Podcasts about ujumbe

  • 21PODCASTS
  • 308EPISODES
  • 26mAVG DURATION
  • 5WEEKLY NEW EPISODES
  • May 15, 2025LATEST

POPULARITY

20172018201920202021202220232024


Best podcasts about ujumbe

Latest podcast episodes about ujumbe

Radio Maria Tanzania
Je, wafahamu sifa za Mwanaume?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 15, 2025 54:31


Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha Sifa za Mwanaume. L'articolo Je, wafahamu sifa za Mwanaume? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, ni sifa zipi ambazo mwanaume anapaswa kuwa nazo?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later May 15, 2025 48:45


Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha Sifa za Mwanaume. L'articolo Je, ni sifa zipi ambazo mwanaume anapaswa kuwa nazo? proviene da Radio Maria.

Habari za UN
05 MEI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 10:52


Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani,  VoTAN      uliofanyika wiki iliyopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), fursa ni yake Rawhiyeh, mkimbizi kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israel ambaye anasimulia kwa uchungu madhila yanayowakumba yeye na familia yake baada ya kupoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Habari za UN
MONUSCO yapatia wanawake wakimbizi DRC mafunzo ya ushoni

Habari za UN

Play Episode Listen Later May 5, 2025 2:31


Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO). Sharon Jebichii na taarifa kamili.

Habari za UN
29 APRILI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 29, 2025 11:44


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari  na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati  kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magumu zaidi. Mzingiro huu unamaanisha kwamba familia nzima, watu saba au wanane wanalazimika kushirikiana kopo moja la maharagwe au njegere”.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limezitaka nchi za Kaskazini Magharibi mwa Afrika kuongeza ufuatiliaji na kuchukua hatua za mapema kudhibiti makundi ya nzige wa jangwani. Hii ni baada ya nzige wakubwa na makundi madogo kutoka ukanda wa Sahel kuhamia maeneo ya kusini mwa Sahara, hasa katikati ya Algeria, magharibi mwa Libya, na kusini mwa Tunisia tangu Februari hadi Machi mwaka huu.Na katika mashinani fursa ni yake Maruping Onkemetse Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Msaada wa Familia, shirika linaloongozwa na wanawake wa asili  katika Wilaya ya Gantsi, kijiji cha Chobokwane nchini Botswana anayeshiriki mkutano unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wa Jukwaa la Watu wa Asili akizungumzia alichojifunza hadi sasa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Ujumbe wa Ernest Makulilo kuhusu siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 23, 2025 3:31


Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri, kuhusu siku ya leo iliyoanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO mnamo mwaka 1995.

Radio Maria Tanzania
Fahamu mchakato wa kumpata Papa mpya.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 23, 2025 48:39


Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), akizungumzia mchakato wa kumpata Papa mpya. L'articolo Fahamu mchakato wa kumpata Papa mpya. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu sifa 15 za akina mama katika Familia.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 15, 2025 57:57


Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu la Mwanza, akiendelea kutufundisha juu sifa 15 za akina mama na leo akifafanua kwa undani sifa ya 15. L'articolo Fahamu sifa 15 za akina mama katika Familia. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Je, unafahamu sifa za akina mama katika Familia?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 11, 2025 56:43


Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kutufundisha juu ya sifa za akina mama akijikita zaidi katika sifa namba 13, 14 na 15. L'articolo Je, unafahamu sifa za akina mama katika Familia? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu sifa 15 za akina mama.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 9, 2025 51:58


Ungana nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kutufundisha juu ya sifa 15 za akina mama akielezea sifa namba 13, 14 na 15. L'articolo Fahamu sifa 15 za akina mama. proviene da Radio Maria.

