Radio Maria Tanzania

Follow Radio Maria Tanzania
Share on
Copy link to clipboard

Connecting to Apple Music.

Radio Maria Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania


    • Oct 24, 2025 LATEST EPISODE
    • weekdays NEW EPISODES
    • 43m AVG DURATION
    • 2,011 EPISODES


    Search for episodes from Radio Maria Tanzania with a specific topic:

    Latest episodes from Radio Maria Tanzania

    Je, ni halali kiongozi wa Kanisa kujihusisha na Siasa?

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 28:06


    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, leo tunaungana na Frater Daud Fungameza kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, akijibu swali la msikilizaji linalosema Kanisa au kiongozi wa Kanisa kujihusisha na harakati za kisiasa au chama cha kisiasa inaruhusiwa? L'articolo Je, ni halali kiongozi wa Kanisa kujihusisha na Siasa? proviene da Radio Maria.

    Fahamu historia ya neno Misa

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 27:17


    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, leo tunaungana na Frater Daud Fungameza kutoka Seminari  Kuu ya Mtakatifu Augustino  Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, akijibu swali la msikilizaji linalosema neno Misa lilianza kutumika lini?  L'articolo Fahamu historia ya neno Misa proviene da Radio Maria.

    Fahamu sababu 10 za kuzaa mtoto mwingine

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 57:55


    Karibu uungane nami  Joyce Jonatus katika kipindi cha Pro Life Utetezi wa Uhai, mwezeshaji ni Godfly Mkaikuta, akitufundisha juu ya sababu 10 za kuzaa mtoto mwingine  L'articolo Fahamu sababu 10 za kuzaa mtoto mwingine proviene da Radio Maria.

    Fahamu majukumu na wajibu wa Mlei?

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 56:19


    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Utume wa Walei, mwezeshaji ni Bi. Rose Gerald Katibu wa Kamati ya Uinjilishaji Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam, akitufundisha juu ya wajibu wa Walei na majukumu yao.  L'articolo Fahamu majukumu na wajibu wa Mlei? proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu sifa ya Mama Bikra Maria Malkia wa Imani?

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 26:09


    Karibu katika kipindi cha Tafakari Nasi, leo tunaungana na Padre  Gidion Kitamboya kutoka Parokia ya Mtakatifu Luka Mwinjili Hembahemba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, akitufundisha juu ya Bikra Maria Malkia wa Imani. L'articolo Je, unafahamu sifa ya Mama Bikra Maria Malkia wa Imani? proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu maisha ya Mtakatifu Bartolongo?

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 57:58


    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi,Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula {C.PP.S}, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya maisha ya Mtakatifu mpya Mtakatifu Bartolongo. L'articolo Je, unafahamu maisha ya Mtakatifu Bartolongo? proviene da Radio Maria.

    Nena nami Bwana Dominika ya 29 ya mwaka C wa Kanisa.

    Play Episode Listen Later Oct 24, 2025 57:09


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Nena nami Bwana, ikiwa ni mafundisho kutoka kwa Mababa wa Kiroho kwa namna ya kipekee wanaonene nasi siku hii ya leo ni Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Iringa, Askofu Christopher Ndizeye wa  Jimbo Katoliki […] L'articolo Nena nami Bwana Dominika ya 29 ya mwaka C wa Kanisa. proviene da Radio Maria.

    Amka na Mama kipindi cha Kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na nane}

    Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 57:58


    Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku ya Bwana, hakika kuimba ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli. L'articolo Amka na Mama kipindi cha Kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na nane} proviene da Radio Maria.

    Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na saba}

    Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 57:38


    Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku mpya ya Bwana, hakika ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli.  L'articolo Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na saba} proviene da Radio Maria.

    Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na sita}

    Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 56:58


    Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku mpya ya Bwana, hakika kuimba ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli.   L'articolo Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka {sehemu ya tisini na sita} proviene da Radio Maria.

    Fahamu heri za Utakatifu katika maisha ya Mwanadamu

    Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 50:07


    Karibu uungane nami Peter katika kipindi cha Fahamu wito wako, mwezeshaji Padre Innocent Bahati Mushi kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Jimbo Kuu Katoliki Arusha, akitufundisha juu ya Heri za utakatifu furahini na kushangilia. L'articolo Fahamu heri za Utakatifu katika maisha ya Mwanadamu proviene da Radio Maria.

