Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana
Vile Mwanabaharia Swaleh Yahya alipata kisanga akiwa baharini na ndugi yake na Mtalii
Vile kijana Murad Swaleh aliingilia Dawa za Kulevya tokea utotoni na kueza kujitoa baadae
Vile Mwanahabari alipoteza macho yake kwa ugonjwa unaoitwa Glaucoma
Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama. Kufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo. Fatuma Hamisi mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Salex Transition Academy.Yeye ni mwanafunzi wa gredi ya 6 na pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira katika shule hiyo. Mwandishi:Athuman Luchi
Licha ya idadi ya wanawake katika taalum ya teknologia kuwa ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanaume, wanawake wameonekana kupambana ili kukabiliana na tofauti hiyo. Ripoti kutoka benki kuu ya dunia inaonyesha kuwa wanawake wako chini ya thuluthi moja ya wafanyikazi ulimwenguni katika nyanja zinazohusiana na teknolojia. Ambapo wanashikilia asilimia 28 ya kazi zote za kompyuta na hisabati, na asilimia15.9 ya kazi za uhandisi na usanifu Mwandishi:Nuru Mwalimu
Makala haya yanazungumzia kuhusu uchafuzi wa bahari hasa katika eneo la Mbuyuni-Mji wa Kale kaunti ya Mombasa. Eneo hilo limeathirika na maji taka yanayotoka katika nyumba zinazopakana na ufuo wa bahari.Makala haya yametayarishwa na Ruth Keah.
17-year-old Jane is among the children with mental disabilities who were molested and impregnated. Jane is currently raising a three-month-old baby boy. By Rose Tawa.
Mabadiliko ya Tabia Nchi yameathiri sana wakulima na wafugaji hatua inayo wafanya wengi kukumbwa na tatizo la afya ya Akili.Kufuatia hatua hio sasa baadhi ya wakulima wanajizatiti kukabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na mabadiliko hayo.Sasa wakulima hao,wamejitosa katika ufugaji wa nyuki na vipepeo,huku wengine wakifanya biashara ndogo ndogo za kukimu mahitaji ya familia. Athuman Luchi,ametuandalia makala hayo aliyoyapa jina la Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change
Makala haya yanazungumzia kuhusu hatua ambazo zimepigwa na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa dhulma za mtandaoni zinaripotiwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu ujangili unaofanyiwa viumbe vya baharini. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu mbinu ya Rangi ambayo wanabodaboda kaunti ya Mombasa wanatumia kutofautisha sehemu wanazohudumu kama njia moja ya kukabiliana na visa vya uhalifu. Makala yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi za mashirika mbalimbali ambayo yamekuja pamoja kukabiliana na uvuvi wa kutumia mbinu haramu katika eneo la Shimoni Kwale. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Ukataji wa miti kiholela umesababisha mabadiliko ya tabianchi,kiangazi,mmomonyoko wa udongo,mafuriko na ongezeko la hewa chafu hatua inayochangia athari mbali mbali kwa jamii. Kufuatia mabadiliko hayo ya tabia nchi,sasa jamii imejitokeza kuja na mbinu mbali mbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Makundi ya wanawake na vijana katika kaunti ya kwale yanaendeleza mpango wa upanzi wa miti,walioupa jina la Mti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kila boma. By Rose Tawa.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jamii ilivyoungana kulinda mazingira hasa mikoko katika eneo la Mida Creek Dabaso. Hatua iliyowafanya kujenga mkahawa juu juu ya mikoko na kwasasa mkahawa huo umekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka humu nchini na hata nje ya nchi. Mtayarishi ni Ruth Keah.
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuathiri kila mtu kila siku,kufuatia hayo watu wenye ulemavu wamejikita katika mbinu mbali mbali za kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi jijini Mombasa.Mwanahabri wetu Nuru Mwalimu ametuandalia makala yanayosimulia juhudi za watu wenye ulemavu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi mbalimbali ambazo wanahabari wa Radio wanafanya kuhakikisha kuwa habari wanazopeperusha hewani ni za uhakika. Yametayarishwa na Ruth Keah
Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha mtu kupoteza fahamu kwa muda. Ugonjwa huu unaweza kumsababishia mtu kufanya vitendo visivyokuwa vya kawaida kama vile kuanguka, kufifitika na hata baadhi ya wagonjwa kutojielewa. Kulingana na takwimu kutoka kwa shirika la afya dunia WHO, takriban watu milioni 50 duniani wanaugua maradhi haya, na kuyafanya kuwa miongoni mwa maradhi maarufu zaidi ya ubongo duniani.
