POPULARITY
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, au ICT inaendelea kutawala na kuunda fursa mpya, lakini wanawake bado wanakumbana na changamoto kubwa ya upungufu wa uwakilishi. Hata hivyo, wanawake wanavuka mipaka na sasa Bi. Joy, msichana kutoka Nairobi Kenya, ambaye ni mtaalamu katika teknolojia ya kidijitali, amekalia nafasi muhimu katika kubadili mtindo wa maisha kupitia elimu ya ICT. Katika mahojiano na washirika wetu Radio Domus, alizungumzia umuhimu wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya teknolojia ili kutengeneza mustakabali mpya wa kidijitali, na kubadili dunia kwa njia ya kidigitali na usawa. Sharon Jebichii na Makala zaidi
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata ya Umoja wa Mataifa inayolenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Je, wajumbe wa Umoja wa Mataifa hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na mmjoa wao Balozi Yabesh Monari wa Kenya, lakini kwanza ni muhtasari wa habari na ufafanuzi wa maneno.Mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio jipya la Urusi dhidi Ukraine lililosababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto na mwanamke mjamzito. Bwana Schmale amesema shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya makazi jijini Kyiv na maeneo ya jirani ni ukiukaji wa kutisha wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba matumizi haya ya nguvu yasiyo na maana lazima yakome.Wiki ya Chanjo Duniani ikiwaimeanza leo, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO, na la kuhudumia Watoto, UNICEF, na Ubia wa chanjo duniani, Gavi wametoa onyo kwamba milipuko ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo inaongezeka kwa kasi. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, anasema, “Chanjo zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 150 katika kipindi cha miongo mitano iliyopita. Kupunguzwa kwa ufadhili wa afya ya kimataifa kumeweka hatarini mafanikio haya yaliyopatikana kwa juhudi kubwa.”Na ikiwa pia leo Siku ya kimataifa wasichana katika Teknolojia ya mawasiliano, ICT, Mshauri wa masoko ya kidijitali nchini Kenya Maryann Mwangi akizungumza na washirika wetu Redio Domus amehimiza wasichana kujikita kwenye ICT kwani huu ndio mustakabali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Katika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
Katika juhudi za kuimarisha ubunifu na ushindani wa kilimo biashara barani Afrika, Kenya kwa kushirikiana na Ufaransa zimeanzisha mpango wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia kwa wakulima wanawake, yakiangazia Akili Mnemba (AI) kuongeza thamani ya mazao, mpango umefikia zaidi ya vikundi na mashirika 1200 ya wanawake wakulima na kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kuongeza ubora, usindikaji na masoko.
Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
Msikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za kuhamishia wakimbizi eneo salama zaidi.Mashinani anasalia nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni yanavyowawezesha wanawake na wasichana kujimudu kimaisha. Karibu
Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Baadhi ya wasichana wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya ni wanufaika wa mpango huu. Sharon Jebiichi na maelezo zaidi.Zamzam Hussein,aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera. Ni mkimbizi mwenye asili ya Somalia na sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya akiwa na ndoto ya kuwa daktari. Kupitia mpango huu ambao ni sehemu ya programu ya PROSPECTS ambao ni ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao Zamzam Hussein ameweza kukumbatia sayansi.“Nilikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera na nikamaliza elimu yangu mwaka wa 2024. Nilijiunga na shule hiyo Agosti 2021. Nilichopenda zaidi nikiwa shuleni ni maktaba, maabara ya sayansi na maabara ya kompyuta. Napenda kuwashauri wasichana wadogo wanaosoma shuleni na walio wakimbizi wafanye kazi kwa bidii bila kujali changamoto wanazokabiliana nazo. Watatimiza ndoto zao na waweze kufanikiwa katika siku za usoni. Nataka kuwa daktari kwa sababu nilipokuwa shule ya upili nilijifunza mambo mengi kuhusiana na matibabu. Ningependa kuwashukuru wafadhili wetu kwa sababu bila wao nisingekuwa hapa.”Mpango huu wa STEM umetoa msaada wa rasilimali kama vile kuajiri walimu zaidi wa sayansi, kutoa mafunzo kwa walimu, kutoa vifaa vya sayansi kwa ajili ya maabara ya shule na kuanzisha programu ya maabara ya mtandaoni (virtual lab) ambapo wanafunzi wanaweza kufanya majaribio ya sayansi kwenye mtandao wa intaneti. Kupitia video iliyorekodiwa na UNICEF, Patrick Njogu, Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Hagadera anasema,“Nimemfundisha Zamzam na wasichana wengine ili waweze kutimiza ndoto na malengo yao. Wasichana wamekuwa wakikabiliana na changamoto kama vile ndoa za mapema. UNICEF imekuwa ya manufaa zaidi kwao. Kwa sasa walimu wawili zaidi wa sayansi wameajiriwa. Mbali na hayo imekuwa ikiendesha mafunzo ya walimu, imetoa vifaa vya sayansi kwa ajili ya maabara ya shule na kuanzisha programu ya maabara ya mtandaoni (virtual lab). Programu hii ya mtandao (virtual lab) imetengeneza uhusiano nzuri wa wanafunzi katika masomo ya sayansi.”
Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana mwenye umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Ikiwa Umoja wa Mataifa unaunga mkono masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hisabati, au STEM, Angela Tabiri ni mwanahisabati bora duniani, Mtafiti na Mhadhiri kutoka Chuo cha African Institute for Mathematical Sciences (AIMS) kilichoko Accra nchini Ghana Magharibi mwa bara la Afrika, amekuwa akitoa mchango katika kuhakikisha wasichana nchini humo wanapata elimu ya hisabati kupitia taasisi yake ya FemAfricMaths. Kwa kufanya hivyo anatimiza lengo namba 4 ya Malengo endelevu ya Umoja Mataifa(SDGs) linalohimiza elimu bora kwa wote na lile namba 5 linalozungumzia usawa wa kijinsia. Kutoka mjini Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania, Sabrina Moshi wa redio washirika Saut Fm amefanya mahojiano na mtaalamu huyo. Angela anaanza kwa kueleza namna alivyokuwa na ndoto hadi kuanzisha FemAfricMaths ili kuwasaidia wasichana barani Afrika.
Teknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
Teknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
Tutaangazia historia ya muziki wa Afrika, tukiangalia mabadiliko makubwa yaliyotokea kabla na baada ya kuibuka kwa teknolojia. Muziki wa Afrika ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu, na umetumika kwa karne nyingi kama njia ya kuwasiliana, kusherehekea, na kuponya.
VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani. Tunasherehekea miaka 150 ya shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU, tunatambua umuhimu wa moja ya mifano ya mapema zaidi ya ushirikiano wa kimataifa. Ni Masahiko Metoki, Mkurugenzi Mkuu wa UPU katika ujumbe wake wa siku hii adhimu akiongeza kuwa..“Kile kilichoanza na wanachama 22 sasa inajumuisha nchi 192, kikionesha uthabiti wa ushirikiano wa kimataifa.”Miaka 150 wamekumbana na changamoto, vita, majanga mabadiliko ya kasi ya teknolojia ya kidijitali. Lakini wanafanya nini?“Leo hii UPU inaongoza juhudi za kufanya huduma za posta kuwa za kisasa na bora. Inatoa fursa kwa nchi kushirikishana ufahamu, kusaka majawabu na kukabili changamoto za sasa. Moyo wetu wa ushirikiano ndio umetusaidia kugeuza vikwazo kuwa fursa na kufanya huduma za posta kuendana na dunia inayobadilika.”Na zaidi ya yote…“Awali tuliona ongezeko la mawasiliano ya kidijitali kuwa ni tishio kwani kiwango cha utumaji wa barua kwa njia ya posta kilipungua. Lakini sasa tunaona fursa za utajiri. Mtandao mkubwa wa UPU umesaidia kupanuka kwa huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao, huduma za kifedha, kijamii na kidijitali, ikihakikisha ufikiaji wa kila mtu duniani hata wale walio ndani zaidi hawaachwi nyuma.”Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, UPU imehimili changamoto kwa kuwa bunifu, jumuishi na kusongesha ushirikiano wa kimataifa.“Katika siku hii muhimu, hebu na tusherehekee na tupongeze kazi ya shirika la Posta duniani ya kuondoa umbali na kuunganisha dunia.”
Tiba Salama Digital Health App shirika la kijamii la lilalolenga kutumia teknolojia kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, wanaolea na watoto.Lengo kuu ni kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa vifo vya wajawazito na watoto wadogo kwa kuoresha huduma za afya hususani kwa maeneo ya pembezoni yenye upatikanaji hafifu wa huduma za msingi za afya.Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza Simon Mashauri, Mkurugenzi na Mwazilishi wa shirika hilo lenye makao yake makuu mkoani Tanga, kaskazini mashariki mwa Tanzania.
Katika dunia ya sasa ambapo ukuaji wa teknolojia ni wa kasi ya juu, wabunifu katika jamii za pwani nchini Kenya, wamekumbatia matumizi ya teknolojia katika kupiga jeki juhudi za kupunguza taka kwenye mazingira wanayoishi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Nairobi Kenya ambako tutamsikiamwanamuziki nyota, mjasiriamali na mwanaharakati wa haki za wanawake Lizi Ogumbo. Pia tunakuletea habari kwa ufufpi na mashinani.Vurugu dhidi ya wapinzani wa serikali nchini Venezuela zimefurutu ada, imesema tume huru ya uchunguzi ikitaja kukamatwa, ukatili wa kingono na utesaji kama mbinu zitumiwazo na serikali ya Rais Nicolas Maduro ili aendelee kuweko madarani.Mwaka 2024 ukiripotiwa kuwa na idadi kubwa ya chaguzi kwenye nchi zaidi ya 60 ambako zaidi ya watu bilioni 1 watapiga kura kuchagua viongozi wao wa umma, wataalamu wa Umoja wa Mataia wanaelezea hofu yao juu ya kitendo cha watu kutoweshwa katika kipindi hicho ili kunyamazisha demokrasia, kitendo ambacho wamesema kinabinya uhuru wa kupiga kura.Na hii leo matokeo ya utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa yameonesha kuwa licha ya majanga yanayoendelea kukumba dunia, nchi wanachama zimeendelea kujizatiti kuanzisha huduma za serikali mtandao ili wananchi waweze kupata huduma mbali mbali kidijitali, ambapo ripoti inazitaja Denmark, Estonia na Singapore kushika nafasi ya juu kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, kwa mawanda na ubora wa huduma za serikali mtandaoni.Katika mashinani Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini Bangladesh Stefan Liller anatueleza kiwango cha athari za mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Huko Paris, Ufaransa kumekamilika mkutano wa wiki moja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ukipatiwa jina Wiki ya Kujifunza Masuala ya Kidijitali au Digital Learning Week ambapo hoja ya Akili Mnemba kudhibiti habari potofu na za uongo imepatiwa kipaumbele.Mkutano huo ulimulika mchango wa teknolojia ya kidijitali katika elimu inayolenga maendeleo badala ya kuyadumaza. Mathalani ni kwa jinsi gani mifumo ya kidijitali inaweza kukabiliana na taarifa potofu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Simon Wanda, Afisa Programu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni amefafanua nafasi ya teknolojia kwenye kukabili taarifa hizo.“Mifumo hii inaweza kuchambua na kutathmini yale yanayowekwa kwenye matandao na kutambua taarifa za uongo au za kupotosha.”Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Doris Mwikali, Mwanasheria na mtetezi wa elimu kutoka Kenya. Tukamuuliza maoni yake kuhusu nafasi ya teknolojia za kidijitali kwa vijana."Ninafahamu kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi kampuni za mitandao ya kijamii zinavyopambana na habari potofu na za uongo. Lakini nadhani kuna zana mpya za akili mnemba zinazotumika na baadhi ya kampuni, kuhakiki taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa haitakuwa na mchango mkubwa ikilinganishwa na kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua jukumu la kudhibiti habari potofu kwenye majukwaa yao, Bado kuna jukumu kubwa kwa akili mnemba katika uhakiki wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, na hiyo imefanywa na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali."Nikarejea kwa Bwana Wanda na kumuuliza maoni yake kuhusu maendeleo ya akili mnemba au AI na ujumuishaji wa sauti kutoka pande zote wakati wa kusongesha AI.“Zipo jamii nyingi zetu za kiafrika kama wamaasai wa Kenya na Tanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na elimu ya asili kuhusu kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni elimu inayofaa kutopuuzwa katika makuzi haya ya teknolojia. Hivyo, hili ni suala la kuhoji sana hasa tunapozingatia kwamba maendeleo katika teknolojia yasiegemee eneo moja la elimu tu, ambayo ni elimu ya magharibi, na kupuuza elimu ya kiasili, ambayo ni tunu.”
