Podcasts about ufugaji

  • 6PODCASTS
  • 43EPISODES
  • 13mAVG DURATION
  • 1MONTHLY NEW EPISODE
  • Feb 17, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about ufugaji

Latest podcast episodes about ufugaji

Habari za UN
17 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 17, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu kwa wakimbizi na raia wa Sudan, na maradi wa lishe bora kwa watotot nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Kutokana na hali tete ya kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo Februari 17 jijini Genea, Uswisi, wamezindua mipango ya misaada ya kibinadamu na wakimbizi kwa mwaka huu 2025 kwa Sudan, wakihitaji jumla ya dola bilioni 6 kusaidia karibu watu milioni 26 ndani ya Sudan na kanda nzima.Mradi unaoendeshwa na serikali ya kenya  na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania anakuletea mnufaika wa mafunzo ya ufugaji bora wa mbuzi.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, nampisha Hellen Bulandi kutoka zambia ambaye ni mnufaika wa mpango wa uhamisho wa fedha taslim wa shirika hilo kwenda kwa jamii  ambao umewezesha watoto kwenda shule kupitia mapato yatokanayo na uwekezaji katika kilimo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Mradi wa ufugaji bora wa mbuzi umenikwamua – Mfugaji Kigoma

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 17, 2025 4:06


Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania linaendelea kutekeleza Programu ya pamoja kwa mkoa wa Kigoma KJP iliyoanza kutekelezwa nchini humo mwaka 2017 na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto za kipekee za mkoa huo ikiwemo zitokanazo na kuhifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.Miongoni mwa miradi inayotekeleza ni ule wa kupatia wananchi mafunzo ya ufugaji bora wa mbuzi ili waweze kuinua kipato chao na vile kuimarisha lishe kwenye familia.Kupitia video ya FAO, utamsikia mnufaika wa mafunzo hayo kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Habari za UN
FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 18, 2024 2:50


Mradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia. Tupate simulizi zaidi katika makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha kupitia video ya FAO Tanzania.

Habari za UN
25 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 9:47


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, na Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC la kukarabati daraja linalounganisha barabara muhimu. Makala tunakwenda nchini Tanznaia na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza?Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo.Makala inatupeleka Tanzania kwake Hamad Rashid wa redio washirika Kidstime FM ya mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo akizungumza na wanufaia wa mafunzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO la ufugaji kuku bila kutumia dawa.Na mashinani tunakwenda Kenya kusikia harakati za viongozi wa dini ya kiislamu kukabiliana na ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 

Habari za UN
Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 3:55


Nchini Tanzania wanufaika wa  mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao  ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA  ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.

Habari za UN
Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 21, 2024 3:20


Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu  siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali  kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.

Radio Maria Tanzania
Ni, kwa namna gani ufugaji Nyuki husaidia Wanawake kujikwamua kiuchumi?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jul 31, 2024 28:45


Karibu uungane nami Agatha Kisimba katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo ambapo leo tuko na Bi. Claudia Morand, Mkurugenzi wa Kampuni ya Acla Honey Enterprises akiongelea na kuelezea juu ya Wanawake na fursa ya ufugaji nyuki katika kujikwamua kiuchumi.                                 L'articolo Ni, kwa namna gani ufugaji Nyuki husaidia Wanawake kujikwamua kiuchumi? proviene da Radio Maria.