    Je, Unazifahamu changamoto za mlango wa nyumba aminifu?

    Play Episode Listen Later Oct 23, 2025 51:02


    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu, Wawezeshaji ni Katekisita Castory Matimla, Benedict Kessy, Monica Kessy na Paschal Maziku kutoka Familia ni Nyumba Aminifu, wakitufundisha juu ya mlango wa nyumba aminifu na changamoto zake. L'articolo Je, Unazifahamu changamoto za mlango wa nyumba aminifu? proviene da Radio Maria.

    Unafahamu sababu zinazosababisha kupata ugongwa wa mtoto wa Jicho?

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 44:04


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Ijue Afya yako, mwezeshaji wa kipindi ni Daktari Catherine Mlale kutoka Hospitali ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Ifakara, Jimbo Katoliki Ifakara, akitufundisha juu ya ugonjwa wa mtoto wa Jicho. L'articolo Unafahamu sababu zinazosababisha kupata ugongwa wa mtoto wa Jicho? proviene da Radio Maria.

    Je, unaufahamu ujumbe wa Amani wa Papa Benedict wa 15?

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 57:28


    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji Padre Dominic Mavula C.PP.S,  Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitueleza juu ya ujumbe wa Amani wa Papa Benedict wa 15   L'articolo Je, unaufahamu ujumbe wa Amani wa Papa Benedict wa 15? proviene da Radio Maria.

    papa pp radio maria karibu ujumbe mkurugenzi
    Fahamu ujumbe wa amani wa Mama Bikira Maria kwa wanadamu?

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 54:46


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa Katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji Padre Dominic Mavula C.PP.S,  Mkurugenzi wa Matamgazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya  ujumbe wa Mama Bikira Maria kuhusu Amani. L'articolo Fahamu ujumbe wa amani wa Mama Bikira Maria kwa wanadamu? proviene da Radio Maria.

    Ifahamu Dominika ya Kimisionari na umuhimu wake?

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 44:27


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania {TEC},  Mwezeshaji Padre Alfred Kwene, akitufundisha juu ya Dominika ya Kimisionari 2025 na wajibu wetu sisi Waamini. L'articolo Ifahamu Dominika ya Kimisionari na umuhimu wake? proviene da Radio Maria.

    Je, unaufahamu ujumbe wa Mapapa na Watakatifu kuhusu Rozari Takatifu?

    Play Episode Listen Later Oct 17, 2025 55:07


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shikishi, Mwezeshaji  Padre Deodatus Katunzi, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akitufundisha juu ya Watakatifu na Mapapa wanazungumza nini kuhusu Rozari Takatifu. L'articolo Je, unaufahamu ujumbe wa Mapapa na Watakatifu kuhusu Rozari Takatifu? proviene da Radio Maria.

    radio maria karibu ujumbe mkurugenzi
    Je, unafahamu maana ya sherehe ya kutukuka kwa msalaba?

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 27:08


    Karibu uungane nami Paschal Patrick, katika kipindi cha Tafakari ya Mama Bikira Maria, Mwezeshaji  Askofu Method Kilaini Askofu Msaidizi Mstaafu Jimbo Katoliki  Bukoba akitufundisha juu ya Kutukuka kwa Msalaba L'articolo Je, unafahamu maana ya sherehe ya kutukuka kwa msalaba? proviene da Radio Maria.

    Ewe mwanamke je, unaufahamu uthubutu wako katika Uchumi?

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 29:13


    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo, leo tutakuwa na mwezeshaji Bi. Eneless Mwinami Afsa Program kutoka Mwanza, akitufundisha juu ya Uthubutu wa mwanamke Kiuchumi. L'articolo Ewe mwanamke je, unaufahamu uthubutu wako katika Uchumi? proviene da Radio Maria.

    Je, unaufahamu uzuri wa Mama Bikira Maria?

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 52:17


    Karibu uungane nami Esther Magai, katika kipindi cha Tumsifu  Maria, Mwezeshaji ni Padre Fabian Ngeleja Paroko wa Parokia ya Nyamanolo Jimbo Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya Uzuri wa Mama Maria.   L'articolo Je, unaufahamu uzuri wa Mama Bikira Maria? proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu umuhimu wa Lishe wakati wa Uzee?

