POPULARITY
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa ujumbe mzito wa Mwaka Mpya kwa ulimwengu akisema ulimwengu uko katika njia panda, ukikabiliwa na machafuko, sintofahamu na migawanyiko mikubwa na hivyo kutoa wito kwa wanadamu kuinuka pamoja kwa ajili ya haki, ubinadamu na amani. Karibu Anold Kayanda kwa maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Katika ujumbe wake wa video uliosambazwa leo asubuhi saa za New York, Marekani, kwa ajili ya mwaka mpya wa 2026, Katibu Mkuu wa Umoja wa Maraifa anauanza ujumbe wake kwa kusema, “tunapoingia mwaka mpya, dunia iko njia panda.” Amesema dunia inakumbwa na vurugu zinazoendelea, athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukiukwaji wa kimfumo wa sheria za kimataifa hali ambayo, kwa mujibu wake, inatishia misingi inayounganisha binadamu kama familia moja ya dunia.Guterres amesema watu kote ulimwenguni wanaendelea kujiuliza iwapo viongozi wao wanasikiliza kilio cha wananchi na kama wako tayari kuchukua hatua za dhati kukabiliana na changamoto hizi.Akigeukia takwimu, Katibu Mkuu ameeleza kuwa matumizi ya kijeshi duniani yamefikia dola trilioni 2.7, ongezeko la karibu asilimia kumi kiwango ambacho ni mara kumi na tatu zaidi ya misaada yote ya maendeleo, na kinacholingana na Pato la Bidhaa za ndani la Bara zima la Afrika.Amesema ongezeko hilo linatokea wakati dunia ikishuhudia mizozo mikubwa kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu Vita Vikuu Vya Pili Vya Dunia.Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu ametoa wito kwa dunia kutumia mwanzo wa mwaka mpya kuweka vipaumbele sahihi, akisisitiza kuwa ulimwengu salama hujengwa kwa kuwekeza zaidi katika kupambana na umaskini badala ya kuwekeza katika vita.Guterres amesisitiza kuwa dunia ina rasilimali za kutosha kuinua maisha ya watu, kuponya sayari na kujenga mustakabali wa amani na haki, endapo tu zitatumika ipasavyo.Kwa mwaka 2026, amewataka viongozi wa dunia kuwa makini zaidi na kufanya uamuzi unaoweka mbele maslahi ya watu na mazingira badala ya kuendeleza mateso.Aidha, amewahimiza raia wote duniani kushiriki kikamilifu katika kujenga dunia bora, akisema mustakabali wa ubinadamu unategemea ujasiri wa pamoja wa kuchukua hatua.Katika kuhitimisha ujumbe wake, Katibu Mkuu ametoa wito wa mshikamano kwa ajili ya haki, ubinadamu na amani duniani.
Mwaka 2025 umeelezwa kuwa mwaka wa kihistoria kwa sekta ya afya duniani. Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe uliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO,Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, wakati akitoa tathmini yake ya mwisho ya mwaka 2025. Taarifa zaidi na Sabrina Saidi. Karibu Sabrina..(TAARIFA YA SABRINA SAIDI) Asante Flora,Akizungumza kutokea makao makuu ya WHO mjini Geneva, Uswisi, Dkt. Tedros amesema mwaka 2025 umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na changamoto nzito kwa afya ya dunia, huku akisisitiza kwamba dunia bado inahitaji uwepo wa WHO. (Clip 1-Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Kweli mwaka 2025 umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa na changamoto nyingi kwa afya ya dunia na kwa WHO. Mafanikio makubwa zaidi yalikuwa kupitishwa kwa Mkataba wa WHO wa kukabiliana na milipuko ya magonjwa, ambao ni mfano wa nguvu ya ushirikiano wa kimataifa pale nchi zinapochagua kushirikiana badala ya kugawanyika. Pia, mwaka huu WHO imethibitisha nchi 13 kufanikiwa kutokomeza magonjwa, ikatoa miongozo kuhusu tiba mpya kama Lenacapavir kwa kinga dhidi ya VVU na matibabu ya GLP-1 kwa utipwatipwa,na ikachukua hatua dhidi ya majanga 48 katika nchi na maeneo 79, ikiwemo Gaza, Sudan na Ukraine.”Akizungumzia changamoto, Dkt. Tedros amesema kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa na bajeti kumeathiri sekta ya afya duniani, lakini ameeleza kuwa hali hiyo pia inaleta fursa mpya.(Clip 2- Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Lakini ndani ya changamoto hizi pia kuna fursa. Ni fursa kwa nchi kuondokana na utegemezi wa misaada na kujenga mifumo ya afya inayojitegemea, na ni fursa kwa WHO kuwa taasisi imara zaidi na inayojipanga kwa siku zijazo. Dunia bado inahitaji WHO, na WHO itaendelea kushikilia maono yake ya msingi kuhakikisha kiwango cha juu kabisa cha afya kinapatikana kwa wote, si kama upendeleo wa wachache, bali kama haki ya kila mtu.”Dkt. Tedros amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa WHO itaendelea kushirikiana na nchi wanachama ili kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo za afya duniani.