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa ngombe wa Maziwa

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Ufugaji wa ngombe wa Maziwa

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Kuku

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Ufugaji wa Kuku

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Ngombe

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Ufugaji wa Ngombe

Habari za UN
Bahari ni sehemu ya suluhisho la matatizo lukuki katika jamii - FAO

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 7, 2023 0:02


Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.Bahari, ni makazi ya asilimia 80 ya majani ya wanyama, ambayo yanatumika kama chanzo muhimu cha wananchi kujipatia riziki na pia lishe kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Rasilimali za Uvuvi na Ufugaji wa samaki kutoka FAO Manuel Barange, anasema kwa utajiri uliopo baharini, “Hakuna tatizo hata moja ambalo tunalo ulimwenguni iwe kwenye mabadiliko ya tabianchi, umasikini au uhakika wa chakula ambalo linaweza kutatuliwa bila kuzingatia baharí kama sehemu ya suluhisho” Manuel anasema kwa sasa zaidi ya watu milioni 800 wameathiriwa na njaa kote ulimwenguni, vyakula vya baharini vilivyo sheheni lishe ya hali ya juu ni suluhisho la kushughulikia njaa na utapiamlo, “Ufugaji wa samaki umekuwa mfumo wa uzalishaji wa chakula unaokua kwa kasi zaidi katika kipindi cha  miongo mitano iliyopita. Ulaji pia wa vyakula vya majini umekuwa ukiongezeka maradufu ya kiwango cha ongezeko la watu katika miongo ya hivi karibuni.”Katika kuhakikisha kila nchi inajitosheleza na kuweza kuhimili ongezeko la uhitaji wa vyakula vya majini FAO inahamasisha utekelezaji wa mkakati wa Mabadiliko ya Buluu Blue Transformation unaolenga kuimarisha mifumo ya vyakula vya majini katika kulisha idadi ya watu inayoongezeka duniani kwa kutoa mifumo ya kisheria, sera na usaidizi wa kiufundi inayohitajika ili kuendeleza ukuaji na uvumbuzi, “Mpango wa Mabadiliko ya Bluu ni dira kutoka FAO ambayo imeanza na kanuni mbili kubwa. Kwanza ni kukubali kwamba vyakula vya majini ni sehemu ya suluhisho la njaa na utapiamlo. Pili ni utambuzi kwamba mabadiliko yanafanyika hata bila sisi kufanya lolote.”Mpango wa Mabadiliko ya Buluu umependekeza msururu wa hatua zilizoundwa kusaidia ustahimilivu katika mifumo ya chakula cha majini na kuhakikisha uvuvi na ufugaji wa samaki unakuwa kwa njia endelevu huku hakuna mtu anayeachwa nyuma, hususan jamii zinazotegemea sekta hiyo.Masuala mengine yanayoangaziwa na mabadiliko hayo ni pamoja na sera na desturi zinazofaa kwa mabadiliko ya tabianchi na mazingira, pamoja na ubunifu wa kiteknolojia.

RadioRahma
Uhifadhi wa Mikoko kupitia ufugaji wa Nyuki

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 11:07


Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini. Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu. Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

mombasa kijiji makala wakazi ufugaji
RadioRahma
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part One

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 7:53


Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

RadioRahma
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two

RadioRahma

Play Episode Listen Later Oct 21, 2022 9:57


Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni. Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha. Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Habari za UN
Mradi wa FAO Thailand warejesha si tu vibua bali pia ufugaji wa kamba wadogo umeimarika

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 5, 2022 2:19


Nchini Thailand, neema imerejea tena kwa wafugaji wa Kamba wadogo baada ya mradi wa FAO wa teknolojia mpya ya kuchuja maji na kulisha viumbe hao kusaidia kuondoa changamoto waliyopata awali ya milipuko ya magonjwa kutokana na uchafu wa maji kwenye mabwawa wanayofugia. Taarifa iliyoandaliwa na FAO ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO inasomwa na Ibrahim Rojalla wa televisheni washirika Mamlaka TV inafafanua zaidi. Mradi unatekelezwa kwenye jimbo la Khiri Khan nchini Thailand kwenye mabwawa ya kisasa ya ufugaji samaki, mfugaji akitembea kwenda kuvua samaki kwa kutumia wavu unaonin'ginizwa kwenye njia anamopita, iliyojengwa kwa wavu juu ya mabwawa hayo. Samaki wamenasa nyavuni na kando ni mashine maalumu yenye magurudumu ya chuma na mfumo wa kutumia hewa inayopuliza maji . Inapita juu ya maji kwa lengo la kuchuja uchafu. Awali kabla ya teknolojia hii, walitumia siku hadi 10 kusafisha maji ambayo yanachafuliwa si tu na mabaki ya vyakula vya kamba hawa wadogo bali pia uchafu wa haja zao kubwa. Uchujaji usiokuwa fanisi hapo awali ulisababisha milipuko ya magonjwa na mabwawa kufungwa. Kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo wamepatiwa mashine hii ya kuchuja uchafu, halikadhalika mfumo wa kisasa wa kupatia samaki chakula badala ya kumwaga kwenye bwawa. Kirana Leesakulpran, mama wa watoto wawili na ambaye amekuwa akifuga samaki aina ya Kamba kwa zaidi ya miaka 30 anasema, “tangu tuanze kutumia teknolojia hii, tunapata kamba wengi zaidi, faida imeongezeka na maisha ya ukulima ni endelevu zaidi.” Nchini Thailand zaidi ya watu milioni 23, takribani asilimia 34 ya watu wote hawana uhakika wa kupata chakulia na FAO kupitia mradi wa kusaidia uchumi utokanao na shughuli za baharini na majini, inasaidia Thailand kuongeza tija kwenye ufugaji samaki kwa kudhibiti pia uvuvi wa kibiashara. Theerapong Thammasara ni mvuvi mdogo ambaye anaona mabadiliko ya kiwango cha uvuvi kabla na baada ya mradi. (Sauti ya Theerapong Thammasara) “Nadhani ni kwa sababu ya kanuni zote zinazotekelezwa. Meli kubwa za uvuvi haziruhusiwi kufika maili tatu kutoka pwani. Na kuna sheria kuhusu ukubwa wa nanga. Hizi ni sababu ya kurejea tena kwa vibua.” Ama hakika katika soko tuliloingia kupitia video ya FAO, vibua ni wakubwa na wengi na bila shaka lengo la kutokomeza uhaba wa chakula na lishe bora litafikiwa.  