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 56:02


    Karibu uungane nami Martin Joseph, katika kipindi cha Chakula na Lishe, Mwezeshaji wa Kindi ni Bi. Nusula Salum Afsa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania, akitufundisha juu ya Lishe wakati wa Uzee.   L'articolo Je, unafahamu umuhimu wa Lishe wakati wa Uzee? proviene da Radio Maria.

    Mkatoliki je, unaifahamu historia ya Kanisa?

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 58:01


    Karibu uungane nami Paschal Patrick, katika kipindi cha Historia ya Kanisa, mwezeshaji ni Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Msitaafu Jimbo la Bukoba,  akitufundisha Historia juu ya Mapinduzi ya Ufaransa na Kanisa. L'articolo Mkatoliki je, unaifahamu historia ya Kanisa? proviene da Radio Maria.

    Fahamu umuhimu wa nyumba aminifu katika kuhubiri Injili

    Play Episode Listen Later Oct 10, 2025 57:38


    Karibu uungane nami Martin Joseph, katika kipindi cha Familia Bora Nyumba Aminifu, wawezeshaji ni Wanafamilia Bora na Nyumba Aminifu, ambapo watatufundisha juu ya Mlango wa Nyumba aminifu katika Kuhubiri Injili. L'articolo Fahamu umuhimu wa nyumba aminifu katika kuhubiri Injili proviene da Radio Maria.

    Mkatoliki Unafahamu nguvu ya Rozari Takatifu ndani ya Familia?

    Play Episode Listen Later Oct 9, 2025 53:20


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S,  Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya Rozari Takatifu nguvu ya Familia ya Mungu.     L'articolo Mkatoliki Unafahamu nguvu ya Rozari Takatifu ndani ya Familia? proviene da Radio Maria.

    Kwanini Wakristo wengi hawazingatii Sala ya Hija?

    Play Episode Listen Later Oct 9, 2025 27:19


    Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, Mwezeshaji ni Frater Jacob Mkandawile kutoka Parokia ya Bikira Maria wa Bwawa la Mtela Migoli Jimbo Katoliki Iringa, akijibu swali la Msikilizaji linalosema kwanini Wakristo Wakatoliki hawazingatii sana Sala ya Hija. L'articolo Kwanini Wakristo wengi hawazingatii Sala ya Hija? proviene da Radio Maria.

    Fahamu maana ya Msalaba na historia yake?

    Play Episode Listen Later Oct 9, 2025 27:09


    Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, Mwezeshaji ni Frater Daud Fungameza kutoka Parokia ya Songwe Jimbo Katoliki Mbeya, akijibu swali la Msikilizaji linalosema nini maana ya Msalaba? historia yake na lini ishara ya Msalaba ilianza na kutumika, pia kwanini kunatofauti juu ya Upande wa kichwa cha Yesu wa kuegemea […] L'articolo Fahamu maana ya Msalaba na historia yake? proviene da Radio Maria.

    Je,unafahamu maana ya Mavazi wanayovaa Mapadre kabla ya kanzu ya Padre?

    Play Episode Listen Later Oct 9, 2025 25:20


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, Mwezeshaji wa kipindi ni Frater Benedict Luvanga kutoka Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Ruaha Jimbo Katoliki Iringa, akijibu swali la Msikilizaji linalosema Nini maana ya Mavazi madogo wanayovaa Mapadre kama Mshipi, kitambaa Mgongoni na Kifuani vinavyovaliwa kabla ya Kanzu ya Padre.  L'articolo Je,unafahamu maana ya Mavazi wanayovaa Mapadre kabla ya kanzu ya Padre? proviene da Radio Maria.

    Nena nami Bwana Dominika ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba

    Play Episode Listen Later Oct 9, 2025 59:44


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Nena Nami Bwana, Wawezezaji wa kipindi ni Wahashamu Maaskofu na Mapadre kutoka Majimbo mbalimbali,Wakitufundisha juu ya Sikukuu ya Kutukuka Kwa Msalaba Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristo. L'articolo Nena nami Bwana Dominika ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu utakatifu juu ya ulimwengu wa kidijitali?

    Play Episode Listen Later Sep 18, 2025 52:45


    Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Katikisimu Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Kagera akitufundisha juu ya Utakatifu  katika Ulimwengu wa Kidijitali. L'articolo Je, unafahamu utakatifu juu ya ulimwengu wa kidijitali? proviene da Radio Maria.

    radio maria karibu ulimwengu mkurugenzi
    Je,unafahamu mapinduzi ya fikra katika kanisa?

