Podcasts about jamii

  • 60PODCASTS
  • 309EPISODES
  • 18mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 15, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about jamii

Latest podcast episodes about jamii

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Uchakataji wa plastiki katika kuhifadhi mazingira ya bahari na kupata mapato

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later May 15, 2025 9:49


Jamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo  mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.

SBS Swahili - SBS Swahili
Nafasi za baraza la waziri za tangazwa: Nani yuko ndani, nani yuko nje?

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 13, 2025 9:13


Tanya Plibersek ame shushwa cheo nakupewa wizara ya Huduma za Jamii, wakati Anthony Albanese anatangaza baraza lake la mawaziri, atakao fanya kazi nao katika muhula wake wa pili serikalini.

Nyumba ya Sanaa
Msanii sweet Brown wa Beni DRC na mziki wa jamii

Nyumba ya Sanaa

Play Episode Listen Later May 10, 2025 20:08


Sanaa ya muziki ni dawa inayofariji na kusaidia kutuma ujumbe wa amani kwa jamii amesema msanii wa miondoko mchanganyiko Gloire Tsongo almaarufu sweet Brown fresh Leader mjini Beni katika mkowa wa Kivu kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari wa RFI Kiswahili Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo hilo mwezi february mwaka huu

Habari za UN
08 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2025 11:12


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuatia kuendelea kwa mvutano wa majirani, India na Pakistani, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Philemon Yang, ametoa wito wa kuzitaka nchi hizo mbili kuchukua tahadhari na kuepuka hatua zinazoweza kuongeza mzozo. Balozi Yang anasisitiza mazungumzo ya amani na kufuata sheria za kimataifa ndiyo njia pekee ya kusuluhisha migogoro.”Na katika jifunze Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
Kutimiza azimio la watu wa jamii za asili ni jukumu la mataifa yote duniani - Adam Ole Mwarabu

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 8, 2025 6:48


Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.

Habari za UN
Maoni kutoka washiriki kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa jamii za asili UNPFII

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 30, 2025 3:24


Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.

Habari za UN
Jamii inapaswa kusikiliza na kujifunza kutoka kwa vijana

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 16, 2025 3:42


Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) linafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo limeanza tarehe 15 Aprili na linatarajiwa kukamilika tarehe 17 Aprili 2025. Vijana kutoka nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa masuala ya maendeleo na Uchumi wanakuja pamoja kujadili changamoto mbalimbali na namna bora ya kupatia ufumbuzi katika kuubadilisha ulimwengu kuwa mahali penye usawa zaidi na endelevu chini ya mwongozo wa Ajenda ya mwaka 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).  Miongoni mwa wanaohudhuria jukwaa hilo ni Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amefanyiwa mahojiano na Leah Mushi na hapa anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano huo.

Radio Maria Tanzania
Je, kwanini vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaendela kushamiri katika Jamii?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 14, 2025 21:14


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Jinsia na maendele0, leo tunazungumzia mada juu ya kwanini vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vinaendelea katika Jamii licha ya elimu inayoendela kutolewa? L'articolo Je, kwanini vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaendela kushamiri katika Jamii? proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Vijana tuna jukumu muhimu katika maendeleo ya jamii zetu tuchangamkie fursa: Winfred Njiru

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 3:26


Umoja wa Mataifa unaendelea kuchagiza vijana kujitokeza na kushiriki katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu katika jamii zao na ndio maana wiki iliyopita majadiliano ya viongozi wastaafu kuhusu maendeleo endelevu ya Club De Madrid yaliyofanyika Nairobi Kenya yalitoa fursa kwa vijana kupaza sauti zao kuhusu jinsi wataavyochangia kufanikisha malengo hayo.  Winfred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor alizungumza na Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi na kumueleza matahali Kenya vijana wanapaswa kufanya nini ili kuchangia katika maendeleo.

SBS Swahili - SBS Swahili
Sean MMG "mitandao yaki jamii imefanya iwe rahisi kwa vijana kama sisi kutokea katika muziki"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 10, 2025 7:38


Wasanii maarufu kutoka Kenya; Sean MMG, Ssaru na Tipsy Gee walitembelea studio yet hivi karibuni wakati wa ziara yao ya Australia.