Habari za UN
Ripoti ya FAO yaonesha mchango wa uvuvi na ufugaji wa samaki katika kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa chakula

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 29, 2022 2:26


Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiwa katika siku ya tatu hii leo huko Lisbon nchini Ureno Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ongezeko kubwa la ufugaji wa samaki sambamba na uvuvi wa kimataifa umesababisha mazao ya vyakula vya majini kuwa kwenye rekodi ya juu katika kuchangia kwa kiasi uhakika wa chakula na lishe katika karne hii ya Ishirini na moja. Taarifa ya Leah Mushi. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya FAO iliyotolewa leo kwenye miji ya Lisbon Ureno na Roma Italia ikinukuu Ripoti ya mwaka huu wa 2022 kuhusu Hali ya uvuvi na mazao ya majini au SOFIA.  Akizungumzia ripoti hiyo Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu amesema jumla ya uvuvi na ufugaji wa samaki ulifikia kiwango cha juu cha tani milioni 214 mwaka 2020 ikijumuisha tani milioni 178 za wanyama wa majini na tani 36 za mwani.  Uvuvi na ufugaji wa samaki huchangia katika ajira, biashara na maendeleo ya kiuchumi. Jumla ya mauzo ya kwanza ya thamani ya uvuvi na ufugaji wa samaki na wanyama wa majini kwa mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa dola bilioni 406, ambapo dola bilioni 265 zilitokana na uzalishaji wa ufugaji wa samaki.  FAO imesema ukuaji wa uvuvi na ufugaji wa samaki ni muhimu duniani kote katika jitihada za pamoja za kumaliza njaa na utapiamlo lakini kunatakiwa kufanyika mabadiliko ili kukabiliana na changamoto zilizopo.  Dongyu amesema wakati sekta hiyo ikizidi kukuwa “kunahitajika mabadiliko ili kuwa na sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu zaidi, yenye ushirikishaji na usawa kwakuwa biashara ya kutumia vyakula vya majini ni muhimu ikiwa tunataka kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa”.  “Lazima tubadili mifumo ya chakula kitokanacho na kilimo ili kuhakikisha vyakula vya majini vinavunwa kwa uendelevu, maisha yanalindwa na makazi ya majini na viumbe hai vinalindwa”  Na ili kupata suluhisho la changamoto za uzalishaji huo Mkurugenzi Mkuu wa FAO anayehusika na Idara ya Uvuvi na Ufugaji wa samaki Manuel Barange amesema kunahitajika  mabadiliko ya bulu “Ni mchakato unaoendeshwa na malengo ambapo wanachama na washirika wa FAO wanaweza kuongeza mchango wa mifumo ya chakula cha majini ili kuimarisha uhakika wa chakula , lishe bora na lishe kwa gharama nafuu huku ikibaki ndani ya mipaka ya ikolojia” 