    Play Episode Listen Later Sep 18, 2025 55:57


    Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu Jimbo Katoliki Bukoba, akitufundisha juu ya Mwangaza wa Kanisa Kitaifa.   L'articolo Je,unafahamu mapinduzi ya fikra katika kanisa? proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu changamoto ya Afya ya akili kwa kijana?

    Play Episode Listen Later Sep 18, 2025 47:33


    Karibu uungane nami Joyce Jonatus katika kipindi cha Jukwaa la Vijana, Mwezeshaji  wetu ni Daktari Katanta Razalusi, Mwandamizi wa Masuala ya Uzazi na Familia na Mwenyekiti wa Watoa Huduma za Afya Wakatoliki Jimbo Kuu Katoliki  Dar es Salaam, akitufundisha juu ya changamoto ya Afya ya Akili kwa Vijana.  L'articolo Je, unafahamu changamoto ya Afya ya akili kwa kijana? proviene da Radio Maria.

    Fahamu changamoto ya afya ya akili kwa vijana.

    Play Episode Listen Later Sep 10, 2025 47:33


    Karibu uungane nami Joyce Jonatus katika kipindi cha Jukwaa la Vijana, mwezeshaji  Daktari Katanta Lazarus Simwanza, Mshauri mwandamizi wa maswala ya afya ya uzazi, malezi na familia lakini pia ni Mwenyekiti wa watoa huduma za afya wakatoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, anazungumzia juu ya vijana na changamoto ya afya ya akili. L'articolo Fahamu changamoto ya afya ya akili kwa vijana. proviene da Radio Maria.

    Fahamu historia ya Tanzania Humanitarian Fund (THF), Mfuko wa Hisani wa kusaidia Mahitaji ya Binadamu Tanzania na utendaji kazi wake.

    Play Episode Listen Later Aug 28, 2025 36:19


    Karibu uungane nami Joyce Jonatus katika kipindi cha Elimu Jamii, Wawezeshaji ni Dokta Apiov Lwiwa kiongozi THF-Morogoro , Bi.Mary Gilbert Masudi  Mratibu wa THF pamoja na Bi. Mariana Consalves kutoka Mfuko wa Hisani wa Kusaidia Mahitaji ya Kibinadamu Tanzania. L'articolo Fahamu historia ya Tanzania Humanitarian Fund (THF), Mfuko wa Hisani wa kusaidia Mahitaji ya Binadamu Tanzania na utendaji kazi wake. proviene da Radio Maria.

    Amri 10 za Mungu zimeandikwa wapi katika Biblia Takatifu?

    Play Episode Listen Later Aug 11, 2025 56:50


    Karibu katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini , Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, ambapo ameendelea kujibu maswali mbalimbali yaliyoilizwa na msikilizaji.   Mtangazaji ni Patrick Pascal Tibanga – Radio Mbiu  L'articolo Amri 10 za Mungu zimeandikwa wapi katika Biblia Takatifu? proviene da Radio Maria.

    Ninawezaje kuwasaidia masikini wakati mimi pia ni msikini?

    Play Episode Listen Later Aug 7, 2025 27:33


    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, Swali linahoji hivi; Kanisa linahimiza kuwasaidia watu masikini, sasa mimi nitawezaje kuwasaidia wakati mimi mwenyewe ni masikini? Na je Matajiri hawahitaji kusaidiwa?  Swali limejibiwa na Frateri Peter Peter kutoka Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.   Mtangazaji wako ni Esther Magai Hangu L'articolo Ninawezaje kuwasaidia masikini wakati mimi pia ni msikini? proviene da Radio Maria.

    Biblia inatufundisha nini katika kuvumilia na kupokea Mateso na changamoto katika maisha?

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2025 31:00


    Kipindi Cha Mbiu ya Heri MADA ni Matumaini katika Mateso kadiri ya maandiko Matakatifu katika Maisha ya Mkristo. Mafundisho haya yanatolewa na frateri Fransic Kulamiwa, Kutoka Seminari ya familia Takatifu Mwendakulima, yeye anatoka Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. L'articolo Biblia inatufundisha nini katika kuvumilia na kupokea Mateso na changamoto katika maisha? proviene da Radio Maria.