Radio Maria Tanzania
Hizo ndizo sifa za Mwanamke katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 57:22


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya Sifa ya kumi na tano zaWanawake. L'articolo Hizo ndizo sifa za Mwanamke katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Ukiwekeza kiuchumi kwa mwanamke basi umewekeza katika jamii: Janet Mbene mshiriki CSW69

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 21, 2025 5:42


Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unakunja jamvi leo hapa makao makuu ya Umoja wa  Mataifa New York Marekani baada ya mjadala wa wiki mbili kutathimini hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia miaka 30 baada ya azimio la Beijing la usawa wa kijinsia nah atua za utekelezaji. Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wakishiri wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania

Habari za UN
20 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 20, 2025 12:27


Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani ni Finland na ya mwisho kabisa ni Afghanistani. Katika 10 bora zenye furaha hakuna hata moja ya Afrika, ilihali kwenye 10 za mwisho nchi za Afrika ni 7 ambazo ni Lesotho, Comoro, Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Malawi na Sierra Leone.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukikaribia ukingoni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tumemuuliza mshiriki Wakili Rosemary Mwaipopo kutoka Tanzania mkutano umekidhi kiu yake ya kusongesha usawa wa kijinsia?Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Mabadiliko chanya katika jamii yanakuja kwa kueleweshana - Dkt. Gwajima

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2025 2:05


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima,  ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Anold Kayanda wa Idhaa hii amekutana naye na miongoni mwa mambo mengi amemuuliza ni kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto nyingi zinazoukabili usawa wa kijinsia nchini humo?

Habari za UN
17 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 17, 2025 11:28


Hii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa      mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69. Ili kufanikisha lengo la usawa wa kijinsia Umoja wa Mataifa unasisitiza ushiriki wa wanaume katika mchakato hasa kwa kuzingatia kuwa mfumo dume miaka nenda miaka rudi umekuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo, Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wanaume wanaoshiriki mkutano huo kusikia maoni yake.Na katika mashinani baadhi ya washiriki wa mkutano wa CSW69 wakizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo, wametoa wito wa mshikamano na msichana na mwanamke yeyote anayepitia changamoto kote duniani hususani wale wanaorejea shuleni baada ya kusitisha masomo kutokana na ujauzito kabla ya wakati. Mshiriki wa kwanza ni Nasra Kibukila anayewakilisha Mtandao wa Elimu Tanzania, TEN/Met.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  

Siha Njema
Kukata kiu ya jamii zinazoishi mpaka wa Kenya na Somalia ,waathiriwa wa mgogoro

Siha Njema

Play Episode Listen Later Feb 25, 2025 8:57


Mamia ya wakaazi wa kaskazini  mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na  upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali  hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee  of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa  kilomita chache na msitu wa Boni  ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi  na kujificha .

VOA Express - Voice of America
Mratibu wa mkoa katika Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania anaelezea mtazamo wake na changamoto wanazopitia wanandoa katika jamii zetu. - Februari 21, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 21, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Radio Maria Tanzania
Fahamu madhara yanayo tokea ukiukwaji wa kutenda Haki katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 53:15


Karibu ungana nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Maadili yetu, Wawezeshaji ni Mafrateri mbalimbali kutoka Jimbo kuu Katoliki Tabora, wakituongoza kujifunza juu ya mada Matokeo ya kukiuka misingi ya Haki za Binadamu.    L'articolo Fahamu madhara yanayo tokea ukiukwaji wa kutenda Haki katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu faida za kuwahudumia Watu wengine wanaokuzunguka katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 18, 2025 55:14


Ungana nami John Samky, katika Kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu  Wawezeshaji ni Wakufunzi kutoka Familia bora katika Nyumba Aminifu, wakiendelea kutufundisha Umuhimu wakuwahubiria Majirani Habari Njema. L'articolo Je, wafahamu faida za kuwahudumia Watu wengine wanaokuzunguka katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 14, 2025 4:58


Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii

VOA Express - Voice of America
Waandishi wa habari wanaelezea mtazamo wao iwapo redio bado ina mchango mkubwa kwa jamii katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani. - Februari 13, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 13, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

katika siku habari jamii redio mtazamo maadhimisho
VOA Express - Voice of America
Mwanaharakati wa ukeketaji Tanzania anasema kuna mafanikio makubwa katika utoaji elimu kwa jamii ili kuzuia ukeketaji nchini humo. - Februari 10, 2025

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Feb 10, 2025 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
Umeme wa uhakika wanufaisha wanafunzi na jamii nchini Senegal

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 31, 2025 3:17


Senegal, taifa lenye watu zaidi ya milioni 18.5 liko kwenye mwelekeo wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme. Benki ya Dunia inasema kiwango cha kupata umeme kwenye taifa hilo sasa ni asilimia 84. Wakati huu ambapo asilimia zaidi ya 30 ya jamii za vijijini hazina huduma hiyo, serikali kwa kushirikiana na wadau kama vile Benki ya Dunia na sekta binafsi imechukua hatua na mabadiliko yameanza kuonekana. Je ni yapi? Assumpta Massoi anaelezea kwenye makala hii.

Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu Padre anaruhusiwa kufanyabiashara au kuajiriwa katika taasisi zingine katika Jamii?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Jan 22, 2025 29:23


Karibu katika Kipindi cha Maswali ya Imani ukiwa nami Frateri Kelvin Paschal Mwalabu, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Katoliki Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Je, Padre anaruhusiwa kuajiriwa na kufanya Biashara? L'articolo Je, wafahamu Padre anaruhusiwa kufanyabiashara au kuajiriwa katika taasisi zingine katika Jamii? proviene da Radio Maria.

Habari za UN
UNICEF Burundi: Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 8, 2025 3:29


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa kituo cha afya kiko karibu na sisi kwa hiyo si lazima tena kulipa nauli kwa ajili ya mashahidi. Sasa ni rahisi kwetu kusajili watoto wetu baada tu ya kuzaliwa. Hata mume wangu hajui kama niko naandikisha hapa wakati huu. Anadhani nitapata tu chanjo ya mtoto lakini nitakapomuonesha cheti cha kuzaliwa cha mtoto wetu, atafurahi sana. Hatalazimika tena kwenye ofisi za serikali na kulipa faranga za Burundi 10,000 kwa ajili ya usafiri. Ni faida kwetu.” UNICEF pia inasaidia katika kuandikisha watoto ambao walichelewa kusajiliwa katika umri mdogo na hiyo imesaidia sana watoto walio katika mazingira magumu kupata huduma za msingi za kijamii ambazo hapo awali walikuwa nazikosa kwa kuwa hawana utambulisho wowote unaotambuliwa kiserikali. Katika mkoa wa Bugabira jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, tunakutana na Jean Baptiste Mutaniyonka baba wa mtoto mwanafunzi Karerwa Olivier anaeleza changamoto walizokuwa wanakumbana nazo hapo awali kabla ya huduma ya usajili kuletwa karibu. “Mara ya kwanza nilipoenda kwenye ofisi za mkoa kusajili ilikuwa imefungwa kwa sababu ya sikukuu. Mara ya pili, mashahidi walitutaka kuwapatia faranga za Burundi elfu kumi nila mmoja. Sikuwa na fedha hiyo kwa hiyo ilibidi tuahirishe hiyo miadi ili tutafute pesa.” Mzazi huyu ili kuonesha namna cheti cha kuzaliwa kilivyo na umuhimu mkubwa katika maisha ya mtoto nchini Burundi anasema, “bila cheti cha kuzaliwa mtoto hana haki ya kupata kupata huduma ya bure katika hospitali. Tulikuwa tunaondoka bila bila kupata matibabu. Na katika hali kama hiyo tuligeukia katika tiba za asili au katika maduka ya dawa. Ilikuwa hivyo hivyo katika shule. Watoto wangu walikuwa wanarejeshwa nyumbani kwa kukosa cheti cha kuzaliwa.” Huyo ni Olivier Karerwa mwenyewe, mtoto wa Jean Mutaniyonka. Olivier amesajiliwa kupitia mradi huu wa UNICEF na anasema anataka kuwa mwalimu atakapohitimu masomo yake. Anne Rwasa ni bibi anazungumzia ilivyo rahisi sasa kumuhudumia mjukuu wake akisema, lakini leo mtoto  awe na homa au kuumwa tumbo tunakimbia katika kituo cha afya ambako anapata huduma ya bure ya afya.” Mradi huu wa UNICEF Burundi wa kuunganisha taarifa za watoto za serikali ili ziweze kusomeka pia katika taasisi nyingine kama vile vituo vya afya umepata  pia usaidizi kutoka kwa kamati ya UNICEF ya Uingereza.  

Habari za UN
Papua New Guinea: Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake zapatiwa  ‘muarobaini'