Karibu katika Makala haya ya mwisho kabisa katika mwaka 2025, ambapo kama ilivyo ada hukupa nafasi kutathmini ni mada gani iiokugusa katika kipindi cha mwaka 2025, lakini pia hutowa nafasi kwa waskilizaji ktoa salam za mwisho wa mwaka 2025
Matukio makubwa ya wiki hii ni pamoja na maadhimisho ya sikukuu ya krisimasi duniani mataifa kadhaa yakikabiliwa na shida za kiusalama, kasi ya kampeni za uchaguzi nchini Uganda, waasi wa AFC/M23 na mapigano yao mkowani Kivu kusini mashariki mwa DRC, kesi ya uhaini inayomkabili makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Macxhar kuahirishwa hadi January 06; mashambulizi ya vikosi vya Marekani dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Nigeria, na pia hali nchini Ukraine na Cambodia.
Makala hii ya habari rafiki rafiki ijumaa ya desemba 26 2025 ni siku ya mada huru; tunakupa fursa kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwako wiki hii. Unaweza pia kuzungumzia kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya redio juma hili. Nahodha wa Habari Rafiki Ruben Lukumbuka, moja kwa moja kutoka Studio maridai namba2.
Makala hii ya habari rafiki rafiki ijumaa ya desemba 26 2025 ni siku ya mada huru; tunakupa fursa kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwako wiki hii. Unaweza pia kuzungumzia kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya redio juma hili. Nahodha wa Habari Rafiki Ruben Lukumbuka, moja kwa moja kutoka Studio maridai namba2.
Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyabiashara.
Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyabiashara.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa ujumbe wa kulinda amani nchini DRC, wakati mapigano yakiongezeka mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mashambulizi mapya ya waasi wa M23. Uamuzi huu unakuja wakati mjadala ukiendelea kuhusu ufanisi wa MONUSCO nchini humo. Je, unaamini hatua hii itasaidia au ujumbe huo umepoteza uaminifu na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli? Je, umoja wa Mataifa unapaswa kufikiria upya mkakati wake wa kulinda amani nchini DRC?
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa ujumbe wa kulinda amani nchini DRC, wakati mapigano yakiongezeka mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mashambulizi mapya ya waasi wa M23. Uamuzi huu unakuja wakati mjadala ukiendelea kuhusu ufanisi wa MONUSCO nchini humo. Je, unaamini hatua hii itasaidia au ujumbe huo umepoteza uaminifu na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli? Je, umoja wa Mataifa unapaswa kufikiria upya mkakati wake wa kulinda amani nchini DRC?
Karibu katika Makala yetu ya leo Jumapili Desemba 21, wakati tukielekea kutamatisha mwaka 2025, ambapo nakukumbusha baadhi ya makala tulizokuwa nazo mwaka huu, utapata kuskiliza makala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini pia sehemu ya makala kuhusu mambo ambayo ni miiko kutoka makabila mbalimbali, na mwisho kabisa nitakuletea burudani ya Muziki kutoka kwake. Mimi ni A LI Bilali bienvenue ama Karibu
Katika Makala haya mtagazaji wako Ali Bilali anakukumbusha baadhi ya makala zilizoruka hewani katika mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya kwanza.