King Cam's Ujumbe Podcast
Unlocking Ancient Egyptian Wisdom: King Cam Ujumbe Podcast w/ The Khemetic Nation

King Cam's Ujumbe Podcast

Play Episode Listen Later Apr 8, 2025 71:23


Radio Maria Tanzania
Hizo ndizo sifa za Mwanamke katika Jamii.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 57:22


Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya Sifa ya kumi na tano zaWanawake. L'articolo Hizo ndizo sifa za Mwanamke katika Jamii. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Ni kwa namna gani maneno ya Yesu yanavyotufundisha kwamba maadui wa mtu wanaweza kuwa watu

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 57:21


Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha Maadui wa mtu. L'articolo Ni kwa namna gani maneno ya Yesu yanavyotufundisha kwamba maadui wa mtu wanaweza kuwa watu proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Huo ndio uhusiano kati Imani na Jubilee kuu mwaka 2025.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 27:50


Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami  Frateri Peter Peter, Kutoka  Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Songea  nikijibu swali la Msikilizaji linalosema kuhusu Muundelezo wa Ujumbe wa Kwaresma mwaka huu 2025 sura ya tatu ? L'articolo Huo ndio uhusiano kati Imani na Jubilee kuu mwaka 2025. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Ifahamu sifa ya Mwanamke.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 57:21


Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya Sifa ya  Mwananke. L'articolo Ifahamu sifa ya Mwanamke. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Ufahamu Ujumbe wa Kwaresma mwaka huu 2025 kutoka TEC

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Apr 3, 2025 27:05


Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami  Frateri Peter Peter, Kutoka  Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Songea  nikijibu swali la Msikilizaji linalosema kuhusu Ujumbe wa Kwaresma mwaka huu? L'articolo Ufahamu Ujumbe wa Kwaresma mwaka huu 2025 kutoka TEC proviene da Radio Maria.

Habari za UN
Ujumbe wa Katibu Mkuu UN Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma Kuhusu Usonji

Habari za UN

Play Episode Listen Later Apr 2, 2025 1:40


Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote. Anold Kayanda anaeleza zaidi.

Radio Maria Tanzania
Mwanamke na msichana wanatofautianaje?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 20, 2025 49:36


Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya utofauti ya Mwananke na Wasichana. L'articolo Mwanamke na msichana wanatofautianaje? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Ni vigezo gani vinavyotumika kutofautisha kati ya mwanamke na msichana?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 20, 2025 56:43


Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya utofauti ya Mwananke na Wasichana. L'articolo Ni vigezo gani vinavyotumika kutofautisha kati ya mwanamke na msichana? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu utofauti kati ya Mwanamke na Wasichana

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 18, 2025 55:46


Karibu uungane nami Martin Joseph katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha juu ya utofauti ya Mwananke na Wasichana. L'articolo Fahamu utofauti kati ya Mwanamke na Wasichana proviene da Radio Maria.

Habari za UN
14 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 14, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox's Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa lakini kwanza ni makala ambapo Assumpta Massoi anazungumza na mshiriki wa CSW69 kutoka Cote D'Ivoire.Na katika mashinani Felicite Djoukouo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wadau wa Maendeleo nchini Cameroon ambaye anashiriki mkutano wa CSW69 hapa Umoja wa Mataifa anaelezea matarajio yake ya mkutano huu utakaomalizika tarehe 21 mwezi huu wa Machi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!  

Habari za UN
13 MACHI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 13, 2025 11:00


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii imezungumza na Lucy Gidamis, Wakili ambaye kwa sasa anafanya kazi na shirika la Msichana Initiative nchini Tanzania akijikita katika kutetea na kutekeleza haki za wanawake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno Wakfu.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya duniani WHO na la kuhudumia watoto UNICEF yametangaza kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa surua barani ulaya, jumla ya wagonjwa 127,350 waliripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40.Na hii leo ikiwa ni chungu cha 10 cha Ramadhan, ikikamilisha fungu la kwanza kati ya mafungu matatu ambapo ni siku 30 za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameanza ziara yake ya siku nne nchini Bangladesh ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka wa kushiriki Ramadhan na jamii za waislamu walio kwenye changamoto mbalimbali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua neno Wakfu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Habari za UN
Haki Elimu - Ujumbe wetu mkuu kwenye CSW69 ni elimu kwa mtoto wa kike

Habari za UN

Play Episode Listen Later Mar 12, 2025 3:40


Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China  mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.