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 3, 2025 2:08


Kila mwaka, mamia ya wanawake nchini Papua New Guinea, taifa la visiwani katika bahari ya Pasifiki, hushutumiwa kimakosa kuwa ni wachawi. Matokeo yake hukumbwa na ukatili miongoni mwa wanajamii. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP nchini humo, limechukua hatua.Kiongozi mkubwa wa Kijiji chetu alifariki dunia, na tulipoenda kwenye maziko, ambapo kila mtu alisema sisi ni wachawi na tulikula moyo wake. Ni kauli ya Annabele, jina lake halisi limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake akielezea tuhuma zilizowakabili kwenye jamii yao ya jimbo la Enga nchini Papua New Guinea, hadi kushambuliwa kwa nondo za moto na nyumba zao kuteketezwa kwa moto. Video ya UNDP inamnukuu akisema kuwa walikuwa 9, ambapo wanne walifariki dunia na watano akiwemo Annabele, walinusurika, “kesho yake asubuhi Askofu na wenzake walifika, halikadhalika jeshi na polisi, na ndio walituokoa.” Askofu huyo Justine Soongie Dayosisi ya Wabag jimboni Enga anasema walipowachukua waliambiwa wahakikishe hawarudi kijijini, “sababu kubwa ya mtu kutuhumiwa ni jamii kukosa uelewa kuhusu chanzo cha kifo. Watu wengi hawafahamu kuwa mtu anaweza kufa kutokana na kiharusi. Watu wetu wa Enga watauliza ni nani amesababisha?” Annabelle baada ya kuokolewa alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ambayo hata hivyo bado ana kovu na maumivu. Kisha walipelekwa nyumba salama zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki kwa ufadhili wa UNDP, ambako waliishi kwa miezi takribani mitano wakipatiwa mavazi, malazi na chakula. Askofu Justine Soongie anasema,“baada ya miezi kadhaa hospitalini, tunarudi kwa familia na jamii na kuzungumza nao mara kadhaa. Tunawaelimisha kuwa ni kosa kumtuhumu mtu uchawi, kuna sheria, na hana pahala pengine pa kwenda, hivyo atarudi.” Jamii ilieleweshwa na Annabelle kwenye video anaonekana tayari yuko kijijini na sasa analima shamba na hata anasema hata mazao anayolima akivuna, anapika na wanajamii wanakula pamoja naye. 

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Dampo la Nkumba- Tishio kwa ziwa Victoria na maisha ya jamii za Uganda

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Dec 26, 2024 10:01


Makala haya yanazungumzia jinsi dampo la Taka la Nkumba nchini Uganda limekuwa tishio la kimazingira  kwa ziwa victoria ambalo ndilo chanzo kuu cha mto Nile.Baada ya dampo la Kiteezi jijini Uganda kuporomoka Agosti 9 mwaka wa 2024 na kuwauwa watu kadhaa,serikali nchini humo ilitoa amri taka zote kutoka Kampala ielekezwe Nkumba karibu na ziwa  ,hatua hiyo ikiongeza uchafuzi zaidi wa mazingira .

Radio Maria Tanzania
Fahamu umuhimu na furaha wa Mtoto anapozaliwa katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Dec 18, 2024 55:24


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Pro-Life, leo Studio niko na wawezeshaji kutoka Pro Life Tanzania, wakitufundisha muendelezo  juu Noeli na Thamani ya Uhai. L'articolo Fahamu umuhimu na furaha wa Mtoto anapozaliwa katika Jamii. proviene da Radio Maria.

VOA Express - Voice of America
Mtaalamu wa afya Theophil Wangata anaelezea namna jamii inavyopaswa kuzingatia vyakula wanavyokula kila siku hususan wakati wa sikukuu. - Desemba 16, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 16, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

VOA Express - Voice of America
Vijana takribani 30,000 katika Mkoa wa Tanga nchini Tanzania hawataki kutafuta kazi wala masomo, je hali hii inaashiria nini katika jamii? - Desemba 13, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 13, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

VOA Express - Voice of America
Vijana wa Afrika mashariki wanaeleza namna wanavyotumia rasilimali ya udongo katika kuleta maendeleo kwa jamii wanazoishi. - Desemba 05, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Dec 5, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
Kiswahili kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali duniani

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 2, 2024 10:14


Kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali ni moja ya masuala yanayopigiwa chepuo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa dhamira ya kuhakikisha utambulisho wa jamii unarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Mkoa wa Tanga uliopo Kaskazini mwa Tanzania umekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha hilo kupitia vifaa mbalimbali vya kitamaduni ambavyo vimekuwa vikitumika enzi na enzi katika jamii na sio tu kukuza lugha ya Kiswahili bali kuhakikisha inaendelea kwa vizazi na vizazi . Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wanaohakikisha utamaduni huo haupotei, ungana nao katika makala hii kupata undani.

VOA Express - Voice of America
Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na unyanyasaji mwingine nchini Tanzania unaongezeka, kulingana na taasisi ya Macho kwa Jamii. - Novemba 19, 2024

VOA Express - Voice of America

Play Episode Listen Later Nov 19, 2024 29:59


VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.

