janga la tsunami kwenye bahari ya Hindi mwaka 2004, janga ambalo lilisababisha dunia kuamua kuwekeza katika mifumo ya kutoa maonyo mapema.“Miongo kadhaa baadaye, uamuzi huo umelipa,” amesema Katibu Mkuu akitolea mfano tetemeko kubwa la ardhi lililokumba pwani ya Urusi mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu akisema, “lilisababisha tahadhari kwa mamilioni ya watu kuanzia pwani za Japani hadi visiwa vilivyoko bahari ya Pasifiki hadi California.”Ingawa hivyo amesema madhara ya janga hilo la tsunami yanaendelea kubadilika kutokana na mabadiliko kadhaa ikiwemo yale ya tabianchi.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa akieleza kuwa kuheshimu baharí ni kutambua nguvu yake anasema,  “kiwango cha maji ya bahari kikiongezeka, na idadi ya watu wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari ikiongezeka, mifumo ya kutoa maonyo mapema nayo inahitaji uwekezaji zaidi na kuboreshwa,”Ni kwa mantiki hiyo amesema hilo ndio lengo la mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mfumo wa Tahadhari kwa Wote ulioanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anafikiwa na mpango wa utoaji onyo mapema dhidi ya tsunami ifikapo mwaka 2027.Maadhimisho ya mwaka huu ni ya 10, ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha siku hii kupitia azimio namba 70/203 la mwaka 2005.

california tsunamis hindi guterres umoja katika siku julai lakini wote japani elimu mataifa mkuu maadhimisho
Habari za UN
UNMISS yasaidia katika utoaji wa elimu ya uraia nchini Sudan Kusini

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 22, 2025 3:34


Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi. Leah Mushi anatuletea taarifa ikiangazia namna Sudan Kusini inavyojiandaa na uchaguzi wake mkuu mwakani 2026. 

katika vijana elimu unmiss uchaguzi sudan kusini
Habari za UN
10 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 10:38


Hii leo jaridani tunaangazia mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel, sauti za wanawake nchini Kenya ambazo zimeanza kusikika kwa uthabiti, zikililia haki, heshima, na usawa, na Puja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imekaribisha uamuzi wa Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel kumtangaza Maria Corina Machado kiongozi wa upinzani nchini Venezuela kuwa mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel, kwa kutambua kazi yake ya kuendeleza matumaini ya demokrasia ya watu wa Venezuela.Katika kila kona ya Kenya, sasa sauti za wanawake zimeanza kusikika kwa uthabiti, zikililia haki, heshima, na usawa. Kupitia msaada wa mashirika ya kimataifa kama shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), mabadiliko yanaanza kushika kasi.Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliongeza kwenye orodha ya turathi za dunia za tamaduni zisizoshikika au kugusika, Puja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike aitwaye Durga dhidi ya jini Mahishasura, ikiwa ni ishara ya ushindi wa mema dhidi ya maovu"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Sasa Pooja Durga si ibada tu ya kidini bali inasongesha SDGs

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 4:09


Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliongeza kwenye orodha ya turathi za dunia za tamaduni zisizoshikika au kugusika, Pooja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike aitwaye Durga dhidi ya jini Mahishasura, ikiwa ni ishara ya ushindi wa mema dhidi ya maovu. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

bali sdgs pooja durga sasa umoja elimu ibada mataifa shirika
Habari za UN
06 OKTOBA 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 6, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya makazi duniani, kazi za walimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu na afya ya uzazi hasa wakati wa kujifungua na kuepusha vifo kupiti uvujaji damu.Leo ni Siku ya Makazi Duniani, na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuchukua hatua za haraka kujenga miji jumuishi, imara na salama hasa kwa mamilioni ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi wanasema miji sasa ndiyo inabeba mzigo mkubwa wa migogoro duniani lakini pia ndiyo kitovu cha suluhisho.Uongozi wa kugawana majukumu na mashauriano ya kina na walimu ni mambo muhimu katika kuboresha ustawi wa waelimishaji na matokeo ya kujifunza ya wanafunzi, amesema Carlos Vargas, Mkuu wa Kitengo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Walimu kwa Elimu 2030 katika UNESCO.Mashirika ya afya duniani yametoa miongozo mipya yenye lengo la kuokoa maisha ya maelfu ya wanawake wanaopoteza maisha kutokana na kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua hali inayojulikana kama postpartum haemorrhage au PPH.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

unesco guterres umoja hii pph carlos vargas siku wanawake elimu mataifa mkuu oktoba shirika kimataifa walimu mashirika
Habari za UN
UNESCO: Uongozi shirikishi ni muhimu kwa mafanikio ya walimu na matokeo ya wanafunzi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 6, 2025 2:06


Uongozi wa kugawana majukumu na mashauriano ya kina na walimu ni mambo muhimu katika kuboresha ustawi wa waelimishaji na matokeo ya kujifunza ya wanafunzi, amesema Carlos Vargas, Mkuu wa Kitengo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Walimu kwa Elimu 2030 katika UNESCO.

unesco carlos vargas elimu mkuu kimataifa walimu
Habari za UN
Angelique Kidjo, Mwanamuziki, asimulia safari yake ya elimu akiunga mkono wito wa UNICEF kwa viongozi wa Afrika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 1, 2025 3:22


Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima. Anold Kayanda anaeleza zaidi.