Radio Maria Tanzania
Fahamu ujumbe wa Kwaresima kwa mwaka 2025.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 6, 2025 45:14


Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Kutoka TEC, Mwezeshaji ni Padre Clement Kihiyo, Katibu Mtendaji kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania, akizungumzia ujumbe wa kwaresima kwa mwaka 2025. L'articolo Fahamu ujumbe wa Kwaresima kwa mwaka 2025. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu ujumbe wa siku ya Wanawake duniani 2025.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Mar 4, 2025 25:29


Karibu uungane nami Agatha Kisimba katika kipindi maalaumu cha Jinsia na Maendeleo, ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka March 08, Mwaka huu 2025 ikiwa na kauli mbiu ya Wanawake na Wasichana tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji. L'articolo Fahamu ujumbe wa siku ya Wanawake duniani 2025. proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Adui yetu ni nani kulingana na Bibilia Takatifu?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 27, 2025 53:38


Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha Maadui wa mtu. L'articolo Adui yetu ni nani kulingana na Bibilia Takatifu? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Fahamu maadui wa mtu ndani ya Kanisa Katoliki?

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 26, 2025 53:52


Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika  kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo nipo na Padre Titus Amigu  kutoka  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akitufundisha Maadui wa mtu. L'articolo Fahamu maadui wa mtu ndani ya Kanisa Katoliki? proviene da Radio Maria.

Radio Maria Tanzania
Zifahamu sifa Kumi na Tano za Wanawake.

Radio Maria Tanzania

Play Episode Listen Later Feb 20, 2025 41:53


Ungana na Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu Katoliki Mwanza katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, leo sifa za kumi na tano za Wanawake yaani akina mama. L'articolo Zifahamu sifa Kumi na Tano za Wanawake. proviene da Radio Maria.

Habari za UN
03 FEBRUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Feb 3, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kutoka Sudan wengi wakiwa ni wanawake na watoto na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linawasaidia.Na katika mashinani  Lodja Salizre, Mkimbizi wa ndani katika kambi ya Loda jimboni Ituri kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC akileleza ni kwa jinsi gani vita inayoendelea vimeameathiri yeye na familia yake na jinsi ambavyo uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo inavyosaidia maisha ya kila siku ya wakazi wake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
27 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2025 9:59


Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DRC yanosababishwa na kundi la waasi la M23 mjini Goma. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa mauaji ya halaiki tutasikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa.Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO kwa kushirikiana na polisi wa kitaifa wa nchi hiyo  PNC wameongeza doria katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bushagara jimboni Kivu Kaskazini kufuatia ongezeko la vitisho na mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa M23.Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania ambako katika kuhamasisha elimu iliyo salama inayolenga kumlea na kumfundisha mtoto kwa njia chanya zisizoumiza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF) linamuangazia Mwalimu Magesa Stanslaus ambaye ambaye amebadilika kutoka katika matumizi ya viboko na sasa anatumia motisha tofauti kuwarekebisha wanafunzi wake.Na mashinani fursa ni yake Miguel Ángel Moratinos, Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Muungano wa Ustaarabu Umoja wa Mataifa UNAOC akitoa ujumbe kuhusu mauaji ya halaiki na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
MONUSCO na polisi wa DRC waongeza doria katika kambi ya Bushagara kufuatia machafuko mapya ya M23

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 27, 2025 2:16


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO kwa kushirikiana na polisi wa kitaifa wa nchi hiyo  PNC wameongeza doria katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bushagara   jimboni Kivu Kaskazini kufuatia ongezeko la vitisho na mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa M23. Flora Nducha na taarifa zaidi

Habari za UN
23 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 23, 2025 10:00


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kumulika mausala ya AI kwenye elimu tukielekea siku ya kimataifa ya elimu inayoangazia matumizi ya AI na changamoto zake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, umethibitisha kuwa waasi wa M23 wametwaa baadhi ya maeneo jimboni Kivu Kusini, miongoni mwao ikiwa mji wa Minova, ukisema hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto na familia zao wanaorejea kaskazini mwa Gaza baada ya kuanza utekelezaji wa usitishaji mapigano wanakutana na uharibifu mkubwa na kuporomoka kwa miundombinu.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema limefanikiwa kuhamisha msaada wa kwanza wa chakula kuingia Sudan kwa ajili ya kulisha watu 80,000 kwa mwezi mmoja kupitia mto Nile.Na katikakujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya msemo “HIVI KWELI KISAUNI KUTOTA MVINDE?”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Habari za UN
Huu ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na AI-Guterres