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya haki za binadamu na maandamano ya amani nchini Tanzania, siku ya kujitolea tukikuletea ujumbe wa mfanyakazi wa kujitolea, na elimu jumuishi kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini Ethiopia.Wakati Tanzania ikijiandaa kwa maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Desemba siku ya maadhimisho ya Uhuru, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imetoa tahadhari na wito kwa serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Seif Magango ni msemaji wa ofisi ya Haki za binadamu ametufafanulia kuhusu tamko lao.Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui “Kila Mchango Una Umuhimu.” Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026.Katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, jitihada za kuimarisha makuzi na elimu kwa watoto wenye ulemavu zinaendelea kuleta matumaini mapya, kupitia programu inayoungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, na Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF. Je nini kinafanyika?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui“Kila Mchango Una Umuhimu.” Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania Sabrina Saidi amezungumza na kijana ambaye anajitolea katika Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania YUNA Je kasema nini?.
Kwa taarifa zaidi tunakuelekeza katika tovuti ya sbs.com.au/swahili.
Mwaka wa masomo unapokamilika, maelfu ya wanafunzi wa kimataifa wanaandikishwa kwa kazi za likizo. Hata hivyo, iwapo mambo yataenda kombo, wataalam wanaonya kuwa wachache wanaelewa haki zao za kisheria au jinsi ya kupata mishahara ambayo haijalipwa.
Leo tumezingatia tuzo za CAF 2025, AS FAR yaibuka washindi wa kombe la Ligi ya Afrika ya kina dada, kuanza kwa michuano ya klabu bingwa Afrika kwa wanaume huku AS FAR ikinyakua taji la kina dada, matokeo ya mechi za kufuzu AFCON U17 ukanda wa Cecafa, Curacao yakuwa taifa dogo zaidi kuwahi kufuzu Kombe la Dunia huku Marekani ikizindua mfumo maalum wa kutoa visa kwa wanunuaji tiketi.
Kadri maelfu ya vijana wanaposherehekea kumaliza Mwaka wa 12, wanakumbushwa juu ya hatari zinazokuja na unywaji pombe, hasa nje ya nchi. Wazazi na marafiki wa waathiriwa wa sumu ya methanol, Bianca Jones na Holly Bowles, wamejiunga na juhudi mpya za usalama, wakiwatia moyo wasafiri vijana kuchukua maamuzi salama zaidi.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kajiado iliyoko Kusini na Kusini magharibi mwa jiji la Nairobi nchini Kenya kumulika upatikanaji wa huduma za choo na hasa choo safi na salama ambazo bado ni kizungumkuti kote dunianini.Katibu Mkuu wa Umoja wa, António Guterres,akizungumza na waandishi wa habari hii leo ametoa onyo kali COP30 huko Belém, Brazil, akisisitiza dharura ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Amesema “Jamii zilizo mstari wa mbele zinaangalia zikiesabu nyumba zao zilizozamishwa na mafuriko mavuno yaliyoshindikana, vyanzo vya maisha vilivyopotea na kuuliza kwa kiasi gani zaidi wateseke . Wamesikia visingizio vya kutosha, sasa wanatakahatua”.Leo ni Siku ya mtoto Duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Sikilizeni watoto, simameni kwa ajili ya haki za kila mtoto, kila siku.” Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo ya Hali ya Watoto Duniani 2025 sanjari na maadhimisho haya inaonya kwamba zaidi ya watoto milioni 417, sawa na mtoto 1 kati ya 5 katika nchi za kipato cha chini na cha kati, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu angalau katika maeneo mawili ya msingi ya maisha.Mkutano wa wanaharakati vijana wavumbuzi kutoka kila pembe ya dunia umeaanza leo mjini Geneva Uswisi ukibeba mafda kuu “Kutoka Hashtag hadi Hatua”, ukisherehekea vijana wanaobadilisha maisha ya jamii zao kupitia zana za kidijitali na majukwaa ya mtandaoni. Mwaka huu, washindi wa uvumbuzi huo wanatoka nchi mbalimbali, ikiwemo Côte d'Ivoire, India, Lebanon, Japan, na Brazil, wakitambuliwa kwa kazi zao zenye athari kubwa chanya. Waandaaji wa Jukwaa hilo amba oni Umoja wa Mataifa wanasema tukio hili lina lengo la kuhamasisha vijana wengi zaidi kubadilisha ushiriki wao wa mtandaoni kuwa hatua halisi zinazoboresha jamii, kuthibitisha kuwa uanaharakati wa kidijitali unaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Na katka kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MTAWALIA.”Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Nena nami Bwana, ikiwa ni mafundisho kutoka kwa Mababa wa Kiroho kwa namna ya kipekee wanaonene nasi siku hii ya leo ni Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Iringa, Askofu Christopher Ndizeye wa Jimbo Katoliki […] L'articolo Nena nami Bwana Dominika ya 29 ya mwaka C wa Kanisa. proviene da Radio Maria.