Habari za UN
UN Tanzania yatoa elimu ya amani na utangamano kwa wanafunzi kuelekea

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 19, 2025 2:30


Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu  “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.” Katika warsha hiyo, baadhi ya wanafunzi wameeleza walichojifunza na namna elimu hiyo inavyoweza kuwanufaisha katika maisha yao ya kila siku. Shuhuda wetu katika mafunzo ni Sabrina Saidi anatupasha ilivyokuwa

dar tanzania dunia salaam sasa umoja katika siku elimu mataifa kimataifa jumapili septemba
Habari za UN
UNICEF yahimiza Taliban kuruhusu wasichana Afghanistan kuendelea na masomo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 17, 2025 2:42


Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”  Leah Mushi na taarifa zaidi.

The Ugandan Boy Talk Show
How Troy Elimu is Changing Uganda's Fashion, Music and Creative Industry | TUBTS Podcast

The Ugandan Boy Talk Show

Play Episode Listen Later Sep 8, 2025 58:46


In this episode of The Ugandan Boy Talk Show, we sit down with Troy Elimu — visionary creative director, entrepreneur, and the mind behind Denim Cartel & Kente Creations. From designing some of the biggest stages in Uganda's events industry to styling Africa's top artists, Troy has built a reputation as one of the most innovative voices in the African creative scene.He opens up about his journey through fashion, set & interior design, and now music, with the release of his Levitate Collection and debut EP Cartel BIZNESS. We dive deep into:The African creative scene and global presenceNavigating life as a multi-disciplinary creativeThe role of spirituality in his art and visionHis latest fashion & music projects shaping cultureIf you're passionate about African fashion, music, and creativity, this episode is packed with inspiration and insight.✨ Don't forget to subscribe for more conversations with Uganda's most inspiring voices.

Habari za UN
MINUSCA washiriki kutoa elimu ya usalama barabarani CAR

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 5, 2025 2:41


Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....​(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu kama "moto taxi" nchini CAR na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.Kwa mujibu wa MINUSCA Hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama na kujenga uhusiano mwema kati ya vikosi vya usalama na raia.​Akizungumza kuhusu umuhimu wa hatua hii, Kamanda wa Mkoa wa Plateaux(PLATIU) na Bas-Oubangui(BA OBANGI), Douflé Avi Chico( DOFLE AVII CHIKO BERNAA) Bernard, amesema,CUT- Sauti ya Douflé Avi Chico Bernard“Kwa kushirikiana na MINUSCA, kupitia brigedi yao ya magari, tunafanya kazi ya kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara, waendesha pikipiki au teksi, ili kupunguza ajali nyingi ambazo kwa bahati mbaya zinagharimu maisha ya watu. Tutaendelea na kampeni hizi kubwa ili kurekebisha hali hii.”​Kwa upande wa watumiaji wa barabara, dereva wa pikipiki za abiria, Jean Terence Bokassa (JANI TEREE BOKASA), ameomba serikali iimarishe udhibiti wa sekta hiyo.CUT- Sauti ya Jean Terence Bokassa“Tunaomba serikali ihakikishe usalama wa waendesha pikipiki za abiria kwa sababu sisi ni watu kama wengine. Tunatoka nje kutafuta riziki, lakini maisha yetu yako hatarini. Tungependa serikali itusaidie kwa kuwafundisha ndugu zetu ambao hawana leseni ya udereva kanuni za barabarani ili kuhakikisha usalama wao.”Nattss.. Sauti za magari honi nk.​Doria hii ya pamoja inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na ISF, wote wakiwa wamejitolea kulinda raia na kupunguza ajali za barabarani na MINUSCA inasema wananchi wakipata uelewa wa kutosha basio sio tu barabara zitakuwa salama bali pia idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vitapungua.

car afrika anga umoja polisi isf kila kwa bangui sauti elimu jamhuri mataifa kamanda ujumbe septemba wizara
Habari za UN
19 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 19, 2025 10:41


Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi pamoja kuhakikisha wanatoa fursa ya ufikiaji wa kibinadamu kwa watuwenye uhitaji na kunakuwepo na uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu zikijumuisha ulinzi kwa wahudumu wa kibinadamu na wa Umoja wa Mataifa”.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi ya kundi la waasi wa Allied Democratic Forces, ADF kati ya tarehe 9 na 16 Agosti, katika maeneo ya Beni na Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, yaliyoua raia 52, wakiwemo wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamehusisha utekaji nyara, uporaji, na uchomaji wa nyumba na magari, na kuwaacha wakazi ambao tayari wako katika hali ngumu ya kibinadamu katika mateso zaidi.Na katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya wahudumu wa binadamu, huduma na kujitolea kwa wanachama 270 wa Kikozi cha Polisi cha walinda amani kutoka Ghana wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), wakiwemo maafisa wanawake 63, ilitambuliwa kwa kutunukiwa Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Heshima kwa juhudi zao, zikiwa ni pamoja na kuwalinda raia, kuwezesha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kukuza haki za binadamu na kujenga amani. Bismark Achaab, Msimamizi Mkuu wa Kitengo hicho anatoa shukrani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
Mgao wa mlo wavutia wanafunzi nchini Uganda kujifunza zaidi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 8, 2025 1:54


Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Sabrina Moshi na maelezo zaidi.

Habari za UN
08 AGOSTI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 8, 2025 9:56


Jaridani leo tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza, na mradi wa mlo shuleni unaowezesha watoto kuendelea na masomo nchini Uganda. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu.Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali  umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Makala inakupeleka Mtwara, kusini mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.Na katika mashinani Patriciah Akinyi, Mwathirika wa jeraha linaloweza kuzuilika wakati wa kujifungua ambaye pia ni mnufaika wa matibabu ya upasuaji wa kurekebisha jeraha hilo la fistula nchini Kenya inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA, anasimulia kilichomkumba.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

SBS Swahili - SBS Swahili
Australia Yafafanuliwa: pengo la elimu yawa Australia wa Asili na njia ya mbele

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Jul 25, 2025 16:44


Elimu ni njia yakupata fursa ila, kwa muda mrefu wanafunzi wa Asili nchini Australia, wame kabiliana na vizuizi vya kupata mafanikio.

australia asili njia pengo yawa elimu
Habari za UN
Mradi wa UNFPA wa michezo na elimu warejesha matumaini kwa vijana wakimbizi wa DRC nchini Burundi

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 9, 2025 3:11


Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), kwa kushirikiana na serikali ya Burundi, limekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), walioko kwenye kambi ya Musenyi, mkoani Rutana huko Burundi. Kupitia michezo, tamaduni, na shughuli za elimu ya afya ya uzazi, vijana hawa wamepata matumaini mapya na fursa ya kujenga maisha yao upya. Mradi huu unaangazia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana walioko katika mazingira magumu ili kuwasaidia kufikia ndoto zao.

burundi drc umoja congo drc unfpa vijana elimu jamhuri mataifa shirika michezo kidemokrasia
Habari za UN
08 JULAI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 8, 2025 10:03


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 kumsikia Mkurugenzi wa TEN/MET Nasra Kibukila kuhusu jitihada zao za kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wanapata elimu bora, jumuishi na yenye usawa, kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa elimu ndani na nje ya nchi.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesikitishwa sana na mauaji ya jana ya watu wapatao 10, sambamba na uporaji na uharibifu wa mali wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi na katika kaunti nyingine 16.Huko Geneva, Uswisi kumeanza mkutano wa siku 4 kuhusu matumizi ya Akili Mnemba au AI kwa maslahi ya wote ambapo Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano, ITU, Doreen Bogdan-Martin ameuliza washiriki ni jambo gani wanafanya AI ihudumie ubinadamu.?Na kuelekea kumbukizi yamauaji ya Srebrenica tarehe 11 mwezi huu wa julai, Umoja wa Mataifa unakumbuka mauaji hayo yaliyofanyika wakati wa vita vilivyofuatia baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Yugoslavia. Zaidi ya watu 100,000 huko Bosnia na Herzegovina waliuawa kati ya mwaka 1992 na 1995, wengi wao wakiwa waislamu wa Bosnia. Umoja wa Mataifa unasema mauaji ya Srebrenica ni moja ya vipindi vya kiza zaidi vya vita.Na katika mashinani tunakupeleka katika miji ya mpakani ya Matar na Muon katika eneo la Gambella nchini Ethiopia ambako maelfu ya wakimbizi wamewasili kutoka Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini wakikimbia vita na njaa, na sasa wanasubiri usajili na usaidizi kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula. Nyandow Wie Deng ni mmoja akisimulia yaliyomkumba.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

ai kenya ethiopia tanzania bosnia nairobi matar yugoslavia jimbo itu herzegovina srebrenica zaidi umoja hii haki muon julai elimu mataifa serikali shirika mkurugenzi gambella sudan kusini doreen bogdan martin