Habari za UN
Esneda kutoka jamii ya Yukpa asema haogopi vitisho kutetea eneo la jamii yao ya asili nchini Colombia

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 15, 2024 3:39


Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao. Esneda Saveedra, Kiongozi wa jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia akiwa anazungumza akiketi ndani ya msitu na kando ya mto Maracas., anasema hana hofu ya kutetea ardhi hii.Ardhi anayozungumzia ni eneo hilo la mto Maracas anayotetea dhidi ya vitisho kutoka kwa waharibifu wa mazingira kufuatia yale yaliyojadiliwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, COP16 uliomalizika Ijumaa iliyopita huko mjini Cali nchini Colombia."Sina hofu ya kutetea ardhi hii. Yale niliyopitia kama mtoto, changamoto zote hizo, yalinipa nguvu, yalinipa ujasiri, na yakaondoa hofu yangu."Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatupatia taswira ya juu ya eneo la makazi ya jamii ya Yukpa, msitu mnene na kisha kwenye mto Maracas, shughuli zinaendelea, wengine wakiogelea, wengine wakivua samaki, mama mmoja akisafisha kuku aliyemaliza kumchuna.Esneda anaeleza umuhimu wa mto huu kwa maisha ya jamii yake na anaendelea kujitahidi ili kulinda mazingira hayo."Huu ni mto Maracas, ambapo watu wetu, mababu zangu, walivua samaki kwa ajili ya chakula kila siku. Waliharibu mazingira kwa kukata miti yote, na matokeo yake, mto ulianza kukauka. Leo, mto Maracas hauna mtiririko wa maji kama ulivyokuwa zaidi ya miaka 20 iliyopita."Katika juhudi zake, Esneda ameanzisha mazungumzo na maafisa wa serikali katika manispaa ya Becerril, akijaribu kuleta mabadiliko na uelewa juu ya umuhimu wa kuhifadhi ardhi na utamaduni wa watu wa Yukpa."Kumekuwa na uratibu, kazi ya pamoja, na jambo muhimu zaidi kwangu kama mwanamke wa Yukpa imekuwa kuleta ufahamu kuhusu watu wa Yukpa na ardhi yetu. Mabadiliko ya tabianchi yametufikisha kwenye tatizo kubwa zaidi, ambalo ni upotevu wa mazao na ukosefu wa chakula. Leo hatuna chakula cha kutosha katika jamii zetu. Tunaendelea kupambana, lakini pia tuko hapa kusaidia dunia nzima kuendelea kupambana na kulinda mazingira, ardhi, na hewa. Na kusema: 'Tupo hapa kuchangia kwa ajili ya ubinadamu, kwa ulimwengu mzima.'"Harakati zake zimekumbwa na vitisho.“Walinitishia hapa kwa kuzungumza, na kwa kusema ukweli. Mama yangu alikuwa kiongozi thabiti—na bado ni kiongozi thabiti. Na nilipokuwa mdogo, nilimsindikiza kwenye michakato yake yote ya harakati, mipango na uongozi. Niliendeleza njia hiyo ya uongozi kwa sababu niliona ni muhimu. Ilikuwa ni wajibu wangu. Nilijiambia, ‘mimi ni mwanamke ambaye nimezaliwa kutetea eneo hili.”Kwa Esneda, kulinda ardhi ya Yukpa ni zaidi ya wajibu; ni dhamira ya kuhifadhi urithi wa mababu zake. Katika changamoto za kila siku, Esneda anabaki imara kwa matumaini kuwa jamii yake na mchango wao katika kuhifadhi mazingira utatambuliwa ulimwenguni.

Radio Maria Tanzania
Zifahamu tabia mbaya na madhara yake katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Nov 7, 2024 52:48


Karibu uungane nami John Samky katika kipindi cha Uraibu, Mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, leo anatufundisha juu ya madhara ya tabia mbaya katika jamii. L'articolo Zifahamu tabia mbaya na madhara yake katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Jamii Pwani ya Kenya wapinga mradi wa nyuklia kutokana na athari kwa mazingira

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 29, 2024 9:17


kenya jamii mazingira
Radio Maria Tanzania
Ni, kwa namna gani Familia husaidia kuimarisha Usawa wa Kijinsia katika jamii?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Oct 21, 2024 27:21


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo leo  tupo na Ndugu Anectus Asingizibwe, Mwenyekiti wa Kampeni kupinga ukatili shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii (SMAUJATA) Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa  Pwani akituongoza kujifunza mchango wa Mifumo ya Familia katika kuimarisha usawa wa Kijinsia. L'articolo Ni, kwa namna gani Familia husaidia kuimarisha Usawa wa Kijinsia katika jamii? proviene da Radio Maria.