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku mpya ya Bwana, hakika kuimba ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli. L'articolo Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na sita} proviene da Radio Maria.
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku mpya ya Bwana, hakika ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli. L'articolo Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na saba} proviene da Radio Maria.
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku ya Bwana, hakika kuimba ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli. L'articolo Amka na Mama kipindi cha Kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na nane} proviene da Radio Maria.
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na tathmini ya timu za Afrika ambazo zimefuzu Kombe la Dunia 2026 na ni nani ambao wana nafasi ya kufuzu kuelekea raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu, FIFA yateua wajumbe kutoka CECAFA, Herita Ilunga ndiye mkurugenzi mpya wa FECOFA nchini DRC, kocha wa zamani wa Yanga Nassredine Nabi waachana na Kaizer Chiefs, nyota tajika wa tenisi duniani wabwagwa kwenye mashindano ya Wuhan Open, Rovapera kustaafu mchezo wa kuendesha magari
Hii leo jaridani tunaangazia tunzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer, juhudi za wapiga picha wanawake kwenye maeneo yenye mizozo katika kusongesha amani na usalama, na wafugaji Samburu nchini Kenya.Mwaka huu, Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer imekwenda kwa Olukemi Ibikunle, afisa wa magereza kutoka Nigeria anayehudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO. Tunzo hii inatambua mchango wake mkubwa katika kazi za haki na magereza kwenye operesheni za kulinda amani, pamoja na ujasiri wake wa kuvunja vizingiti vya kijinsia katika maeneo yanayoongozwa na wanaume.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuna maonesho ya picha 32 zinazoonesha harakati za wanawake kwenye maeneo yenye mizozo kusongesha amani na usalama, kwa mujibu wa azimio namba 1325 lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa miaka 25 iliyopita. Maonesho ya picha hizi zilizopigwa na wanawake yamepatiwa jina Kupitia Lensi Yake na yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau ili kudhihirisha ujasiri wa wanawake katikati ya mazingira hatarishi, wakihaha kuleta amani kwenye maeneo yao.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya wanatekeleza mradi unaowashirikisha wananchi wa Kauti ya Samburu katika kuhakika kuna upatikanaji wa chakula kwani eneo hilo linahali ya ukame ikiwa ni hatua mojawapo ya kutafsiri na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs huko mashinani. Tuungane na Sheilah Jepngetich anayetuletea tarifa hii iliyoandaliwa na UNICEF Kenya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Mwaka huu, Tunzo ya Umoja wa Mataifa ya “Muonesha njia” au kwa kiingereza Trailblazer imekwenda kwa Olukemi Ibikunle, afisa wa magereza kutoka Nigeria anayehudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO. Tunzo hii inatambua mchango wake mkubwa katika kazi za haki na magereza kwenye operesheni za kulinda amani, pamoja na ujasiri wake wa kuvunja vizingiti vya kijinsia katika maeneo yanayoongozwa na wanaume. Flora Nducha na taarifa zaidi
Makubaliano yaliyosimamiwa na mashirika ya kimataifa, likiwemo UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, halikadhalika Mpango wa afya wa Clinton (CHAI), Wits RHI na Maabara ya Dkt. Reddy, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa Lenacapavir kwa gharama nafuu.Dawa hii, inayodungwa mara mbili pekee kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, jambo muhimu hasa kwa wale wanaopata changamoto kutumia dawa za kila siku.Video ya UNITAID inaonesha maabara yenye teknolojia ya hali ya juu, ambamo wanasayansi wanaandaa dawa hiyo inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID, Tenu Avafia, anasema hatua hii ni ushindi mkubwa kwa jamii zinazohitaji kinga ya muda mrefu dhidi ya VVU."Tumeitikia wito kutoka kwa jamii na nchi tunazohudumia kwa kuhakikisha dawa hii inapatikana kwa gharama nafuu. Tunatarajia usambazaji wa toleo la bei nafuu la dawa hii kuanza kufikia mwaka 2027, chini ya miaka miwili tu tangu idhini kutolewa katika nchi za kipato cha juu — kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa."Akizungumza kuhusu hatua hii muhimu, Carmen Pérez Casas, Mkuu wa Mikakati Mwandamizi wa UNITAID, anasema:"Kwa kushirikiana na watengenezaji wa dawa mbadala, tumefanikisha bei nafuu mapema zaidi. Lakini bado tunahitaji kusaidia nchi na jamii kwa kuongeza upatikanaji."UNITAID inasema kwa msaada wa mashirika kama PEPFAR ambao ni mfuko wa Rais wa MArekani wa usaidizi wa dharura dhidi ya UKIMWI, pamoja na mfuko wa kimataifa na wakfu wa Gates, hatua hii inaleta matumaini ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU duniani.