    Ifahamu fadhila ya msamaha katika Maandiko Matakatifu

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2025 30:52


    Msikilizaji mpendwa karibu uungane na Frater Justine Galus Mwanaka, Kutoka Jimbo Katoliki Iringa, Mseminari katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Familia Takatifu Mwendakulima, Jimbo Katoliki Kahama ambapo anatufundisha juu ya fadhila ya msamaha, ni kupitia kipindi cha Mbiu ya Heri. Karibu sana. L'articolo Ifahamu fadhila ya msamaha katika Maandiko Matakatifu proviene da Radio Maria.

    Zifahamu chunguzi na tathimini katika utegemezi wa matumizi ya dawa za kulevya

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2025 54:33


    Msikilizaji mpendwa karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi Cha Uraibu, ambacho huandaliwa na kuletwa kwetu na Padre Richard Matanda Tesha Kutoka Jimbo Katoliki Moshi, katika kipindi hiki Padre Matanda amezungumzia juu ya “Uchunguzi na tathimini katika utegemezi wa matumizi ya dawa za kulevya”. Karibu kwa Elimu zaidi. L'articolo Zifahamu chunguzi na tathimini katika utegemezi wa matumizi ya dawa za kulevya proviene da Radio Maria.

    Zifahamu Sifa za wazazi wawajibikaji katika kutoa malezi kwa watoto

    Play Episode Listen Later Aug 6, 2025 44:25


    Karibu msikilizaji mpendwa usikilize kipindi cha Kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambapo Sista Anagladness Mrumah, katibu wa Shirika la Utoto Mtakatifu Taifa, anazungumzia kwa undani juu ya mada hiyo. Mimi ni Happiness Mlewa ninakualika kwa niaba yake L'articolo Zifahamu Sifa za wazazi wawajibikaji katika kutoa malezi kwa watoto proviene da Radio Maria.

    Fahamu kuhusu utajiri wa pekee ndani ya Kanisa Kuu la Mama Bikira Maria Mkuu.

    Play Episode Listen Later Aug 5, 2025 53:20


    Karibu katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa matangazo Radio Maria Tanzania anafundisha juu ya heshima kwa Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu.  Mtangazaji wako ni Esther Magai Hangu L'articolo Fahamu kuhusu utajiri wa pekee ndani ya Kanisa Kuu la Mama Bikira Maria Mkuu. proviene da Radio Maria.

    Fahamu utaratibu wa kufunga ndoa ndani ya kanisa Katoliki (Sheria namba 1112 -1118)

    Play Episode Listen Later Aug 5, 2025 57:42


    karibu katika kipindi cha Sheria za Kanisa, kinaandaliwa na kuletwa kwako na Padre Ladislaus Mgaya, Mtaalamu na Mwanasheria wa  sheria za kanisa Kutoka Jimbo Katoliki Njombe anaendelea kufundisha kuhusu taratibu za kufunga ndoa (Sheria namba 1112 -1118) Mtangazaji wako ni mimi Esther Magai Hangu  L'articolo Fahamu utaratibu wa kufunga ndoa ndani ya kanisa Katoliki (Sheria namba 1112 -1118) proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu Ishara ya njia ya msalaba ilifundishwa na nani?

    Play Episode Listen Later Aug 5, 2025 30:04


    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, swali linahoji hivi; Sala ya Baba yetu ilifundishwa na Bwana wetu Yesu Kristo, Je, ishara ya njia ya msalaba katika Kanisa ilifundishwa na nani? Swali limeulizwa na Laurent Michael kutoka Jimbo Katoliki la Sumbawanga Na limejibiwa na Frateri Daudi Fungameza kutoka Parokia ya ya Songwe Jimbo Kuu Katoliki […] L'articolo Je, unafahamu Ishara ya njia ya msalaba ilifundishwa na nani? proviene da Radio Maria.

    fahamu nyenzo anazotumia Roho Mtakatifu kutugusa na kugusa wengine.

    Play Episode Listen Later Aug 3, 2025 53:25


    karibu usikilize kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa ambapo Mhashamu Josaphat Lui Lebulu, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha anafundisha juu ya nyenzo anazotumia Roho  Mtakatifu kutugusa na kugusa wengine. kukualika kwa niaba yake mimi ni Joyce Jonatus. L'articolo fahamu nyenzo anazotumia Roho Mtakatifu kutugusa na kugusa wengine. proviene da Radio Maria.