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa vipi wataalamu wa kemia wanahusiana na ujasiriamali? Kama ndivyo, basi vivyo hivyo kwa Assumpta Massoi akiwa Manama, nchini Bahrain akishiriki Jukwaa la Nne la Uwekezaji kwa Wajasiriamali, WEIF2024 lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO, Ofisi ya Uendelezaji wa Biashara, ITPO nchini humo, alikutana na Profesa Ruth Wanjau, Mtafiti na Mshauri wa Masuala ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Alimuuliza maswali kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye jukwaa hilo na nini anafanya kusongesha ujasiriamali.
Msikilizaji kwa mujibu wa Jukwaa la dunia la uchumi, World Economic Forum, ujio wa teknolojia mpya kama akili mnemba (Artuificial inteligency), ikiwa zitatumika vizuri, zitasaidia kujenga uchumi wenye ushindani, unaostahimili changamoto na endelevu.Katika makala ya gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili Kuibuka au ugunduzi wa teknolojia na ushawishi wake katika kukuza uchumi.
Msikilizaji kwa mujibu wa Jukwaa la dunia la uchumi, World Economic Forum, ujio wa teknolojia mpya kama akili mnemba (Artuificial inteligency), ikiwa zitatumika vizuri, zitasaidia kujenga uchumi wenye ushindani, unaostahimili changamoto na endelevu.Katika makala ya gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili Kuibuka au ugunduzi wa teknolojia na ushawishi wake katika kukuza uchumi.
VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake.
Kipindi hiki kitakusaidia kujifunza tafrisi ya misamiati ya kitechnologia. Karibu sana na natumai utanufaika.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametimiza ahadi yake ya kuunda Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi wakati huu ambapo teknolojia ya Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence' imeshaanza kugonganisha vichwa vya watu kuhusu nafasi yake katika maendeleo duniani. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Guterres Bodi hii mpya aliyoiunda ni kwa ajili ya kuwashauri viongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mafanikio katika sayansi na teknolojia na jinsi ya kutumia manufaa ya maendeleo haya na kupunguza hatari zinazoweza kutokea. Bwana Guterres anaamini maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yanaweza kuunga mkono juhudi za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu lakini pia yanaleta wasiwasi wa kimaadili, kisheria na kisiasa, wasiwasi ambao unahitaji ufumbuzi wa kimataifa. Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi ambayo Bwana Guterres anaamini pia kuwa itaimarisha jukumu la Umoja wa Mataifa kama chanzo cha kuaminika cha data na ushahidi wa kisayansi itajumuisha kundi la Maprofesa wanasayansi saba mashuhuri duniani. Maprofesa hao ni Profesa Yoshua Bengio, Profesa Sandra Díaz, Profesa Saleemul Huq, Profesa Fei-Fei Li, Profesa Alan Lightman, Profesa Thuli Madonsela, na Profesa Thomas C. Südhof. Pia kundi jingine ni Wanasayansi Wakuu wa mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, na Mjumbe wa Katibu Mkuu kuhusu Teknolojia. Mmoja wa wanaounda Bodi hiyo, Profesa Yoshua Bengio, Mkurugenzi wa Kisayansi wa Taasisi ya Mila - Quebec AI ambaye pia ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Montréal anatoa ahadi akisema, “Uamuzi wa Katibu Mkuu wa kuanzisha Bodi ya Ushauri wa Kisayansi unasisitiza kujitolea bila kuyumba kwa viongozi wa Umoja wa Mataifa kwa kanuni za mbinu za kisayansi. Ninatazamia kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupaza sauti kwa ajili ya sera zinazotegemea sayansi na kufanya uamuzi.” Kupitia juhudi zao za ushirikiano, Bodi na Mtandao wake utawaunga mkono viongozi wa Umoja wa Mataifa katika kutazamia, kuzoea, na kutumia maendeleo ya hivi karibuni ya kisayansi katika kazi yao kwa watu, sayari na ustawi. Bodi itafanya kazi kama kitovu cha mtandao wa mitandao ya kisayansi. Lengo ni kuwa na muunganiko bora kati ya jumuiya ya kisayansi na kufanya uamuzi katika Umoja wa Mataifa. Kwa upande wake Bi. Ismahane Elouafi, Mwanasayansi Mkuu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo anasema, "Kwa kuhakikisha kwamba sera na programu za Umoja wa Mataifa zimeanzishwa kwa msingi wa ushahidi na utaalamu bora wa kisayansi uliopo, Bodi itachukua jukumu muhimu katika kutatua matatizo changamano ya kimaadili, kijamii na kisiasa yanayowasilishwa na maendeleo ya haraka ya kisayansi na kiteknolojia." Ikumbukwe mwezi Julai mwaka huu, kwa mara ya kwanza Baraza la Usalama lilikuwa na mjadala mahususi kuhusu Akili Mnemba na mstakabali wake katika amani na usalama duniani na kabla yake, Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia moja ya matamko yake ya kisera ya Ajenda Yetu ya Pamoja, alitoa ahadi ambayo imetimia kwa kuunda Bodi hii ya kumshauri katika masuala ya kisayansi.