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 22, 2025 3:20


Viongozi wa kimataifa wa masuala ya kisiasa na biashara wanaokutana Davos Uswisi kwa ajili ya jukwaa la kiuchumi duniani WEF, leo wamekabiliwa na ukweli mchungu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akilaani ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokosa mwelekeo, ikikabiliwa na hatari mbili kubwa ambazo ni mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiyodhibitiwa. Flora Nducha na taarifa zaidiAkizungumza katika Jukwaa hilo la kila mwaka la Kiuchumi Duniani Katibu Mkuu amewaonya viongozi wa dunia na wakuu wa biashara kuhusu vitisho viwili vinavyoongezeka kwa ubinadamu mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiodhibitiwa amesema “Kunapokuja suala la tishio la kimataifa nyuklia sio tishio pekee. Leo hii tunakabiliwa na matishio mawili makubwa ambayo yanahitaji kupewa uziti Mkubwa wa kimataifa na hatua kwa sababu yanatishia kubadili kabisa maisha tunayoyajua, janga la mabadiliko ya tabianchi na upanuzi wa kasi wa wigo wa akili mnemba.”Akikosoa ukosefu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hizi kubwa, Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja haraka ili kushughulikia dunia aliyoiita  dunia inayokosa mwelekeo “Hebu tukabili ukweli , leo hii watu wengi wanapoitazama dunia hawaoni ushirikiano mkubwa wala maarifa ya kutosha . Licha yah atua zilizopigwa uwekezaji katika nishati jadidifu , teknolojia na masuala ya  kiafya ni dunia na matatizo yetu mengi yanazidi kuwa mbaya”Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Guterres amelinganisha uraibu wa dunia kwa nishati ya mafuta na mnyama wa Frankenstein, akisisitiza madhara yake makubwa.Amebainisha kuwa baadhi ya bandari kuu za mafuta duniani ziko hatarini kutokana na viwango vya bahari kuongezeka, jambo linalosababishwa na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi asilia.Katibu Mkuu amekemea viwanda na taasisi za kifedha zinazosuasua kwenye ahadi zao za tabianchi, akisema hii ni kukosa maono na usaliti wa sayansi na watumiaji wanaotafuta uendelevu.Akizungumzia hatari na fursa za AI, Guterres ameelezea kama upanga wa makali mawili. Ingawa inatoa matumaini katika kubadilisha sekta za afya, kilimo, na elimu, ameonya kuhusu hatari kubwa ikiwa haitadhibitiwa.Amesema AI isiyodhibitiwa inaweza kuvuruga uchumi, kudhoofisha imani kwa taasisi, na kuongeza ukosefu wa usawa.Guterres amehitimisha kwa kutoa wito wa mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto hizi muhimu akisema “kubadili mwelekeo wa taasisi kunahitaji kubadili fikra kwa sababu tunakabiliwa na changamoto kubwa zinazoweza kuiangamiza dunia na sishawishiki kwamba viongozi wanalielewa hili.”Amesisitiza umuhimu wa kurekebisha mifumo ya utawala wa kimataifa ili kukabiliana ipasavyo na migogoro ya kisasa, akionya kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu lakini bado haupo katika kiwango cha kutosha.Ujumbe wake ni bayana kwamba sasa ni wakati wa kuchukua hatua za pamoja na za haraka.

Alfajiri - Voice of America
Ujumbe wa Wamarekani ziarani nchini Rwanda kutafuta fursa za uwekezaji - Januari 22, 2025