Habari za UN
FAO yawapigia chepuo wavuvi wadogo na wafugaji wa samaki

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 1, 2022 3:06


Mkutano wa siku nne wa wakuu wa nchi zenye bahari duniani, umeanza leo huko Roma Italia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo -FAO limetoa wito kwa wasomi, serikali, mashirika ya kiraia na sekta binafsi kutambua umuhimu wa wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki, ambao ni sehemu muhimu ya uvuvi. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Happiness Palangyo wa Redio washirika Kids Time FM ya Morogoro Tanzania (Taarifa ya Hapiness Palangyo ) Bahari, inachukua jumla ya  asilimia 70 ya uso wa dunia na kusaidia maisha ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Lakini bahari inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uvuvi wa kupita kiasi, uchafuzi wa bahari na mabadiliko ya tabianchi na hivyo vyote vinatishia uwezo wa bahari kuendelea kutoa huduma muhimu za mfumo wa ikolojia na rasilimali muhimu za chakula. Wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki ni sehemu muhimu ya mifumo ya chakula duniani na inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kulinda bahari, hata hivyo, hawatambuliwi au kueleweka vyema kama anavyoeleza mvuvi José Tejeda Dumé kutoka Santo Domino, DOMINICAN REPUBLIC. “Sekta fulani zinatupuuza. Hawaoni kwamba mvuvi huamka saa 10 alfajiri na kukumbana na dhoruba na mvua. Ni lazima aende baharini ili kuwapatia rizki watoto wake.” FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP imejitolea kuimarisha shughuli za uvuvi wa kisanaa, kuhakikisha kuwa watu wanaohusika katika sekta hii wanapata usaidizi na kutambuliwa ipasavyo kama anavyoeleza  Vera Agostini, Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uvuvi na Ufugaji wa samaki cha FAO "Uvuvi mdogo mdogo na ufugaji wa samaki hautambuliki kuwa ni muhimu sana. Tukiangalia tu baadhi ya takwimu zinaweza kukusaidia kuelewa, zinaweza kutusaidia sote kuelewa kwamba asilimia 90 ya wanaojihusisha na uvuvi ni wale ambao ni wavuvi wadogo, watu milioni 60 na asilimia 40 ya hao ni wanawake. Kwa hivyo, kwa kweli ni sehemu muhimu ya uvuvi, lakini hazitambuliki na hazithaminiwi. Tunahitaji kupata neno kuhusu umuhimu wao, na tunahitaji kuwasaidia watoa maamuzi kutambua hilo na kuchukua hatua”. Agostini ameongeza kuwa FAO inaamini mifumo ya chakula cha majini ni sehemu muhimu ya mifumo ya chakula duniani. Kwa nini? ( Sauti ya Vera Agostini, Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uvuvi na Ufugaji wa samaki cha FAO) “Kwa sababu wao huboresha lishe, haswa kwa walio hatarini zaidi, ni sehemu muhimu ya ukuaji wa uchumi, na hutoa suluhisho ambazo hupunguza kiwango cha uharibifu wa mazingira cha mifumo ya chakula. Kwa hivyo, mkutano huu wa kilele ni fursa muhimu sana kuleta ajenda hiyo ya mabadiliko ya bluu na kushiriki katika mazungumzo na kundi tofauti la wadau watakaokuwepo”. FAO imejidhatiti kuimarisha shughuli za uvuvi wa kisanaa, kuhakikisha kuwa watu wanaohusika katika sekta hii wanapata usaidizi na kutambuliwa ipasavyo.