Makala haya kuhusu Uji wa chekechea yametayarishwa na Baya Kitsao.
Makala ya habari ghushi kuhusu Corona ambazo zilikuwa zikisambaa kuwa madaktari wa kienyeji walikuwa wakitibu virusi vya Corona. Imetayarishwa na Baya Kitsao.
Makala ya Dosari Ya Shilingi yalioandaliwa na Oscar Ochieng yanahusu madeni katika kaunti ya Mombasa. Makala haya yanazamia sababu zinazopelekea kaunti hii kushuhudia madeni ya kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ya kifedha iliyopita wakati ambapo utawala wa sasa umeunda jopo kung'amua ukweli kuhusu madeni hayo.
Kwa mara nyingi sekta ya usambazaji wa gasi safi imechukuliwa kama kazi inayofanywa na wanaume. Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake kutoka kaunti ya Mombasa waliojiingiza katika sekta hiyo na kujipatia kipato na kuimarisha maisha yao. Mtayarishi wa makala haya ni Ruth Keah.
Hali ya kiangazi na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kukumba sehemu mbali mbali humu nchini, hivyo basi inasababisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mazao ya chakula.Hali hii imeathiri mapato na kupanda kwa bei za vyakula. Katika kutafuta suluhu zinazowezekana kukabili hali hii, kikundi cha wanawake wakulima kutoka eneo la Lunga Lunga,walianzisha mradi unaoitwa "agrivoltaics,"yaani kutumia paneli za jua katika ukulima ambao husaidia kukabiliana na hali ya ukame unaozidi kuongezeka.
Kaunti ya Kilifi katika miaka ya hivi karibuni imetajwa kuwa Moja wapo ya kaunti zinazoongoza Kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba za mapema nchini. Takwimu kutoka kwa mfumo wa taarifa za afya nchini yaani Kenya Health Information System zikionyesha kuwa jumla ya wasichana 4,909 walio na umri wa kati ya miaka 15-18 walipata mimba katika kipindi Cha mwezi Januari Hadi Agosti Mwaka 2021. Na kama anavyosimulia Ali Mwalimu kwenye makala haya, mashirika mbalimbali kaunti ya Kilifi yamejitokeza kukabiliana na tatizo hilo.
Licha ya kuwa na haki ya urithi pindi mwanawake anapofiliwa na mumewe, jamii imekua tishio kubwa kwa kina mama pindi wanapofiliwa kutona na mila na desturi potofu katika jamii huku takwimu nchini zikionesha kuwa takriban wajane milioni 8 nchini wametelekezwa kutokana na mila potofu na umaskini. Mwandish: Nuru Mwalim.
Makala haya yanahusu wanawake wanaopata mafunzo ya kujikimu kimaisha wakati ambapo suala la ajira limekuwa changamoto nchini. Kando na kujikimu ki maisha, mafunzo wanayopata vile vile yanalenga kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakazi wengi ukanda wa pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.
Wakazi wengi ukanda wa Pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.
Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo, Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi. Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao. Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo, Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi. Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Kila mwaka Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ni maalumu kwa kuelimisha jamii kuhusu ulemavu wa kuona, athari zake na njia za kuzuia matatizo ya macho. Mwaka huu,siku hiyo iliadhimishwa tarehe 13 mwezi wa Oktoba. Makala haya ambayo yametayarishwa na Ruth Keah, yanazungumzia kuhusu mwanamke ambaye ana changamoto ya kuona lakini amepuuza changamoto hiyo na anahudumia jamii kwa njia mbalimbali.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya. Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa. Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Tangu ya kuanzishwa kwa Mradi wa Skills Mtaani eneo bunge la Mvita zaidi ya Vijana 11,000 wamenufaika na mradi huo na sasa wengine wameajiriwa na wengine wamefungua biashra zao. Mwanahabari wetu Athuman Luchi ametuandalia makala,kuhusu mradi huo.
Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini. Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu. Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.
Makala haya yanaangazia juhudi za kijana kutoka kaunti ya Kilifi-Kenya anayeng'aa katika soka ya kimataifa licha ya kuwa mlemavu. Licha ya kukatazwa kucheza na wazazi wake, hakufa moyo na kuendeleza kipaji chake na kwasasa anategemewa na familia yake kutokana na kipato anachopata kutokana na kucheza soka.
Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo. Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo. Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Mirundiko ya takataka sio tu katika nchi kavu bali pia baharini kwa miaka mingi imekuwa shida kubwa kuthibiti, taka za baharini zikichangia kuharibika kwa miamba ya matumbawe. Lakini katika Kijiji cha Mkwiro kaunti ya Kwale Ukanda wa pwani, baadhi ya taka za baharini na zile za nchi kavu zimegeuzwa kuwa thamani kwa kutumia mchakato mbadala wa kutengeneza chupa za matumbawe. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.
Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu nchini Kenya asilimia 0.3% ya watu wanaugua ulemavu wa akili jijini Mombasa. Wengi wa wenye ulemavu wa akili ukumbwa na unyanyapa,msongo wa mawazo na utengwa katika jamii,hivyo wanajipata wakirandaranda mitaani. Juma Ali ni kijana mwenye umri wa miaka 30, aliyepona matatizo ya akili yaliyomsumbua kwa muda wa miaka 5. Anasema alianza kurukwa na akili baada ya kumpoteza mchumba wake katika ajali ya barabarani.Anataja kifo hicho kilimfanya kukabwa na msongo wa mawazo na kuanza kutembea uchi na kushambulia watu. Mwandishi:Athuman Luchi.
Watoto wengi wenye matatizo ya akili upitia unyanyasaji wa kingono,kupachikwa ujauzito na wengi wa wanao bakwa usalia kimya wasijue wapi pa kuripoti kisa hicho,Mariam mwenye umri wa miaka 16 ni kati ya watoto wenye ulemavu wa akili walionajisiwa na kupachikwa mimba. Mariam ambalo si jina lake kamili alibakwa na kusalia kimya bila hata kumjulisha mamake. Kwa Sasa Mariam analea mtoto mvulana mwenye umri wa miezi mitatu.Anataja kuwa alikuwa ameenda msalaani kujisaidia na huko ndiko alikumbana na jamaa aliyemdhulumu kwa kumbaka. Mwandishi:Athuman Luchi
Bara la afrika limemulikwa sana katika ukuaji wa miundo msingi yake katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi na upanuzi wa barabara. Licha ya miradi hiyo kurahisisha usafiri kwa mwananchi,bado kuna changamoto kubwa kwa jamii ya watu wenye ulemavu kutokana na ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwao. Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya. Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa. Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea. Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya. Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa. Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea. Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi ya jamii zilizotengwa. Na ili kuimarisha uwakilishi wao katika ulingo wa siasa,Kumekuwa na kila juhudi kuhakikisha kuwa makundi yaliyotengwa yamepata nafasi sawa za uwakilishi. Hata hivyo kulingana na matokeo yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 humu nchini Kenya, hayakuwapendeza watu wenye ulemavu. Kama anavyoarifu mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.
Kutokana na ajali nyingi za barabarani zinazoshuhudiwa humu nchini hasa kwa watu wanaotembea, Serikali iliweka mikakati ya kupunguza ajali hizo kwa kujenga madaraja ya juu ili mwananchi atumie kwa usalama wake mwenyewe. Lakini licha ya hatua hiyo ya serikali, bado kuna baadhi ya watu wanaopuuza kutumia daraja hizo,mwishowe huishia kutiwa nguvuni na polisi ama askari wa kaunti kwa kukiuka sheria. Mhariri wetu Ruth Keah amefanya mahojiano na baadhi ya watu walioshikwa na kueleza yaliyojiri mikononi mwa maafisa hao wa usalama.