Habari za UN
16 OKTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 9:54


Hii leo jaridani tunaangazi siku ya chakula duniani ikitupeleka jijini Roma Italia kufuatilia maadhimisho yake. Pia tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanhaha kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Makala tunakwengda nchini DRC na mashinani Sierra Leone, kulikoni?Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto ikiwemo Candy mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino. Baba yake alifika kwenye kambi hiyo na anatusimulia kupitia video ya UNICEF Kenya.Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP la kusaidia wanawake wakimbizi kuondokana na ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika.Mashinani tunamsikia Mpishi Mkuu Fatmata Binta kutoka kabila la wafugaji wanaohamahama la fulani nchini Sierra Leone anaeleza jinsi ushirikiano wake na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, kuhusu ni kwa jinsi gani FAO umemwezesha kusambaza manufaa ya fonio, nafaka asili ya Afrika , inayoweza kuwa suluhisho la changamoto za ukosefu wa chakula na tabianchi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Habari za UN
Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 2:01


Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto.  Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa  mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo  jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho  ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza  niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia changamoto zinazowazuia watoto wenye ulemavu na familia zao kupokea msaada muhimu wanaohitaji wakati wa majanga na dharura.Akiwa mwingi wa furaha, Eric anasema, “imechukua muda wa miaka sita ambapo nimekuwa nikizunguka tu kuhusu miwani. Mahali nilipoenda hapo awali, niliambiwa kulipia shilingi elfu arobaini ($313) lakini sikuweza kupata hiyo pesa. Nimefurahi kwamba leo nimepewa bila gharama yoyote.”Baada ya uchunguzi na mawaidha mbalimbali katika hii kambi, Eric na mwanaye Candy hawakuweza kuificha furaha yao kwa kupata suluhisho la tatizo ambalo limewaathiri kwa miaka sita.Hatimaye, Candy alipewa miwani yake maalum ili kumsaidia kuona vizuri zaidi.“Nimefurahia sana sina jukumu tena la  kutafuta pesa za kununua miwani. Na nimefurahi pia mtoto wangu atakuwa na wakati rahisi. Amefurahia kabisa na anaipenda sana miwani yake. Amesema anajihisi vizuri. Kwa sababu ana miwani, natumaini anaweza kucheza bila shida yoyote, bila kujali kuhusu jua kwa sababu miwani inamkinga.”

Radio Maria Tanzania
Je, ni sifa gani za mtoto mwenye afya ya akili?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Oct 11, 2024 42:14


Ungana nami Judith Mpalanzi, katika kipindi cha Malezi na makuzi ya Vijana, Mwezeshaji ni Sister Theresia Karugaba kutoka Ofisi za haki za Binadamu kitengo cha maendeleo ya Jamii, Jimbo Katoliki Zanzibar, akiendelea kutuelimisha juu ya afya ya akili kwa Watoto. L'articolo Je, ni sifa gani za mtoto mwenye afya ya akili? proviene da Radio Maria.

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
DRC:Jamii ya mbilikimo wakemea uharibifu wa misitu unaofanywa na makundi ya waasi

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Play Episode Listen Later Oct 9, 2024 10:08


Habari za UN
Baada ya kimbunga Beryl Wasamaria na IOM waishika mkono jamii ya Carriacou

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 16, 2024 1:45


Kimbunga Beryl, kilichopiga tarehe 1 Julai 2024, kimewaacha wakazi wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada, na athari kubwa . Kufuatia changamoto zinazowakabili wasamaria kutoka maeneo mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) wamewasaidia kurejesha matumaini kama anavyosimulia Anthony St. Hilaire manusura wa kimbunga hicho. Anthony aliyekumbwa na hofu kubwa wakati mawimbi makali ya bahari na upepo wa kimbunga Beryl vilipoanza kusambaratisha nyumba yake anasema hakika hali ilikuwa si hali, kwani akijua fika kulikuwa na hatari ya kupoteza maisha ."Awali, upepo ulianza kuvuma kwa nguvu, tukafunga kila kitu. Kisha kina cha bahari kilianza kupandana mawimbi kugonga madirisha na mlango. Ilibidi tufungue mlango ili kupunguza kasi ya upepo na maji."Anthony anaendelea kueleza jinsi alivyorejea nyumbani baada ya kimbunga, na akakuta kila kitu kimekwenda na maji"Haikuwa rahisi. Rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuwa kila kitu kimesafishwa. Nilipofika, karibu nilie. Akaniambia usijali, haya ni mambo ya kidunia. Tumebakiwa na jambo kubwa zaidi ambalo ni uhai."Pamoja na maafa hayo na athari zake IOM ikishirikiana na wadau wengine wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha familia zenye uhitaji mkubwa hazikati tamaa , zinakuwa na matumaini na kuapata misaada haraka iwezekanavyo.