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNESCO kuhusu teknolojia na pia afya ya wanawake wajawazito nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Australia na mashinani Roma nchini Italia, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu ufuatiliaji wa teknolojia katika elimu GEM 2023 imetaka mifumo ya elimu kote duniani siku zote kuhakikisha kwamba matakwa ya wanaojifunza yanakuwa katika kitovu cha teknolojia na kwamba teknolojia zitumike kusaidia elimu inayotokana na mwingiliano wa binadamu badala ya kulenga kuwa mbadala wake.Vita nchini Sudan ambayo sasa imedumu kwa zaidi ya siku 100 imeshuhudia zaidi ya watu milioni 3 wakiyakimbaia makazi yao kwenda kusaka hifadhi katika miji mingine pamoja na nchi Jirani.Makala tunaangazia Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ambao wako ukimbizini Australia baada ya kuukimbia utawala wa Taliban nchini mwao Afghanistan.Na katika mashinani ikiwa mkutano wa viongozi kuhusu mifumo ya upatikanaji wa chakula unakunja jamvi leo huko Roma nchini Italia tutasikia ujumbe unaotaka jumuiya ya kimataifa kubuni njia mpya za kukabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu ufuatiliaji wa teknolojia katika elimu GEM 2023 imetaka mifumo ya elimu kote duniani siku zote kuhakikisha kwamba matakwa ya wanaojifunza yanakuwa katika kitovu cha teknolojia na kwamba teknolojia zitumike kusaidia elimu inayotokana na mwingiliano wa binadamu badala ya kulenga kuwa mbadala wake. Ripoti hiyo mwaka 2023 ya GEM inashughulikia matumizi ya teknolojia katika elimu duniani kote kupitia muktadha wa umuhimu, usawa, uthabiti na uendelevu.UNESCO inasema teknolojia inabadilika haraka kuliko inavyowezekana kutathminiwa na bidhaa za teknolojia ya elimu hubadilika kila baada ya miezi 36, kwa wastani huku ushahidi mkubwa ukitoka katika nchi tajiri zaidi.Mathalani ripoti inasema “Nchini Uingereza, asilimia 7 ya makampuni ya teknolojia ya elimu yalikuwa yamefanya majaribio yaliyodhibitiwa bila mpangilio, na asilimia 12 yalikuwa yametumia uthibitishaji wa watu wengine. Pia utafiti uliofanywa kwa walimu na wasimamizi katika majimbo 17 ya Marekani ulmeonyesha kuwa ni asilimia 11 tu waliomba tathimini ya ushahidi kabla ya kupitishwa.Katika miaka 20 iliyopita, wanafunzi, waelimishaji na taasisi wamepitisha na kukumbatia kwa kiasi kikubwa zana za teknolojia ya kidijitali.Audrey Azoulay, mkurugenzi mkuu wa UNESCO anaonya kwamba "Mapinduzi ya kidijitali yana uwezo usiopimika lakini, kama vile onyo ambavyo limekuwa likitolewa kuhusu jinsi yanavyopaswa kudhibitiwa katika jamii, tahadhari sawa lazima izingatiwe jinsi mapinduzi hayo yanavyotumiwa katika elimu. Matumizi yake lazima yawe kwa ajili ya uzoefu ulioimarishwa wa kujifunza na kwa ajili ya ustawi wa wanafunzi na walimu, si kwa madhara kwao. Matakwa ya mwanafunzi yawe kipaumbele cha kwanza na yawasaidie walimu. Kuunganishwa mtandaoni sio mbadala wa mwingiliano wa wanadamu.”Azoulay amesisitiza kuwa “Kutumia teknolojia kunaweza kuboresha baadhi ya aina za kujifunza katika baadhi ya miktadha. Ripoti hiyo inataja ushahidi unaoonyesha kuwa manufaa ya kujifunza hutoweka ikiwa teknolojia itatumiwa kupita kiasi au kutokuwepo kwa mwalimu aliyehitimu. Kwa mfano, kusambaza kompyuta kwa wanafunzi hakuboreshi hali ya kujifunza ikiwa walimu hawatahusika katika tajriba ya ufundishaji. Simu za rununu shuleni pia zimeonekana kuwa kero katika kujifunza, lakini ni chini ya robo ya nchi tu ndizo zimepiga marufuku matumizi ya simu hizo shuleni.”Duniani kote ripoti imesema idadi ya watu wanaotumia mtandao wa intaneti imeongezeka kutoka asilimia 16 mwaka 2005 hadi asilimia 66 mwaka 2022.
Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote.Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema lengo lake ni kuwaenzi wanawake na wanaume kote duniani ambao huwajibika kwa jukumu muhimu zaidi la kutoa huduma kwa umaa.Amesema maadhimisho ya siku ya mwaka huu yanakuja wakati Dunia iko katikati ya kuelekea ukomo wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na hivyo amesisitiza kuwa “ Watumishi wa umma na taasisi wanazoziunga mkono zitakuwa muhimu zaidi huku ulimwengu ukiharakisha hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo yako yanakwenda kombo.”Ameichagiza dunia kwamba ili kutimiza malengo hayo “ Teknolojia lazima iwe kiini cha kuongeza kasi hii ya utekelezaji. Kila siku, teknolojia mpya zinaibuka ambazo zinashikilia uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Inapotumiwa na utumishi wa umma wenye ujuzi, uliowezeshwa na wenye vifaa, teknolojia inaweza kuboresha ufikiaji na ufanisi wa huduma za umma, huku ikisukuma maendeleo kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.”Amehitimisha ujumbe wake kwa wito kwamba “Wakati tukiadimisha siku hii muhimu hebu tusherehekee sio tu kazi ya utumishi wa umma kote duniani lakini tutafute njia mpya za kutumia ubunifu katika kazi zetu na kuenzi uwajibikaji wa watumishi hao wa kufanyakazi kwa ushirikiano ili kujenga mustakbali bora kwa watu wote.”
Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Utumaji fedha kwa familia ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia manufaa ambayo ujumuishaji wa kidijitali na kifedha unapohusishwa na utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, huzisaidia familia zinazopokea fedha kufikia Malengo yao ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD, asilimia 14 ya idadi ya watu duniani, au watu bilioni 1, hutuma au kupokea fedha. Hiyo ni sawa na wafanyakazi wahamiaji milioni 200 wanaotuma fedha kwa wanafamilia milioni 800 kote duniani. David Casian ni mwanadiaspora wa Tanzania anayeishi kwa miaka mingi nchini Marekani anaeleza namna matumizi ya dijitali yamesaidia sana katika utumaji fedha nyumbani, “Teknolojia ya kidijitali kitu cha kwanza walichofanya ni kuondoa mambo ya katikati mengi ambayo yalikuwa yanatuzuia na imeleta ufanisi. Katika muda mdogo tu unaweza ukatuma pes ana mpokeaji akapokea kule nyumbani na kama kuna tatizo la haraka likatatuliwa. Kwa hiyo hivi ni vitu vya muhimu sana tunapenda dijitali kwa sababu kweli imeleta mapinduzi makubwa na tumeweza kufanya mambo mengi kwa wakati mchache.” Aidha Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaeleza kuwa mwaka jana 2022, utumaji fedha kimataifa kwa mataifa ya kipato cha chini na cha kati ulifikia dola bilioni 626. Wastani wa kila mwezi wa dola za Marekani 200 hadi 300 zinazotumwa na wafanyakazi wahamiaji husaidia familia nyingi duniani kote na mwanadiaspora huyu David Casian ni shuhuda wa hilo, “Pesa tunazotuma nyumbani zinasaidia wanafamili kwa upande wa mmoja mmoja lakini pia zinasaidia jamii nzima ya watu wetu. Mtu anaweza akawa anaumwa ukatuma pesa akaweza kutibiwa. Ukatuma pesa mtoto amerudishwa kwa ada shuleni unatuma. Unatuma pesa kwa ajili ya mambo ya uchumi labda mtu anahitaji hela kwa ajili ya kufungua kabiashara kidogo ili aweze kujikimu na hii inasaidia kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na vile vile kwa taifa kuijumla. Kwa hiyo ni kitu kizuri na ni kitu cha kukiendeleza na kushukuru kwamba dijitali kwakweli imeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya utumaji pesa.”
Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.Kutoka jijini Mwanza kaskazini-magharibi mwa Tanzania, Evarist Mapesa alikutana na Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Sayansi wa Maji na Mazingira yake na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bahati Mayoma, akitaka kufahamu athari za taka za plastiki kwa viumbe hai waishio kwenye maji na hapa mhadhiri huyo anaeleza.
Ni Alhamisi ya tarehe 30 ya mwezi Machi mwaka 2023, mwezi Machi siku ya kimataifa ya kutotupa taka na ni siku ya mada kwa kina ambayo leo inatupeka Kenya kumulika jitihada za shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO za kumuinua mwanamke mkulima kwa kutumia ubunifu na teknolojia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na katika kipengele cha Jifunze Kiswahili tutamsikia Profesa Aldin Mutembei, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere.Ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya kutozalisha na kutupa taka kiholela, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika wa kuacha kugeuza sayari dunia dampo na badala yake kila mtu azingatie matumizi ya ten ana tena ya bidhaa kadri inavyowezekana. Guterres amesema huu ni wakati wa kuamka na kusongesha harakati za kiuchumi zisizozalisha taka na wakati huo huo wateja na walaji wajenge tabia ya kutumia bidhaa tena na tena kabla ya kuitupa ili kupunguza kiwango cha taka kinachozalishwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema halina budi kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi nchini Burundi kwa sababu ya ukata unaolikabili.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tunakuletea ripoti kutoka kwa mwandishi wetu George Musubao kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO.Katika katika kipengele cha Jifunze Kiswahili tutamsikia Profesa Aldin Mutembei, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukifikia tamati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huku moja ya mikakati ni kuhakikisha kunakuweko matumizi endelevu ya maji, mmoja wa washiriki kutoka Rwanda amezungumzia vile ambavyo teknolojia ya kusafisha maji taka ili yaweze kutumika tena na tena inaweza kuwa mkombozi kwenye eneo lao. Mshiriki huyo Andrew Mpuhwe Rucyahana ambaye ni Naibu Meya wa wilaya ya Musanze katika jimbo la Kaskazini nchini Rwanda amesema hayo akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Bwana Rucyahana anasema kule Musanze anakotoka ni eneo lenye shughuli nyingi za kitalii na likipokea wageni wengi wanaofika hivyo ni lazima kuwe na kiasi kikubwa cha maji tena maji safi. “Ushiriki wangu kwenye huu mkutano utaniwezesha kukutana na watu wengine na kufahamu ni vipi tunaweza kufanikisha wilaya ya Musanze iwe na maji safi na salama hasa kwa kuzingatia eneo letu liko milimani na tunapokea watalii wengi,” amesema Naibu Meya huyu wa Musanze. Hapa kwenye mkutano tunaweza kubadilishana mawazo ni vipi watu wanajenga miundombinu ya maji. Tuna maji mengi lakini hayatoshi, tungali na kazi kubwa ya kufanya ili tufikishe maji safi kwa watu wote, anasema Bwana Rucyahana akitaja changamoto ni uhaba wa fedha za kuwezesha kujenga miundombinu ya kufikisha maji milimani. “Tunahitaij kupata maji yaliyo safi. Mfano tupate teknolojia ya kupeleka maji milimani ambako kuna hoteli zinazopokea wageni wengi. Tuna malengo ya kufikisha maji kwa wakazi wote wa wilaya ya Musanze ifikapo mwaka 2024.” Hoja ya kutumia maji tena na tena ilitajwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi, ambaye alisema teknolojia hiyo ni moja ya mambo muhimu ya kuepusha kupoteza maji. “Tunatakiwa kukomesha haraka upotevu wa maji. Kuwa na mzungumko wa matumizi ya maji, yaani kuyatumia tena na tena badala ya kuchimba mengine, huo ndio unapaswa kuwa mwelekeo,” Naibu Meya huyu wa Musanze anasema katika eneo lao watu wanatumia maji mara moja tu “unaona maji mengi yanaharibika. Lakini tayari kuna teknolojia ya kusafisha maji ili yatumike tena na tena mara mbili au tatu. Teknolojia hii ni gharama kubwa Afrika. Kwa Musanze teknolojia hiyo inatumika kwenye hotel za gharama ya juu . Lakini si katika hoteli za bei ya gharama ya chini au kwenye makazi ya watu wenye uwezo mdogo ambao ni wengi.” Ni kwa mantiki hiyo anaamini kuwa kupitia mkutano wa maji anaweza kupata watu wenye teknolojia wanaweza kuipeleka na kuiuza huko Musanze. Lakini juu ya yote wito wake ni kwa watu kutambua kuwa maji ni maisha yetu, kukosa maji ni kukosa maisha. Watu wote tusaidiane ili tuwe na maji safi na mengi barani Afrika.