Alfajiri - Voice of America

Play Episode Listen Later Jan 22, 2025 29:59


rwanda ujumbe
Habari za UN
13 JANUARI 2025

Habari za UN

Play Episode Listen Later Jan 13, 2025 9:57


Hii leo jaridani tunaangazia ripoti mpya kuhusu hali ya usalama na afya ya watoto kote duniani, na amnai na usalama nchini Syria. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ripoti mpya ya kila mwaka kuhusu mustakabali wa watoto ambayo imetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, imeonya kwamba dunia inaingia katika zama mpya za majanga kwa watoto.Wasyria wana matarajio makubwa kwa nchi yao, na hamu kubwa ya watu kutoka katika kila nyanja ya jamii kuja pamoja na kuunda katiba mpya, ambayo lazima ianze na mazungumzo ya kitaifa yaliyo jumuishi. Hayo ni kwa mujibu wa Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, ambaye amekuwa Damascus kukutana na wajumbe kadhaa wa mamlaka ya mpito ili kuhakikisha Wasyria wote wana uwezo wa kushiriki katika mustakbali wa nchi hiyo.Makala inatupeleka nchini Uganda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa muda sasa limekuwa likifanya jukumu muhimu katika kuwezesha usajili wa watoto.Na mashinani fursa ni yake Antoinette Nzale, mkimbizi wa ndani katika kijiji cha Fataki iliyoko Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, DRC akishuhudia jinsi ambavyo juhudi za pamoja za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na wanajeshi wa serikali FARDC zinavyowawezesha wakimbizi wa ndani kuanza kurejea katika mazingira yao ya awali taratibu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  

Habari za UN
24 DESEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Dec 24, 2024 12:51


Hii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono na kijinsia kwenye mizozo. Pia tunakuletea muhtasari wa había za Sudan, Uganda na Tanzania, Mashinani tunarejea Sudan.Ripoti ya Kamati ya Tathmini ya Viwango vya Njaa (IPC) iliyotolewa leo inaeleza kwamba imegundua kuwa kuna maeneo matano zaidi nchini Sudan ambayo yanakabiliwa na baa la njaa kati ya mwezi huu wa Desemba na Mei mwaka ujao wa 2025. Ripoti hiyo imeyataja maeneo hayo kuwa ni ya Darfur Kaskazini yaani Um Kadadah, Melit, El Fasher, Twawisha, na Al Lait.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa EURO milioni 1 kutoka serikali ya Ujerumani ili kusaidia shughuli za lishe na ustawi kwa zaidi ya wakimbizi na wasaka hifadhi 254,000 nchini Uganda ambayo inawahifadhi wakimbizi milioni 1.7.Na Kikosi cha 7 cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 7 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA) kimerejea nyumbani Tanzania kikijivunia kuwa kikosi cha kwanza cha nchi hiyo kupokea barua ya pongezi kutoka Umoja wa Mataifa.Mashinani fursa ni yake Najwa Mohamed, mama mjamzito kutoka Jabal Moya nchini Sudan ambaye amepoteza makazi yake kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo na kulieleza Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi,  UNFPA kwamba hali ni ngumu hasa kwa wanawake wajawazito.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!   

Habari za UN
26 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 26, 2024 11:25


Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mgogoro Lebanon, Afya ya kinywa, na Ujumbe wa Katibu Mkuu kutoka Portugal akihutubia Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, (UNAOC). Mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza kumsikia muathirika wa vita ya Israel.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Habari za UN
25 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 9:47


Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, na Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC la kukarabati daraja linalounganisha barabara muhimu. Makala tunakwenda nchini Tanznaia na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza?Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo.Makala inatupeleka Tanzania kwake Hamad Rashid wa redio washirika Kidstime FM ya mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo akizungumza na wanufaia wa mafunzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO la ufugaji kuku bila kutumia dawa.Na mashinani tunakwenda Kenya kusikia harakati za viongozi wa dini ya kiislamu kukabiliana na ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 

Habari za UN
MONUSCO yaitikia ombi la Meya wa Beni, Kivu Kaskazini DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 25, 2024 1:39


Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo. Maelezo kamili anayo George Musubao kutoka Beni, katika taarifa hii tuliyoitoa kwenye ukurasa wa X wa MONUSCO. 