Jioni - Voice of America
Papa Francis ametembelea Papua New Guinea na kutoa wito kuhusu rasilimali za asili zitumike kunufaisha jamii nzima nchini humo. - Septemba 07, 2024

Jioni - Voice of America

Play Episode Listen Later Sep 7, 2024 29:59


Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

Build Better Brands
Empowering Black Businesses: Jamii's Community-Driven Success Story

Build Better Brands

Play Episode Listen Later Aug 1, 2024 34:18


Danielle spoke with Courtney Ismain, Co-Founder of Jamii, which is a community and home for black British creators and makers. Jamii is a discovery platform for British brands on the up. A discount card that is a community giving users up to 40% off. They want to introduce you to the small businesses who know what you need.KEY TAKEAWAYSCourtney shares how Jamii came about from the first wave of the Black Lives Matter movement and how off the back of that, there was a growing interest in where people could find black-owned businesses. The Jamii card, which is a discount card, incentivises people to go off the beaten track and discover new black-owned businesses they might not have heard of before.Jamii is impact-driven and community is a really important part of what they do. Courtney explains how they always try to be easily accessible to make people feel involved and be action-led. Courtney explains how Clear Channel approached Jamii to collaborate on their Compass initiative, aimed at supporting black-owned businesses. Together, they launched a competition that attracted hundreds of applicants, with ten winners receiving two weeks of free high-street advertising.BEST MOMENTS‘Customers, businesses and organisations alike, are able to kind of identify what we're about and align themselves with our mission and the opportunities present themselves because I guess these people who agree with our mission, they make themselves known and then we're able to work together, if that makes sense'.‘The way we work with businesses, we kind of have a package called partnership. These are all the businesses that are our partners. We list their products and we send them regular opportunities'.‘We decided that we want to refresh Jammie membership a little bit so something that we did in February was we hosted a focus group with some of our ride or die members. Honestly speaking, we're not trying to hide anything or make maybe membership look better than it is'.‘We reached out to Airbnb. We asked them for a donation for a grant fund so they gave us 20,000 pounds and we were able to distribute that to four businesses, 5000 pounds each'.CONNECT WITH THE GUESTJamii website: https://lovejamii.com/Search ‘ukjamii' on social mediaABOUT THE HOST - DANIELLE CLARKEDanielle Clarke is a Brand Strategist and spends her time consulting and working with health and wellness business owners to help them attract and retain their ideal customers.GRAB YOU 3 ACTIONABLE STEPS FOR BRAND GROWTH: https://danielle-clarke.ck.page/b1043e5d05WORK WITH DANIELLE TO BUILD THE BRAND STRATEGIES YOUR BUSINESS NEEDS TO GROW: https://calendly.com/d/48p-6ck-vy4CONNECT WITH DANIELLE ON LINKEDIN: https://www.linkedin.com/in/danielle-clarke-brand-strategy-consultant/SUPPORT THE SHOW: https://www.buymeacoffee.com/danielleclarke This show was brought to you by: The Media Insiders Hosted on Acast. See acast.com/privacy for more information.

My Daily Business Coach Podcast
Supporting independent Black-owned businesses with Courtney Ismain of Jamii

My Daily Business Coach Podcast

Play Episode Listen Later Jun 12, 2024 48:35


In this episode, Fiona chats with Courtney, co-founder of Jamii, a platform supporting black-owned businesses. They talked about the challenges faced and the community-centric mission that drives their business forward. Tune in!You'll Learn How To:Building partnerships with major organisations The role of community in business growth Effective marketing strategiesThe impact of media coveragePersonal development and its influence on business confidenceAdvice for entrepreneurs facing lack of representation in their industryThe importance of maintaining authenticity and passion in businessImportance of Community Courtney's personal background and operational role in the businessChallenges and stereotypes faced by black-owned businessesPartnership and support from larger organisationsThe impact of the Black Lives Matter movement on businessMasterclasses and initiatives to support black entrepreneursFuture aspirations for inclusivity and broad support in business practicesGet started on a more successful and sustainable small business with our range of free tools at mydailybusiness.com/freestuffConnect and get in touch with My Daily BusinessMy Daily Business ShopMy Daily Business Free Weekly PlannerMy Daily Business Waitlist

SBS Swahili - SBS Swahili
Bajeti yashughulikia maswala muhimu kwa jumuiya zatamaduni nyingi ila maelezo ya ziada yana hitajika

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later May 17, 2024 11:00


Jamii za wahamiaji na wakimbizi zimekaribisha mipango katika bajeti ya shirikisho ila, wame sema maelezo zaidi yanahitajika kuhusu mikakati iliyo lengwa kwa wanachama wa jumuiya.