Kikao cha 67 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW67 kielekea tamati, mwaka huu 2023 kikiwa kimebeba mada uvumbuzi, mabadiliko ya kiteknolojia, na elimu katika zama hizi za kidigitali kwa ajili ya kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote. Mijadala mingi katika mkutano huu imelenga kuwawezesha na kuhakikisha watoto wa kike wanaingia kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati au STEM ili hapo baadaye waweze kuchangia katika ubunifu wa teknolojia katika enzi hizi za dunia ya kidijitali. Kwa muktadha huo, kamisheni hali ya wanawake wakishirikiana na serikali za nchi mbalimbali na mashirika yasio ya kiserikali iliwaalika na kuwajuimisha watoto wa kike katika kikao hicho ili waweze kuwakilisha wanafunzi wenzao, na mmoja wa wanafunzi hao kutoka Tanzania amepata fursa ya kuzungumza na Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa katika mahojiano kandoni mwa mkutano huo na kumuelezea matarajio yake katika ulimwengu huu wa kidijitali ni yapi, na ana ujumbe gani kwa wasichana wenzake lakini anaanza kwa kujitambulisha..
Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 ukiendelea na maudhui makuu yakiwa ni namna ugunduzi na teknolojia ya dijitali inaweza kuchangia kumkwamua mwanamke, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nayo inaendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu kule watokako hali iko namna gani na nini kinafanyika ili kuhakikisha teknolojia ya kidijitali inatumika kivitendo badala ya kusalia kwenye makabrasha au kumilikiwa na wachache na hivyo kuzidi kuongeza pengo la kidijitali. Miongoni mwa washirii ambao Idhaa hii imezungumza nao ni Neema Lugangira, mbunge wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, nchini Tanzania akiwakilisha mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika mahojiano yake na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Bi. Lugangira amezungumzia ni kwa kiwango gani teknolojia ya kidijitali inatumika Bungeni na zaidi ya yote mikakati yake ya kuona intaneti inafikia wengi walio pembezeno. Lakini kwanza anamulika matumizi ya teknolojia kwa ujumla wake nchini Tanzania.
Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja wawakilishi kutoka serikali, mashirika ya kiraia yanayotambuliwa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC pamoja na vijana.Mwenyekiti wa mkutano huo Balozi Mathu Joyini ambaye ni Mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa washiriki ni wanawake kutoka kona mbali mbali za dunia pamoja na vijana na zaidi ya yote na maudhui ni mabadiliko ya ugunduzi na teknolojia na nafasi yake katika zama hizi za kidijitali ili kufanikisha usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake na maudhui amesema yamekuja wakati muafaka.. "Teknolojia za kidijitali zinaleta fursa za kipekee katika kuwezesha wanawake na wasichana. Lakini vilevile zinaleta changamoto mpya kubwa kwa haki za wanawake na wasichana. Teknolojia inaenda kwa kasi lakini mfumo wa maadili duniani bado haujarekebishwa." Hivyo amesema, "Tunatumaini kuwa na hitimisho la kijasiri ambalo linaweka maadili na viwango vya kusongesha mbele ili kuhakikisha wanawake wanawakilishwa kwenye nyanja ya teknolojia. Elimu pia ambayo inawaruhusu kushiriki katika ubunifu na mifumo anuai iliyoko, na kwamba wanawake na wasichana wanapatiwa fursa ya kubuni, kuendeleza na kutumia teknolojia." Mkutano huo ulioanza leo tarehe 6 Machi utamalizika tarehe 17 mwezi huu wa Machi ambapo pia wajumbe watatathmini changamoto na fursa za kufikia usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wa vijijini, maudhui yatokanayo na mkutano wa 62 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW62.
Miaka miwili iliyopita, wakulima nchini Peru walikuwa na hofu ya kwamba janga la COVID-19 lingalifuta kabisa masoko yao waliyozoea kuuza mazao kama vile kakao na malimao. Walizoea kuuza sokoni lakini COVID-19 ilifuta masoko hayo kutokana na vizuizi vya kutembea.Hata hivyo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD kupitia mradi wa kuchechemua kilimo vijijini baada ya COVID-19 ulileta nuru na sasa wakulima hawaamini kile wakipatacho. Ni kwa vipi basi? Ungana na Assumpta kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD.