Kila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
Kila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya mechi za kufuzu kombe la dunia la mwaka ujao, mechi za kufuzu mashindano ya vilabu bingwa kwa kina dada ukanda wa CECAFA, mashindano ya CECAFA Kagame Cup, wanariadha watatu wa Uganda kukosa Riadha za Dunia mwezi huu nchini Japan, rais wa Marekani Donald Trump kuhudhuria fainali ya wanaume ya US Open, Luis Suarez apewa adhabu ya mechi sita baada ya kumtemea mate mwanachama wa benchi la ufundi ya klabu ya Seattle Sounders.
Mnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
Mwaka jana pekee, zaidi ya kesi 3200 za ulaghai wa mapenzi zili ripotiwa nawa Australia.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini kumsikia mgeni wetu Prof. Wallah Bin Wallah, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili kutoka Kenya ambaye anamulika umuhimu wa vitabu katika kukuza lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari, msaada wa kuokoa maisha umefika Gaza. Baada ya wiki 11 za kizuizi kutoka kwa mamlaka za Israeli, malori 198 yaliyobeba chakula, dawa na unga wa ngano yameingia leo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameiitaja hatua hiyo kuwa ya muhimu sana, huku malori 90 yakipakuliwa usiku kwa ajili ya kusambazwa haraka.Mwaka 2024, vita havikuishia kwenye uwanja wa mapambano pekee vilivunja nyumba, masoko na shule. Kuanzia Gaza hadi Ukraine, Sudan hadi Myanmar na zaidi ya raia 36,000 walipoteza maisha yao katika mizozo 14 ya kivita kulimgana na ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa Baraza la Usalama hii leo linalojadili ulinzi wa raia katika mizozo ya silaha.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DAHARI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha ulinzi wa raia na kupanua teknolojia na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea.Makala ambayo inamulika majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yamejikita na ufadhili wa maendeleo, Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid.Na mashinani leo utamsikia mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Bayero jimboni Kano nchini Nigeria anayeshiriki mkutano wa majadiliano ya ufadhili wa maendeleo endelevu unaofanyika Nairobi Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Je, unajua kwa nini wanasayansi hutumia mwaka wa mwanga badala ya kilomita kupima umbali wa nyota na miili mingine ya anga?
Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Mwaka 1995 huko Beijing, China kwenye mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake lilipitishwa Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji, ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kusongesha haki za wanawake. Mwaka huu wa 2025 ikiwa ni miaka 30 baadaye, tathmini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa nchi zimesonga mbele katika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake, kuanzia kuharamaisha ubaguzi kwenye ajira hadi mipango ya kuhimili tabianchi inayozingatia jinsia. Lakini bado kuna vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisiasa na ndio maana wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu wa 2025 kipaumbele ni kusongesha uwezeshaji, haki na usawa. Ni katika kumulika harakati hizo, Assumpta Massoi anakupeleka Singida nchini Tanzania kwenye maadhimisho yaliyoambatana na ujengeaji uwezo.
Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula. Selina Jerobon na taarifa zaidi..