Habari za UN
Tutumie elimu tulizonazo kwa vitendo kwa ajili ya ustawi wa jamii zetu – Dkt. Anthony Kiiza 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2022 3:48


Ufugaji na kilimo ni moja ya mambo mtambuka ambayo yakifanikiwa yanachangia katika kufanikisha idadi kubwa ya malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kati ya 17 ambayo yanalengwa kufikiwa ifikapo mwishoni mwa muongo huu, mwaka 2030.   Mathalani lengo namba moja linazungumzia kutokomeza umaskini, namba mbili linaongelea kutokomeza njaa, namba tatu linaongelea afya bora, namba saba linazungumzia nishati bora na ambayo ni nafuu na lengo namba nane likizungumzia ukuaji wa uchumi. Malengo yote hayo yanaguswa moja kwa moja na kilimo.   Kwa msingi huo, kijana daktari wa mifugo nchini Uganda, Dkt. Anthony Kiiza anasema hajutii kuwekeza katika kilimo na ufugaji kwani hiyo inampa fursa ya kukuza uchumi wake huku akitekeleza utaalamu wake kwa vitendo. Zaidi ya hayo, anahamasisha vijana wenzake kujihusisha na shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ili kukuza uchumi wao na wajamii zinazowazunguka. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amezungumza na kijana huyo katika makala ifuatayo.  

Habari za UN
Nchini Zimbabwe FAO kuhakikisha ufugaji samaki una tija shambani hadi mezani 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 2, 2022 2:13


Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa teknolojia ya ufugaji wa Samaki nchini Zimbabwe imekua bado lengo la kufanikisha uhakika wa chakula kwa kuhakikisha Samaki anafika mezani bado linakabiliwa na changamoto kwa kuwa gharama ya ufugaji ni ya juu halikadhalika gharama ya kitoweo hicho. Kariba nchini Zimbabwe katika mabwawa ya ufugaji Samaki yanayomiliwa na Lake Harvest Farm, teknolojia ni ya kisasa kuanzia shambani hadi kiwandani ikiwemo uchambuzi wa samaki aina ya sato.  Kutoka Kariba tunaingia Karoi, shamba lingine lingine la ufugaji samaki likimilikiwa na kampuni ya ufugaji samaki ya Edeni, na mmiliki wake Hafra Nanhanga, naye anafuga sato na anasema, “nilipoingia kwenye ufugaji wa sato, nilidhani ni rahisi, hasa tulipoanza kujenga mabwawa tulijua tunaweza kuchimba tu mashimo yetu na kujenga kuta, kumbe tunahitaji mashine za kuchimba.”  Tariro Chari, Meneja Mkuu wa shamba la Lake Harvest  anasema samaki anafugwa majini kwa kati ya miezi sita hadi tisa kulingana na uzito anaotaka mnunuzi wa kati ya gramu 300 hadi 900 na “suala kubwa kwa mfugaji yoyote wa sato ni lishe ya Samaki, kwa sababu chakula kinagharimu asilimia 60 ya gharama zote za uendeshaji.”  Kwa kutambua kuwa Zimbabwe ni nchi isiyo na baharí, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO lilianzisha mradi wa kusaidia wafugaji wa Samaki ili kuongeza kipato na kuimarisha afya kupitia kitoweo cha Samaki, mradi unaoitwa FISH4ACP uliobuniwa na shirika la nchi za Afrika, Karibea na PAsifiki, na kutekelezwa na FAO.  Mradi unawekeza kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji wa Samaki kuanzia shambani hadi mezani lakini bado ulaji samaki nchini Zimbabwe ni wastani wa kilo 2.6 kwa mtu mmoja kwa mwaka ilhali katika nchi za ukanda huo wastani wa ulaji ni kilo 6.   Gilles Van De Walle wa kitengo cha ufugaji Samaki FAO anasema, “tunataka kufanya kazi kuanzia kwenye boti au kwenye nyavu hadi kwa walaji. Tunataka huu mnyororo uwe na manufaa kama inavyotakiwa.”  FAO imetangaza mwaka 2022 kuwa mwaka wa kimataifa wa uvuvi wa kienyeji na ufugaji wa Samaki. 

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
RadioRahma
Tamu Tamu ya asali yapotea kwa ukame

RadioRahma

Play Episode Listen Later Nov 21, 2021 14:56


Mbali na kuwa mdudu mkali wapo waliozama katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya uzalishaji wa asali kwa matumizi mbalimbali ikiwemo dawa. Ikumbukwe kuwa si wengi wenye ujasiri na ukakamavu wa kufuga nyuki kutokana na dhana na kasumba kuwa ni wadudu hatari kufuga licha ya kuwa na manufaa tele. Ufugaji wa nyuki hauna mahitaji mengi ikilinganishwa na ufugaji mwengine wowote cha msingi ni mfugaji kuwa na mizinga. Kama ukulima na ufugaji wengine wowote ule Nyuki pia hutegemea mvua kwa sababu nyuki hutegemea maua kama chakula na wakati wa mvua ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali hushamiri. By:Mwanaharusi Rashid