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana katika sayansi, na msaada wa binadamu mashariki ya kati kwa waathirika wa tetemeko la ardhi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Misri, kulikoni? Uwepo wa idadi kubwa ya wanawake na wasichana katika sekta ya sayansi ni faida kuwa kwa sekta ya sayansi na jamii kwa ujumla amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza kuchagiza wanawake na wasicha kuingia zaidi katika sekta hiyo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupeleka na kusambaza misaada nchini Uturuki au Türkiye na Syria ili kusaidia walioathiriwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea Jumatatu wiki hii na kujeruhi, kuua maelfu na kuharibu miundombinu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lina lengo la kuwafikia watu nusu milioni katika nchi zote mbili ijapokuwa kuna changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo.Makala tunakupeleka mkoa wa Njombe, kusini mwa Tanzania ambako huko leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya mikunde duniani, ngazi ya kitaifa na John Kibambala wa redio washirika KIDS Time FM amezungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Itipingi katika halmashauri ya wilaya ya Njombe, ambao ni wanufaika wa mradi wa kilimo cha bustani na mlo shuleni unaopatia kipaumbele kilimo na mlo wa mazao aina ya mikunde, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo.Na katika mashinani nampisha Dkt. Menatallah Elserafy kutoka Misri, ambaye ni Profesa msaidizi na mtafiti wa kuzingatia taratibu za ukarabati wa vinasaba au DNA katika Kituo cha Genomics cha Jiji la Sayansi na Teknolojia la Zuwail nchini humo. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakwenda mashariki ya kati na nchini Ukraine. Makala tutaelekea nchini Tanzania na mashinani tutasikia ujembe wa mchehemuzi wa vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na pia mwanasayansi.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa muda wa Misaada ya Kibinadamu nchini Syria El- Mostafa Benlamlih amesema ingawa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada wanafanya kila juhudi kusaidia wananchi walioathiriwa na matetemeko ya ardhi lakini hali ni mbaya kwani hawapati msaada ya kutosha.Mwishoni mwa mwezi huu wa Februari tarehe 24, utatimia mwaka mmoja tangu uvamizi wa sasa wa Urusi kwa Ukraine. Nchini Ukraine, moja ya sekta zilizoathiriwa sana na vita hii ni kilimo Anold Kayanda anamwangazia mkulima mmoja katika mkoa wa Odesa kusini magharibi mwa nchi. Makala tunakwenda mkoani Njombe nchini Tanzania kutathmini harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO za kuchagiza kilimo cha bustani kikijumuisha kilimo cha mikunde kama njia mojawapo ya kuimarisha afya na ustawi wa jamii.Na katika mashinani Gitanjali Rao, Mchehemuzi wa vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na pia mwanasayansi anatoa maoni yake kuhusu nini kifanyike ili kuwapa wasichana na wanawake fursa nyingi za masomo na kazi katika sekta ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, au STEM.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema wataendelea kujifunza kutoka nchi ambazo zimeanza kutumia teknoljia hiyo ya GMO kwa sababu serikali ya Tanzania haiwezi kuingia kwenye mjadala wa kutumia au kutokutumia teknolojia hiyo bila kufahamu undani wake
Je ni kwa vipi teknolojia ya nyuklia inaweza kuleta tofauti katika uzalishaji wa chakula wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kugonga vichwa vya watu na kubisha hodi kila uchao? Baadhi ya watu wakisikia nyuklia kinachowajia kichwani ni mabomu ya nyuklia, lakini nchini Kenya, wanasayansi na wakulima wanaelezea kwa maneno yao wenyewe vile ambavyo sayansi ya nyuklia inasaidia kupambana na uhaba wa chakula na maji. Kuanzia uzalishaji wa mbegu mpya zinazohimili ukame hadi teknolojia za kutambua ni muda gani muafaka kumwagilia mazao. Utaalamu huu unafanyika kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya nyuklia, IAEA. Ungana basi na Leah Mushi kwenye Makala hii iliyoandaliwa na IAEA.
Hii leo katika Habari za UN tunamulika haki za binadamu hasa za watu wenye ukoma, kisha teknolojia, wakimbizi na wahamiaji Rwanda na amani na usalama. kwa kina!Watu wenye ukoma na familia zao wamesubiri muda mrefu sana ili haki zao za kuwa na ulemavu ziweze kutambuliwa kitaifa na kimataifa, amesema mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo kwa ripoti yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Janga la COVID 19 lilipotangazwa mwaka 2019 lilizua taharuki kila kona ya dunia lakini changamoto zilizoletwa na janga hilo zilikuwa fursa kwa vijana nchini Zimbabwe ambao walikuja na wazo la shule mtandaoni na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP likawapatia fedha ili watekeleze wazo na kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.Makala inatupeleka katika eneo la Nyarugenge mjini Kigali Rwanda ambako katika pitapita yake Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya mafundi cherahani wahamiaji kutoka Jamhuri ya Kimekrasia ya Congo DRC walioingia Rwanda kusaka mustakbali bora ikiwemo amani na usalama na kujitafutia riziki kwa sababu ya changamoto za usalama zinazoendelea nchini mwao.Mashinani tutasikia ujumbe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ushiriki wa wanawake na vijana katika ujenzi wa amani na kuleta maendeleo.Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi
Kesho kutwa Ijumaa huko nchini India, Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itakutana nchini India kutathmini vitisho vipya duniani vitokanavyo na teknolojia mpya. Mkutano huo wa siku mbili ni wa kwanza kufanyika nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tangu mwaka 2015. Happiness Pallangyo wa Redio washirika Uhai FM kutoka Tabora Tanzania anafafanua zaidi.Mjadala utajikita kwenye maeneo matatu makuu ambayo ni mosi; Intaneti na mitandao ya kijamii; Pili, Ufadhili wa mitandao ya kigaidi duniani na tatu; kuenea kwa matumizi ya mifumo ya angani isiyo na rubani kama vile droni.Umoja wa Mataifa unasema teknolojia hizo mpya zinakua kwa kasi kubwa na zinatumika mara kwa mara katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo kwenye usalama wa taifa na kukabili ugaidi.Hata hivyo teknolojia hizo zinatumiwa vibaya na vikundi vya kigaidi kwa manufaa yao binafsi yasio na nia njema.Mkutano pia utakuwa ni jukwaa la kubadilishana mawazo ya jinsi teknolojia inaweza kusaidia kukabili kusambaa kwa maudhui ya kigaidi mtandaoni na kukabili pia simulizi za kigaidi.Hofu nyingine iliyoko na itakayomulikwa ni matumizi kwa nia mbaya ya uchapishaji wa chapa tatu au 3D, maroboti, akili bandia na mifumo ya angani isiyo na usimamizi.Kwa sasa India ndio inashikilia kiti cha Uenyekiti wa Kamati hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Mwakilishi wa Kudumu wa India Kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ruchira Kamboj ambaye ndiye Mwenyekiti amesema,(Sauti ya Ruchira Kamboj)“Ugaidi katika aina zote zile, katika muonekano wowote ule ni moja ya vitisho vikubwa zaidi vya amani na usalama duniani. Kitendo chochote cha kigaidi hakiwezi kuhalalishwa kwa misingi ya nia yoyote ile, wakati uliofanyika, pahali ilipofanyika na ni nani aliyetekeleza. Kamati imejizatiti kupambana na janga hili katika ngazi ya kimataifa.”Kutokana na ugumu wa suala zima, na kasi ya mapinduzi yake, matarajio ni kwamba wajumbe watakuwa na nyaraka ya mwisho ambayo itatoa mwelekeo wa jinsi magaidi wanatumia teknolojia, kwa lengo la kufunga simulizi zao na matumizi ya teknolojia.Kamati ya kukabili ugaidi ya Baraza la Usalama la UN iliundwa kwa kauli moja tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2001, kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani tarehe 11 Septemba 2001 na wanachama ni wajumbe wote 15 wa Baraza la Usalama.