Mwaka wa shule wa 2025 uli anza Jummanne 28 Januari katika majimbo ya Queensland na Kusini Australia, wanafunzi wa shule za msingi na upili walirejea shuleni Jumatano 29 Januari katika jimbo la Victoria na Wilaya ya Kaskazini.
Mwaka wa shule wa 2025 ume anza hii leo Jummanne 28 Januari katika majimbo ya Queensland na Kusini Australia, wanafunzi wa shule za msingi na upili wanatarajia kurejea shuleni kesho Jumatano 29 Januari katika jimbo la Victoria na Wilaya ya Kaskazini.
Leo jaridani: Mwaka 2024 ulighubikwa na machungu lakini kuna matumaini 2025 asema Guterres.UNMAS yaondolea hofu wakulima Beni, DRC kwa kutegua masalia ya mabomu.Makala inatupeleka Uganda kusikiliza msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Ashiimwe Baganiza mwenye ndoto ya kuwa wakili ili kuwatetea wanawake.Mashinani ni mradi wa Siku 1000 wa UNICEF Zambia.
Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg nchini Rwanda, na juhudi za kuchunguza virusi vya VVU nchini Ghana. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua.Makala inatupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyokoko Kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya kukukutanisha na mkimbizi kutoka Somalia anayetumia mpira wa kikapu anatumia mpira wa vikapu kuhamasisha jamii yake na kupinga mil ana desturi zisizofaa.Mashinani ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mpira wa Kikapu, fursa ni yake Danny Batachoka, mwanariadha wa Paralimpiki kutoka Goma nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo, DRC ambaye kupitia video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO, anasema ana ndoto ya kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa mpira wa vikapu katika kitengo chake.” Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mafanikio katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU na juhudi za vijana wakimbizi nchini Uganda kuhakikisha hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Gaza.Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ethiopia kumulika mwelekeo wa usajili wa watoto wanapozaliwa na faida zake. Na mashinani Maram, mama kutoka Deir al-Balah Gaza, ambako familia zinahaha kuokoa mali zao na kukarabati mahema yao yaliyoharibiwa na upepo mkali na maji ya mvua wakati huu wa msimu wa baridi, na kuleta athari kwa watoto wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miongo mingi imekuwa ikiwakaribisha watu wanaokimbia machafuko bila kujali utaifa wao. Kitu ambacho ni kikubwa na cha kipekee kuhusu nchi hii ni kwamba wakati wakimbizi wanapowasili hapa hupewa ardhi, mahali pa kuishi na hata kulima mazao kwa ajili ya kujikimu. Wana uhuru wa kutembea na haki ya kuajiriwa. Hawajatengwa lakini wanaishi ndani ya jamii inayowahifadhi. Sera hii ya Uganda inawaruhusu wakimbizi kujumuishwa katika huduma za kitaifa ambapo wanafaidika na elimu na huduma za afya.”Lakini Kutokana na changamoto za fedha Moulid anasema ukarimu huo sasa uko njia panda"Tatu: Ukarimu wa Uganda uko hatarini kwani wakimbizi zaidi wanaingia kutoka nchi jirani. UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, liko mashinani kufanya kazi na Serikali ya Uganda kusaidia kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu hawa. Hata hivyo, rasilimali ni chanche. Tunahitaji msaada wenu ili Uganda iendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa dunia nzima.”Kwa nyjibu wa UNHCR licha ya idadi kubwa ya watu na rasilimali kidogo, sera za Uganda zinammanisha kwamba wakimbizi ni sehemu ya maisha ya kijamii na kiuchumi na ongezeko la rasilimali litakidhi haja za waliopo sasa na watakaokuja.
Hii leo jaridani tunaangazia serikali ya mpito nchini Syria na wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ethiopia kumulika mwelekeo wa usajili wa watoto wanapozaliwa na faida zake. Na mashinani fursa ni yake Mkombola Melio, mhudumu wa afya ambaye pia ni mnufaika wa mradi wa maji na usafi uitwao RUWASA au Rural Water and Sanitation project inaofadhiliwa na Benki ya Dunia Afrika nchini Tanzania akisema mradi huo umezisaidia jamii kuondokana na maambukizi yanayosababisha magonjwa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Janga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.