Habari za UN
Mradi wa ufugaji wa sungura na kuku wae ndelea kutumika kupamba na udumavu Tanzania

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 17, 2021 3:27


Lishe duni kote duniani ni tishio kubwa kwa ustawi wa binadamu kutokana na uhaba wa chakula kwa upande mmoja, na wakati mwingine ukosefu tu wa elimu kuhusu matumizi bora ya vyakula vinavyopatikana katrika jamii. Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs, kwa namna tofauti tofauti yanalenga pamoja na mambo mengine, kuliondoa tatizo hili ili kuwaokoa afya za watu hususani watoto duniani kote. Lengo namba moja la Maendeleo endelevu linaongelea kutokomeza umaskini, lengo namba mbili likiongelea kutokomeza njaa na la tatu likitaka kuwahakikishia wanadamu afya na ustawi bora. Ni kupitia msingi huo, mashirika mbalimbali duniani kama Save the Children wanatekeleza miradi yenye lengo la kutokomeza njaa na kustawisha lishe endelevu kama anavyosimulia John Kabambala wa redio washirika wetu, Tanzania KidsTime FM ya Morogoro Tanzania kuhusu mradi wa USAID Lishe Endelevu unaotekelezwa katika mikoa minne ya Tanzania. 

Habari za UN
Kijana msomi ageukia ufugaji wa nzi ili kunusuru wafugaji wa samaki 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 17, 2021 4:36


Vijana katika sehemu mbalimbali duniani wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kubonga bongo na kusongesha maendeleo yao pale walipo kwa kubaini suluhisho la changamoto zinazokabili jamii inayowazunguka. Miongoni mwao ni Dayana Olembe kutoka Tanzania ambaye baada ya kubaini kuwa wafugaji wa kuku na samaki wanapata shida kupata protini ya kile wanachofuga, akaamua kuingia katika biashara ya ufugaji wa nzi. Ni kweli utashangaa nzi? Ndio! Anafuga nzi, kulikoni?Ungana basi na Devotha Songorwa wa radio washirika Kids Time FM ya nchini Tanzania ambaye alizungumza naye na kuandaa makala ifuatayo.

Habari za UN
Ninatumia nishati ya jua katika ufugaji wa samaki - George Muga

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 13, 2021 3:21


Moja ya masuala yaliyojadiliwa kandoni mwa Mkutano wa ngazi ya juu ya siasa kuhusu maendeleo endelevu unaoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ni pamoja na namna waafrika wengi wanavyopambana na njia za zamani za nishati na hivyo kutafuta njia mbadala kama vile matumizi ya nishati ya jua.  Mfano halisi ni huko nchini Kenya ambako mfugaji wa Samaki amepata mafanikio makubwa baada kuwekeza  kwenye vifaa vya nishati ya jua. George Muga anaelezea manufaa yaliyotokana na hatua aliyoichukua na pia kuwashauri wale walio na miradi inayotumia umeme.

Habari za UN
Elimu yangu ya Chuo Kikuu nimeihamishia katika ufugaji wa kuku – Veronica Kyalo 

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 30, 2021 3:17


Kama ambavyo lengo namba 8 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linazungumzia kazi bora na ukuaji wa uchumi, Veronica Kyalo wa nchini Kenya, pamoja na kuwa miaka nane iliyopita tayari alikuwa na elimu ya juu baada ya kupata shahada ya chuo kikuu katika masuala ya uhasibu, hakupata kazi iliyo bora na hivyo hali yake kiuchumi haikuwa nzuri.