Habari za UN
05 NOVEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Nov 5, 2024 11:39


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita,  tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia  harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Habari za UN
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 16, 2024 1:47


Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini  yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, vya aina mbalimbali vipatikane kwa wote, na kuhifadhi tamaduni za jadi za chakula.” Ujumbe huo wa mkuu wa FAO unafanana na ujumbe wa Papa Francis ambaye amesisitiza wafanya uamuzi wa kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa lazima wasikilize matakwa ya wale walio chini kabisa katika mnyororo wa chakula.Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia video amesema, "kuna kitu hakiko sawa katika ulimwengu ambao njaa na utapiamlo ni ukweli wa maisha kwa mabilioni ya watoto, wanawake na wanaume." Akasema ulimwengu usio na njaa unawezekana, lakini "mifumo ya chakula inahitaji mabadiliko makubwa," ili kuwa na ufanisi zaidi, ujumuishi, mnepo na endelevu.Gérardine Mukeshimana, Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ametoa wito wa "uwekezaji wa haraka, wa pamoja na thabiti kwa wakulima maskini wa vijijini kutambua kwa ngazi ya chini kabisa haki yao ya msingi ya chakula chenye lishe." Akabainisha kuwa wakulima wadogo wanazalisha karibu nusu ya chakula cha dunia, ingawa pia wanakabiliwa na njaa na umaskini.Mfalme Letsie III wa Lesotho, ambaye ni Balozi Mwema Maalum wa FAO katika upande wa lishe anaeleza anavyoiunga mkono FAO kwa “kujaribu kuwa mtetezi mwaminifu na mwenye kujitolea katika masuala ya lishe, katika masuala ya uhakika wa chakula.” Anasema, “na mara kwa mara, mimi hutembelea sehemu nyingine za bara la Afrika nikivaa kofia yangu ya FAO, hasa kuhimiza serikali na viongozi kama bara kuwekeza zaidi katika masuala ya lishe na masuala ya uhakika wa chakula.”. 

AWR Swahili / Kiswahili / لغة سواحلية

Ujumbe wa Mbinguni

mungu ujumbe
Habari za UN
Wiki mbili za kusaka usalama DRC, mkimbizi asimulia madhila na atakacho.

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 7, 2024 2:23


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani.  Cicey Kariuki na taarifa zaidiRusayo ni eneo lililo na makazi ya muda ya wakimbizi   mjini Goma katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miongoni mwa  wakimibizi wa ndani wanaishi kwenye makazi haya ni Sebororo, mwanamke mwenye  miaka 38 akitembea na watoto wake.Sebororo pamoja na wananawe watano wanaishi kwenye makazi ya pamoja na familia nyingine 90 huku wakisubiri kutengewa nyumba katika eneo hilo. Mama huyu anaeleza jinsi alivyojikuta katika makazi ya wakimbizi. Anasema,“tulianza kukimbia kuktoka kule tarehe tano mwezi wa kumi, awali walikuwa wanakuja lakini hawakuua watu, lakini leo hii wanaua watoto,wanaume na wanawake, sisi yalitushinda maanake wengine walikuwa pia wanatekweteza mimea.”Sebororo na watoto wake watano walitembea kwa wiki mbili kutafuta usalama, baada ya wapiganaji kuvamia kijiji chao cha Kiseguru katika Mkoa wa Kivu Kaskazini. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2024 pekee, zaidi ya watu 940,000 walilazimika kukimbia kutokana na ukatili, uliofanywa na makundi mengi yenye silaha yasiyo ya kiserikali huku familia nyingi zikifurushwa mara kadhaa. Kwa sasa anachokitamani zaidi Sebroro ni amani. “Haja yetu sisi ni watusaidie kwa kusimamisha vita ili turejee kwetu kwa sababu watu wanaisha.”Anasema.Kufurika kwa watu katika makazi haya ya muda kumezua  wasiwasi mkubwa miongoni mwa wahudumu wa kibinadamu kufuatia hatari ya kuenea kwa magonjwa, ikiwa ni pamoja na virusi vya homa ya nyani au mpox.Ruven Menikdiwela, Kamishna Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR ambaye alitembelea eneo hilo na kukutana na familia mbalimbali za wakimbizi na kusikiliza wasiwasi wao, anasema, “leo asubuhi, nilizungumza na mwanamke huyu ambaye ana watoto wadogo watano. Alitembea kwa wiki mbili kufika katika eneo hili, bado anasubiri huduma, bado anasubiri watoto wake watibiwe, na bado anasubiri chakula. Ninatambua kwamba hii ni hali ya kawaida kwa watu wote wanaoishi katika eneo hili. Kila mmoja ana majanga yake binafsi, kwa hivyo hizi siyo tu takwimu, bali kuna hadithi za kibinafsi nyuma ya kila moja ya hizi takwimu na majanga ya kibinafsi na majanga yanayoendelea pia, kwa sababu hatuoni suluhisho lolote kwenye mustakabali.”Katika ziara yake kwenye makazi haya, Ruven Menikdiwela, pia alifanya vikao na wadau kadhaa akiwemo Waziri mkuu, mamlaka za mkoa na mashirika ya umoja wa Mataifa. Ujumbe wake ulikuwa wazi kwamba amani ndiyo suluhisho endelevu na dhabiti zaidi, na inahitajika kwa dharura. “Pande zote zinapaswa kukutana na kujadiliana kutoa fursa kwa amani, ili watu hawa wote, mamilioni ya watu waliolazimika kuhama, waweze kurudi nyumbani au kuunganishwa na jamii mahali walipo, na waweze kuishi kwa amani pamoja kama jamii moja.”