SBS Swahili - SBS Swahili
Viongozi wadini, Waziri Mkuu waomba uwepo wa heshima na maelewano katika jamii

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Apr 26, 2024 10:32


Viongozi kutoka jumuiya za wayahudi, waislamu na wakristo mjini Sydney wame kemea kwa pamoja vurugu na maneno yakugawanya ambayo yame ibuka kufuatia matukio mawili ya shambulizi ya visu mjini Sydney.

SBS Swahili - SBS Swahili
Delphine "Jamii imepokea kazi zetu vizuri ila, tunahitaji waje tushirikiane nao zaidi"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Sep 3, 2023 7:27


Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika viwanja kwa Sydney Olympic Park kwa tamasha ya Africultures 2 Septemba 2023.

SBS Swahili - SBS Swahili
Justin "Covid ilisaidia watu wengi kujitambulisha katika jamii yawakenya Victoria"

SBS Swahili - SBS Swahili

Play Episode Listen Later Aug 17, 2023 11:32


Ni kawaida kwa wahamiaji na watu walio wasili Australia kama wakimbizi, kujiunga na vikundi vya jumuiya za asili yao.

Habari za UN
Watu wa jamii ya asili ni muarobaini wa majanga yanayokumba dunia-Türk

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jul 17, 2023 0:02


Watu wa jamii ya asili wanaweza kutuongoza katika harakati za kukabiliana na misukosuko na majanga yanayokabili zama zetu hivi sasa, amesema hii leo  huko mjini Geneva, Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk akihutubia mkutano wa 16 wa wataalamu wa haki za watu wa jamii ya asili. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Bwana Türk amesema uwezo wao katika kunusuru dunia hivi sasa ni dhahiri shahiri kwa kuzingatia ziara yake ya mapema mwaka huu huko Kenya, Colombia, Ecuador na Venezuela ambako watu wa jamii ya asili walimwelezea sio tu changamoto wanazokumbana nazo kama vile kupokonywa ardhi za asili za mababu zao bali pia harakati zao wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mathalani uchimbaji madini unavyoharibu mazingira yao ya asili na kukiuka haki zao na maeneo yao kuvamiwa kijeshi, akisema vitendo hivyo lazima vikome kwa kuwa kusongesha haki za watu wa jamii ya asili na kulinda na kupaza sauti zao ni jukumu muhimu la ofisi yake ya kutetea haki.Ametolea mfano jinsi watoto wa jamii ya asili ya Huitoto nchini Colombia ambao mama yao alikufa kwenye ajali ya ndege mwezi uliopita, lakini kwa muongozo waliopata wakati wa makuzi kutoka kwa mama na bibi yao ya jinsi ya kuishi kwenye mazingira na mimea, wanyama na misitu ya mvua, wameweza kuishi bila kutetereka.Bwana Turk amesema ni wazi kuwa simulizi hiyo ya Watoto inadhihirisha kuwa ufahamu wa mababu, hasa wa jamii ya asili una mafunzo mengi kwa dunia ya sasa hasa wakati huu inapozidi kukabiliwa na misukosuko ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi.Ametanabaisha kuwa ajabu ni kwamba wanawake wa jamii ya asili ambao ndio wana uhusiano mahsusi na mazingira huwa wa kwanza kuenguliwa pindi miradi mikubwa inapoanzishwa kwenye jamii zao.Hivyo Kamishna Mkuu huyo wa Haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa kujumuisha sauti zao katika harakati za kitaifa, kikanda na kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili hatimaye hoja ya hakuna chochote kuhusu sisi bila sisi iweze kuwa ya uhalisia.Takwimu za  Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa duniani kote kunakadiriwa kuweko kwa watu milioni 476 wa  jamii ya asili.Idadi hiyo ni sawa na asilimia 6.2 ya watu wote duniani na wanakabiliwa na umaskini, ubaguzi, kutengwa na kupokonywa mali zao. Kutokana na mazingira hayo, shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO linasema watu wa jamii ya asili ni asilimia 18.2 ya watu hohehahe duniani.