Habari za UN
Peninah Wanja, msomi wa ufugaji ahudumia wafugaji Kenya kidijitali

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jun 10, 2021 3:42


Uvumbuzi ni moja ya malengo 17 ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Vumbuzi mbalimbali zinazotokea duniani hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia, kwa asilimia kubwa zinachangia katika kubadilisha maisha ya watu kuwa mazuri kiuchumi, kiafya au katika maisha yao kila siku na hivyo kukuza ustawi wa wakazi wa ulimwengu. Nchini Kenya uvumbuzi uliofanywa na Peninah Wanja wa Apu ya simu kwa jina DigiCow umewasadia wakulima wafugaji wa ng'ombe kupata huduma muhimu kwa njia rahisi na ya haraka kwa kuwaunganisha wakulima na wataalamu wa afya ya mifugo.

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Faida za ufugaji wa kuku

AWR - Jarida la redio ya Waadvenista Ulimwenguni

Faida za ufugaji wa kuku

Habari za UN
Aliyesomea umeme hakuamini alivyoingia katika ufugaji kuku

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 4, 2021 1:38


Nchini Tunisia, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo duniani, IFAD umeleta nuru kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu nchini humo ambao baada ya kuhitimu wameshindwa kupata ajira na sasa wamejiajiri wenyewe upitia miradi ya ikiwemo ya ufugaji kuku. Anold Kayanda na taarifa zaidi.  

Habari za UN
Mradi wa ufugaji kuku kunusuru misitu Madagascar

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 26, 2020 1:55


Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO huko nchini Madagascar linatekeleza mradi wa kuhakikisha kuwa wakazi wanaoishi karibu na eneo la hifadhi la Makira wanakuwa na uhakika wa kupata mlo bora bila kusambaratisha eneo hilo la hifadhi. 

Habari za UN
Mradi wa uvuvi na ufugaji ni mkombozi kwa jamii Nigeria

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 6, 2020 2:08


Mradi wa FISH4ACP ambao una lengo la kuimarisha uvuvi na ufugaji samaki barani Afrika, Karibea na Pasifiki ukifadhiliwa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, umesaidia kuinua uchumi kama anavyoeleza mmoja wa wanufaika nchini Nigeria Bi Yahya Olunbumi.

Habari za UN
Mwanahabari ajikwamua kupitia ufugaji wa sungura Uganda

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 2, 2020 3:54


Kupiga vita umaskini ni jukumu la kila mtu kujipigania kwa kusaka vyanzo mbadala vya mapato. Vijana wengi nwanakabiliwa na changamoto ya pato duni na mara nyingine hata kufikia kuandamana wakitaka nyongeza ya mishahara kwa wale waliobahatika kupata kazi.

uganda kupiga ufugaji
AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Kutunza kumbu kumbu kwa ufugaji wa kuku

memory ufugaji
AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa Samaki

samaki ufugaji
AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji unaweza kuwa chanzo cha mapato

kuku ufugaji
AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ufugaji wa ngombe wa maziwa

ufugaji
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 13, 2016 9:18


Ufugaji wa samaki wa kisasakwenye visima au mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani na Ufugaj huu wa samaki ni sawa kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Katika makala haya ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa juma hili itangazia kwa ujumla kwa juu ya ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki wa kisasa 

dunia katika yako fahamu samaki mazingira kesho ufugaji
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Sehemu ya Pili:Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 13, 2016 9:59


Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani kote inchi kama .Niwazi tumeona baadhi ya inchi nyingi zikizidi kuzalisha nafasi nyingi za ajira kwa shughuli hizi pamoja na kukuza kipato cha mhusika mmoja mmoja, jamii flani na taifa kwa ujumla. Katika kuiangalia fursa hii katika sehemu yetu ya pili na ya mwisho ya makala yetu ya Mazingira Leo Dunia Yako Kesho kwa juma hili tutaangalia juu ya mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki wa kisasa 

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho - Fahamu FaidaUfugaji wa nyuki wa kisasa kwa Mazingira

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Sep 1, 2016 10:11


Ufugaji wa nyuki wa kisasa unoazingatia matumizi ya vifaa bora ambao huzalisha asali bora lakini pia husaidia katika utunzaji wa Mazingira lakini pia licha ya kusaidia kutunza mazingira, nyuki ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai vyote, kwani husaidia katika uchavushaji wa mimea.Makala ya Mazingira Leo,Dunia yako Kesho inagazia juu ya faida za Ufugaji wa nyuki wa kisasa katika utunzaji wa Mazingira

dunia makala yako fahamu mazingira kesho ufugaji