    Maisha ni Safari (Richard sehemu ya 2)

    Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 57:38


    Karibu uungane na Bwana Richard  katika kipindi cha maisha ni safari akielezea akielezea safari ya maisha yake hii ni sehemu ya 2.  Mtangazaji wako ni mimi Martin Joseph. L'articolo Maisha ni Safari (Richard sehemu ya 2) proviene da Radio Maria.

    Maisha ni Safari (Richard Sehemu ya 1)

    Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 54:45


    Karibu uungane na Bwana Richard katika kipindi cha Maisha ni Safari akielezea  safari ya maisha yake. Mimi ni Mtangazaji wako Martin Joseph. L'articolo Maisha ni Safari (Richard Sehemu ya 1) proviene da Radio Maria.

    Fahamu sababu ya kuweka Msalaba katika kaburi la Mkristo.

    Play Episode Listen Later Aug 1, 2025 20:54


    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, maswali yatakayojibiwa yameulizwa na Judith kutoka Jimbo Kuu la Dar es Salaam akihoji hivi;  Kwanini kwa Wakristo mtu akifariki wanawekewa Msalaba kwenye kaburi?  Naomba kuelewa, maana ya nadhiri, na pia inaweza kuondolewa na mtu au na Mungu? Yanajibiwa na Frateri Barnabasi Myushi, kutoka Parokia Bikira Maria Mpalizwa mbinguni […] L'articolo Fahamu sababu ya kuweka Msalaba katika kaburi la Mkristo. proviene da Radio Maria.

    Je, unafahamu Msalaba ni nguvu ya wowkovu wetu?

    Play Episode Listen Later Jul 30, 2025 55:55


    Ungana nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja anapoendelea kufundisha juu ya thamani ya ukombozi wetu. L'articolo Je, unafahamu Msalaba ni nguvu ya wowkovu wetu? proviene da Radio Maria.

    radio maria nguvu ungana mkurugenzi
    Amka na Mama kipindi cha Kawaida cha mwaka (sehemu ya themanini na saba)

    Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 56:24


    Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha amka na Mama ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za kuanzisha siku mpya na Bwana,hakika kuimba ni kusali mara mbili njooni tumwimbie Bwana katika Roho na kweli. L'articolo Amka na Mama kipindi cha Kawaida cha mwaka (sehemu ya themanini na saba) proviene da Radio Maria.

    Je, ni kwa namna gani Familia inakua chanzo cha ulemavu kwa mtoto?

    Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 47:26


    Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Elimu Jamii, ambapo Sista Angela Jeremiah, Mkurugenzi Kituo cha Utengemao (Mazoezi tiba)cha Antonia Verna – Kawe jijini Dar es Salaam anatoa elimu juu ya Familia kama chanzo cha ulemavu. L'articolo Je, ni kwa namna gani Familia inakua chanzo cha ulemavu kwa mtoto? proviene da Radio Maria.

    Fahamu vizuri nguvu ya wokovu wetu

    Play Episode Listen Later Jul 29, 2025 42:36


    Karibu katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera anafundisha juu ya thamani ya wowkovu wetu akiangazia kipengele cha nguvu ya wowkovu.   Mtangazaji wako ni Esther Magai Hangu  L'articolo Fahamu vizuri nguvu ya wokovu wetu proviene da Radio Maria.

    Mfahamu Mtakatifu Martha Dada yake na Lazaro aliyefufuliwa na Bwana wetu Yesu Kristo.

    Play Episode Listen Later Jul 28, 2025 30:33


    Karibu katika kipindi cha Tafakari ya Bikira Maria, Mwezeshaji ni Mhshamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba leo anatuongoza kuangazia maisha ya Mtakatifu Martha.   Mtangazji wako ni Beatrice Audax  L'articolo Mfahamu Mtakatifu Martha Dada yake na Lazaro aliyefufuliwa na Bwana wetu Yesu Kristo. proviene da Radio Maria.

    Claim Radio Maria Tanzania

    In order to claim this podcast we'll send an email to with a verification link. Simply click the link and you will be able to edit tags, request a refresh, and other features to take control of your podcast page!

    Claim Cancel