Habari za UN
01 OKTOBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Oct 1, 2024 11:00


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79, umekunja jamvi jana Jumatatu, tunaangazia sehemu ya pili ya mahojiano na mmoja wa washiriki wa mjadala huo waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na sauti za mashinani, kulikoni?Baada ya siku 6 za viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa hotuba kuhusu masuala muhimu yanayogusa dunia hivi sasa, wakizingatia maudhui ya kutomwacha nyuma mtu yeyote, hatimaye Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi Jumatatu ya Septemba 30 jijini New York, Marekani.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limesema kufuatia tangazo la serikali ya Rwanda juu ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya marburg tarehe 27 mwezi uliopita, hadi sasa watu 8 wamefariki dunia kati ya 26 waliothibitishwa kuugua ugonjwa huo, mara ya kwanza kuripotiwa Rwanda. Rwanda inashirikiana na wadau ikiwemo WHO kudhibiti kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba. Asilimia 70 ya wagonjwa ni wahudumu wa afya kutoka vituo viwili vya afya kwenye mji mkuu Kigali.Na baada ya jeshi la Israeli hapo jana kujulisha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Mpito nchini Lebanon, UNIFIL juu ya nia yake ya kuanza mashambulizi ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah nchini humo, hii leo ujumbe huo umesema licha ya hatari inayoendelea ya mashambulizi, walinda amani wamejipanga. UNIFIL imesema mara kwa mara wanabadili mwenendo na operesheni zao na tayari wana mipango ya kutekeleza iwapo itahitajika kufanya hivyo. IDF na Hezbollah wamekuwa wanashambuliana kusini mwa Lebanon.Mashinani leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe kutoka kwa mmoja ya wazee, ana maoni gani?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Habari za UN
13 SEPTEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 13, 2024 9:40


Hii leo jaridani tunaangazia chanjo za polio katika ukanda wa Gaza, na kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Makala inatupeleka nchini CAR na mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia, kulikoni?Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umesimikwa kwenye bustani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhakikisha kilichotokea hakitosahaulika na      asilani kisitokee tena.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo CAR (MINUSCA).Na katika mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia ambapo kupitia video ya UNICEF, tunakutanisha na Ariet, mtoto wa umri wamiaka 10 aliyekumbwa na utekaji baada ya kijiji chake kuvamiwa. Ariet anaeleza jinsi alivyofurahi baada ya kupata msaada wa UNICEF, ili kurejea kwenye maisha ya kawaida.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

Habari za UN
Walinda amani wa Tanzania wang'ara katika ulinzi wa amani nchini Afrika ya Kati, CAR

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 13, 2024 2:33


Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSCA) kimetunukiwa nishani za Umoja wa Mataifa mnamo tarehe10 Septemba 2024. Afisa Habari wa kikosi hicho, Kapteni Emanuel Ngonela alikuwa shuhuda na ametuandalia makala hii.