Kijana Gibson Kawago kutoka Tanzania ambaye ni miongoni mwa vijana 17 walioteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa viongozi vijana wa kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema atatumia kipindi cha miaka miwili cha nafasi hiyo kusongesha hatua kwa tabianchi ikiwemo kutumia ugunduzi wake kuchakata betri chakavu za kompyuta kutengeneza betri za kuzalisha umeme katika kulinda na kuhifadhi mazingira. Nina furaha sana kuteuliwa na nitakuwa balozi mwema Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akiwa Dar es salaam nchini Tanzania, Gibson amesema amepokea kwa furaha kubwa uteuzi huu akisema, “nina furaha kubwa sana kuweza kuteuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kutambua mchango wangu kwenye kutatua matatizo katika jamii hii ninayotoka. Kijana huyu mwenye umri wa miaka 27 ambaye sasa anamiliki kampuni ya WAGA inayotengeneza betri hizo amesema anaamini kilichomfanya ateuliwe ni kazi yake ya kulinda mazingira na kubuni mbinu za nishati salama. “Sisi tunajihusisha kuchakata betri za kompyuta mpakato, sasa hivi watu wakibadilisha betri kwenye kompyuta zao wanazitupa na zinachafua mazingira, na mara nyingi zikiingia kwenye udongo huleta madhara kwa afya ya binadamu,” amesema Gibson. Betri hizo zikiisha umeme huchajiwa kwa sola Wanachofanya WAGA ni kuchakata hizo betri na kutengeneza kasha la betri ambalo hutumiwa na wananchi wa vijijini kutumia kupata nishati mbadala na wanachaji kwa sola. Betri hiyo hutumika katika kuwasha taa na hata kuwasha televisheni. Kifuatacho ni nini? Gibson amesema kipindi cha miaka miwili cha nafasi hiyo ya kijana kiongozi wa kusongesha SDGS, atajitahidi kuwa balozi mzuri kuhakikisha vijana wenzake wanafahamu jinsi gani ya kutunza mazingira na wanajua ni jinsi gani watatafuta fursa tofauti kutatua matatizo katika jamii zao na kuhakikisha wanatunza mazingira yao. Kifo cha bibi yangu kilinichochea kutafuta jawabu la nishati Gibson anasema chanzo cha yeye kujikuta kwenye ubunifu huo ni kifo cha bibi yake. “Kuna siku nikiwa kijijini nilikuwa natumia simu yangu kumuonesha bibi picha za harusi. Katikati betri ikaisha na hatukuwa na umeme. Kesho yake nikasafiri umbali mrefu hadi mjini kupata betri.” Anasema hata hivyo aliporejea nyumbani alikuta bibi yake amefariki dunia kwa kuwa hali yake ya kiafya haikuwa nzuri. “Kwa hiyo wakati napata maumivu yale na kuwaza ni watu wangapi wanapata matatizo hayo nje nilipofika Dar es salaam wakati nasoma Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Ufundi, DIT nikaanza kutafiti ni kwa vipi naweza kutengeneza betri inayohifadhi umeme,” amesema Gibson. Amesema alisaka mafunzo kwenye mtandao na hatimaye akaweza kutambua jinsi ya kuchakata betri chakavu za kompyuta mpakato ili kuzalisha umeme. Sasa betri zinawasha televisheni na taa vijijini Kwa mujibu wa Gibson, anatengeneza makasha ya betri kutokana na betri chakavu za Lithium na Ion, na betri. “Nimeweza kutengeneza betri kubwa ambazo inawezesha mtu wa kijijini kuweza kuwasha televisheni, kuwasha taa zake na kuweza kutumia na ikiisha anaweza kuchaji kwa nishati ya jua au sola.
Ikiwa leo Agosti 9 ni siku ya Kimataifa ya watu wa jamii ya asili dunani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa siku hii, ametoa wito kwa ulimwengu kuzidisha zaidi sauti za wanawake wa jami ya asili kwani wana mchango mkubwa duniani. Taarifa Zaidi na Anold Kayanda. Ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia video ya ujumbe wake akianza kwa kueleza kinachoangaziwa katika Siku ya Kimataifa ya Watu wa asili Duniani ya mwaka huu, kwani kuhusu jukumu la wanawake wa jamii za asili katika kuhifadhi na kupitisha maarifa ya jadi kutoka kizazi hadi kizazi. “Wanawake wa jamii za asili ni watunzaji wa maarifa ya mifumo ya chakula na dawa asilia. Ni mabingwa wa lugha na tamaduni za asili. Wanalinda mazingira na haki za binadamu za watu wa asili.” Anaeleza Guterres. Bwana Guterres anatoa ushauri kwamba ili kujenga mustakabali ulio sawa na endelevu ambao haumwachi mtu nyuma, lazima dunia izipe nafasi zaidi sauti za wanawake wa jamii za asili na kwamba maarifa asilia ya kitamaduni yanaweza kuleta ufumbuzi kwa changamoto zetu nyingi. Akitoa mfano wa hivi karibuni wa namna alivyoshuhudia haya anayoyasema, Katibu Mkuu Guterres anakumbushia alipokuwa ziarani hivi karibuni nchini Suriname, kwamba alijifunza kwa kuona kabisa jinsi watu wa jami za asili wanavyolinda msitu wao wa mvua na bainuai yake tajiri. Kwa msingi wa hayo yote, Katibu Mkuu anatoa wito kwamba katika Siku hii ya Kimataifa, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa watekeleza Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa jamii za asili na kuendeleza maarifa asilia kwa manufaa ya wote.