Habari za UN
UNMISS: Wananchi wa kaunti ya Nasir watakiwa kuepuka mapigano ili wapelekewe maendeleo

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 1:56


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

sudan hata wfp umoja sekta lakini mataifa maendeleo unmiss shirika ujumbe kaunti wananchi septemba sudan kusini
Habari za UN
09 SEPTEMBA 2024

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 9, 2024 9:58


Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Habari za UN
Wachunguzi wa haki za binadamu wataka kuongezwa kwa vikwazo vya silaha Sudan - UN

Habari za UN

Play Episode Listen Later Sep 6, 2024 1:54


Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono.  Ni mbobevu wa sheria duniani, Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Ujumbe huo Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa Mataifa wa kutafuta ukweli kuhusu yanayoendelea Sudan akiwaeleza waaandishi wa habari leo kwamba, "tangu katikati ya Aprili mwaka 2023, mzozo wa Sudan umeenea hadi majimbo 14 kati ya 18 na kuathiri nchi nzima na ukanda huo, na kuwafanya Wasudan milioni nane kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na mzozo huo, na milioni mbili - zaidi ya milioni mbili – kulazimishwa kukimbilia nchi jirani.”Katika ripoti yao hii ya kwanza tangu Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipounda jopo hilo mwaka jana 2023, wajumbe hawa wamesisitiza kwamba pande zote mbili zinazohasimiana yaani wanajeshi wa Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), pamoja na washirika wao, wanahusika na mashambulizi makubwa, ya kiholela na ya moja kwa moja yaliyohusisha mashambulizi ya anga na makombora dhidi ya raia, shule, hospitali, mitandao ya mawasiliano na miundombinu mingine muhimu ya maji na umeme ikionesha kutozingatia kabisa ulinzi wa wasio wapiganaji.Joy Ngozi Ezeilo, mmoja wa wajumbe wa jopo hilo la wataalamu huru anaeleza kwamba, waathirika walisimulia kushambuliwa wakiwa kwenye nyumba zao na kutishiwa kifo au kuumizwa kwa ndugu au watoto wao kabla ya kubakwa na zaidi ya mtu mmoja.”Wachunguzi hao licha ya kupendekeza uwekaji zaidi wa vikwazo vya silaha kwa Sudan, pia wamehimiza kuanzishwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani na ama kiwe chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa au mamlaka nyingine ya kikanda.

Habari za UN
Monusco yafadhili ujenzi wa zahanati katika gereza kuu la Beni,DRC

Habari za UN

Play Episode Listen Later Aug 28, 2024 1:56


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,  DRC, MONUSCO, umeboresha huduma za afya kwenye Gereza Kuu la Beni, jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika kwa kujenga zahanati iliyoboresha sit u mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya bali pia huduma za matibabu kwa wafungwa. Cecily Kariuki anasimulia zaidi(Taarifa ya Cecily Kariuki)Video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, zamani Twitter inaonesha jengo la zahanati hiyo likiwa la rangi nyeupe na buluu, wahudumu wa afya wakiwa na makoti meupe, masafi kabisa, halikadhalika mazingira ya kituo hiki.Miongoni mwao ni Dkt. Michel Muhindo ambaye hawezi kuficha furaha yake.(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Msaada huu wa zahanati ni ahueni kubwa kwetu sisi tunaofanya kazi hapa, na hata kwa wafungwa, kwa sababu wanapatiwa huduma nzuri ya uchunguzi, na tunafanikiwa kutoa majibu mazuri na tunawatibu ipasavyo. Tunakadiria kwamba kweli ilikuwa inahitajika.”Je, hali ilikuwa vipi kabla ya maboresho haya?(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Kabla ya kupata huduma hii ya matibabu, yaani zahanati hii, kulikuwa tu na vyumba ambavyo tulikuwa tunawaweka wagonjwa kwa ajili ya uchunguzi. Lakini hakukuwa na maabara, wala ofisi nzuri za ushauri. Tulikuwa na wakati mgumu sana, kulikuwa na kelele. Ilibidi kuwa makini sana ili kuweza kusikiliza wafungwa wagonjwa.”Sasa wafungwa wanapata huduma kwa nafasi kabisa..(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Hii inapunguza muda wa huduma kwa wafungwa katika zahanati hii. Sasa kuna maeneo maalumu yaliobainishwa vizuri. Tunaweza kusema: hiyo ni maabara, hicho ni chumba cha uchunguzi wa wagonjwa, hicho ni chumba cha daktari, kwa wauguzi, pamoja na mapokezi ambapo tunaweza kuwakaribisha wafungwa wanaokuja kwa ushauri wa matibabu.”